SWALI:
Jazaakallah kheir kwa jibu la swali langu. Alhamdulillah nimefanikiwa kufikia uamuzi wa kuoa mke wa pili...Allah awalipe jazaa ya kheir kwa ushauri wenu kwangu kulifanya hili ambao kwa namna moja ama nyingine umechangia kufikia maamuzi haya...naomba dua zenu inshaallah.
Nina ombi lingine: Hapa chuoni nimepata fursa ya kufikiriwa kuwa katika undergraduate medical student innovative programme ambapo unachagua a unique title, unaiandikia proposal ambayo inapitiwa na professor..ikipita kwake wapewa fund na facilities husika ili kufanya hiyo experiment.
Nimefikiria niifanye experiment inayohusu physiology (tunatumia wanyama
JIBU:
Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu 'anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.
Tunashukuru kwa swali lako
Kuchunga haki za wanyama ni jambo ambalo Uislamu umelipa nafasi na kulisisitiza. Wanyama wana haki zao kwetu pamoja na kwamba wameumbwa kwa ajili yetu.
Ama kuhusu kutaka kujua Aayah na Hadiyth ya jambo hilo la kufanya utafiti kwa kuwafanyia majaribio wanyama, hakuna Aayah au Hadiyth ya moja kwa moja ambayo inaeleza suala hilo ila kuna msingi wa Kiislamu kuhusu utendaji wa majaribio yako au yenu kwa kutumia wanyama, ni muhimu kufahamu kuwa inaruhusiwa kutumia wanyama kufanyia majaribio hayo ya kisayansi, ikiwa utumiaji wake utakuwa na manufaa kwa binaadamu. Lakini kuweko na mipaka ya kuhitajika kwake na pia watumiliwe kwa upole na huruma bila ya ukatili na bila ya kuwatesa.
Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa alihi wa sallam) amesema:
((إن الله كتب الإحسان على كل شيء . فإذا قتلتم فأحسنوا القتلة وإذا ذبحتم فأحسنوا الذبحة ، وليحد أحدكم شفرته وليرح ذبيحته)) صحيح الترمذي و قال الشيخ الإلباني صحيح
((Allah Amefaradhisha ihsaan kwa kila kitu, kwa hiyo mnapoua (wanyama) fanyeni ihsaan katika uuaji na mnapochinja fanyeni ihsaan katika uchinjaji, basi atie makali mtu kisu chake na ampunguzie (amuondoshee makali) kichinjo chake)) [Swahiyh At-Tirmidhiy na Shaykh Al-Albaaniy pia kasema ni Swahiyh]
Kuchunga mipaka hiyo ni kwa mfano ikiwa itapatikana matokeo baada ya jaribio la mnyama mmoja, basi hapana haja tena kutumia wanyama wengine kufanya jaribio
Tumepata mafunzo kutoka katika kisa maarufu kilichotajwa kwenye Hadiyth ambacho kulikuwa na mwanamke ambaye ingawa alikuwa ni Mcha mungu, lakini makazi yake yakawa motoni kwa kutokumfanyia ihsani paka.
Kadhalika kuna mtu mmoja alikwenda kwa Shaykhul Islaam Ibn Taymiya na kulalamika kwamba sisimizi wengi wameingia nyumbani kwake na akamuuliza
Hata hivyo, kwa ajili ya umuhimu wa mada yenyewe na pia unaweza kupata mahusiano ya Aayah na Hadiyth ya suala
Na Allaah Anajua zaidi
Links
[1] https://www.alhidaaya.com/sw/taxonomy/term/101
[2] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F4090&title=Kufanya%20Majaribio%20Ya%20Fiziolojia%20Ya%20Wanyama