Ipi Bora Kusoma Qur-aan Au Tafsiyr Katika I`tikaaf?
Shaykh Swaalih Al-Fawzaan
SWALI:
Ipi bora kwa mwenye kukaa I´tikaaf, kusoma Qur-aan tu au kusoma Tafsiyr na kuizingatia?
JIBU:
Kusoma Qur-aan ni bora zaidi kwa kuwa kisomo chake kina fadhila katika Ramadhwaan kuliko (miezi mengine). Ama kusoma tafsiri anaweza kufanya hilo wakati mwingine si katika hali ya I´tikaaf. Usomaji wa Qur-aan ubora wake ni wakati wa I´tikaaf, na kujishughulisha kwake kusoma Qur-aan huku anahifadhi ni bora zaidi kuliko kusoma Tafsiyr.
[Al-Mawqi’ Ar-Rasmiy - Shaykh Swaalih Al-Fawzaan] [4]
Asome Qur-aan Pekee Na Aache ‘Amali Nyengine Kama Kutafuta ‘Ilmu Na Da’wah?
Imaam Al-Albaaniy (Rahimahu-Allaah)
SWALI: Kutoka Kwa Sakiynah, Bint Muhammad Naaswir Ad-Diyn Al-Albaaniy.
Nimesoma kuwa pindi Ramadhwaan inapoanza baadhi ya ‘Ulamaa wanajishughulisha na kusoma Qur-aan tu, pia hata watu wenye ‘ilmu wanafanya hali kadhalika kujishughulisha na Qur-aan tu na wanaacha hata kutoa Fataawa kwa watu. Je, ni sahihi? Je, nami naweza nikaenda nje mwezi huu kwa ajili ya (kujifunza) Qur-aan na nikaacha kusoma Hadiyth, nisome maana ya Qur-aan, darsa za Qur-aan na mengine zaidi ya hayo?
JIBU:
Jibu lako ee binti wangu, ni kama ulivyohisi na jibu lake ni kama maneno ya Ibn Taymiyyah. Hili la kwanza.
La pili - kuhusisha huku jambo hili, halina asili katika Sunnah - lakini kilichoko katika Sunnah ni kinajulikana kwenye Swahiyh Al-Bukhaariy na Muslim ni kukithirisha sana kusoma Qur-aan katika mwezi wa Ramadhwaan.
Ama kuhusisha tu katika mwezi wa Ramadhwaan kusoma Qur-aan bila 'Ibaadah nyingine kama kutafuta elimu, kufundisha Hadiyth, na kubainisha maana yake, jambo hili halina asili. Kadhalika kunaingia maudhui ya kutoa swadaqah, Zakaah, kuwatendea watu wema nk. Kujishughulisha na kisoma (tu) ni jambo halina asili. Jambo lenye asili ni kukithirisha kusoma.
[Fatwa Hukmu Twalab Al-‘Ilm Fiy Ramadhwaan] [7]
Lipi Bora Kufanya Katika Mchana Wa Ramadhwaan; Kusoma Qur-aan Au Kuswali Sunnah
Imaam Ibn Baaz (Rahimahu-Allaah)
SWALI:
Kitendo gani bora kufanya katika siku za Ramadhaan, kusoma Qur'aan au kuswali Swalah za Sunnah?
JIBU:
Ilikuwa ni mwongozo wa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ilikuwa ni kufanya aina nyingi ‘ibaadah katika Ramadhaan. Jibriyl alikuwa akimsomesha Qur-aan wakati wa usiku. Na Jibriyl alipokutana naye alikuwa mkarimu katika swadaqah kuliko upepo unaovuma. Alikuwa ni mtu mkarimu kabisa kuliko wote na alikuwa zaidi mkarimu katika mwezi wa Ramadhaan.
Wakati huu wa Ramadhaan alikuwa akitoa swadaqah zaidi na alikuwa akifanya ihsaan kwa watu, akisoma Qur-aan zaidi, akiswali zaidi, akifanya dhikir na akikaa I'tkaaf.
Huu ndio mwongozo wa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) katika maudhui hii na katika mwezi huu mtukufu.
Kuhusu kitendo gani bora kufanya kusoma Qur-aan au kuswali zaidi, inatofautiana kutokana na hali ya mtu na uwezo huo unarudi kwa Allaah (‘Azza wa Jalla) kwani Yeye ni Mwenye kuzunguka kila kitu (kwa ujuzi Wake).
[Al-Mawqi’ Ar-Rasmiy – Imaam Ibn Baaz] [9]
Anayemfuturisha Mwenye Swawm Ramadhwaan Au Sunnah Anapata Thawabu
Shaykh ´Abdul-Muhsin Al-‘Abbaad
SWALI:
Hadiyth: "Mwenye kumfuturisha mwenye swawm ana ujira mfano wake."
Je, Hadiyth imekusudiwa thawabu zake ni khaswa kwa Swawm ya Ramadhwaan?
JIBU:
Ni dalili kwamba ni Swiyaam zote (anapata mtu thawabu).
[Bawaabah Al-Haramayni Ash-Shariyfayni] [11]
Links
[1] https://www.alhidaaya.com/sw/taxonomy/term/261
[2] http://www.alhidaaya.com/sw/
[3] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F8395&title=Fataawaa%3A%20%20Kukithirisha%20%27Ibaadah%20Na%20%27Amali%20Ramadhwaan
[4] http://www.alfawzan.af.org.sa/node/2654
[5] http://www.alfawzan.af.org.sa/node/2654%C2%A0
[6] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F8397&title=01-Shaykh%20Swaalih%20Al-Fawzaan%3A%20Ipi%20Bora%20Kusoma%20Qur-aan%20Au%20Tafsiyr%20Katika%20I%60tikaaf%3F
[7] http://www.ajurry.com/vb/showthread.php?t=19969
[8] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F8398&title=02-Imaam%20Al-Albaaniy%3A%20Asome%20Qur-aan%20Pekee%20Na%20Aache%20%E2%80%98Amali%20Nyengine%20Kama%20Kutafuta%20%E2%80%98Ilmu%20Na%20Da%E2%80%99wah%3F
[9] http://www.binbaz.org.sa/fatawa/1052
[10] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F8399&title=03-Imaam%20Ibn%20Baaz%3A%20Lipi%20Bora%20Kufanya%20Katika%20Mchana%20Wa%20Ramadhwaan%3B%20Kusoma%20Qur-aan%20Au%20Kuswali%20Sunnah%20%20
[11] http://www.alharamain.gov.sa/index.cfm?do=cms.scholarallsubjects&schid=
[12] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F8400&title=04-Shaykh%20%C2%B4Abdul-Muhsin%20Al-%E2%80%98Abbaad%3A%20Anayemfuturisha%20Mwenye%20Swawm%20Ramadhwaan%20Au%20Sunnah%20Anapata%20Thawabu