Siki au ndimu - 3 Vijiko vya supu
* Ukipenda muache na ngozi bila ya kumchuna au mtoe ngozi.
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
- Changanya tangawizi na thomu, pilipili mbichi pamoja na vitu vyote vingine katika kibakuli.
- Mpasue kuku kidogo (slit) kila mahali kuweka njia ya kuweka huo mchanganyiko wa rojo la kuvumbika.
- Mtie hilo rojo kila sehemu na muacha avumbike (marinade) kwa muda wa masaa mengi katika friji.
- Paka mafuta kidogo katika treya umuweke kuku, kisha mchome katika oveni moto wa 450º kwa muda wa dakika 45 hadi awive.
- Mtoe na umuweke katika sahani ya kupakulia ukipambia na saladi upendavyo.