SWALI:
Ndugu zangu na nawatakia kila la kheri alhidaaya wote na Mwenyezi Mungu awajaliye kila la kheri na mzidi kutusaidia....inshaalah ameen swala langu ni: mimi ni bint wa kisilam ambae sijaolewa, kwa bahati nzuri nimekuja kuposwa ila huyo mwanamme sijaridhika nae kwa uzuri wake, na wazazi wameamua kuniozesha kwa nguvu bila ya ridhaa yangu na sijui nifanye nini kwahiyo naomba mnisaidie na ikiwezekana mnijibu haraka iwezekanavyo maasalam...
JIBU:
Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.
Shukrani zetu za dhati kwa dada yetu kwa swali lako. Kuhusu suala lako kuna tofauti baina ya wanazuoni kuhusu kumlazimisha binti bikira aliye baleghe. Ipo kauli ya kukubalika
Na mfano wake ni ile Hadiyth ya Jaabir (Radhiya Allaahu ‘anhuma), ambayo ndani yake ipo ibara: “…akawatenganisha” (an-Nasaa’iy).
Shaykh wa Uislam Ibn Taymiyah amesema: “Kuozeshwa kwake pamoja na kuchukia kwake Nikaah inakwenda kinyume na msingi na akili. Allaah (Subhaanahu wa Ta‘ala) Hajampatia walii nafasi ya kumlazimisha kuuza au kuajiri ila kwa idhini yake wala kwa chakula, kinywaji na kivazi ambacho hataki. Vipi walii atamlazimisha kuishi na anayemchukia. Na hakika Allaah (Subhaanahu wa Ta‘ala) Amejaalia baina ya wanandoa mapenzi na rehema ikiwa haipatikani ila kwa kumkasirisha na kumkimbiza, ni mapenzi na rehema gani katika
Hivyo, Uislamu umewakataza kabisa wazazi kumlazimisha binti
Ushauri wetu wa mwanzo ambao tunaweza kukupatia ni kuswali rakaa mbili kumtaka ushauri Allaah Aliyetukuka. Tawadha vizuri na uswali Sunnah hiyo ya Istikhaarah na uombe du’aa yake mwisho wa Swalah na Allaah Aliyetukuka Atakuongoza kwa lililo la kheri. Huenda ukamchukia kumbe ana kheri nawe na mara nyingine huenda ukampenda mtu kumbe ni shari kwako. Allaah Aliyetukuka Anatuambia: “Huenda mkachukia kitu nacho ni kheri kwenu. Na huenda mkapenda kitu nacho ni shari kwenu. Na Allaah Anajua na nyinyi hamjui” (2: 216).
Nasaha ambayo tunaweza kukupatia ingawa kwanza ni kutaka kufahamu, je, kati ya wazazi wako wawili – mama na baba ni yupi aliyeshikilia
Ikiwa njia ya kuzungumza na wazazi wote imeshindikana na wameshikilia msimamo wao ule ule inabidi utafute jamaa wa karibu
Ikiwa njia hiyo imeshindikana itabidi
Ikiwa hayo yote yameshindikana utakuwa kweli hutaki nikaha hiyo itabidi uende kwa Qaadhi na umweleze shida zako.
Twatumai kuwa hutafika kote huko bali utapata faraja na wepesi wa
Tunakuombea kwa Allaah Akiyetukuka Akusaidie na Akuepushe kwa lile usilolitaka, Aamiyn.
Na Allaah Anajua zaidi
Links
[1] https://www.alhidaaya.com/sw/taxonomy/term/56
[2] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F2123&title=Hajaridhika%20Na%20Mume%20Aliyeozeshwa%20Kwa%20Nguvu