119-Hiswnul-Muslim: Du’aa Ya Siku Ya ‘Arafah

Hiswnul-Muslim

119-Du’aa Ya Siku Ya ‘Arafah

www.alhidaaya.com

 

 

 Bonyeza Hapa Usikilize

 

[237]

 

Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وسلم) amesema:

 

خَيْرُ الدُّعَاءِ دُعَاءُ يَوْمِ عَرَفَةَ، وَخَيْرُ مَا قُلْتُ أَنَا وَالنَّبِيُّونَ مِنْ قَبْلِي

Du’aa bora kabisa ni du’aa ya siku ya ’Arafah. Na bora ya niliyoyasema mimi na Manabii kabla yangu ni 

 

لا إِلَهَ إلاَّ اللهُ وَحْدَهُ لا شَريكَ لَهُ، لَهُ المُلْكُ ولَهُ الحَمْدُ وهُوَ عَلَى كُلِّ شَيْءٍ قَديرٌ.

 

Laa ilaaha illa Allaahu Wahdahu laa shariyka Lah. Lahul Mulku walahul Hamdu wa Huwa ’alaa kulli shay-in Qadiyr.

 

 

Hapana mwabudiwa wa haki ila Allaah hali ya kuwa Peke Yake hana mshirika. Ni Wake Ufalme na ni Zake Himdi, Naye juu ya kila kitu ni Muweza.[1]

 

 

 

[1]Hadiyth ya ‘Abdullaah bin ‘Amru bin Al-‘Aasw (رضي الله عنهما)  - At-Tirmidhiy [3585] na Al-Albaaniy (رحمه الله) ameipa daraja ya Hasan katika Swahiyh At-Tirmidhiy (3/184) na katika Al-Ahaadiyth Asw-Swahiyhah (4/6)

 

 

Share