046-Hiswnul-Muslim: Du’aa Akitokewa Mtu Na Jambo Asiloridhika Au Akishindwa Kufanya Jambo

Hiswnul-Muslim

046-Du’aa Akitokewa Mtu Na Jambo Asiloridhika Au Akishindwa Kufanya Jambo

 www.alhidaaya.com

 

 

 

 Bonyeza Hapa Usikilize

 

 

 [144]

قَدَّرَ اللهُ وَما شـاءَ فَعَـلَ

Qadara-Allaahu wamaa Shaa Fa’ala

 

Amepanga Allaah na Analolitaka Anafanya[1]

 

 


[1]Hadiyth ya Abu Hurayrah (رضي الله عنه),

 

قَالَ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم: ((المُؤْمنُ القَوِيُّ خَيرٌ وَأَحَبُّ إِلَى اللهِ مِنَ المُؤْمِنِ الضَّعيفِ، وَفي كُلٍّ خَيرٌ. احْرِصْ عَلَى مَا يَنْفَعُكَ، واسْتَعِنْ بِاللهِ وَلا تَعْجَزْ. وَإنْ أَصَابَكَ شَيءٌ فَلا تَقُلْ لَوْ أنّي فَعَلْتُ كَانَ كَذَا وَكَذَا، وَلَكِنْ قُلْ: قَدرُ اللهِ، وَمَا شَاءَ فَعلَ؛ فإنَّ لَوْ تَفْتَحُ عَمَلَ الشَّيطَانِ)). رواه مسلم

Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وسلم) amesema: ((Muumini mwenye nguvu ni bora na anapendeza zaidi kwa Allaah kuliko Muumini dhaifu, na wote wana kheri. Fanya pupa kwa kile kitakachokunufaisha na taka msaada kwa Allaah wala usichoke na kikikupata kitu chochote kibaya basi usiseme: ”Lau kama ningefanya kadha na kadha yasingenitokea haya” lakini sema: 

قَدَّرَ اللهُ وَما شـاءَ فَعَـلَ

Qadara-Allaahu wamaa Shaa Fa’ala” kwani [neno la] ”Lau” linafungua amali za shaytwaan)) – Muslim (4/2052) [2664].

 

 

 

Share