Kababu Za Mayai Ya Kuchemsha

Kababu Za Mayai Ya Kuchemsha

Vipimo

Mayai yaliochemshwa - 6

Nyama ya kusaga - 1 1/2 Ratili (LB)

Tangawizi na Kitunguu saumu(thomu) iliyosagwa - 1 kijiko cha Supu

Pilipili mbichi ya Kusaga - 1

Mafuta - 2 Vijiko Vya Supu

Unga wa mahindi (Constarch) - 1 Kijiko cha Supu

Chumvi - Kiasi

Bizari ya manjano - 1/4 kijiko cha chai

Dania ya unga - 1/4 Kijiko cha chai

Bizari ya Pilau - 1/4 Kijiko cha chai

Namna ya kutayarisha na kupika

  1. Changanya nyama na vitu vyake kisha gawanya madonge 6 yaliyosawa.
  2. Chukuwa donge moja tia ndani yake yai uliochemsha na lifunike vizuri.
  3. Ukisha maliza yote panga kwenye treya la kupikia katika jiko la oveni nyunyizia mafuta kidogo na choma moto wa 375F kwa muda wa dakika 25.
  4. Yakishaiva epua na kisha ukate kama ilivyo kwenye picha .Tayari kuliwa .         

 

Share