SWALI
Assalam Alaykum
Naomba kupatiwa jibu la suala langu lifuatalo. Mama katika familia amepika chakula na baada ya kuliwa kilisababisha kuumwa na kufariki kwa mume wake na mtoto wake mmoja. Huyu mama yeye hakula hiki chakula sababu hakipendi na ni kawaida yake kutokula chakula hicho na pia madaktari wamethibitisha kuwa vifo hivyo vimesababishwa na “food poisoning” ilotokana na vimelea (bacteria). Jee katika mazingira hayo huyu mama anayo haki ya kurithi mali ya mumewe? Wabillah Tawfiq
JIBU:
Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu 'anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.
Shukrani kwa ndugu yetu kwa swali lako hilo kuhusu jambo ambalo linaonekana ni kama la jinai. Jinai ya nafsi inafahamika kuwa ni uadui kwa mwanadamu kwa kutoa roho yake, au kuviharibu baadhi ya viungo vyake, au kumsababishia jeraha mwilini mwake.
Ni haramu kuitoa roho ya mwanadamu bila ya haki au kukiharibu kiungo miongoni mwa viungo vyake au kusababisha madhara yoyote kwa mwili wake. Hakuna kosa kubwa mno baada ya shirki na ukafiri zaidi ya kumuua Muislamu. Hii ni kwa mujibu wa kauli ya Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala): “Na mwenye kumuua Muumini kwa kukusudia, basi malipo yake ni Jahanamu humo atadumu, na Allaah Amemkasirikia, na Amemlaani, na Amemuandalia adhabu kubwa” (4: 93).
Kumwaga damu ya mwanadamu mwengine hata asiyekuwa Muislamu haifai pasi na haki, kwani Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) Anasema: “Kwa sababu ya hayo Tuliwaandikia Wana wa Israili ya kwamba aliyemuua mtu bila ya yeye kuua, au kufanya uchafuzi katika nchi, basi ni kama amewaua watu wote. Na mwenye kumuokoa mtu na mauti ni kama amewaokoa watu wote” (5: 32).
Na kauli yake (Swalla Llaahu 'alayhi wa sallam): “Kosa la kwanza kuhukumiwa siku ya Qiyaama litahusu damu” (al-Bukhaariy, an-Nasaa’iy, Ibn Maajah na al-Haakim).
Wanachuoni na mafakihi wote wameigawa jinai katika sehemu tatu. Nazo ni kama zifuatazo:
Huyu anawajibika mambo yafuatayo:
- Anapata dhambi.
- Hatokuwa mwenye kurithi.
- Anafaa atoe kafara.
- Atoe diya au apate msamaha.
Huyu naye anakuwa:
- Mwenye kupata dhambi kwani ameua nafsi iliyo haramu.
- Diya nzito.
“Mwenye kuua kwa shibhul ‘Amd ima kwa fimbo au kijiwe anafaa atoe fidia ya ngamia mia moja, arobaini miongoni mwao wakiwa na mimba” (Ahmad, Abu Daawuud, an-Nasaa’iy na Ibn Maajah).
Kifo cha watu kula chakula inakuwa ni bahati mbaya kwani mke hakukusudia hilo kabisa. Katika hilo linaweza kuja swali: Je aliyenunua chakula ni nani? Mara nyingi inawezekana kuwa ni mume mwenyewe au mtumishi, kazi ya mke ilikuwa ni kupika tu chakula kile alichotaka mume au alichoamua yeye mwenyewe. Kwa hiyo, mke huyu atarithi wala hatawajibika kafara yoyote.
Mbali na kusema hayo tungependa kujua kulikuwa na uhusiano gani baina ye mke na aliyefariki. Je, uhusiano wake ulikuwa mzuri au hawakuwa ni wenye uhusiano mwema?
Na Allaah Anajua zaidi
Links
[1] https://www.alhidaaya.com/sw/taxonomy/term/34
[2] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F457&title=Mama%20Amesababisha%20Kifo%20Cha%20Mume%20Je%2C%20Anayo%20Haki%20Kurithi%3F