11-Fadhila Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Allaah Amemfanya Kuwa Khaliyl Wake

Fadhila Za  Nabiy  (صلى الله عليه وآله وسلم)

 

11-Allaah Amemfanya Kuwa Khaliyl Wake

 

www.alhidaaya.com

 

 

عَنْ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ الْحَارِثِ النَّجْرَانِيِّ، قَالَ حَدَّثَنِي جُنْدَبٌ ، قَالَ سَمِعْتُ النَّبِيَّ صلى الله عليه وسلم قَبْلَ أَنْ يَمُوتَ بِخَمْسٍ وَهُوَ يَقُولُ: ((إِنِّي أَبْرَأُ إِلَى اللَّهِ أَنْ يَكُونَ لِي مِنْكُمْ خَلِيلٌ فَإِنَّ اللَّهَ تَعَالَى قَدِ اتَّخَذَنِي خَلِيلاً كَمَا اتَّخَذَ إِبْرَاهِيمَ خَلِيلاً وَلَوْ كُنْتُ مُتَّخِذًا مِنْ أُمَّتِي خَلِيلاً لاَتَّخَذْتُ أَبَا بَكْرٍ خَلِيلاً، أَلاَ وَإِنَّ مَنْ كَانَ قَبْلَكُمْ كَانُوا يَتَّخِذُونَ قُبُورَ أَنْبِيَائِهِمْ وَصَالِحِيهِمْ مَسَاجِدَ أَلاَ فَلاَ تَتَّخِذُوا الْقُبُورَ مَسَاجِدَ إِنِّي أَنْهَاكُمْ عَنْ ذَلِكَ ))‏.‏

Imetoka kwa ‘Abdullah bin Al-Haarith An-Najraaniyy ambaye amesema:  “Jundub amenihadithia kwamba: Nimemsikia Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akisema kabla siku tano za kufariki kwake:  ((Mimi niko huru mbele ya Allaah kwenu kuwa na Khaliyl.  Kwani Allaah Ta’aalaa Amenifanya kuwa Khaliyl kama Alivyomfanya Ibraahiym kuwa Khaliyl. (Rafiki kipenzi mwandani) Na ingelikuwa kumfanya mtu katika ummah wangu kuwa Khaliyl basi ningelimfanya Abuu Bakr kuwa Khaliyl (wangu). Tahadharini! Walio kabla yenu walikuwa wakifanya makaburi ya Manabii wao na watu wema wao kuwa ni mahali pa ‘ibaadah! Basi msifanye makaburi kuwa ni mahala pa ‘ibaadah hakika mimi nakukatazeni hivyo!)) [Muslim]

 

Maana ya Khaliyl: Amesema Shaykhul-Islaam ibn Taymiyyah:  “Ukhaliyl ni mapenzi kamilifu yanayolazimikana na ‘Ubuwdiyyah: (kumwabudu Allaah kikamilifu), na kutoka kwa Rabb Subhaanahu, ni ukamilifu wa  Ar-Rubuwbiyyah (Uola) kwa waja Wake wanaompenda Naye Anawapenda” [Risaalah Al-‘Ubuwdiyyah]

 

 

Sifa hiyo aliyopewa Nabiy Ibraahiym (‘Alayhis-salaam) kuwa ni Khaliyl wa Allaah imethibiti katika kauli ya Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

 

وَمَنْ أَحْسَنُ دِينًا مِّمَّنْ أَسْلَمَ وَجْهَهُ لِلَّـهِ وَهُوَ مُحْسِنٌ وَاتَّبَعَ مِلَّةَ إِبْرَاهِيمَ حَنِيفًا ۗ وَاتَّخَذَ اللَّـهُ إِبْرَاهِيمَ خَلِيلًا ﴿١٢٥﴾

Na nani aliye bora zaidi kwa Dini kuliko yule aliyejisalimisha kwa Allaah naye ni mtendaji mazuri na akafuata millah ya Ibraahiym aliyejiengua na upotofu akaelemea Dini ya haki. Na Allaah Amemchukua Ibraahiym kuwa ni kipenzi. [An-Nisaa: 125]

 

Na Hadiyth nyenginezo:

 

عَنْ عَبْدِ اللَّهِ، عَنِ النَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم قَالَ: ((لَوْ كُنْتُ مُتَّخِذًا مِنْ أَهْلِ الأَرْضِ خَلِيلاً لاَتَّخَذْتُ ابْنَ أَبِي قُحَافَةَ خَلِيلاً وَلَكِنْ صَاحِبُكُمْ خَلِيلُ اللَّهِ ))

Imepokelewa kutoka kwa ‘Abdullaah kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:  ((Ingelikuwa kumfanya mtu katika dunia hii kuwa Khaliyl, basi ningelimfanya Ibn Abiy Quhaafah (Abu Bakr Asw-Swiddiyq Radhwiya Allaahu ‘anhu) kuwa ni Khalily (wangu) lakini Swahibu wenu ni Khaliyl wa Allaah)) [Muslim]

 

Katika usimulizi wa Sunan Ibn Maajah, Wakiy’ amesema kuhusu “Swahib wenu” amekusudia yeye mwenyewe Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam).

 

 

Na katika Riwaayah nyengine:

 

 

عَنْ عَبْدِ اللَّهِ، قَالَ قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم : ((أَلاَ إِنِّي أَبْرَأُ إِلَى كُلِّ خِلٍّ مِنْ خِلِّهِ وَلَوْ كُنْتُ مُتَّخِذًا خَلِيلاً لاَتَّخَذْتُ أَبَا بَكْرٍ خَلِيلاً إِنَّ صَاحِبَكُمْ خَلِيلُ اللَّهِ ‏))

 

((Mimi niko huru kutokana na utegemezi wa marafiki wote wapenzi na wandani. Ingelikuwa napaswa kumfanya mtu kuwa Khaliyl (Rafiki kipenzi mwandani), basi ningelimfanya Abuu Bakr. Hakika Allaah Amemfanya Swahib yenu kuwa Khaliyul Wake)) [Muslim]

 

 

 

Share