Nguzo Za Swalaah Na Yaliyo Waajib Katika Swalaah
SWALI:
Ni vitendo gani katika Swalaah ni Sunnah na vipi ni Fardhi? Nitashukuru mkinieleza kwa Salaa za rakaa mbili, tatu na nne.
Jazzakallahu Khayr
JIBU:
AlhamduliLLaah - Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aala) Rabb wa walimwengu, Swalaah na salamu zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho.
Tunashukuru kwa swali lako zuri. Nasi tutakuongezea jibu la nguzo ‘Rukn’ za Swalaah kwa faida yako na wengi wengine. Na tutajibu kuhusu Sunnah za Swalaah kwenye jibu jengine kwa sababu ni mengi ambayo yamegawanywa katika Sunnah za maneno ‘As-Sunnan Al-Qawliyyah’ na Sunnah za vitendo ‘As-Sunnan Al-Fi’iliyyah’ hadi baadhi ya ‘Ulamaa wanasema hizo Sunnah zinazidi 50. Hivyo pokea majibu kuhusu yaliyo Nguzo na Waajib katika Swalaah kwa leo.
Nguzo za Swalaah ni 14: Nguzo ni zile ambazo ukiswali na ukaziacha kwa makusudi Swalaah yako inabatilika, na ikiwa umeacha kwa kusahau, Swalaah yako pia itakuwa haikukamilika hadi urejee kitendo chenyewe au urejee rakaa na kisha mwishoni utoe Sajdatus-Sahw. Lakini ukiwa umesahau nguzo ya Takbiyratul-Ihraam, basi Swalaah yako basi itakubidi uiswali Swalaah upya tokea mwanzo.
Nguzo hizo 14 ni hizi zifuatazo:
Wametofautiana sana wanachuoni kuhusiana mambo yaliyo waajib.
Ama hapa tutaweka yale yaliyotajwa ambayo yanaelekea kuwa na nguvu zaidi.
Kwanza kabla hatujataja mambo yenyewe, tunapaswa kujua kuwa mambo ya Waajib ni yale ambayo vilevile atakapoacha mtu kwa makusudi hubatilika Swalaah yake, na atakapoacha kwa kusahau inamtosheleza yeye kusujudu Sijda mbili za kusahau ‘Sujuudus-Sahw’.
Na hayo mambo ya Waajib ni 8 kama yafuatayo:
Hizi ndizo maarufu zaidi kwa wanachuuoni.
Ama mambo ya Waajib ambayo yametajwa katika kitabu cha ‘Swahiyhu Fiqhis-Sunnah’ kwa dalili mbalimbali za Aayah na Hadiyth ni 9 kama yafuatayo:
Na Allaah Anajua zaidi
Links
[1] https://www.alhidaaya.com/sw/taxonomy/term/78
[2] http://www.alhidaaya.com/
[3] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F2185&title=Nguzo%20Za%20Swalaah%20Na%20Yaliyo%20Waajib%20Katika%20Swalaah