Njia Kumi Za Kuhifadhi Qur-aan – 2
Kutoka
“كيف تحفظ القرآن في عشر خطوات – حسن أحمد بن أحمد همام”
Imekusanywa na Ukht Haliymah ‘Abdullaah
Alhidaaya.com [2]
2. Hatua Ya Pili: Umuhimu Wa Kupokea Na Kuisikia Kutoka Mdomoni
Qur-aan Tukufu siyo kama vitabu vingine ambayo inatosha kutazama na kuisoma ambayo mtu anajitegemea nafsi yake kwani huwezi kutazama katika Musw-haf na kutamka lafdhi bali inahitajika katika kuisoma Qur-aan na Kuihifadhi kuipokea na kusomeshwa kutoka kwenye mdomo wa wasomi na wajuzi wa Tajwiyd (elimu iliyopokelewa kutoka kwa Nabiys Swalla Allaahu ‘alayhi aalihi wa sallam).
Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa):
وَإِنَّكَ لَتُلَقَّى الْقُرْآنَ مِن لَّدُنْ حَكِيمٍ عَلِيمٍ ﴿٦﴾
Na hakika wewe unapokea Qur-aan kutoka kwa Mwenye hikmah wa yote, Mjuzi wa yote. [An-Naml: 6]
Alikuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akiwatamkisha Swahaba zake Qur-aan, Imekuja kutoka kwa ‘Aliy (Radhwiya Allaahu ‘anhu) kuwa aliwaambia Swahaba: “Hakika Rasuli wa Allaah anawaamrisha, asome kila mmoja wenu kama alivyofundishwa.”
Na hakuna yeyote aliyehifadhi Qur-aan kwa jitihada zake binafsi bila ya kuchukua kwa Mashaykh ila atakuwa mwenye kukosea katika kisomo chake, tuchukulie Musw-haf ya Rasm (mchoro/ maandishi) ya ‘Uthmaaniy haisomwi kama ilivyoandikwa baadhi ya herufi mfano neno “Asw-Swallawaata, Az-Zakawaata.” Hiyo waaw haitamkwi bali inasomwa “Asw-Swallaata, Az-Zakaata” hivyo katika masharti ya kisomo Sahihi ni kuisoma kutoka kwa Shaykh au Mwalimu.
3. Hatua Ya Tatu: Umuhimu Wa Kuihifadhi Kwa Tajwiyd
Anasema Ibn Jawziy:
“Na kuisoma kwa Tajwiyd ni jambo la lazima, na asiyeisoma Qur-aan kwa Tajwiyd anapata madhambi.”
Na maana ya Tajwiyd ni kuchunga hukmu za kisomo zilizopo katika vitabu vya Tajwiyd katika Idghaam, Idhwhaar, Ikhfaa, Ghunnah, Madd na kuchunga Makhaarij (sehemu za kutoa herufi) na nyinginezo. Kwani Qur-aan Kariym inatofautiana na vitabu vingine, ni Maneno ya Allaah na kwa mpangilio huu amepokea Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kutoka kwa Jibriyl kutoka kwa Allaah (‘Azza wa Jalla) na hivyo ndivyo ilivyotufikia.
Imepokewa kutoka kwa Ibn Mas’uwd alikuwa mtu anamsomea neno lake Allaah:
إِنَّمَا الصَّدَقَاتُ لِلْفُقَرَاءِ
[At-Tawba: 60]
Alisoma neno
لِلْفُقَرَاءِ
bila ya kuvuta Madd, akasema Ibn Mas’uwd: “Sivyo hivyo alivyonifundisha Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam), akamwelekeza avute Madd baada ya herufi ya raa.
Haina maana uzame katika elimu ya Tajwiyd kwa undani kupita kiasi, muhimu uweze kuisoma Qur-aan kwa hukmu na kujua Tafsiyr yake ili uweze kuifanyia kazi.
Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa):
الَّذِينَ آتَيْنَاهُمُ الْكِتَابَ يَتْلُونَهُ حَقَّ تِلَاوَتِهِ أُولَـٰئِكَ يُؤْمِنُونَ بِهِ ۗ وَمَن يَكْفُرْ بِهِ فَأُولَـٰئِكَ هُمُ الْخَاسِرُونَ ﴿١٢١﴾
Wale Tuliowapa Kitabu wanakisoma kwa haki ipasavyo ya kusomwa kwake; hao ndio wanaokiamini, na atakayekikanusha basi hao ndio waliokhasirika. [Al-Baqarah: 121]
4. Hatua Ya Nne: Kuchagua Wakati Na Sehemu Munaasib Kwa Kuhifadhi
Kuweka wakati munaasib kwa kuhifadhi ni njia muhimu inayosaidia kuhifadhi. Na wakati wa kuhifadhi inatofautiana kati ya mtu na mtu kuna anayefadhilisha wakati wa Alfajiri au wakati wa Sahar (kabla ya alfajiri) au baada ya Maghrib.
Inapasa uchunge yafuatayo:
5-Hatua Ya Tano: Kupangilia Mwanzo Wa Hifdhi (Kuhifadhi)
Kusudio je mwanzo wa kuhifadhi utakuwa mwanzo wa Musw-haf (Al-Faatihah na Al-Baqarah) au mwisho wa Musw-haf (An-Naas), na hili linatofautiana kutokana na uwezo wa mtu ikiwa mtu ana uwezo mzuri wa kusoma bora aanze mwanzo na ikiwa yupo mwanzo katika kusoma bora aanze na Suwrat An-Naas.
Natija ya wote wawili kwa Uwezo wa Allaah ni kufikia katika kuhifadhi Kitabu cha Allaah, wangapi wameanza na Surah ndogo na wamefanikiwa kufika mwisho.
6-Hatua ya Sita: Kuweka Idadi Ya Aayah
Uwezo wa kuhifadhi ni Kipaji kutoka kwa Allaah na inatofautiana uwezo huu kati ya mtu na mtu kikubwa kinachonasihiwa mwanzo wa kuhifadhi ni kuweka idadi kamili hata kama una uwezo zaidi.
Kuna mtu anaweza kuhifadhi katika kikao kimoja ukurasa mzima katika Musw-haf kisha siku ya pili ameshasahau baadhi ya Aayah alizohifadhi na kuna mwengine anahifadhi kila siku Aayah tano hazidishi na inakuwa Hifdhi yake ni yenye nguvu.
Amepokea Abu ‘Umar Ad-Daaniy katika “Al-Bayaan” kutoka kwa ‘Uthmaan na Ibn Mas’uwd na Ubay bin Ka’ab kwamba:
“Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akiwafundisha Aayah kumi hazidishi zingine mpaka wajifundishe yaliyomo na kuifanyia kazi, Anawafundisha Qur-aan na kuifanyia kazi kwa wakati mmoja.”
Kutoka kwa Abu ‘Abdir-Rahmaan As-Sulamiy anasema:
“Tulikuwa tukijifundisha Aayah kumi katika Qur-aan hatuchukui zingine baada yake mpaka tujue halaal yake na haraam yake, amri yake na makatazo.”
Na katika kuweka idadi ya Aayah ni kutokana na kutofautiana urefu wake. Mfano tuchukulie “Aayatud-Dayn” ambayo ni Aayah ndefu kuliko zote katika hali hii inapendekezwa kuhifadhi Aayah kuendana na idadi ya mistari. Ama ikiwa Aayah ni ndogo ndogo mfano Suwrah As-Swaaffaat, ‘Abasa, At-Takwiyr na zinginezo jiwekee Aayah kumi au tano katika kikao kimoja.
Na ukisoma Tafsiyr kuhusu maana ya maneno ni jambo litakalokusaidia katika kuhifadhi.
7-Hatua Ya Saba: Namna Ya Kuhifadhi Aayah
Fuata hatua zifuatazo:
8-Hatua Ya Nane: Kuunganisha Baina Ya Aayah
9-Hatua Ya Tisa: Baada Ya Kumaliza Kuhifadhi Suwrah
Baada ya kumaliza kuhifadhi Suwrah kamili usihamie Suwrah nyingine mpaka uhakikishe unasoma vizuri uliyohifadhi mwanzo.
10-Hatua Ya Kumi: Kurejea Hifdhi Iliyopita
Tanbihi Muhimu: Tahadhari Na Kupuuzia Wakati
Wakati ni umri wa mwana-Aadam na maisha yake katika hii dunia nayo ni Rasilimali na biashara yake na Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) hivyo jiepushe na Taswiyf (Nita…) na kujishughulisha na Qur-aan na vitu vingine mfano kusema “Kesho nitahifadhi, kesho nitasoma n.k.”
Jihadhari pia na kuacha Hifdhi yako ya kila siku na kusema hakuna neno “kesho nitahifadhi” bali zingatia wakati wako na usiahirishe Hifdhi ili usije ukazoea na ukapoteza wakati wako bure. Fahamu kuhifadhi Kitabu Cha Allaah haikubaliani na kupoteza wakati na kufuata matamanio.
Jiepushe Na Vizuizi (Vikwazo) Vifuatavyo:
Kumbuka Kwamba…
Usitusahau katika Du’aa zako, Tunamuomba Allaah Atukubalie, Atuongoze na Du’aa yetu ya mwisho ni
الْحَمْدُ لِلَّـهِ رَبِّ الْعَالَمِينَ ﴿٢﴾
Links
[1] https://www.alhidaaya.com/sw/taxonomy/term/237
[2] http://www.alhidaaya.com
[3] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F3177&title=Njia%20Kumi%20Za%20Kuhifadhi%20Qur-aan%20-%202