Hukmu Ya Kuambizana ”Ramadhwaan Kariym”
Shaykh Swaalih Al-Fawzaan
SWALI:
Kauli kusema "Ramadhwaan Kariym". Je, Kariym si Allaah?
JIBU:
Hili halina asli. Kusema "Ramadhwaan Kariym" hili halina asli. Ama kusema "Ramadhwaan Shariyf", "Ramadhwaan Mubaarak", "Ramadhwaan ´Adhiym" haya maneno yamekuja katika Ahaadiyth. Hakuna ubaya. Ama Ramadhwaan Kariym hili sijui kama lina asli.
[Al-Mawqi’ Ar-Rasmiy li Shaykh Swaalih bin Fawzaan] [5]
Kuacha Kufunga Ramadhwaan Kwa Ajili Ya Kazi Ngumu
Imaam Ibn ‘Uthaymiyn (Rahimahu-Allaah)
SWALI:
Yapi maoni yako kuhusu ugumu wa kazi ya mtu na ikawa vigumu kwake kufunga. Je inajuzu kwake kukata Swawm?
JIBU:
Maoni yangu ni yeye kuvunja Swawm yake kutokana kazi hii ni haraam kwake kuvunja Swawm, haijuzu kuacha kufunga. Haijuzu kwa mtu kulinganisha kazi yake na Swawm, anatakiwa kuchukua likizo kazini wakati wa Ramadhwaan, ili iwe kwake rahisi kuweza kufunga.
Swawm ya Ramadhwaan ni katika nguzo za Uislamu na haijuzu kwake kuacha kufunga (kwa sababu ya kazi).
[Hukumu ya Kiislamu juu ya nguzo za Uislamu, mj. 2, uk. 630]
Miaka Mingapi Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) Alifunga Ramadhwaan
Imaam An-Nawawiy (Rahimahu-Allaah)
SWALI:
Ni miaka mingapi Mtume (Swala Allaahu ’alayhi wa sallam) alifunga mwezi wa Ramadhwaan?
JIBU:
Alifunga (Ramadhwaan) miaka tisa. Swawm ilifaradhishwa mwezi wa Sha’baan mwaka wa 2 baada ya Hijrah.
[Fataawa Imaam An-Nawawiy, uk. 55]
Miji Ambayo Masaa ya kufunga Swawm Ni Marefu Sana
Imaam Ibn ‘Uthaymiyn (Rahimahu-Allaah)
SWALI:
Tuko katika Mji ambapo jua halizami mpaka saa 3:30 au 4:00 (saa tatu au saa nne) za usiku. Ni lini tunatakiwa tufungue Swawm?
JIBU:
Utafufungua Swawm kufuturu wakati jua linapozama. Maadamu tu mko na mchana na usiku kwa masaa 24, unawajibika kufunga swiyaam, hata kama masaa ni marefu kiasi gani.
[Fataawa Islaamiyah uk. 276, mj. 2]
Msafiri Kuswali Rawaatib Katika Ramadhwaan
Shaykh Al-Ghudayyaan
SWALI:
Je, msafiri ataswali swalah ya Rawaatib (Swalaah za Sunnah) katika mwezi wa Ramadhwaan, na vipi kuhusu thawabu kutokana na mwezi huu?
JIBU:
Msafiri katika Ramadhwaan ataswali Dhuhr na Alasiri pamoja na afupishe (yaani dhuhr rakaa 2 na Alasiri 2). Na atasawli Maghrib rakaa 3 aichange na ‘Ishaa kwa kuswali rakaa 2; wala asiswali Rawaatib (Swalaah za Sunnah). Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa anaposafiri, alikuwa anaswali (Sunnah ya) Witr na Rakaa mbili za asubuhi tu. Na ni maalumu kuwa msafiri na mgonjwa (kutokana na hadiyth ya Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) wanaandikiwa wote thawabu kwa yale ambayo walikuwa na ada kuyafanya kama wakaazi. Kwa msafiri, huandikia thawabu ya Swalaah yake kikamilifu, na huandikiwa thawabu ya kila Swalaah ambayo ameiswali kwa wakati wake. Endapo atajumuisha na kufupisha. Kwa mfano (alipokuwa kwake) alikuwa akiswali Swalaah ya Dhwuhaa n.k, huandikia thawabu kwa yale yote aliyokuwa akiyafanya kama mkaazi kwa sababu yuko safirni. Hali kadhalika kwa mgonjwa huandikiwa kwa yale alikuwa akiyafanya wakati alikuwa na afya yake.
Msafiri Wa Mara Kwa Mara Katika Ramadhwaan
Shaykh Al-Luhaydaan
SWALI:
Mimi ni muendesha lori na huendesha kutwa nzima kutoka mji hadi mji. Je, naingia katika hukmu ya masafiri au nalazimika kufunga Swawm ya mwezi wa Ramadhwaan?
JIBU:
Inajuzu mtu kufunga siwyaam hata kama yuko safarini, isipokuwa tu kama mtu atahofia madhara katika afya yake. Maadamu kazi yako hii ni ya kila siku, inajuzu kwako kufunga swiyaam ikiwa kama huhofii madhara. Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akitoka yeye na Maswahaba wake katika Ramadhwaan wakienda Vitani - Miongoni mwao pako waliokuwa wakifunga swiyaa wala hakuwakataza kama ilivyokuja katika Hadiyth. Anasema mmoja katika Maswahaba: "Tulikuwa tukisafiri pamoja na Nabiy (Swala Allaahu 'alayhi wa aalihi sallam) baadhi yetu tunafunga swiyaam na wengine wanakula - Kulikuwa hakuna tatizo kwa yule aliyefunga, na yule ambaye hakufunga.”
Kwa hiyo hakuna matatizo, bali ni bora zaidi (kwa yule msafiri ambae ndio kazi yake) afunge wakati wa safari isipokuwa tu kama atahofia madhara kwenye afya yake.
Muislamu Kufungua Mgawaha (Hoteli) Au Duka Mchana Wa Ramadhwaan
Shaykh Al-Luhaydaan
SWALI:
Ipi hukmu ya Muislamu kufungua Mgahawa (hoteli) mji wa makafiri mchana wa Ramadhwaan kwa ajili ya kuwauzia makafiri sehemu ambapo kunaishi Waislamu pia. Je, inajuzu?
JIBU:
Ndio, hakuna matatizo kwa Muislamu kufungua mgahawa wake au duka ambalo wanauza chakula n.k, kwa kuwauzia wale ambao hawaingii katika hii hukmu (ya kufunga) kama Mayahudi, Manaswara, (Waislamu Wasafiri n.k), lakini asiwauzie chakula Waislamu ambao wamefunga. Asiwauzie Waislamu ambao anajua kabisa kwamba watakila mchana, ama akijua kuwa atakihifadhi chakula hicho mpaka wakati wa adhaana hakuna tatizo (kumuuzia). Hakuna ubaya kwake kuwauzia chakula au kinywaji hata Waislamu ambao hawakuwajibika na Swawm mchana wa Ramadhwaan.
Mwanamke Anayelazimishwa Kujimai Wakati Wa Ramadhwaan
Imaam Ibn Qudaamah Al-Maqdisiy
SWALI:
Ikiwa mwanamke atalazimishwa jimai, halazimiki kulipa kafara, bali analazimika kulipa tu siku hiyo?
JIBU:
Muhannaa kasema: "Nilimuuliza Ahmad kama mwanamke aliyebakwa analazimika kulipa siku hiyo. Akasema: "Ndiyo." Pia nikamuuliza kama analazimika kulipa kafara, akasema: "Hapana!"
Maoni haya anakubaliana nayo pia al-Hasan, Ath-Thawriy, Al-Awza'iy na Hanafiyyah.
Kulingana na swali hili, inamuhusu pia mwanamke ambaye kaingiliwa wakati amelala.
Maalik kasema kuhusiana na mwanamke aliyelala: "Ni juu yake kulipa siku hiyo, ila hatolipa kafara. Ama kuhusiana na mwanamke ambaye amelazimishwa kujimai, analazimika kulipa siku hiyo na kutoa kafara.”
Ash-Shaafi'iy, Abuu Ath-Thawriy na Ibnul-Mundhir wanasema ikiwa ataingiliwa jimai kwa matisho, basi wana maoni sawa na sisi.
[Al-Mughniy (4/376) Daar 'Alaam-il-kutub, 1419/1999]
Mwanamke Alikuwa Mgonjwa Akafariki Naye Hakufunga Ramadhwaan
Shaykh Swaalih Al-Fawzaan
SWALI:
Mwanamke kasibiwa na maradhi akafariki naye hakufunga Ramadhwaan na wala hakulipa, je alipiwe?
JIBU:
Ikiwa aliacha kufunga swiyaam kwa ajili ya maradhi na akafa kwayo, hana juu yake kitu.
Fataawa Shaykh Al-Fawzaan [14]
Swawm Na Mazoezi Ya Kiaskari Katika Ramadhwaan
Shaykh Al-Ghudayaan
SWALI:
Najua kuwa kupigana katika Ramadhwaan haijuzu. Je, hili linahusu pia mazoezi ya Kiaskari (mazoezi ya ngumi n.k.)?
JIBU:
Hapana! Mazoezi ya kiaskari hakuna tatizo.
Swiyaam Ya Gurupu Kwa Ajili Ya Kushaj-ishana
Imaam Ibn ´Uthaymiyn
SWALI:
Ipi hukumu ya Swiyaam ya gurupu, kama kukusanyika gurupu la watu na kukubaliana kufunga swiyaam masiku maalumu kama Jumatatu na Al-Khamiys na hivyo kwa jili ya kusaidizana katika wema na taqwa; kwa kuwa mtu ni dhaifu katika nafsi yake anapata nguvu kwa ndugu zake. Ipi hukumu ya hilo?
JIBU:
Naona kuwa si katika Sunnah na ni aina ya bid´ah, ikiwa watakubaliana hilo. Kwa mfano ikiwa tunakataa Takbiyrah za pamoja au dhikr za pamoja, basi Swawm pia ni ‘ibaadah, haifai kuifunga kwa pamoja.
Lakini ikiwa bila ya makubaliano, basi hakuna neno. Kwa mfano imetokea tumefunga siku ya Jumatatu, hivyo wakasema baadhi yetu kuwaambia wengine: “Waliofunga futari itakuwa kwa fulani na tunakubaliana kufuturu kwake”, hivi hakuna ubaya kwa kuwa si jambo lililopangwa na mkusanyiko wao sio ´ibaadah.
‘Ibaadah kufungwa kwa jamii au pekee ni katika jambo liliomo katika Shariy’ah. Na kwa hili lau kama Allaah Asingetuwekea Shari´yah kuswali jamaa´ah, tusingeliswali jama´ah, ingekuwa kuswali jama´ah ni bid´ah. Lakini Allaah Katuwekea hilo katika Shariy´ah. Hali kadhalika Swawm ya pamoja (kundi) na kukubaliana hilo kabla ni aina ya bid’ah.
Baadhi ya watu wanaweza kuuliza kuhusu Swawm ya Ramadhwaan, je si tunafunga pamoja? Ni kweli, lakini hivyo ndivyo ilivyofaradhishwa. Imefaradhishwa kufunga watu wote katika mwezi huu.
Mimi naona mtu aache hivyo (kufunga kwa gurupu) na mtu awe mwenye kumuomba Allaah (´Azza wa Jalla) na ajihesabu nafsi yake. Na ikiwa mtu hawezi kufanya ´ibaadah ila mpaka apate msaada katika fimbo, yaani mpaka waifanye wengine, azima yake itakuwa dhaifu.
Mtoto Anawajibika Kufunga Swiyaam?
Imaam Ibn ‘Uthaymiyn (Rahimahu-Allaah)
SWALI:
Ipi hukumu Swawm ya mtoto?
JIBU:
Swawm ya mtoto kama tulivyosema, ni mustahab (imependekezwa) na si waajib. Mtoto akifunga, anapewa thawabu; na ikiwa ataacha kufunga, hapati dhambi. Hata hivyo, inatakikana kwa mlezi wake kumuamrisha kufunga ili azowee.
[Fataawaa fiy Ahkaam Asw-Swiyaam, uk. 84]
Watoto Waamrishwe Swiyaam Wanapofikisha Miaka Saba
Imaam Ibn Baaz (Rahimahu-Allaah)
SWALI:
Je, mvulana ambaye kakomaa anapaswa kuamrishwa swiyaam? Je, Swawm yake ni sahihi ikiwa atabaleghe wakati wa Swawm (katika Ramadhwaan)?
JIBU:
Ikiwa wavulana na wasichana wanafikisha umri wa miaka saba wanapaswa kuamrishwa kuanza swiyaam ili wajizoeze. Wazazi wao ni juu yao kuwaamrisha Swawm hali kadhalika kama wanavyopasa kuwaamrisha Swalah. Wanapobaleghe, Swawm imewawajibikia. Ikiwa watakomaa wakati wa Swawm, siku zao (wanazofunga) ni sahihi. Ikiwa mvulana atafikisha miaka kumi na tano mchana wakati yuko na Swawm, siku yake ni sahihi. Mwanzo wa siku hiyo (Swawm kwake) ilikuwa ni Sunnah na mwisho wake itakuwa ni waajib ikiwa tayari kishatokwa na nywele za sehemu za siri au kishaanza kutokwa na manii. Hali kadhalika inawahusu wanawake ambao wanabaleghe kwa kutokwa na damu ya hedhi.
[Fataawa Ibn Baaz Hukmu Amr Asw-Swabiy Al-Mumayyiz Bisw-Swiyaam] [19]
Kuwafunza Watoto Katika Ramadhwaan
Shaykh ‘Abdullaah Al-Ghudayyaan
SWALI:
Watoto wengi wanapuuza mambo ya Dini yao. Upi umri ambao ni wajibu kwa wale wanaowafunza (hao watoto wanapaswa kuzingatia)? Na ipi nasiha yako kwa kuwapeleka watoto Masjid katika Ramadhwaan? Watoto ambao wako baina ya miaka 7 mpaka 13.
JIBU:
Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Kila mmoja wenu ni mchunga na kila mmoja ataulizwa alichokichunga, kiongozi wa watu ni mchunga na ataulizwa kwa alichokichunga, mwanamme ni mchunga wa familia yake na ataulizwa kwa alichokichunga, mwanamke ni mchunga wa nyumba ya mume wake na watoto wake naye ataulizwa alichokichunga, na mtumwa ni mchunga wa mali ya bwana wake naye ataulizwa kuhusu uchungaji wake”.
Na Anasema Allaah (Jalla wa 'Alaa):
”Enyi mlio amini! Jilindeni nafsi zenu na ahali zenu na Moto.” (66:6)
Na anasema Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi sallam):
”Kalamu imesimamishwa kwa watu aina tatu: akasema mmoja wao ni “mtoto mpaka abalehe.”
Kwa mwanamke mpaka abalehe. Na kwa mwanume (mara nyingi) hubalehe anapofikisha miaka 15, au anaota nywele za sehemu ya siri. (Mwanaume na mwanamke) wanapoanza kutokwa na manii, mwanamke anatofautiana na mwanamume, kwa kuwa yeye mwanamke hubalehe kwa hedhi. Hizi ndizo alama za kubalehe (kwa mwanaume na mwanamke).
Ama kabla ya kubalehe, si wajibu kwao Swalaah (na Swawm). Lakini waanze kufunzwa (na kupewa mazoezi), kama alivyosema Nabiy (Swaala Allaahu 'alayhi wa aalihi sallam). "Waamrisheni watoto wenu Swalaah wanapofika miaka 7, na wapigeni wakifikisha miaka 10 na watenganisheni kwenye vitanda". Kwa hiyo inatakiwa kwa baba ampeleke mtoto wake Masjid anapofikisha 7. Ama kabla ya kufikisha miaka hiyo anakuwa mtoto hana ile niyyah (hamu). Ama atapofikisha miaka 7, hapo anaponuia Swalaah, niyyah yake inakuwa Sahihi, na anaponuia Swawm niyyah yake inakuwa sahihi. Lakini mtoto kuweka niyyah kabla ya (kufikisha) miaka 7, mtoto halizingatii hili.
Katika msingi huu - mzazi amfunze mtoto wake sawa akiwa ni mwanaume au mwanamke. Na kama watoto hawana hamu ile ya kujifunza, ni vizuri awaletee jirani, au mtu kwenye Masjid ambaye anaweza kuwafunza watoto wake, (na kwa mama) kumleta mwanamke awafunze mabanati wake.
Aliyefariki Katika Ramadhwaan Amaliziwe Swiyaam Siku Zilobakia?
Imaam Ibn ‘Uthaymiyn (Rahimahu-Allaah)
www.alhidaaya.com [22]
SWALI:
Ikiwa Muislamu alifunga baadhi ya siku katika Ramadhwaan kisha akafariki, je inampasa mtu mwenye jukumu la mambo yake (baada ya kufa kwake) ammalizie Swawm (ya siku zilizobakia za Ramadhwaan) kwa ajili yake?
JIBU:
Hapana! Haimpasi mwenye jukumu la mambo yake kummalizia Swawm (za siku zilizobakia za Ramadhwaan) kwa ajili yake wala kulisha masikini kwa ajili yake. Hii ni kwa sababu mtu anapofariki vitendo vyake vyote vinakatika kama alivyosema Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ((Mwana Aadam anapofariki ‘amali zake zote hukatika isipokuwa matatu: Swadaqah inayoendelea, elimu inayoendelea kunufaisha na mtoto mwema anayemuombea)).
Kwa kutokana na Hadiyth hii, mtu akifariki katika hali iliyotajwa katika Swali, haina haja amaliziwe siku zilizobakia za Ramadhwaan au kulisha masikini na wanaohitaji kwa ajili yake. Na hata kama alifariki katikati ya siku na alikuwa amefunga basi haina haja kumlipia siku ile wala kulisha masikini au watu wanaohitaji kwa siku ile kwa ajili yake.
[Imaam Ibn ‘Uthaymiyn - Fataawa Ramadhwaan – Mjalada 2, Ukurasa 645, Fatwa Namba 649; Fiqh al-Ibaadaat libni 'Uthaymiyn - Ukurasa 203]
Anayemuona Mtu Anakula Ramadhwaan Kwa Kusahau Amkumbushe?
Imaam Ibn Baaz (Rahimahu-Allaah)
SWALI:
Je, nimkumbushe mtu ambaye anakula na kunywa (Ramadhwaan) kwa kusahau?
JIBU:
Ndiyo, anatakiwa amtanabahishe ikiwa anamuona mtu huyo anakula au kunywa na amwambie “Wewe umefunga”. Amtanabahishe kwa sababu ni munkari, munkari ulio wazi.
Hata kama mtu ni mwenye kughufuriwa kwa sababu ya kusahau kwake, si katika wakati ule. Anatakiwa kukumbushwa mtu kama huyo.
[Nuwr 'Alaa Ad-Darb, Fatwa na. 9834]
Du’aa "Allaahumma Balighnaa Ramadhwan", Haikuthibiti
Imaam Ibn ‘Uthaymiyn (Rahimahu Allaah)
SWALI:
Imaam aliulizwa kuhusu Hadiyth iliyotaja du’aa:
"اللهم بارك لنا في رجب وشعبان وبلغنا رمضان"
“Ee Allaah Tubarikie katika Rajab na Sha’baan na Tufikishe Ramadhwaan”
JIBU:
Hii ni dhaifu wala haikuthibiti kutoka kwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam).
Na akasema tena Imaam Ibn 'Uthaymiyn (Rahimahu Allaah):
"Hakuna Hadiyth Sahihi ambayo inazungumzia fadhila za Rajab.
Mwezi wa Rajab hauna tofauti yeyote na mwezi wa Jumaadaa Al-Aakhirah ambao (ni mwezi) wa kabla yake, isipokuwa tu ni kuwa ni katika moja ya miezi mitukufu tu. Vinginevyo, hakuna Swawm iliyowekewa katika shariy'ah katika mwezi huu, na wala hakuna Swalaah au 'Umrah au chochote ambacho kimewekewa shariy'ah.
(Mwezi wa Rajab) ni kama miezi mingine tu.
[Liqaa Al-Baab Al-Maftuwh , 26/174]
Na katika sehemu nyingine anasema Imaam Ibn 'Uthaymiyn (Rahimahu Allaah) kuhusiana na khutbah hiyo:
"Mimi nawaambia (hali ya kuwa) nabainisha haki ya kuwa, mwezi wa Rajab hauna Swalaah maalum, si katika usiku wa Ijumaa ya kwanza ndani yake na wala hauna Swawm katika siku ya kwanza ndani yake wala katika siku zilizobakia, bali uhakika ni kuwa (mwezi wa Rajab) ni kama miezi mingine kuhusiana na ufanyaji 'ibaadah, ijapokuwa ni mmoja kati ya miezi minne mitukufu.
Na wamejiliwaza na Hadiythi dhaifu zinazozungumzia kuihusu; kilichopokewa kwa Mtume kuwa alikuwa akisema inapoingia Mwezi wa Rajab:
"اللهم بارك لنا في رجب وشعبان وبلغنا رمضان"
“Ee Allaah Tubarikie katika Rajab na Sha’baan na Tufikishe Ramadhwaan”
Lakini hili enyi ndugu, sikilizeni ninayosema: Hii ni Hadiyth dhaifu munkar, haisihi kutoka kwa Rasuli (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam).
Hivyo basi, hapaswi mtu kuomba du'aa hii kwa sababu haijasihi kutoka kwa Rasuli (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam).
http://binothaimeen.net/content/5425 [25]
Du’aa Ya Mwezi Wa Rajab Sha’baan na Ramadhwaan Haikuthibiti
Imaam Ibn ‘Uthaymiyn (Rahimahu Allaah)
SWALI:
Je, ni Sunnah kusoma du’aa:
اللهم بارك لنا في رجب وشعبان و بلغنا رمضان .
“Ee Allaah Tubarikie katika Rajab na Sha’baan na Tufikishe Ramadhwaan”
JIBU:
Haikuthibiti fadhila za Rajab katika Hadiyth Swahiyh, wala haikuthibiti kufadhilisha mwezi wa Rajab na Jumaadaa Al-Aakhirah ambao ni mwezi wa kabla yake, isipokuwa ni mwezi mtukufu tu!
Wala hakuna Swiyaam iliyowekewa Shariy’ah wala Swalaah wala ‘Umrah wala chochote kile.
Mwezi wa Rajab ni kama miezi mingineyo tu.
[Liqaa Al-Baab Maftuwh (26/174)]
Kupongezana Kwa Kuambiana “Kullu ‘Aamin Wa Antum Bikhayr”
Imaam Ibn ‘Uthaymiyn (Rahimahu Allaah)
www.alhidaaya.com [22]
Aliulizwa Imaam Ibn ‘Uthaymiyn (Rahimahu Allaah):
“Je, husemwa (katika kupongezana) ‘Kullu ‘aamin wa antum bikhayr’?
Akajibu (Rahimahu Allaah):
“Kullu ‘aamin wa antum bikhayr’ haisemwi si katika ‘Iyd Al-Adhw-haa wala katika ‘Iyd Al-Fitwr.”
[Liqaa Al-Baab Al-Maftuwh, 202]
Kupeana Pongezi Za ‘Iyd Kabla Ya Siku Ya ‘Iyd Kufika
Shaykh Al-Fawzaan (Hafidhwahu Allaah)
www.alhidaaya.com [22]
Aliulizwa Ash-Shaykh Al-‘Allaamah Swaalih bin Fawzaan Al-Fawzaan (Hafidhwahu Allaah):
“Kumeenea baina ya watu katika masiku haya, jumbe mbalimbali kupitia simu za mikononi zilizokusanya makatazo ya kupongezana siku ya ‘Iyd kwa siku moja au mbili kabla; na kwamba hivyo ni bid’ah, je, ni ipi rai yako ee mwenye fadhila?”
Akajibu (Hafidhwahu Allaah):
“Sielewi maneno haya. Haya yanayoenezwa. Sielewi kama yana asli yoyote.
Na pongezi inaruhusiwa, katika siku ya ‘Iyd au baada yake. Ama kabla ya siku ya ‘Iyd, sielewi kwamba imepatikana kufanywa hilo na As-Salaf (waja wema waliotangulia); kwamba wao walikuwa wakipongezana siku kabla ya ‘Iyd kufika.
Vipi mtu atapongeza jambo ambalo halijafanyika? Pongezi huwa ni katika siku ya ‘Iyd yenyewe au baada yake. Pamoja na kuwa (jambo hili la kupongezana) hakuna dalili (iliyopokelewa kutoka kwa Rasuli ‘Alayhis Swalaatu was Salaam) kuhusu hilo, lakini Imaam Ahmad (Rahimahu Allaah) amesema ‘Mimi sianzi (kupongeza), lakini namjibu atakayenianza kunipongeza.’
Na’am.”
http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/thnih.mp3 [29]
Kupongezana "Kullu 'Aamin Wa Antum Bikhayr" Haimo Katika Shariy'ah
Shaykh Al-Fawzaan (Hafidhwahu Allaah)
www.alhidaaya.com [22]
Aliulizwa Shaykh Al-Fawzaan (Hafidhwahu Allaah):
“Je, kupongezana kwa kuambiana “Kullu ‘aamin wa antum bikhayr” katika masiku haya ni jambo lililo katika shariy’ah?”
Akajibu (Hafidhwahu Allaah):
“Hapana. Si jambo lililo katika shariy’ah, na wala hili halijuzu.”
[Al-Ijaabaat Al-Muhimmah Fiy Al-Mashaakil Al-Mudlahimmah, uk. 229]
Links
[1] https://www.alhidaaya.com/sw/taxonomy/term/261
[2] http://www.alhidaaya.com/sw/
[3] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F8370&title=Fataawaa%3A%20Hukmu%20Mbali%20Mbali%20Za%20Swawm
[4] http://www.alhidaaya.com
[5] http://www.alfawzan.af.org.sa/allmohadrat?page=4
[6] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F8371&title=01-Shaykh%20Swaalih%20Al-Fawzaan%3A%20Kuambizana%20%E2%80%9DRamadhwaan%20Kariym%E2%80%9D
[7] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F8372&title=02-Imaam%20Ibn%20%E2%80%98Uthaymiyn%3A%20Kuacha%20Kufunga%20Ramadhwaan%20Kwa%20Ajili%20Ya%20Kazi%20Ngumu
[8] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F8377&title=03-Imaam%20An-Nawawiy%3A%20Miaka%20Mingapi%20Nabiy%20%28Swalla%20Allaahu%20%27alayhi%20wa%20aalihi%20wa%20sallam%29%20Alifunga%20Ramadhwaan
[9] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F8378&title=04-Imaam%20Ibn%20%E2%80%98Uthaymiyn%3A%20Miji%20Ambayo%20Masaa%20ya%20kufunga%20Swawm%20Ni%20Marefu%20Sana
[10] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F8379&title=05-Shaykh%20Al-Ghudayyaan%3A%20Msafiri%20Kuswali%20Rawaatib%20Katika%20Ramadhwaan
[11] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F8380&title=06-Shaykh%20Al-Luhaydaan%3A%20Msafiri%20Wa%20Mara%20Kwa%20Mara%20Katika%20Ramadhwaan
[12] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F8381&title=07-Shaykh%20Al-Luhaydaan%3A%20Muislamu%20Kufungua%20Mgawaha%20%28Hoteli%29%20Au%20Duka%20Mchana%20Wa%20Ramadhwaan%20%20
[13] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F8382&title=08-Imaam%20Ibn%20Qudaamah%20Al-Maqdisiy%3A%20Mwanamke%20Anayelazimishwa%20Kujimai%20Wakati%20Wa%20Ramadhwaan
[14] http://www.alfawzan.af.org.sa/allftwa
[15] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F8383&title=09-Shaykh%20Swaalih%20Al-Fawzaan%3A%20Mwanamke%20Alikuwa%20Mgonjwa%20Akafariki%20Naye%20Hakufunga%20Ramadhwaan
[16] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F8384&title=10-Shaykh%20Al-Ghudayaan%3A%20Swawm%20Na%20Mazoezi%20Ya%20Kiaskari%20Katika%20Ramadhwaan
[17] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F8385&title=11-Imaam%20Ibn%20%C2%B4Uthaymiyn%3A%20Swiyaam%20Ya%20Gurupu%20Kwa%20Ajili%20Ya%20Kushaj-ishana
[18] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F8387&title=12-Imaam%20Ibn%20%E2%80%98Uthaymiyn%3A%20Mtoto%20Anawajibika%20Kufunga%20Swiyaam%3F
[19] https://binbaz.org.sa/fatawa/427
[20] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F8388&title=13-Imaam%20Ibn%20Baaz%3A%20Watoto%20Waamrishwe%20Swiyaam%20Wanapofikisha%20Miaka%20Saba
[21] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F8389&title=14-Shaykh%20%E2%80%98Abdullaah%20Al-Ghudayyaan%3A%20Kuwafunza%20Watoto%20Katika%20Ramadhwaan
[22] http://www.alhidaaya.com/
[23] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F8500&title=15-Imaam%20Ibn%20%E2%80%98Uthaymiyn%3A%20Aliyefariki%20Katika%20Ramadhwaan%20Amaliziwe%20Swiyaam%20Siku%20Zilobakia
[24] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F8560&title=16-Imaam%20Ibn%20Baaz%3A%20Anayemuona%20Mtu%20Anakula%20Ramadhwaan%20Kwa%20Kusahau%20Amkumbushe%3F
[25] http://binothaimeen.net/content/5425
[26] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F8568&title=17-Imaam%20Ibn%20%E2%80%98Uthaymiyn%3A%20Du%E2%80%99aa%20%22Allaahumma%20Balighnaa%20Ramadhwan%22%2C%20Haikuthibiti
[27] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F8569&title=18-Imaam%20Ibn%20%E2%80%98Uthaymiyn%3A%20Du%E2%80%99aa%20Ya%20Mwezi%20Wa%20Rajab%20Sha%E2%80%99baan%20na%20Ramadhwaan%20Haikuthibiti
[28] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F8570&title=19-Imaam%20Ibn%20%E2%80%98Uthaymiyn%3A%20Kupongezana%20Kwa%20Kusema%20%22Kullu%20%27Aamin%20Wa%20Antum%20Bikhayr%22
[29] http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/thnih.mp3
[30] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F8573&title=20-Shaykh%20Al-Fawzaan%3A%20Kupeana%20Pongezi%20Za%20%E2%80%98Iyd%20Kabla%20Ya%20Siku%20Ya%20%E2%80%98Iyd%20Kufika
[31] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F8572&title=21-Shaykh%20Al-Fawzaan%3A%20Kupongezana%20%20%22Kullu%20%27Aamin%20Wa%20Antum%20Bikhayr%22%20Haimo%20Katika%20Shariy%27ah