Keki Ya Stroberi Ya Vipande Vya Mraba
Vipimo:
Unga - 2 Vikombe vya chai
Sukari - ½ kikombe
Siagi (butter) - 2/3 kikombe
Kijazio (Filling)
Malai ya jibini (Cream Cheese ) - 1LB
Sukari - ¾ kikombe
Mayai - 2
Ndimu - 1 kijiko cha chai
Jamu ya stroberi (Strawberry jam) - 1 kikombe
Stroberi (fresh) zilizokatwa ndogo ndogo - 1 kikombe
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
Gamba (Crust) - Au tumia ya tayari.
Kijazio (Filling)
1. Changanya malai ya jibini na sukari katika mashine ya keki (Cake mixer) hadi iwe laini.
2. Tia mayai na ndimu ukiendelea kuipiga katika mashine.
3. Pakaza jamu juu ya gamba (curst) na mwagia stroberi ulizokatakata juu yake.
4. Mwagia mchanganyiko wa malai ya jibini (cream cheese mixture) juu ya stroberi.
5. Pika (bake) kwa muda wa dakika 25-30 au zaidi hadi itue yote igande.
6. Itoe ipoe katika rafu ya kupozea (cooling rack).
7. Kata vipande vipande weka katika sahani zikiwa tayari kuliwa.
Links
[1] https://www.alhidaaya.com/sw/taxonomy/term/106
[2] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F2332&title=Keki%20Ya%20Stroberi%20Ya%20Vipande%20Vya%20Mraba%20