Anaambiwa Nani Aayah
قُلْ إِن كَانَ لِلرَّحْمَـٰنِ وَلَدٌ فَأَنَا أَوَّلُ الْعَابِدِينَ﴿٨١﴾
Alhidaaya.com [2]
SWALI:
Assalaam aleykum,
Alhamdulillah kua Allah mtakatifu ametupa uzima na uhai mpaka sasa. In shaa Allaah tuwe wenye kuongoka na nyinyi mlipwe wema kwa kutusaidia. Kwenye Suuratu-zzukhruf Aya ya 81: "Sema: Ingeli kuwa Rahmani ana mwana, basi mimi ningeli kuwa wa kwanza kumuabudu."
Je haya maneno alikua anaambiwa Nabiy Issa awambie watu au ilikua anaambiwa nani, kwani katika aya za juu zinaelezea kuja nabii Issa alayhi ssalaam na uongofu kutoka kwa Allah subhaanahu wataala. Kama anaambiwa Nabiy Issa itanisaidia kuwathibitishia rafiki zangu wa kikiristo kua Nabiy Issa si mwana wa Allaah
Jazaakumullahu khair.
JIBU:
AlhamduliLLaah Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aala) Rabb wa walimwengu, Swalaah na Salaam zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho.
Hiyo ni Aayah katika Suwrah Az-Zukhruf
قُلْ إِن كَانَ لِلرَّحْمَـٰنِ وَلَدٌ فَأَنَا أَوَّلُ الْعَابِدِينَ﴿٨١﴾
Sema (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم): Kama ingelikuwa Ar-Rahmaan Ana mwana (kama mnavyodai), basi mimi ningekuwa wa mwanzo katika waja (Wake). [Az-Zukhruf: 81]
Kabla hajutaelezea Aayah hiyo, labda tuanze kwa kufahamisha vigawanyo vya Suwrah hii ya Az-Zukhruf. Miongoni mwa dondoo ni kuwa:
Hizi ni baadhi ya dondoo kuhusiana na Suwrah hiyo.
Ama tukirudi katika swali lako ni kuwa maana ya Aayah hiyo ni jawabu kutoka kwa Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) aliyepewa Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kuwajibu watu wake Ma-Quraysh waliokuwa mushrikina. Na maana yake ni kuwa lau Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) Angekuwa na mtoto kama mnavyodai basi mimi (Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ningekuwa wa kwanza katika waja Allaah kukanusha madai hayo. Kwa maana nyingine ni kuwa Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) Hana mtoto kabisa wala Hastahiki kuwa na sifa hiyo.
Bali Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) Anasema:
وَقَالُوا اتَّخَذَ الرَّحْمَـٰنُ وَلَدًا ﴿٨٨﴾
Na wamesema: “Ar-Rahmaan Amejifanyia mwana.”
لَّقَدْ جِئْتُمْ شَيْئًا إِدًّا ﴿٨٩﴾
Kwa yakini mmeleta jambo kuu ovu na la kuchukiza mno! [Maryam: 88-90]
Na Allaah Anajua zaidi
Links
[1] https://www.alhidaaya.com/sw/taxonomy/term/33
[2] http://www.alhidaaya.com
[3] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F3359&title=Anaambiwa%20Nani%20Aayah%3A%20%20%D9%82%D9%8F%D9%84%D9%92%20%D8%A5%D9%90%D9%86%20%D9%83%D9%8E%D8%A7%D9%86%D9%8E%20%D9%84%D9%90%D9%84%D8%B1%D9%91%D9%8E%D8%AD%D9%92%D9%85%D9%8E%D9%80%D9%B0%D9%86%D9%90%20%D9%88%D9%8E%D9%84%D9%8E%D8%AF%D9%8C%20%D9%81%D9%8E%D8%A3%D9%8E%D9%86%D9%8E%D8%A7%20%D8%A3%D9%8E%D9%88%D9%91%D9%8E%D9%84%D9%8F%20%D8%A7%D9%84%D9%92%D8%B9%D9%8E%D8%A7%D8%A8%D9%90%D8%AF%D9%90%D9%8A%D9%86%D9%8E