كتاب الزواج
Kitabu Cha Ndoa
Abu Maalik Kamaal Bin As-Sayyid Saalim
Imetarjumiwa na 'Abdullaah Mu'aawiyah (Abu Baasim)
Alhidaaya.com
Swahiyh Fiqh As-Sunnah
كِتَابُ الزَّوَاجِ
Kitabu Cha Ndoa
Alhidaaya.com [3]
01-Himizo Na Raghibisho La Kuoa:
1- Allaah Ta’aalaa Amesema:
"وَلَقَدْ أَرْسَلْنَا رُسُلًا مِّن قَبْلِكَ وَجَعَلْنَا لَهُمْ أَزْوَاجًا وَذُرِّيَّةً"
“Na kwa yakini Tulituma Rusuli kabla yako, na Tukawajaalia wawe na wake na dhuria”. [Ar-Ra’ad: 38]
2- Allaah Ta’aalaa Amesema:
"وَأَنكِحُوا الْأَيَامَىٰ مِنكُمْ وَالصَّالِحِينَ مِنْ عِبَادِكُمْ وَإِمَائِكُمْ"
“Na waozesheni wajane miongoni mwenu na walio Swalihina kati ya watumwa wenu wanaume na wajakazi wenu”. [An-Nuwr: 32]
3- Allaah Ta’aalaa Amesema:
"فَانكِحُوا مَا طَابَ لَكُم مِّنَ النِّسَاءِ مَثْنَىٰ وَثُلَاثَ وَرُبَاعَ"
“Basi oeni waliokupendezeni katika wanawake wengine; wawili au watatu au wanne”. [An-Nisaa: 03]
4- Allaah Ta’aalaa Amesema:
"وَمِنْ آيَاتِهِ أَنْ خَلَقَ لَكُم مِّنْ أَنفُسِكُمْ أَزْوَاجًا لِّتَسْكُنُوا إِلَيْهَا وَجَعَلَ بَيْنَكُم مَّوَدَّةً وَرَحْمَةً ۚ إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَآيَاتٍ لِّقَوْمٍ يَتَفَكَّرُونَ"
“Na katika Ishara Zake ni kwamba Amekuumbieni katika jinsi yenu wake ili mpate utulivu kwao, na Amekujaalieni baina yenu mapenzi na rahmah. Hakika pana katika hayo, bila shaka mazingatio kwa watu wanaotafakari”. [Ar-Ruwm: 21]
5- Hadiyth ya Anas kuhusiana na kisa cha watu watatu ambao:
"قَالَ أَحَدُهُمْ: أَمَا أَنا فَإِنِّي أُصَلِّي اللَّيْلَ أَبَدًا، وَقَالَ آخَرُ: أَنا أَصُومُ الدَّهْرَ وَلَا أُفْطِرُ، وَقَالَ آخرُ: أَنَا أَعْتَزِلُ النِّسَاءَ فَلَا أَتَزَوَّجُ أَبَدًا، فَجَاءَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ إِلَيْهِمْ فَقَالَ: أَنْتُمُ الَّذِينَ قُلْتُمْ كَذَا وَكَذَا، أَمَا وَاللَّهِ إِنِّي لَأَخْشَاكُمْ لِلَّهِ وَأَتْقَاكُمْ لَهُ، لَكِنِّي أَصُومُ وَأُفْطِرُ، وَأُصَلِّي وَأَرْقُدُ، وَأَتَزَوَّجُ النِّسَاءَ، فَمَنْ رَغِبَ عَنْ سُنَّتِي فَلَيْسَ مِنِّي"
“Mmoja wao alisema: Ama mimi, hakika nitaswali siku zote swalaah za usiku. Na mwingine akasema: Mimi nitafunga mwaka mzima na sitokula mchana. Na wa tatu akasema: Mimi nitakaa mbali na wanawake, sitooa abadan. Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akaja na kuwauliza: Nyinyi ndio mliosema kadha wa kadha? Naapa kwa Allaah kwa ukweli kwamba mimi ndiye ninayemwogopa na kumcha zaidi Allaah kuliko nyinyi nyote, lakini ninafunga na ninakula mchana, ninaswali na ninalala, na ninaoa wanawake. Basi yeyote atakayejiengua na njia na mwenendo wangu, basi huyo yuko mbali nami”. [Hadiyth Swahiyh. Al-Bukhaariy (5063) na Muslim (1401)]
6- Ma’aqil bin Yasaar: “Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
"تَزَوَّجُوا الْوَدُودَ الْوَلُودَ فَإِنِّي مُكَاثِرٌ بِكُمُ الْأُمَم"
“Oeni mwanamke mwenye penzi la dhati, mwenye rutuba ya kizazi, kwani mimi nitajifakhiri kwa wingi wenu mbele ya umma zilizotangulia (Siku ya Qiyaamah)”. [Swahiyh. Imekharijiwa na Abu Daawuwd (2050), An-Nasaaiy (6/65) na wengineo]
7- Ibn Mas-‘uwd: “Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alituambia:
"يَا مَعْشَرَ الشَّبَابِ، مَنِ اسْتَطَاعَ مِنْكُمُ الْبَاءَةَ فَلْيَتَزَوَّجْ ، وَمَنْ لَمْ يَجِدْ فَعَلَيْهِ بِالصَّوْمِ فَإِنَّهُ لَهُ وِجَاءٌ"
“Enyi rika la vijana! Atakayeweza gharama za kuolea miongoni mwenu basi aoe, kwani kuoa kunaliinamisha jicho na kunailinda tupu, na ambaye hatoweza, basi afunge, kwani funga kwake ni kata kiu ya matamanio ya jimai”. [Hadiyth Swahiyh. Al-Bukhaariy (5065) na Muslim (1400)]
8- Abu Dharr: “Nabiy (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
"وَفِي بُضْعِ أَحَدِكُمْ صَدَقَةٌ، قَالُوا: يَا رَسُولَ اللَّهِ، أَيَأْتِي أَحَدُنَا شَهْوَتَهُ وَيَكُونُ لَهُ فِيهَا أَجْرٌ؟ قَالَ: أَرَأَيْتُمْ لَوْ وَضَعَهَا فِي حَرَامٍ أَكَانَ عَلَيْهِ فِيهِ وِزْرٌ؟ فَكَذَلِكَ إِذَا وَضَعَهَا فِي الْحَلَالِ كَانَ لَهُ أَجْرٌ"
“Na mmoja wenu akimuingilia mkewe anapata pia thawabu. Wakauliza: Ee Rasuli wa Allaah! Inakuwaje mmoja wetu akidhi matamanio yake halafu apate na thawabu juu!? Akawaambia: Niambieni, itakuwaje kama atayaweka katika haramu, je, si atapata madhambi kwa kufanya hivyo? Ndivyo hivyo hivyo, akiyaweka kwenye halali, basi anapata thawabu pia ”. [Hadiyth Swahiyh. Imekharijiwa na Muslim (1006) na Abu Daawuwd (1286)]
9- ‘Abdullaah bin ‘Amri: “Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
"الدُّنْيَا مَتَاعٌ، وَخَيْرُ مَتَاعِ الدُّنْيَا الْمَرْأَةُ الصَّالِحَةُ"
“Dunia ni starehe, na starehe bora zaidi ya dunia ni mwanamke mwema”. [Hadiyth Swahiyh. Muslim (1467)]
10- Sa’iyd bin Jubayr: “Ibn ‘Abbaas aliniuliza:
"هَلْ تَزَوَّجْتَ؟ قُلْتُ: لاَ. قَالَ: فَتَزَوَّجْ، فَإِنَّ خَيْرَ هَذِهِ الأُمَّةِ أَكْثَرُهَا نِسَاءً"
“Je una mke? Nikamwambia sina. Akaniambia: Basi oa, kwani mbora wa umma huu (Rasuli Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ndiye aliyeoa wake wengi zaidi”. [Isnaad yake ni Swahiyh]
Swahiyh Fiqh As-Sunnah
كِتَابُ الزَّوَاجِ
Kitabu Cha Ndoa
Alhidaaya.com [3]
02-Ni Haramu Mwanaume Kuhasiwa (Kuondoshwa Korodani Mtu Asiwe Na Matamanio Tena Ya Kujimai):
1- Sa’iyd bin Abiy Waqqaasw amesema:
"لَقَدْ رَدَّ ذَلِكَ ـ يَعْنِي النَّبِيَّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ ـ عَلَى عُثْمَانَ، وَلَوْ أَجَازَ لَهُ التَّبَتُّلَ لاَخْتَصَيْنَا".
“Hakika -(Rasuli Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam)- alimkatalia hilo ‘Uthmaan bin Madh-’uwn, na lau angelimkubalia utawa wa kutooa, basi tungelihasiwa”. [Hadiyth Swahiyh. Imekharijiwa na Al-Bukhaariy (5074) na Muslim (1402)]
Neno “tungelihasiwa”, lina maanisha kabla ya kukatazwa jambo hilo.
2- ‘Abdullaah bin Mas-‘uwd amesema:
"كُنَّا نَغْزُو مَعَ رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ وَلَيْسَ لَنَا نِسَائُنَا، فَقُلْنَا: أَلاَ نَسْتَخْصِي؟ فَنَهَانَا عَنْ ذَلِكَ، ثُمَّ رَخَّصَ لَنَا أَنْ نَنْكِحَ الْمَرْأَةَ بِالثَّوْبِ، ثُمَّ قَرَأَ عَلَيْنَا: يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لاَ تُحَرِّمُوا طَيِّبَاتِ مَا أَحَلَّ اللَّهُ لَكُمْ وَلاَ تَعْتَدُوا إِنَّ اللَّهَ لاَ يُحِبُّ الْمُعْتَدِينَ"
“Tulikuwa tunashiriki vita pamoja na Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) bila ya wake zetu. Tukashaurizana: Je, kwa nini tusihasi? Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akatukataza kufanya hilo. Kisha akaturuhusu tuoe mwanamke (kwa muda [mut’a]) hata kwa mahari ya nguo. Halafu akatusomea:
"يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تُحَرِّمُوا طَيِّبَاتِ مَا أَحَلَّ اللَّـهُ لَكُمْ وَلَا تَعْتَدُوا ۚ إِنَّ اللَّـهَ لَا يُحِبُّ الْمُعْتَدِينَ"
“Enyi walioamini! Msiharamishe vilivyo vizuri Alivyokuhalalishieni Allaah, na wala msipindukie mipaka. Hakika Allaah Hapendi wapindukao mipaka”. [Hadiyth Swahiyh. Imekharijiwa na Al-Bukhaariy (5075)]
Kuhasiwa mwanadamu ni haramu bila makhitilafiano baina ya ‘Ulamaa.
Swahiyh Fiqh As-Sunnah
كِتَابُ الزَّوَاجِ
Kitabu Cha Ndoa
Alhidaaya.com [3]
03-Baadhi Ya Faida Za Kuoa:
1- Ni kutekeleza Amri ya Allaah Ta’aalaa.
2- Ni kufuata Sunnah ya Nabiy (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Mitume waliotangulia.
3- Kunavunja matamanio ya jimai na kuyainamisha chini macho.
4- Kunalinda tupu na zinaa na kuwaheshimisha wanawake.
5- Kunazuia kuenea zinaa na machafu kwa Waislamu.
6- Kunaongeza idadi ya Waislamu ambao Nabiy (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) atajifaharisha kwa wingi wao kwa Manabii na umma zilizotangulia.
7- Kwa jimai ya halali, mke na mume hulipwa thawabu na Allaah.
8- Kunawakilisha jambo alilolipenda Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) aliyesema:
"حُبِّبَ إِلَىَّ مِنْ دُنْيَاكُمْ الطِّيبُ والنِّسَاءُ"
“Nimependezeshwa katika dunia yenu mafuta mazuri na wanawake”. [Imekharijiwa na An-Nasaaiy (7/61), Ahmad (3/285) na wengineo. Kuna maneno kuhusiana na Sanad yake]
9- Kunawezesha kupata watoto ambao watawafaa wazazi kwa du’aa baada ya kufariki.
10- Kunapelekea kuingia Peponi kutokana na uombezi wa watoto. Swahaba mmoja alimsikia Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akisema:
"يُقَالُ لِلْوَلَدَانِ يَوْمَ القِيَامَةِ: ادْخُلُوا الجَنَّةَ، قَالَ: فَيَقُوْلُونَ: يا رَبّ حَتَّى يَدْخُلَ آبَاؤُنَا وأُمَّهَاتُنَا، قَالَ: فَيَأْتُوْنَ، قَالَ: فَيَقُولُ اللهُ عزَّ وجَلَّ: مَالِيْ أَرَاهُمْ مُحْبَنْطِئِيْنَ ادْخُلُوا الجَنَّةَ، قَالَ: فَيَقُوْلُونَ: يا رَبّ آبَاؤُنَا وأُمَّهَاتُنَا، قَالَ: فَيَقُولُ: ادْخُلُوا الجَنَّةَ أَنْتُمْ وآباؤُكُم"
“Watoto wataambiwa waingie Peponi Siku ya Qiyaamah lakini watasema: Ee Rabbi wetu, mpaka waingie baba zetu na mama zetu. Wazazi wao wataletwa, na Allaah Ta’aalaa Atasema: Mbona nawaona wamevimba kwa hasira, ingieni Peponi. Watasema: Ee Rabbi wetu, baba zetu na mama zetu. Allaah Atawaambia: Ingieni Peponi nyinyi na wazazi wenu”. [Hadiyth Hasan. Imekharijiwa na Ahmad (4/105)]
11- Kunapatikana kizazi cha Waumini watakaolinda nchi za Kiislamu na kuwaombea maghfira Waumini.
12- Yanapatikana mapenzi, huruma na utulivu kati ya mke na mume na manufaa mengineyo ambayo Allaah Ta’aalaa Pekee Anayajua.
Swahiyh Fiqh As-Sunnah
كِتَابُ الزَّوَاجِ
Kitabu Cha Ndoa
Alhidaaya.com [3]
04-Hukumu Ya Kuoa:
Waislamu wote kwa itifaki wamekubaliana kwamba kuoa ni jambo la halali, kisha ‘Ulamaa wakakhitilafiana kuhusu hukmu yake katika kauli tatu:
Ya kwanza: Ni wajibu kwa kila mwenye uwezo mara moja tu katika maisha yote. Ni madhehebu ya Daawuwd Adh-Dhwaahiriy na Ibn Hazm, na pia ni kauli ya baadhi ya Salaf. Dalili yao ni amri zilizoelezwa kwenye baadhi ya Aayaat na Hadiyth zilizotangulia ambazo zinaraghibisha kuoa. Wamesema asili ya amri hizo ni uwajibu, kwa kuwa hakuna matini nyingine zilizozitoa nje ya duara hilo.
Ya pili: Ni jambo linalopendeza. Ni madhehebu ya ‘Ulamaa walio wengi, Jumhuwr ya Maimamu wanne na wengineo.
Wamezichukulia amri za kuoa kama ni za himizo la jambo linalopendeza. Wakasema katika Kauli Yake Ta’aalaa:
"فَانكِحُوا مَا طَابَ لَكُم مِّنَ النِّسَاءِ"
“Basi oeni waliokupendezeni katika wanawake wengine”, kwamba Allaah Ta’aalaa Amelifungamanisha jambo la kuoa na mtu kupendezewa nalo. Hivyo basi, ambaye nafsi yake haikupendezwa na kuoa, basi hakuna ubaya kwake. Na hapo hapo, Allaah Akasema:
"مَثْنَىٰ وَثُلَاثَ وَرُبَاعَ"
“Wawili au watatu au wanne”, na hili si wajibu kwa itifaki ya ‘Ulamaa, hivyo basi inaonyesha kwamba jambo lenyewe si faradhi, bali linapendeza.
Hoja yao imejibiwa kwamba lililofungamanishwa na kupendezewa ni amri ya kuoa zaidi ya mke mmoja, yaani inapendeza mtu kuongeza wa pili, wa tatu n.k, na si kwa asili ya ndoa yenyewe ya mke mmoja.
Jumhuwr wamesema: Vile vile Kauli Yake Ta’aalaa:
"فَوَاحِدَةً أَوْ مَا مَلَكَتْ أَيْمَانُكُمْ"
basi mmoja tu au ambao mikono yenu ya kulia imewamiliki. [An-Nisaa: 03]
Ya tatu: Hukmu yake inatofautiana kwa mujibu wa hali ya mtu. Hili ni mashuhuri kwa Wamaalik, Mashaafi’i na Mahanbali. Wamesema:
(a) Ndoa inakuwa ni waajib kwa mtu ambaye ana hamu na kiu ya tendo la kujimai na anajihofia kufanya zinaa kama hatooa. Mtu huyu ni lazima aizuie nafsi yake na haramu, na njia ya kuzuia ni kuoa, kwani jambo ambalo wajibu hautimii ila kwalo, basi linakuwa ni lazima.
(b) Ndoa inakuwa ni jambo lenye kupendeza kwa mtu mwenye hamu ya jimai lakini ana uwezo wa kujidhibiti asiweze kufanya zinaa. Mtu huyu kuoa kwake inakuwa ni bora zaidi kuliko kujikita kwenye ibada za sunnah. Hii ni kauli ya Jumhuwr, kinyume na Ash-Shaafi’iy, yeye anasema kujikita kwenye ibada za sunnah ni bora zaidi kuliko kuoa katika hali hii.
(c) Ndoa inakuwa ni haramu kwa mtu ambaye hajiwezi kwa tendo la ndoa na mkewe, lakini pia uwezo wake ni duni mno katika matumizi ya maisha.
Ninasema: “Kuoa ni moja kati ya sunnah zilizokokotezwa mno. Ndoa ni mwenendo wa Mitume wote kama tulivyoona katika Aayaat na Hadiyth zilizotangulia ambazo zinaraghibisha jambo hili. Na hapana shaka kuwa kama mtu atahofia kuzini na uwezo wa kuoa anao, basi itakuwa ni waajib kuoa. Ama kufanya baadhi ya vigawanyo vyake kuwa ni jambo mubaah, hii inakuwa ni kuzikinga dalili na kuyarejesha maraghibisho mengi yaliyotajwa kwenye Qur-aan na Sunnah. Kadhalika, haifai kuifanya ndoa kuwa haramu kwa asiyejiweza katika tendo la ndoa, kwani ndoa ina malengo mengineyo ambayo yanaweza kupatikana ikiwa mke ataridhia udhaifu huo wa mume wake. Allaah Ndiye Ajuaye zaidi”.
Swahiyh Fiqh As-Sunnah
كِتَابُ الزَّوَاجِ
Kitabu Cha Ndoa
Alhidaaya.com [3]
05-Mwanamke Anaweza Kukataa Kuolewa:
Ni kwa Hadiyth y a Abu Sa’iyd:
"إِنَّ رَجُلاً أَتَى بابْنَةٍ له إِلى النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ فَقَالَ: إِنَّ ابْنَتِي هذه أَبَتْ أَنْ تَتَزَوَّجَ، قَالَ: فَقَالَ لَهَا: أَطِيْعِيْ أَبَاكِ، فَقَالَت: لا، حَتَّى تُخْبِرَنِي ما حَقُّ الزَّوْجِ على زَوْجَتِهِ؟ فَرَدَّتْ عليه مَقَالَتَهَا، فَقَالَ: حَقُّ الزَّوْجِ على زَوْجَتِه: أَنْ لَوْ كَانَ به قُرْحَةً فَلَحَسَتْهَا أَوْ ابْتَدَرَ منخراه صَدِيْدًا أَوْ دَمًا ثُمَّ لَحَسَتْهُ مَا أَدَّتْ حَقَّهُ، فَقَالَتْ: وَالذيْ بَعَثَكَ بالحق، لا أتَزَوَّجُ أَبَدًا، فَقَالَ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: لا تُنْكِحُوْهُنَّ إِلاَّ بإِذْنِهِنَّ"
“Mtu mmoja alikwenda na binti yake kwa Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akamwambia: Binti yangu huyu amekataa kuolewa. Rasuli akamwambia binti: Mtii baba yako. Binti akasema: Sikubali, mpaka unieleze ni ipi haki ya mke kumtekelezea mumewe? Akakariri maneno hayo kwa Rasuli. Rasuli akamwambia: Haki ya mke kumtekelezea mumewe ni kuwa, ikiwa mumewe ana kidonda naye akakipangusa kwa ulimi wake, au kikatumbuka usaha au damu kisha akailamba, basi anakuwa bado hajatekeleza haki yake. Binti akasema: Naapa kwa Yule Ambaye Amekutuma kwa haki, kamwe sitoolewa. Na Rasuli akasema: Msiwaozeshe isipokuwa kwa ridhaa yao”. [Hadiyth Hasan. Imekharijiwa na Ibn Abiy Shaybah (17116)]
Swahiyh Fiqh As-Sunnah
كِتَابُ الزَّوَاجِ
Kitabu Cha Ndoa
Alhidaaya.com [3]
06-Wanawake Ambao Ni Haramu Kuwaoa:
Wanawake hawa Allaah Ta’aalaa Amewataja katika Aayaah hizi tatu:
"وَلَا تَنكِحُوا مَا نَكَحَ آبَاؤُكُم مِّنَ النِّسَاءِ إِلَّا مَا قَدْ سَلَفَ ۚ إِنَّهُ كَانَ فَاحِشَةً وَمَقْتًا وَسَاءَ سَبِيلا ● حُرِّمَتْ عَلَيْكُمْ أُمَّهَاتُكُمْ وَبَنَاتُكُمْ وَأَخَوَاتُكُمْ وَعَمَّاتُكُمْ وَخَالَاتُكُمْ وَبَنَاتُ الْأَخِ وَبَنَاتُ الْأُخْتِ وَأُمَّهَاتُكُمُ اللَّاتِي أَرْضَعْنَكُمْ وَأَخَوَاتُكُم مِّنَ الرَّضَاعَةِ وَأُمَّهَاتُ نِسَائِكُمْ وَرَبَائِبُكُمُ اللَّاتِي فِي حُجُورِكُم مِّن نِّسَائِكُمُ اللَّاتِي دَخَلْتُم بِهِنَّ فَإِن لَّمْ تَكُونُوا دَخَلْتُم بِهِنَّ فَلَا جُنَاحَ عَلَيْكُمْ وَحَلَائِلُ أَبْنَائِكُمُ الَّذِينَ مِنْ أَصْلَابِكُمْ وَأَن تَجْمَعُوا بَيْنَ الْأُخْتَيْنِ إِلَّا مَا قَدْ سَلَفَ ۗ إِنَّ اللَّـهَ كَانَ غَفُورًا رَّحِيمًا ● وَالْمُحْصَنَاتُ مِنَ النِّسَاءِ إِلَّا مَا مَلَكَتْ أَيْمَانُكُمْ ۖ كِتَابَ اللَّـهِ عَلَيْكُمْ ۚ وَأُحِلَّ لَكُم مَّا وَرَاءَ ذَٰلِكُمْ أَن تَبْتَغُوا بِأَمْوَالِكُم مُّحْصِنِينَ غَيْرَ مُسَافِحِينَ ۚ فَمَا اسْتَمْتَعْتُم بِهِ مِنْهُنَّ فَآتُوهُنَّ أُجُورَهُنَّ فَرِيضَةً ۚ وَلَا جُنَاحَ عَلَيْكُمْ فِيمَا تَرَاضَيْتُم بِهِ مِن بَعْدِ الْفَرِيضَةِ ۚ إِنَّ اللَّـهَ كَانَ عَلِيمًا حَكِيمًا"
“Na wala msiwaoe wanawake waliowaoa baba zenu isipokuwa yaliyokwisha pita. Hakika hayo yalikuwa ni uchafu na chukizo na njia ovu• Mmeharamishiwa (kuwaoa) mama zenu, na mabinti zenu, na dada zenu, na shangazi zenu, na makhalati zenu (mama wakubwa na wadogo), na mabinti wa kaka, na mabinti wa dada, na mama zenu ambao wamekunyonyesheni, na dada zenu kwa kunyonya, na mama wa wake zenu, na watoto wenu wa kambo walio katika ulinzi wenu waliozaliwa na wake zenu ambao mmewaingilia● Lakini ikiwa hamkuwaingilia basi hakuna dhambi (kuwaoa). Na (mmeharamishwa) wake wa watoto wenu waliotoka katika migongo yenu, na kuwaoa dada wawili kwa wakati mmoja, isipokuwa yaliyokwisha pita. Hakika Allaah daima Ni Mwingi wa Kughufiria, Mwenye Kurehemu. Na (Mmeharamishiwa pia) wanawake walio katika ndoa isipokuwa iliyowamiliki mikono yenu ya kuume. Ni Shariy’ah ya Allaah kwenu. Na mmehalalishiwa wengineo wasiokuwa hao, mtafute (kuwaoa) kwa mali zenu mkijistahi pasi na kuzini. Basi mliostarehe nao, wapeni mahari yao kuwa ni waajib. Na wala si dhambi kwenu katika mliyoridhiana baada ya kukamilika ya wajibu. Hakika Allaah daima Ni Mjuzi wa yote, Mwenye hikmah wa yote.” [An-Nisaa: 22-24]
Wanawake hawa walioharamishwa wako aina mbili:
1- Walioharamishwa kuwaoa milele. Hawa mwanaume haruhusiwi kuwaoa abadani.
2- Walioharamishwa kwa muda. Hawa mwanaume haruhusiwi kuwaoa wanapokuwa katika hali maalum, na hali hii inapoondoka, hapo wanahalalika.
Swahiyh Fiqh As-Sunnah
كِتَابُ الزَّوَاجِ
Kitabu Cha Ndoa
Alhidaaya.com [3]
07-Wanawake Walioharamika Kuwaoa Milele: Walio Haramu Kwa Sababu Ya Nasaba (Hawa Ni Saba):
1- Mama (wamama): Hawa ni wale ambao kuna fungamano la uzao kati yao na mwanaume kwa upande wa mama au baba. Ni kama mama zake, mama za baba zake na mababu zake kwa upande wa kuumeni na kikeni na kwenda juu.
2- Mabinti: Hawa ni wale walionasibishwa kwa mtu kwa kuwazaa. Ni kama mabinti zake aliowazaa yeye, au mabinti wa binti zake (wajukuu) na kwenda chini.
3- Madada: Hawa ni wa pande zote.
4- Mashangazi: Hawa ni dada wa baba na kwenda juu. Hapa anaingia pia shangazi ya baba yake na shangazi ya mama yake.
5- Makhalati: Hawa ni dada za mama yake au mama wa baba zake (mabibi).
6,7- Mabanati wa kaka na mabanati wa dada. Hawa ni kutoka pande zote hata kama daraja yao itashuka.
Ibn ‘Abbaas amesema:
"حُرِّمَ مِنَ النَّسَبِ سَبْعٌ وَمِنَ الصِّهْرِ سَبْعٌ، ثُمَّ قَرَأَ: حُرِّمَتْ عَلَيْكُم أُمَّهَاتكُم [الْآيَة]"
“Walioharamishwa kwa sababu ya nasaba ni saba, na kutokana na uhusiano wa ndoa ni saba”. Kisha akasoma aayaah ya 23 ya Suwrat An-Nisaa. [Al-Bukhaariy (5105) na At-Twabariy katika “At-Tafsiyr” (8/141), na Al-Haakim (2/304)]
Na ili kulijua suala hili kwa wepesi, kidhibiti chake ni: “Kwamba akaribu wote wa mwanaume kwa upande wa nasaba ni haramu kwake ila wanne: Mabanati wa ami yake, mabanati wa mjomba wake, mabanati wa shangazi yake na mabanati wa khalati yake”.
Wanne hawa, Allaah Ta’aalaa Alimhalalishia Rasuli Wake (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) Alipomwambia:
"يَا أَيُّهَا النَّبِيُّ إِنَّا أَحْلَلْنَا لَكَ أَزْوَاجَكَ اللَّاتِي آتَيْتَ أُجُورَهُنَّ وَمَا مَلَكَتْ يَمِينُكَ مِمَّا أَفَاءَ اللَّـهُ عَلَيْكَ وَبَنَاتِ عَمِّكَ وَبَنَاتِ عَمَّاتِكَ وَبَنَاتِ خَالِكَ وَبَنَاتِ خَالَاتِكَ اللَّاتِي هَاجَرْنَ مَعَكَ"
“Ee Nabiy! Hakika Sisi Tumekuhalalishia wake zako ambao uliwapa mahari yao, na wale iliyomiliki mkono wako wa kuume katika wale (mateka) Aliokuruzuku Allaah, na mabinti wa ‘ammi zako, na mabinti wa mashangazi zako, na mabinti wa wajomba zako, na mabinti wa makhalati zako ambao wamehajiri pamoja nawe”. [Al-Ahzaab: 50]
Swali: Je, Inafaa Mtu Kumwoa Binti Yake Wa Zinaa?
Jumhuwr ya ‘Ulamaa wanaona kwamba haijuzu mtu kumwoa binti yake wa zinaa. Wanasema kuwa binti huyu anaingia ndani ya Kauli Yake Ta’aalaa:
"حُرِّمَتْ عَلَيْكُمْ أُمَّهَاتُكُمْ وَبَنَاتُكُمْ"
“Mmeharamishiwa (kuwaoa) mama zenu, na mabinti zenu”. [An-Nisaa: 23]
Bali hata Jumhuwr wamevutana vikali kuhusiana na mtu aliyemwoa binti yake wa zinaa, je huyu atauawa au la? Ahmad amesema atauawa!!
Katika kesi hii, ni haramu pia mtu kumwoa dada yake wa zinaa, au binti ya mtoto wake wa kiume wa zinaa, au binti ya binti yake wa zinaa, au binti ya kaka yake au dada yake wa zinaa. Hii ni kauli ya ‘Ulamaa wote.
Swahiyh Fiqh As-Sunnah
كِتَابُ الزَّوَاجِ
Kitabu Cha Ndoa
Alhidaaya.com [3]
08-Walioharamishwa Kwa Sababu Ya Uhusiano Wa Ndoa (Hawa Ni Wanne):
1- Mke wa baba:
Ibn ‘Abbaas:
"كَانَ أَهْلُ الجَاهِلِيَّةِ يُحَرَمُوْنَ مَا يَحْرُمُ إِلا امْرَأَةَ الأبِ والجَمْعُ بَيْنَ الأُخْتَيْن، قَالَ: فَأَنْزَلَ اللهُ عَزَّ وَجَلَّ: وَلَا تَنكِحُوا مَا نَكَحَ آبَاؤُكُم مِّنَ النِّسَاءِ إِلَّا مَا قَدْ سَلَفَ وَأَن تَجْمَعُوا بَيْنَ الْأُخْتَيْنِ"
“Watu wa enzi ya ujahili walikuwa wanaharamisha yaliyo haramu isipokuwa mke wa baba na kuoa dada wawili kwa wakati mmoja, hili lilikuwa halali. Allaah ‘Azza wa Jalla Akateremsha: “Na wala msiwaoe wanawake waliowaoa baba zenu isipokuwa yaliyokwisha pita”. Na Kauli Yake: “Na kuwaoa dada wawili kwa wakati mmoja”. [Tafsiyr At-Twabariy (8/132) kwa Sanad Swahiyh]
Katika Aayah tajwa ya kwanza, Allaah Ta’aalaa Amekataza mtu kumwoa mwanamke ambaye aliolewa na baba yake. Lakini Allaah Hakubainisha kusudio la neno “nikaah” kwa baba, je ni kufunga naye ndoa, au kumuingilia? ‘Ulamaa kwa upande wao wamesema kwa sauti moja kwamba mwanamke aliyefunga ndoa na baba, ni haramu kuolewa na mtoto wake wa kiume hata kama baba hajamuingilia, na uharamu huu unakuwa ni wa milele. Na pia ni haramu kwa baba kumwoa mwanamke ambaye mtoto wake wa kiume amefunga naye ndoa hata kama hakumgusa.
Al-Baraa amesema:
"لَقِيْتُ عَمِّي وَمَعَهُ رَايَةٌ فَقُلْتُ: أَيْنَ تُرِيدُ؟ فَقَالَ: بَعَثَنِي رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ إِلَى رَجُلٍ نَكَحَ امْرَأَةَ أَبِيهِ فَأَمَرَنِي أَنْ أَضْرِبَ عُنُقَهُ وَآخُذَ مَالَهُ"
“Nilikutana na ami yangu akiwa na bendera, nikamuuliza: Unaelekea wapi? Akasema: Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amenituma niende kwa mtu ambaye amemwoa mke wa baba yake. Ameniamuru nimfyeke shingo na nitwae mali yake”. [Swahiyh Lishawaahidihi. Imkekharijiwa na Abu Daawuwd (4457), Ad-Daaramiy (2/153), Al-Haakim (4/357) na Al-Bayhaqiy (8/208). Sheikh wetu amesema ni Swahiyh]
Adhabu ya mwenye kumwoa mke wa baba yake ni kuuawa na kutwaliwa mali yake kwa mujibu wa Hadiyth hii.
2- Mama wa mke (mama mkwe):
Mtu akishafunga tu ndoa na binti, basi mama ya binti anakuwa ni haramu kwake kumwoa kwa mujibu wa kauli ya Jumhuwr ya ‘Ulamaa. Na hii ni kwa Neno Lake Ta’aalaa:
"وَأُمَّهَاتُ نِسَائِكُمْ"
“Na mama za wake zenu”. [An-Nisaa: 23]
Mwanaume akimuingilia mke wake, basi mama yake anakuwa ni haramu kwake. Na hapa anaingia vile vile mama ya mama wa mkewe, na mama ya baba yake.
3- Binti ya mke (binti wa kambo):
Sharti ya kuharamika, ni mwanaume kumuingilia mama ya binti. Ikiwa mama yake atafunga ndoa na mtu, na mtu huyu asiwahi kumuingilia, basi mtu huyu anaweza kumwoa binti yake. Na hii ni kwa Kauli Yake Ta’aalaa:
"وَرَبَائِبُكُمُ اللَّاتِي فِي حُجُورِكُم مِّن نِّسَائِكُمُ اللَّاتِي دَخَلْتُم بِهِنَّ فَإِن لَّمْ تَكُونُوا دَخَلْتُم بِهِنَّ فَلَا جُنَاحَ عَلَيْكُمْ"
“Na watoto wenu wa kambo (wa kike) walio katika ulinzi wenu waliozaliwa na wake zenu ambao mmewaingilia ● Lakini ikiwa hamkuwaingilia basi hakuna dhambi (kuwaoa)”. [An-Nisaa: 23]
Ninasema: “Kauli yenye nguvu ya ‘Ulamaa ni kwamba Kauli Yake Ta’aalaa:
"اللَّاتِي فِي حُجُورِكُم"
(walio chini ya ulinzi wenu)
kwa maana ya wanaoishi nanyi katika nyumba zenu, hili halizingatiwi kuwa ni sharti la kuharamisha kumwoa binti ya mke, bali uharamu unabaki pale pale hata kama ataishi mbali na mama yake. Kuishi mama na bintiye au wanawe kiujumla ndilo jambo lililozoeleka zaidi. Linalotilia nguvu haya, ni kwamba Allaah Ta’aalaa Ameweka wazi kwa kusema:
"فَإِن لَّمْ تَكُونُوا دَخَلْتُم بِهِنَّ"
(Lakini ikiwa hamkuwaingilia)
na Hakusema:
"فَإِنْ لَمْ يَكُنَّ في حُجُوْرِكُمْ"
(Lakini ikiwa hawako chini ya ulezi wenu),
kwa maana kuwa kumuingilia mama yake ni sharti kuu ya kuharamika kumwoa binti na si kuishi kwake ndani ya nyumba ya mume wa mama yake. Allaah Ndiye Ajuaye zaidi”.
Wanajumuishwa kwenye hukumu hii mabinti wa mabinti wa mke na mabinti wa watoto wake wa kiume.
4- Mke wa mtoto wa kiume wa kutoka mgongoni mwako:
Haijuzu mwanaume kumwoa mke wa mtoto wake wa kiume wa kutoka mgongoni kwake kutokana na Neno Lake Ta’aalaa:
"وَحَلَائِلُ أَبْنَائِكُمُ الَّذِينَ مِنْ أَصْلَابِكُمْ"
“Na (mmeharamishwa) wake wa watoto wenu waliotoka katika migongo yenu”.
Anaingia ndani ya Aayaah hii vile vile mke wa mtoto wa kiume wa kunyonya. Ama Neno Lake Ta’aalaa:
"الَّذِينَ مِنْ أَصْلَابِكُمْ"
“Waliotoka katika migongo yenu”,
kwa kusema hivi, Allaah Amewatoa kando watoto wa kupanga ambao watu walikuwa wakiwalea na kuwafanya kama watoto wao wa damu wakati wa enzi ya ujahili. Na hii pia inabainishwa wazi na Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) aliposema:
"يَحْرُمُ مِنْ اَلرَّضَاعَةِ مَا يَحْرُمُ مِنْ اَلنَّسَبِ"
“Lililo haramu kwa sababu ya kunyonya ni haramu pia kwa sababu ya nasaba”. [Angalia Tafsiyr Ibn Kathiyr (1/471), At-Twabariy (8/149) na Al-Ummu (5/35)]
Faida:
Mabinti wa mke wa baba na mke wa mtoto wa kiume, ni ruksa kwa mtu kuwaoa, yaani, inafaa mtu kumwoa binti ya mke wa baba yake, na binti wa mke wa mtoto wake wa kiume. Na hii ni kwa mujibu wa itifaki ya ‘Ulamaa.
Na ili kuwahifadhi kirahisi wanawake walioharamishwa kwa sababu ya ukwe, tunaweza kusema: Wanawake wote wanaotokana na uhusiano wa ndoa ni halali kwa mwanaume isipokuwa wanne: Mke wa baba yake, mama wa mke wake, binti ya mkewe ambaye amemuingilia, na mke wa mwanaye.
Swahiyh Fiqh As-Sunnah
كِتَابُ الزَّوَاجِ
Kitabu Cha Ndoa
Alhidaaya.com [3]
09-Walioharamishwa Kwa Sababu Ya Kunyonya:
Allaah Ta’aalaa Amesema:
"وَأُمَّهَاتُكُمُ اللَّاتِي أَرْضَعْنَكُمْ وَأَخَوَاتُكُم مِّنَ الرَّضَاعَةِ"
“Na mama zenu ambao wamekunyonyesheni, na dada zenu kwa kunyonya”. [An-Nisaa: 23]
Na neno lake Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kuhusiana na binti ya Hamzah:
"إِنَّهَا لَا تَحِلُّ لِي، إِنَّهَا اِبْنَةُ أَخِي مِنْ اَلرَّضَاعَةِ، وَيَحْرُمُ مِنْ اَلرَّضَاعَةِ مَا يَحْرُمُ مِنْ اَلنَّسَبِ"
“Yeye si halali kwangu, ni binti ya kaka yangu wa kunyonya, na lililo haramu kwa sababu ya kunyonya ni haramu pia kwa sababu ya nasaba”. [Al-Bukhaariy (2645) na Muslim (1447)]
Kwa Hadiyth hii, tunapata kujua kwamba walioharamishwa kutokana na kunyonya ni wale wale walioharamishwa kutokana na unasaba. Na pia, mwanamke mnyonyeshaji, anawekwa daraja moja na mama mzazi, yaani anakuwa ni kama mama mzazi. Hivyo basi, wanawake walioharamishwa kwa mwanaume kwa sababu ya kunyonya ni hawa wafuatao:
1- Mwanamke aliyemnyonyesha, na mama yake mzazi (hawa wanakuwa ni mama zake).
2- Mabinti wa mwanamke aliyemnyonyesha, ni sawa waliozaliwa kabla yake au baada yake (hawa watakuwa ni dada zake).
3- Dada wa aliyemnyonyesha (huyu anakuwa ni khalati yake).
4- Binti ya binti wa aliyemnyonyesha (huyu anakuwa ni binti ya dada yake).
5- Mama ya mume wa mnyonyeshaji ambaye maziwa yake yamepatikana kutokana na mimba iliyotokana na mume huyo (mama huyo anakuwa ni bibi yake).
6- Dada ya mume wa mnyonyeshaji (huyu anakuwa ni shangazi yake).
7- Binti ya mtoto wa kiume wa mnyonyeshaji (huyu ni binti ya kaka yake).
8- Binti ya mume wa mnyonyeshaji hata kama ni wa mke mwingine (huyu ni dada wa kunyonya kutokana na baba).
9- Dada za mume wa mnyonyeshaji (hawa ni mashangazi zake).
10- Mke mwingine wa mume wa mnyonyeshaji (huyu ni mke wa baba yake).
11- Mke wa mtoto aliyenyonya ni haramu kwa mume wa mnyonyeshaji (huyu ni mke wa mtoto wake).
Kwa kuwa sababu ya uharamisho ni maziwa ambayo yanapatikana kwa mwanamke kutokana na mimba aliyoipata kutokana na mumewe. Na mtoto anapoyanyonya, anakuwa ni sehemu ya sehemu za anayemnyonyesha.
Kati ya yanayoonyesha hayo, ni kwamba Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alimwamuru ‘Aaishah amruhusu kuingia kwake Aflah kaka wa Abul Qa’iys ambaye ni ami yake wa kunyonya. [Al-Bukhaariy (5103) na Muslim (1445)]
Imenukuliwa kwamba Ibn ‘Abbaas:
"سُئِلَ عَنْ رَجُلٍ، كَانَتْ لَهُ امْرَأَتَانِ فَأَرْضَعَتْ إِحْدَاهُمَا غُلاَمًا وَأَرْضَعَتِ الأُخْرَى جَارِيَةً فَقِيلَ لَهُ هَلْ يَتَزَوَّجُ الْغُلاَمُ الْجَارِيَةَ؟ فَقَالَ لاَ، اللِّقَاحُ وَاحِدٌ"
“Aliulizwa kuhusu mtu mwenye wake wawili. Mke mmoja akamnyonyesha mtoto wa kiume mtumwa na mwingine binti kijakazi. Je, mtoto huyo anaweza kumwoa binti kijakazi? Akasema hapana, kwa sababu mume ni mmoja”. [Maalik (2/602), At-Tirmidhiy (1149) na wengineo kwa Sanad Swahiyh iliyoishia kwa Ibn ‘Abbaas]
Hii ndio kauli ya Maswahaba na Fuqahaa wote. [Al-Ummu (5/34), Al-Badaai’u (4/3), Al-Mughniy (6/572), na Jaami’u Ahkaamin Nisaa (3/53)]
12- Ikiwa mwenye kunyonyeshwa ni binti, basi mume wa mwanamke mnyonyeshaji haruhusiwi kumwoa (huyu ni baba yake), na kaka wa mume wa mwanamke mnyonyeshaji (huyu ni ami yake), na baba yake (huyu ni babu yake).
Faida:
Uharamu unamhusu tu mtoto aliyenyonya na wala haumhusu yeyote katika nduguze. Kwa mfano, dada yake wa kunyonya hawi ni dada wa kaka yake. Qaaidah katika hili inasema: “Walionyonya ziwa moja wanakuwa ni ndugu”. Kwa mfano, kaka wa aliyenyonyeshwa ambaye hakunyonya naye ziwa moja, anaruhusiwa kumwoa binti ya mwanamke aliyemnyonyesha kaka yake, kwa kuwa binti huyu anazingatiwa kuwa ni ajnabiya kwake ingawa ni dada wa kaka yake kwa kunyonya. Allaah Ndiye Ajuaye zaidi.
Swahiyh Fiqh As-Sunnah
كِتَابُ الزَّوَاجِ
Kitabu Cha Ndoa
Alhidaaya.com [3]
10-Masharti Ya Uharamu (Umahram) Kwa Sababu Ya Kunyonya: Idadi Ya Manyonyesho Ya Kuleta Uharamu (Umahram): Kauli Ya Kwanza:
‘Ulamaa wamekhitilafiana kuhusu idadi ya manyonyesho ya kufikisha kwenye uharamu ambayo yanathibiti kwayo hukmu ya kunyonya katika kauli nne:
Ya kwanza:
Nyonyesho moja na zaidi linaharamisha. Ni kauli ya Jumhuwr, Ibn Al-Musayyib, Al-Hasan, Az-Zuhriy, Qataadah, Al-Awzaaiy, Ath-Thawriy na Al-Layth. Dalili zao ni:
1- Ujumuishi wa Kauli Yake Ta’aalaa:
"وَأُمَّهَاتُكُمُ اللَّاتِي أَرْضَعْنَكُمْ وَأَخَوَاتُكُم مِّنَ الرَّضَاعَةِ"
“Na mama zenu ambao wamekunyonyesheni, na dada zenu kwa kunyonya”. [An-Nisaa: 23]
2- Ujumuishi wa kauli ya Nabiy (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam):
"إِنَّما الرَّضَاعَةُ مِنَ المَجَاعَةِ"
“Nyonyesho kamili ni lile la (kumshibisha) mtoto mwenye njaa”. [Al-Bukhaariy (5102) na Muslim (1455)]
3- Neno lake Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam):
"يَحْرُمُ مِنَ اَلرَّضَاعِ مَا يَحْرُمُ مِنْ اَلنَّسَبِ"
“Lililo haramu kwa sababu ya kunyonya ni haramu pia kwa sababu ya nasaba”. [Hadiyth Swahiyh. Imetajwa nyuma]
4- Hadiyth ya ‘Uqbah bin Al-Haarith aliyesema:
"تَزَوَّجْتُ امْرَأَةً فَجَاءَتْنَا امْرَأَةٌ سَوْدَاءُ فَقَالَتْ إِنِّي قَدْ أَرْضَعْتُكُمَا. فَأَتَيْتُ النَّبِيَّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ فَأَخْبَرْتُهُ فَقُلْتُ: إِنِّي تَزَوَّجْتُ فُلاَنَةَ بِنْتَ فُلاَنٍ فَجَاءَتْنِي امْرَأَةٌ سَوْدَاءُ فَقَالَتْ: إِنِّي قَدْ أَرْضَعْتُكُمَا. فَأَعْرَضَ عَنِّي فَأَتَيْتُهُ مِنْ قِبَلِ وَجْهِهِ فَقُلْتُ: إِنَّهَا كَاذِبَةٌ. قَالَ: وَكَيْفَ بِهَا وَقَدْ زَعَمَتْ أَنَّهَا قَدْ أَرْضَعَتْكُمَا دَعْهَا عَنْكَ"
“Nilioa mwanamke kisha akatujia mwanamke mmoja mweusi akatuambia: Nimekunyonyesheni. Nikamwendea Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) nikamwambia: Nimemwoa fulani binti fulani, halafu akatujia mwanamke mweusi akaniambia: Mimi nimewanyonyesheni, naye ni mwongo. Rasuli akanipa mgongo nami nikamjia mbele ya uso wake nikamwambia: Hakika yeye ni mwongo. Akasema: Wewe vipi unamuingilia mkewe na huyo mwanamke amedai kwamba amewanyonyesheni! Mwache mkeo”. [Al-Bukhaariy (2659), At-Tirmidhiy (1151) na An-Nasaaiy (3330)]
Wamesema kwamba Aayaat na Hadiyth hizi na nyinginezo hazikutaja idadi maalum.
5- Wamezijibu riwaayah ambazo zimeainisha idadi ya manyonyesho yenye kuharamisha (ambayo yatakuja elezewa mbeleni) kwamba idadi yake imetofautiana na ile iliyotajwa na ‘Aaishah, hivyo ni wajibu kurejea kwenye idadi ndogo zaidi iliyotajwa.
6- Toka kwa ‘Amru bin Diynaar amesema:
"أَتُحَرِّمُ رَضْعَةُ أَوْ رَضْعَتَانِ؟ فَقَالَ: مَا نَعْلَمُ الأُخْتَ من الرَّضَاعَةِ إِلا حَرَامًا، فَقَالَ رَجُلُ: إِنَّ أَمِيْرَ المُؤْمِنِيْنَ -يُرِيْدُ ابن الزُّبَيْرِ- يَزْعُمُ أَنَّهُ لا تُحَرِّمُ رَضْعَةٌ ولا رَضْعَتَانِ"
Nilimsikia Ibn ‘Umar alipoulizwa swali na mtu lisemalo: Je, nyonyesho moja linaharamisha au mawili? Akajibu: Hatumtambui dada wa kunyonya kwa jingine isipokuwa ni haramu kuolewa. Mtu yule akasema: Amiri wa Waumini -yaani Ibn Az-Zubayr- anadai kwamba nyonyesho moja au mawili hayaharamishi. Ibn ‘Umar akamwambia: Hukmu ya Allaah ni bora zaidi kuliko hukmu yako na hukmu ya Amiri wa Waumini”. [Isnadi yake ni Swahiyh. Imekharijiwa na Abdulrazzaaq (7/467) na Al-Bayhaqiy (7/458)]
7- Kwa vile kitendo hiki kinahusiana na uharamu wa milele, idadi haijazingatiwa kama ulivyo uharamu wa mama za wake.
Swahiyh Fiqh As-Sunnah
كِتَابُ الزَّوَاجِ
Kitabu Cha Ndoa
Alhidaaya.com [3]
11-Masharti Ya Uharamu (Umahram) Kwa Sababu Ya Kunyonya: Idadi Ya Manyonyesho Ya Kuleta Uharamu (Umahram): Kauli Ya Pili:
Manyonyesho matatu na zaidi yanaharamisha. Ni riwaayah ya tatu toka kwa Ahmad, kauli ya Ahlu Adh-Dhwaahir, Is-haaq, Abu ‘Ubayd, Abu Thawr na Ibn Al-Mundhir. Dalili zao ni:
1- Hadiyth ya ‘Aaishah: “Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
"لا تُحَرِّمُ اَلْمَصَّةُ وَالْمَصَّتَانِ"
“Kunyonya mtoto mara moja au mara mbili hakuharamishi”. [Hadiyth Swahiyh. Imekharijiwa na Muslim (1450), Abu Daawuwd (2063), At-Tirmidhiy (1150), An-Nasaaiy (6/101) na Ibn Maajah (1941)]
2- Hadiyth ya Ummul Fadhwl amesema:
"دَخَلَ أَعْرَابِيٌّ عَلَى نَبِيِّ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ وَهُوَ فِي بَيْتِي فَقَالَ: يَا نَبِيَّ اللَّهِ إِنِّي كَانَتْ لِي امْرَأَةٌ فَتَزَوَّجْتُ عَلَيْهَا أُخْرَى فَزَعَمَتِ امْرَأَتِي الأُولَى أَنَّهَا أَرْضَعَتِ امْرَأَتِي الْحُدْثَى رَضْعَةً أَوْ رَضْعَتَيْنِ. فَقَالَ نَبِيُّ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: لاَ تُحَرِّمُ الإِمْلاَجَةُ وَالإِمْلاَجَتَانِ"
“Bedui alikuja kwa Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) naye yuko nyumbani kwangu akasema: Ee Nabiy wa Allaah! Nilikuwa na mke halafu nikamwolelea mke mwenza. Mke wangu mkubwa akadai kwamba amemnyonyesha mke huyo mdogo nyonyesho moja au mawili. Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akasema: Nyonyesho moja au mawili hayaharamishi”. [Hadiyth Swahiyh. Imekharijiwa na Muslim (1451), Ahmad (6/339) na Al-Bayhaqiy (7/455)]
Swahiyh Fiqh As-Sunnah
كِتَابُ الزَّوَاجِ
Kitabu Cha Ndoa
Alhidaaya.com [3]
12-Masharti Ya Uharamu (Umahram) Kwa Sababu Ya Kunyonya: Idadi Ya Manyonyesho Ya Kuleta Uharamu (Umahram): Kauli Ya Tatu:
Manyonyesho matano na zaidi ndiyo yanayoharamisha. Ni madhehebu ya Ash-Shaafi’iy, Ahmad na Ibn Hazm. Ni kauli pia ya ‘Atwaa na Twaawuws. Imepokewa vile vile toka kwa ‘Aaishah, Ibn Mas-‘uwd na Ibn Az-Zubayr. Dalili ni:
1- Hadiyth ya ‘Aaishah:
" كانَ فِيمَا أُنْزِلَ مِنَ الْقُرْآنِ: عَشْرُ رَضَعَاتٍ مَعْلُومَاتٍ يُحَرِّمْنَ. ثُمَّ نُسِخْنَ بِخَمْسٍ مَعْلُومَاتٍ"
“Ilikuwa katika yaliyoteremshwa katika Qur-aan ni: “Manyonyesho kumi yaliyothibitika yanaharamisha”. Kisha yakafutwa kwa matano yaliyothibitika. Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akafariki nayo yakabaki yakisomwa kwenye Qur-aan”. [Hadiyth Swahiyh. Imekharijiwa na Muslim (1452) na Abu Daawuwd (2062)]
An-Nawawiy kasema: “Maana yake ni kwamba kufutwa manyonyesho matano kulikuja mwisho mwisho kabla ya kufariki Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi. Na kwa vile habari ya kufutwa ilikuwa haijawafikia watu wengi, waliendelea kusoma "خَمْسُ رَضَعَاتٍ" kama ni sehemu ya Qur-aan, lakini ilipowafikia baada ya hapo habari ya kufutwa, waliachana na kisomo hicho na wakakubaliana kwa pamoja kwamba hilo halisomwi”.
Ninasema: “Hii ni Qur-aan iliyofutwa kisomo lakini hukmu yake ikabakia kama Aayah ya kupigwa mawe mzinifu”.
2- Hadiyth ya ‘Aaishah kuhusiana na kisa cha Sahlah bint Suhayl, kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alimwambia:
.
"أَرْضِعِي سَالِمًا خَمْسَ رَضَعَاتٍ فَيَحْرُمُ بِلَبَنِهَا"
“Mnyonyeshe Saalim manyonyesho matano, atakuwa mahram kwa kunyonya”.
[Abdulrazzaaq ameikhariji kwa tamko hili (13886), Maalik (1284) na Ahmad (6/201). Asaaniyd zake hazikuungana, na asili yake iko kwa Muslim (1453)]
Kwa kifupi kuhusiana na Hadiyth hii ni kwamba Abu Hudhayfah bin ‘Utbah na mkewe Sahlah bint Suhayl, walimlea Saalim huyu akiwa mtoto wa kupanga kama ilivyokuwa enzi ya ujahilia na akawa kama mtoto wao wa kuzaa. Saalim akakua na kubaleghe, na hapo ikashuka Aayah ya tano ya Suwrat Al-Ahzaab iliyobatilisha uhalali wa kuwafanya watoto wa kupanga kama watoto wa kuzaa. Hapo bi Sahlah akakimbilia kwa Rasuli kutaka kujua mambo yatakuwaje kwa kuwa Saalim ameshakuwa kama ni mtoto wao wa kuzaa, anaishi nao pamoja, anakula nao, anaingia vyumbani vyao bila ukakasi wowote na kadhalika. Sasa mambo yatakuwaje? Ndipo Rasuli akamwambia amnyonyeshe manyonyesho matano na ukubwa wake huo, na hapo atakuwa mahram yake. Hii ilikuwa ni kesi maalum inayomhusu Saalim tu pasi na mwingine yeyote.
3- ‘Aaishah amesema:
"لاَ يُحَرِّمُ دُونَ خَمْسِ رَضَعَاتٍ مَعْلُومَاتٍ "
“Manyonyesho chini ya matano yaliyothibitika, hayamfanyi mtoto mwenye kunyonya kuwa mahram”. [Isnaad yake ni swahiyh]
Swahiyh Fiqh As-Sunnah
كِتَابُ الزَّوَاجِ
Kitabu Cha Ndoa
Alhidaaya.com [3]
13-Masharti Ya Uharamu (Umahram) Kwa Sababu Ya Kunyonya: Idadi Ya Manyonyesho Ya Kuleta Uharamu (Umahram): Kauli Ya Nne:
"لاَ يُحَرِّمُ إِلا عَشْرِ رَضَعَاتٍ مَعْلُومَاتٍ فَأَكْثَرَ"
“Hayaharamishi isipokuwa manyonyesho kumi na zaidi yaliyothibiti”. Hili limepokewa toka kwa ‘Aaishah na Hafswa (Radhwiya Allaah ‘anhumaa).
1- Toka kwa Saalim:
"أَنَّ عَائِشَةَ أُمَّ الْمُؤْمِنِينَ أَرْسَلَتْ بِهِ وَهُوَ يَرْضَعُ إِلَى أُخْتِهَا أُمِّ كُلْثُومٍ بِنْتِ أَبِي بَكْرٍ الصِّدِّيقِ فَقَالَتْ: أَرْضِعِيهِ عَشْرَ رَضَعَاتٍ حَتَّى يَدْخُلَ عَلَىَّ. قَالَ سَالِمٌ: فَأَرْضَعَتْنِي أُمُّ كُلْثُومٍ ثَلاَثَ رَضَعَاتٍ ثُمَّ مَرِضَتْ فَلَمْ تُرْضِعْنِي غَيْرَ ثَلاَثِ رَضَعَاتٍ فَلَمْ أَكُنْ أَدْخُلُ عَلَى عَائِشَةَ مِنْ أَجْلِ أَنَّ أُمَّ كُلْثُومٍ لَمْ تُتِمَّ لِي عَشْرَ رَضَعَاتٍ"
“Kwamba Mama wa Waumini ‘Aaishah alimpeleka -akiwa ananyonya- kwa dada yake Ummu Kulthum bint Abi Bakr As-Swiddiyyq na kumwambia: Mnyonyeshe manyonyesho kumi ili aweze kuingia kwangu. Saalim anasema: Ummu Kulthum akaninyonyesha mara tatu halafu akaugua, na hakuninyonyesha tena isipokuwa mara hizo tatu. Sikuwa nikiingia kwa ‘Aaishah kutokana na kwamba Ummu Kulthum hakunikamilishia manyonyesho kumi”. [Isnaad yake ni swahiyh. Imekharijiwa na Maalik katika Al-Muwattwa (1278), Abdulrazzaaq (7/469) na Al-Bayhaqiy (7/457)]
2- Swafiyyah bint Abiy ‘Ubayd (mke wa ‘Abdullaah bin ‘Umar) amesema:
"أَنَّ حَفْصَةَ أُمَّ الْمُؤْمِنِينَ أَرْسَلَتْ بِعَاصِمِ بْنِ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ سَعْدٍ إِلَى أُخْتِهَا فَاطِمَةَ بِنْتِ عُمَرَ بْنِ الْخَطَّابِ تُرْضِعُهُ عَشْرَ رَضَعَاتٍ لِيَدْخُلَ عَلَيْهَا وَهُوَ صَغِيرٌ يَرْضَعُ فَفَعَلَتْ فَكَانَ يَدْخُلُ عَلَيْهَا"
“Kwamba Mama wa Waumini Hafswah alimpeleka ‘Aaswim bin ‘Abdillaah bin Sa’ad akiwa mdogo ananyonya kwa dada yake Faatwimah bint ‘Umar bin Al-Khattwaab amnyonyeshe manyonyesho kumi ili awe mahram yake na aweze kuingia kwake bila tatizo. Akamnyonyesha, naye (‘Aaswim) akawa anaingia kwake bila ukakasi wowote”. [Isnaad yake ni swahiyh. Imekharijiwa na Maalik katika Al-Muwattwa (1279), Abdulrazzaaq (7/470) na Al-Bayhaqiy (7/457)].
Ninasema: “Kauli yenye nguvu ni ya wale waliosema kuwa manyonyesho matano yaliyothibiti, ndiyo yanamfanya mtoto kuwa mahram. Ni kwa Hadiyth ya ‘Aaishah ya kunasikhiwa manyonyesho kumi na kubaki matano. Pia Hadiyth hii inazatitiwa na Hadiyth ambazo hazikuainisha idadi, hivyo hayo matano yanaingizwa ndani yake. Ama Hadiyth zilizotaja manyonyesho mawili, Hadiyth hizo haziko wazi katika kuharamisha manyonyesho matatu au manne. Lakini pia riwaayah ya manyonyesho matano iko wazi, hivyo inakuwa ni mhimili wa kuegemewa. Na kwa maneno haya, dalili zinapangika na wala hazikinzani”.
Faida:
Imeandikwa katika Al-Mughniy (7/547): “Ikiwa mwanamke atapata maziwa kutokana na mimba aliyoipata toka kwa mumewe, kisha akamnyonyesha mtoto manyonyesho matatu halafu maziwa yake yakakatika, kisha akaja kuolewa na mume mwingine na akapata maziwa kutokana naye, kisha akamnyonyesha mtoto manyonyesho mawili, hapo anakuwa ni mama yake bila mvutano wowote kwa wenye kusema kwamba manyonyesho matano yanaharamisha, lakini yeyote katika waume wawili hawi ni baba wa mtoto, kwa kuwa hakukamilisha idadi ya manyonyesho yanayotokana na maziwa yake. Kwa maana wa kwanza, mtoto alipata matatu tu, nayo hayatoshi, na wa pili akaambulia mawili, nayo pia hayafikishi kiwango cha kuleta umahram na mtoto huyo, lakini mwanamke huyo alipata yote matano”.
Swahiyh Fiqh As-Sunnah
كِتَابُ الزَّوَاجِ
Kitabu Cha Ndoa
Alhidaaya.com [3]
14-Mpaka Wa Muda Wa Kunyonya Ili Umahramu Upatikane:
‘Ulamaa wana kauli nyingi kuhusiana na umri unaozingatiwa wa kumfanya mnyonyaji awe maharimu kwa anayemnyonyesha. Kati ya kauli hizo, ziko tatu mashuhuri zaidi:
Kauli Ya Kwanza: Unyonyeshaji unaoharamisha ni ule wa miaka miwili ya mwanzo tu.
Hii ni kauli ya Jumhuwr ya ‘Ulamaa wakiwemo Maalik, Ash-Shaafi’iy, Ahmad, Is-haaq, Abu Thawr na Al-Awzaa’iy. Pia ni kauli ya ‘Umar na mwanawe ‘Abdullaah, Ibn Mas-‘uwd, Ibn ‘Abbaas, Abu Muwsaa na wake wa Nabiy (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) isipokuwa ‘Aaishah. Dalili zilizotolewa kuhusu kauli hii ni:
1- Kauli Yake Ta’aalaa:
"وَالْوَالِدَاتُ يُرْضِعْنَ أَوْلَادَهُنَّ حَوْلَيْنِ كَامِلَيْنِ"
“Na wazazi wa kike wanyonyeshe watoto wao miaka miwili kamili.” [Al-Baqarah: 233]
Wanasema kwamba haya ni maelekezo toka kwa Allaah Ta’aalaa kwa wamama kuwa wawanyonyeshe watoto wao unyonyeshaji ulio kamili nao ni miaka miwili. Hivyo basi, unyonyeshaji wenye kuharamisha na ambao unapita njia ya unasaba ni ule uliokamilisha miaka miwili, na baada ya hapo, umahram haupatikani. [Angalia Tafsiyr Al-Qurtwubiy (Al-Baqarah: 233) na Ibn Kathiyr]
2- Hadiyth ya ‘Aaishah:
"أَنَّ النَّبِيَّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ دَخَلَ عَلَيْهَا وَعِنْدَهَا رَجُلٌ فَكَأَنَّهُ تَغَيَّرَ وجْهُهُ، كأَنَّهُ كَرِهَ ذَلِكَ فَقَالَت: إِنَّه أخي، فَقَالَ: "اُنْظُرْنَ مَنْ إِخْوَانُكُنَّ، فَإِنَّمَا اَلرَّضَاعَةُ مِنْ اَلْمَجَاعَةِ"
“Kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) aliingia ‘Aaishah na kumkuta mwanaume, akawa kama uso wake umebadilika, kana kwamba hilo limemchukiza. Nikamwambia: Huyu ni ndugu yangu. Akasema: “Hakikisheni vizuri kuwajua nani kaka zenu, kwani hakika kunyonya ni pale maziwa tu yanapokuwa ndio lishe pekee ya kumshibisha mtoto kutokana na njaa”. [Hadiyth Swahiyh. Imekharijiwa na Al-Bukhaariy (5102) na Muslim (1455)]
Yaani, uharamu (umahram) unaotokana na kunyonya ni ule wa mtoto anapokuwa bado mdogo hajala kitu kingine zaidi ya maziwa ambayo ndiyo yanayomshibisha na kumwondoshea njaa.
3- Ummu Salamah amesema: Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
"لَا يُحَرِّمُ مِنَ الرِّضَاعِ إِلَّا مَا فَتَقَ الْأَمْعَاءَ فِي الثَّدْيِ وَكَانَ قبل الْفِطَام"
“Umahramu wa kunyonya haupatikani mpaka mtoto anyonye ziwa, na maziwa yapenye na kuingia kwenye machango yake, isitoshe, kunyonya kuwe kabla ya muda wa kuachishwa mtoto ziwa”. [Hadiyth Swahiyh. Imekharijiwa na At-Tirmidhiy (1162) na Ibn Maajah (6/214)]
4- ‘Abdullaah bin Diynaar amesema:
"جَاءَ رَجُلٌ إِلَى عَبْدِ اللَّهِ بْنِ عُمَرَ وَأَنَا مَعَهُ عِنْدَ دَارِ الْقَضَاءِ يَسْأَلُهُ عَنْ رَضَاعَةِ الْكَبِيرِ، فَقَالَ عَبْدُ اللَّهِ بْنُ عُمَرَ: جَاءَ رَجُلٌ إِلَى عُمَرَ بْنِ الْخَطَّابِ فَقَالَ: إِنِّي كَانَتْ لِي وَلِيدَةٌ وَكُنْتُ أَطَؤُهَا فَعَمَدَتِ امْرَأَتِي إِلَيْهَا فَأَرْضَعَتْهَا فَدَخَلْتُ عَلَيْهَا فَقَالَتْ: دُونَكَ فَقَدْ وَاللَّهِ أَرْضَعْتُهَا. فَقَالَ عُمَرُ: أَوْجِعْهَا وَأْتِ جَارِيتَكَ فَإِنَّمَا الرَّضَاعَةُ رَضَاعَةُ الصَّغِيرِ"
“Mtu mmoja alikuja kwa ‘Abdullaah bin ‘Umar nami nikiwa naye kwenye ofisi ya mashtaka na hukumu na akamuuliza kuhusu hukmu ya kumnyonyesha mtu mzima. ‘Abdullaah bin ‘Umar akamwambia: Mtu mmoja alikuja kwa ‘Umar bin Al-Khattwaab akamwambia: Mimi nilikuwa na kijakazi, na nilikuwa ninamuingilia, na mke wangu akamwendea na kumnyonyesha. Nami nilipoenda kwa kijakazi, mke wangu akaniwahi na kuniambia: Usimkaribie tena, naapa kwa Allaah, hakika nimemnyonyesha. Umar akasema: Kamtie adabu, na muingilie kijakazi wako, kwani hakika kunyonya kunakoleta umahram, ni kunyonya mtoto akiwa mdogo”. [Isnaad yake ni swahiyh. Imekharijiwa na Maalik (1289), Abdulrazzaaq (7/462) na Al-Bayhaqiy (7/461)]
5- Ibn ‘Umar amesema:
"لاَ رَضَاعَةَ إِلاَّ لِمَنْ أُرْضِعَ فِي الصِّغَرِ وَلاَ رَضَاعَةَ لِكَبِيرٍ"
“Umahram wa kunyonya haupatikani ila kwa aliyenyonyeshwa udogoni, hakuna umahram wa kunyonya kwa mkubwa”. [Isnaad yake ni swahiyh. Imekharijiwa na Maalik (1282), Abdulrazzaaq (7/465) na Ibn Jariyr katika At-Tafsiyr (4956)]
6- Mtu mmoja alikuja kwa Ibn Mas-‘uwd akamwambia: Nilikuwa na mke wangu, kisha ziwa lake likajaa na maziwa yakawa hayatoki. Nikaanza kulinyonya titi lake na kutema maziwa yake . Kisha nikamwendea Abu Muwsaa ili nimuulize kuhusu hili, naye akanijibu kwamba mke wangu amekuwa si halali tena kwangu. Akasema: Akasimama (Ibn Mas-‘uwd), nasi tukasimama pamoja naye, akatuongoza hadi kwa Abu Muwsaa. Tulipofika alimuuliza Abu Muwsaa: Umemjibu nini huyu? Akamweleza fatwaa aliyomjibu. Ibn Mas-‘uwd akaukamata mkono wa yule mtu na kumuuliza Abu Muwsaa: Je, huyu ni mtoto mchanga? Kunyonya kunakoleta umahram ni kule kunakojenga nyama na damu. Abu Muwsaa akasema: Msiniulize tena chochote madhali mwanachuoni huyu mkubwa yuko nanyi”. [Isnaad yake ni swahiyh. Imekharijiwa na Abdulrazzaaq (7/463), Al-Bayhaqiy (7/461) na At-Twabariy (4958)]
7- Ibn ‘Abbaas amesema:
"لا رضَاعَ إِلاَّ ما كَانَ في حَوْلَيْنِ"
“Unyonyaji mtoto hauzingatiwi (ukaleta umahram) ila ule uliofanyika katika miaka miwili”. [Isnaad yake ni swahiyh. Imekharijiwa na Sa’iyd bin Mansouwr katika Sunanih (980) na Al-Bayhaqiy (7/462)]
8- Wake wa Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) waliikataa kauli ya ‘Aaishah ya kupatikana umahram kwa kumnyonyesha mkubwa. Hili litazungumziwa mbeleni.
Kauli Ya Pili: Unyonyeshaji unaoharamisha ni ule ulio katika muda wa miezi thelathini (miaka miwili na nusu).
Haya ni madhehebu ya Abu Haniyfah, na hujja yake ni Kauli ya Allaah Ta’aalaa:
"وَحَمْلُهُ وَفِصَالُهُ ثَلَاثُونَ شَهْرًا"
“Kuibeba mimba na kuachishwa kwake kunyonya ni miezi thelathini”. [Al-Ahqaaf: 15]
Kauli ya tatu: Kumnyonyesha mkubwa kunaharamisha kama kunavyoharamisha kumnyonyesha mdogo.
Ni madhehebu ya Adh-Dhwaahiriyyah, ‘Atwaa na Al-Layth. Hii pia ni kauli ya ‘Aaishah (Radhwiya Allaah ‘anhaa). Dalili ya kauli hii ni Hadiyth ya ‘Aaishah kuhusu Sahlah bint Suhayl ambaye alikwenda kwa Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na kumwambia”:
"إِنِّي أَرَى فِي وَجْهِ أَبِي حُذَيْفَةَ مِنْ دُخُولِ سَالِمٍ - وَهُوَ حَلِيفُهُ-. فَقَالَ النَّبِيُّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: أَرْضِعِيهِ. قَالَتْ: وَكَيْفَ أُرْضِعُهُ وَهُوَ رَجُلٌ كَبِيرٌ، فَتَبَسَّمَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ وَقَالَ: قَدْ عَلِمْتُ أَنَّهُ رَجُلٌ كَبِيرٌ"
“Sahlah binti Suhayl alikuja kwa Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akamwambia: Ninaona alama ya maudhiko kwenye uso wa Abu Hudhayfah kutokana na kuingia Saalim kwetu (naye ni mwanaye wa kumlea, si wa kumzaa). Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akamwambia: Mnyonyeshe. Akamuuliza: Nitamnyonyesha vipi mtu mzima?! Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akatabasamu na kumwambia: Mimi ninajua kwamba yeye (Saalim) ni mtu mzima” . [Hadiyth Swahiyh. Imekharijiwa na Muslim (1453)]
Jumhuwr wameijibu Hadiyth hii kwa majibu kadhaa. Kati yake ni:
1- Hili ni tukio mahsusi linalomhusu Sahlah na Saalim, haliwahusu wengine. Na ndiyo sababu hata wake wengine wa Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) walimkatalia ‘Aaishah kutolea dalili tukio hili. Imepokelewa toka kwa ‘Urwah:
"أَبَى سَائِرُ أَزْوَاجِ النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ أَنْ يَدْخُلَ عَلَيْهِنَّ بِتِلْكَ الرَّضْعَةِ أَحَدٌ مِنَ النَّاسِ - يُرِيدُ رَضَاعَةَ الْكَبِيرِ - وَقُلْنَ لِعَائِشَةَ وَاللَّهِ مَا نُرَى الَّذِي أَمَرَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ سَهْلَةَ بِنْتَ سُهَيْلٍ إِلاَّ رُخْصَةً فِي رَضَاعَةِ سَالِمٍ وَحْدَهُ مِنْ رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ وَاللَّهِ لاَ يَدْخُلُ عَلَيْنَا أَحَدٌ بِهَذِهِ الرَّضْعَةِ وَلاَ يَرَانَا"
“Wake wote wa Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) walikataa aingie nyumbani kwao yeyote ambaye amenyonyeshwa nyonyesho hilo (la ukubwani), na wakamwambia ‘Aaishah: “Tunaapa kwa Allaah kwamba hatuoni lile ambalo Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amemwamuru Sahlah bint Suhayl isipokuwa ni ruksa maalum toka kwa Rasuli ya kumnyonyesha Saalim tu pasina mwengine. Tunaapa kwa Allaah kwamba hatutamruhusu yeyote aliyenyonyeshwa nyonyesho hili kuingia nyumbani kwetu, na wala hatotuona”. [Hadiyth Swahiyh. Imekharijiwa na An-Nasaaiy (6/106), Maalik (1288), Ahmad (6/269) na Al-Bayhaqiy (7/459). Iko pia kwa Muslim (1454) na wengineo toka Hadiyth ya Ummu Salamah].
2- Tukio hilo limenasikhiwa (limefutwa hukmu yake) na halizingatiwi, na hususan tarehe yake ikiwa haijulikani wala wakati wake.
Ninasema: “Kauli yenye nguvu ni kwamba nyonyesho linalozingatiwa na lenye kuacha athari ni lile la miaka miwili ya kwanza ya umri wa mtoto kama walivyosema Jumhuwr. Lakini, endapo patakuwepo dharura isiyoepukika ya mtu kuwa lazima aingie kwa mwanamke ambaye inakuwa ni vigumu kujisitiri asimwone, hapa ili kumfanya awe mahram yake, kutakuwa hakuna kizuizi cha kuitumia Hadiyth hii ya Sahlah na Saalim, na hasa tukizingatia kwamba linalojuzu kwa dharura halijuzu kwa jingine. Na haya ni madhehebu ya Shaykhul Islaam Ibn Taymiyyah (Rahimahul Laah), na ni chaguo la Ash-Shawkaaniy. Haya ninayoyasema ni kauli ya nne baada ya tatu zilizotangulia ambapo ndani yake zinajumuika Hadiyth zote katika suala hili bila ya kuzipuuza baadhi yake. Allaah Ndiye Ajuaye zaidi”.
Swahiyh Fiqh As-Sunnah
كِتَابُ الزَّوَاجِ
Kitabu Cha Ndoa
Alhidaaya.com [3]
15-Sifa Ya Nyonyesho Lenye Kuleta Umahram:
Je, ni lazima mtoto anyonye ziwa lenyewe (titi)?
Jumhuwr ya ‘Ulamaa wanasema kwamba maziwa ya mnyonyeshaji yanaleta umahram ni sawa mtoto akiyanyonya toka kwenye titi, au akakamuliwa kwenye chombo akanyweshwa, au akanyweshwa kwa mrija kupitia mdomoni au puani au kwa njia yoyote ile iwayo, muhimu tu maziwa yafike tumboni na yawe ndio lishe yake na chakula chake, yamshibishe, yaoteshe misuli na yakuze mifupa yake. Na hii ni kwa neno Lake Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam):
"إِنَّما الرَّضَاعَةُ مِنَ المَجَاعَةِ"
“Nyonyesho lizingatiwalo, ni lile la (kushibisha) njaa ya mtoto”. [Al-Bukhaariy (5102) na Muslim (1455)]
Ibn Hazm ana rai nyingine kuhusiana na hili. Anasema kwamba kiini cha mtoto kuwa mahram kwa anayemnyonyesha ni kile kinachoitwa kunyonya. Na kunyonya kunakojulikana na wote ni mtoto kulitia ziwa mdomoni na akanyonya maziwa. Ama yule aliyekamuliwa maziwa, halafu akayanywa kwa kutumia chombo, au aliyekamuliwa kwenye mdomo wake akayameza, au maziwa yakachanganywa na mkate au chakula, hayo yote hayaleti umahram wowote!!
Ninasema: “Haya ni madhehebu ya Al-Layth, Daawuwd na Adh-Dhwaahiriyyah. Lakini kauli ya Jumhuwr ndio yenye nguvu zaidi, kwa kuwa linalozingatiwa ni mtoto kunyanywa maziwa na kuingia tumboni kwa njia yoyote ile. Na kama atakunywa na maziwa yakaishia mdomoni tu halafu akayatema, basi maziwa hayo hayaleti umahramu. Allaah Ndiye Ajuaye zaidi”.
Faida:
Msichana Bikra Akitokwa Na Maziwa Halafu Akamnyonyesha Mtoto Wa Kiume, Je, Mtoto Huyo Atakuwa Mahram Yake?
Mwanamke akitokwa na maziwa bila kuingiliwa, ni sawa akiwa bikra au amewahi kuolewa, basi maziwa yataleta umahram kwa mujibu wa Jumhuwr ya ‘Ulamaa. Mtoto aliyenyonyeshwa na hao, atakuwa ni mtoto wao, kwa kuwa hayo ni maziwa ya mwanamke ambayo yanaleta umahram sawa na yale yaliyotokana na kujimaiwa, na maziwa ya mwanamke yameumbwa kwa ajili ya lishe ya mtoto. Na hili ni jambo la nadra kutokea, na likitokea, basi umahram unabaki palepale.
Swahiyh Fiqh As-Sunnah
كِتَابُ الزَّوَاجِ
Kitabu Cha Ndoa
Alhidaaya.com [3]
16-Wanawake Walioharamika Kwa Muda: 1- Dada Ya Mke:
Kwa mujibu wa itifaki ya ‘Ulamaa, mwanaume haruhusiwi kuoa madada wawili kwa wakati mmoja. Allaah Anasema:
"وَأَن تَجْمَعُوا بَيْنَ الْأُخْتَيْنِ إِلَّا مَا قَدْ سَلَفَ"
“Na (mmeharamishiwa) kuwaoa dada wawili kwa wakati mmoja, isipokuwa yaliyokwisha pita”. [An-Nisaa: (23)]
Lakini ikiwa mkewe atafariki au akamtaliki, basi hapo ataruhusiwa kumwoa dada yake.
Ummu Habiybah bint Abiy Sufyaan alimwambia Rasuli:
"يَا رَسُولَ اللَّهِ، أَنْكِحْ أُخْتِي هَمْنَة بنت أبي سُفْيَان، فَقَالَ: أَوَتُحِبِّينَ ذَاكَ؟ قَالَتْ: نَعَمْ، لَسْتُ بِمُخْلِيَةٍ بِكَ، وَأَحَبُّ مَنْ شَارَكَنِي فِي خَيْرٍ أُخْتِي . قَالَ: فَإِنَّهَا لاَ تَحِلُّ لِي"
“Ee Rasuli wa Allaah! Mwoe dada yangu Hamnah bint Abiy Sufyaan. Rasuli akamuuliza: Unaridhia hilo? Akasema: Na’am, mimi si mke pekee kwako, nina wakewenza wenzangu, na mtu ambaye ningependa zaidi ashirikiane nami katika kheri hii ni dada yangu. Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akamwambia: Hilo kwangu si halali”. [Hadiyth Swahiyh. Imekharijiwa na Al-Bukhaariy (5101) na Muslim (1449)]
Wanalingana katika hili madada wa baba mmoja mama mmoja, au baba mmoja mama tofauti, au mama mmoja baba tofauti, au pia wawe kwa nasaba au kwa kunyonya.
Faida Mbili:
Ya kwanza: Mtu akioa mwanamke halafu akamwoa dada yake, ndoa hii ya pili itakuwa ni batili, na ya kwanza itabaki sahihi, ni sawa akiwa amemuingilia au hajamuingilia. Ni lazima amtaliki huyo wa pili. Na kama ana kijakazi anamuingilia, na kijakazi huyu ana dada yake, basi haruhusiwi kumuingilia dada yake huyu ila kama atamuuza, au atamwozesha au atamwacha huru (huyo anayemuingilia), hapo dada yake huyo atakuwa ni halali kwake.
Na kama atawaoa wote wawili kwa aqdi moja, ndoa itafisidika.
Ya pili: Ikiwa kafiri aliyeoa dada wawili kwa pamoja atasilimu, huyu itabidi abaki na mmoja tu na amtaliki mwingine.
Swahiyh Fiqh As-Sunnah
كِتَابُ الزَّوَاجِ
Kitabu Cha Ndoa
Alhidaaya.com [3]
17- Wanawake Walioharamika Kwa Muda: 2-Khalati Ya Mke Au Shangazi Yake:
Abu Hurayrah: “Kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
"لَا يُجْمَعُ بَيْنَ الْمَرْأَة وعَمَّتِهَا وَلَا بَينَ الْمَرْأَة وخَالَتِهَا"
“Mwanamke haolewi ndoa moja na shangazi yake wala na khalati yake”. [Hadiyth Swahiyh. Imekharijiwa na Al-Bukhaariy (5109) na Muslim (1408)]
Jaabir kasema:
"نَهَى رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ أَنْ تُنْكَحَ الْمَرْأَةُ عَلَى عَمَّتِهَا أَوْ خَالَتِهَا"
“Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amekataza shangazi au khalati kuwa mke mwenza wa mwanamke.” [Hadiyth Swahiyh. Al-Bukhaariy (5108) na An-Nasaaiy (6/98)]
Kwa muktadha huu, kwa mujibu wa ‘Ijmaa ya ‘Ulamaa, si halali mtu kumkusanya mwanamke na shangazi yake au khalati yake ndani ya ndoa moja, ni sawa awe shangazi au khalati wa kweli au wa kimajazi. Wa kimajazi ni dada wa baba wa baba, na baba wa babu na kwenda juu. Au dada wa mama wa mama (bibi), na mama wa bibi kwa upande wa mama na kwa upande wa baba na kwenda juu. Hawa wote ni haramu kuwakusanya ndani ya ndoa moja.
Swahiyh Fiqh As-Sunnah
كِتَابُ الزَّوَاجِ
Kitabu Cha Ndoa
Alhidaaya.com [3]
18-Wanawake Walioharamika Kwa Muda: 3-Mke Wa Mtu, Au Mwanamke Ambaye Bado Yuko Kwenye Eda Isipokuwa Mateka, Na Mke Wa Kafiri Akisilimu:
Hii ni kwa Kauli Yake Ta’aalaa:
"وَالْمُحْصَنَاتُ مِنَ النِّسَاءِ إِلَّا مَا مَلَكَتْ أَيْمَانُكُمْ"
“Na (mmeharamishiwa pia) wanawake walio katika ndoa isipokuwa iliyowamiliki mikono yenu ya kuume”. [An-Nisaa: 24]
Maana ya aayah hii ni kwamba mmeharamishiwa wanawake walioolewa isipokuwa wale iliyowamiliki mikono yenu ya kiume kwa kuwateka vitani. Mwanamke akitekwa vitani, ndoa yake na mumewe kafiri inavunjika, na atakuwa halali kwa Waumini unapomalizika muda wa kujua kama ana kitu tumboni au la (istibraa), nayo ni hedhi moja. Maana hii inazatitiwa na Hadiyth ya Abu Sa’iyd Al-Khudriyy:
"أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يَوْمَ حُنَيْنٍ بَعَثَ جَيْشًا إِلَى أَوْطَاسٍ فَلَقُوا عَدُوًّا فَقَاتَلُوهُمْ فَظَهَرُوا عَلَيْهِمْ وَأَصَابُوا لَهُمْ سَبَايَا، فَكَأَنَّ نَاسًا مِنْ أَصْحَابِ النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ تَحَرَّجُوا مِنْ غِشْيَانِهِنَّ مِنْ أَجْلِ أَزْوَاجِهِنَّ مِنَ الْمُشْرِكِينَ، فَأَنْزَلَ اللَّهُ تَعَالَى فِي ذَلِكَ: وَالْمُحْصَنَاتُ مِنَ النِّسَاء إِلَّا مَا ملكت أَيْمَانكُم، أَيْ فَهُنَّ لَهُمْ حَلَالٌ إِذَا انْقَضَتْ عِدَّتُهُنَّ"
“Kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alituma jeshi Siku ya Hunayn kwenda Awtwaas. Na huko walikutana na maadui wakapambana nao, wakawashinda nguvu na wakawateka wanawake wao. Ikawa kama vile Maswahaba wa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) wanaona ukakasi kuwaingilia kwa sababu ya waume zao washirikina. Na hapo Allaah ‘Azza wa Jalla Akateremsha Kauli Yake:
"وَالْمُحْصَنَاتُ مِنَ النِّسَاءِ إِلَّا مَا مَلَكَتْ أَيْمَانُكُمْ"
“Na (mmeharamishiwa pia) wanawake walio katika ndoa isipokuwa iliyowamiliki mikono yenu ya kuume”. [An-Nisaa: 24]
Yaani, wanawake hao ni halali kwenu zinapomalizika eda zao. [Hadiyth Swahiyh. Imekharijiwa na Muslim (1456), Abu Daawuwd (2155), An-Nasaaiy (6/110) na At-Tirmidhiy (1132)]
Ibn ‘Abbaas amesema:
"كُلُّ ذاتِ زَوْجٍ إِتْيَانُهَا زِنَا إِلاّ ما سُبِيَتْ"
“Kumuingilia mwanamke yeyote mwenye mume ni zinaa isipokuwa aliyetekwa”. [Isnaad yake ni swahiyh. Imekharijiwa na Ibn Jariyr katika Tafsiyr yake (8961)].
Naye Ibn Mas-‘uwd amesema kuhusiana na aayah hii:
كُلُّ ذَاتِ زَوْجٍ عَلَيْكَ حَرَامٌ إِلاَّ أَنْ تَشْتَرِيَهَا أَوْ مَا مَلَكَتْ يَمِيْنُكَ"
“Mwanamke yeyote mwenye mume ni haramu kwako isipokuwa kama utamnunua, au aliyemilikiwa na mkono wako wa kuume (kijakazi)”. [Wapokezi wake wanaaminika. Imekharijiwa na Ibn Jariyj (8972), isipokuwa riwaayah ya Ibraahiym aliyoipokea toka kwa Ibn Mas-‘uwd imekatika]
Mwanamke ambaye mume wake alikuwa kafiri kisha akasilimu, huyu anaingia ndani ya duara la wanawake walioolewa, kwa kuwa kusilimu kwake kunamtenganisha yeye na mume wake mushrik. Na hii ni kwa Neno Lake Allaah Ta’aalaa:
"يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِذَا جَاءَكُمُ الْمُؤْمِنَاتُ مُهَاجِرَاتٍ فَامْتَحِنُوهُنَّ ۖ اللَّـهُ أَعْلَمُ بِإِيمَانِهِنَّ ۖ فَإِنْ عَلِمْتُمُوهُنَّ مُؤْمِنَاتٍ فَلَا تَرْجِعُوهُنَّ إِلَى الْكُفَّارِ ۖ لَا هُنَّ حِلٌّ لَّهُمْ وَلَا هُمْ يَحِلُّونَ لَهُنَّ ۖ وَآتُوهُم مَّا أَنفَقُوا ۚ وَلَا جُنَاحَ عَلَيْكُمْ أَن تَنكِحُوهُنَّ إِذَا آتَيْتُمُوهُنَّ أُجُورَهُنَّ ۚ وَلَا تُمْسِكُوا بِعِصَمِ الْكَوَافِرِ وَاسْأَلُوا مَا أَنفَقْتُمْ وَلْيَسْأَلُوا مَا أَنفَقُوا ۚ ذَٰلِكُمْ حُكْمُ اللَّـهِ ۖ يَحْكُمُ بَيْنَكُمْ ۚ وَاللَّـهُ عَلِيمٌ حَكِيمٌ"
“Enyi walioamini! Wanapokujieni Waumini wa kike waliohajiri basi wajaribuni. Allaah Ni Mjuzi zaidi wa iymaan zao. Kisha mkiwatambua kuwa ni Waumini, basi msiwarejeshe kwa makafiri. Wao si wake halaal kwao, na wala wao waume hawahalaliki kwao. Na wapeni (makafiri mahari) waliyotoa. Na wala si dhambi kufunga nao nikaah mkiwapa mahari yao. Na wala msiwaweke wanawake makafiri katika fungamano la ndoa. Na takeni mlichotoa (katika mahari), nao watake walichotoa. Hiyo ndio Hukumu ya Allaah, Anahukumu baina yenu. Na Allaah Ni Mjuzi wa yote, Mwenye hikmah wa yote. [Al-Mumtahinah: 10]
Swahiyh Fiqh As-Sunnah
كِتَابُ الزَّوَاجِ
Kitabu Cha Ndoa
Alhidaaya.com [3]
19-Wanawake Walioharamika Kwa Muda: 4-Aliyeachwa Talaka Tatu:
Mwanamke huyu hawezi kuwa halali tena kwa mumewe ila baada ya kuolewa na mume mwingine ndoa sahihi. Na hii ni kwa Neno Lake Ta’aalaa:
" فَإِن طَلَّقَهَا فَلَا تَحِلُّ لَهُ مِن بَعْدُ حَتَّىٰ تَنكِحَ زَوْجًا غَيْرَهُ ۗ فَإِن طَلَّقَهَا فَلَا جُنَاحَ عَلَيْهِمَا أَن يَتَرَاجَعَا إِن ظَنَّا أَن يُقِيمَا حُدُودَ اللَّـهِ ۗ وَتِلْكَ حُدُودُ اللَّـهِ يُبَيِّنُهَا لِقَوْمٍ يَعْلَمُونَ"
“Na akimtaliki (mara ya tatu), basi hatokuwa halali kwake baada ya hapo mpaka aolewe na mume mwengine. Akimtaliki (au akifariki) hapatokuwa dhambi juu yao wawili kurejeana wakidhani kwamba watasimamisha Mipaka ya Allaah. Na hiyo ni Mipaka ya Allaah Anaibainisha kwa watu wanaojua”. [Al-Baqarah: 230]
Hili litakuja kufafanuliwa kwa mapana zaidi katika hukumu za talaka In Shaa Allaah.
Swahiyh Fiqh As-Sunnah
كِتَابُ الزَّوَاجِ
Kitabu Cha Ndoa
Alhidaaya.com [3]
20-Wanawake Walioharamika Kwa Muda: 5-Mpagani Mpaka Asilimu:
Ni kwa Neno Lake Ta’aalaa:
"وَلَا تَنكِحُوا الْمُشْرِكَاتِ حَتَّىٰ يُؤْمِنَّ ۚ وَلَأَمَةٌ مُّؤْمِنَةٌ خَيْرٌ مِّن مُّشْرِكَةٍ وَلَوْ أَعْجَبَتْكُمْ"
“Na wala msiwaoe wanawake washirikina mpaka waamini. Na mjakazi Muumini ni bora kuliko mshirikina japo akikupendezeni”. [Al-Baqarah: 221]
Na Amesema tena Allaah Ta’aalaa:
"وَلَا تُمْسِكُوا بِعِصَمِ الْكَوَافِرِ"
“Na wala msiwaweke wanawake makafiri katika fungamano la ndoa”. [Al-Mumtahinah: 10]
Ndani ya aayah hizi mbili, kuna katazo la kuoa wanawake makafiri mpaka wasilimu. Katika Hadiyth ya Al Mis-war bin Al-Makhramah -kuhusiana na Suluhu ya Al-Hudaybiyah-, ni kwamba iliposhuka Kauli Yake Ta’aalaa:
"وَلَا تُمْسِكُوا بِعِصَمِ الْكَوَافِرِ"
“Na wala msiwaweke wanawake makafiri katika fungamano la ndoa.
‘Umar aliwataliki wake zake wawili wakati huo ambao alikuwa nao wakati wa ushirikina, na Mu’aawiyah bin Abiy Sufyaan akamwoa mmoja wao, na mwingine akaolewa na Swafwaan bin ‘Umayyah”. [Hadiyth Swahiyh. Imekharijiwa na Al-Bukhaariy (2734)]
Swahiyh Fiqh As-Sunnah
كِتَابُ الزَّوَاجِ
Kitabu Cha Ndoa
Alhidaaya.com [3]
21-Kuoa Wanawake Wa Ahlul Kitaab Kuko Nje Ya Duara La Uharamisho:
Allaah Ta’aalaa Amesema:
"الْيَوْمَ أُحِلَّ لَكُمُ الطَّيِّبَاتُ ۖ وَطَعَامُ الَّذِينَ أُوتُوا الْكِتَابَ حِلٌّ لَّكُمْ وَطَعَامُكُمْ حِلٌّ لَّهُمْ ۖ وَالْمُحْصَنَاتُ مِنَ الْمُؤْمِنَاتِ وَالْمُحْصَنَاتُ مِنَ الَّذِينَ أُوتُوا الْكِتَابَ مِن قَبْلِكُمْ إِذَا آتَيْتُمُوهُنَّ أُجُورَهُنَّ مُحْصِنِينَ غَيْرَ مُسَافِحِينَ وَلَا مُتَّخِذِي أَخْدَانٍ"
“Leo mmehalalishiwa vilivyo vizuri. Na nyama iliyochinjwa na waliopewa Kitabu ni halali kwenu, na nyama mliyochinja nyinyi ni halali kwao. Na (mmehalalishiwa pia) wanawake waungwana wema katika Waumini na wanawake waungwana wema katika wale waliopewa Kitabu kabla yenu; mtakapowapa mahari yao bila kuwa maasherati wala kuchukua hawara”. [Al-Maaidah: 05]
Jumhuwr ya ‘Ulamaa wamesema kwamba makusudio ya "الْمُحْصَنَاتُ" hapa ni wanawake wema wachaji, ni sawa wakiwa waungwana au vijakazi. Hivyo basi, kwa muktadha huu, wanawake wa Kiyahudi na Kinaswara hawaingii ndani ya haramisho la Kauli Yake Ta’aalaa:
وَلَا تَنكِحُوا الْمُشْرِكَاتِ
“Na wala msiwaoe wanawake washirikina”. Na huu pia ni msimamo wa Jumhuwr ya Maswahaba.
1- Ash-Sha’abiy amesema:
"تَزَوَّجَ أَحَدُ السِّتَّةِ مِنْ أَصْحَابِ الشُّورَى يَهُودِيَّةً"
“Mmoja wa watu sita aliowateua ‘Umar kushauriana ili kuchagua Khalifah baada yake alimwoa mwanamke wa Kiyahudi”. [Isnaad yake ni swahiyh. Imekharijiwa na Sa’iyd bin Manswuwr katika “Sunanih” (717)]
2- Jaabir aliulizwa kuhusu mwanaume wa Kiislamu kumwoa mwanamke wa Kiyahudi au Kinaswara akasema:
"تَزَوَّجْنَاهُنَّ زَمَانَ الفَتْحِ بِالكُوْفَةَ معَ سَعْدِ بن أَبِيْ وَقَّاص، وَنَحْنُ لا نَكَادُ نَجِدُ المُسْلِمَاتِ كثِيْرًا، فلَمَّا رَجَعْنَا طَلَّقْنَاهُنَّ"
“Wakati wa ukombozi wa Makkah, tuliwaoa pamoja na Sa’ad bin Abiy Waqqaasw huko Kufah. Ilikuwa ni vigumu sana kwetu kuwapata wanawake wa Kiislamu. Tuliporudi, tuliwataliki”. [Isnaad yake ni swahiyh. Imekharijiwa na Ash-Shaafi’iy katika “Al-Ummu” (5/8) na Al-Bayhaqiy (7/172)]
3- Abu Waail kasema:
"تَزَوَّجَ حُذَيْفَةُ يَهُوْدِيَّةً فَكَتَبَ إِلَيْهِ عُمَرٌ: طَلِّقْهَا، فَكَتَبَ إِلَيْهِ: لِمَ؟ أَحَرَامٌ هِيَ؟ فَكَتَبَ إِلَيْهِ: لا، وَلكِنِّيْ ×ِفْتُ أَنْ تَعَاطَوا المُوْمِسَاتِ مِنْهُنَّ"
“Hudhayfah alioa mwanamke wa Kiyahudi na ‘Umar akamwandikia barua ya kumwamuru amtaliki. Naye akaandika kuuliza sababu kwa nini mwanamke huyo awe haramu. Akamjibu akisema: Hapana, si haramu, lakini nimehofia msije mkaoa makahaba kati yao”. [Isnaad yake ni swahiyh. Imekharijiwa na Sa’iyd bin Manswuwr (716) na Al-Bayhaqiy (7/172)]
Baadhi ya ‘Ulamaa pamoja na Ash-Shaafi’iy wanaona kwamba Baniy Israaiyl ambao wanafuata dini ya Uyahudi au Unaswara, hao wanawake wao wanaolewa na wanyama waliochinja wanaliwa. Ama yule ambaye amefuata dini yao naye si katika wao, ni sawa akiwa Mwarabu au taifa jingine lolote, basi hao wanawake wao hawaolewi wala walivyochinja haviliwi. Hii pia ni kauli ya ‘Aliy bin Abi Twaaalib (Radhwiya Allaah ‘anhu) na baadhi ya Masalaf.
Toka kwa ‘Ubaydah toka kwa ‘Aliy, amesema:
"لا تُؤْكَلُ ذَبَائِحُ نَصَارى العَرَبِ، فَإِنَّهُمْ لا يَتَمَسَّكُونَ مِنَ النَّصْرَانِيَّةِ إِلا بِشُرْبِ الخَمْرِ"
“Vilivyochinjwa na Manaswara wa Kiarabu haviliwi, kwa kuwa wao hawashikamani na unaswara ila kwa kunywa tembo tu”. [Isnaad yake ni swahiyh. Imekharijiwa na ‘Abdulrazzaaq (6/72) na Al-Bayhaqiy (9/217)]
Lakini maneno haya hayana dalili toka kwenye Qur-aan au Sunnah Marfuw’ah. Ama kauli ya ‘Aliy, hiyo inapingana na kauli ya Maswahaba wengineo, bali hata Ibn ‘Abbaas amesema: “Kuleni nyama iliyochinjwa na Bani Taghlab na oeni wanawake wao, kwani Allaah Ta’aalaa Anasema:
"يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تَتَّخِذُوا الْيَهُودَ وَالنَّصَارَىٰ أَوْلِيَاءَ ۘ بَعْضُهُمْ أَوْلِيَاءُ بَعْضٍ"
”Enyi walioamini! Msifanye Mayahudi na Manaswara marafiki wandani. Wao kwa wao ni marafiki wandani”. [Al-Maaidah: 51]
Na lau kama wasingelikuwa miongoni mwao isipokuwa kwa urafiki, basi pia wangelikuwa ni miongoni mwao”. [Isnaad yake ni swahiyh. Imekharijiwa na Ibn Abiy Shaybah katika Al-Muswannaf (3/477) na Al-Bayhaqiy (9/217)]
Mtumishi wa ‘Umar alimwandikia barua akimweleza kwamba kuna watu kule aliko wanaojulikana kama “As-Saamirah” ambao wanasoma Taurati na wanapumzika siku ya jumamosi, lakini hawaamini kufufuliwa. Akamuuliza kama inafaa kula nyama zao walizochinja. ‘Umar akamjibu na kumweleza kwamba hao ni sehemu ya Ahlul Kitaab. [Isnaad yake ni swahiyh. Imekharijiwa na Abdulrazzaaq (7/187) na Al-Bayhaqiy (7/173)]
Ninasema: “Nyuma kidogo tumeeleza kwamba ‘Umar alimwamuru Hudhayfah amtaliki mwanamke wa Kiyahudi aliyekuwa amemwoa. Agizo hilo kama ilivyobainika halikuwa kwa ajili ya kuharamisha ndoa kama hiyo, bali ‘Umar alikuwa anachelea Wanaume wa Kiislamu kuja kuoa wanawake makahaba katika hao. Hili ni jambo la kuzingatiwa na kutanabahiwa pamoja na kujuzu kwake. Allaah Ndiye Ajuaye zaidi”.
Swahiyh Fiqh As-Sunnah
كِتَابُ الزَّوَاجِ
Kitabu Cha Ndoa
Alhidaaya.com [3]
22-Mwanamke Wa Kiislamu Ni Haramu Kuolewa Na Kafiri:
Hii ni sawa ikiwa mwanaume ni katika Ahlul Kitaab au dini nyingine kutokana na Neno Lake Ta’aalaa:
"وَلَا تَنكِحُوا الْمُشْرِكَاتِ حَتَّىٰ يُؤْمِنَّ ۚ وَلَأَمَةٌ مُّؤْمِنَةٌ خَيْرٌ مِّن مُّشْرِكَةٍ وَلَوْ أَعْجَبَتْكُمْ ۗ وَلَا تُنكِحُوا الْمُشْرِكِينَ حَتَّىٰ يُؤْمِنُوا ۚ وَلَعَبْدٌ مُّؤْمِنٌ خَيْرٌ مِّن مُّشْرِكٍ وَلَوْ أَعْجَبَكُمْ ۗ أُولَـٰئِكَ يَدْعُونَ إِلَى النَّارِ ۖ وَاللَّـهُ يَدْعُو إِلَى الْجَنَّةِ وَالْمَغْفِرَةِ بِإِذْنِهِ"
“Na wala msiwaoe wanawake washirikina mpaka waamini. Na mjakazi Muumini ni bora kuliko mshirikina japo akikupendezeni. Na wala msiwaozeshe (wanawake wa Kiislamu) wanaume washirikina mpaka waamini. Na mtumwa Muumini ni bora kuliko mshirikina japo akikupendezeni. Hao wanaitia katika moto na Allaah Anaitia katika Jannah na maghfirah kwa Idhini Yake”. [Al-Baqarah: 221]
Swahiyh Fiqh As-Sunnah
كِتَابُ الزَّوَاجِ
Kitabu Cha Ndoa
Alhidaaya.com [3]
23-Wanawake Walioharamika Kwa Muda: vi-Mwanamke Mzinifu Mpaka Atubie:
Mwanamke huyu hedhi moja inatosha kujua kama ana kitu tumboni au la. Allaah Ta’aalaa Amesema:
"الزَّانِي لَا يَنكِحُ إِلَّا زَانِيَةً أَوْ مُشْرِكَةً وَالزَّانِيَةُ لَا يَنكِحُهَا إِلَّا زَانٍ أَوْ مُشْرِكٌ ۚ وَحُرِّمَ ذَٰلِكَ عَلَى الْمُؤْمِنِينَ"
“Mwanamme mzinifu hafungi nikaah isipokuwa na mwanamke mzinifu au mwanamke mshirikina, na mwanamke mzinifu haolewi isipokuwa na mwanamme mzinifu au mshirikina. Na imeharamishwa hivyo kwa Waumini”. [An-Nuwr: 03]
‘Ulamaa wamekhitilafiana katika ufahamu wa aayah hii tukufu. Ni kwamba je, aayah inabeba dhana ya kwamba jambo hili ni baya na si zuri, au inabeba dhana ya kuharamisha? Na je neno “hivyo” katika aayah linarejea kwenye zinaa au ndoa?
Jumhuwr kinyume na Ahmad bin Hanbali wanaona kwamba dhana ya aayah inabeba ashirio la kwamba jambo hilo si zuri na ni baya, lakini si kuliharamisha. Na kwa msingi huu, wamejuzisha mtu kumwoa mwanamke mzinifu kwa sababu hizi zifuatazo walizozitaja:
1- Mwonekano wa aayah sio unaokusudiwa, kwa kuwa kama utachukuliwa kama ulivyo, basi italazimu kusema kwamba mwanaume mzinifu wa Kiislamu anafaa kumwoa mwanamke mpagani, na mwanamke mzinifu wa Kiislamu anafaa kuolewa na mwanaume wa kipagani, na haya mawili hayaruhusiwi kama ilivyotangulia nyuma.
2- Wametolea dalili Hadiyth ya mtu ambaye alimweleza Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kuhusu tabia ya mkewe akimwambia:
" إِنَّهَا لاَ تَرُدُّ يَدَ لاَمِسٍ، فقَالَ له: طَلِّقْهَا. فقَالَ: إِنِّي لاَ أَصْبِرُ عَنْهَا، فَقَالَ: فَأَمْسِكْهَا"
“Yeye hamkatai mtu yeyote anayemgusa. Rasuli akamwambia: Mwache. Akasema: Siwezi kuishi bila kuwa naye. Akamwambia: Basi endelea kuishi naye”. [Hasanun Bitwuruqihi. Imekharijiwa na Abu Daawuwd (2049), An-Nasaaiy (6/170) na Al-Bayhaqiy (7/154-155)]
Ninasema: “Aayah kubeba dhana ya kuharamisha kumwoa mwanamke mzinifu (kahaba) kunatiliwa nguvu na sababu ya kuteremka aayah yenyewe. Sababu yenyewe ni hii:
أَنَّ مَرْثَدَ بْنَ أَبِي مَرْثَدٍ وَكَانَ رَجُلاً يَحْمِلُ الأَسْرَى مِنْ مَكَّةَ حَتَّى يَأْتِيَ بِهِمُ الْمَدِينَةَ، قَالَ: وَكَانَتِ امْرَأَةٌ بَغِيٌّ بِمَكَّةَ يُقَالُ لَهَا عَنَاقُ وَكَانَتْ صَدِيقَةً لَهُ وَإِنَّهُ كَانَ وَعَدَ رَجُلاً مِنْ أُسَارَى مَكَّةَ يَحْمِلُهُ قَالَ : فَجِئْتُ حَتَّى انْتَهَيْتُ إِلَى ظِلِّ حَائِطٍ مِنْ حَوَائِطِ مَكَّةَ فِي لَيْلَةٍ مُقْمِرَةٍ . قَالَ: فَجَاءَتْ عَنَاقُ فَأَبْصَرَتْ سَوَادَ ظِلِّي بِجَنْبِ الْحَائِطِ، فَلَمَّا انْتَهَتْ إِلَىَّ عَرَفَتْهُ فَقَالَتْ: مَرْثَدُ فَقُلْتُ مَرْثَدُ . فَقَالَتْ: مَرْحَبًا وَأَهْلاً هَلُمَّ فَبِتْ عِنْدَنَا اللَّيْلَةَ . قَالَ قُلْتُ: يَا عَنَاقُ حَرَّمَ اللَّهُ الزِّنَا . قَالَتْ: يَا أَهْلَ الْخِيَامِ هَذَا الرَّجُلُ يَحْمِلُ أَسْرَاكُمْ . قَالَ: فَتَبِعَنِي ثَمَانِيَةٌ، وَسَلَكْتُ الْخَنْدَمَةَ، فَانْتَهَيْتُ إِلَى كَهْفٍ أَوْ غَارٍ فَدَخَلْتُ، فَجَاءُوا حَتَّى قَامُوا عَلَى رَأْسِي فَبَالُوا فَطَلَّ بَوْلُهُمْ عَلَى رَأْسِي وَأَعْمَاهُمُ اللَّهُ عَنِّي . قَالَ: ثُمَّ رَجَعُوا وَرَجَعْتُ إِلَى صَاحِبِي فَحَمَلْتُهُ وَكَانَ رَجُلاً ثَقِيلاً حَتَّى انْتَهَيْتُ إِلَى الإِذْخِرِ فَفَكَكْتُ عَنْهُ كَبْلَهُ فَجَعَلْتُ أَحْمِلُهُ وَيُعِينُنِي حَتَّى قَدِمْتُ الْمَدِينَةَ، فَأَتَيْتُ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ فَقُلْتُ: يَا رَسُولَ اللَّهِ! أَنْكِحُ عَنَاقًا مَرَّتَيْنِ، فَأَمْسَكَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ وَلَمْ يَرُدَّ عَلَىَّ شَيْئًا حَتَّى نَزَلَتِ : الزَّانِي لاَ يَنْكِحُ إِلاَّ زَانِيَةً أَوْ مُشْرِكَةً وَالزَّانِيَةُ لاَ يَنْكِحُهَا إِلاَّ زَانٍ أَوْ مُشْرِكٌ وَحُرِّمَ ذَلِكَ عَلَى الْمُؤْمِنِينَ ، فَقَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ : يَا مَرْثَدُ الزَّانِي لاَ يَنْكِحُ إِلاَّ زَانِيَةً أَوْ مُشْرِكَةً وَالزَّانِيَةُ لاَ يَنْكِحُهَا إِلاَّ زَانٍ أَوْ مُشْرِكٌ فَلاَ تَنْكِحْهَا". هَذَا حَدِيثٌ حَسَنٌ غَرِيبٌ لاَ نَعْرِفُهُ إِلاَّ مِنْ هَذَا الْوَجْهِ.
Ametuhadithia ‘Abdu bin Humayd, ametuhadithia Rawh bin ‘Ubaadah toka kwa ‘Ubaydullaa bin Al-Akhnas amesema: Amenieleza ‘Amri bin Shu’ayb akipokea toka kwa baba yake toka kwa babu yake aliyesema: Kulikuwa na mtu ajulikanaye kama Marthad. Kazi yake ilikuwa ni kuwabeba na kuwatorosha mateka toka Makkah kuwaleta Madiynah. Na hapo Makkah alikuwepo mwanamke kahaba aitwaye ‘Anaaq ambaye alikuwa ni hawara yake Marthad (kabla hajasilimu). Marthad alikuwa amemwahidi mtu mmoja katika mateka wa Makkah kuwa atambeba (kumtorosha). [Marthad anasema]: Nikaja hadi nikaishilia katika kivuli cha kuta kati ya kuta za Makkah katika usiku angavu wa nuru ya mwezi. ‘Anaaq akaja, akaona weusi wa kivuli changu pembeni ya ukuta. Aliponifikia, alinitambua akasema: Ni Marthad! Nami nikasema ni (mimi) Marthad. Akasema: Karibu sana, njoo basi ulale kwetu usiku huu. Nikamwambia: Ee ‘Anaaq! Allaah Ameharamisha zinaa! (Hapo hapo) akapiga ukelele na kusema: Enyi watu wa makhema! Huyu hapa mtu anayewatorosha mateka wenu. Watu wanane wakaniandama, nikapita Al-Khandamah, nikakimbilia pangoni na kuingia. Wakaja mpaka wakasimama juu ya kichwa changu (mdomo wa pango) lakini Allaah Aliwaziba macho wasiweze kuniona. Kisha wakaondoka, nami nikarudi kwa mwenzangu, nikambeba, naye alikuwa mzito. Nikamfuata mwingine, nikamfungua minyonyoro yake, nikaanza kumbeba huku akinilemea na kunichosha mpaka nikawasili Madiynah. Nikamwendea Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) nikamwambia: Ee Rasuli wa Allaah! Je, naweza kumwoa ‘Anaaq? Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akanyamaza, hakujibu kitu mpaka iliposhuka:
"الزَّانِي لَا يَنكِحُ إِلَّا زَانِيَةً أَوْ مُشْرِكَةً وَالزَّانِيَةُ لَا يَنكِحُهَا إِلَّا زَانٍ أَوْ مُشْرِكٌ ۚ وَحُرِّمَ ذَٰلِكَ عَلَى الْمُؤْمِنِينَ"
“Mwanamme mzinifu hafungi nikaah isipokuwa na mwanamke mzinifu au mwanamke mshirikina, na mwanamke mzinifu haolewi isipokuwa na mwanamme mzinifu au mshirikina. Na imeharamishwa hivyo kwa Waumini”. [An Nuwr (24:3)]
Na hapo Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akamwambia: Ee Marthad! Mwanamme mzinifu hafungi nikaah isipokuwa na mwanamke mzinifu au mwanamke mshirikina; na mwanamke mzinifu haolewi isipokuwa na mwanamme mzinifu au mshirikina, basi usimwoe:. [At-Tirmidhiy Mujallad Wa Ukurasa wa 152]
Hadiyth hii ni Hasan Ghariyb, haijulikani isipokuwa kwa picha hii.
Toka kwa Abu Hurayrah: “Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
"لَا يَنْكِحُ اَلزَّانِي اَلْمَجْلُودُ إِلَّا مِثْلَهُ "
“Mzinifu aliyepatikana na kosa la zinaa na akachapwa viboko, haoi isipokuwa mfano wake”. [Hadiyth Hasan. Imekharijiwa na Abu Daawuwd (2052), Al-Haakim (2/193) na Al-Bayhaqiy (7/156)]
Hata yule pia mwenye sifa ya mwenendo huu mchafu mitaani, asiruhusiwe kuoa binti anayejiheshimu.
Na haya ni madhehebu ya Qataadah, Is-Haaq, Ibn ‘Ubayd, na Ahmad, na Sheikh wa Uislamu ameyakhitari.
Swahiyh Fiqh As-Sunnah
كِتَابُ الزَّوَاجِ
Kitabu Cha Ndoa
Alhidaaya.com [3]
24-Haijuzu Kumwoa Mwanamke Mzinifu (Kahaba) Ila Kwa Masharti Mawili:
La kwanza:
Atubie kikweli na aachane na tabia hiyo. Kwa kuwa, kama atatubia, atakuwa ameondokewa na sifa ambayo ilikuwa ni sababu ya kuharamishwa kumwoa kwa mujibu wa aayah tukufu. Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
"التَّائِبُ مِنَ الذَّنْبِ كَمَنْ لَا ذَنْبَ لَهُ"
“Aliyetubia dhambi ni kama ambaye hakutenda dhambi”. [Al-Albaaniy ameihasanisha. Imekharijiwa na Ibn Maajah (4250), Ibn Al-Ja’ad (1/266), Al-Qadhwaaiy katika “Ash-Shihaab” (1/97), na At-Twabaraaniy (10/150)]
Ya pili:
Asiwe na chochote tumboni, na hili litathibitishwa kwa kupata hedhi moja. Hili ni sharti kwa Ahmad na Maalik kutokana na neno lake Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kuhusiana na wanawake waliotekwa vitani:
"لاَ تُوطَأُ حَامِلٌ حَتَّى تَضَعَ وَلاَ غَيْرُ ذَاتِ حَمْلٍ حَتَّى تَحِيضَ حَيْضَةً"
“Mjamzito haingiliwi mpaka ajifungue, na asiye mjamzito mpaka apate hedhi moja”. [Hasanun Bitwuruqihi. Imekharijiwa na Abu Daawuwd (2157) na Ahmad (3/62)]
Kijakazi au mwanamke aliyetekwa vitani, ni lazima ihakikishwe kwamba hana kitu tumboni kabla hajaingiliwa, na mwanamke mzinifu pia kabla hajaolewa. Allaah Ndiye Ajuaye zaidi.
Swahiyh Fiqh As-Sunnah
كِتَابُ الزَّوَاجِ
Kitabu Cha Ndoa
Alhidaaya.com [3]
25-Wanawake Walioharamika Kwa Muda: vii-Mwanamke Aliyehirimia Mpaka Afunguke Na Ihraam:
Si halali kwa mwanaume au mwanamke aliyehirimia Hajji kufunga ndoa wakiwa katika ihraam. Yeyote kati yao akifunga ndoa, basi ndoa ni batili. Haya ni madhehebu ya Jumhuwr. Ni kutokana na Hadiyth ya ‘Uthmaan bin ‘Affaan (Radhwiya Allaah ‘anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
"لا يَنْكِحُ اَلْمُحْرِمُ، وَلَا يُنْكحُ، وَلَا يَخْطُبُ"
“Aliyehirimia haoi, wala haozeshwi, wala hachumbii”. [Hadiyth Swahiyh. Imekharijiwa na Muslim (1409), At-Tirmidhiy (840), Abu Daawuwd (1841), An-Nasaaiy (5/292) na Ibn Maajah (1966)]
Swahiyh Fiqh As-Sunnah
كِتَابُ الزَّوَاجِ
Kitabu Cha Ndoa
Alhidaaya.com [3]
26-Wanawake Walioharamika Kwa Muda: viii-Mke Wa Tano Ikiwa Mtu Ana Wake Wanne Tayari:
Allaah Ta’aalaa Amesema:
"فَانكِحُوا مَا طَابَ لَكُم مِّنَ النِّسَاءِ مَثْنَىٰ وَثُلَاثَ وَرُبَاعَ"
“Basi oeni waliokupendezeni katika wanawake wengine; wawili au watatu au wanne”. [An-Nisaa: 03]
Idadi ya mwisho aliyoruhusiwa Muislamu kuoa ni wanawake wanne tu, haruhusiwi kuongeza zaidi ya hapo. Kuoa zaidi ya wanawake wanne kwa wakati mmoja, au kuoa bila mahari, kumeruhusiwa kwa sifa mahsusi kwa Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) tu.
Ikiwa mushrik atasilimu naye ana wake zaidi ya wanne, basi ataamuriwa awaache awatakao ili idadi ibakie wanne tu. Ibn ‘Umar amesema:
"أَنَّ غَيْلَانَ بْنَ سَلَمَةَ أَسْلَمَ وَلَهُ عَشْرُ نِسْوَةٍ، فَأَسْلَمْنَ مَعَهُ، فَأَمَرَهُ اَلنَّبِيُّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ أَنْ يَتَخَيَّرَ مِنْهُنَّ أَرْبَعًا"
“Kwamba Ghiylaan bin Salamah Ath-Thaqafiy alisilimu akiwa na wake kumi aliowaoa enzi ya ujahiliya, na wake zake hao walisilimu pamoja naye. Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akamwamuru achague wanne tu kati yao ili abaki nao”. [Maimamu wameitia kasoro pamoja na mwonekano wa kuwa ni sahihi. Imekharijiwa na At-Tirmidhiy (1128), Ibn Maajah (1953), Ahmad (2/13) na wengineo]
Atakayeoa mke wa tano wakati anao wanne tayari, ndoa yake hiyo ya tano itakuwa ni batili. Na kwa mujibu wa kauli ya Maalik na Ash-Shaafi’iy, mtu huyo atastahiki adhabu ya kisharia ikiwa anajua uharamu wa kufanya hivyo. Az-Zuhriy amesema: “Atapigwa mawe kama atakuwa anajua hilo, na kama hajui, basi atapewa adhabu ndogo zaidi kati ya mbili ambayo ni kuchapwa mbati, na mwanamke huyo ni lazima alipwe mahari, watatenganishwa kati yao, na hawatakusanyika tena pamoja milele”.
Swahiyh Fiqh As-Sunnah
كِتَابُ الزَّوَاجِ
Kitabu Cha Ndoa
الأَنْكِحَةُ الفَاسِدَةُ شَرْعًا
Nikaah (Ndoa) Ambazo Ni Batili Kisharia
Alhidaaya.com [3]
27: Ndoa ya “Shighaar”:
Hii ni ndoa ambayo mtu anamwozesha mtu mwingine binti yake, au dada yake, au mfano wa hao, kwa sharti kwamba mtu huyo naye amwozeshe yeye binti yake au dada yake na kadhalika, ni sawa kwa mahari au bila mahari.
‘Ulamaa wote wameharamisha aina hii ya ndoa. Jopo la ‘Ulamaa (Jumhuwr) wamesema kwamba ndoa hii ni batili kutokana na dalili zifuatazo:
1- Hadiyth ya Jaabir:
"نَهَى رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ عَنِ الشِّغَارِ"
“Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ameharamisha (ndoa ya) “Shighaar”. [Hadiyth Swahiyh. Imekharijiwa na Muslim (1417)]
2- Toka kwa Abu Hurayrah:
"نَهَى رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ عَنِ الشِّغَارِ، وَالشِّغَارُ أَنْ يَقُولَ الرَّجُلُ لِلرَّجُلِ: زَوِّجْنِي ابْنَتَكَ وَأُزَوِّجُكَ ابْنَتِي، أَوْ زَوِّجْنِي أُخْتَكَ وَاُزوِّجُكَ أُخْتِي"
“Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ameharamisha “Shighaar”. Akasema Abu Hurayrah: “Shighaar” ni mtu kumwambia mtu mwingine: Niozeshe binti yako nami nikuozeshe binti yangu. Au: Niozeshe dada yako nami nikuozeshe dada yangu”. [Hadiyth Swahiyh. Imekharijiwa na Muslim (1416), An-Nasaaiy (6/112) na Ibn Maajah (1884]
3- Toka kwa Al-A’araj:
"أَنَّ الْعَبَّاسَ بْنَ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ الْعَبَّاسِ، أَنْكَحَ عَبْدَ الرَّحْمَنِ بْنَ الْحَكَمِ ابْنَتَهُ وَأَنْكَحَهُ عَبْدُ الرَّحْمَنِ ابْنَتَهُ، وَكَانَا جَعَلاَ صَدَاقًا، فَكَتَبَ مُعَاوِيَةُ إِلَى مَرْوَانَ يَأْمُرُهُ بِالتَّفْرِيقِ بَيْنَهُمَا، وَقَالَ فِي كِتَابِهِ: هَذَا الشِّغَارُ الَّذِي نَهَى عَنْهُ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم"
“Kwamba Al-‘Abbaas bin ‘Abdillaah bin Al-‘Abbaas alimwozesha ‘Abdulrahmaan bin Al-Hakam binti yake, na yeye ‘Abdulrahmaan akamwozesha binti yake, na walikuwa wamepangiana mahari. Mu’aawiya akamwandikia Marwaan na kumwamuru avunje ndoa hiyo. Akasema kwenye barua hiyo: Hii ni “Shighaar” ambayo Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ameikataza”. [Hadiyth Hasan. Imekharijiwa na Abu Daawuwd (2075)]
4- Neno lake Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam):
"مَنِ اشْتَرَطَ شَرْطًا لَيْسَ فِي كِتَابِ اللَّهِ فَهْوَ بَاطِلٌ، وَإِنِ اشْتَرَطَ مِائَةَ شَرْطٍ، شَرْطُ اللَّهِ أَحَقُّ وَأَوْثَقُ"
“Mwenye kushurutisha sharti lolote ambalo haliko katika Sharia za Allaah basi ni batili, hata akishurutisha masharti mia moja. Sharti la Allaah ndilo lenye haki zaidi na lenye fungamano zaidi”. [Hadiyth Swahiyh. Imekharijiwa na Al-Bukhaariy (2155) na Muslim (1504)]
5- Kushurutisha mapasiano kati ya watu hao wawili kunapelekea uharibifu mkubwa katika ndoa hii, kwa sababu mwanamke hapa analazimishwa kuolewa na mtu ambaye pengine hakumpenda au asiyemtaka. Inakuwa ni kuweka mbele maslahi ya mawalii juu ya maslahi ya wanawake, na hii ni dhulma kwao. Lakini pia, wanawake hawa wanakosa mahari, hawayapati kama wanavyopata wanawake wengine. Huu ndio uhalisia wa wanaume wenye kushabikia ndoa hii ya kuchukiza. Isitoshe, baada ya ndoa, kunazuka misuguano, mivutano na magomvi, na hii ni katika adhabu za papo kwa hapo kwa wote wenye kukhalifu Sharia ya Allaah. [Sehemu ya Risala ya Al-‘Allaamah Ibn Baaz (RahimahuL Laah yenye anuani: “Ndoa ya Shighaar”]
كِتَابُ الزَّوَاجِ
Kitabu Cha Ndoa
الأَنْكِحَةُ الفَاسِدَةُ شَرْعًا
Ndoa Ambazo Ni Batili Kisharia
Alhidaaya.com [3]
28: Ndoa Ya Mhalalishaji:
Mhalalishaji ni mtu ambaye anamwoa mwanamke aliyeachwa talaka tatu, halafu anamtaliki ili aweze kuhalalika kwa mume wa awali. Allaah Ameiharamisha ndoa hii, ndoa hii ni katika madhambi makubwa, na Allaah Amemlaani mtekelezaji (mwenye kuoa kuhalalisha) na mwenye kutekelezewa (mume wa awali).
1- Ibn Mas-‘uwd amesema:
"لَعَنَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ الْمُحِلَّ وَالْمُحَلَّلَ لَهُ"
“Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amemlaani mwenye kuoa kwa lengo la kuhalalisha ndoa (baada ya talaka tatu) na mwenye kuhalalishiwa”. [Hadiyth Swahiyh. Imekharijiwa na At-Tirmidhiy (1120), An-Nasaaiy (6/149), na Ahmad (1/448)]
‘Ulamaa wote wakiwemo Maalik, Ash-Shaafi’iy, Ahmad, Al-Layth, Ath-Thawriy, Ibn Al-Mubaarak na wengineo, wanasema kwamba ndoa hii ya mtu kumwoa mwanamke aliyeachwa talaka tatu ili ahalalike kwa mtalaka wake ni batili. Ni kauli pia ya ‘Umar bin Al-Khattwaab, mwanae ‘Abdullaah, na ‘Uthmaan bin ‘Affaan katika Maswahaba. [Bidaayatul Mujtahid (2/102), Al-Mughniy (6/645), Nihaayatul Muhtaaj (6/282), Al-Muhallaa (10/180), Sunan At-Tirmidhiy (3/420) na Rawdhwat At-Twaalibiyna (7/126)]
2- ‘Umar bin Al-Khattwaab amesema:
"لا أُوتَى بِمُحَلِّلٍ وَبِمُحَلَّلَةٍ إِلاّ رَجَمْتُهُمَا"
“Siletewi aliyeoa ili kuhalalisha ndoa ya talaka tatu wala aliyeolewa kwa lengo hilo ila huwapa adhabu ya kupopolewa kwa mawe”. [Isnaad yake ni swahiyh. Imekharijiwa na ‘Abdulrazzaaq (6/265) na Sa’iyd bin Manswuwr (1992)]
3- Ibn ‘Umar aliulizwa kuhusu mwanamke (aliyeachwa talaka tatu) kuhalalishiwa mumewe aliyemtaliki akajibu: “Hilo ni uchafu na zinaa”. [Isnaad yake ni swahiyh. Imekharijiwa na ‘Abdulrazzaaq katika Al-Muswannaf (10776)]
Hapa ni mamoja ikiwa atashurutishwa amtaliki mwanamke huyo ili ahalalike kwa mumewe wa kwanza, au asishurutishwe lakini akanuwia kuhalalisha, ndoa itakuwa batili tu.
4- Toka kwa Naafi’i:
"جاءَ رجلٌ إلى ابنِ عمرَ فسألَهُ عن رجلٍ طلَّقَ امرأتَهُ ثلاثًا فتزوَّجَها أخٌ لَهُ من غيرِ مُؤامرةٍ منهُ ليُحلَّها لأخيهِ، هل تحلُّ للأوَّلِ؟ فقالَ: لا إلَّا نِكاحَ رَغبةٍ كنَّا نعدُّ هذا سِفاحًا على عَهْدِ رسولِ اللَّهِ صلَّى اللَّهُ عليهِ وسلَّمَ"
“Mtu mmoja alikuja kwa Ibn ‘Umar na kumuuliza kuhusu mtu ambaye amemtaliki mkewe talaka tatu, kisha nduguye akamwoa bila wenyewe kupanga hilo ili aje kuhalalika kwa nduguye, je atahalalika kwa wa kwanza? Akasema: Hapana, isipokuwa kama itakuwa ni ndoa ya utashi wa kuendelea kuishi naye muda mrefu (kama atampendeza). Tulikuwa tunalizingatia hili wakati wa enzi ya Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kama ni zinaa”. [Hadiyth Swahiyh. Imekharijiwa na Al-Haakim (2/199) na Al-Bayhaqiy (7/208)]
Faida:
Linaloangaliwa katika kutofaa ndoa hii ni niya ya mume wa pili (mhalalishaji), na huyu hakosi moja ya hali mbili:
Ya kwanza: Anuwie kumwoa mwanamke kisha amtaliki ili ahalalike kwa mume wake wa kwanza, ni sawa akiwa ameshurutishwa hilo au la, hapa ndoa itakuwa haifai, na itakuwa ni yenye kulaaniwa.
Ya pili: Ashurutishwe kumtaliki mwanamke kabla ya kufunga naye ndoa, kisha yeye akanuwia kinyume na alivyoshurutishwa, yaani akakusudia kuishi na mwanamke huyo maisha yake yote, hapa ndoa inakuwa ni sahihi, kwa kuwa nia ya kuhalalisha na sharti lake havipo. [Ibn ‘Aabidiyna (3/411) na Rawdhwat At-Twaalibiyna (7/126)]
Niya Ya Mume Wa Awali Na Ya Mwanamke Mwenyewe Haizingatiwi:
Kwa sababu mume wa kwanza hana tena lake jambo katika kufungwa ndoa hiyo au kuvunjwa, yeye ni mtu wa kando (ajnabi) kama walivyo wengine wa kando. Hali kadhalika kwa mwanamke, kwa kuwa mamlaka ya talaka na kuendelea na ndoa yako kwa mume wa pili, na si kwake. Kati ya yanayotilia nguvu hili ni:
"جَاءَتِ امْرَأَةُ رِفَاعَةَ إِلَى رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ فَقَالَتْ: إِنَّ رِفَاعَةَ طَلَّقَنِي فَأَبَتَّ طَلاَقِي، وَإِنِّي تَزَوَّجْتُ بَعْدَهُ عَبْدَ الرَّحْمَنِ بْنَ الزَّبِيرِ وَمَا مَعَهُ إِلاَّ مِثْلُ هُدْبَةِ الثَّوْبِ. فَضَحِكَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ وَقَالَ: "لَعَلَّكِ تُرِيدِينَ أَنْ تَرْجِعِي إِلَى رِفَاعَةَ، لاَ، حَتَّى يَذُوقَ عُسَيْلَتَكِ وَتَذُوقِي عُسَيْلَتَهُ"
“Mke wa Rifaa’at alikuja kwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akamwambia: Ee Rasuli wa Allaah! Hakika Rifaa’at amenitaliki talaka zote tatu. Nami baada ya kuniacha, nimeolewa na ‘Abdulrahmaan bin Az-Zubayr ambaye hana ila mfano wa ncha ya nguo (uume wake dhaifu sana). Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akacheka na kumwambia: Inaonyesha unataka kurudi kwa Rifaa’at. Hapana huwezi kurudi, mpaka (‘Abdulrahmaan) aonje utamu wako na wewe uonje utamu wake (yaani akuingilie)]. [Al-Bukhaariy (2639) na Muslim (1433)]
Hapa Rasuli hakuizingatia niya yake.
Swahiyh Fiqh As-Sunnah
كِتَابُ الزَّوَاجِ
Kitabu Cha Ndoa
الأَنْكِحَةُ الفَاسِدَةُ شَرْعًا
Ndoa Ambazo Ni Batili Kisharia
Alhidaaya.com [3]
29: Ndoa Ya Mut’a:
Hii ni ndoa ambayo mtu anamwoa mwanamke kwa muda maalum, ni sawa ikiwa siku moja au mbili au zaidi, kwa kumpa mwanamke chochote kama fedha na mfano wake (kama mahari).
Katika enzi ya Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ndoa hii ilikuwa ni halali, kisha Allaah Ta’aalaa Aliifuta kupitia kwa ulimi wa Rasuli Wake (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam), naye akaiharamisha uharamu wa milele mpaka Siku ya Qiyaamah. Huu ndio msimamo wa Jumhuwr ya ‘Ulamaa kuanzia kwa Maswahaba, Maimamu waliofuatia baada yao na wengineo. [Al-Mudawwanah (2/196), Bidaayatul Mujtahid (2/101), Nihaayatul Muhtaaj (5/71) na Al-Mabsuwtw (5/152)].
Taarifa zimetofautiana kuhusiana na wakati ambapo ndoa hii ya Mut’a ilifutwa. Kati yake ambazo ni sahihi ni:
1- Ilifutwa Khaybar:
Imepokewa kwa njia sahihi kwamba ‘Aliy alimwambia Ibn ‘Abbaas:
"أَنَّ النَّبِيَّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ نَهَى عَنِ الْمُتْعَةِ وَعَنْ لُحُومِ الْحُمُرِ يَوْمَ خَيْبَرَ "
“Kwamba Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikataza (ndoa ya) mut-‘a na nyama ya punda wa mjini walipokuwa Khaybar”. [Hadiyth Swahiyh. Al-Bukhaariy (5115) na Muslim (1407)]
Kisha Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) aliruhusu mut-’a baada ya hapo, lakini habari ya ruksa hiyo haikumfikia ‘Aliy, na yeye akabaki na Hadiyth ya kuharamisha aliyoisikia toka kwa Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) siku ya Khaybar. [Fat-hul Baariy (9/168)]
2- Ilifutwa Mwaka Wa Ufunguzi Wa Makkah:
Imepokelewa toka kwa Ar-Rabiy’i bin Saburata kwamba baba yake alishiriki vita pamoja na Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) siku ya Ukombozi wa Makkah. Amesema: Tukakaa hapo usiku na michana 30 (wiki mbili), na Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akaturuhusu ndoa ya mut-‘a. Kwa ruksa hiyo, mimi nikaoa msichana kwa ndoa hiyo, na sikuwahi kutoka ila Rasuli akawa ameshaiharamisha”. [Hadiyth Swahiyh. Imekharijiwa na Muslim (1406)]
Na katika tamko jingine:
"فَكُنَّ مَعَنَا [يَعْنِي النِّسَاءُ اللاتِيْ اسْتَمْتَعُوا بِهِنَّ] ثَلاثًا ثُمَّ أَمَرَنَا رَسُولُ الله صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ بِفِرَاقِهِنَّ"
“Wakawa pamoja nasi (yaani wanawake waliowaoa kwa mut-‘a) kwa siku tatu, kisha Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akatuamuru tuwaache”. [Hadiyth Swahiyh. Imekharijiwa na Muslim (1406) na Al-Bayhaqiy (7/202)]
Na katika tamko jingine:
"أَمَرَنَا رَسُولُ الله صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ بِالمُتْعَةِ عَامَ الفَتْحِ حِيْنَ دَخَلْنَا مَكَّةَ ثُمَّ لَمْ نَخْرُجْ مِنْهأ حَتَّى نَهَانَا عَنْهَا"
“Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alituamuru tuoe mut-‘a mwaka wa ukombozi tulipoingia Makkah, kisha hatukutoka humo, ila akawa ameshatuharamishia”. [Hadiyth Swahiyh. Imekharijiwa na Muslim (1406)]
3- Ilifutwa Mwaka Wa Awtwaas:
Toka kwa Salamah bin Al-Akwaa:
"رَخَّصَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ عَامَ أَوْطَاسٍ فِي الْمُتْعَةِ ثَلَاثًا ثُمَّ نَهَى عَنْهَا"
“Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) aliruhusu mut-‘a Mwaka wa Awtwaas siku tatu, kisha akaipiga marufuku”. [Hadiyth Swahiyh. Imekharijiwa na Muslim (1405), Al-Bayhaqiy (7/204) na Ibn Hibaan (1451)]
Kisha marufuku hii ikawa ya milele hadi Siku ya Qiyaamah.
Zindushi Mbili:
1- Jaabir bin ‘Abdullaah amesema:
"كُنَّا نَسْتَمْتِعُ بِالْقُبْضَةِ مِنَ التَّمْرِ وَالدَّقِيقِ الأَيَّامَ عَلَى عَهْدِ رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ وَأَبِي بَكْرٍ حَتَّى نَهَى عَنْهُ عُمَرُ فِي شَأْنِ عَمْرِو بْنِ حُرَيْثٍ"
“Tulikuwa tunaoa mut-‘a kwa mahari ya konzi ya tende na unga kwa masiku kadhaa wakati wa uhai wa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Abu Bakr mpaka alipoikataza ‘Umar kutokana na ndoa ya ‘Amri bin Hurayth”. [Hadiyth Swahiyh. Imekharijiwa na Muslim (1405) na Abu Daawuwd (2110)]
Hili linajengewa uwezekano wa kuwa waliofunga ndoa za mut-‘a katika enzi hiyo ya Abu Bakr na ‘Umar, walikuwa hawajapata habari ya kufutwa na kuharamishwa ndoa hii. [Sharhu Ma’aaniy Al-Aathaar (3/27) na Sharhu Muslim (3/555)]
2- Imethibiti toka kwa Ibn ‘Abbaas (Radhwiya Allaah ‘anhumaa) ya kwamba yeye alikuwa anaona uhalali wa ndoa ya mut-‘a kama iko dharura. Toka kwa Abu Hamzah:
"سَمِعْتُ ابْنَ عَبَّاسٍ، سُئِلَ عَنْ مُتْعَةِ النِّسَاءِ، فَرَخَّصَ فَقَالَ لَهُ مَوْلًى لَهُ إِنَّمَا ذَلِكَ فِي الْحَالِ الشَّدِيدِ وَفِي النِّسَاءِ قِلَّةٌ أَوْ نَحْوَهُ. فَقَالَ ابْنُ عَبَّاسٍ نَعَمْ."
“Nilimsikia Ibn ‘Abbaas akiulizwa kuhusu ndoa ya mut-‘a, naye akaruhusu. Mwachwa huru wake akauliza: Je, hiyo ni katika hali ya mtu kuzidiwa sana (na matamanio), au wanawake kuwa wachache au mfano wake? Ibn ‘Abbaas akajibu: Na’am”. [Hadiyth Swahiyh. Imekharijiwa na Al-Bukhaariy (5116), At-Twahaawiy (3/26) na Al-Bayhaqiy (7/204)]
Jibu hili ni katika misimamo nadra ya kipekee ya Mwanachuoni huyu mkubwa Ibn ‘Abbaas, na Allaah bila shaka Atamlipa kwa ijtihadi yake hii. Ama sisi, bila shaka tutaendelea kushikamana na taarifa iliyotufikia toka kwa Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ya kwamba ndoa hii ni haramu. Na Ibn ‘Abbaas kwenda kinyume na Jumhuwr ya Maswahaba hakuziharibu dalili za kuharamisha, na sisi pia hatuna udhuru wowote wa kutozitumia. Allaah Ndiye Ajuaye zaidi.
Nini Afanye Aliyeoa Ndoa Ya Mut-‘a?
Tumeshasema kwamba ndoa ya mut-‘a haifai, ni batili. Hivyo basi, atakayefunga ndoa hii, ni lazima aachane mara moja na mwanamke aliyemwoa, kwa kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) aliwaamuru waliooa ndoa ya mut-‘a watengane na wanawake waliowaoa kama ilivyo katika Hadiyth ya Sabrah.
Nini Hukmu Ya Mwanaume Anayeoa Mwanamke Akiwa Na Niya Ya Kumwacha Baada Ya Muda?
Jambo hili wanalifanya wanaume wengi wanaosafiri kwenda nje. Huko wanaoa wakiwa na niya ya kuwaacha wake zao wakati wa kurejea makwao unapowadia. ‘Ulamaa wote wanasema kwamba ndoa hii ni sahihi ikiwa atamwoa bila sharti (la muda) hata kama niya yake ni kumwacha baada ya muda. Wanasema kwamba mtu huyo anaweza kweli kunuwia hivyo lakini asije kufanya, au asinuwie kitu lakini akaja kukifanya.
Al-Awzaa’iy amekwenda kinyume nao. Anasema hiyo ni ndoa ya mut-‘a. Pia ni chaguo la Al-‘Allaamah Ibn ‘Uthaymiyn. [Al-Istidhkaar (16/301)]
Huenda kauli hii ya Al-Awzaaiy ikawa na mantiki zaidi. Na inatiliwa nguvu na kauli ya Ibn ‘Umar iliyogusiwa nyuma kidogo alipoulizwa kuhusu mtu ambaye alitaka kumwoa mke wa nduguye ili amhalalishie, naye akasema: “Hapana, isipokuwa kama itakuwa ni ndoa ya utashi wa kuendelea kuishi naye (kama atampendeza). Tulikuwa tunalizingatia hili wakati wa enzi ya Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kama ni zinaa na uchafu”.
Kuongezea na hilo, aina hii ya ndoa inakuwa na ghushi na udanganyifu ndani yake, inazalisha uadui na chuki, inaondosha kuaminiana kati ya Waislamu, inaitweza nafsi na kuitosa ndani ya dimbwi la matamanio, mbali na uharibifu mkubwa unaozalikana. Na kwa matatizo haya, ndoa hii inastahiki kuwa batili.
Swahiyh Fiqh As-Sunnah
كِتَابُ الزَّوَاجِ
Kitabu Cha Ndoa
الأَنْكِحَةُ الفَاسِدَةُ شَرْعًا
Ndoa Ambazo Ni Batili Kisharia
Alhidaaya.com [3]
30: Ndoa Ya Siri (Ndoa Isiyosajiliwa Rasmi):
Ndoa inayokusudiwa hapa ni ile tabia iliyoenea kati ya vijana ambapo kijana hutokea akafanya mahusiano na msichana ambaye anaweza kuwa ni mwanafunzi mwenzake chuoni. Mahusiano kati yao yanakuwa ni ya siri bila yeyote kujua, au wanaweza kujua baadhi ya marafiki wao wa karibu sana. Kisha wawili hao huanza kufanya mapenzi katika sehemu yoyote ya siri, halafu msichana anarudi nyumbani kwao kama kawaida bila wazazi wake kujua chochote kinachoendelea. Mahusiano haya yanakuwa kwenye karatasi tu ambayo inakuwa haitambuliwi na vyombo husika vya dola, na mashahidi wao wanakuwa ni hao hao marafiki zao mafasiki.
Ndoa hii ni batili, bali kiuhalisia ni zinaa, kwa kuwa imekosa sharti miongoni mwa shuruti za ndoa ambayo inakuwa haifai bila kuwepo, nayo ni idhini ya walii wa mwanamke. Qur-aan na Hadiyth za Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) zimeshurutisha uwepo wa walii ili ndoa iwe sahihi. Na huu ndio msimamo wa Jumhuwr ya ‘Ulamaa. Na kwa msingi huu, ndoa hii ni lazima ivunjwe.
Swahiyh Fiqh As-Sunnah
كِتَابُ الزَّوَاجِ
Kitabu Cha Ndoa
الصِّفَاتُ المطْلُوْبَةُ في الزَّوْجَينِ
Sifa Ambazo Mke Na Mume Wanatakiwa Kuwa Nazo:
Alhidaaya.com [3]
31. Sifa Ambazo Inapendeza Mke Kuwa Nazo: Mke
1- Awe ameshika dini:
Ni kwa Kauli Yake Ta’aalaa:
"وَلَأَمَةٌ مُّؤْمِنَةٌ خَيْرٌ مِّن مُّشْرِكَةٍ وَلَوْ أَعْجَبَتْكُمْ"
“Na mjakazi Muumini ni bora kuliko mshirikina japo akikupendezeni”. [Al-Baqarah: 221]
Na kwa kauli ya Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa sallam):
"فَاظْفَرْ بِذَات الدِّيْنِ تَرِبَتْ يَدَاكَ"
“Basi mpanie mwenye dini, (la sivyo) utaharibikiwa”. [Hadiyth Swahiyh]
2- Akiwa ni mwenye dini, jamala, nasaba njema na mali, itakuwa ni bora zaidi:
Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
"تُنْكَحُ الْمَرْأَةُ لِأَرْبَعٍ: لِمَالِهَا وَلِحَسَبِهَا وَلِجَمَالِهَا وَلِدِينِهَا، فَاظْفَرْ بِذَاتِ الدِّيْنِ تَرِبَتْ يَدَاكَ"
“Mwanamke huolewa kwa moja ya mambo manne: Kwa mali yake, kwa hadhi yake, kwa uzuri wake, na kwa dini yake. Basi mpanie mwenye dini, (la sivyo) utaharibikiwa”. [Al-Bukhaariy (5090) na Muslim (1466)]
3- Awe mpole mwenye huruma:
Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
"خَيْرُ نسَاء رَكِبْنَ الْإِبِلَ صَالحَ نِسَاء قُرَيْش أَحْنَاهُ عَلَى وَلَدٍ فِي صِغَرِهِ وَأَرْعَاهُ عَلَى زَوْجٍ فِي ذَاتِ يَدِهِ"
“Wanawake bora zaidi waliopanda ngamia, ni wanawake wema wa Kiquraysh. Wana huruma mno kwa watoto wadogo, na wanasimamia vyema mali za waume zao”. [Al-Bukhaariy (5082) na Muslim (2527)]
4- Inapendeza zaidi akiwa bikra:
Ni pale Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alipomuuliza Jaabir bin ‘Abdillaah alipooa: Je, ni bikra au mkubwa (aliyewahi kuolewa)? Akamwambia: Ni mkubwa. Akamwambia:
فَهَلاَّ بِكْرًا تُلاَعِبُهَا وَتُلَاعِبَكَ"
“Kwa nini usioe bikra ukamchezea naye akakuchezea?” [Al-Bukhaariy (5079) na Muslim (715)]
Ni vyema mno kuoa bikra isipokuwa kama kuna sababu ya nguvu ya kuoa mwanamke aliyewahi kuolewa, kama kupata ukwe wa watu wema, au kumliwaza aliyefiwa na mume wake, au kulea mayatima na mfano wa hayo.
5- Awe mzuri, mtiifu na mwaminifu:
Ni kwa Hadiyth ya Abu Hurayrah kwamba Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) aliulizwa kuhusu mwanamke aliye bora zaidi, akajibu:
"الَّتِي تَسُرُّهُ إِذَا نَظَرَ، وَتُطِيعُهُ إِذَا أَمَرَ، وَلَا تُخَالِفُهُ فِيمَا يَكْرَهُ فِيْ نَفْسِهَا وَلَا فِيْ مَالِهِ"
“Ni yule ambaye mumewe anafurahi anapomwangalia, anamtii anapomwamrisha, na haendi kinyume naye katika yale asiyopenda yeye kuwa nayo wala katika mali yake”. [Hadiyth Swahiyh. Imekharijiwa na An-Nasaaiy (6/68) na Ahmad (7373)]
6- Awe mwenye penzi na mwenye kizazi:
Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amehimiza hili kama zilivyogusia Hadiyth zilizotangulia nyuma.
Swahiyh Fiqh As-Sunnah
كِتَابُ الزَّوَاجِ
Kitabu Cha Ndoa
الصِّفَاتُ المطْلُوْبَةُ في الزَّوْجَينِ
Sifa Ambazo Mke Na Mume Wanatakiwa Kuwa Nazo:
Alhidaaya.com [3]
32: Sifa Ambazo Inapendeza Mume Kuwa Nazo: Mume
1- Awe ameshika dini:
Ni kwa Kauli Yake Ta’alaa:
"وَلَعَبْدٌ مُّؤْمِنٌ خَيْرٌ مِّن مُّشْرِكٍ وَلَوْ أَعْجَبَكُمْ"
“Na mtumwa Muumini ni bora kuliko mshirikina japo akikupendezeni”. [Al-Baqarah: 221]
2- Awe amehifadhi kiasi fulani Kitabu cha Allaah ‘Azza wa Jalla:
Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alimwozesha mtu mmoja katika Maswahaba wake kwa Qur-aan kidogo aliyohifadhi. [Hadiyth Swahiyh. Imekharijiwa na Al-Bukhaariy (5029) na Muslim (1425)]
3- Awe na nyenzo za kuolea kwa aina zake mbili ambazo ni uwezo wa kujimai, na gharama za kuolea pamoja na kipato cha kuendeshea maisha.
Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amewahimiza vijana kuoa wakati wanapokuwa na uwezo wa mahitajio ya ndoa. Alimwambia Faatwimah bint Qays:
"وَأَمَّا مُعَاوِيَةُ فَصُعْلُوكٌ لاَ مَالَ لَه"ُ
“Ama Mu’aawiya, huyo ni masikini hohehahe, hana chochote”. [Muslim (1480), An-Nasaaiy (3245) na Abu Daawuwd (2284)]
5- Awe mwenye muamala mwema kwa wanawake:
Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alisema kuhusiana na Abu Jahm:
"أَمَّا أَبُو جَهْمِ فَرَجُلٌ لا يَضَعُ عَصَاهُ عَنْ عَاتِقِهِ، وَلكِنْ انْكِحِي أُسَامَةَ"
“Ama Abu Jahm, yeye ni mtu ambaye hashushi fimbo yake begani (yaani anapiga sana, au anasafiri sana), mwache Usamah akuoe”. [Muslim (1480), An-Nasaaiy (3245) na Abu Daawuwd (2284)]
5- Mwanamke afurahi akimwona:
Ili asipate hisia ya kichefuchefu na kupoteza hamu naye, lakini pia asije kukufuru neema anazopata toka kwa mumewe.
6- Asiwe tasa:
Ni kwa Hadiyth zinazogusia fadhla ya kuwa na watoto.
7- Alingane viwango na mwanamke:
Ulingano huu ni mfanano na usawa katika aina hizi zifuatazo:
(a) Ulingano wa dini: Hili ni sharti muhimu la kuswihi kwa ndoa kwa makubaliano ya ‘Ulamaa. Haifai mwanamke wa Kiislamu kuolewa na kafiri kwa ‘Ijmaa ya ‘Ulamaa.
Lakini pia haitakikani kwa Muislamu kumwozesha binti yake mwema mtu fasiki, kwani Allaah Ta’aalaa Amesema:
"الْخَبِيثَاتُ لِلْخَبِيثِينَ وَالْخَبِيثُونَ لِلْخَبِيثَاتِ ۖ وَالطَّيِّبَاتُ لِلطَّيِّبِينَ وَالطَّيِّبُونَ لِلطَّيِّبَاتِ ۚ أُولَـٰئِكَ مُبَرَّءُونَ مِمَّا يَقُولُونَ ۖ لَهُم مَّغْفِرَةٌ وَرِزْقٌ كَرِيمٌ"
“Kauli ovu inaendana na watu waovu, na watu waovu wanaendana na kauli ovu. Na kauli njema inaendana na watu wema, na watu wema wanaendana na kauli njema. Hao wametakaswa na tuhuma za wanayoyasema, watapata maghfirah na riziki karimu”. [Nuur: 26]
Hili pamoja na ubaya wake, lakini halizuii kuswihi kwa ndoa.
2- Ulingano wa nasaba: Hili limetiliwa maanani sana na Jumhuwr ya ‘Ulamaa kinyume na Imaam Maalik.
3- Ulingano wa mali. Allaah Ta’aalaa Amesema:
"الرِّجَالُ قَوَّامُونَ عَلَى النِّسَاءِ بِمَا فَضَّلَ اللَّـهُ بَعْضَهُمْ عَلَىٰ بَعْضٍ وَبِمَا أَنفَقُوا مِنْ أَمْوَالِهِمْ"
“Wanaume ni wasimamizi juu ya wanawake kwa kuwa Allaah Amefadhilisha baadhi yao kuliko wengine na pia kwa ambayo wanatoa katika mali zao”. [An-Nisaa: 34]
Hili limezingatiwa na ‘Ulamaa wa Kihanafiy, Kihanbali na Kishaafi’iy. ‘Ulamaa wa Kimaaliki hawajalizingatia hili. Wanasema kwamba mali ni kitu kinachoweza kuondoka kama afya na kuja ugonjwa. Hivyo basi, mwanamke mwenye uwezo wa mali, anaweza kuolewa na mume fakiri.
4- Ulingano wa uhuru: (Yaani muungwana kwa muungwana na mtumwa kwa kijakazi). Limezingatiwa hili na Jumhuwr ya ‘Ulamaa kinyume na Maalik.
5- Ulingano wa kazi: (Mume mwenye kazi duni sana haendani na mwanamke mwenye wadhifa wa juu kama injinia au daktari).
Hili limezingatiwa kwa umuhimu mkubwa pia na ‘Ulamaa wa Kihanafiy, Kihanbali na Kishaafi’iy.
6- Kusalimika na kasoro zozote mbaya. Ni kama ukoma, mbalanga, wendawazimu na kadhalika.
Lakini Je, Ulingano Huu Ni Sharti Ya Kusihi Kwa Ndoa?
‘Ulamaa wana kauli mbili kuhusiana na shurutisho la ulingano huu. Kauli iliyo sahihi zaidi ni ya Jumhuwr ya ‘Ulamaa akiwemo Abu Haniyfah, Maalik, Ash-Shaafi’iy na Ahmad, lakini pia imesimuliwa toka kwa ‘Umar na Ibn Mas-‘uwd (Radhwiya Allaah ‘anhumaa). Kauli hii inasema kwamba ulingano si sharti ya kuswihi ndoa kwa mujibu wa dalili zifuatazo:
1- Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alimwozesha Zaynab binti Jahsh (toka ukoo mtukufu wa Asad) Zayd bin Haarithah (ambaye alikuwa ni mtumwa mwachwa huru wa Rasuli). Kisa chao kimeelezewa katika Qur-aan Tukufu ambapo Allaah Anasema:
"وَإِذْ تَقُولُ لِلَّذِي أَنْعَمَ اللَّـهُ عَلَيْهِ وَأَنْعَمْتَ عَلَيْهِ أَمْسِكْ عَلَيْكَ زَوْجَكَ وَاتَّقِ اللَّـهَ وَتُخْفِي فِي نَفْسِكَ مَا اللَّـهُ مُبْدِيهِ وَتَخْشَى النَّاسَ وَاللَّـهُ أَحَقُّ أَن تَخْشَاهُ ۖ فَلَمَّا قَضَىٰ زَيْدٌ مِّنْهَا وَطَرًا زَوَّجْنَاكَهَا"
“Na pale ulipomwambia yule ambaye Allaah Amemneemesha nawe ukamneemesha: Mshikilie mkeo, na mche Allaah! Na ukaficha katika nafsi yako ambayo Allaah Ametaka kuyafichua, na unakhofu watu, na hali Allaah Ana haki zaidi umkhofu. Basi Zayd alipomaliza haja kwake Tukakuozesha”. [Al-Ahzaab: 37]
2- Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ambaye ni wa ukoo wa Haashimiy, aliwaozesha mabinti zake wawili kwa ‘Uthmaan bin ‘Affaan ambaye ni Mquraysh. Amesema (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam):
"إِنَّ اللَّهَ اصْطَفَى كِنَانَةَ مِنْ وَلَدِ إِسْمَاعِيلَ، وَاصْطَفَى قُرَيْشًا مِنْ كِنَانَةَ، وَاصْطَفَى مِنْ قُرَيْشٍ بَنِى هَاِشِمٍ، وَاصْطَفَانِي مِنْ بَنِي هَاشِمٍ"
“Hakika Allaah Amewateua Kinaanah toka kwa watoto wa Ismaa’iyl, na Amewateua Maquraysh toka kwa Kinaanah, na Amewateua Baniy Haashim toka kwa Maquraysh, na Ameniteua mimi toka kwa Baniy Haashim”. [Hadiyth Swahiyh. Muslim (2276) na At-Tirmidhiy (3605)]
3- Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alimwozesha Usaamah bin Zayd (mwachwa huru) Faatwimah bint Qays ambaye ni Mquraysh. Hadiyth kuhusiana na hili imeelezewa nyuma.
4- Toka kwa Abu Maalik Al-Ash’ariyy, kwamba Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
"أَرْبَعٌ فِي أُمَّتِي مِنْ أَمْرِ الْجَاهِلِيَّةِ لَا يَتْرُكُونَهُنَّ: الْفَخْرُ فِي الْأَحْسَابِ، وَالطَّعْنُ فِي الْأَنْسَابِ، وَالِاسْتِسْقَاءُ بِالنُّجُومِ، وَالنِّيَاحَةُ"
“Mambo manne ya kijahiliya yako katika umma wangu, hawatoyaacha: Kujifaharisha kwa hadhi, kudharau nasaba za wengine, kuomba mvua kwa nyota (kuitakidi kuwa ndizo sababu), na kuomboleza kwa malalamiko”. [Muslim: (934) na wengineo]
5- Neno Lake Ta’aalaa:
"وَأَنكِحُوا الْأَيَامَىٰ مِنكُمْ وَالصَّالِحِينَ مِنْ عِبَادِكُمْ وَإِمَائِكُمْ ۚ إِن يَكُونُوا فُقَرَاءَ يُغْنِهِمُ اللَّـهُ مِن فَضْلِهِ ۗ وَاللَّـهُ وَاسِعٌ عَلِيمٌ"
“Na waozesheni wajane miongoni mwenu na walio Swalihina kati ya watumwa wenu wanaume na wajakazi wenu. Wakiwa mafakiri Allaah Atawatajirisha katika Fadhila Zake. Na Allaah Ni Mwenye Wasaa, Mjuzi wa yote”. [An-Nuwr: 32]
Umasikini wa mposaji usiwe ndiyo sababu ya kumkatalia, kwani kuna uwezekano mkubwa wa kutengenekewa hali siku za mbeleni.
6- Hadiyth ya Abu Sa’iyd: Kwamba Zaynab, mke wa Ibn Mas-‘uwd alikwenda kwa Rasuli na kumwambia:
"يَا رَسُولَ اَللَّهِ، إِنَّكَ أَمَرْتَ اَلْيَوْمَ بِالصَّدَقَةِ، وَكَانَ عِنْدِي حُلِيٌّ لِي، فَأَرَدْتُ أَنْ أَتَصَدَّقَ بِهِ فَزَعَمَ اِبْنُ مَسْعُودٍ أَنَّهُ وَوَلَدُهُ أَحَقُّ مَنْ تَصَدَّقْتُ بِهِ عَلَيْهِمْ، فَقَالَ اَلنَّبِيُّ صلى الله عليه وسلم: "صَدَقَ اِبْنُ مَسْعُودٍ، زَوْجُكِ وَوَلَدُكِ أَحَقُّ مَنْ تَصَدَّقْتِ بِهِ عَلَيْهِمْ".
“Ee Rasuli wa Allaah! Hakika wewe umetuamrisha leo tutoe swadaqah, nami nilikuwa na kidani changu nikataka kukitoa. Lakini Ibn Mas-‘uwd akadai kwamba yeye na wanaye wana haki zaidi ya kupewa swadaqah hiyo. Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akamwambia: Amesema kweli Ibn Mas-‘uwd. Mumeo na wanao wanastahiki zaidi swadaqah yako”. [Al-Bukhaariy (1462) na Muslim (1000)]
Hadiyth hii inaonyesha kwamba Bi Zaynab alikuwa na hali nzuri zaidi ya kifedha kuliko mumewe Ibn Mas-‘uwd.
7- Hadiyth ya Abu Hurayrah:
"أَنَّ أَبَا هِنْدٍ، حَجَمَ النَّبِيَّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ فِي الْيَافُوخِ، فَقَالَ النَّبِيُّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ:" يَا بَنِي بَيَاضَةَ، أَنْكِحُوا أَبَا هِنْدٍ وَانْكِحُوا إِلَيْه"
“Kwamba Abu Hind alimuumika Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) katikati ya kichwa chake. Na Rasuli akasema: Enyi Bani Bayaadha! Mwozesheni Abu Hind (banati zenu), na nyinyi oeni kwake (banati zake)”. [Hadiyth Hasan. Abu Daawuwd (2102), Al-Haakim (2/164) na Al-Bayhaqiy (7/136)]
Abu Hind hana uhusiano na Baniy Bayaadha, bali alikuwa mtumwa kwao kisha wakamwacha huru. Lakini pia alikuwa ni muumikaji, na kazi hii ilikuwa ndiyo duni zaidi kuliko zote kwa wakati huo.
8- Hadiyth ya ‘Aaishah aliyesema:
"اشْتَرَيْتُ بَرِيرَةَ فَاشْتَرَطَ أَهْلُهَا وَلاَءَهَا فَذَكَرْتُ ذَلِكَ لِلنَّبِيِّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ فَقَالَ: أَعْتِقِيهَا فَإِنَّ الْوَلاَءَ لِمَنْ أَعْطَى الْوَرِقَ. قَالَتْ فَأَعْتَقْتُهَا، فَدَعَاهَا رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ فَخَيَّرَهَا مِنْ زَوْجِهَا فَقَالتْ: لَوْ أَعْطَانِيْ كذا وكذا مَا ثبتُّ عِنْدَهُ"
“Nilimnunua Bariyrah, lakini wanaommiliki walishurutisha kwamba fungamano lake libakie kwao. Nikamweleza Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallama) hilo naye akaniambia: Mwache huru, kwa sababu fungamano linakuwa kwa yule aliyelipa pesa, nami nikamwacha huru. Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akamwita na kumkhiyarisha kati ya kubaki na mumewe au kuvunja ndoa, naye akasema: Hata akanipa nini sibaki naye”. [Hadiyth Swahiyh. Al-Bukhaariy (2536) na Muslim (1504)]
Mumewe alikuwa ni mtumwa, na Bariyrah baada ya kuachwa huru, akawa muungwana, ndiyo maana Rasuli akamkhiyarisha. Na kama mumewe angekuwa muungwana, basi Rasuli asingemkhiyarisha, bali angebakia kwa mumewe.
Na katika Hadiyth ya Ibn ‘Abbaas:
"فَقَالَ النَّبِيُّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: لَوْ راجعته، فَقَالَتْ: يَا رَسُولَ اللَّهِ تَأْمُرُنِي؟ قَالَ: إِنَّمَا أَشْفَعُ قَالَتْ: لَا حَاجَةَ لِي فِيهِ"
“Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akamwambia: Natamani lau ungelirejea uishi naye. Akasema: Je hiyo ni amri ewe Rasuli wa Allaah? Akamwambia: Hapana, bali ni ombi. Akasema: Sina haja naye”. [Al-Bukhaariy (5283), Abu Daawuwd (2231), An-Nasaaiy (8/245) na Ibn Maajah (2075)]
9- Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
"إِذَا جَاءَكُمْ مَنْ تَرْضَوْنَ دِينَهُ وَخُلُقَهُ فَأَنْكِحُوهُ، إِلاَّ تَفْعَلُوا تَكُنْ فِتْنَةٌ فِي الأَرْضِ وَفَسَادٌ كَبِيْرٌ"
“Akiwajieni mnayemridhia dini yake na tabia yake, basi mwozesheni. Na kama hamtofanya, basi utakuwepo mtafaruku na uharibifu mkubwa ardhini”. [At-Tirmidhiy (1090) na wengineo. Ina asaaniyd dhaifu, lakini matini nyingine za kisharia zinaipa nguvu]
Ahmad katika riwaayah yake mashuhuri, Ath-Thawriy na baadhi ya ‘Ulamaa wa Kihanafiy, wanasema kwamba ulingano wa viwango ni sharti. Wametoa dalili ambazo baadhi yake hazijathibiti. Ama zilizothibiti, hizo haziko wazi katika kushurutisha hilo, lakini pia hazina nguvu ya kupinga Hadiyth zilizotangulia.
Faida:
Ya kwanza:
Kwa wale wenye kushurutisha ulingano, haki hiyo inakuwa ni ya mwanamke na mawalii. Kwa maana kwamba ikiwa mwanamke na walii wake wataridhia kutokuweko ulingano huo, basi ndoa ni sahihi. Si Imaam Ahmad wala mwingine yeyote katika ‘Ulamaa aliyesema kwamba itakuwa ni batili. [Zaadul Ma’aad (5/161) na Jaami’u Ahkaamin Nisaa (3/284)]
Ya pili:
Wengi katika wanaoshurutisha ulingano ili ndoa iswihi, wanaona kwamba ulinganio ni sharti lazimisho, kwa maana kwamba nikaha itakuwa ni lazima kama ulinganio upo, na kama itafungwa bila kuwepo ulinganio lakini kwa ridhaa ya mwanamke na mawalii, basi itaswihi. Lakini kama mmoja wa mawalii hatoridhia, basi ndoa haitofungwa, itafutwa.
Ya tatu:
Ulingano unazingatiwa kwa mwanamume tu na si kwa mwanamke. Ikiwa mtu atamwoa mwanamke ambaye harandani naye, basi hakuna tatizo, kwa kuwa usimamizi unakuwa mkononi kwake, watoto watanasibishwa naye, na talaka anaimiliki. Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alioa kwenye makabila tofauti ya Waarabu na hakuna aliye sawa naye kwa dini wala kwa nasaba, na pia alilala na vijakazi. Na yeye anasema:
"مَنْ كَانَتْ عِنْدَهُ جَارِيَةٌ فَعَلَّمَهَا وَأَحْسَنَ تَعْلِيمَهَا وَأَحْسَنَ إِلَيْهَا، ثُمَّ أَعْتَقَهَا وَتَزَوَّجَهَا فَلَهُ أَجْرَانِ"
“Atakayekuwa na kijakazi, kisha akamfundisha na akamwelimisha vyema, na isitoshe akamtendea wema, halafu akamwacha huru na kumwoa, basi ana ujira mbili”. [Hadiyth Swahiyh. Al-Bukhaariy (2544), Muslim (154). Angalia Al-Mughniy (6/487), Al-Mabsuwtw (5/29) na Jaami’u Ahkaamin Nisaa (3/287)]
Links
[1] https://www.alhidaaya.com/sw/taxonomy/term/284
[2] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11189&title=10A-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20%20%D9%83%D8%AA%D8%A7%D8%A8%20%D8%A7%D9%84%D8%B2%D9%88%D8%A7%D8%AC%20Kitabu%20Cha%20Ndoa%20%20
[3] http://www.alhidaaya.com/
[4] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11686&title=01-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20Kitabu%20Cha%20Ndoa%3A%20Himizo%20Na%20Raghibisho%20La%20Kuoa
[5] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11687&title=02-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20Kitabu%20Cha%20Ndoa%3A%20Ni%20Haramu%20Mwanaume%20Kuhasiwa%20%28Kuondoshwa%20Korodani%20Mtu%20Asiwe%20Na%20Matamanio%20Tena%20Ya%20Kujimai%29
[6] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11688&title=03-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20Kitabu%20Cha%20Ndoa%3A%20Baadhi%20Ya%20Faida%20Za%20Kuoa
[7] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11689&title=04-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20Kitabu%20Cha%20Ndoa%3A%20Hukumu%20Ya%20Kuoa
[8] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11690&title=05-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20Kitabu%20Cha%20Ndoa%3A%20Mwanamke%20Anaweza%20Kukataa%20Kuolewa
[9] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11691&title=06-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20Kitabu%20Cha%20Ndoa%3A%20Wanawake%20Ambao%20Ni%20Haramu%20Kuwaoa
[10] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11692&title=07-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20Kitabu%20Cha%20Ndoa%3A%20Wanawake%20Walioharamika%20Kuwaoa%20Milele%3A%20Walio%20Haramu%20Kwa%20Sababu%20Ya%20Nasaba%20%28Hawa%20Ni%20Saba%29
[11] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11693&title=08-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20Kitabu%20Cha%20Ndoa%3A%20Walioharamishwa%20%20Kwa%20Sababu%20Ya%20Uhusiano%20Wa%20Ndoa%20%28Hawa%20Ni%20Wanne%29
[12] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11694&title=09-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20Kitabu%20Cha%20Ndoa%3A%20Walioharamishwa%20Kwa%20Sababu%20Ya%20Kunyonya
[13] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11695&title=10-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20Kitabu%20Cha%20Ndoa%3A%20Masharti%20Ya%20Uharamu%20%28Umahram%29%20Kwa%20Sababu%20Ya%20Kunyonya%3A%20Idadi%20Ya%20Manyonyesho%20Ya%20Kuleta%20Uharamu%20%28Umahram%29%3A%20%20Kauli%20Ya%20Kwanza
[14] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11696&title=11-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20Kitabu%20Cha%20Ndoa%3A%20Masharti%20Ya%20Uharamu%20%28Umahram%29%20Kwa%20Sababu%20Ya%20Kunyonya%3A%20Idadi%20Ya%20Manyonyesho%20Ya%20Kuleta%20Uharamu%20%28Umahram%29%3A%20%20Kauli%20Ya%20Pili
[15] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11697&title=12-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20Kitabu%20Cha%20Ndoa%3A%20Masharti%20Ya%20Uharamu%20%28Umahram%29%20Kwa%20Sababu%20Ya%20Kunyonya%3A%20Idadi%20Ya%20Manyonyesho%20Ya%20Kuleta%20Uharamu%20%28Umahram%29%3A%20%20Kauli%20Ya%20Tatu
[16] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11698&title=13-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20Kitabu%20Cha%20Ndoa%3A%20Masharti%20Ya%20Uharamu%20%28Umahram%29%20Kwa%20Sababu%20Ya%20Kunyonya%3A%20Idadi%20Ya%20Manyonyesho%20Ya%20Kuleta%20Uharamu%20%28Umahram%29%3A%20%20Kauli%20Ya%20Nne
[17] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11699&title=14-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20Kitabu%20Cha%20Ndoa%3A%20Mpaka%20Wa%20Muda%20Wa%20Kunyonya%20Ili%20Umahramu%20Upatikane
[18] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11700&title=15-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20Kitabu%20Cha%20Ndoa%3A%20Sifa%20Ya%20Nyonyesho%20Lenye%20Kuleta%20Umahram
[19] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11701&title=16-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20Kitabu%20Cha%20Ndoa%3A%20Wanawake%20Walioharamika%20Kwa%20Muda%3A%20i-Dada%20Ya%20Mke
[20] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11702&title=17-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20Kitabu%20Cha%20Ndoa%3A%20Wanawake%20Walioharamika%20Kwa%20Muda%3A%20ii-Khalati%20Ya%20Mke%20Au%20Shangazi%20Yake%3A
[21] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11703&title=18-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20Kitabu%20Cha%20Ndoa%3A%20Wanawake%20Walioharamika%20Kwa%20Muda%3A%20iii-Mke%20Wa%20Mtu%2C%20Au%20Mwanamke%20Ambaye%20Bado%20Yuko%20Kwenye%20Eda%20Isipokuwa%20Mateka%2C%20Na%20Mke%20Wa%20Kafiri%20Akisilimu
[22] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11704&title=19-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20Kitabu%20Cha%20Ndoa%3A%20Wanawake%20Walioharamika%20Kwa%20Muda%3A%20iv-Aliyeachwa%20Talaka%20Tatu
[23] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11705&title=20-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20Kitabu%20Cha%20Ndoa%3A%20Wanawake%20Walioharamika%20Kwa%20Muda%3A%20v-Mpagani%20Mpaka%20Asilimu
[24] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11706&title=21-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20Kitabu%20Cha%20Ndoa%3A%20Kuoa%20Wanawake%20Wa%20Ahlul%20Kitaab%20Kuko%20Nje%20Ya%20Duara%20La%20Uharamisho
[25] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11707&title=22-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20Kitabu%20Cha%20Ndoa%3A%20Mwanamke%20Wa%20Kiislamu%20Ni%20Haramu%20Kuolewa%20Na%20Kafiri
[26] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11708&title=23-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20Kitabu%20Cha%20Ndoa%3A%20Wanawake%20Walioharamika%20Kwa%20Muda%3A%20vi-Mwanamke%20Mzinifu%20Mpaka%20Atubie
[27] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11709&title=24-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20Kitabu%20Cha%20Ndoa%3A%20Haijuzu%20Kumwoa%20Mwanamke%20Mzinifu%20%28Kahaba%29%20Ila%20Kwa%20Masharti%20Mawili
[28] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11710&title=25-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20Kitabu%20Cha%20Ndoa%3A%20Wanawake%20Walioharamika%20Kwa%20Muda%3A%20vii-Mwanamke%20Aliyehirimia%20Mpaka%20Afunguke%20Na%20Ihraam
[29] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11711&title=26-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20Kitabu%20Cha%20Ndoa%3A%20Wanawake%20Walioharamika%20Kwa%20Muda%3A%20%20viii-Mke%20Wa%20Tano%20Ikiwa%20Mtu%20Ana%20Wake%20Wanne%20Tayari
[30] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11736&title=27-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20Kitabu%20Cha%20Ndoa%3A%20Ndoa%20Ambazo%20Ni%20Batili%20Kisharia%3A%20Ndoa%20Ya%20Shighaar
[31] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11731&title=28-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20Kitabu%20Cha%20Ndoa%3A%20Ndoa%20Ambazo%20Ni%20Batili%20Kisharia%3A%20Ndoa%20Ya%20Mhalalishaji
[32] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11732&title=29-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20Kitabu%20Cha%20Ndoa%3A%20Ndoa%20Ambazo%20Ni%20Batili%20Kisharia%3A%20Ndoa%20Ya%20Mut%E2%80%99a
[33] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11733&title=30-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20Kitabu%20Cha%20Ndoa%3A%20Ndoa%20Ambazo%20Ni%20Batili%20Kisharia%3ANdoa%20Ya%20Siri%20%28Ndoa%20Isiyosajiliwa%20Rasmi%29
[34] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11780&title=31-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20Kitabu%20Cha%20Ndoa%3A%20Sifa%20Ambazo%20Mke%20Na%20Mume%20Wanatakiwa%20Kuwa%20Nazo%3A%20Mke
[35] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11781&title=32-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20Kitabu%20Cha%20Ndoa%3A%20Sifa%20Ambazo%20Mke%20Na%20Mume%20Wanatakiwa%20Kuwa%20Nazo%3A%20Mume