106-Hiswnul-Muslim: Anachopaswa Kusema Mtu Ikimfikia Khabari Ya Kufurahisha Au Ya Kusikitisha

Hiswnul-Muslim

106-Anachopaswa Kusema Mtu Ikimfikia Khabari Ya Kufurahisha Au Ya Kusikitisha

www.alhidaaya.com

 

 

Bonyeza Hapa Usikilize

 

[218]

 

Alikuwa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وسلم) ikimfikia khabari ya kufurahisha akisema:

 

الْحَمْـدُ للهِ الَّذي بِنِـعْمَتِهِ تَتِـمُّ الصّـالِحَات

 

AlhamduliLLaahiL-Ladhiy Bini’matihi tattimusw-swaalihaat

 

Himdi Anastahiki Allaah Ambaye kwa neema Yake yanatimia mambo mema.

 

Na ikimjia khabari ya kusikitisha kusema:

 

الْحَمْـدُ للهِ على كُـلِّ حاَلٍ

Alhamdu-liLLaahi ‘alaa kulli haal

 

Himdi Anastahiki Allaah kwa hali zote[1]

 

 

 

[1]Hadiyth ya ’Aaishah (رضي الله عنها)   - Ibn As-Sunniy katika ‘Amal Al-Yawm wal-Laylah [378], Al-Haakim akaisahihisha (1/499) na ameisahihisha Al-Albaaniy (رحمه الله) katika  Swahiyh Al-Jaami’ (4/201) [4640]. Taz pia Swahiyh Ibn Maajah [3081].

 

 

Share