Aiskrimu Ya Kokteli Ya Vanilla
Vipimo:
Tikiti maji (water melon) - ¼
Shammaam (tikiti, cantelope) - ½
Papai - 1
Embe - 1
Peya (pear) - 2
Tofaha (apple) - 2
Machungwa - 2
Plamu (plums) - 3
Pichi (peaches) - 3
Zabibu - Kiasi
Tango - 1
Matunda yoyote mengineyo upendayo - Kiasi
Aiskrimu ya vanilla - 1 L
Namna Ya Kutayarisha
Menya matunda yanayohitaji kumenywa.
Katakata matunda yote isipokuwa zabibu ikiwa ni ndogo ndogo. Ikiwa ni kubwa kubwa katakata pia.
Changanya matunda yote vizuri katika bakuli kubwa.
Teka kiasi weka katika gilasi.
Chota (scoop) aiskrimu, weka juu ya matunda.
Weka katika treya ikiwa tayari kuliwa.
Kidokezo:
Tumia matunda yoyote mengineyo upendayo.
Kipimo hiki ni kiasi cha gilasi 12 au zaidi.
Links
[1] https://www.alhidaaya.com/sw/taxonomy/term/43
[2] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F2842&title=Aiskrimu%20Ya%20%20Kokteli%20Ya%20Vanilla%20%20