132-Hiswnul-Muslim: Katika Mambo Ya Kheri Na Adabu Kwa Jumla (Na Kinga Ya Watoto Dhidi Ya Mashaytwaan)

Hiswnul-Muslim

132-Katika Mambo Ya Kheri Na Adabu Kwa Jumla

(Na Kinga Ya Watoto Dhidi Ya Mashaytwaan)

www.alhidaaya.com

 

 

Bonyeza Hapa Usikilize

 

[267]

 

قَالَ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّم: ((إِذَا كَانَ جُنْحُ اللَّيْلِ أَوْ أَمْسَيْتُمْ فَكُفُّوا صِبْيَانَكُمْ، فَإِنَّ الشّيَاطِيَ تَنْتَشِرُ يَنْتَشِرُ حِينَئِذٍ، فَإِذَا ذَهَبَ سَاعَةٌ مِنْ اللَّيْلِ فَخَلُّوهُمْ، وَأَغْلِقُوا الْأَبْوَابَ وَاذْكُرُوا اسْمَ اللَّهِ فَإِنَّ الشَّيْطَانَ لَا يَفْتَحُ بَابًا مُغْلَقًا، وَأَوْكُوا قِرَبَكُمْ وَاذْكُرُوا اسْمَ اللَّهِ، وَخَمِّرُوا آنِيَتَكُمْ وَاذْكُرُوا اسْمَ اللَّهِ وَلَوْ أَنْ تَعْرضُوا عَلَيْهَا شَيْئًا، وَأَطْفِئُوا مَصَابِيحَكُم))

Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وسلم) amesema: ((Ikiingia jioni [yaani jua linapokuchwa wakati wa Magharibi] wazuieni watoto wenu kutoka toka nje kwani mashaytwaan wanatawanyika nyakati hizo. Ukishapita wakati waacheni.  Na fungeni milango yenu na mtajeni Allaah mnapoifunga [mseme: BismiLLaah], kwani shaytwaan hafungui mlango uliofungwa.  Na fungeni viriba vyenu vya maji, na mtajeni Allaah [mseme: BismiLLaah]. Na funikeni vyombo vyenu na mtajeni Allaah [semeni: BismiLLaah]  (funikeni) hata kama ni kwa kuwekea kitu ju.  Na zimeni taa zenu[1]

 

وَصَلَّى اللهَ وَسَلَّمَ وَبَارَكَ عَلى نَبِيِّنَا مُحَمَّدٍ وَعَلى آلِهِ وَأَصْحَابِهِ أَجْمَعِينَ

Wa swalla Allaahu aa sallama wa Baaraka ‘alaa Nabiyyinaa Muhammadi wa ‘alaa aalihi wa aswhaabihi ajma’iyna

 

 

 

 

 

[1]  Al-Bukhaariy pamoja na al-Fat-h (10/88), Muslim (3/1595)

 

 

Share