Sifa Na Akhlaaq Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)
01-Zuhd Yake: Kauli Zake Kuhusu Zuhd (Kuipa Mgongo Dunia)
Alhidaaya.com [4]
Juu ya kuwa yeye Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alikuwa ndiye mtu mtukufu kabisa mbele ya Swahaba zake, na ndio kiongozi wao, lakini hali na maisha yake yalikuwa ni ya Zuhd ya ajabu; kwani ukitambua jinsi alivyoishi katika nyumba duni kabisa na kutokuwa na vifaa na fanicha za kifakhari nyumbani mwake, au kutokuwa na nguo za kifakhari, au kutokuwa na mali yoyote ile hadi kufariki kwake. Bali la ajabu zaidi ni kufikia hadi miezi ya kutokuwa na chakula nyumbani mwake.
Na hayo ni mafunzo na kigezo kizuri kwetu katika zama hizi kuwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alitambua lengo la kuumbwa kwake, kwahiyo akaelewa kuwa nyenzo hizo ni za kumpelekea yeye kumwabudu Rabb wake na kutafuta Aakhirah yake, na wala havikuwa ni vitu vya kuvipapia na kuvikusanya katika maisha ya dunia. Na ndio maana katika kauli zake kuhusu Zuhd, amedhihirisha na kufundisha kuwa maisha haya ya duniani ni ya muda mfupi tu wa kupita, hivyo hajataka kumiliki mafao au vitu vya kumstarehesha wala hakutaka anasa za maisha mafupi ya dunia bali alipendelea maisha ya Aakhirah ambayo ndio ya maisha ya kudumu milele. Akaamini na kufuata kauli kadhaa za Rabb Allaah (سبحانه وتعالى) wake Anazosema:
وَمَا هَـٰذِهِ الْحَيَاةُ الدُّنْيَا إِلَّا لَهْوٌ وَلَعِبٌ ۚ وَإِنَّ الدَّارَ الْآخِرَةَ لَهِيَ الْحَيَوَانُ ۚ لَوْ كَانُوا يَعْلَمُونَ ﴿٦٤﴾
Na huu uhai wa dunia si chochote isipokuwa ni pumbao na mchezo; na hakika Nyumba ya Aakhirah bila shaka hiyo ndiyo yenye uhai wa kweli hasa (wa milele), lau wangelikuwa wanajua! [Al-‘Ankabuwt: 64]
Na pia Kauli Yake Allaah (سبحانه وتعالى):
اعْلَمُوا أَنَّمَا الْحَيَاةُ الدُّنْيَا لَعِبٌ وَلَهْوٌ وَزِينَةٌ وَتَفَاخُرٌ بَيْنَكُمْ وَتَكَاثُرٌ فِي الْأَمْوَالِ وَالْأَوْلَادِ ۖ كَمَثَلِ غَيْثٍ أَعْجَبَ الْكُفَّارَ نَبَاتُهُ ثُمَّ يَهِيجُ فَتَرَاهُ مُصْفَرًّا ثُمَّ يَكُونُ حُطَامًا ۖ وَفِي الْآخِرَةِ عَذَابٌ شَدِيدٌ وَمَغْفِرَةٌ مِّنَ اللَّـهِ وَرِضْوَانٌ ۚ وَمَا الْحَيَاةُ الدُّنْيَا إِلَّا مَتَاعُ الْغُرُورِ ﴿٢٠﴾
Jueni kwamba uhai wa dunia ni mchezo na pumbao na mapambo, na kufakharishana baina yenu na kushindana kukithiri katika mali na watoto; ni kama mfano wa mvua inayowafurahisha wakulima mimea yake, kisha yananyweya, basi utayaona yamepiga manjano, kisha yanakuwa mabua yaliyonyauka na kupondekapondeka. Na Aakhirah kuna adhabu kali, na maghfirah kutoka kwa Allaah na radhi. Na uhai wa dunia si chochote isipokuwa ni sterehe fupi za kughuri. [Al-Hadiyd: 20]
Na Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):
مَن كَانَ يُرِيدُ حَرْثَ الْآخِرَةِ نَزِدْ لَهُ فِي حَرْثِهِ ۖ وَمَن كَانَ يُرِيدُ حَرْثَ الدُّنْيَا نُؤْتِهِ مِنْهَا وَمَا لَهُ فِي الْآخِرَةِ مِن نَّصِيبٍ﴿٢٠﴾
Yeyote yule aliyekuwa anataka mavuno ya Aakhirah Tunamzidishia katika mavuno yake; na yeyote yule aliyekuwa anataka mavuno ya dunia, Tutampa humo, lakini Aakhirah hatokuwa na fungu lolote. [Ash-Shuwraa (42: 20)]
Na Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):
بَلْ تُؤْثِرُونَ الْحَيَاةَ الدُّنْيَا ﴿١٦﴾
Bali mnakhiari uhai wa dunia.
وَالْآخِرَةُ خَيْرٌ وَأَبْقَىٰ ﴿١٧﴾
Na hali Aakhirah ni bora zaidi ya kudumu. [Al-A’laa (87: 16-17).
Na Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):
وَمَا أُوتِيتُم مِّن شَيْءٍ فَمَتَاعُ الْحَيَاةِ الدُّنْيَا وَزِينَتُهَا ۚ وَمَا عِندَ اللَّـهِ خَيْرٌ وَأَبْقَىٰ ۚ أَفَلَا تَعْقِلُونَ ﴿٦٠﴾
Na chochote mlichopewa katika vitu, basi ni starehe za uhai wa dunia na mapambo yake. Na yaliyoko kwa Allaah ni bora zaidi na yakubakia. Je, basi hamtii akilini? [Al-Qaswasw (28: 60)]
Na Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):
مَن كَانَ يُرِيدُ حَرْثَ الْآخِرَةِ نَزِدْ لَهُ فِي حَرْثِهِ ۖ وَمَن كَانَ يُرِيدُ حَرْثَ الدُّنْيَا نُؤْتِهِ مِنْهَا وَمَا لَهُ فِي الْآخِرَةِ مِن نَّصِيبٍ﴿٢٠﴾
Yeyote yule aliyekuwa anataka mavuno ya Aakhirah Tunamzidishia katika mavuno yake; na yeyote yule aliyekuwa anataka mavuno ya dunia, Tutampa humo, lakini Aakhirah hatokuwa na fungu lolote. [Ash-Shuwraa (42: 20)]
Naye (صلى الله عليه وآله وسلم) kuli zake:
عَنْ عَبْدِ اللَّهِ ابن مسعود (رضي الله عنه) قَال: نَامَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ عَلَى حَصِيرٍ فَقَامَ وَقَدْ أَثَّرَ فِي جَنْبِهِ، فَقُلْنَا يَا رَسُولَ اللَّهِ! لَوْ اتَّخَذْنَا لَكَ وِطَاءً. فَقَالَ: ((مَا لِي وَمَا لِلدُّنْيَا؟ مَا أَنَا فِي الدُّنْيَا إِلاَّ كَرَاكِبٍ اسْتَظَلَّ تَحْتَ شَجَرَةٍ ثُمَّ رَاحَ وَتَرَكَهَا)) الترمذي وقال: حَدِيثٌ حَسَنٌ صَحِيحٌ
Imepokelewa kutoka kwa ‘Abdullaah bin Mas’uwd (رضي الله عنه) amesema: “Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alilala kwenye jamvi la mtende likamfanyia alama ubavuni mwake tukasema: Ee Rasuli wa Allaah! Tukufanyie godoro laini? Akasema: ((Mimi na dunia wapi? Mfano wangu na dunia ni kama mpandaji (anayesafiri kwa mnyama) aliyepumzika kivulini chini ya mti, [muda mfupi tu] kisha akaondoka na kukiacha)). [At-Tirmidhiy na amesema Hadiyth Hasan Swahiyh]
Na pia,
عن المُسْتَوْرِد بن شَدَّاد رضي الله عنه، قَالَ: قَالَ رسول الله صلى الله عليه وسلم: (( مَا الدُّنْيَا في الآخِرَةِ إِلاَّ مِثْلُ مَا يَجْعَلُ أَحَدُكُمْ أُصْبُعَهُ في اليَمِّ، فَلْيَنْظُرْ بِمَ يَرْجِعُ ! )) رواه مسلم.
Imepokewa kutoka kwa Al-Mustawrid bin Shaddaad (رضي الله عنه) kuwa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: "Dunia si chochote katika Aakhirah isipokuwa ni kama mfano wa mtu anayetia kidole chake (Yahyaa aliashiria kidole cha Shahaada) katika bahari, basi naangalie kiasi gani cha maji kimechota." [Muslim na wengineo. Hadiyth imesimuliwa kwa Isnaad mbalimbali na zote zimesimuliwa na Al-Mustawrid bin Shaddaad ndugu wa Baniy Fihr]
Na pia,
عن أنس رضي الله عنه : أن النبي صلى الله عليه وسلم، قَالَ: (( اللَّهُمَّ لاَ عَيْشَ إِلاَّ عَيْشَ الآخِرَةِ )) متفقٌ عَلَيْهِ .
Na imepokewa kutoka kwa Anas (رضي الله عنه) kuwa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: "Ee Allaah! Hakuna maisha isipokuwa maisha ya Aakhirah [Al-Bukhaariy na Muslim]
Na pia,
عن جابر رضي الله عنه : أنَّ رسول الله صلى الله عليه وسلم مَرَّ بالسُّوقِ وَالنَّاسُ كَنَفَتَيْهِ ، فَمَرَّ بِجَدْيٍ أَسَكَّ مَيِّتٍ ، فَتَنَاوَلَهُ فَأَخَذَ بِأُذُنِهِ ، ثُمَّ قَالَ : (( أَيُّكُم يُحِبُّ أنْ يَكُونَ هَذَا لَهُ بِدرْهَم ؟ )) فقالوا : مَا نُحِبُّ أنَّهُ لَنَا بِشَيْءٍ وَمَا نَصْنَعُ بِهِ ؟ ثُمَّ قَالَ : (( أَتُحِبُّونَ أَنَّهُ لَكُمْ ؟ )) قَالُوا : وَاللهِ لَوْ كَانَ حَيّاً كَانَ عَيْباً ، إنَّهُ أسَكُّ فَكَيْفَ وَهُوَ ميِّتٌ ! فقال : (( فوَاللهِ للدُّنْيَا أهْوَنُ عَلَى اللهِ مِنْ هَذَا عَلَيْكُمْ )) رواه مسلم .
Imepokewa kutoka kwa Jaabir (رضي الله عنه) kuwa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alipita sokoni pamoja na Swahaba zake alimuona mbuzi mdogo amekufa na masikio yake yamekatwa. Alikishika katika masikio na kuuliza: "Nani anayemtaka (huyu mbuzi aliyekufa) kwa dirhamu moja?" Wakasema: "Hatutaki huyo awe ni wetu kwa chochote (hata bure). Na je, tutamfanya nini? " Kisha akasema: "Je, mngependa awe wenu bure?" Wakasema: "Wa-Allaahi! Hata kama angekuwa hai angekuwa na kasoro, vipi akiwa maiti?" Akasema (صلى الله عليه وآله وسلم) "Wa-Allaahu! dunia ni duni zaidi mbele ya Allaah kuliko huyu juu yenu." [Muslim]
Na pia,
عن أَبي العباس سهل بن سعد الساعدي رضي الله عنه ، قَالَ : جَاءَ رَجُلٌ إِلَى النبي صلى الله عليه وسلم ، فقال : يَا رسولَ الله ، دُلَّنِي عَلَى عَمَلٍ إِذَا عَمِلْتُهُ أحَبَّنِي اللهُ وَأحَبَّنِي النَّاسُ ، فقال : (( ازْهَدْ في الدُّنْيَا يُحِبّك اللهُ ، وَازْهَدْ فِيمَا عِنْدَ النَّاسِ يُحِبّك النَّاسُ )) حديث حسن رواه ابن ماجه وغيره بأسانيد حسنة .
Imepokewa kutoka kwa Abu Al-'Abbaas Sahl bin Sa'd As-Saa'idiy (رضي الله عنه) kuwa: Alikuja mtu kwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akasema: "Ee Rasuli wa Allaah, nijulishe mimi amali ambayo nikiifanya Allaah atanipenda na watu watanipenda." Akasema: "Kuwa na Zuhd (Upe nyongo ulimwengu) atakupenda Allaah, na vipe nyongo viliomo mikononi mwa watu watakupenda watu." [Hadiyth Hasan - Ibn Maajah na wengineo kwa Isnaad nzuri]
Na pia,
عن سهلِ بن سعد الساعدي رضي الله عنه ، قَالَ : قَالَ رسول الله صلى الله عليه وسلم: (( لَوْ كَانَت الدُّنْيَا تَعْدِلُ عِنْدَ الله جَنَاحَ بَعُوضَةٍ ، مَا سَقَى كَافِراً مِنْهَا شَرْبَةَ مَاءٍ )) رواه الترمذي ، وقال : (( حديث حسن صحيح )) .
Imepokewa kutoka kwa Sahl bin Sa'ad As-Saa'idiy (رضي الله عنه) kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: "Lau kama uliwengu ungekuwa na thamani sawa na bawa la mbu mbele ya Allaah, hangempatia kafiri maji ya kunywa hata kiasi cha mkono mmoja." [At-Tirmidhy, na akasema ni Hadiyth Hasan Sahiyh]
Na pia,
عن عبد الله بن مسعود رضي الله عنه ، قَالَ : قَالَ رسول الله صلى الله عليه وسلم: (( لاَ تَتَّخِذُوا الضَّيْعَةَ فَتَرْغَبُوا في الدُّنْيَا )) رواه الترمذي ، وقال : (( حديثٌ حسنٌ )) .
Imepokewa kutoka kwa Ibn Mas-'uwd (رضي الله عنه) kuwa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: "Msiwe ni wenye kupapia raslimali (zisizohamishika) na hivyo kupendelea dunia." [At-Tirmidhy, na akasema ni Hasan]
Akawakhofia sana Swahaaba zake wasije kughilibiwa na anasa za dunia wakaacha Zuhd:
عن أَبي سعيد الخدري رضي الله عنه ، قَالَ : جلس رسولُ الله صلى الله عليه وسلم عَلَى الْمِنْبَرِ ، وَجَلَسْنَا حَوْلَهُ ، فقال : (( إنَّ ممَّا أخَافُ عَلَيْكُمْ مِنْ بَعْدِي مَا يُفْتَحُ عَلَيْكُمْ مِنْ زَهْرَةِ الدُّنْيَا وَزِينَتِهَا )) متفقٌ عَلَيْهِ .
Imepokewa kutoka kwa Abu Sa'iyd al-Khudriy (رضي الله عنه) amesema: Alikaa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) kwenye mimbar nasi tukakaa duara (tukiwa tumemzunguka), akasema: "Kwa hakika yale ninayowaogopea nyinyi baada yangu ni kufunguliwa kwenu utajiri na kuvutiwa na dunia na mapambo yake." [Al-Bukhaariy na Muslim]
Sifa Na Akhlaaq Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)
02-Zuhd Yake:
Akiomba Du’aa Kuambatanishwa Na Masikini Kufishwa Nao Na Kufufuliwa Nao
Alhidaaya.com [4]
Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alikuwa akiomba Du’aa ya kuambatanishwa daima na mafakiri na masikini, kufishwa nao na kufuliwa nao kwa sababu hali ya Masikini kawaida ni hali duni ambayo haina mafao ya dunia sawa na maisha ya mtu mwenye sifa ya Zuhd. Akiomba du’aa:
اللَّهُمَّ أَحْيِنِي مِسْكِينًا وَأَمِتْنِي مِسْكِينًا وَاحْشُرْنِي فِي زُمْرَةِ الْمَسَاكِينِ يَوْمَ الْقِيَامَةِ
Ee Allaah Nijaalia uhai wa umaskini na nifishe nikiwa maskini na nifufue pamoja na kundi la masaakini Siku ya Qiyaamah.” [At-Tirmidhiy, Ibn Maajah]
Na Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akathibitisha kuwa wengi wa makaazi ya Jannah (Peponi) watakuwa ni Masikini na Mafakiri:
عن ابن عباس وعِمْرَانَ بن الحُصَيْنِ رضي الله عنهما ، عن النبي صلى الله عليه وسلم ، قَالَ: (( اطَّلَعْتُ في الجَنَّةِ فَرَأيْتُ أكْثَرَ أهْلِهَا الفُقَرَاءَ ، وَاطَّلَعْتُ في النَّارِ فَرَأيْتُ أكْثَرَ أهْلِهَا النِّسَاءَ )) متفقٌ عَلَيْهِ من رواية ابن عباس ، ورواه البخاري أيضاً من رواية عِمْرَان بن الحُصَيْن .
Imepokewa kutoka kwa Ibn 'Abbaas na 'Imraan Ibn Al-Huswayn (رضي الله عنهما) kuwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: "Nilichungulia Jannah nikaona watu wake wengi ni mafakiri. Na nikatizama Motoni nikaona watu wake wengi ni wanawake." [Al-Bukhaariy, Muslim na At-Tirmidhiy]
Sifa Na Akhlaaq Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)
03-Zuhd Yake:
Akiomba Du’aa Ya Kujaaliwa Rizqi Ya Kumtosheleza Tu
Alhidaaya.com [4]
Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alikuwa akimuomba Allaah (سبحانه وتعالى) rizki ya kumtosheleza tu basi akiomba du’aa:
اللَّهُمَّ اجْعَلْ رِزْقَ آلِ مُحَمَّدٍ قُوتًا
Ee Allaah ijaalie rizki ya Ahl wa Muhammad iwe ya kutosheleza tu.” [Muslim]
Na akataja katika Hadiyth yanayompasa bin Aadam kutosheka nayo:
عن أَبي عمرو ، ويقالُ : أَبو عبدِ الله ، ويقالُ : أَبو ليلى عثمان بن عفان رضي الله عنه : أنَّ النبي صلى الله عليه وسلم ، قَالَ : (( لَيْسَ لاِبْنِ آدَمَ حَقٌّ في سِوَى هذِهِ الخِصَالِ : بَيْتٌ يَسْكُنُهُ ، وَثَوْبٌ يُوارِي عَوْرَتَهُ ، وَجِلْفُ الخُبز وَالماء )) رواه الترمذي ، وقال : (( حديث صحيح )) .
Imepokewa kutoka kwa Abu 'Amru (رضي الله عنه) Inasemwa ni Abu 'Abdillaah, na inasemwa Abu Laylaa 'Uthmaan bin 'Affaan (رضي الله عنه) kuwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: "Bin Aadam hana haki ya kuwa na zaidi ya vitu aina tatu: nyumba atakayoishi, na mavazi ya kusitiri uchi wake na kipande cha mkate na maji." [At-Tirmidhy, na akasema ni Hadiyth Swahiyh]
Sifa Na Akhlaaq Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)
04-Zuhd Yake: Alikosa Chakula Nyumbani Mwake Hadi Kufikia Miezi Miwili
Kulifikia ukosekanaji wa chakula nyumbani mwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) kwa siku nzima au masiku au hadi miezi kupita! Basi hakika hii pia ni sifa ya Zuhd ya ajabu mno kuimiliki mtu!
وعن النعمان بن بشير رضي الله عنهما ، قَالَ : ذَكَرَ عُمَرُ بْنُ الخَطَّابِ رضي الله عنه ، مَا أَصَابَ النَّاسُ مِنَ الدُّنْيَا ، فَقَالَ : لَقَدْ رَأيْتُ رسول الله صلى الله عليه وسلم يَظَلُّ الْيَوْمَ يَلْتَوِي مَا يَجِدُ مِنَ الدَّقَلِ مَا يَمْلأ بِهِ بَطْنَهُ . رواه مسلم .
Imepokewa kutoka kwa An-Nu'maan bin Bashiyr (رضي الله عنهما) ambaye amesema: Alitaja 'Umar bin Al-Khattaab (رضي الله عنه) yale yaliyowafikia watu katika hii dunia, akasema: "Hakika nilimuona Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akipitisha siku zake akiwa na njaa hana hata tende (hata) mbaya ya kuondoa njaa yake." [Muslim]
Mpaka katika hali yake ya kuaga dunia hakuwa na chakula nyumbani mwake:
عن عائشة رضي الله عنها ، قالت : تُوفي رسول الله صلى الله عليه وسلم، وَمَا في بَيْتِي مِنْ شَيْءٍ يَأكُلُهُ ذُو كَبِدٍ إِلاَّ شَطْرُ شَعِيرٍ في رَفٍّ لي ، فَأكَلْتُ مِنْهُ حَتَّى طَالَ عَلَيَّ ، فَكِلْتُهُ فَفَنِيَ . متفقٌ عَلَيْهِ .
Imepokewa kutoka kwa 'Aaishah (رضي الله عنها) amesema: "Aliaga dunia Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) na hakukuwa katika nyumba chakula cha sawa (kwa watu kula) isipokuwa mtama kidogo katika stoo yangu ambao nilikuwa nikiutumia kwa muda. Baadae nilitaka kuupima lakini ukawa umemalizika." [Al-Bukhaariy na Muslim
Bali alikosa chakula nyumbani mwake hadi kufikia siku tatu:
عن عَائِشَة رضي الله عَنْهَا قالت : (مَا شَبِعَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ ثَلَاثَةَ أَيَّامٍ تِبَاعًا مِنْ خُبْزِ بُرٍّ حَتَّى مَضَى لِسَبِيلِهِ) رواه البخاري ومسلم
‘Aaishah (رضي الله عنها) amesema: “Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) hakupatapo kula mkate wa ngano mpaka kufariki kwake.” [Muslim na wengineo]
Na pia,
فاطِمةَ ناوَلَتْ رسولَ اللهِ صلَّى اللهُ عليه وسلَّمَ كِسْرةً مِن خُبزِ شَعيرٍ، فقال: هذا أوَّلُ طعامٍ أكَلَهُ أبوكِ مِن ثَلاثةِ أيَّامٍ.
Na pia pindi mwanawe Faatwimah (رضي الله عنها) alipompatia kipande cha mkate wa shayiri alisema Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): “Hiki ni chakula cha kwanza baba yako anakula tokea siku tatu.” [Hadiyth ya Anas bin Maalik ameikusanya Imaam Ahmad -Hadiyth Hasan]
Bali kulikosekana chakula nyumbani mwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) hadi kufikia miezi!
عَنْ عُرْوَةَ، عَنْ عَائِشَةَ، أَنَّهَا كَانَتْ تَقُولُ: "وَاللَّهِ يَا ابْنَ أُخْتِي إِنْ كُنَّا لَنَنْظُرُ إِلَى الْهِلاَلِ ثُمَّ الْهِلاَلِ ثُمَّ الْهِلاَلِ ثَلاَثَةَ أَهِلَّةٍ فِي شَهْرَيْنِ وَمَا أُوقِدَ فِي أَبْيَاتِ رَسُولِ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم نَارٌ" قَالَ: قُلْتُ: يَا خَالَةُ فَمَا كَانَ يُعَيِّشُكُمْ؟ قَالَت: الأَسْوَدَانِ التَّمْرُ وَالْمَاءُ إِلاَّ أَنَّهُ قَدْ كَانَ لِرَسُولِ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم جِيرَانٌ مِنَ الأَنْصَارِ وَكَانَتْ لَهُمْ مَنَائِحُ فَكَانُوا يُرْسِلُونَ إِلَى رَسُولِ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم مِنْ أَلْبَانِهَا فَيَسْقِينَاهُ .
Amehadithia ‘Urwah kuwa ‘Aaishah (رضي الله عنها) alikuwa akimwambia: “Ee mwana wa dada yangu! Tulikuwa tukiutazama mwandamo wa mwezi, kisha mwezi mwengine kisha mwezi mwengine, miandamo mitatu katika miezi miwili na ilhali katika nyumba za Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) hakujaashwa moto (wa kupikia chakula). (‘Urwaa) Akasema: Nikamuuliza: “Ee Khaalat yangu, je, mliweza kuishi kwa vipi?” Akasema: “Vyeusi viwili: tende na maji isipokuwa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alikuwa ana jirani katika Answaariy walikuwa wana mbuzi na walikuwa wakimletea Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) maziwa yake akawa anatunywesha.” [Al-Bukhaariy, Muslim na wengineo]
Sifa Na Akhlaaq Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)
05-Zuhd Yake: Akibaki Na Njaa Na Chakula Chake Kilikuwa Duni
Alhidaaya.com [4]
Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alikuwa akibaki na njaa yeye pamoja na ahli zake, na aghlabu ya chakula chake kilikuwa ni duni. Hadiyth kadhaa zimethibiti kuhusu hali hizi, miongoni mwazo ni Hadiyth zifuatazo:
Aghlabu ya chakula chao kilikuwa ni mkate wa shayiri:
عن ابن عباس رضي الله عنهما قال : "كَانَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يَبِيتُ اللَّيَالِي الْمُتَتَابِعَةَ طَاوِيًا ، وَأَهْلُهُ لاَ يَجِدُونَ عَشَاءً ، وَكَانَ أَكْثَرُ خُبْزِهِمْ خُبْزَ الشَّعِيرِ" رواه الترمذي (2360) وحسنه الألباني في صحيح الترمذي .
Imepokelewa kutoka kwa Ibn ‘Abbaas (رضي الله عنهما) ambaye amesema: “Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alikuwa akipitisha nyusiku kadhaa na ilhali ahli zake hawakupata chakula cha usiku, na aghlabu ya chakula chao kilikuwa ni mkate wa shayiri.” [At-Tirmidhiy na ameisahihisha Al-Albaaniy]
Hakupata kula nyama ya kuoka wala mkate mwembamba:
حَدَّثَنَا مُحَمَّدُ بْنُ سِنَانٍ، حَدَّثَنَا هَمَّامٌ، عَنْ قَتَادَةَ، قَالَ: "كُنَّا عِنْدَ أَنَسٍ وَعِنْدَهُ خَبَّازٌ لَهُ فَقَالَ مَا أَكَلَ النَّبِيُّ صلى الله عليه وسلم خُبْزًا مُرَقَّقًا وَلاَ شَاةً مَسْمُوطَةً حَتَّى لَقِيَ اللَّهَ". البخاري
Ametuhadithia Muhammad bin Sinaan, ametuhadithia Hammaam, kutoka kwa Qataadah amesema: Tulikuwa kwa Anas na mwokaji mikate alikuwa pamoja naye. Anas akasema: “Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) hakupata kula mkate mwembamba wala mbuzi wa kuokwa mpaka kukutana kwake na Allaah (kufariki kwake).” [Al-Bukhaariy]
Hakupata kula supu ya nyama ya kuwashibisha siku tatu mfululizo:
عَنْ عَائِشَةَ رضى الله عنها قَالَتْ: "مَا فَعَلَهُ إِلاَّ فِي عَامٍ جَاعَ النَّاسُ، أَرَادَ أَنْ يُطْعِمَ الْغَنِيُّ الْفَقِيرَ، وَإِنْ كُنَّا لَنَرْفَعُ الْكُرَاعَ بَعْدَ خَمْسَ عَشْرَةَ، وَمَا شَبِعَ آلُ مُحَمَّدٍ صلى الله عليه وسلم مَنْ خُبْزِ بُرٍّ مَأْدُومٍ ثَلاَثًا".
‘Aaishah (رضي الله عنها) amesema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) hakufanya hivyo (yaani: kukataza uhifadhi wa nyama ya Udhwhiya kwa siku tatu) isipokuwa (aliruhusu kuhifadhi nyama) ili tajiri awalishe masikini. Lakini baadaye tulikuwa tunaweka makongoro (ya mbuzi) zaidi ya siku kumi na tano. Familia ya Muhammad haikupata kula mkate wa ngano kwa nyama au supu ya kuwashibisha kwa siku tatu mfululizo.” [Al-Bukhaariy]
Faida:
‘Aaishah (رضي الله عنها) aliulizwa katika Hadithi hii kuhusu ukatazaji wa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) kula nyama ya Udhwhiyah baada ya siku tatu. Akasema kuwa Nabiy aliamrisha hivyo yaani kuhifadhi nyama ya Udhwhiyah. (Kuchinjwa mnyama siku ‘Iydul-Adhwhaa) kwa siku tatu katika mwaka uliokuwa ni mwaka wa njaa ili tajiri waweze kulisha maskini nyama ya Udhwhiyah.
Sifa Na Akhlaaq Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)
06-Zuhd Yake:
Ilifika Siku Hapakuwa Na Chakula Nyumbani Mwake Isipokuwa Tende Moja Tu!
Alhidaaya.com [4]
Wake zake Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) nao walijifunza Zuhd na wakakhiari hata kujikhini wenyewe kwa kidogo mno walichonacho na badala yake wakawapatia Maskini waliokuja kuomba kwao. Basi pindi mwanamke maskini mmoja alipofika nyumba ya Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) kuomba Swadaqah au chakula, alimkuta Mama wa Waumini ‘Aaishah (رضي الله عنها) ambaye hakusita kuigawa tende moja iliyokuwa ndio chakula pekee kilichopatika nyumbani mwake:
عَنْ عَائِشَةَ رضى الله عنها قَالَتْ: دَخَلَتِ امْرَأَةٌ مَعَهَا ابْنَتَانِ لَهَا تَسْأَلُ، فَلَمْ تَجِدْ عِنْدِي شَيْئًا غَيْرَ تَمْرَةٍ فَأَعْطَيْتُهَا إِيَّاهَا، فَقَسَمَتْهَا بَيْنَ ابْنَتَيْهَا وَلَمْ تَأْكُلْ مِنْهَا، ثُمَّ قَامَتْ فَخَرَجَتْ، فَدَخَلَ النَّبِيُّ صلى الله عليه وسلم عَلَيْنَا، فَأَخْبَرْتُهُ فَقَالَ: "مَنِ ابْتُلِيَ مِنْ هَذِهِ الْبَنَاتِ بِشَىْءٍ كُنَّ لَهُ سِتْرًا مِنَ النَّارِ" البخاري و مسلم
Kutoka kwa ‘Aaishah (رضي الله عنها) ambaye amesema: “Mama mmoja pamoja na binti zake wawili walikuja kwangu wakiomba (Swadaqah), lakini hakukuta chochote nilichonacho isipokuwa tende moja. Nikampa naye akaigawanya kwa binti zake, naye mwenyewe hakula chochote, kisha akasimama na akaenda zake. Kisha Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akaja nami nikampa taarifa hii. Akasema: “Yeyote anayekabiliwa na mtihani kwa binti zake, naye akawakirimu kwa wema, basi mabinti hao watakuwa ni kinga dhidi ya Moto wa Jahannam.” [Al-Bukhariy, Muslim na wengineo]
Kujikhini kwa aina hii ni ‘amali njema kabisa Aipendayo Allaah (سبحانه وتعالى) Ambaye Aliteremsha Aayah kwa sababu ya kisa kilichotokea katika nyumba ya Abuu Twalhah Al-Answaariy na mkewe Ummu Sulaym ambao walijikhini kula chakula ilhali wao walikuwa na njaa, lakini badala yake wakawaachia wageni wao wale. Kisa chao hicho kilimfurahisha mno Allaah (سبحانه وتعالى) hadi kwamba Akateremsha Aayah:
عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ، . أَنَّ رَجُلاً، مِنَ الأَنْصَارِ بَاتَ بِهِ ضَيْفٌ فَلَمْ يَكُنْ عِنْدَهُ إِلاَّ قُوتُهُ وَقُوتُ صِبْيَانِهِ فَقَالَ لاِمْرَأَتِهِ نَوِّمِي الصِّبْيَةَ وَأَطْفِئِي السِّرَاجَ وَقَرِّبِي لِلضَّيْفِ مَا عِنْدَكِ - قَالَ - فَنَزَلَتْ هَذِهِ
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Hurayrah (رضي الله عنه) kwamba mtu alilala usiku kama mgeni kwa mtu mmoja katika Answaariy ambaye hakuwa na chakula isipokuwa chakula cha watoto wake akamwambia mkewe: “Laza watoto na zima taa karibisha wageni kwa (chakula) ulichonacho.” Ikateremka kauli ya Allaah (سبحانه وتعالى):
وَيُؤْثِرُونَ عَلَىٰ أَنفُسِهِمْ وَلَوْ كَانَ بِهِمْ خَصَاصَةٌ ۚ وَمَن يُوقَ شُحَّ نَفْسِهِ فَأُولَـٰئِكَ هُمُ الْمُفْلِحُونَ﴿٩﴾
Na wanawapendelea kuliko nafsi zao japokuwa wao wenyewe wanahitaji. Na yeyote anayeepushwa na ubakhili na tamaa ya uchu wa nafsi yake, basi hao ndio wenye kufaulu. [Al-Hashr: 9]
Na Anasema pia Allaah (سبحانه وتعالى):
فَاتَّقُوا اللَّـهَ مَا اسْتَطَعْتُمْ وَاسْمَعُوا وَأَطِيعُوا وَأَنفِقُوا خَيْرًا لِّأَنفُسِكُمْ ۗ وَمَن يُوقَ شُحَّ نَفْسِهِ فَأُولَـٰئِكَ هُمُ الْمُفْلِحُونَ﴿١٦﴾
Basi mcheni Allaah muwezavyo, na sikilizeni; na tiini na toeni (kwa ajili ya Allaah) ni kheri kwa ajili ya nafsi zenu. Na yeyote anayeepushwa na ubakhili na tamaa ya uchu wa nafsi yake, basi hao ndio wenye kufaulu. [At-Taghaabun: 16]
Naye Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akatufunza kuwa Iymaan haipatikani isipokuwa mtu ampendelee nduguye kile anachokipendelea nafsi yake:
عَنْ أَنَسٍ (رضي الله عنه) عَنْ النَّبِيِّ (صلى الله عليه و آله وسلم) قَالَ: ((لاَ يُؤْمِنُ أَحَدُكُمْ حَتَّى يُحِبَّ لإِخِيهِ مَا يُحِبُّ لِنَفْسِهِ)) متفق عليه
Imepokelewa kutoka kwa Anas (رضي الله عنه) kwamba Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: ((Hatoamini mmoja wenu mpaka ampendelee nduguye anayojipendelea nafsi yake)) [Al-Bukhaariy na Muslim]
Na huko ndio kufikia wema wa uhakika kama Anavyosema Allaah (سبحانه وتعالى):
لَن تَنَالُوا الْبِرَّ حَتَّىٰ تُنفِقُوا مِمَّا تُحِبُّونَ ۚ وَمَا تُنفِقُوا مِن شَيْءٍ فَإِنَّ اللَّـهَ بِهِ عَلِيمٌ ﴿٩٢﴾
Hamtoweza kuufikia wema mpaka mtoe katika vile mnavyovipenda. Na kitu chochote mnachotoa basi hakika Allaah kwacho ni Mjuzi. [Aal-’Imraan 92]
Sifa Na Akhlaaq Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)
07-Zuhd Yake: Akifunga Jiwe Tumboni Mwake Kwa Sababu Ya Njaa
Alhidaaya.com [4]
Njaa ni jambo gumu mtu kulivumilia kwani huenda likampeleka mtu kula yaliyokuwa ya haraam pindi akikosa chakula. Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alikuwa akifunga tumbo lake kwa kitambaa ili kuzuia njaa:
عن أَنَس بْن مَالِكٍ قال: جِئْتُ رَسُولَ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم يَوْمًا فَوَجَدْتُهُ جَالِسًا مَعَ أَصْحَابِهِ يُحَدِّثُهُمْ وَقَدْ عَصَّبَ بَطْنَهُ بِعِصَابَةٍ ، قَالَ أُسَامَةُ وَأَنَا أَشُكُّ عَلَى حَجَرٍ ، فَقُلْتُ لِبَعْضِ أَصْحَابِهِ: لِمَ عَصَّبَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم بَطْنَهُ؟ فَقَالُوا: مِنَ الْجُوعِ . فَذَهَبْتُ إِلَى أَبِي طَلْحَةَ وَهُوَ زَوْجُ أُمِّ سُلَيْمٍ بِنْتِ مِلْحَانَ فَقُلْتُ يَا أَبَتَاهُ ، قَدْ رَأَيْتُ رَسُولَ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم عَصَّبَ بَطْنَهُ بِعِصَابَةٍ فَسَأَلْتُ بَعْضَ أَصْحَابِهِ فَقَالُوا مِنَ الْجُوعِ . فَدَخَلَ أَبُو طَلْحَةَ عَلَى أُمِّي فَقَالَ هَلْ مِنْ شَىْءٍ فَقَالَتْ نَعَمْ عِنْدِي كِسَرٌ مِنْ خُبْزٍ وَتَمَرَاتٌ فَإِنْ جَاءَنَا رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم وَحْدَهُ أَشْبَعْنَاهُ وَإِنْ جَاءَ آخَرُ مَعَهُ قَلَّ عَنْهُمْ .
Anas bin Maalik (رضي الله عنه) amesema: Nilimtembelea Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) siku moja na nikamkuta amekaa pamoja na Swahaba zake akiongea nao, na alikuwa amejifunga tumbo lake kwa kitambaa. Usaamah alisema: “Nina shaka kama kulikuwa na jiwe juu yake (tumbo lake) au la. Niliuliza baadhi ya Swahaba zake: Kwanini Rasuli amejifungakitambaa tumboni mwake?” Wakasema: “Kutokana na njaa.” Nikaenda kwa Abuu Talha ambaye ni mume wa Umm Sulaym binti Milhaan, nikamwambia: “Ee Baba, nimemuona Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amefunga tumbo lake kwa kitambaa. Nikawauliza baadhi ya Swahaba zake wamesema ni kwa sababu ya njaa. Hapo Abuu Talha akamwendea mama yangu akamuuliza: “Je kuna chochote cha kula?” Akasema: “Naam nnavyo vipande vya mkate na baadhi ya tende. Atakapotujia Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) pekee yake tutaweza kumpa na vitamshibisha, lakini ikiwa atakuja pamoja wenginewe basi havitawatosheleza.” [Muslim]
Na alikuwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akiomba du’aa ifuatayo ya kujikinga na njaa:
اللَّهُمَّ إِنِّي أَعُوذُ بِكَ مِنَ الْجُوعِ فَإِنَّهُ بِئْسَ الضَّجِيعُ وَأَعُوذُ بِكَ مِنَ الْخِيَانَةِ فَإِنَّهَا بِئْسَتِ الْبِطَانَةُ
Ee Allaah, hakika mimi najikinga Kwako na njaa kwani hiyo ni mbaya mno kulala nayo, na najikinga Kwako khiyana kwani hiyo ni dhamira ovu. [Abuu Daawuwd, An-Nasaaiy, Ibn Maajah, Swahiyh An-Nasaaiy (3/1112)]
Na miongoni mwa mambo matatu aliyoyaomba katika Hadiyth mojawapo, amwaombea Ummah wake wasiangamizwe kwa sababu ya njaa:
قَالَ صلى الله عليه وسلم " سَأَلْتُ رَبِّي ثَلاَثًا فَأَعْطَانِي ثِنْتَيْنِ وَمَنَعَنِي وَاحِدَةً سَأَلْتُ رَبِّي أَنْ لاَ يُهْلِكَ أُمَّتِي بِالسَّنَةِ فَأَعْطَانِيهَا وَسَأَلْتُهُ أَنْ لاَ يُهْلِكَ أُمَّتِي بِالْغَرَقِ فَأَعْطَانِيهَا وَسَأَلْتُهُ أَنْ لاَ يَجْعَلَ بَأْسَهُمْ بَيْنَهُمْ فَمَنَعَنِيهَا "
Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Nilimuomba Rabb Wangu mambo matatu, Amenipa mawili, na Amenikatalia moja. Nilimuomba Rabb wangu Asiuangamize Ummah wangu kwa sababu ya njaa, Akanitakabalia hili, nikamuomba Ummah wangu usiangamizwe kwa kugharikishwa (mafuriko) Akanitakabalia hili, na nikamuomba Rabb wangu kwamba kusimwagwe damu yoyote miongoni mwa watu wa Ummah wangu, lakini Hakunitakabalia hili.” [Muslim]
Sifa Na Akhlaaq Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)
08-Zuhd Yake: Njaa Ilimtoa Nje
Alhidaaya.com [4]
Siku moja au usiku mmoja, pindi njaa ilipomzidi Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alitoka nje, akakutana na Swahaba zake ambao nao pia wametoka nje kwa sababu ya kubanwa na njaa:
عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ، قَالَ خَرَجَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم ذَاتَ يَوْمٍ أَوْ لَيْلَةٍ فَإِذَا هُوَ بِأَبِي بَكْرٍ وَعُمَرَ فَقَالَ " مَا أَخْرَجَكُمَا مِنْ بُيُوتِكُمَا هَذِهِ السَّاعَةَ " . قَالاَ الْجُوعُ يَا رَسُولَ اللَّهِ . قَالَ " وَأَنَا وَالَّذِي نَفْسِي بِيَدِهِ لأَخْرَجَنِي الَّذِي أَخْرَجَكُمَا قُومُوا " . فَقَامُوا مَعَهُ فَأَتَى رَجُلاً مِنَ الأَنْصَارِ فَإِذَا هُوَ لَيْسَ فِي بَيْتِهِ فَلَمَّا رَأَتْهُ الْمَرْأَةُ قَالَتْ مَرْحَبًا وَأَهْلاً . فَقَالَ لَهَا رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم " أَيْنَ فُلاَنٌ " . قَالَتْ ذَهَبَ يَسْتَعْذِبُ لَنَا مِنَ الْمَاءِ . إِذْ جَاءَ الأَنْصَارِيُّ فَنَظَرَ إِلَى رَسُولِ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم وَصَاحِبَيْهِ ثُمَّ قَالَ الْحَمْدُ لِلَّهِ مَا أَحَدٌ الْيَوْمَ أَكْرَمَ أَضْيَافًا مِنِّي قَالَ - فَانْطَلَقَ فَجَاءَهُمْ بِعِذْقٍ فِيهِ بُسْرٌ وَتَمْرٌ وَرُطَبٌ فَقَالَ كُلُوا مِنْ هَذِهِ . وَأَخَذَ الْمُدْيَةَ فَقَالَ لَهُ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم " إِيَّاكَ وَالْحَلُوبَ " . فَذَبَحَ لَهُمْ فَأَكَلُوا مِنَ الشَّاةِ وَمِنْ ذَلِكَ الْعِذْقِ وَشَرِبُوا فَلَمَّا أَنْ شَبِعُوا وَرَوُوا قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم لأَبِي بَكْرٍ وَعُمَرَ " وَالَّذِي نَفْسِي بِيَدِهِ لَتُسْأَلُنَّ عَنْ هَذَا النَّعِيمِ يَوْمَ الْقِيَامَةِ أَخْرَجَكُمْ مِنْ بُيُوتِكُمُ الْجُوعُ ثُمَّ لَمْ تَرْجِعُوا حَتَّى أَصَابَكُمْ هَذَا النَّعِيمُ " . مسلم
Amehadithia Abuu Hurayrayh (رضي الله عنه) kwamba: Siku moja Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alitoka mchana mmoja, au usiku, akakutana na Abuu Bakr na ‘Umar (رضي الله عنهما) akawauliza: “Jambo gani lililokutoeni majumbani mwenu wakati huu?” Wakasema: “Ni njaa ee Rasuli wa Allaah!” Akasema: “Nami naapa kwa Ambaye nafsi yangu imo Mkononi Mwake, nami pia lililonitoa ni kama lililowatoa nyinyi. Twendeni!” Wakafuatana naye hadi nyumbani kwa mtu miongoni mwa Answaariy, lakini hawakumkuta nyumbani kwake. Mkewe alipomuona (Rasuli wa Allaah) alimwambia: “Marhaban wa Ahlan” (Karibu). Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akamwambia: “Yuko wapi fulani?” Akajibu: Amekwenda kututafutia maji matamu.” Mara yule Answaariy akaja akamtazama Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) na Swahaba zake akasema: “AlhamduliLLaah! Leo hakuna mwenye wageni watukufu kama mimi!” Akaondoka kisha akarudi na kichala cha tende tosa, tende kavu na tende mbivu, Akwaambia: “Kuleni!” Akachukua kisu lakini Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akamwambia: “Usichinje mbuzi wa maziwa.” Akawachinjia wakala mbuzi yule na wakala katika kile kichala cha tende na wakanywa. Waliposhiba na wakamaliza kiu chao, Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akawaambia Abuu Bakar na ‘Umar (رضي الله عنهما): “Naapa kwa Ambaye nafsi yangu imo Mkononi Mwake, mtaulizwa Siku ya Qiyaamah juu ya neema hii. Njaa imewatoa majumbani mwenu, kisha hamkurejea mpaka mkapata neema hii.” [Muslim]
Na alifundisha du’aa ya kumumobea mtu anayekupa chakula au kinywaji useme:
اللّهُـمَّ أَطْعِمْ مَن أَطْعَمَني، وَاسْقِ مَن سَقانِي
Allaahumma Atw-’im man atw-’amaniy Wasqi man saqaaniy
Ee Allaah Mlishe aliyenilisha na Mnywishe aliyeninyweisha [Hadiyth ya Al-Miqdaad bin Al-Aswad (رضي الله عنه) - Muslim (3/126) [2055], Ahmad]
Sifa Na Akhlaaq Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)
09-Zuhd Yake:
Amefariki Hali Ya Kuwa Hapakuwa Na Chakula Nyumbani Mwake Isipokuwa Chakula Duni
www.alhidaaya.com [13]
عَنْ عَائِشَةَ، قَالَتْ تُوُفِّيَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم وَمَا فِي بَيْتِي مِنْ شَىْءٍ يَأْكُلُهُ ذُو كَبِدٍ، إِلاَّ شَطْرُ شَعِيرٍ فِي رَفٍّ لِي، فَأَكَلْتُ مِنْهُ حَتَّى طَالَ عَلَىَّ، فَكِلْتُهُ فَفَنِيَ.
‘Aaishah (رضي الله عنها) amesema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alifariki ilhali hakuna kitu ndani ya nyumba yangu ambacho mtu aliye hai angeweza kula, isipokuwa shayiri iliyokuweko katika rafu. Kwa hivyo, nilikula hiyo kwa muda mrefu kwa kuipimia, na (baada ya kipindi kifupi) ikamalizika. [Al-Bukhaariy, Muslim]
Na pia,
عَنْ عَائِشَةَ، زَوْجِ النَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم قَالَتْ لَقَدْ مَاتَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم وَمَا شَبِعَ مِنْ خُبْزٍ وَزَيْتٍ فِي يَوْمٍ وَاحِدٍ مَرَّتَيْنِ .
‘Aaishah mke wa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alifariki hali yakuwa hakuwahi kushiba mkate na mafuta ya zaytuni mara mbili kwa siku.” [Muslim]
Na pia,
عَنْ عَائِشَةَ، أَنَّهَا قَالَتْ مَا شَبِعَ آلُ مُحَمَّدٍ صلى الله عليه وسلم مِنْ خُبْزِ شَعِيرٍ يَوْمَيْنِ مُتَتَابِعَيْنِ حَتَّى قُبِضَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم .
‘Aaishah (رضي الله عنها) amesema: Familia ya Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم) haikushiba mkate wa shayiri siku mbili kufuatana mpaka kufariki kwake.” [Al-Bukhaariy, Muslim]
Sifa Na Akhlaaq Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)
10-Zuhd Yake Godoro Na Mto Wake Ulikuwa Duni
Alhidaaya.com [4]
Hadiyth zifuatazo zinaelezea kuhusu godoro na mto aliokuwa akilalia Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم):
عن عَائِشَةَ، قَالَتْ كَانَ وِسَادَةُ رَسُولِ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم الَّتِي يَتَّكِئُ عَلَيْهَا مِنْ أَدَمٍ حَشْوُهَا لِيفٌ .
Amesimulia ‘Aaishah (رضي الله عنها) kwamba “Mto wa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) aliokuwa akiulalia ulitengenezwa kwa ngozi ya mnyama iliyojazwa magamba ya mtende.” [Muslim]
Na Hadiyth ndefu ya ‘Umar bin Al-Khatwwaab (رضي الله عنه) pindi Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alipojitenga mbali na wakeze:
“…Mlangoni wa chumba chake kulikuwa na mtumwa, ambaye nilikwenda kwake, nikamwambia: “Niombee ruhusa kwake ili niweze kuingia”. Akaniruhusu na nikaingia ili kumuona Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akiwa amejinyoosha juu ya jamvi lililoacha alama ubavuni mwake. Chini ya kichwa chake kulikuwa na mto wa ngozi, ndani yake mna usumba na kulikuwa na ngozi zilizokuwa zimetundikwa na majani kwa ajili ya kutengeneza ngozi. [Al-Bukhaariy]
Na pia kutoka kwa ‘Aaishah (Radhwiya Allaahu ‘anhaa) amesema: “Mto wake aliokuwa akilalia usiku, ulikuwa ni wa ngozi uliojazwa ufumwele.” [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Abu Daawuwd (4146) na At-Tirmidhiy. Iko katika Swahiyhul Jaami’i (4714)].
Na kuhusu godoro lake:
عن عائشة رضي الله عنها ، قالت : كَانَ فِرَاشُ رسول الله صلى الله عليه وسلم مِنْ أُدْمٍ حَشْوُهُ لِيفٌ . رواه البخاري .
Imepokewa kutoka kwake 'Aaishah (Radhwiya Allaahu 'anhaa) kwamba amesema: "Godoro la Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) lilikuwa limetengenezwa kwa ngozi iliyotiwa magamba ya mtende." [Al-Bukhaariy]
Sifa Na Akhlaaq Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)
11-Zuhd Yake: Amefariki Hakuacha Mali
Alhidaaya.com [4]
وعن عمرو بن الحارث أخي جُوَيْرِيّة بنتِ الحارِث أُمِّ المُؤْمِنِينَ ، رضي الله عنهما ، قَالَ : مَا تَرَكَ رسولُ الله صلى الله عليه وسلم عِنْدَ مَوْتِهِ دِيناراً ، وَلاَ دِرْهَماً ، وَلاَ عَبْداً ، وَلاَ أَمَةً ، وَلاَ شَيْئاً إِلاَّ بَغْلَتَهُ الْبَيضَاءَ الَّتي كَانَ يَرْكَبُهَا ، وَسِلاَحَهُ ، وَأرْضاً جَعَلَهَا لاِبْنِ السَّبِيلِ صَدَقَةً . رواه البخاري .
Imepokewa kutoka kwa 'Amri bin Al-Haarith, kaka yake Juwayriyyah bint Al-Haarith, Mama wa Waumini ambaye amesema: "Hakuacha Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) wakati wa kufariki hata dinari moja wala dirhamu wala mjakazi wala kijakazi wala kitu kingine chochote isipokuwa nyumbu wake mweupe aliyekuwa akipanda na silaha zake na ardhi aliyoiacha kama sadaqah kwa wasafiri." [Al-Bukhaariy]
Na alikuwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akisema:
لَا نُورَثُ، مَا تَرَكْنَاهُ صَدَقَةٌ
haturithiwi na tunachoacha ni sadaka. [Al-Bukhaariy, Muslim]
وقال عمرو بن الحارث رضي الله عنه : "مَا تَرَكَ النَّبِىُّ صلى الله عليه وسلم إِلاَّ سِلاَحَهُ وَبَغْلَتَهُ الْبَيْضَاءَ ، وَأَرْضًا تَرَكَهَا صَدَقَةً" رواه البخاري
‘Amr bin Al-Haarith (Radhwiya Allaahu 'anhu) amesema: Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam hakuacha chochote (baada ya kifo chake) isipokuwa ngao yake, nyumbu wake mweupe, na kipande cha ardhi ambacho alikiacha kwa ajili ya sadaka.” [Al-Bukhaariy]
Sifa Na Akhlaaq Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)
12-Zuhd Yake: Hakujifakharisha Kwa Mavazi Akakataza Mtu Kujivuna Kwayo
Alhidaaya.com [4]
Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alikataza kujivuna au kujifakharisha kwa mavazi yake, Hadiyth zfuatazo zinathibitisha:
حَدَّثَنَا آدَمُ، حَدَّثَنَا شُعْبَةُ، حَدَّثَنَا مُحَمَّدُ بْنُ زِيَادٍ، قَالَ سَمِعْتُ أَبَا هُرَيْرَةَ، يَقُولُ قَالَ النَّبِيُّ ـ أَوْ قَالَ أَبُو الْقَاسِمِ ـ صلى الله عليه وسلم " بَيْنَمَا رَجُلٌ يَمْشِي فِي حُلَّةٍ، تُعْجِبُهُ نَفْسُهُ مُرَجِّلٌ جُمَّتَهُ، إِذْ خَسَفَ اللَّهُ بِهِ، فَهْوَ يَتَجَلَّلُ إِلَى يَوْمِ الْقِيَامَةِ ".
Ametuhadithia Aadam, ametuhadithis Muhammad bin Ziyaad, amesema: Nimemsikia Abuu Hurayrah akisema: Nabiy (Au Abul-Qaasim) (صلى الله عليه وآله وسلم) alisema: “Mtu mmoja alikuwa akitembea na kujiona kwa jinsi alivyokuwa amevaa na jinsi alivyozichana nywele zake, ghafla Allaah Akamdidimiza ardhini, kwa hiyo anaendelea kudidimia mpaka Siku ya Qiyaamah.” [Al-Bukhaariy]
Na pia amekataza kuburuza nguo kwa majivuno:
عَنِ ابْنِ عُمَرَ ـ رضى الله عنهما ـ أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم قَالَ " لاَ يَنْظُرُ اللَّهُ إِلَى مَنْ جَرَّ ثَوْبَهُ خُيَلاَءَ ".
Imepokewa kwa Ibn ‘Umar (رضي الله عنهما) kuwa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Allaah Hamuangalii mwenye kuburuza nguo yake kwa kiburi.” [Al-Bukhaariy]
Na pia,
Kutoka kwa ‘Abdullaah bin ‘Umar (Radhiya Allaahu ‘anhumaa) anasema kwamba Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Mtu mmoja alipokuwa anatembea, huku anaburuza nguo yake kwa kibri, alifanywa amezwe na ardhi na ataendelea kudidimia ndani yake mpaka siku ya Qiyaamah” [Al-Bukhaariy]
Links
[1] https://www.alhidaaya.com/sw/taxonomy/term/285
[2] http://alhidaaya.com/sw/
[3] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F10307&title=Sifa%20Na%20Akhlaaq%20Za%20Nabiy%20%28%D8%B5%D9%84%D9%89%20%D8%A7%D9%84%D9%84%D9%87%20%D8%B9%D9%84%D9%8A%D9%87%20%D9%88%D8%A2%D9%84%D9%87%20%D9%88%D8%B3%D9%84%D9%85%29%3A%20Zuhd%20Yake%3A
[4] http://www.alhidaaya.com/sw/
[5] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F10372&title=01-Sifa%20Na%20Akhlaaq%20Za%20Nabiy%20%28%D8%B5%D9%84%D9%89%20%D8%A7%D9%84%D9%84%D9%87%20%D8%B9%D9%84%D9%8A%D9%87%20%D9%88%D8%A2%D9%84%D9%87%20%D9%88%D8%B3%D9%84%D9%85%29%3A%20Zuhd%20Yake%3A%20Kauli%20Zake%20Kuhusu%20Zuhd%20%28Kuipa%20Mgongo%20Dunia%29%20%20%20
[6] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F10373&title=02-Sifa%20Na%20Akhlaaq%20Za%20Nabiy%20%28%D8%B5%D9%84%D9%89%20%D8%A7%D9%84%D9%84%D9%87%20%D8%B9%D9%84%D9%8A%D9%87%20%D9%88%D8%A2%D9%84%D9%87%20%D9%88%D8%B3%D9%84%D9%85%29%3A%20Zuhd%20Yake%3A%20Akiomba%20Du%E2%80%99aa%20Kuambatanishwa%20Na%20Masikini%20Kufishwa%20Nao%20Na%20Kufufuliwa%20Nao
[7] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F10374&title=03-Sifa%20Na%20Akhlaaq%20Za%20Nabiy%20%28%D8%B5%D9%84%D9%89%20%D8%A7%D9%84%D9%84%D9%87%20%D8%B9%D9%84%D9%8A%D9%87%20%D9%88%D8%A2%D9%84%D9%87%20%D9%88%D8%B3%D9%84%D9%85%29%3A%20Zuhd%20Yake%3A%20Akiomba%20Du%E2%80%99aa%20Ya%20Kujaaliwa%20Rizqi%20Ya%20Kumtosheleza%20Tu
[8] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F10375&title=04-Sifa%20Na%20Akhlaaq%20Za%20Nabiy%20%28%D8%B5%D9%84%D9%89%20%D8%A7%D9%84%D9%84%D9%87%20%D8%B9%D9%84%D9%8A%D9%87%20%D9%88%D8%A2%D9%84%D9%87%20%D9%88%D8%B3%D9%84%D9%85%29%3A%20Zuhd%20Yake%3A%20Alikosa%20Chakula%20Nyumbani%20Mwake%20Hadi%20Kufikia%20Miezi%20Miwili
[9] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F10376&title=05-Sifa%20Na%20Akhlaaq%20Za%20Nabiy%20%28%D8%B5%D9%84%D9%89%20%D8%A7%D9%84%D9%84%D9%87%20%D8%B9%D9%84%D9%8A%D9%87%20%D9%88%D8%A2%D9%84%D9%87%20%D9%88%D8%B3%D9%84%D9%85%29%3A%20Zuhd%20Yake%3A%20Akibaki%20Na%20Njaa%20Na%20Chakula%20Chake%20Kilikuwa%20Duni%20%20
[10] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F10377&title=06-Sifa%20Na%20Akhlaaq%20Za%20Nabiy%20%28%D8%B5%D9%84%D9%89%20%D8%A7%D9%84%D9%84%D9%87%20%D8%B9%D9%84%D9%8A%D9%87%20%D9%88%D8%A2%D9%84%D9%87%20%D9%88%D8%B3%D9%84%D9%85%29%3A%20Zuhd%20Yake%3A%20Ilifika%20Siku%20Hapakuwa%20Na%20Chakula%20Nyumbani%20Mwake%20Isipokuwa%20Tende%20Moja%20Tu%21
[11] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F10378&title=07-Sifa%20Na%20Akhlaaq%20Za%20Nabiy%20%28%D8%B5%D9%84%D9%89%20%D8%A7%D9%84%D9%84%D9%87%20%D8%B9%D9%84%D9%8A%D9%87%20%D9%88%D8%A2%D9%84%D9%87%20%D9%88%D8%B3%D9%84%D9%85%29%3A%20Zuhd%20Yake%3A%20Akifunga%20Jiwe%20Tumboni%20Mwake%20Kwa%20Sababu%20Ya%20Njaa
[12] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F10379&title=08-Sifa%20Na%20Akhlaaq%20Za%20Nabiy%20%28%D8%B5%D9%84%D9%89%20%D8%A7%D9%84%D9%84%D9%87%20%D8%B9%D9%84%D9%8A%D9%87%20%D9%88%D8%A2%D9%84%D9%87%20%D9%88%D8%B3%D9%84%D9%85%29%3A%20Zuhd%20Yake%3A%20Njaa%20Ilimtoa%20Nje%20
[13] http://www.alhidaaya.com
[14] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F10380&title=09-Sifa%20Na%20Akhlaaq%20Za%20Nabiy%20%28%D8%B5%D9%84%D9%89%20%D8%A7%D9%84%D9%84%D9%87%20%D8%B9%D9%84%D9%8A%D9%87%20%D9%88%D8%A2%D9%84%D9%87%20%D9%88%D8%B3%D9%84%D9%85%29%3A%20Zuhd%20Yake%3A%20Amefariki%20Hali%20Ya%20Kuwa%20Hapakuwa%20Na%20Chakula%20Nyumbani%20Mwake%20%20Isipokuwa%20Chakula%20Duni
[15] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F10623&title=10-Sifa%20Na%20Akhlaaq%20Za%20Nabiy%20%28%D8%B5%D9%84%D9%89%20%D8%A7%D9%84%D9%84%D9%87%20%D8%B9%D9%84%D9%8A%D9%87%20%D9%88%D8%A2%D9%84%D9%87%20%D9%88%D8%B3%D9%84%D9%85%29%3A%20Zuhd%20Yake%3A%20Godoro%20Na%20Mto%20Wake%20Ulikuwa%20Duni
[16] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F10629&title=11-Sifa%20Na%20Akhlaaq%20Za%20Nabiy%20%28%D8%B5%D9%84%D9%89%20%D8%A7%D9%84%D9%84%D9%87%20%D8%B9%D9%84%D9%8A%D9%87%20%D9%88%D8%A2%D9%84%D9%87%20%D9%88%D8%B3%D9%84%D9%85%29%3A%20Zuhd%20Yake%3A%20Amefariki%20Hakuacha%20Mali
[17] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F10732&title=12-Sifa%20Na%20Akhlaaq%20Za%20Nabiy%20%28%D8%B5%D9%84%D9%89%20%D8%A7%D9%84%D9%84%D9%87%20%D8%B9%D9%84%D9%8A%D9%87%20%D9%88%D8%A2%D9%84%D9%87%20%D9%88%D8%B3%D9%84%D9%85%29%3A%20Zuhd%20Yake%3A%20Hakujifakharisha%20Kwa%20Mavazi%20Akakataza%20Mtu%20Kujivuna%20Kwayo%20%20