001-Al-Faatihah: Utangulizi Wa Suwrah
Alhidaaya.com [2]
Imeteremka: Makkah kwa itifaki ya ‘Ulamaa.
Idadi Ya Aayah: 7
Jina La Suwrah: Al-Faatihah:
Suwrah imeitwa Al-Faatihah (Ufunguo), na yanayodalilisha ni kutajwa kwake katika Hadiyth zilizonukuliwa katika Fadhila za Suwrah. Na Suwrah imeitwa Al-Faatihah (Ufunguo), kutokana na Suwrah kuwa ya mwanzo katika Mswahafu.
Majina Yake Mengineyo: (i) Ummul-Qur-aan (Mama wa Qur-aan) (ii) AlhamduliLlaah (Himdi Anastahiki Allaah) (iii) Asw-Swalaah (Swalaah, duaa) (iv) Ash-Shifaa (shifaa, poza, tiba) (v) Ar-Ruqyah (kinga) (vi) Sab‘ul-Mathaaniy (Aayah saba zinazokaririwa na kusomwa) (vii) Al-Qur-aan Al-‘Adhwiym (Qur-aan Adhimu) (viii) Ummul-Kitaab (Mama wa Kitabu).
Miongoni Mwa Makusudio Ya Suwrah:
1-Kuthibitisha kuwa wanaadam wote ni waja wa Allaah (سبحانه وتعالى) [Al-Mukhtaswar Fiy Tafsiyr Al-Qur-aan Al-Kariym]
2-Kuthibitishwa kumwabudu Allaah (سبحانه وتعالى) kwa ikhlaasw.
3-Kuwakumbusha waja kwamba wao ni waja, na Anaepaswa kuabudiwa na kuombwa msaada ni Allaah (سبحانه وتعالى).
4-Kubainisha hali za watu na njia iliyonyooka.
Miongoni Mwa Maudhui Ya Suwrah:
1-Suwrah imefunguliwa kwa kutajwa Sifa za Allah (عز وجل).
2-Imetajwa Siku ya Malipo.
3-Imethibitishwa Kumpwekesha Allaah (سبحانه وتعالى) katika ibaada na katika kuomba msaada.
4-Inaelekeza kuomba hidaaya ya kuongozwa katika njia iliyonyooka.
5-Imetambulisha njia iliyonyooka, ambayo ni njia ya walioneemeshwa na waliohidika.
6-Suwrah imekhitimishwa kwa kuelekeza kujiepusha na njia ya wale walioghadhibikiwa na Allaah na waliopotea.
Fadhila Za Suwrah:
1-Ni Suwrah Tukufu Kabisa:
عَنْ أَبِي سَعِيدِ بْنِ الْمُعَلَّى رضى الله عنه ـ قَالَ كُنْتُ أُصَلِّي فَمَرَّ بِي رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم فَدَعَانِي فَلَمْ آتِهِ حَتَّى صَلَّيْتُ، ثُمَّ أَتَيْتُهُ فَقَالَ " مَا مَنَعَكَ أَنْ تَأْتِيَ أَلَمْ يَقُلِ اللَّهُ يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اسْتَجِيبُوا لِلَّهِ وَلِلرَّسُولِ إِذَا دَعَاكُمْ - ثُمَّ قَالَ: لأُعَلِّمَنَّكَ أَعْظَمَ سُورَةٍ فِي الْقُرْآنِ قَبْلَ أَنْ أَخْرُجَ ". فَذَهَبَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم لِيَخْرُجَ فَذَكَرْتُ لَهُ. وَقَالَ مُعَاذٌ حَدَّثَنَا شُعْبَةُ، عَنْ خُبَيْبٍ، سَمِعَ حَفْصًا، سَمِعَ أَبَا سَعِيدٍ، رَجُلاً مِنْ أَصْحَابِ النَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم بِهَذَا، وَقَالَ هِيَ {الْحَمْدُ لِلَّهِ رَبِّ الْعَالَمِينَ} السَّبْعُ الْمَثَانِي.
Amesimulia Abuu Sa’iyd bin Al-Mu’allaa (رضي الله عنه) : Nilikuwa nikiswali, Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akaniita nikawa sikumuitikia mpaka nilipomaliza kuswali. Kisha nikamwendea akaniambia: “Kimekuzuia nini usinijie?” Nikasema: Ee Rasuli wa Allaah, nilikuwa naswali. Akasema: “Kwani Allaah Hakusema:
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اسْتَجِيبُوا لِلَّـهِ وَلِلرَّسُولِ إِذَا دَعَاكُمْ لِمَا يُحْيِيكُمْ ۖ
“Enyi walioamini! Muitikieni Allaah na Rasuli Anapokuiteni kwenye yale yenye kukupeni uhai mwema (wa dunia na Aakhirah).” [Al-Anfaal (8:24)]
Kisha akasema: “Nitakufundisha Suwrah Tukufu kabisa katika Qur-aan kabla hujatoka Msikitini.” Akanikamata mkono, alipotaka kutoka Msikitini, nikamwambia: Ee Rasuli wa Allaah, ulisema utanifundisha Suwrah Tukufu kabisa katika Qur-aan. Akasema: “Naam,
الْحَمْدُ لِلَّـهِ رَبِّ الْعَالَمِينَ ﴿٢﴾
“AlhamduliLLaah (Himdi Anastahiki) Allaah Rabb wa walimwengu.”
Hizo ni (Aayaat) Saba zinazokaririwa (kusomwa) na Qur-aan Adhimu niliyopewa.” [Al-Hijr (15:87) ameipokea Al-Bukhaariy]
2-Swalaah Haitimii Bila Ya Kusomwa Suwrah Al-Faatihah:
‘Ubaadah bin Swaamit (رضي الله عنه) amehadithia kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Hakuna Swalaah kwa asiyesoma (ndani yake) Ufunguo wa Kitabu.” [Al-Bukhaariy, Muslim]
عَنْ عُبَادَةَ بْنِ الصَّامِتِ قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: لَا صَلَاةَ لمن لم يقْرَأ بِفَاتِحَة الْكتاب.
Amesimulia ‘Ubaadah bin Swaamit (رضي الله عنه): Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Hakuna Swalaah kwa asiyesoma (ndani yake) Ufunguo wa Kitabu.” [Al-Bukhaariy, Muslim]
3-Ni Ruqyah (Kinga, Shifaa, Poza, Tiba):
عَنْ أَبِي سَعِيدٍ، أَنَّ رَهْطًا، مِنْ أَصْحَابِ رَسُولِ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم انْطَلَقُوا فِي سَفْرَةٍ سَافَرُوهَا، حَتَّى نَزَلُوا بِحَىٍّ مِنْ أَحْيَاءِ الْعَرَبِ فَاسْتَضَافُوهُمْ، فَأَبَوْا أَنْ يُضَيِّفُوهُمْ، فَلُدِغَ سَيِّدُ ذَلِكَ الْحَىِّ، فَسَعَوْا لَهُ بِكُلِّ شَىْءٍ لاَ يَنْفَعُهُ شَىْءٌ، فَقَالَ بَعْضُهُمْ لَوْ أَتَيْتُمْ هَؤُلاَءِ الرَّهْطَ الَّذِينَ قَدْ نَزَلُوا بِكُمْ، لَعَلَّهُ أَنْ يَكُونَ عِنْدَ بَعْضِهِمْ شَىْءٌ. فَأَتَوْهُمْ فَقَالُوا يَا أَيُّهَا الرَّهْطُ إِنَّ سَيِّدَنَا لُدِغَ، فَسَعَيْنَا لَهُ بِكُلِّ شَىْءٍ، لاَ يَنْفَعُهُ شَىْءٌ، فَهَلْ عِنْدَ أَحَدٍ مِنْكُمْ شَىْءٌ فَقَالَ بَعْضُهُمْ نَعَمْ، وَاللَّهِ إِنِّي لَرَاقٍ، وَلَكِنْ وَاللَّهِ لَقَدِ اسْتَضَفْنَاكُمْ فَلَمْ تُضَيِّفُونَا، فَمَا أَنَا بِرَاقٍ لَكُمْ حَتَّى تَجْعَلُوا لَنَا جُعْلاً. فَصَالَحُوهُمْ عَلَى قَطِيعٍ مِنَ الْغَنَمِ، فَانْطَلَقَ فَجَعَلَ يَتْفُلُ وَيَقْرَأُ الْحَمْدُ لِلَّهِ رَبِّ الْعَالَمِينَ حَتَّى لَكَأَنَّمَا نُشِطَ مِنْ عِقَالٍ، فَانْطَلَقَ يَمْشِي مَا بِهِ قَلَبَةٌ. قَالَ فَأَوْفَوْهُمْ جُعْلَهُمُ الَّذِي صَالَحُوهُمْ عَلَيْهِ، فَقَالَ بَعْضُهُمُ اقْسِمُوا. فَقَالَ الَّذِي رَقَى لاَ تَفْعَلُوا حَتَّى نَأْتِيَ رَسُولَ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم فَنَذْكُرَ لَهُ الَّذِي كَانَ، فَنَنْظُرَ مَا يَأْمُرُنَا. فَقَدِمُوا عَلَى رَسُولِ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم فَذَكَرُوا لَهُ فَقَالَ " وَمَا يُدْرِيكَ أَنَّهَا رُقْيَةٌ أَصَبْتُمُ اقْسِمُوا وَاضْرِبُوا لِي مَعَكُمْ بِسَهْمٍ ".
Amesimulia Abuu Sa’iyd Al-Khudriyy (رضي الله عنه): Kikundi cha Swahaba wa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) walitokea kwenda safari mpaka wakafika katika sehemu miongoni mwa sehemu za Waarabu. Wakaomba wapokelewe kama wageni wao, lakini (watu wa kabila hilo) walikataa kuwapokea. Kisha mtemi wa kabila hilo aliumwa na nyoka (au nge), naye akapewa matibabu ya aina yote lakini hakuna kilichomfaa. Baadhi yao wakasema: Je, hamtakwenda kwa kile kikundi (wasafiri) walioteremka kwenu ili muone kama mmoja wao ana chochote (cha kumtibu mtemi)? Wakawaendea na kuwaambia: Enyi kikundi! Mtemi wetu ameumwa na nyoka (au nge) nasi tumemtibu kwa kila kitu (tulicho nacho) lakini hakuna kilichomnufaisha. Je, yupo miongoni mwenu aliye na chochote (cha kumtibu)? Mmoja wao akajibu: Naam, hakika mimi najua kutibu kwa ruqyah. Lakini wa-Allaahi, tulikuombeni mtupokee kama wageni wenu lakini mlikataa. Sitamtibu mgonjwa wenu kwa ruqyah mpaka mtufanyie malipo! Kwa hiyo, wakakubali kuwalipa wasafiri wale kundi la kondoo. (Swahaba huyo) akaenda nao (watu wa kabila hilo kwa mtemi) akatemea mate (alipongatwa) huku anamsomea Suwrah Al-Faatihah mpaka mgonjwa huyo akatibika na kuanza kutembea kama kwamba hakuwa mgonjwa (kabla ya hapo). Pindi wale watu wa kabila walipowalipa pato waliokubaliana, baadhi yao (Swahaba) wakasema: Gaweni (kondoo). Lakini yule aliyetibu kwa ruqyah akasema: Msifanye hivyo mpaka tuende kwa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) kumtajia yaliyotokea ili tuone atakavyotuamuru. Wakaenda kwa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) na wakamtajia kisa chao, naye (صلى الله عليه وآله وسلم) akasema: “Mlijuaje kuwa Suwratul-Faatihah ni ruqyah? Mmepatia! Gawanyeni (mlichopata) na nigaieni sehemu yangu.” [Al-Bukhaariy]
4-Hajapatapo Kupewa Nabiy Yeyote Suwrah Al-Faatihah, Isipokuwa Nabiy Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم):
عَنِ ابْنِ عَبَّاسٍ، قَالَ بَيْنَمَا جِبْرِيلُ قَاعِدٌ عِنْدَ النَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم سَمِعَ نَقِيضًا مِنْ فَوْقِهِ فَرَفَعَ رَأْسَهُ فَقَالَ هَذَا بَابٌ مِنَ السَّمَاءِ فُتِحَ الْيَوْمَ لَمْ يُفْتَحْ قَطُّ إِلاَّ الْيَوْمَ فَنَزَلَ مِنْهُ مَلَكٌ فَقَالَ هَذَا مَلَكٌ نَزَلَ إِلَى الأَرْضِ لَمْ يَنْزِلْ قَطُّ إِلاَّ الْيَوْمَ فَسَلَّمَ وَقَالَ أَبْشِرْ بِنُورَيْنِ أُوتِيتَهُمَا لَمْ يُؤْتَهُمَا نَبِيٌّ قَبْلَكَ فَاتِحَةُ الْكِتَابِ وَخَوَاتِيمُ سُورَةِ الْبَقَرَةِ لَنْ تَقْرَأَ بِحَرْفٍ مِنْهُمَا إِلاَّ أُعْطِيتَهُ .
Amesimulia Ibn ‘Abbaas (رضي الله عنهما) : Jibriyl (عليه السلام) alipokuwa na Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alisikia sauti kutoka juu. Jibriyl (عليه السلام) akatazama juu akasema: “Huo ni mlango wa mbinguni umefunguliwa na haujapatapo kufunguliwa isipokuwa leo.” Malaika akateremka kupitia humo akasema: “Huyu Malaika ameteremka ardhini, hajapatapo kuteremka kamwe isipokuwa leo.” Akasalimia kisha akasema: “Pokea bishara ya nuru mbili ulizopewa ambazo hakuna Nabii aliyepewa kabla yako: Ufunguo wa Kitabu (Al-Faatihah), na Aayah (mbili) za mwisho wa Suwratul-Baqarah. Hutosoma herufi humo ila utapewa (ujira).” [Muslim]
5-Suwrah Al-Faatihah, Haijateremshwa Katika Tawraat Wala Katika Injiyl Wala Katika Zabuwr, Wala Hakuna Mfano Wake Katika Qur-aan:
عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رضي الله عنه أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ لأُبَيِّ بْنِ كَعْبٍ : أَتُحِبُّ أَنْ أُعَلِّمَكَ سُورَةً لَمْ يَنْزِلْ فِي التَّوْرَاةِ وَلَا فِي الْإِنْجِيلِ وَلَا فِي الزَّبُورِ وَلَا فِي الْفُرْقَانِ مِثْلُهَا ؟ قَالَ : نَعَمْ ، يَا رَسُولَ اللَّهِ ، قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ : كَيْفَ تَقْرَأُ فِي الصَّلَاةِ ؟ قَالَ : فَقَرَأَ أُمَّ الْقُرْآنِ . فَقَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ : (وَالَّذِي نَفْسِي بِيَدِهِ مَا أُنْزِلَتْ فِي التَّوْرَاةِ وَلَا فِي الْإِنْجِيلِ وَلَا فِي الزَّبُورِ وَلَا فِي الْفُرْقَانِ مِثْلُهَا) صححه الألباني في صحيح الترمذي .
Amesimulia Abuu Hurayrah (رضي الله عنه): Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alimuuliza ‘Ubayy Bin Ka’b: “Je unapenda nikufundishe Suwrah ambayo haijapata kuteremshiwa katika Tawraat, wala katika Injiyl, wala katika Zabuwr, wala hakuna mfano wake katika Qur-aan?” Akasema: Naam ee Rasuli wa Allaah. Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akamuuliza: “Unasoma nini katika Swalaah?” Akasema: Akasoma (Suwrah) ya Ummul-Kitaab (Al-Faatihah). Kisha Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akasema: “Naapa kwa Ambaye nafsi yangu imo Mikononi Mwake! Haijapata kuteremshwa katika Tawraat, wala katika Injiyl, wala katika Zabuwr wala hakuna mfano wake katika Qur-aan.” [At-Tirmidhiy na ameisahihisha Al-Albaaniy katika Swahiyh At-Tirmidhiy
6-Allaah (سبحانه وتعالى) Ameigawa Suwrah Al-Faatihah Sehemu Mbili; Sehemu Yake Na Sehemu Ya Mja Anayeisoma:
عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ (رضي الله عنه) عَنْ النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: ((مَنْ صَلَّى صَلاَةً لَمْ يَقْرَأْ فِيهَا بِأُمِّ الْقُرْآنِ فَهِيَ خِدَاجٌ)) ثَلاَثًا ((غَيْرُ تَمَامٍ)) فَقِيلَ لإِبِي هُرَيْرَةَ: إِنَّا نَكُونُ وَرَاءَ الإِمَامِ؟ فَقَالَ: اقْرَأْ بِهَا فِي نَفْسِكَ فَإِنِّي سَمِعْتُ رَسُولَ اللَّهِ (صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّم)َ يَقُولُ: ((قَالَ اللَّهُ تَعَالَى قَسَمْتُ الصَّلاَةَ بَيْنِي وَبَيْنَ عَبْدِي نِصْفَيْنِ، وَلِعَبْدِي مَا سَأَلَ. فَإِذَا قَالَ الْعَبْدُ (الْحَمْدُ لِلَّهِ رَبِّ الْعَالَمِينَ) قَالَ اللَّهُ تَعَالَى: حَمِدَنِي عَبْدِي، وَإِذَا قَالَ (الرَّحْمَنِ الرَّحِيمِ) قَالَ اللَّهُ تَعَالَى: أَثْنَى عَلَيَّ عَبْدِي، وَإِذَا قَالَ (مَالِكِ يَوْمِ الدِّينِ) قَالَ: مَجَّدَنِي عَبْدِي، وَقَالَ مَرَّةً فَوَّضَ إِلَيَّ عَبْدِي، فَإِذَا قَالَ (إِيَّاكَ نَعْبُدُ وَإِيَّاكَ نَسْتَعِينُ) قَالَ: هَذَا بَيْنِي وَبَيْنَ عَبْدِي وَلِعَبْدِي مَا سَأَلَ ))
Amesimulia Abuu Hurayrah (رضي الله عنه): Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Atakayeswali Swalaah bila ya kusoma humo mama wa Qur-aan (Suwratul-Faatihah) basi ina kasoro.” Alikariri mara tatu: “Haikutimia.” Mtu mmoja alimwambia Abuu Hurayrah: (Hata) tukiwa nyuma ya Imaam? Akasema: Isome mwenyewe (kimya kimya) kwani nilimsikia Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akisema: “Allaah (تعالى) Amesema: Nimeigawa Swalaah baina Yangu na mja Wangu nusu mbili, mja Wangu atapata yale aliyoyaomba. Mja anaposema:
الْحَمْدُ لِلَّـهِ رَبِّ الْعَالَمِينَ ﴿٢﴾
“AlhamduliLLaah (Himdi Anastahiki) Rabb wa walimwengu.”
Allaah (تعالى) Husema: Mja Wangu kanihimidi. Na anaposema:
الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ ﴿٣﴾
“Mwingi wa Rehma, Mwenye Kurehemu.”
Allaah (تعالى) Husema: Mja wangu kanisifu na kunitukuza kwa wingi. Na anaposema:
مَالِكِ يَوْمِ الدِّينِ ﴿٤﴾
“Mfalme wa Siku ya Malipo.”
Allaah (تعالى) Husema: Mja wangu kaniadhimisha. Na mara moja alisema: Mja wangu ameniaminisha. Na anaposema:
إِيَّاكَ نَعْبُدُ وَإِيَّاكَ نَسْتَعِينُ ﴿٥﴾
“Wewe Pekee tunakuabudu na Wewe Pekee tunakuomba msaada.”
Husema: Hii ni baina Yangu na mja Wangu na mja Wangu atapata kile alichokiomba. Na anaposema:
اهْدِنَا الصِّرَاطَ الْمُسْتَقِيمَ ﴿٦﴾ صِرَاطَ الَّذِينَ أَنْعَمْتَ عَلَيْهِمْ غَيْرِ الْمَغْضُوبِ عَلَيْهِمْ وَلَا الضَّالِّينَ ﴿٧﴾
“Tuongoze njia iliyonyooka. Njia ya wale Uliowaneemesha, si ya walioghadhibikiwa wala waliopotea.”
Tuongoze njia iliyonyooka, njia ya wale Uliowaneemesha, si ya walioghadhibikiwa wala waliopotea, Husema: Hii ni ya mja Wangu na mja Wangu atapata kile alichokiomba.” [Muslim, Maalik, At-Tirmidhiy, Abuu Daawuwd, An-Nasaaiy na Ibn Maajah]
7-Suwrah Al-Faatihah Ina Aayah Saba Zinazokaririwa Kusomwa:
عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ ـ رضى الله عنه ـ قَالَ قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم " أُمُّ الْقُرْآنِ هِيَ السَّبْعُ الْمَثَانِي وَالْقُرْآنُ الْعَظِيمُ ".
Amesimulia Abu Hurayrah (رضي الله عنه): Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Ummul-Qur-aan (Mama wa Qur-aan) ni Aayah saba zinazokaririwa mara kwa mara na Qur-aan Adhimu (Yaani Suwrah Al-Faatihah). [Al-Bukhaari]
Faida:
1-Suwrah Al-Faatihah ni Suwrah Adhimu kabisa kuliko Suwrah zote za Qur-aan.
2-Suwrah ya Al-Faatihah ina msingi wa Dini na matawi yake: Aqiydah (itikadi), ibaada, Sharia (hukumu), kuitakidi na kuiamini Siku ya Mwisho, kuamini Majina Mazuri ya Allaah (عزّ وجلّ) na Sifa Zake Kamilifu, Kumpwekesha Allaah (سبحانه وتعالى) katika kumuabudu na katika Isti’aanah (kumuomba msaada), na katika kuomba duaa, na kumwelekea Yeye Allaah (سبحانه وتعالى) kumuomba hidaaya ya kuongozwa katika njia iliyonyooka kwa kunyenyekea Kwake, na kumuomba kuwa miongoni mwa wema waliotangulia ambao wameneemeshwa, na kuomba kujiepuesha na njia ya walioghadhibikiwa (na Allaah) na waliopotea.
3-Ni Suwrah ambayo inajumuisha Qur-aan nzima. Na ndio maana ikawa ni Suwrah ambayo Muislamu anapaswa kuisoma katika Swalaah zake zote za faradhi na katika Swalaah za Sunnah, na ikawa hukumu yake ni faradhi (lazima), yaani: Bila ya kuisoma, Swalaah haikamiliki.
4-Suwrah imejumuisha Tawhiyd zote tatu: (i) Tawhiyd Ar-Rubuwbiyyah (Kumpwekesha Allaah katika Uola [Rabb], Uumbaji, Ufalme, Uendeshaji wa mambo yote ya ulimwengu na walimwengu, Utoaji rizki n.k) (ii) Tawhiyd Al-Uluwhiyyah (Kumpwekesha Allaah katika ibaada). (iii) Tawhiyd ya Asmaa wa Asw-Swifaat (Kumpwekesha Allaah katika Majina Yake Mazuri kabisa na Sifa Zake).
5-Suwrah Al-Faatihah (1), ni miongoni mwa Suwrah tano zinazoanzia kwa AlhamduliLlaah. Nyenginezo ni Al-An’aam (6), Al-Kahf (18), Saba-a (34) na Faatwir (35).
002-Al-Baqarah: Utangulizi Wa Suwrah
Alhidaaya.com [2]
Imeteremka: Madiynah kwa itifaki ya ‘Ulamaa.
Idadi Ya Aayah: 286
Jina La Suwrah Al-Baqarah:
Suwrah imeitwa Al-Baqarah (Ng’ombe), na yanayodalilisha ni kutajwa kwake katika Hadiyth zilizonukuliwa katika Fadhila za Suwrah. Na pia kwa kutajwa kwake katika Aayah namba (67).
Miongoni Mwa Makusudio Ya Suwrah:
1-Kulithibitisha jambo la ukhalifa (urithisaji wa kutawala) katika ardhi, kwa kuusimamisha Uislamu, na watu wote kunyenyekea kwa Allaah (سبحانه وتعالى), na kuchukua tahadhari juu ya hali iliyowatokea Bani Israaiyl. [Al-Mukhtaswar Fiy Tafsiyr Al-Qur-aan Al-Kariym]
2-Kuelezea baadhi ya sifa za wanafiki.
3-Kuelezea baadhi ya sifa za Mayahudi katika itikadi zao, na katika kuasi amri za Allaah na Rasuli wao, na mengineyo waliyoyafanyia inadi.
4-Kubainisha umuhmu wa ‘Aqiydah na kubainisha misingi yake.
5-Kubainisha dalili zenye kuthibitisha Tawhiyd ya Allaah na Uwezo Wake wa kila kitu, na hoja za wazi kabisa za kuthibitisha kufufuliwa.
6-Kubainisha baadhi ya Sharia za Kiislamu katika ibaada mbalimbali, maswala ya ndoa, na miamala ya kifedha, au adhabu kutokana na makosa mbalimbali, yasiyokuwa hayo.
Miongoni Mwa Maudhui Ya Suwrah:
1-Suwrah imefunguliwa kwa herufi zinazojulikana kama الحروف المقطعة (Al-Huruwf Al-Muqatw-twa’ah), ambazo hakuna ajuaye maana zake isipokuwa Allaah (سبحانه وتعالى). Rejea Tanbihi ya namba (2:1). Kisha ikathibitisha kwamba Qur-aan haina shaka ndani yake, na kwamba ni mwongozo, na kuwasifu Waumini wanaomkhofu Rabb wao kwa ghaibu, na wanaosimamisha Swalaah na kutoa Zakaah. Pia wanaoamini yote Aliyoyateremsha Allaah, na wanoamini Siku ya Mwisho, kisha wakabashiriwa kuwa hao ndio waliohidiwa na waliofaulu.
2-Imebainisha aina za watu, ambao ni Waumini, makafiri na wanafiki na zimetajwa baadhi ya kufru na uasi wao.
3-Wameusiwa watu wote kumuabudu Rabb wao, na zikatajwa dalili zinazothibitisha kuwa Anaestahiki kuabudiwa ni Allaah Pekee, na kuwapa tahadhari watakaoabudu ghairi ya Allaah. Kisha Waumini wamebashiriwa Jannaat za kudumu walizoandaliwa na Allaah (سبحانه وتعالى).
4-Imetajwa majadiliano kati ya Allaah (سبحانه وتعالى) na Malaika kuhusu Kumuumba Nabiy Aadam (عليه السّلام), na Aadam kupewa ukhalifa hapa ardhini, na jinsi Ibliys alivyokataa amri ya Allaah (سبحانه وتعالى) kumsujudia Aadam na kumshawishi kwake Aadam akamtelezesha, na tawbah ya Aadam (عليه السّلام).
5-Imetajwa sehemu ya kisa cha Nabiy Muwsaa (عليه السّلام) na kufadhilishwa kwa wana wa Israaiyl katika hali kadhaa, kama kuokolewa na mateso ya Firawni, kuwekewa kivuli, kuteremshiwa al-manna na as-salwaa na kadhaalika. Na imetajwa baadhi ya maasi yao, na inda zao za kutaka kumuona Allaah waziwazi. Imetajwa pia shirki zao za kumwabudu ndama, na zikatajwa baadhi ya adhabu zao.
6-Kimetajwa kisa cha Al-Baqarah (Ng’ombe) na imebainishwa Uwezo wa Allaah (سبحانه وتعالى) wa kuhuisha na kufisha.
7-Wamebashiriwa adhabu watu wa Kitabu kutokana na kubadilisha Maneno ya Allaah kwa kutaka manufaa ya dunia, na kukanusha Kitabu cha Allaah kwa kujitenga nacho na kumkanusha Nabiy Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم).
8-Wamebashiriwa adhabu wana wa Israaiyl kwa kuvunja kwao baadhi ya ahadi na fungamano kadhaa walizofungamana na Allaah, na kuamini kwao sehemu ya Kitabu na kukanusha mengineyo. Pia uasi wao wa kuwakanusha na kuwaua baadhi ya Rusuli. Pia kuasi kwao katika mambo kadhaa, na kukhiari kwao uhai wa dunia.
9-Allaah (سبحانه وتعالى) Amemwambia Rasuli Wake (صلى الله عليه وآله وسلم), awaambie waliomfanyia uadui Jibriyl (عليه السّلام), watambue kwamba yeye ndiye aliyeiteremsha Qur-aan kwake (صلى الله عليه وآله وسلم). Hivyo basi, kumfanyia kwao uadui Allaah na Rusuli Wake, na Malaika Wake khasa Malaika wawili Jibriyl na Miykaaiyl, kwamba wao ni maadui wa Allaah. Na Allaah (سبحانه وتعالى) Akamliwaza Rasuli Wake (صلى الله عليه وآله وسلم) kwa kuthibitisha kuwa Qur-aan ni ya haki na imetoka Kwake.
10-Imetolewa tahadharisho la kuwafuata mashaytwaan wanaofundisha watu uchawi (2:102), na la kufuata twaghuti (2:256-257).
11-Allaah (سبحانه وتعالى) Amefichua chuki na uhasidi wa waliopewa Kitabu (Mayahudi na Manaswara), kuchukia kheri na Fadhila za Allaah Alizomteremshia Nabiy Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم), na kwamba wanatamani Waislamu wawe makafiri kama wao.
12-Radd kwa makafiri kumsingizia Allaah kuwa kajichukulia mwana, ilhali Allaah Ametakasika na hayo!
13-Imetanabahishwa kwamba watu waliopewa Kitabu hawataridhia mpaka Waislamu wafuate mila zao, na wameonywa Waislamu kutokuwafuata au kufuata matamanio yao, bali wameamrishwa wathibitike katika Dini ya haki.
14-Imetajwa Allaah kumtahini Nabiy Ibraahiym (عليه السّلام) kwa maneno. Na kuhusu ujenzi wa Al-Ka’bah alipojenga Nabiy Ibraahiym na mwanawe Ismaa’iyl, na du’aa walizoziomba kuwaombea vizazi vyao, na kumuomba Allaah Awapelekee Rasuli atakayewasomea Aayah Zake, na kuwafunza Hikma na kuwatakasa.
15-Imetajwa wasia wa Nabiy Ibraahiym (عليه السّلام) kwa wanawe, kisha Ya’quwb (عليه السّلام) kuwausia watoto wake watahadhari na wathibitike katika Tawhiyd ya Allaah (سبحانه وتعالى) hadi kufariki kwao.
16-Waislamu wamefaridhishwa Swibghah (Dini) ya Allaah yenye kuwaongoza katika ‘Aqiydah sahihi na mwenendo mzuri upasao wa Kiislamu. Rejea faida katika Aayah namba (138).
17-Suwrah hii imetaja faradhi zote za Muislamu (Shahaada, Swalaah, Zakaah, Swawm na Hajj). Hizi zimetajwa katika sehemu mbalimbali za Suwrah, kuanzia mwanzo wake na kwengineko. Pia, Suwrah imedhihirisha Sharia nyingi upande wa ibaada, yanayohusiana na Swalaah kama umuhimu wa kusimamisha Swalaah, na Qiblah cha Waislamu. Swawm na kuteremshwa Qur-aan ndani ya Ramadhwaan. Pia baadhi ya hukmu za Hajj.
18-Imedhihirishwa miamala, kadhaa kama mas-ala ya kisasi, uharamu wa riba kisha baada ya haramisho la riba ikafuatia Aayah ya mwisho kabisa kuteremshwa katika Qur-aan. (2:281). Pia miamala ya deni na Aayah ya deni ikawa ni Aayah ndefu zaidi kuliko Aayah zote katika Qur-aan. Pia miamala ya rehani na mengineyo. Na katika upande wa familia, mambo ya ndoa, talaka, hedhi, eda, mama kumnyonyesha mwanawe, viapo (vya kujitenga na wake zao) na hukmu nyenginezo.
19-Suwrah imeweka wazi matukio ya kuhuisha wafu ambayo yanadhihirisha Uwezo wa Allaah (سبحانه وتعالى) wa Kufufua wafu. Miongoni mwa hayo, ni kisa cha aliyeuwawa katika Bani Israaiyl na kuhusiana na Al-Baqarah (ng’ombe). Kisa cha wale waliokufa kwa radi. Kisa cha wale waliotoka katika majumba yao wakiwa maelfu kwa maelfu ilihali wanaogopa kufa Allaah (سبحانه وتعالى) Akawafisha kisha Akawafufua. Kisa cha yule aliyepita kwenye kijiji kikiwa magofu matupu, Allaah (سبحانه وتعالى) Akamfisha miaka mia kisha Akamfufua (2:259). Na kisa cha Nabiy Ibraahiym (عليه السّلام) na ndege waliokatwa vipande vipande na jinsi Allaah (سبحانه وتعالى) Alivyowafufua ndege hao kwa Kuunga vipande hivyo na mbele ya macho yake (2:260).
20-Wametahadharishwa watu kutokumfuata shaytwaan anayeelekeza katika uasi na machafu.
21-Wamebashiriwa Waja wa Allaah (سبحانه وتعالى) ambao wamejaaliwa hikma kwa kunena na kutenda yaliyo haki, kwamba hao wamejaaliwa kheri nyingi mno.
22-Imeelezea pia kisa cha Twaalutw na Jaalutw wakiwa pamoja na watukufu katika Bani Israaiyl baada ya Nabiy Muwsaa (عليه السّلام) na ikadhihirisha Uwezo wa Allaah (سبحانه وتعالى) ya kuwapa ushindi waja wake wema kama Nabiy Daawuwd (عليه السّلام) katika kisa hicho cha Twaalutw na Jaalutw.
23-Imetajwa Aayah tukufu kabisa ambayo ni Aayatul-Kursiy. Na wakatahadharishwa Waislamu kutokumfuata twaghuti wasije kutoka katika nuru wakaingia vizani.
24-Imeelezea kisa cha mfalme Nimruwdh aliyehojiana na Nabiy Ibraahiym (عليه السّلام) kuhusu Rabb wake, akaangamizwa kwa kutakabari kwake kujifanya yeye ndiye mwenye uwezo wa kuhuisha na kufisha.
25-Imetajwa utoaji wa swadaqa kwa wingi na fadhila zake, na Allaah Akapiga mfano wa asiyetoa swadaqa na khasara zake. Na Waumini wameamrishwa kutoa vilivyo vizuri badala ya kutoa vilivyoharibika katika rizki za Allaah Alizomjaalia mtu. Na pia wamesifiwa wanaojizuia kuomba omba.
26-Imetaja uharamisho wa riba na ikatajwa Aayah ya mwisho kuteremshwa ambayo ni Aayah namba (281).
27-Imetajwa Aayah ndefu kabisa katika Qur-aan, nayo ni Aayah ya deni, Aayah namba (282).
28-Suwrah imekhitimishwa kwa kutajwa Aayah mbili ambazo zina fadhila adimu kama ilivyothibiti katika Hadiyth za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم).
Fadhila za Suwrah:
Hadiyth mbalimbali zimethibiti, miongoni mwazo ni:
1-Atakayesoma Usiku Aayah Mbili Za Mwisho Zinamtosheleza:
حَدَّثَنَا عُمَرُ بْنُ حَفْصٍ، حَدَّثَنَا أَبِي، حَدَّثَنَا الأَعْمَشُ، قَالَ حَدَّثَنِي إِبْرَاهِيمُ، عَنْ عَلْقَمَةَ، وَعَبْدِ الرَّحْمَنِ بْنِ يَزِيدَ، عَنْ أَبِي مَسْعُودٍ الأَنْصَارِيِّ، قَالَ قَالَ النَّبِيُّ صلى الله عليه وسلم " الآيَتَانِ مِنْ آخِرِ سُورَةِ الْبَقَرَةِ مَنْ قَرَأَ بِهِمَا فِي لَيْلَةٍ كَفَتَاهُ ".
Amesimulia Abuu Mas‘uwd Al-Answaariyy: Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Atakayesoma usiku Aayah mbili za mwisho wa Suwratul-Baqarah zitamtosheleza.” Yaani: zinamtosheleza kumkinga na kila baya na kila lenye kumdhuru. [Al-Bukhaariy na Muslim]
2-Shaytwaan Haingii Nyumba Inayosomwa Suwrah Al-Baqarah:
عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ، أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم قَالَ " لاَ تَجْعَلُوا بُيُوتَكُمْ مَقَابِرَ وَإِنَّ الْبَيْتَ الَّذِي تُقْرَأُ فِيهِ الْبَقَرَةُ لاَ يَدْخُلُهُ الشَّيْطَانُ " . قَالَ أَبُو عِيسَى هَذَا حَدِيثٌ حَسَنٌ صَحِيحٌ
Amesimulia Abuu Hurayrah (رضي الله عنه): Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Msifanye nyumba zenu makaburi. Kwa hakika shaytwaan haingii nyumba ambayo husomwa humo Suwratul-Baqarah.” [At-Tirmidhiy Hadiyth Hasan Swahiyh] Na katika Riwaayah ya Muslim, Hadiyth (780): “Shaytwaan anakimbia nyumba inayosomwa ndani yake Suwratul-Baqarah.”
عن سَهْل بن سعد قال: قال رسولُ الله صلى الله عليه وآله وسلم : إِنَّ لِكُلِّ شَيْءٍ سَنَامًا، وَإِنَّ سَنَامَ القُرْآنِ سُورَةُ الْبَقَرَةِ، مَنْ قَرَأَهَا فِي بَيْتِهِ لَيْلًا لَمْ يَدْخُلِ الشَّيْطَانُ بَيْتَهُ ثَلَاثَ لَيَالٍ، وَمَنْ قَرَأَهَا نَهَارًا لَمْ يَدْخُلِ الشَّيْطَانُ بَيْتَهُ ثَلَاثَةَ أَيَّامٍ
Amesimulia Sahl bin Sa’d (رضي الله عنه): Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Kila kitu kina kinara, na Al-Baqarah ndio kinara cha Qur-aan. Atakayesoma Al-Baqarah usiku nyumbani kwake, shaytwaan hatoingia ndani ya nyumba yake nyusiku tatu. Na atakayesoma mchana ndani ya nyumba yake, shaytwaan hatoingia ndani ya nyumba hiyo kwa siku tatu.” [Atw-Twabaraaniy (6/163), Ibn Hibbaan (2/78) na Ibn Mardawayh, Swahiyh At-Targhiyb (2/314)]
3-Suwrah Al-Baqarah Ni Taa Mbili Zitakazomuombea Mtu Siku Ya Qiyaamah, Na Kushikamana Nayo Ni Baraka, Kuicha Ni Majuto, Na Wachawi Hawaiwezi:
عن ابي أُمَامَةَ الْبَاهِلِيُّ قَالَ سَمِعْتُ رَسُولَ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم يَقُولُ " اقْرَءُوا الْقُرْآنَ فَإِنَّهُ يَأْتِي يَوْمَ الْقِيَامَةِ شَفِيعًا لأَصْحَابِهِ اقْرَءُوا الزَّهْرَاوَيْنِ الْبَقَرَةَ وَسُورَةَ آلِ عِمْرَانَ فَإِنَّهُمَا تَأْتِيَانِ يَوْمَ الْقِيَامَةِ كَأَنَّهُمَا غَمَامَتَانِ أَوْ كَأَنَّهُمَا غَيَايَتَانِ أَوْ كَأَنَّهُمَا فِرْقَانِ مِنْ طَيْرٍ صَوَافَّ تُحَاجَّانِ عَنْ أَصْحَابِهِمَا اقْرَءُوا سُورَةَ الْبَقَرَةِ فَإِنَّ أَخْذَهَا بَرَكَةٌ وَتَرْكَهَا حَسْرَةٌ وَلاَ تَسْتَطِيعُهَا الْبَطَلَةُ " . قَالَ مُعَاوِيَةُ بَلَغَنِي أَنَّ الْبَطَلَةَ السَّحَرَةُ .
Amesimulia Abuu Umaamah Al-Baahiliy (رضي الله عنه): Nimemsikia Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akisema: “Someni Qur-aan kwani itakuja Siku ya Qiyaamah ikiwa ni shafaa’ah (kiombezi) kwa watu wake wanaoisoma na kutekeleza (amri zake). Someni taa mbili: Al-Baqarah na Aal-‘Imraan kwani zitakuja Siku ya Qiyaamah kama kwamba ni maumbile ya mawingu, au sehemu mbili za mawingu, au makundi mawili ya ndege waliotandaza mbawa zao wakiruka. Zitawatetea watu wake (walioshikamana nazo) siku hiyo. Someni Suwratul-Baqarah, kwani kushikamana nayo ni baraka, na kuiacha kwake ni majuto, na wachawi hawawezi kuihifadhi kwa moyo.” [Muslim (804)]
Rejea pia Utangulizi wa Suwrah Aal-‘Imraan kupata fadhila nyenginezo zinazohusiana na Suwrah hii ya Al-Baqarah.
Faida:
Suwrah hii ni Suwrah ndefu kabisa kuliko Suwrah zote za Qur-aan. Ndani yake kuna hukmu za faradhi kadhaa kama Swalaah, Swiyaam za Ramadhwaan, Hajj, na hukmu nyenginezo ambazo Waislamu wanazihitaji katika maisha yao ya kijamii ya kila siku.
Pia zimetajwa maudhui mbalimbali, pamoja visa kadhaa, vikiwemo visa vyenye kudalilisha miujiza ya Allaah na Uwezo Wake wa kuhuisha na kufisha. Kisa kimojawapi ni kisa cha Al-Baqarah (Ng’ombe), ambacho ni kuhusu mtu aliyemuua mwenzie zama za Nabiy Muwsaa (عليه السّلام), ikawa hakujulikana nani aliyemuua mtu huyo. Basi Allaah (سبحانه وتعالى) Akawaamrisha wana wa Israaiyl wamchinje ng’ombe, kisha wampige maiti huyo kwa kipande cha sehemu ya ng’ombe. Kisha Allaah (سبحانه وتعالى) Akumhuisha mtu huyo, nae akawa hai na akataja mtu aliyemuua. Na hii ni ushahidi wa Uwezo wa Allaah (سبحانه وتعالى) kuwa ni Muweza wa kufufua wafu baada ya kufa kwao na Muweza wa kila kitu. Rejea Aayah (67-73).
Na katika kutofautisha na Suwrah nyenginezo, ni kuweko ndani yake Aayatul-Kursiyy ambayo ni Aayah Tukufu kabisa ya Qur-aan. Pia Aayah mbili za mwisho wa Suwrah, ambazo amepewa Nabiy Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم) pekee katika Manabii, alipokuwa mbingu ya saba katika Safari ya Al-Israa na Al-Mi’raaj.
003-Aal-Imraan: Utangulizi Wa Suwrah
Alhidaaya.com [2]
Imeteremka: Madiynah kwa itifaki ya ‘Ulamaa.
Idadi Za Aayah: 200
Jina La Suwrah:
Imeitwa Aal-‘Imraan (Familia Ya ‘Imraan), na yanayodalilisha ni kutajwa kwake katika Hadiyth zilizonukuliwa katika Fadhila za Suwrah, na pia kutajwa kwake katika Aayah namba (35).
Miongoni Mwa Makusudio Ya Suwrah:
1-Uthibitisho kwamba Dini ya Kiislamu ndio ya Dini ya haki. Radd (kujibu kwa kukanusha) kwa shubuhaat (tuhuma) za Watu wa Kitabu (Mayahudi na Naswara). Kuwathibitisha Waumini. [Al-Mukhtaswar Fiy Tafsiyr Al-Qur-aan Al-Kariym]
2-Kuthibitisha Tawhiyd ya Allaah (سبحانه وتعالى) ya kwamba Allaah ni Mmoja, na kusimamisha dalili na hoja juu ya hilo
3-Kubainisha ‘Al-Walaa na Al-Baraa (kupendana na kuchukiana kwa ajili ya Allaah), na tahadhari juu ya kumtawalisha asiye kuwa Muumini.
4-Kuchambua hali za Ahlul-Kitaab na baadhi ya itikadi zao na maasi yao.
5-Kuupa umuhimu upande wa malezi, na maelekezo kwa Waumini.
Miongoni Mwa Maudhui Ya Suwrah:
1-Suwrah imefunguliwa kwa herufi zinazojulikana kama الحروف المقطعة (Al-Huruwf Al-Muqatw-twa’ah), ambazo hakuna ajuaye maana zake isipokuwa Allaah (سبحانه وتعالى). Rejea Al-Baqarah (2:1). Kisha imethibitishwa kwamba Allaah ni Mmoja, na imeithibitishwa aina tatu za Tawhiyd: (i) Tawhiyd Al-Uluwhiyyah (Kumpwekesha Allaah katika ibaada). (ii) Tawhiyd Ar-Rubuwbiyyah (Kumpwekesha Allaah katika Uola Wake). (iii) Tawhiyd Asmaa Wasw-Swifaat (Kumpwekesha Allaah katika Majina Yake Mazuri Na Sifa Zake Kamilifu)
2-Imebainishwa watu walivyogawanyika kuhusu kuzifahamu Aayah zenye maana za wazi, na zisizokuwa wazi maana zake.
3-Wametahadharishwa makafiri wanaompinga Allaah na Rasuli Wake (صلى الله عليه وآله وسلم) kwamba: Ufalme, nguvu, vyeo, watoto, mali, havitawasaidia mbele ya Adhabu ya Allaah, na kwamba mwisho wao ni khasara ya wazi Duniani na Aakhiirah. Na Allaah Akawapigia mifano ya Makafiri waliotangulia na wataokuja baada yao, na jinsi utavyokuwa mwisho wao.
4-Kumetajwa kutokea kwa Vita vitukufu vya Badr na Uhud. Na katika vita vya Uhud, kuna maelezo ya matukio ya vita hivi na mafunzo waliyopata Waumini walipoenda kinyume na matakwa ya Rasuli wao (صلى الله عليه وآله وسلم) katika mbinu za kupigana kwenye vita hivyo vya Uhud ikasababisha kushindwa kwa Waislamu. Vita hivyo vilibainisha na kuwafichua wazi Waumini wakweli na wanafiki.
5-Vimetajwa vitu vinavyopendwa zaidi na nafsi ya mwanaadam, na kutanabahishwa kwamba hivyo vyote ni vitu vya starehe fupi ya kilimwengu na pambo lake lenye kutoweka. Lakini kwa Allaah (سبحانه وتعالى) kuna marejeo mazuri na thawabu adhimu ambazo Allaah Amewaandalia wenye taqwa, nayo ni Jannah yenye uhai wa starehe na neema za kudumu milele.
6-Imethibitishwa umuhimu wa Tawhiyd ya Allaah (سبحانه وتعالى) na ndani yake imetaja mara nne Kalimah ya Tawhiyd ya Allaah (سبحانه وتعالى):
لَا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ
Na imeeleza pia Amri ya Allaah kwa Rasuli Wake (صلى الله عليه وآله وسلم) awalinganie kwenye neno la sawasawa, ambalo ni neno la Tawhiyd.
7-Suwrah inaongoza katika hidaaya, kwani inawalingania watu wote kwenye Dini moja ya Uislamu na inawaambia kuhusu malipo watakayopewa watu wema na adhabu watakazopewa makafiri na kwamba Allaah (عزّ وجلّ) Haridhii dini yeyote ile isipokuwa Dini ya Kiislamu.
8-Suwrah imetaja kuhusu mke wa ‘Imraan, Bi Hannah na kumzaa kwake Maryam mama wa Nabiy ‘Iysaa (عليه السّلام). Imeelezewa kisha cha Nabiy Zakariyyaa (عليه السّلام) na kuzaliwa kwa Yahyaa. Pia kuzaliwa kwa ‘Iysaa (عليهم السّلام). Rejea Aayah (36).
9-Kuna uchambuzi wa hali za Ahlul-Kitaab (Watu wa Kitabu; Mayahudi na Manaswaara), na kuufedhehesha uovu na upotevu wao, ukiwemo kumpinga Nabiy ‘Iysaa (عليه السّلام) na yaliyowatokea ambayo ni kutofautiana katika Dini zao, na maovu waliyoyafanya, ya kuzikadhibisha Aayaat za Allaah, na kuwauwa Manabii Wake, na wale wanaolingania haki. Na pia kule kugoma kwao kuhukumiwa na Kitabu cha Allaah.
10-Suwrah inawajadili Watu wa Kitabu kwa dalili, ushahidi na hoja za waziwazi kabisa za kuthibitisha kuwa Dini ya Kiislamu ndio Dini ya haki iliyokuja kukhitimisha Dini za Manabii wote waliotangulia. Basi Suwrah inakanusha upinzani wao dhidi ya Tawhiyd ya Allaah na ukanushaji wao wa Dini ya mwisho ya Kiislamu.
11-Suwrah imeeleza majadiliano yao juu ya Nabiy Ibraahiym (عليه السّلام) na kuwabainishia haki kwenye jambo lake (Ibraahiym), na kutaja sifa zao nyingi ambazo walikuwa nazo (Ahlul-Kitaab), kama vile walivyokuwa wakitaka kuwapoteza Waislam, na kule kuzipinga kwao Aayaat za Allaah, na kule kuchanganya kwao haki na baatwil, na kuingiza maneno yao kwenye Kitabu chao, kwa lengo la kuwarubuni na kuwadanganya Waumini, na yasiyokuwa hayo.
12-Imebainishwa kuwa Ahlul-Kitaab wa awali waliomwamini Allaah na kumwamini Nabiy Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم) hawako sawa, na kwamba wako kati yao wanasoma Aayaat za Allaah (سبحانه وتعالى) usiku na mchana, na wanaamini Siku ya mwisho, wanaamrisha mema na kukataza mabaya.
13-Suwrah imetoa tanbihi juu ya ‘Aqiydah ya Al-Walaa Wal-Baraa (kupendana na kuchukiana kwa ajili ya Allaah), na kulisisitiza hilo, na tahadhari juu ya kuwapenda wasiokuwa Waumini.
14-Imebainishwa kuwa mapenzi ya Allaah yana alama na dalili zake, ikiwemo kumfuata Rasuli Wake (صلى الله عليه وآله وسلم) na kumpenda Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) na kumtii.
15-Imeeleza pia khabari za Manabii na kwamba daraja zao ni za juu, na kwamba Allaah (سبحانه وتعالى) Aliwachagua.
16-Imetajwa pia adabu nyingi za malezi, wasia wa kumcha Allaah (سبحانه وتعالى), kushikamana na Dini ya Allaah, kuacha kutengana na kukhtalifiana, na kuwaamrisha Waumini walinganie kheri, na kuwahimiza kutoa mali zao kwa njia ya Allaah.
17-Imetajwa baadhi ya Hukmu za Kisharia kama vile Jihaad, kuzuia watu kula riba, na adhabu za wanaozuia Zakaah.
18-Waumini wamefunzwa subra na wameshajiishwa kuhusu subra katika hali za neema na hali za misiba ya nafsi na mali na dhiki nyenginezo.
19-Imetajwa kuhusu Shuhadaa na fadhila zao. Hali kadhaalika imetajwa malipo watakayopata Waumini nayo ni Jannah na mapokezi mazuri humo kutoka kwa Rabb wao.
20-Imetajwa ukosefu wa adabu wa Mayahudi na dhulma yao kubwa iliyovuka mipaka kwa kumsingizia na kumpachika Allaah (سبحانه وتعالى) sifa ya ufakiri, ilhali Yeye Ni Al-Ghaniyy (Tajiri na Mkwasi Hahitaji lolote), na Allaah (سبحانه وتعالى) Akawaradd kwa hilo na kuwaadhidi adhabu waonje adhabu kali.
21-Wamesifiwa Waumini wenye kutafakari Uumbaji wa Allaah na wenye kumdhukuru Allaah (سبحانه وتعالى) kila nyakati na katika kila hali, na Kumpwekesha Allaah (سبحانه وتعالى) katika kumuomba duaa, na zikatajwa fadhila zao na malipo yao mazuri kabisa ya kuingizwa Jannah.
22-Suwrah imekhitimishwa kwa kuwataka Waumini wavute subira na ribaatw (wabakie imara) na wamche Allaah ili wapate kufaulu. Rejea katika faida ya Aayah ya mwisho kupata fadhila za ribaatw.
Fadhila za Suwrah:
1-Ni Taa Mbili Zitakazokuja Siku Ya Qiyaamah Kuwa Ni Shafaa’ah (Kiombezi) Kwa Wanaoisoma Na Kutekeleza Amri Zake:
عن أبي أُمامةَ الباهليِّ رضِي اللهُ عنه، قال: سمعتُ رسولَ اللهِ صلَّى اللهُ عليه وسلَّمَ يقول : اقْرَؤوا القُرْآنَ؛ فإنَّه يأتي يَومَ القيامةِ شفيعًا لأصحابه، اقرَؤوا الزَّهْرَاوَيْنِ: البقرةَ وسورةَ آلِ عِمْرانَ.
Amesimulia Abuu Umaamah Al-Baahiliy (رضي الله عنه): Nimemsikia Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akisema: “Someni Qur-aan kwani itakuja Siku ya Qiyaamah ikiwa ni shafaa’ah (kiombezi) kwa watu wake wanaoisoma na kutekeleza (amri zake). Someni taa mbili: Al-Baqarah na Aal-‘Imraan. [Muslim]
1-Itakuwa Kama Mawingu Mawili Na Itawatetea Wanaoisoma Na Kutekeleza Amri Zake:
Amesimulia An-Nawwaas bin Sam-‘aan (رضي الله عنه): Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Siku ya kufufuliwa, Qur-aan na watu waliokuwa wakiisoma na kutekeleza mafunzo yake, wataletwa mbele wakitangulizwa na Suwratul-Baqarah na Aal-‘Imraan.” Akasema An-Nawwaas: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akatoa mifano mitatu kwa Suwrah mbili hizi na sikusahau mifano hiyo tokea wakati huo. Alisema Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم): “Zitakuja kama mawingu mawili au vivuli viwili vyeusi kati yake kuna nuru, au makundi mawili ya ndege waliotandaza mbawa zao wakiruka, zitawatetea watu wake (wanaoshikamana nazo).” [Muslim]
Rejea pia Al-Baqarah kupata fadhila inayohusiana na Suwrah hii ya Aal-‘Imraan.
Faida:
Aal-‘Imraan ni baba yake Maryam mama wa Nabiy ‘Iysaa (عليه السّلام). Rejea Aayah (35-37). Mama yake ni ndugu wa Nabiy Zakariyyah (عليه السّلام): Familia ya ‘Imraan ni miongoni mwa familia Alizozifadhilisha Allaah (سبحانه وتعالى) juu ya walimwengu. Rejea Aayah namba (33-34). Na kisa chao kimetajwa kwenye Aayah namba (35-37).
Aayah za mwisho wa Suwrah hii [Aal-‘Imraan: (190-200]) ni Aayah ambazo ameteremshiwa Nabiy Allaah (سبحانه وتعالى) usiku mmoja zikamliza mno. Nazo ni Sunnah za kuzisoma pindi mtu anapoamka kwa ajili ya Tahajjud (kuamka usiku kuswali).
004-An-Nisaa: Utangulizi Wa Suwrah
Alhidaaya.com [2]
Imeteremka: Madiynah isipokuwa Aayah namba (58) imeteremka Makkah baada ya Fat-h (Ukombozi wa) Makkah.
Idadi Za Aayah: 176
Jina La Suwrah: An-Nisaa
Imeitwa An-Nisaa (Wanawake), na inayodalilisha ni kutajwa katika Hadiyth zilizonukuliwa katika Fadhila, na pia kutajwa katika Aayah namba (1), (4) na nyenginezo. Rejea maelezo katika Faida.
Miongoni Mwa Makusudio Ya Suwrah:
1-Kuifanya jamii ya Kiislamu kuwa na mipango, na kujenga mahusiano yake, kuhifadhi haki, kuwahimiza watu juu ya Jihaad, na kubatwilisha madai ya kuuwawa Masiyh ‘Iysaa mwana wa Maryam. [Al-Mukhtaswar Fiy Tafsiyr Al-Qur-aan Al-Kariym]
2-Kuhifadhi haki za waliodhaifu katika jamii nao ni wanawake na yatima.
3-Kubainisha haki za warithi kwa kuwekwa nidhamu za mirathi kuhusu ugawaji wa mali zilizoachwa na aliyefariki.
4-Kuipa umuhimu Aqiydah na Tawhiyd Yake Allaah (سبحانه وتعالى), na kuzungumzia kadhia za imaan, na pia kuzipinga Aqiydah baatwil (potofu).
5-Kuwekwa wazi hoja za kuonyesha usahihi wa Unabiy wa Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم).
6-Kuweka hukmu za uadilifu katika kuhukumu baina ya watu, na kutimiza amana za watu.
7-Kutahadharishwa na wanafiki, na kutajwa baadhi ya sifa zao.
8-Kuongoza katika mambo ya familia, na kupangilia mahusiano kati ya wanandoa wawili, na kutatua matitzo kati yao.
9-Kuitilia umuhimu misingi ya kujenga Dola ya Kiislam, na vinavyoifanya dola kuwa imara na kupigana Jihaad katika Njia ya Allaah.
10-Kuipa umuhimu jambo la kuhifadhi damu za Waislamu na hukmu zake.
11-Kupinga ushirikina wa Manaswara wanaodai kuwa Nabiy ‘Iysaa (عليه السّلام) ni mwabudiwa au mwana wa Allaah.
Miongoni Mwa Maudhui Ya Suwrah:
1-Suwrah imefunguliwa kwa amri ya kumcha Allaah (سبحانه وتعالى), na kubainishwa kwamba wanaadam wote wanatokana na baba mmoja ambaye ni Aadam (عليه السّلام) na mama mmoja Hawaa. Na pia amri ya kuunga undugu wa uhusiano wa damu.
2-Imeelezwa hukmu na haki za wanawake kama mahari, na imeelezea haki za watoto yatima na jinsi ya kuzitunza mali zao.
3-Imebainishwa Sharia ya Allaah (سبحانه وتعالى) ya mirathi katika ugawaji wa mali aliyoacha aliyefariki kwa familia yake wakiwemo na wazazi.
4-Imebainishwa mambo mengi yanayohusu mahusiano ya mwanamke na mwanamume katika ndoa, miongoni mwa hayo ni: (i) Swala la usimamizi (ii) Uhalali wa kuoana (iii) Hukmu ya ruhusa kwa mwanamume kuoa zaidi ya mke mmoja hadi wake wanne, na pindi asipoweza kutimiza haki basi abakie na mmoja tu. (iv) Haki ya mwanamke katika heshima ya kibinaadam (v) mahari (vi) Uharamu wa kumtelekeza mwanamke (vii) Hukmu za kunyonyesha (viii) Maamrisho ya mema na kukemea mambo machafu (ix) Uhalali wa mahusiano na Watumwa wa kike na mengineyo.
5-Aayah namba (36) imekusanya haki kumi nazo ni: (i) Kumwabudu Allaah na kutokumshirikisha na chochote (ii) Kuwafanyia wazazi wawili ihsaan (iii) Haki za arhaam (jamaa wa uhusiano wa damu) (iv) Haki za yatima (v) Haki za masaakini (vi) Haki za jirani wenye uhusiano wa damu (vii) Haki za jirani wasiokuwa na uhusiano wa damu (viii) Haki za swahibu au rafiki (ix) Haki za msafiri aliyeishiwa masurufu (x) Haki za iliyowamiliki mikono ya kulia.
6-Kwenye mambo yanayohusu mali, Suwrah imezungumzia uharamu wa kula mali za watu kwa dhulma, na kuwatahadharisha watu na mambo hayo, na pia kuwahimiza watu watoe katika njia ya Allaah, na Ahadi ya Allaah (سبحانه وتعالى) kutoa adhabu kwa wanaofanya ubakhili au kuwaamrisha watu kufanya ubakhili.
7-Suwrah imebainisha hukmu nyingi za kisharia pamoja na kuweka wazi uwepesi wa Sharia, na kwamba Allaah (سبحانه وتعالى) Amewafanyia takhfifu (wepesi) Waja Wake, kwa kuchunga udhaifu wao, miongoni mwa hukmu hizo ni: (i) Hukmu za Mirathi (ii) Uharamu wa mlevi akiwa amelewa (iii) Wajibu wa kuoga Janaba kwa anayetaka kuswali (iv) Taratibu za Kutayammam na hukmu zake. (v) Mambo ya jinai kama kuua mtu na fidya pamoja na kubainisha heshima (uzito) ya damu ya Muumini, na malipo kwa ataemuua Muumini kwa makusudi. Na mengineyo.
8-Imebainishwa hukmu katika dola ya Kiislamu, ambao ni uadilifu, utii kwa Allaah na Rasuli Wake (صلى الله عليه وآله وسلم) na waliokuwa na mamlaka, na iwe marejeo ya waja inapotokea mizozo; ni Sharia za Allaah kwa kuridhia.
9-Kuna maelezo kuhusu wanafiki na fedheha zao, na kubainisha sifa zao na matendo yao mengi, na nafasi yao ya adhabu kesho Aakhirah, na kwamba wao watakuwa daraja ya chini kabisa motoni.
10-Miongoni mwa maudhui nyenginezo ni: (i) Amri ya kuwa watu wapigane katika njia ya Allaah kwa lengo la kutangaza Kalimah Tukufu ya Allaah, na imetaja fadhila zake kubwa kwa walioenda Jihaad kulinganisha na wasioenda, na inaweka wazi malipo makubwa ya kwenda katika Jihaad (ii) Kuwanusuru wanyonge katika Waumini (iii) Imebainisha baadhi ya hukmu zinazohitajika kuzifahamu kwa anaekwenda Jihaad ikiwemo: Muamala wake pamoja na wale wanaokuja kuomba amani, na hukmu ya Swalaatul-Khawf (Swalaah ya kuhofu katika vita) na kupunguza Swalaah wakiwa vitani.
11-Suwrah imehimiza watu kutenda mema, na kujipamba na tabia njema,
12-Suwrah imezungumzia pia kadhia ya watu kuhukumiana katika Uislamu kwa uadilifu bila ya kupendelea jamaa au tajiri, kutoa ushahidi kwa ajili ya Allaah, kama ulivyo, hata kama madhara yatarudi kwenye nafsi, au kwa wazazi, au kwa ndugu wa karibu, na wala wasifate matamanio ikawa sababu ya kuingia kwenye dhulma (iii) Kutekeleza amana (iv) Mahimizo juu ya Kuwafanyia wema viumbe, na kuchunga haki za wazazi, jirani na ndugu (v) Kuchunga hali za watu wenye mahitaji.
13-Kubainisha uadui wa asili kati ya shaytwaan na mwanaadamu, na jinsi shaytwaan alivyoahidi kuwapoteza baadhi ya waja.
14-Suwrah imehimiza (i) Kumuamini Allaah na Rusuli Wake, na Vitabu Vyake, na kuamini Siku ya Mwisho (ii) Kutekeleza ibaada kwa ajili ya Allaah Pekee na kubainisha uhatari wa ushirikina (iii) Kukataza kuwafanya makafiri kuwa marafiki badala ya Waumini (iv) Amri ya kuwa na taqwa na kushikamana na Dini Yake tukufu.
15-Suwrah imetaja sehemu fulani ya khabari za Manabii wa Allaah (سبحانه وتعالى) .
16-Suwrah imeelezea pia kuhusu Watu wa Kitabu na kubainisha baadhi ya upotevu wao, na adhabu na laana zilizowapata. Pia imetaja baadhi ya tabia yao ya kuvunja ahadi, na kuzikufuru (kuzipinga) Aayah za Allaah. Pia imeelezea miamala yao mibaya na Manabii wa Allaah, ambayo ilipelekea kuwauwa baadhi yao (Manabii), na wengine kuwazidishia sifa, kama walivyofanya kwa Nabiy ‘Iysaa bin Maryam (عليه السلام), na kauli yao ya Utatu.
17-Suwrah imekhitimshwa kwa kubainishwa hukmu ya al-kalaalah (Mirathi ya mtu asiyekuwa na wazazi wala watoto). Rejea Faida:
Fadhila Za Suwrah:
1-Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) Alilia Pindi Ibn Mas’uwd (رضي الله عنه) Alipomsomea Aayah Namba (41):
عَنْ عَبْدِ اللَّهِ قَالَ قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم " اقْرَأْ عَلَىَّ ". قَالَ قُلْتُ أَقْرَأُ عَلَيْكَ وَعَلَيْكَ أُنْزِلَ قَالَ " إِنِّي أَشْتَهِي أَنْ أَسْمَعَهُ مِنْ غَيْرِي ". قَالَ فَقَرَأْتُ النِّسَاءَ حَتَّى إِذَا بَلَغْتُ فَكَيْفَ إِذَا جِئْنَا مِنْ كُلِّ أُمَّةٍ بِشَهِيدٍ وَجِئْنَا بِكَ عَلَى هَؤُلاَءِ شَهِيدًا . قَالَ لِي " كُفَّ ـ أَوْ أَمْسِكْ ـ ". فَرَأَيْتُ عَيْنَيْهِ تَذْرِفَانِ.
Amesimulia ‘Abdullaah bin Mas‘uwd (رضي الله عنه): Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) aliniambia: “Nisomee!” Nikamwambia: Ee Rasuli wa Allaah! Nikusomee na hali (Qur-aan) imeteremshwa kwako? Akasema: “Naam! Lakini mimi napenda kusikia wengine wakiisoma.” Nikasoma Suwratun-Nisaa mpaka nilipofikia Aayah:
فَكَيْفَ إِذَا جِئْنَا مِن كُلِّ أُمَّةٍ بِشَهِيدٍ وَجِئْنَا بِكَ عَلَىٰ هَـٰؤُلَاءِ شَهِيدًا ﴿٤١﴾
“Basi itakuwaje Tutakapoleta kutoka kila ummah shahidi, na Tukakuleta (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) kuwa shahidi juu ya hawa?”
Akasema: “Inatosha, simama hapo.” Nikaona macho yake yanamiminika machozi. [Al-Bukhaariy, Muslim na wengineo]
2-Zimo Aayah Tano Zinazofurahisha Kuliko Dunia Na Yaliyomo Ndani Yake:
عن عبدِ اللهِ بن مَسعودٍ رضِي اللهُ عنه، قال: إنَّ في النِّساء لخمسَ آياتٍ، ما يسرُّني بهنَّ الدُّنيا وما فيها، وقد علِمتُ أنَّ العلماء إذا مرُّوا بها يعرفونها: إِنْ تَجْتَنِبُوا كَبَائِرَ مَا تُنْهَوْنَ عَنْهُ نُكَفِّرْ عَنْكُمْ سَيِّئَاتِكُمْ وَنُدْخِلْكُمْ مُدْخَلًا كَرِيمًا ، وقوله تعالى: إِنَّ اللَّهَ لَا يَظْلِمُ مِثْقَالَ ذَرَّةٍ وَإِنْ تَكُ حَسَنَةً يُضَاعِفْهَا وَيُؤْتِ مِنْ لَدُنْهُ أَجْرًا عَظِيمًا، وقوله تعالى: إِنَّ اللَّهَ لَا يَغْفِرُ أَنْ يُشْرَكَ بِهِ وَيَغْفِرُ مَا دُونَ ذَلِكَ لِمَنْ يَشَاءُ ، وقوله تعالى وَلَوْ أَنَّهُمْ إِذْ ظَلَمُوا أَنْفُسَهُمْ جَاؤُوكَ فَاسْتَغْفَرُوا اللَّهَ وَاسْتَغْفَرَ لَهُمُ الرَّسُولُ لَوَجَدُوا اللَّهَ تَوَّابًا رَحِيمًا ، وقوله تعالى: وَمَنْ يَعْمَلْ سُوءًا أَوْ يَظْلِمْ نَفْسَهُ ثُمَّ يَسْتَغْفِرِ اللَّهَ يَجِدِ اللَّهَ غَفُورًا رَحِيمًا
Amesimulia ‘Abdullaah Bin Mas’uwd (رضي الله عنه): Hakika katika An-Nisaa, kuna Aayah tano ambazo ni bora kwangu kulikoni dunia na yaliyomo ndani yake, na najua kwamba ‘Ulamaa wanapozipitia huzitambua. Nazo ni:
إِن تَجْتَنِبُوا كَبَائِرَ مَا تُنْهَوْنَ عَنْهُ نُكَفِّرْ عَنكُمْ سَيِّئَاتِكُمْ وَنُدْخِلْكُم مُّدْخَلًا كَرِيمًا ﴿٣١﴾
“Mkijiepusha na madhambi makubwa mnayokatazwa Tutakufutieni madhambi yenu madogo na Tutakuingizeni katika mahali patukufu.” [An-Nisaa (4:31)]
إِنَّ اللَّـهَ لَا يَظْلِمُ مِثْقَالَ ذَرَّةٍ ۖ وَإِن تَكُ حَسَنَةً يُضَاعِفْهَا وَيُؤْتِ مِن لَّدُنْهُ أَجْرًا عَظِيمًا ﴿٤٠﴾
“Hakika Allaah Hadhulumu hata uzito au chembe (kama atomu). Na ikiwa ni amali njema Huizidisha na Hutoa kutoka Kwake ujira mkuu kabisa.” [An-Nisaa (4:40)]
إِنَّ اللَّـهَ لَا يَغْفِرُ أَن يُشْرَكَ بِهِ وَيَغْفِرُ مَا دُونَ ذَٰلِكَ لِمَن يَشَاءُ ۚ وَمَن يُشْرِكْ بِاللَّـهِ فَقَدِ افْتَرَىٰ إِثْمًا عَظِيمًا ﴿٤٨﴾
“Hakika Allaah Haghufurii kushirikishwa, lakini Anaghufuria yasiyokuwa hayo kwa Amtakae. Na yeyote atakayemshirikisha Allaah basi kwa yakini amezua dhambi kuu kabisa.” [An-Nisaa (4:48)]
وَمَا أَرْسَلْنَا مِن رَّسُولٍ إِلَّا لِيُطَاعَ بِإِذْنِ اللَّـهِ ۚ وَلَوْ أَنَّهُمْ إِذ ظَّلَمُوا أَنفُسَهُمْ جَاءُوكَ فَاسْتَغْفَرُوا اللَّـهَ وَاسْتَغْفَرَ لَهُمُ الرَّسُولُ لَوَجَدُوا اللَّـهَ تَوَّابًا رَّحِيمًا﴿٦٤﴾
“Na Hatukutuma Rasuli yeyote ila atiiwe kwa Idhini ya Allaah. Na lau wao pale walipojidhulumu nafsi zao wangelikujia (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) wakamwomba Allaah maghfirah na Rasuli akawaombea maghfirah, basi wangelimkuta Allaah Ni Mwingi wa Kupokea Tawbah, Mwenye Kurehemu.” [An-Nisaa (4:64)]
وَمَن يَعْمَلْ سُوءًا أَوْ يَظْلِمْ نَفْسَهُ ثُمَّ يَسْتَغْفِرِ اللَّـهَ يَجِدِ اللَّـهَ غَفُورًا رَّحِيمًا ﴿١١٠﴾
“Na atakayetenda ovu au akajidhulumu nafsi yake, kisha akamwomba Allaah maghfirah, basi atamkuta Allaah Ni Mwingi wa Kughufuria, Mwenye Kurehemu.” [An-Nisaa (4:110)]
[Imepokewa na Sa’iyd bin Manswuur katika Sunan (4/1297), Atw-Twabaraaniy (9/250), (9069), na Al-Haakim (3194). Al-Haythamiy amesema katika Majma’ Az-Zawaaid (7/14): Watu wake ni watu wa Sahih]
3-Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) Aliisoma Katika Qiyaamul-Layl:
عن حُذيفةَ بن اليمانِ، قال: صلَّيتُ مع النبيِّ صلَّى اللهُ عليه وسلَّمَ ذاتَ ليلةٍ، فافتتَحَ البقرةَ، فقلتُ: يركع عند المئةِ، ثم مضى، فقلتُ: يصلي بها في ركعةٍ، فمضى، فقلتُ: يركع بها، ثم افتتح النساءَ فقرأها، ثم افتتح آلَ عمرانَ فقرأها، يقرأ مُترسِّلًا .
Amesimulia Hudhayfah Bin Al-Yamaani (رضي الله عنه) asemaye: “Niliswali na Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) usiku mmoja, akafungua kwa Al-Baqarah nikadhani atarukuu katika Aayah mia (100) za mwanzo, naye akapitiliza. Nikadhani ataimaliza Suwrah yote katika rakaa moja, naye akapitiliza. Nikadhani atarukuu kabla hajaimaliza, kisha akaianza An-Nisaa akaisoma, kisha akaingia Aal-‘Imraan, akaisoma, naye akaisoma kwa utuvu na kwa kituo.” [Hadiyth Swahiyh. Imefanyiwa “ikhraaj” na Muslim (772), An Nasaaiy (1664) na Abu Daawuud (874)]
Faida:
1-Suwrah Kuitwa An-Nisaa:
Sababu nyenginezo za Suwrah kuitwa An-Nisaa (Wanawake), ni kutokana hukmu nyingi zinazohusu wanawake, wakiwemo wake na mabinti. Na imeitwa An-Nisaa kwa sababu zama za Jaahiliyyah (kabla ya Uislamu), wanawake walidhulumiwa mno kwa kunyimwa haki zao. Mfano haki za wake na haki za mirathi. Na kuonewa huko kulikuwa hadi kwamba mume akifariki, basi mke anarithiwa kama zinavyorithiwa mali, kisha huyo anayemrithi humfanya mwanamke huyo atakavyo kama ilivyotajwa katika Asbaab-Nuzuwl (Sababu Za Kuteremshwa) Aayah namba (19). Hivyo basi walidharauliwa mno na wakakosa hadhi katika jamii. Na dhulma zao zilipindukia mipaka hadi kwamba ilikuwa, pindi anapozaliwa mtoto wa kike, huuliwa kwa kuzikwa mzima mzima. Rejea An-Nahl (16:58-59), At-Takwiyr (81:8-9).
Pia imeitwa An-Nisaa (Wanawake) kwa sababu ya kukariri neno la An-Nisaa, ambalo limetajwa kwa umoja na likiwa limeegemezwa kwenye neno lingine, na kwa jambo linalotambulika kuwa kitu chochote kikitajwa sana hiyo inajulisha umuhimu wa hicho kitu. [Tafsiyr Ibn Uthaymiyn – Suwrah An-Nisaa (1/8), Al-Itqaan fiy ‘Uluwmil-Qur-aan cha Imam Swuyutwiy (1/197-198).
Miongoni mwa Aayah zilizotajwa An-Nisaa ni Aayah (3-4), (19), (22), (24), (32), (34) na nyenginezo.
2-Kuhusu Al-Kalaalah (Mirathi ya mtu asiyekuwa na wazazi wala watoto):
عَنْ مَعْدَانَ بْنِ، أَبِي طَلْحَةَ أَنَّ عُمَرَ بْنَ الْخَطَّابِ، خَطَبَ يَوْمَ جُمُعَةٍ فَذَكَرَ نَبِيَّ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم وَذَكَرَ أَبَا بَكْرٍ ثُمَّ قَالَ إِنِّي لاَ أَدَعُ بَعْدِي شَيْئًا أَهَمَّ عِنْدِي مِنَ الْكَلاَلَةِ مَا رَاجَعْتُ رَسُولَ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم فِي شَىْءٍ مَا رَاجَعْتُهُ فِي الْكَلاَلَةِ وَمَا أَغْلَظَ لِي فِي شَىْءٍ مَا أَغْلَظَ لِي فِيهِ حَتَّى طَعَنَ بِإِصْبَعِهِ فِي صَدْرِي وَقَالَ " يَا عُمَرُ أَلاَ تَكْفِيكَ آيَةُ الصَّيْفِ الَّتِي فِي آخِرِ سُورَةِ النِّسَاءِ " . وَإِنِّي إِنْ أَعِشْ أَقْضِ فِيهَا بِقَضِيَّةٍ يَقْضِي بِهَا مَنْ يَقْرَأُ الْقُرْآنَ وَمَنْ لاَ يَقْرَأُ الْقُرْآنَ .
Imesimuliwa Ma’daan Bin Abiy Twalhah Al-Ya’muriyy, amesema: ‘Umar Bin Al-Khattwaab (رضي الله عنه) alikhutubia Siku ya Ijumaa, akamtaja Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) na akamtaja Abu Bakr, kisha akasema: Hakika sitoacha chochote kilicho muhimu zaidi kama jambo la al-kalaalah, na hakuna jambo nililolirejea rejea zaidi kwa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) kama nilivyolirejea jambo la al-kalaalah, na hakuwahi kunisisitiza kwenye jambo lolote kama alivyonisisitiza kwenye al-kalaalah, mpaka alininipiga kifuani kwa vidole vyake, na akasema: “Ee ‘Umar! Hivi haikutoshi wewe Aayah (176) iliyoteremka katika Swawyf (majira ya joto) ambayo iko mwishoni mwa Suwrah An-Nisaa?” ‘Umar akasema: Hakika kama nitaishi, nitatoa hukmu ya kuhusu al-kalaalah, kiasi kwamba kila mtu atakayesoma au asiyesoma Qur-aan ataweza kuihukumu. [Muslim (1617)]
005-Al-Maaidah: Utangulizi Wa Suwrah
Alhidaaya.com [2]
Imeteremka: Madiynah kwa itifaki ya ‘Ulamaa.
Idadi Za Aayah: 120
Jina La Suwrah: Al-Maaidah
Suwrah imeitwa Al-Maaidah (Meza Ya Chakula), na inayodalilisha ni kutajwa katika Hadiyth zilizonukuliwa katika Fadhila, na pia kutajwa katika Aayah namba (112).
Miongoni Mwa Makusudio Ya Suwrah:
1-Amri ya kutaka watu kutekeleza ahadi, na tahadhari ya watu kujifananisha na Ahlul-Kitaab juu ya kutotekeleza ahadi. [Al-Mukhtaswar Fiy Tafsiyr Al-Qur-aan Al-Kariym]
2-Msisitizo juu ya kuhifadhi ahadi na kuzitekeleza.
3-Kubainishwa sharia nyingi.
4-Kuweka mpangilio wa mahusiano juu ya Waislamu wao kwa wao, na juu ya Waislamu na wasiokuwa Waislamu.
Miongoni Mwa Maudhui Ya Suwrah:
1-Suwrah imefunguliwa kwa Maamrisho ya Allaah (سبحانه وتعالى) kwa Waumini, ya kutimizia ahadi zilizotiliwa mkazo, za kuamini sharia za Dini na kuzifuata, na kutekeleza ahadi wanazopeana Waumini katika biashara na mengineyo. Na uharamisho wa kuwinda katika hali ya Ihraam. Pia maamrisho ya kutokuvuka mipaka ya Allaah na alama Alizoziwekea hiyo mipaka Yake. Na mengineyo yanayohusiana na manaasik ya Hajj. Na ikabainishwa uhalali wa kula nyama za wanyama wa mifugo ambao ni ngamia, ng’ombe, mbuzi na kondoo, isipokuwa wale ambao Allaah (سبحانه وتعالى) Amewaelezea kuwaharamishia, ambao ni mfu, damu, nyama ya nguruwe na wengineo kutokana na sababu kadhaa zilizotjawa katika Aayah namba (3).
2-Kisha ikafuatilia amri ya kutowaogopa makafiri, bali Waumini wamwogope Allaah na kwamba Yeye Allaah (سبحانه وتعالى) Ameshawakamilishia Dini Tukufu ya Uislamu, na kuwatimizia Neema Zake kwa Waumini kwa kuwatoa kwenye giza la ujahili na kuwapeleka kwenye nuru ya imaan, na kwamba Amewaridhia kwamba Uislamu ndio Dini, basi Waumini washikamane nayo imara wala wasiiache.
3-Waumini wamebainishiwa kula vilivyo vizuri, na kutaja Jina la Allaah (سبحانه وتعالى) katika kuchinja mnyama. Na uhalali wa kula vyakula vya Ahlul-Kitaab na uhalali wa kuwaoa wanawake wao, na uharamisho wa uzinifu.
4-Imebainishwa hukmu ya kutia wudhuu na hukmu ya tayammum katika hali kadhaa kama janaba, ugonjwa, safari na katika kumaliza haja msalani, na kwamba hayo ni kutokana na Neema Zake Allaah (سبحانه وتعالى) kutaka kuwatwaharisha Waumini ili wapate kumshukuru.
5-Waumini wameamrishwa wawe wasimamizi wa haki kwa ajili ya kuzitafuta Radhi za Allaah. Wawe mashahidi kwa uadilifu, wala kusiwapelekee kuwachukia watu kuacha kufanya uadilifu, na kwamba wafanye uadilifu hata baina ya maadui na vipenzi kwa daraja moja sawasawa. Na tahadhari ya kudhulumu.
6-Imethibitishwa kwamba Hukmu sahihi ni ya Allaah (سبحانه وتعالى) Pekee, na hakuna hukmu nzuri kuliko hukmu ya Allaah, pamoja na kubainisha kuwa kuhukumiwa na hukmu ya Allaah ni wajibu, na kuziacha hukumu zisizokuwa Zake.
7-Kuweka msisitizo juu ya ‘Aqiydah ya Al-Walaa wa Al-Baraa (Kupendana na kuchukiana kwa ajili ya Allaah), na kutilia mkazo juu ya kuwapenda Waumini, pamoja na kutahadharisha juu ya kuwapenda makafiri.
8-Kupangilia mahusiano ya Waislamu wao kwa wao, na Waislam na Mayahudi na Manaswara.
9-Suwrah imebainisha hukumu nyingi za kisharia na kuziweka wazi. Miongoni mwa hizo ni: Hukmu zinazoelezea mambo ya ibaada na miamala, mikataba, kuchinja, kuwinda, kuhirimia Hajj, ndoa ya Ahlul-Kitaab, hukumu ya kuua na kufanya ufisadi katika ardhi, hukmu ya mwizi, hukmu ya mtu ambaye anakaribia kufariki, kuwashuhudisha Waumini waaminifu wawili kuandika wasia wake. Na hukmu nyenginezo.
10-Suwrah imekusanya baadhi ya visa kikiwemo (i) Kisa cha Baniy Israaiyl na Nabiy Muwsaa (عليه السلام) kuwataka watu wake waingie ardhi tukufu iliyotakaswa ambayo ni Bayt Al-Maqdis, na ukaidi wa wao wa kutokumtii Rasuli wao kuingia mji huo, isipokuwa watu wawili waliomkhofu Allaah. Ikatajwa adhabu za hao walioasi amri ya Rasuli wao. (ii) Kisa cha watoto wawili wa Nabiy Aadam; mmoja wao aliyemuua mwenzake, kisha alipokuwa hakujua la kumfanya, Allaah (سبحانه وتعالى) Akamteremshia kunguru, akawa anafukua shimo katika ardhi ili amzike kunguru mwenzake, ikawa ni fundisho la mwana wa Aadam kutambua kumsitiri na kumzika nduguye aliyemuua. (iii) Kisa cha Wahabashi waliomiminikwa na machozi baada ya kusikia Aayah za Allaah (سبحانه وتعالى), na wakayakinika kwamba Kauli hizo ni haki zilizoteremshwa kutoka kwa Allaah. (iv) Kisa cha Maidah (Meza ya Chakula kutoka mbinguni).
11-Onyo na makemeo kwa mwenye kuritadi. Pia wamekemewa Wanazuoni wa Ahlul-Kitaab kutokuwakataza watu wao wanaotenda madhambi.
12-Wamelaaniwa Mayahudi waliompachika sifa mbaya Allaah (سبحانه وتعالى) kwamba Mkono wa Allaah Umefungwa, na hivyo wamemaanisha kuwa Allaah (سبحانه وتعالى) Amewafanyia ubakihili kwa kuwabania na kutokuwapanulia rizki. Walisema hilo wakati walipopatwa na ukame na ukosefu wa mvua. Allaah (سبحانه وتعالى) Akawaahidi kufarikiana wao kwa wao na kuchukiana mpaka Siku ya Qiyaamah.
13-Kubainisha hali za Ahlul-Kitaab na ile sifa yao ya kuvunja ahadi pamoja na kuvibadilisha Vitabu vya Allaah (سبحانه وتعالى) vilivyoteremshwa, na kujadili baadhi ya itikadi zao potovu, ambazo ni: Kusema kuwa Allaah Ana mwana, na kupinga Unabii wa Muhammad.
14-Allaah (سبحانه وتعالى) Amemthibitisha Rasuli Wake (صلى الله عليه وآله وسلم) kutokana na wanaomkanusha Unabii wake, na kumuamrisha anedelea kubalighisha Risala ya Allaah wala asirudi nyuma.
15-Imebainishwa kufru za Manaswara kumsingizia Allaah (سبحانه وتعالى) kwamba Nabiy Iysaa (عليه السّلام) ni mwanawe, na itikadi yao ya utatu. Allaah (سبحانه وتعالى) Akawabainisha hoja za wazi kabisa kwamba Nabiy Iysaa (عليه السّلام) na mama yake ni waja Wake Aliowaumba ambao wanakula na kunywa. Akawataka watubie Kwake ili Awaghufurie kwani Yeye ni Mwingi wa Kughufuria Mwenye Kurehemu.
16-Wamelaaniwa waliokufuru katika Bani Israaiyl kwa maasi yao na kufanya uadui na kufanya ufisadi na udhalimu. Na pia kuridhia kwao kwa maasi na kutokukataza kwao maovu yoyote yaliyokuwa yakitendwa.
17-Imebainishwa hukmu ya kafara ya kiapo na tahadharisho la kuapa ovyo ovyo.
18-Uharamisho wa pombe, kamari, masanamu, kupiga ramli, na imebainishwa hukmu ya mwisho ya ulevi ambayo ni kukoma jambo hilo, na tahadhari ya shaytwaan na uadui wake kwa mwanaadam na uchochezi wake wa kumuingiza katika maasi hayo.
19-Imebainishwa itikadi potofu ya washirikina waliyoyazua ya kuacha kunufaika na baadhi ya wanyama wa mifugo na kuwafanya ni wa masanamu. Na ukaidi wao wa kushikilia kufuata ujahili wa baba zao
20-Imetajwa neema za Allaah (سبحانه وتعالى) juu ya Nabiy ‘Iysaa (عليه السّلام) Alizomjaalia kumuumba bila ya baba tokea utoto wake, na uwezo aliojaaliwa wa kufanya miujiza kadhaa, na kumfundisha kuandika na kusoma, kumfundisha Tawraat na Injiyl na kadhaalika.
21-Suwrah imekhitimishwa kwa kutajwa kisa cha wafuasi wa Nabiy ‘Iysaa (عليه السّلام) kutaka wateremshiwe Al-Maaidah (Meza ya Chakula) kutoka mbinguni wayakinike na iwe ushahidi wao wa ukweli wa Nabiy wa. Nabiy ‘Iysaa (عليه السّلام) aliwaombea kwa Allaah (سبحانه وتعالى) ombi lao hilo na walitimiziwa, wakateremshiwa Al-Maaidah kutoka mbinguni. Kisha Allaah (سبحانه وتعالى) Akatawatahadharisha kuwaadhibu pindi wakikanusha Tawhiyd Yake. Kisha Allaah (سبحانه وتعالى) Akathibitisha malipo mema ya maisha ya kudumu katika Jannah kwa waliompwekesha na waliokuwa wakweli katika niya zao, kwa maneno na matendo yao, na kuwaridhia na kuwajaalia mafanikio makubwa.
Fadhila Za Suwrah:
Ni Suwrah ya mwisho kuteremshwa ila wamekhitilafiana Salaf kuhusu hili. Baadhi ya riwaaya zinasema kuwa ni Suwrah ya mwisho kuteremshwa kama Hadiyth ifuatayo:
عَنْ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ عَمْرٍو، قَالَ آخِرُ سُورَةٍ أُنْزِلَتْ سُورَةُ الْمَائِدَةِ . قَالَ أَبُو عِيسَى هَذَا حَدِيثٌ حَسَنٌ غَرِيبٌ
Amesimulia ‘Abdullaah bin ‘Amrw: Suwrah ya mwisho kuteremshwa ni Al-Maaidah. [At-Tirmidhiy na amesema: Hii ni Hadiyth Hasan Ghariyb]
Riwaaya nyenginezo zimetajwa ni Suwrah An-Naswr kama walivyopokea Imaam Al-Bukhaariy na Muslim. Na riwaaya nyenginezo zimetajwa At-Tawbah. Na Allaah Mjuzi zaidi.
Faida:
Suwrah imeitwa Al-Maaidah (Meza Ya Chakula) kwa kutajwa wafuasi wa Nabiy ‘Iysaa (عليه السّلام) walipomtaka awape dalili itayojulisha ukweli wa Unabii wake, na iwe kama sikukuu kwao, basi wakataka Allaah (سبحانه وتعالى) Ateremshe meza ya chakula kutoka mbinguni. Na hakika Allaah (سبحانه وتعالى) Aliteremsha meza ya chakula kama walivyotaka. Rejea Aayah (112-115).
006-Al-An’aam: Utangulizi Wa Suwrah
Alhidaaya.com [2]
Imeteremka: Makkah kwa itifaki ya ‘Ulamaa.
Idadi Za Aayah: 165
Jina La Suwrah: Al-An’aam.
Suwrah imeitwa Al-An’aam (Wanyama), na inayodalilisha ni kutajwa katika Hadiyth zilizonukuliwa chini katika Fadhila na Faida. Na pia imeitwa Al-An’aam (Wanyama) kutokana na kutajwa wanyama wa aina mbalimbali ambao washirikina waliwatumia kwa shirki na kufru zao na wakawa wanapotaka kuwala hawataji jina la Allaah.
Na amesema Al-Swuyuutwiy: Imeitwa Suwrah Al-An’aam kwa sababu ya ufafanuzi wa hali za wanyama, japo neno Al-An’aam limekuja kwenye Suwrah isiyokuwa hii, lakini ufafanuzi uliokuja katika Aayah (142-144). [Al-Itqaanu fiy Uluwmil-Qur-aan (1/197)] Na pia Aayah (136) (138-139).
Miongoni Mwa Makusudio Ya Suwrah:
1-Kuithibitisha ‘Aqiydah ya Tawhiyd, na kuupinga upotevu wa washirikina. [Al-Mukhtaswar Fiy Tafsiyr Al-Qur-aan Al-Kariym]
2-Kuifanya Aqiydah iwe madhubuti, na kuidhoofisha na kuipinga shirki.
3-Kuwafahamisha watu Utukufu wa Muumba wao, na kusimamisha dalili ya kwamba Allaah (سبحانه وتعالى) Yuko Peke Yake, Naye Ndiye Anayepasa kuabudiwa kwa haki.
4-Kuthibitisha Unabiy wa Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم), na uhakika wa Siku ya Mwisho na malipo yake.
5-Kuwasimamishia hoja washirikina na watu wa bid’ah, na wale wanaokadhibisha kufufuliwa, na kuziondoa shubha ya hayo.
6-Kubainisha ujahili wa washirikina.
Miongoni Mwa Maudhui Ya Suwrah:
1-Suwrah imefunguliwa kwa Kumhimidi Allaah (سبحانه وتعالى) na kubainisha kuwa Anayestahiki shukrani ni Yeye Allaah Pekee, kwani Yeye Ndiye Muanzilishi wa kila kilichomo ulimwenguni. Na kubatilisha athari za washirika kama vile masanamu na majini, kwa kuthibitisha kuwa Allaah Ndiye Muumba wa vyote vilivyomo ulimwenguni, na uumbaji wa binaadam na nidhamu ya maisha yake, ya kufa kwake kwa Hikma Yake Allaah (سبحانه وتعالى) na Ujuzi Wake. Na kumtakasa Allaah kutokana na kumhusisha na mke na mwana.
2-Kuna mawaidha kwa wale wanaopinga Aayah za Qur-aan, na wanaokadhibisha haki na Siku ya Mwisho, na kuwatisha kwamba yatawatokea kama yaliyowatokea watu (wapingaji) waliopita kabla yao, na waliozikufuru Neema za Allaah (سبحانه وتعالى), na kwamba kupinga kwao hakutamdhuru yeyote isipokuwa nafsi zao. Na ahadi ya adhabu zao watazikuta watakapotolewa roho zao kisha tena watakapofufuliwa.
3-Imetajwa sifa ya upumbavu ya washirikina kwa ile rai walioitoa kwa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) ya kumtaka alete vitu vinavyoenda kinyume na mazoea, kwa lengo la kumtingisha Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم). Na kuthitibisha uhakika wa Qur-aan na uhakika wa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) na kwamba watu wa Kitabu wanatambua kuwa ni haki kuliko hata wanavowatambua watoto wao!
4-Suwrah imetaja dalili nyingi za kuonyesha kuwa Allaah ni Mmoja na Mwenye Uwezo, na kwamba Yeye tu Ndiye Mwenye kustahiki kuabudiwa.
5-Washirikina wamekemewa juu ya kupinga kwao ufufuo, na kuwathibitishia kwamba ufufuo upo na kwamba wao baada ya kufufuliwa watakuja kuadhibiwa. Na kwamba waabudiwa wao waliokuwa wakiwaabudu watawakana na watawatenga Siku hiyo, na watakuja kujuta kwa hilo, na wala haiwafai kitu katika maisha ya dunia kwani hawaombi kwa yeyote isipokuwa Allaah wakati wa majanga.
6-Imetajwa mateso ya washirikina na madhalimu kutokana shirki na kufru zao; mateso pale wanapotolewa roho zao na jinsi watakapohudhurishwa motoni. Miongoni mwao ni wale waliodai kuwa wameteremshiwa Wahyi ilhali ni uongo mkubwa kwani hakuna Nabii baada ya Nabiy Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم). Pia imetajwa hali zao watakapofufuliwa na watakapokana shirki zao.
7-Kwenye Suwrah kuna kiliwazo kwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) na kuuthibitisha moyo wake, na kumlingania kuwa na subra kwa kuvumilia changamoto za Urasuli bila kuhisi uchovu wala uvivu, na ni mwongozo juu ya kuwaiga Rusuli waliopita kabla yake, ambao walisubiri pamoja na kupingwa na watu wao.
8-Imebainishwa Hikma ya Allaah juu ya kuwatuma Rusuli, na kwamba hikma kubwa ni kuwabashiria na kuwaonya watu, na wala kazi za Rusuli si kuwafahamisha watu mambo ya ghaibu.
9-Imebainishwa kwamba Allaah Pekee Ndiye Anayehusika kutambua ghaibu.
10-Suwrah imewabainisha wale ambao wanaweza kuitikia na kujibu daawah ya haki, kuwa ni wale wanaosikiliza na kukubali mawaidha. Ni wale ambao nyoyo zao ziko hai, ama wale ambao nyoyo zao zimekufa hawa hawataweza kunufaika na mawaidha, na wala hawakubali mwongozo, ila watambue kuwa hatima yao ni kwa Allaah na watakuja kulipwa juu ya kufru zao na matendo yao maovu.
11-Imebainishwa kuwa ubora wa watu upo katika taqwa ya Allaah na kujinasibisha katika Dini ya Allaah, na kubatilisha kile walichokiweka washirikina, ambayo ni sheria ya upotovu.
12-Kuna makatazo juu ya kukaa na wale wanaozipuuza na kuzifanyia istihzai Aayah za Allaah, na kutokukaa kuongea nao.
13-Kuna amri ya kuwapuuza washirikina, na makatazo ya kuyatukana masanamu na wale wanaoyaabudia ili wasilipize kumtukana Allaah (سبحانه وتعالى).
14-Suwrah pia imebainisha kwamba taqwa ya kweli haipatikani kwa mtu kujinyima vitu vizuri tu, bali kwa kujinyima pia matamanio ya nafsi.
15-Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) amepigiwa mfano pamoja na watu wake, kama mfano wa Nabiy Ibraahiym (عليه السّلام) baba yake pamoja na watu wake, na Manabii na Rusuli wote walikuwa katika mifano hiyo, kuanzia wa mwanzo hadi wa mwisho. Katika Suwrah hii Manabii kumi na nane wametajwa pamoja na Nabiy Ibraahiym (عليه السّلام). Rejea Aayah namba (83-86).
16-Zimetajwa Neema za Allaah (سبحانه وتعالى) kadhaa, ikiwemo neema kwa Ummah kutokana na kuteremshiwa Qur-aan yenye mwongozo kwao, kama Alivyoteremsha Kitabu kwa Muwsaa (عليه السّلام) na kwamba Allaah (سبحانه وتعالى) Amejaalia kuwa ni ummah bora wa mwisho.
17-Suwrah imebainisha fadhila ya Qur-aan na Dini ya Kiislam, na malipo makubwa Aliyoyaweka Allaah (سبحانه وتعالى) kwa mtu atakayeisoma.
18-Suwrah imetajwa Neema nyingi za Allaah (سبحانه وتعالى) ambazo zimewaenea viumbe wa Allaah (سبحانه وتعالى) kama neema za mazao mbalimbali na imetaja funguo za ghaibu.
19-Suwrah imeelezea sifa za Waarabu zama za Ujahiliyyah, pamoja na kubainisha shirki na kufru zao kuhusiana na wanyama. Na Suwrah hii ya Al-An’aam ndio Suwrah pekee katika Qur-aan iliyoelezea kwa kina juu ya hilo.
20-Suwrah imetaja Wasia wa Allaah (سبحانه وتعالى) wa maamrisho kadhaa na makatazo. Rejea Aayah (151-153).
21-Allaah Ametaja katika Suwrah hii ukhalifa (utawala) wa viumbe, na utofauti wa daraja zao, na Allaah (سبحانه وتعالى) Akamalizia kwa kutaja uharaka wa Adhabu Zake kwa wanaostahiki, na Rehma na Maghfirah Yake kwa wanaostahiki kupata.
22-Suwrah imekhitimishwa kwa kuthibitishwa Tawhiyd ya Uluwhiyyah (Kumpwekesha Allaah katika ibaada) kama Swalaah, kuchinja. Na pia kwa kukanusha shirki. Na ikathibitishwa pia Tawhiyd ya Ar-Rubuwbiyyah (Uola; Uumbaji), na kwamba marejeo ya viumbe yatakuwa kwa Allaah Siku ya Qiyaamah ambako kutakuwa na malipo ya matendo mema na maovu, na kubainika Siku hiyo mambo yote waliyokhitilafiana watu katika Dini.
Fadhila Za Suwrah:
عنِ ابنِ عبَّاسٍ رضِي اللهُ عنهما، قالَ: نزَلَتْ سورَةُ الأنعامِ بمَكَّةَ ليلًا جُملةً، حولَها سَبعونَ ألفَ مَلَكٍ، يَجأرُونَ حولَها بالتَّسبيحِ
Amesimulia Ibn ‘Abbaas (رضي الله عنهما): Suwrah nzima ya Al-An’aam imeteremshwa Makkah, usiku, ikifuatiliwa na Malaika elfu sabini wakinyanyua sauti zao kumsabihi Allaah. [Tafsiyr Ibn Kathiyr]
Faida:
1-Suwrah Al-An’aam (6), ni miongoni mwa Suwrah tano zinazoanzia kwa AlhamduliLlaah. Nyenginezo ni Al-Faatihah (1), Al-Kahf (18), Saba-a (34) na Faatwir (35).
2-Ni Suwrah mojawapo yenye kuthibitisha Tawhiyd ya Allaah na kupinga shirki kwa dalili nyingi za wazi kabisa.
3-Suwrah inayodhihirisha ujinga wa washirikina wa Makkah kama ilivyoelezewa katika Hadiyth:
عنِ ابنِ عباسٍ رضي اللهُ عنهما، قال: إذا سَرَّك أنْ تَعلَمَ جَهْلَ العربِ، فاقرَأْ ما فَوقَ الثَّلاثينَ ومِئَةٍ في سورةِ الأنعامِ: قَدْ خَسِرَ الَّذِينَ قَتَلُوا أَوْلَادَهُمْ سَفَهًا بِغَيْرِ عِلْمٍ... إلى قولِه: قَدْ ضَلُّوا وَمَا كَانُوا مُهْتَدِينَ
Imesimuliwa na Ibn Abbas (رضي الله عنهما) amesema: Likikufurahisha wewe kutambua ujinga wa waarabu, basi soma Aayah zilizo zaidi ya mia moja na thelathini ya Suwrah Al-An’aam:
قَدْ خَسِرَ الَّذِينَ قَتَلُوا أَوْلَادَهُمْ سَفَهًا بِغَيْرِ عِلْمٍ وَحَرَّمُوا مَا رَزَقَهُمُ اللَّـهُ افْتِرَاءً عَلَى اللَّـهِ ۚ قَدْ ضَلُّوا وَمَا كَانُوا مُهْتَدِينَ ﴿١٤٠﴾
“Kwa yakini wamekhasirika wale waliowaua watoto wao kwa upumbavu bila ya ujuzi na wakaharamisha vile Alivyowaruzuku Allaah kwa kumtungia uongo Allaah. Kwa yakini wamepotea na wala hawakuwa wenye kuhidika.” [Al-An’aam (6:140)- Hadiyth ameipokea Imaam Al-Bukhaariy]
4-Suwrah imeanzia Aayah ya mwanzo kwa Thanaa ya Allaah (سبحانه وتعالى) kwa Kumhimidi na pia hapo hapo imepinga shirki kwa kumlinganisha Allaah (سبحانه وتعالى) na viumbe. Kisha Suwrah imekhitimishwa kwa kuthibitisha Tawhiyd ya Allaah na imepinga kumshirikisha Allaah. Rejea Aayah (161-163).
007-Al-A’raaf: Utangulizi Wa Suwrah
Alhidaaya.com [2]
Imeteremka: Makkah kwa itifaki ya ‘Ulamaa.
Idadi Za Aayah: 206
Jina La Suwrah: Al-A’raaf
Suwrah imeitwa Al-A’raaf (Mnyanyuko), na inayodalilisha ni kutajwa katika Hadiyth iliyonukuliwa chini katika Fadhila. Na pia kutajwa Al-A’raaf katika Aayah namba (46-48). Nao ni mnyanyuko wa watu watakaokuwa baina ya Jannah na moto.
Miongoni Mwa Makusudio Ya Suwrah:
1-Kushinda haki katika mapambano yake ya baatwili, na kubainisha mwisho wa watu wenye kiburi duniani na Aakhirah. [Al-Mukhtaswar Fiy Tafsiyr Al-Qur-aan Al-Kariym]
2-Kubainisha na kuthibitisha ‘Aqiydah na suala la Tawhiyd na shirk.
3-Kubainisha ‘Aqiydah ya kufufuliwa na marejeo ya viumbe kwa Allaah na hesabu Siku ya Qiyaamah.
4-Kumliwaza Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) kutokana na kukanushwa kwake na makafiri.
5-Kubainishwa hukmu na sharia kwa ujumla, na kwamba Mwenye kutunga sharia ni Mwenye Muumbaji Allaah (سبحانه وتعالى), kama mfano sharia ya kuchukua mapambo Misikitini na kula na kunywa vitu vizuri vilivyo halali, na kukemea mapambo yaliyoharamishwa. Na umuhimu wa kutafakari Aayaat na Ishara, Dalili zinazohusu Uumbaji Wake Allaah (سبحانه وتعالى) na fadhila Zake juu ya Waja Wake..
6-Kubainisha suala la Rusuli kuhusu kufikisha Risala (Ujumbe) ambao umeelezwa katika Suwrah iliyopita. Na suala la majibizano baina ya Rusuli na kaumu zao.
7-Kubainisha kuwa malipo ni kutokana na juhudi na matendo ya mwanaadam. Na kuthibitisha hoja za watu Jannah kwa watu wa motoni. Na kuonya kwamba Siku ya Qiyaamah itakuja kwa ghafla, na Suwrah ilionya juu ya muda huo maalumu uliopangwa na kukadiriwa na Allaah (سبحانه وتعالى) kama Anavyosema Allaah (سبحانه وتعالى) katika Aayah namba (4).
Miongoni Mwa Maudhui Ya Suwrah:
1-Suwrah imefunguliwa kwa herufi zinazojulikana kama الحروف المقطعة (Al-Huruwf Al-Muqatw-twa’ah), ambazo hakuna ajuaye maana zake isipokuwa Allaah (سبحانه وتعالى). Rejea Al-Baqarah (2:1). Kisha ikabainisha Utukufu wa Kitabu cha Allaah na kumliwaza Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) kuwa asitie shaka katika kufikisha Risala kwa watu na kuwaonya, na kwamba ni ukumbusho kwa Waumini.
2-Kuna maharamisho ya kumshirikisha Allaah (سبحانه وتعالى), na kuwasimamishia washirikina hoja ya kwamba Allaah ni Mmoja tu! Na kuwaonya washirikina kwamba, watakuwa na mwisho mbaya hapa duniani na Aakhirah, na kuelezea juu ya kile kitachowatokea washirikina na wale waliowakadhibisha Rusuli wa Allaah.
3-Imetajwa uzito wa mizani za matendo siku ya Qiyaamah, na kuwakumbusha watu juu ya neema ya kuumbwa ardhi, na kumfanya mwanaadam awe mnufaika namba moja wa kheri za ardhini.
4-Imeelezea kuumbwa kwa Aadam, na kukataa kwa Ibliys kumsujudia (Aadam), na Ibliys kuwatia wasiwasi na kuwashawishi Aadam (عليه السّلام) na mkewe ili wale mti waliokatazwa. Kisha muendelezo uliopo juu ya uadui wa shaytwaan kwa mwanaadam. Na watu kutahadharishwa wasijitie katika udanganyifu na hila za shaytwaan kutokana na kuwataka kwake wajinyime mambo ya kheri, na kutumbukia katika yale yanayowasukuma kwenye adhabu huko Aakhirah.
5-Kuna maelezo ya vitisho vya Siku ya Malipo kwa waovu, na Ukarimu wa Allaah kwa wamchao Yeye (سبحانه وتعالى).
6-Kimetajwa Kisa cha Asw-haabul-Al-A’raaf (watu walio kati muinuko kati ya watu wa Jannah na watu wa motoni), na kuwakumbusha watu kufufuliwa na kukaribia ishara zake.
7-Kuna makatazo juu ya kufanya ufisadi katika ardhi. Ardhi ambayo Allaah (سبحانه وتعالى) Ameiweka kwa faida na maslahi kwa wanaadam.
8-Imetajwa sehemu ya visa vya Rusuli wa Allaah katika kulingania kaumu zao washirikina, na kauli za kila Rasuli kwa kaumu zao, na majibu ya washirikina ambayo ni ya ukaidi, inadi na upingaji Risala ya Allaah, na maudhi waliyopata Rusuli wa Allaah kutoka kaumu zao. Imeanza kisa cha Nabiy Nuwh (عليه السّلام). Kisha kisa cha Nabiy Huwd (عليه السّلام) na kuangamizwa kwa watu wa ‘Aad. Kisha kisa cha Nabiy Swaalih (عليه السّلام) na jeuri za watu wa Thamuwd. Kisha kisa cha Nabiy Luutw (عليه السّلام) na watu wake. Kisha kisa cha Nabiy Shu’ayb na watu wa Madyan.
9-Kuna vitisho kwa wanaojiaminisha na makri za Allaah (kwa kuwa Allaah Analipiza makri za waovu), na kuwaonya kwamba wasidanganyike kwa kuona Allaah Anawapa muhula wale wanaomuasi kabla adhabu haijawashukia. Hivyo basi ni fursa yao kuacha ukafiri na ukaidi wao kwani adhabu huwajia kwa ghafla baada ya muhula huo.
10-Imeelezewa sehemu ya kisa cha Muwsaa (عليه السّلام) kwa tafsili, yakiwemo maelezo ya wachawi na kuomba uokovu wana wa Israaiyl. Ametajwa Haruwn (عليه السّلام) ambaye ni ndugu wa Nabiy Muwsaa (عليه السّلام) na kuhusu pindi alipomwachia awaongoze wana wa Israaiyl, na Miyqaat (sehemu na wakati) ya Nabiy Muwsaa (عليه السّلام) kukutana na Allaah. Ikafuatia maelezo ya kuabudiwa ndama na mtu aliyeitwa Saamiriyy ambaye aliwapotosha watu kumwabudu ndama.
11-Imetajwa bishara ya kutumwa kwa Nabiy Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم) na wasifu wa Ummah wake, na fadhila ya Dini hii tukufu.
12-Mna kisa cha As-Sabt; Mayahudi kuvua samaki siku ya Jumamosi ambamo walikatazwa lakini wakavua samaki kwa ujanja, basi Allaah Akawageuza manyani.
13-Kuna mawaidha kwa washirikina kugeuza kwao Tawhiyd ya Allaah na kuingia katika shirki. Allaah (سبحانه وتعالى) Anakumbusha watu kuhusu ahadi ya Alastu, ambayo kila binaadam alifungamana na Allaah wakati walikuwa katika Fitwrah (maumbilie ya asili ya kumpwekesha Allaah) kabla ya kuzaliwa kwao. Ni Ahadi ya kutokumshirikisha Allaah, basi wasije watu Siku ya Qiyaamah kudai kuwa hawakukumbushwa.
14-Ametajwa mtu aliyepewa ilimu lakini shaytwaan akamshawishi akafuata matamanio yake akapotoka. Basi ni hilo ni funzo kwa watu watafakari na watahadhari.
15-Kuna maelezo kuhusu shirki za washirikina, na kwamba waabudiwa wao hawawezi kuumba kitu wala hawawezi kuwanusuru au kuwaitikia wito wao. Hayo ni kinyume na Tawhiyd ya Allaah kwani Allaah Ana Majina Mazuri kabisa na Sifa Zake Zilotukuka ambazo Waumini wameamrishwa watumie katika duaa zao.
17-Kuna Amri ya Allaah (سبحانه وتعالى) kwa Rasuli Wake (صلى الله عليه وآله وسلم) na Waislamu; wawe na subra na kuendeleza wito, na kuwaonya juu ya uchochezi wa shaytwaan.
18-Suwrah imekhitimiswa kwa amri ya kuomba kinga dhidi ya shaytwaan katika kuanza kusoma Qur-aan, na kuisikiliza kwa makini ili imteremkie msomaji, Rehma ya Allaah. Na kumcha Allaah kwa kumdhukuru kwa siri na dhahiri bila ya kughafilika Naye, na kuendelea kumwabudu. Na ikabainishwa kwamba Malaika hawafanyi kiburi kwa kuacha kumwabudu Allaah, bali wao wanaandamana na Amri Zake, wanamtakasa mchana na usiku, na wanamwepusha na mambo yasiyonasibiana na Yeye, na kwamba wanamsujuduia Yeye Peke Yake. Na hapo kuna alama ya Sajdah At-Tilaawa (Sijda ya kusoma Qur-aan).
Fadhila Za Suwrah:
Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) Aliisoma Suwrah Al-A’raaf Katika Swalaah Ya Maghrib:
عن عائِشةَ رَضِيَ اللهُ عنها: أنَّ رَسولَ اللهِ صلَّى اللهُ عليه وسَلَّم قَرَأَ في صلاةِ الـمَغرِبِ بسورةِ الأعرافِ؛ فَرَّقَها في رَكعتَينِ
Amesimulia ‘Aaisha (رضي الله عنها): Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alisoma katika Swalaah ya Maghrib Suwrah Al-A’raaf na akaigawa katika rakaa mbili. [An-Nasaaiy, At-Tirmidhiy]
حَدَّثَنَا أَبُو عَاصِمٍ، عَنِ ابْنِ جُرَيْجٍ، عَنِ ابْنِ أَبِي مُلَيْكَةَ، عَنْ عُرْوَةَ بْنِ الزُّبَيْرِ، عَنْ مَرْوَانَ بْنِ الْحَكَمِ، قَالَ قَالَ لِي زَيْدُ بْنُ ثَابِتٍ مَا لَكَ تَقْرَأُ فِي الْمَغْرِبِ بِقِصَارٍ، وَقَدْ سَمِعْتُ النَّبِيَّ صلى الله عليه وسلم يَقْرَأُ بِطُولِ الطُّولَيَيْنِ
Amesimulia Marwaan Bin Al-Hakam (رضي الله عنه): Zayd bin Thaabit aliniambia: “Kwa nini unasoma Suwrah fupi sana katika Swalaah ya Maghrib, ilhali nilimsikia Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akisoma Suwrah ndefu kati ya Suwrah mbili ndefu?” [Al-Bukhaariy]
008 -Al-Anfaal: Utangulizi Wa Suwrah
Alhidaaya.com [2]
Imeteremka: Madiynah kwa itifaki ya 'Ulamaa.
Idadi Za Aayah: 75
Jina La Suwrah: Al-Anfaal
Suwrah imeitwa Al-Anfaal (Mali Inayopatika Vitani), na inayodalilisha ni kutajwa katika Hadiyth iliyonukuliwa chini katika Faida. Na kutajwa Al-Anfaal (Mali Inayopatika Vitani) katika Aayah namba (1) na (41).
Miongoni Mwa Makusudio Ya Suwrah:
1-Waumini kuneemeka na Nusra ya Allaah kwao katika Vita vya Badr na kubainisha desturi ya Allaah kuwajaalia ushindi Waislamu na kushambuliwa (kwa makafiri). [Al-Mukhtaswar Fiy Tafsiyr Al-Qur-aan Al-Kariym]
2-Maelezo ya vita vya Badr na maamrisho ya maandalizi ya Jihaad, na kubainisha sababu za ushindi wa vita na baadhi ya hukmu za Jihaad na ugawaji wa ghanima (ngawira inayopatikana baada ya kupigana vita) pamoja na matekwa wa vita.
3-Kubainisha hukmu za mahusiano ya jamii, familia kwa maadili na akhlaaq (tabia) njema.
4-Kumtii Allaah na Rasuli Wake (صلى الله عليه وآله وسلم).
Miongoni Mwa Maudhui Ya Suwrah:
1-Suwrah imefunguliwa kwa kubainishwa hukmu za Anfaal (mali inayopatikana katika vita) na ghanima (ngawira inayopatikana baada ya kupigana vita) na uchambuzi wa jinsi ya kuzigawa kwake. Pia maamrisho ya kumcha Allaah kwenye suala hilo na mengineyo, na watu kutakiwa kumtii Allaah na Rasuli Wake (صلى الله عليه وآله وسلم) kwenye jambo la ghanima na mengineyo. Pia kuwaamrisha Waislamu kupatana wao kwa wao, na hilo ndio linakamilisha imaan zao.
2-Waumini wa kweli wamesifiwa na kuwapa bishara ya kuwa watapata daraja na mahali patukufu.
3-Suwrah imetaja jinsi Waislamu walivyotoka kwenda katika Vita vya Badr, na kwamba baadhi yao walichukia jambo hilo, lakini Allaah (سبحانه وتعالى) Akalazimisha kwa Hikma Yake Vita hivi, kwa kuwa Alitaka kuthibitisha haki na Abatilishe baatwil. Pia Suwrah imetaja Nusra ya Allaah walioipata Waumini katika Vita hivi. Pia amri ya kujiandaa na vita, na makatazo ya kukimbia vita na watu kugombana na kutofautiana.
4-Suwrah imeelezea yaliyotokea katika Vita vitukufu vya Badr na miujiza ya Allaah (سبحانه وتعالى) Kuteremsha Malaika tele wawasaidie Waislamu na jinsi gani ilivyokuwa ushindi kwa Waislamu juu ya kuwa idadi yako ilikuwa ni ndogo mno kulingana na idadi ya makafiri. Pia miujiza ya Allaah (سبحانه وتعالى) Kuwarushia makafiri mchanga. Pia miujiza ya Allaah (سبحانه وتعالى) Kuwateremshia Waislamu utulivu juu ya kuwa walikuwa na kiwewe Akawajaalia usingizi mzito mno hadi wakaota usingizini kisha Allaah (سبحانه وتعالى) Akawateremshia mvua ya kujitwaharisha, na Akathibitsha miguu yao ardhini.
5-Maelekezo kwa ulingano wa aina mbalimbali kwa Waumini, na kuwaelekeza kwa kila ulingano kwenye jambo maalum lenye kheri na wao, na kufaulu kwao.
6-Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) amekumbushwa Neema ya Allaah juu yake, pale alipomuokoa na vitimbi vya washirikina wa mji wa Makkah.
7-Suwrah imetaja pia tabia za washirikina ambazo ni ujinga na ukaidi.
8-Imebainishwa kwamba, kuishi kwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) pale Makkah ilikuwa ni amani kwa washirikina, na alipoondoka ndipo ikaja kuwathibitikia adhabu ya dunia kutokana na yale waliyoyafanya ambayo ni kuwazuia watu na Masjid Al-Haraam.
9-Maamrisho ya kuwalingania washirikina kuwataka waache kuufanyia uadui Uislamu na kuwaudhi Waislamu kwa kuwapiga vita, na kutowa tahadhari juu ya wanafiki.
10-Suwrah imetaja hukmu za ahadi kati ya Waislamu wao kwa wao, na kati ya Waislamu na makafiri, na madhara yanayopatikana kutokana na kuvunja ahadi.
11-Kuna uchambuzi wa ghanima (ngawira inayopatikana baada ya kupigana vita) na kubainisha kuwa mwanzoni mwa Suwrah limetajwa hilo kwa ujumla.
12-Suwrah imekhitimishwa kwa kutajwa hukmu ya Waislamu waliohajiri na wakafanya Jihaad katika njia ya Allaah na waliobaki Makkah baada ya Hijrah, na hali ya maisha yao.
Faida:
Suwrah Al-Anfaal imeteremka siku ya Vita vya Badr:
عَنْ سَعِيدِ بْنِ جُبَيْرٍ، قَالَ قُلْتُ لاِبْنِ عَبَّاسٍ سُورَةُ التَّوْبَةِ قَالَ التَّوْبَةُ هِيَ الْفَاضِحَةُ، مَا زَالَتْ تَنْزِلُ وَمِنْهُمْ وَمِنْهُمْ، حَتَّى ظَنُّوا أَنَّهَا لَمْ تُبْقِ أَحَدًا مِنْهُمْ إِلاَّ ذُكِرَ فِيهَا. قَالَ قُلْتُ سُورَةُ الأَنْفَالِ. قَالَ نَزَلَتْ فِي بَدْرٍ. قَالَ قُلْتُ سُورَةُ الْحَشْرِ. قَالَ نَزَلَتْ فِي بَنِي النَّضِيرِ.
Amesimulia Jubayr: Nilimuuliza Ibn ‘Abbaas (رضي الله عنهما): Nini Suwrah At-Tawbah? Akasema At-Tawbah ni fedheha (yaani Suwrah inayofichua maovu yote ya makafiri na wanafiki). Na iliendelea kuteremka; Wa minhum, wa minhum (na miongoni mwao, na miongoni mwao), mpaka wakadhani kuwa Suwrah hiyo haikubakisha hata mtu mmoja isipokuwa atakuwa ametajwa humo.” Nikamuuliza: Nini kuhusu Suwrah Al-Anfaal? Akanijibu “Imeteremka kuhusu Badr.” Nikamuuliza: Suwrah Al-Hashr? Akasema “Imeteremka kuhusiana na Bani Nadhiyr.” [Al-Bukhaariy Kitaab At-Tafsiyr]
009-At-Tawbah: Utangulizi Wa Suwrah
Alhidaaya.com [2]
Imeteremka: Madiynah kwa itifaki ya ‘Ulamaa.
Idadi Za Aayah: 129
Jina La Suwrah: At-Tawbah:
Suwrah imeitwa At-Tawbah (Kutubia), na inayodalilisha ni kutajwa katika Hadiyth iliyonukuliwa chini katika Faida namba (1). Na imeitwa At-Tawbah kutokana na neno hili la tawbah kukariri kwa wingi kuliko Suwrah nyenginezo. Rejea chini katika Faida namba (2).
Pia, Suwrah inajulikana kama Suwrah Al-Baraa-ah kutokana na Hadiyth ifuatayo:
حَدَّثَنَا سُلَيْمَانُ بْنُ حَرْبٍ، حَدَّثَنَا شُعْبَةُ، عَنْ أَبِي إِسْحَاقَ، سَمِعْتُ الْبَرَاءَ ـ رضى الله عنه ـ قَالَ آخِرُ سُورَةٍ نَزَلَتْ بَرَاءَةَ .
Amesimulia Al-Baraa (رضي الله عنه): Suwrah ya mwisho kuteremka ni Baraa-ah. [Al-Bukhaariy Kitaab At-Tafsiyr]
Kuna majina mengineyo ya Suwrah hii, rejea Faida namba (3), ila majina hayo mawili ya At-Tawbah na Al-Baraa ndio yaliyothibiti kuwa ni Tawqifiyy (Imethibiti dalili za Quraan na Sunnah na sio kutokana na rai za watu).
Miongoni Mwa Makusudio Ya Suwrah:
1-Utakaso kutokana na wanafiki na washirikina, na (kwamba inafaa kuwapiga) Jihaad hao, na kufungua mlango wa tawbah kwa watakaotubia.
[Al-Mukhtaswar Fiy Tafsiyr Al-Qur-aan Al-Kariym]
2-Kuweka mchoro wa njia ambayo wanalazimika kuipita hiyo Waumini katika mahusiano yao pamoja na washirikina, na pamoja na Ahlul-Kitaab na wanafiki.
3-Kuwakashifu wanafiki na matendo yao, na kuwafedhehesha mbele ya jamii ya Kiislamu.
4-Kubainisha hukmu nyingi na miongozo ambayo inatakiwa kufuatwa kwa dola changa (inayoanza).
Miongoni Mwa Maudhui Ya Suwrah:
1-Suwrah imefunguliwa kwa kukumbushwa kujiweka mbali na kujitakasa na washirikina, na amri ya kuwapiga vita kwa sababu ya kuvunja ahadi zao, na kuwazuia kuingia Masjidul-Haraam. Makatazo ya kutokuwapenda washirikina hata kama watakuwa ndugu wa karibu.
2-Kuna ishara ya kutokea kwa Vita vya Hunayn, na kuzilea nafsi za Waumini juu ya ukweli wa kumtegemea Allaah (سبحانه وتعالى).
3-Imewatangazia vita Ahlul-Kitaab mpaka walipe kodi, na kwamba wao hawako mbali sana na washirikina, na kwamba mali zao wala nguvu zao hazitawafaa.
4-Radd kwa kauli za Manasawara na Mayahudi juu ya dhulma kubwa ya kumsingizia Allaah (سبحانه وتعالى) kwamba Uzayr na Nabiy ‘Iysaa ni wana wa Allaah.
5-Imetiliwa msisitizo Risala ya haki ya Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم).
6-Wasomi wa Kiyahudi wamekemewa katika kula kwao mali za watu kwa baatwil.
7-Imetajwa heshima ya miezi mitukufu, na kudhibiti kwa miaka ya kisharia, na kubatilisha kuichelewesha miezi (kuibadilisha miezi mitukufu kuiweka si mahala pake), kama ilivyokuwa tabia za Kijaahiliyyah.
8-Kuna mahimizo ya Jihaad na kuwataka watu wajitolee kwa mali na nafsi zao, na kutoielemea dunia na mapambo yake.
9-Imeelezwa Nusrah ya Allaah kwa Rasuli Wake (صلى الله عليه وآله وسلم) akiwa na swahibu yake (Abubakar Asw-Swidddiyq), na jinsi Allaah (سبحانه وتعالى) Alivyowahami kutoonekana na makafiri katika pango.
10-Zimetajwa sifa za wanafiki na tabia zao za kuwafanyia vitimbi Waislamu, na kumuudhi Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) kwa maneno na matendo, na kuamrisha kwao maovu na kukataza wema.
11-Imetajwa ujenzi wa Masjid Dhwiraar uliojengwa na wanafiki kwa lengo la uharibifu, na vitimbi vya wanafiki kwa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم).
12-Imetajwa ujenzi wa Masjid Qubaa uliojengwa kwa lengo la Taqwa na kumtii Allaah (سبحانه وتعالى) na kwamba Msikiti huo ndio bora zaidi Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akasimame na kuswali hapo.
13-Kuna makatazo ya kuwaombea washirikina maghfirah hata kama ni wenye uhusiano wa damu.
14-Imetajwa kukubaliwa kwa tawbah ya wale waliokhalifu (wasioenda) katika Vita vya Tabuwk.
15-Kuna mahimizo ya kutafuta ilimu ya Dini ya Allaah (سبحانه وتعالى) na kuibalighisha Dini kwa watu.
16-Suwrah imekhitimishwa kwa kutajwa sifa nyengineyo ya wanafiki kwamba inapoteremshwa Suwrah, wanafiki huashiriana kwa macho, kwa kuchukia kuteremka kwake kwa sababu ya kutajwa aibu zao na matendo yao, kisha huondoka kuogopa fedheha. Na mwishowe Waislamu wamekumbushwa neema ya Allaah kwao, ambayo ni kutumiwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) kutokana na wao; Nabiy ambaye anawajali Waislamu, na huruma zake juu yao.
Faida:
1-Suwrah ya At-Tawbah ni Suwrah pekee katika Qur-aan ambayo haikuanzwa kwa:
بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيم
Na kuna kauli mbali za ‘Ulamaa kuhusu sababu zake.
2-Suwrah At-Tawbah ni Suwrah ya fedheha kwa sababu ya kufichuliwa maovu ya makafiri na wanafiki:
عَنْ سَعِيدِ بْنِ جُبَيْرٍ، قَالَ قُلْتُ لاِبْنِ عَبَّاسٍ سُورَةُ التَّوْبَةِ قَالَ التَّوْبَةُ هِيَ الْفَاضِحَةُ، مَا زَالَتْ تَنْزِلُ وَمِنْهُمْ وَمِنْهُمْ، حَتَّى ظَنُّوا أَنَّهَا لَمْ تُبْقِ أَحَدًا مِنْهُمْ إِلاَّ ذُكِرَ فِيهَا. قَالَ قُلْتُ سُورَةُ الأَنْفَالِ. قَالَ نَزَلَتْ فِي بَدْرٍ. قَالَ قُلْتُ سُورَةُ الْحَشْرِ. قَالَ نَزَلَتْ فِي بَنِي النَّضِيرِ.
Amesimulia Sa’iyd Bin Jubayr: Nilimuuliza Ibn ‘Abbaas (رضي الله عنهما): Nini Suwrah At-Tawbah? Akasema At-Tawbah ni fedheha (yaani Suwrah inayofichua maovu yote ya makafiri na wanafiki). Na iliendelea kuteremka; Wa minhum, wa minhum (na miongoni mwao, na miongoni mwao), mpaka wakadhani kuwa Suwrah hiyo haikubakisha hata mtu mmoja isipokuwa atakuwa ametajwa humo.” Nikamuuliza: Nini kuhusu Suwrah Al-Anfaal? Akanijibu “Imeteremka kuhusu Badr.” Nikamuuliza: Suwrah Al-Hashr? Akasema “Imeteremka kuhusiana na Bani Nadhiyr.” [Al-Bukhaariy Kitaab At-Tafsiyr]
3-Sababu ya kuitwa At-Tawbah pia ni kutokana na neno hili la tawbah kukariri kwa wingi, kiasi cha mara kumi na saba, hivyo basi ni mara nyingi kuliko Suwrah nyenginezo. Na tawbah mojawapo ni ile Aliyoipokea Allaah (سبحانه وتعالى) kwa Nabiy Wake (صلى الله عليه وآله وسلم) na Muhaajiruwna na Answaar, rejea Aayah (117). Na pia tawbah ya Swahaba watatu waliotubia baada ya makosa yao kutokwenda vita vya Jihaad vya Tabuwk, rejea Aayah (118) kwenye faida tele na Sababun-Nuzuwl (Sababu Ya Kuteremshwa) Aayah Au Suwrah.
4-Suwrah hii imepewa pia majina mengineyo kadhaa kama Al-Suwrah Al-Faadhwihah (fedheha), Suwrah Al-‘Adhaab (adhabu), na majina mengineyo, lakini yaliyothibiti ni mawili tu kama ilivyotangulia kutajwa.
5-Aayah mbili za mwisho za Suwrah At-Tawbah zimepatikana kwa Abuu Khuzaymah Al-Answaariyy (رضي الله عنه):
عَنِ ابْنِ السَّبَّاقِ، أَنَّ زَيْدَ بْنَ ثَابِتٍ، حَدَّثَهُ قَالَ أَرْسَلَ إِلَىَّ أَبُو بَكْرٍ فَتَتَبَّعْتُ الْقُرْآنَ حَتَّى وَجَدْتُ آخِرَ سُورَةِ التَّوْبَةِ مَعَ أَبِي خُزَيْمَةَ الأَنْصَارِيِّ لَمْ أَجِدْهَا مَعَ أَحَدٍ غَيْرِهِ لَقَدْ جَاءَكُمْ رَسُولٌ مِنْ أَنْفُسِكُمْ حَتَّى خَاتِمَةِ بَرَاءَةٌ. حَدَّثَنَا يَحْيَى بْنُ بُكَيْرٍ، حَدَّثَنَا اللَّيْثُ، عَنْ يُونُسَ، بِهَذَا وَقَالَ مَعَ أَبِي خُزَيْمَةَ الأَنْصَارِيِّ.
Amesimulia ‘Ubayd bin As-Sabbaaq (رضي الله عنه): Zayd bin Thaabit (رضي الله عنه) amesema: Abu Bakr (رضي الله عنه) alimtuma mtu kuniita. Hivo nikaanza kuikusanya Qur-aan mpaka nikaipata sehemu ya mwisho ya Suwrah At-Tawbah kutoka kwa Abuu Khuzaymah Al-Answaariyy (رضي الله عنه), na haikupatikana kutoka kwa mtu mwengine yeyote. (Aayah zenyewe ni):
لَقَدْ جَاءَكُمْ رَسُولٌ مِّنْ أَنفُسِكُمْ
“Kwa yakini amekujieni Rasuli anayetokana na nyinyi wenyewe.”
mpaka mwisho wa Suwrah [At-Tawbah (9:128-129) – Hadiyth Ameipokea Imaam Al-Bukhaariy]
010-Yuwnus: Utangulizi Wa Suwrah
Alhidaaya.com [2]
Imeteremka: Makkah kwa itifaki ya ‘Ulamaa.
Idadi Za Aayah: 109
Jina La Suwrah: Yuwnus
Suwrah imeitwa Yuwnus, na inayodalilisha ni kutajwa katika Aayah namba (98) kuhusu kaumu ya Nabiy Yuwnus (عليه السّلام) kwamba ni kaumu pekee ambao waliamini na wakatubia kabla ya kuteremshiwa adhabu.
Miongoni Mwa Makusudio Ya Suwrah:
1-Kuuthibitisha Unabii (na Risala ya) Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم) kwa dalili, na kuwalingania wanaopinga ili waamini, pamoja na kuwatishia (uwepo wa) adhabu. [Al-Mukhtaswar Fiy Tafsiyr Al-Qur-aan Al-Kariym]
2-Kuiweka misingi ya ‘Aqiydah, na kuithibitisha Tawhiyd na Risalah pamoja na kuwakumbusha watu walioghafilika na Aayaat (Ishara, Dalili) za Allaah, kwamba marejeo yao kwa Rabb wao kwa kufufuliwa, kuhesabiwa matendo na malipo yake.
3-Kuwakumbusha viumbe watafakari Tawhiyd ya Allaah ya Ar-Rubuwbiyyah (Uumbaji wa viumbe, Uendeshaji ulimwengu, Utoaji rizki, Uumbaji wa mbingu na ardhi na yaliyomo ndani yake), na hikma Zake.
4-Kulengea katika kuusalimisha moyo kutokana na uthibitisho kwamba Qur-aan ni mawaidha, shifaa (poza, tiba), hidaaya na rehma.
5-Kuradd shubha za washirikina kwa dalili na hoja za wazi.
Miongoni Mwa Maudhui Ya Suwrah:
1-Suwrah imefunguliwa kwa herufi zinazojulikana kama الحروف المقطعة (Al-Huruwf Al-Muqatw-twa’ah), ambazo hakuna ajuaye maana zake isipokuwa Allaah (سبحانه وتعالى). Rejea Al-Baqarah (2:1). Kisha imethibitishwa Risalah ya Nabiy Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم) kutoka kwa Allaah.
2-Imethibitishwa Tawhiyd ya Allaah ya Al-Uluwhiyyah kwamba Yeye Ni Mmoja Pekee na Ndiye Anayepasa kuabudiwa.
3-Imethibitishwa kukusanywa viumbe vyote Siku ya Qiyaamah na jazaa (malipo), na kuna ukumbusho wa kwamba marejeo ya mwisho ya viumbe ni kwake Allaah (سبحانه وتعالى). Na pia wanaadam wamegawanyika makundi mawili; Waumini na makafiri.
4-Imetajwa wazi itikadi za washirikina, na ile misimamo yao kuhusu Qur-aan, pamoja na kutajwa shubha zao na kuziraddi, na kuthibitishwa kuwa Qur-aan ni Kitabu cha Allaah.
5-Zimetajwa baadhi ya adhabu na maangmizi za watu wa nyumati zilizopita, baada ya kumshirikisha Allaah na kuwapinga Rusuli.
6-Imetajwa mazingatio juu ya uwezo Aliouweka Allaaah kwa wanaadam wa kuweza kutembea bara na baharini.
7-Imetolewa mifano ya wazi ya mapambo na starehe za dunia, na kukumbushwa kwamba dunia itaondoka haraka sana.
8-Imetajwa utofauti ya hali za Waumini na makafiri kesho Aakhirah, na kubatwilika kwa viabudiwa vya washirikina.
9-Imethibitishwa kwamba Qur-aan imeteremshwa kutoka kwa Allaah (سبحانه وتعالى), na dalili ya kuwa madai ya wanayoipinga ni uzushi wa wazi, na washirikina wameshindwa kuleta japo Suwrah moja mfano wake.
10-Imethibitishwa kuwa Ilimu ya Allaah imeenea kote na kwa viumbe wote, na kutaja athari za Uwezo wa Allaah (سبحانه وتعالى) uliokuwa wazi.
11-Imewabashiria Vipenzi wa Allaah (سبحانه وتعالى) hapa duniani na Aakhirah.
12-Kuna maamrisho ya kutakiwa kudhihirisha furaha kwa Uislamu na Qur-aan.
13-Kumliwazwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) kwa kutajwa kisa cha Nabiy Nuwh na Nabiy Muwsaa (عليهما السّلام) na kisa cha Bani Israaiyl na watu wa Firawni.
14-Imetajwa kuokoka kwa watu wa Nabiy Yuwnus (عليه السّلام) kwa kuamini kwao, na kutubia kwao, na kwamba kaumu ya Nabiy Yuwnus (عليه السّلام) ni kaumu pekee iliyoamini kabla ya kuteremshiwa adhabu.
15-Ameamrishwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) aelekee katika Dini ya haki ya Allaah, na onyo la kutokumshirikisha Allaah.
15-Imethibitshwa kwamba dhara yoyote ile inayomsibu mtu, hakuna wa kuiondosha isipokuwa Allaah (سبحانه وتعالى). Na kwamba Allaah Akimtakia mtu kheri, basi hakuna wa kuizuia.
16-Suwrah imekhitimishwa kwa kumliwaza Nabiy Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم) avute subira mpaka Allaah (سبحانه وتعالى) Ateremshe Hukmu Yake.
011-Huwd: Utangulizi Wa Suwrah
Alhidaaya.com [2]
Imeteremka: Makkah kwa itifaki ya ‘Ulamaa.
Idadi Za Aayah: 123
Jina La Suwrah: Huwd
Suwrah imeitwa Huwd, na inayodalilisha ni kutajwa katika Hadiyth iliyonukuliwa chini kwenye Faida. Na imeitwa Huwd kutokana na kisa cha Nabiy Huwd (عليه السّلام) kwa kaumu yake ya ‘Aad ingawa pia kisa chake kimetajwa katika Suwrah nyenginezo. Rejea Aayah (50-60).
Miongoni Mwa Makusudio Ya Suwrah:
1-Kumpa thabati Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) (na kumliwaza) pamoja na Waumini kwa visa vya waliotangulia, na makemeo makali kwa wenye kukadhibisha. [Al-Mukhtaswar Fiy Tafsiyr Al-Qur-aan Al-Kariym]
2-Uthibitisho wa daawah ya Nabiy Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم) pamoja na kuthibitisha misingi ya imaan ya Kiislam ya Tawhiyd ya Allaah.
3-Kubashiria na kuonya shirki na maovu, na kukumbushwa viumbe malipo ya mema na maovu Siku ya Qiyaamah.
4-Kubainishwa Desturi ya Allaah (سبحانه وتعالى) kuwaadhibu na kuwaangamiza makafiri wa nyumati zilizopita, na kutajwa sababu za dhulma kwamba, wengi wao walifuata starehe na matamanio yaliyopelekea kwenye uasherati, dhulma, ubadhirifu, ufisadi na kuwafanyia dhihaka Rusuli wa Allaah.
5-Kumthitibisha Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) pamoja na Waumini wabakie imara katika Dini kwa kutolewa kisa cha Nabiy Nuwh (عليه السّلام), kwamba mapenzi yake kwa mwanawe ni tabia ya kibinaadam, na kwamba kuna mipaka ya sharia katika haki za baina ya mzazi na mwana katika kumuasi Allaah (سبحانه وتعالى).
Miongoni Mwa Maudhui Ya Suwrah:
1-Suwrah imefunguliwa kwa herufi zinazojulikana kama الحروف المقطعة (Al-Huruwf Al-Muqatw-twa’ah), ambazo hakuna ajuaye maana zake isipokuwa Allaah (سبحانه وتعالى). Rejea Al-Baqarah (2:1). Kisha imebainishwa kwamba Qur-aan ni Aayah zilizofasiliwa waziwazi kutoka kwa Allaah (سبحانه وتعالى), ikafuatilia kutaja fadhila za Istighfaar. Rejea Aayah namba (3).
2-Imebainishwa kwamba, Allaah (سبحانه وتعالى) Anazitambua siri za viumbe wote na kwamba Allaah (سبحانه وتعالى) Anadhamini rizki zote za viumbe.
3-Imethibitishwa kufufuliwa na jazaa (malipo) ya mema na maovu.
4-Imebainishwa hali za watu katika shida na raha.
5-Imemthibitisha Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) na kumliwaza juu ya maudhi ya watu wake; washirikina wa Makkah.
6-Imebainishwa makundi ya makafiri na Waumini, na kuyapigia mifano.
7-Vimetajwa sehemu ya visa vya Manabii, na kuchambua baadhi ya matukio yao, na yale yaliyojiri pamoja na watu wao, kama vile kisa cha Nuwh, Huwd, Swaalih, Ibraahiym, Luutw, Shu’ayb na Muwsaa (عليهم السّلام).
8-Kuna muongozo juu ya yale yanayoweza kumfanya mtu aishi maisha mazuri, kama vile kuthibitika katika Dini, na kutojiegemeza kwa watu wa dhulma, na kusimamisha Swalaah.
9-Imebainishwa faida ya visa vya Manabii na kuwataja watoto wao kama Nabiy Nuwh (عليه السّلام) na mwanawe aliyegharikishwa. Faida kama hii, ni kwa ajili ya kuuthibitisha moyo wa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) na Waumini wanapokuwa na watu wenye uhusiaono wa damu, wanaomuasi Allaah (سبحانه وتعالى).
10-Suwrah imekhitimishwa kwa kutoa amri ya kuwataka watu watawakkal kwa Allaah kwa kila hali na kwamba Allaah (سبحانه وتعالى) Haghafiliki na matendo yoyote yale; mema au maovu.
Faida:
عَنْ عُقْبَةَ بْنِ عَامِرٍ، قَالَ اتَّبَعْتُ رَسُولَ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم وَهُوَ رَاكِبٌ فَوَضَعْتُ يَدِي عَلَى قَدَمِهِ فَقُلْتُ أَقْرِئْنِي يَا رَسُولَ اللَّهِ سُورَةَ هُودٍ وَسُورَةَ يُوسُفَ . فَقَالَ " لَنْ تَقْرَأَ شَيْئًا أَبْلَغَ عِنْدَ اللَّهِ مِنْ
قُلْ أَعُوذُ بِرَبِّ الْفَلَق وَ قُلْ أَعُوذُ بِرَبِّ النَّاسِ .
Amesimulia ‘Uqbah Bin ‘Aamir (رضي الله عنه): Nilikwenda kwa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akiwa amepanda kipando, nikaweka mkono wangu juu ya mguu wake, nikasema: Nifundishe Suwrah ya Huwd, nifundishe Suwrah ya Yuwsuf. Akasema: "Hutasoma kitu chochote chenye timilifu zaidi (katika kinga) mbele ya Allaah: (Soma):
قُلْ أَعُوذُ بِرَبِّ الْفَلَقِ ﴿١﴾
“Sema: Najikinga na Rabb wa mapambazuko.” [Al-Falaq (113)]
Na
قُلْ أَعُوذُ بِرَبِّ النَّاسِ ﴿١﴾
“Sema: Najikinga na Rabb wa watu.” [An-Naas (114)]
[Hadiyth katika Sunan An-Nasaaiy, Ahmad, Ibn Hibbaan, ameisahihisha Imaam Al-Albaaniy katika Swahiyh An-Nsaaiy (5454)]
012-Yuwsuf: Utangulizi Wa Suwrah
Alhidaaya.com [2]
Imeteremka: Makkah kwa itifaki ya ‘Ulamaa.
Idadi Za Aayah: 111
Jina La Suwrah: Yuwsuf:
Suwrah imeitwa Yuwsuf, na inayodalilisha ni kutajwa kwake Nabiy Yuwsuf (عليه السّلام) mara kadhaa katika Suwrah. Na pia kutajwa katika Hadiyth iliyonukuliwa katika Fadhila na Faida.
Miongoni Mwa Makusudio Ya Suwrah:
1-Mazingatio kwa upole, wa mipangilio ya Allaah (سبحانه وتعالى) kwa vipenzi vyake, na kuwapa utulivu wao, na kuwapa mwisho mwema. [Al-Mukhtaswar Fiy Tafsiyr Al-Qur-aan Al-Kariym]
2-Kumpa kiliwazo Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) na Swahaba wake na kuwapa utulivu katika nafsi zao.
3-Bainisho kwamba njozi njema anayoiona Muumini usingizini ni ya haki, na bainisho kwamba Allaah (سبحانه وتعالى) Hupindua njama za madhalimu, na kwamba Matakwa Yake yanahakiki, na bainisho la Miujiza Yake Allaah (سبحانه وتعالى) katika njia ya kuelezea visa.
4-Kuashiria hadhi, heshima na kujisitiri kwa kujiepusha na machafu, na kumcha Allaah kuingia katika makosa yanayomghadhibisha.
5-Kuthibitisha Tawhiyd ya Allaah; Muumba Mmoja na kwamba Yeye Ni Pekee Anayepasa kuabudiwa kwa haki.
6-Kubainisha kuwa mwisho mwema ni kwa wamchao Allaah, wenye kuvuta subra juu ya mitihani.
Miongoni Mwa Maudhui Ya Suwrah:
1-Suwrah imefunguliwa kwa herufi zinazojulikana kama الحروف المقطعة (Al-Huruwf Al-Muqatw-twa’ah), ambazo hakuna ajuaye maana zake isipokuwa Allaah (سبحانه وتعالى). Rejea Al-Baqarah (2:1). Kisha imetajwa utukufu na sifa ya Qur-aan ya lugha ya Kiarabu na kuanza usimulizi wa kisa cha Nabiy Yuwsuf (عليه السّلام).
2-Ikatajwa kuhusu njozi ya Yuwsuf (عليه السلام), hila za ndugu zake na husda na chuki zao kwake, na makubaliano yao na mpango wa kutaka kumuua.
3-Imeelezea msafara ulioweza kumtoa Nabiy Yuwsuf (عليه السّلام) kisimani, kisha kuuzwa kwake akafika katika nyumba ya al-aziyz (waziri au mfalme wa Misri) na mitihani aliyoipata ya kutongozwa na mke wake kwenye qasri lake na jinsi habari zilivyoenea.
4-Imeelezewa tukio la Yuwsuf (عليه السّلام) kuingia gerezani baada ya kuonekana kuwa hana hatia, na daawah (ulinganiaji) aliyofanya huko.
5-Imeelezewa ndoto aliyoiota mfalme na jinsi Nabiy Yuwsuf (عليه السّلام) alivyoifasiri, na kule kuonekana kuwa Nabiy Yuwsuf (عليه السّلام) hakuwa na kosa hali iliyopelekea yeye kutoka gerezani.
6-Maelezo ya Nabiy Yuwsuf (عليه السّلام) kukutana na ndugu zake Misri bila wao kumtambua, na kuwataka warudi tena safari ya kufika Misri, pamoja na ndugu yao ambaye ni ndugu shakiki wa Yuwsuf (عليه السّلام). Kisha pale alipomzuia nduguye shakiki, kwa mbinu aliyoipanga kutokana na ilhaam aliyofunuliwa na Allaah (سبحانه وتعالى). Na huzuni ya baba yao baada ya tukio hilo.
7-Maelezo ya Yuwsuf (عليه السّلام) alipokutana na ndugu zake kwa mara ya pili, na kule kujitambulisha kwa ndugu zake, na kuwakumbusha juu ya hila walizomfanyia kutaka kumuua, na kwamba yeye amewasamehe. Kisha alipowaagiza kurudi kwa baba yao wakiwa na kanzu yake ili wafikapo, waitupie usoni mwa baba yao, nae akarudi kuona baada ya kupofuka.
8-Imeelezea kuhudhuria kwao nyumbani kwa Yuwsuf baada ya matukio hayo, wakiwa na baba yao, na takrima aliyoifanya Yuwsuf juu yao juu ya kuwa nduguze walimfanyia uadui, lakini kwa kuwa Nabiy Yuwsuf (عليه السّلام) alikuwa ni mwenye subra, mwenye moyo wa kusamehe, mwema na mwenye ihsaan alimnasibisha shaytwaan kuwa ndiye aliyewachochea nduguze kumfanyia uadui.
9-Duaa ya Nabiy Yuwsuf (عليه السّلام) ya kuomba kufishwa na Waislamu na kukutanishwa na Swalihina.
10-Baada ya kisa cha Nabiy Yuwsuf (عليه السّلام), Allaah (سبحانه وتعالى) Anamliwaza Rasuli Wake (صلى الله عليه وآله وسلم) kuwa si watu wengi watakaoamini japo kama atapania na kutilia hima kuwalingania. Hivyo basi, watu wake; washirikina wa Makkah, wataendelea shirki zao, naye asijali kwani adhabu itawafikia tu ya duniani na Qiyaamah kitawasimamia.
11-Amrisho na ukumbusho wa kulingania Dini juu ya nuru za ilimu na utambuzi.
12-Allaah (سبحانه وتعالى) Anaendelea kumliwaza Rasuli Wake Allaah (سبحانه وتعالى) kwa kuwaambia washirikina kwanini wasiende kutembea katika ardhi wajionee jinsi gani hatima ilikuwa ya madhalimu wa awali? Na kwamba hatima yao ilikuwa ni kuangamizwa! Ama Rusuli Wake, Aliwateremshia Nusra Yake Akawaokoa na madhalimu.
13-Suwrah imekhitimishwa kwa ukumbusho kwamba, katika visa vya Rusuli, kuna mazingatio (na mafunzo) kwa wenye akili. Na kwamba Qur-aan haikuwa hadithi zinazotungwa, lakini ni sadikisho la (Vitabu) vya kabla yake na tafsili ya waziwazi ya kila kitu, na ni mwongozo na rehma kwa watu wanaoamini.
Fadhila Za Suwrah:
1-Suwrah Yuwsuf ni Suwrah pekee ambayo imeelezea kwa urefu kisa kamilifu cha Nabiy Yuwsuf (عليه السلام). Hakijatajwa kisa cha Nabiy yeyote katika Qur-aan kwa urefu kama kilivyotajwa kisa hiki cha Nabiy Yuwsuf (عليه السلام) kwenye Suwrah hii. Na Jina la Yuwsuf limetajwa kwa wingi katika Suwrah hii, na limetajwa mara moja tu katika Suwrah Al-An’aam (7:84) na katika Ghaafir (40:34) bila ya maelezo bayana.
2-Rejea Suwrah Yuwsuf (12:4) kupata fadhila za Nabiy huyu mtukufu na kujaaliwa kwake nusu ya ujamali wa dunia.
Faida:
عَنْ عَبْدِ اللَّهِ، قَالَ كُنْتُ بِحِمْصَ فَقَالَ لِي بَعْضُ الْقَوْمِ اقْرَأْ عَلَيْنَا . فَقَرَأْتُ عَلَيْهِمْ سُورَةَ يُوسُفَ - قَالَ - فَقَالَ رَجُلٌ مِنَ الْقَوْمِ وَاللَّهِ مَا هَكَذَا أُنْزِلَتْ . قَالَ قُلْتُ وَيْحَكَ وَاللَّهِ لَقَدْ قَرَأْتُهَا عَلَى رَسُولِ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم فَقَالَ لِي " أَحْسَنْتَ " . فَبَيْنَمَا أَنَا أُكَلِّمُهُ إِذْ وَجَدْتُ مِنْهُ رِيحَ الْخَمْرِ قَالَ فَقُلْتُ أَتَشْرَبُ الْخَمْرَ وَتُكَذِّبُ بِالْكِتَابِ لاَ تَبْرَحُ حَتَّى أَجْلِدَكَ - قَالَ - فَجَلَدْتُهُ الْحَدَّ .
Amesimulia ‘Abdullaah (Bin Mas’uwd) (رضي الله عنه): Nilipokuwa Hims, baadhi ya watu walinitaka niwasomee Qur-aan. Nikawasomea Suwrah Yuwsuf. Mtu mmoja kati yao akasema: Wa-Allaahi! Hivyo sivyo ilivyoteremshwa! Nikamwambia: Ole wako! Wa-Allaahi! Nilimsomea Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akaniambia “Umeisoma vizuri.” Nikawa naongea naye (huyo mtu) nikasikia harufu ya pombe kutoka kwake. Nikamwambia: Je unakunywa pombe na unakadhibisha Kitabu (cha Allaah?). Hutoondoka mpaka nikupige mijeledi! Basi nikampiga mijeledi kwa mujibu wa adhabu ya Sharia (ya uasi wa kunywa pombe) [Muslim]
013-Ar-Ra’d: Utangulizi Wa Suwrah
Alhidaaya.com [2]
Imeteremka: Makkah au Madiynah kwani ‘Ulamaa wamekhitilafiana kuhusu wapi imeteremshwa. Rejea Faida.
Idadi Za Aayah: 43
Jina La Suwrah: Ar-Ra’d
Suwrah imeitwa Ar-Ra’d (Radi), na inayodalilisha ni kutajwa katika Aayah namba (13) kuwa radi inamsabihi (Allaah) na kumhimidi, na Malaika pia (wanamsabihi) kwa sababu ya kumkhofu Allaah (سبحانه وتعالى).
Miongoni Mwa Makusudio Ya Suwrah:
1-Kuwaraddi wanaopinga Wahy na Unabii kwa kuwabainishia mambo yanayoonyesha Uadhimu wa Allaah (سبحانه وتعالى). [Al-Mukhtaswar Fiy Tafsiyr Al-Qur-aan Al-Kariym]
2-Suwrah inathibitisha nguzo tatu za ‘Aqiydah katika nyoyo za Waumini; Allaah (Mtumaji Risala), Rasuli (Mfikishaji Risala kwa watu) na Risala yenyewe (Qur-aan).
3-Suwrah inatoa hoja mbali mbali kwa makafiri kwa dalili na ushahidi wa wazi kabisa za Tawhiyd ya Allaah (سبحانه وتعالى) na uumbaji wa ulimwengu na viliomo. Na ikatoa baadhi ya dalili kwa mifano kadhaa.
4-Kubainisha haki na baatwil; kwamba haki imeimarika na yenye nguvu hata ikifichwa. Na baatwil ni dhaifu haina nguvu wala thamani hata kama ikidhihirika kwa wingi ikatanda na kuenea. Basi baatwil itatoweka tu na haki itahakiki na kuthibitika.
Miongoni Mwa Maudhui Ya Suwrah:
1-Suwrah imefunguliwa kwa herufi zinazojulikana kama الحروف المقطعة (Al-Huruwf Al-Muqatw-twa’ah), ambazo hakuna ajuaye maana zake isipokuwa Allaah (سبحانه وتعالى). Rejea Al-Baqarah (2:1). Kisha imethibitishwa ya kwamba Qur-aan ni ya kweli na imetoka kwa Allaah (سبحانه وتعالى) lakini watu wengi hawaiamini.
2-Zimetajwa dalili za wazi kudhihirisha Tawhiyd ya Allaah (سبحانه وتعالى) na Qudra Yake; kuumba mbingu na ardhi, jua na mwezi, usiku na mchana, Mwenye kujaalia mazao ya aina mbali mbali yanayonyeshewa kwa maji ya aina moja tu! Rejea Aayah namba (4) ya Suwrah hii kwenye maelezo bayana. Na kwamba Yeye Allaah (سبحانه وتعالى) ni Muumbaji Pekee wa kila kitu, na Mwenye Kuhuisha na Kufisha na Mweza kwa kuleta manufaa na madhara.
3-Imeelezea yanayohusu kauli za washirikina yanayoungamana na kufufuliwa, pamoja na kuwaraddi.
4-Imebainishwa ukamilifu wa Ilimu ya Allaah (سبحانه وتعالى) na kwamba Yeye (سبحانه وتعالى) ni Mjuzi wa kila kitu, ya dhahiri na ya siri.
5-Imethibitishwa kwamba Allaah (سبحانه وتعالى) Ndiye Anayestahiki kuabudiwa na kuombwa duaa. Na kwamba waabudiwa wa washirikina na duaa zao kwao haziwafai chochote kwani waabudiwa hao hawawaitikii chochote.
6-Imepigwa mifano miwili ya haki na baatwil, na kuweka mafungamano kati ya mwisho wa wafuasi wa haki na wafuasi wa baatwili, pamoja na sifa zao.
7-Kuna amri ya kutimiza ahadi, kuunga ambayo Ameyaamrisha Allaah (سبحانه وتعالى), kumkhofu Rabb, kuogopa malipo mabaya, kuvuta subra kwa kutaka Wajihi wa Allaah, kusimamisha Swalaah, kutoa mali kwa siri na dhahiri, kulipiza mema baada ya uovu. Basi jazaa yake ni Jannah (Pepo) na maamkizi ya Salaam kutoka kwa Malaika. Na katazo la kuvunja ahadi na kutokuunga ambayo Ameyaamrisha Allaah (سبحانه وتعالى) na kufanya ufisadi katika ardhi. Basi jazaa yake ni laana ya Allaah (سبحانه وتعالى) na makazi mabaya Aakhirah. Rejea Aayah (21-25) na faida zake.
8-Imeelezea baadhi ya rai za makafiri na matakwa yao ya kiburi na fitnah, na kuwaraddi.
9-Imebainishwa mwisho mwema kwa wenye taqwa, na mwisho mbaya kwa wanaomkadhibisha Allaah (سبحانه وتعالى).
10-Suwrah imekhitimishwa kwa kumliwaza Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) kutokana na kukanushwa kwake na watu wake; washirikina wa Makkah. Basi Allaah (سبحانه وتعالى) Anamthibitishia kwamba Yeye Anamtosheleza kuwa Shahidi wake juu ya urongo wao, na ushahidi wa wenye ilimu ya Kitabu miongoni mwa Mayahudi na Manaswara walioamini Unabii wake, wakatoa ushahidi bila kuuficha.
Faida:
1-‘Ulamaa wamekhitalifiana kuhusu wapi kuteremka kwake. Wapo wanaosema imeteremka Makkah kutokana na maudhui na sifa za Suwrah zilizoteremshwa Makkah ambazo zinataja shirki, makafiri kutokuamini kufufuliwa, kukadhibisha Risala ya Allaah na jazaa zao motoni. Na baadhi ya ‘Ulamaa wamesema imeteremka Madiynah.
2-Ni Suwrah mojawapo inayotaja dalili za Tawhiyd ya Allaah (سبحانه وتعالى) kwa kina zaidi.
3-Imetajwa Jina la Suwrah (Radi) kuwa inamsabihi (Allaah) na kumhimidi na Malaika pia (wanamsabihi) kwa sababu ya kumkhofu. Na kusoma duaa mtu anaposikia radi nayo ni:
سُبْـحانَ الّذي يُسَبِّـحُ الـرَّعْدُ بِحَمْـدِهِ، وَالملائِكـةُ مِنْ خيـفَته.
Rejea Suwrah Ar-Ra’d (13:13)
014-Ibraahiym: Utangulizi Wa Suwrah
Alhidaaya.com [2]
Imeteremka: Makkah kwa itifaki ya ‘Ulamaa.
Idadi Za Aayah: 52
Jina La Suwrah: Ibraahiym
Suwrah imeitwa Ibraahiym, na inayodalilisha ni kutajwa kisa chake Nabiy Ibraahiym (عليه السّلام) katika Aayah namba Aayah (35-41). Rejea Faida.
Miongoni Mwa Makusudio Ya Suwrah:
1-Kuthibitisha usimamizi wa Rusuli juu ya kubainisha na kubalighisha (daawah) na kuwatishia adhabu wanaopuuza kuwafuata na kuwakadhibisha. [Al-Mukhtaswar Fiy Tafsiyr Al-Qur-aan Al-Kariym]
2-Kuthibitisha kwamba Qur-aan ni Kitabu kinachoongoza katika njia iliyonyooka, kwa kumtoa mtu kutoka katika viza na kumuingiza katika nuru.
3-Bainisho kwamba Rusuli wote wametumwa kuthibitisha Tawhiyd ya Allaah.
4-Kubainisha udanganyifu na ukhaini wa shaytwaan kwa mwanaadam, kwamba Siku ya Qiyaamah, atawakanusha aliowapotosha.
5-Allaah (سبحانه وتعالى) Kuwathibitisha Waja Wake Waumini duniani na Aakhira kwa al-qawl ath-thaabit (kauli thabiti). Ama madhalimu, wao Allaah (سبحانه وتعالى) Anawapotosha kwa sababu ya kujiepusha kwao na mawaidha Yake, kwa kufuata matamanio yao, na kutajwa adhabu zao Aakhirah.
6-Kukumbusha Neema za Allaah (سبحانه وتعالى) kwa waja, na kuwahimiza juu ya kushukuru kwa neema hizo, na tahadhari ya kuzipinga neema na kuzikufuru.
Miongoni Mwa Maudhui Ya Suwrah:
1-Suwrah imefunguliwa kwa herufi zinazojulikana kama الحروف المقطعة (Al-Huruwf Al-Muqatw-twa’ah), ambazo hakuna ajuaye maana zake isipokuwa Allaah (سبحانه وتعالى). Rejea Al-Baqarah (2:1). Kisha imethibitishwa kwamba Qur-aan ni Kitabu cha hidaaya na ubainifu, na kwamba kinaongoza na kuwahidi watu kutoka katika viza na kuingia katika nuru. Na imebainishwa Ufalme wa Allaah (سبحانه وتعالى) wa mbingu na ardhi. Na kwamba Allaah (سبحانه وتعالى) Amewatuma Rusuli kwa lugha za watu wake ili waifahamu Risala Yake.
2-Kimesimuliwa sehemu ya kisa cha Muwsaa (عليه السلام), na neema za Allaah kwa watu wake pale Alipowaokoa kutokana na Firawni. Na kutajwa kwa khabari za baadhi ya Rusuli pamoja na watu wao waliowapinga Risala ya ya Allaah na malipo yao ya adhabu kwa kuwakadhibisha Rusuli wa Allaah.
3-Kuna mahojiano kati ya watu wa motoni; wadhaifu na wale waliofanya kiburi. Na mjadala wa shaytwaan na watu aliowapotosha huko motoni, na kwamba shaytwaan huko Aakhirah, anakana udanganyifu wake na ahadi zake kwa watu waliomfuata.
4-Imetajwa hali za watu wa Jannah na neema za milele.
5-Umepigwa mfano na Allaah (سبحانه وتعالى) wa neno zuri la Tawhiyd, kuwa ni kama mti mzuri. Neno hilo linamaanisha kushuhudia kwamba:
لاَ إِلَه إِلاَّ اللَّه وَأَنَّ مُحَمَّدًا رَسُول اللَّه
Hapana mwabudiwa wa haki isipokuwa Allaah na Muhammad ni Rasuli Wake.
Rejea Aayah namba (14-15) kwenye maelezo bayana kuwa mti huo ni kama mtende. Kisha Allaah (سبحانه وتعالى) Anapiga mfano wa neno baya kuwa ni sawa na mti mbaya. Kisha Allaah (سبحانه وتعالى) Anatofautisha baina ya hayo mawili kwamba: Anawathibitisha wale walioamini kwa al-qawl ath-thaabit katika uhai wa dunia na Aakhirah, na kinyume chake, Anawaacha madhalimu wapotoke. Rejea Aayah namba (27) kwenye maelezo kuhusu maana ya kauli hii inayohusiana na maswali matatu atakayoulizwa mtu kaburini.
6-Suwrah imetaja hali za makafiri ambao walizibadilisha neema za Allaah (سبحانه وتعالى) na kuzikufuru.
7-Suwrah imetaja pia baadhi ya neema za Allaah za Uumbaji wa ulimwengu na viliomo Akamalizia kusema kuwa Neema Zake haziwezi kuorodheshwa katika hesabu. Rejea Aayah namba (34) kwenye uchambuzi wa Neema za Allaah (سبحانه وتعالى).
8-Kuna khabari za Nabiy ya Ibraahiym (عليه السلام) na kumwabudu kwake Allaah (سبحانه وتعالى). Na khofu ya dhuria wake kuabudu masanamu. Na kuwaacha dhuria wake katika bonde la Makkah akiwaombea wao na watu rizki na nyoyo zao zielekee kupenda kufika na kuweko huko. Pia shukurani zake kwa Allaah (سبحانه وتعالى) kumjaalia wana wawili Ismaa’iyl na Is-haaq. Kisha duaa zake kujiombea mwenyewe na dhuria wake kusimamisha Swalaah na kuwaombea Waumini maghfirah. Rejea Aayah namba (41).
9-Suwrah imekhitimishwa kwa Aayah zinazotaja hali za makafiri na madhalimu zitakavyokuwa Siku ya Qiyaamah na aina za adhabu zao.
Faida:
Baadhi ya kisa cha Nabiy Ibraahiym (عليه السّلام) kimetajwa katika Suwrah hii pindi alipokuwa Makkah na ahli zake; mkewe Haajar na mwanawe Ismaa’iyl, na kutajwa shukurani zake kwa Allaah (سبحانه وتعالى) kumruzuku wana wawili ambao ni Ismaa’iyl na Is-haaq, na duaa alizoomba. Rejea tanbihi za Aayah namba (35) na (41).
015-Al-Hijr: Utangulizi Wa Suwrah
Alhidaaya.com [2]
Imeteremka: Makkah kwa itifaki ya ‘Ulamaa.
Idadi Za Aayah: 99
Jina La Suwrah: Al-Hijr.
Suwrah imeitwa Al-Hijr (Eneo lilioko baina ya Sham na Hijaaz), na inayodalilisha ni kutajwa watu wa Al-Hijr katika Aayah namba (80). Hawa ni kina Thamuwd ambao walitumiwa Nabiy Swaalih (عليه السّلام) kuwalingania Tawhiyd ya Allaah.
Miongoni Mwa Makusudio Ya Suwrah:
1-Kuwaahidi adhabu wale wote wanaoifanyia istihzai Qur-aan. Ahadi ya Allaah juu ya kuihifadhi Qur-aan, kwa kumuunga mkono Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) na kumthibitisha. [Al-Mukhtaswar Fiy Tafsiyr Al-Qur-aan Al-Kariym]
2-Kuthibitisha Uadhama wa Qur-aan kuwa ni Kitabu kinachobainisha na kuongoza katika njia ilyonyooka, na thibitisho la kuhifadhika kutokana na kubadilishwa.
3-Kuthibitisha Tawhiyd ya Allaah na kubainisha Uwezo Wake Allaah (سبحانه وتعالى) kwa kusimamisha hoja dhidi ya makafiri kwa kueleza Aayaat (Ishara, Dalili) za mbinguni na ardhini. Pia Uwezo Wake Allaah (سبحانه وتعالى) wa Kuhuisha na Kufisha na kuthibitishwa kukusanywa kwa ajili ya kuhesabiwa matendo na malipo yao ya adhabu.
4-Bainisho kwamba asili ya mwanaadam ni kutokana na udongo. Na bainisho kuhusu ushawishi na uchochezi wa shaytwaan kwa mwanaadam.
5-Bainisho kwamba mauti na uhai yako Mikononi mwa Allaah Pekee.
6-Kumliwaza Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) na kumthibitisha pamoja na Waumini.
Miongoni Mwa Maudhui Ya Suwrah:
1-Suwrah imefunguliwa kwa herufi zinazojulikana kama الحروف المقطعة (Al-Huruwf Al-Muqatw-twa’ah), ambazo hakuna ajuaye maana zake isipokuwa Allaah (سبحانه وتعالى). Rejea Al-Baqarah (2:1). Kisha imewaonya washirikina kuhusu kumzulia kwao Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) kuwa ni majnuni (mwendawazimu) kwa sababu hakuwaletea Malaika wa kumsaidia na kuwapa khabari za Allaah (سبحانه وتعالى), ilhali Malaika hawashuki ila kwa hikma na amri ya Allaah (سبحانه وتعالى).
2-Suwrah imewatahadharisha washirikina kwamba, watajutia matendo yao maovu ya kujishughulisha kwao na maisha ya dunia na kuzama kwao humo, na kutokusilimu kwao.
3-Suwrah imethibitisha kuwa Allaah (سبحانه وتعالى) Ameteremsha Qur-aan na Ameahidi kuihifadhi kutokana na kubadilishwa au kupotoshwa Aayah zake.
4-Imebainishwa kwamba wale wanaomkadhibisha Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم), wanamkadhibisha kwa inda, inadi na ukafiri tu, wala si kwa kukosa dalili zinazoonyesha ukweli wake (صلى الله عليه وآله وسلم).
5-Makafiri wamesimamishiwa hoja kwa kuelezea ishara za ulimwengu zinazoashiria Tawhiyd ya Allaah (سبحانه وتعالى) na Uadhimu Wake, na Qudra Yake ya Uumbaji wa mbingu na ardhi na kujaalia nyota mbinguni, na kuhifadhi vilivyomo mbinguni kwa kuwarushia vimondo mashaytwaan, na kuthibitishwa milima ardhini, na kurahisisha njia ardhini, na kujaaliwa rizki kwa kupeleka pepo za rehma zinazorutubisha na kuteremsha maji ya kumwagilia na kuihuisha ardhi, na kwamba Allaah (سبحانه وتعالى) Ndiye Anayehuisha na Kufisha na watakusanywa makafiri hao Siku ya Qiyaamah kuadhibiwa.
6-Ukumbusho kwamba kuumbwa kwa mwanaadam ni kutokana na udongo mkavu. Na ndivyo alivyoumbwa Aadam (عليه السّلام), na kuamrishwa Malaika kumsujudia Aadam (عليه السّلام), na kuelezea kiburi cha Ibliys kukataa kumsujudia na kufukuzwa kwake Peponi.
7-Kumetajwa baadhi ya maelezo ya visa vya Rusuli wa Allaah, kama vile: Ibraahiym, Luutw, Shu’ayb na Swaalih (عليهم السلام).
8-Suwrah imewatahadharisha makafiri na moto wa Jahannam na adhabu kali za Allaah (سبحانه وتعالى), na kuwabashiria Waumini Jannah na Rehma za Allaah.
9-Suwrah imekhitimishwa kwa Amri ya Allaah (سبحانه وتعالى) kwa Rasuli Wake (صلى الله عليه وآله وسلم) kushikamana na kuendelea kubalighisha Risala Yake, wala asijali kukengeushwa na washirikina na istihzai zao, na kumliwaza Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) kwamba Yeye Allaah (سبحانه وتعالى) Anatosheleza dhidi ya istihzai zao. Kisha ikamalizikia kwa amrisho la kuendelea kumwabudu Allaah (سبحانه وتعالى) mpaka itakapomfikia yakini (mauti).
016-An-Nahl: Utangulizi Wa Suwrah
Alhidaaya.com [2]
Imeteremka: Makkah kwa itifaki ya ‘Ulamaa.
Idadi Za Aayah: 128
Jina La Suwrah: An-Nahl
Suwrah imeitwa An-Nahl (Nyuki), na inayodalilisha ni kutajwa katika Aayah namba (68).
Miongoni Mwa Makusudio Ya Suwrah:
1-Ukumbusho juu ya neema unaoonyesha (Uadhimu wa) Mwenye kuneemesha. [Al-Mukhtaswar Fiy Tafsiyr Al-Qur-aan Al-Kariym]
2-Kuwaraddi washirikina, kuwakemea shirki zao na kuwaonya.
3-Kusimamisha dalili juu ya Tawhiyd ya Allaah (سبحانه وتعالى) na kwamba Sharia ya Uislamu inatokana na asili ya Dini ya Nabiy Ibraahiym (عليه السّلام).
4-Kuthibitisha ukweli wa Nabiy Wake (صلى الله عليه وآله وسلم) na ukweli wa yale aliyokuja nayo.
5-Kubainisha Neema mbali mbali za Allaah kwa Waja Wake.
6-Kubainisha sifa za Waumini na washirikina na kuthibitisha kufufuliwa Siku ya Qiyaamah na jazaa za Waumini duniani na Aakhirah, na adhabu za washirikina duniani na Aakhirah kutokana na shirki na kufru zao,.
7-Kusisitiza wema na ihsaan kwa watu, kutimiza ahadi hata ikiwa lengo ni kuwalingania katika Dini ya Allaah kuwafahamisha ukafiri wao na ushirikina wao. Pia matahadharisho ya kutenda machafu na munkari na dhulma.
Miongoni Mwa Maudhui Ya Suwrah:
1-Suwrah imefunguliwa kwa kuthibitisha kwamba Siku ya Qiyaamah ni kweli na kwamba haina shaka kutokea kwake. Na Allaah (سبحانه وتعالى) Ametakasika na Ametukuka kwa Uluwa kutokana na wanayomshirikisha.
2-Imethibitishwa Tawhiyd ya Allaah (سبحانه وتعالى) ya Al-Uluwhiyyah (Kumpwekesha Allaah katika ibaada) kwamba hapana mwabudiwa wa haki ila Yeye Allaah (سبحانه وتعالى). Na uthibitisho wa Tawhiyd ya Ar-Rubuwbiyyah (Uola, Uumbaji na kadhaalika) kwa kubainisha Qudra ya Allaah katika kuumba mbingu, ardhi, wanaadam, na wanyama. Pia kulidhalilisha jua na mwezi, usiku na mchana, na vinginevyo.
3-Zimetajwa Neema nyingi na mbalimbali za Allaah (سبحانه وتعالى) kwa wanaadam. Miongoni mwazo ni wanyama na vinavyopatikana kwao ambavyo ni vipando vya watu, na kubebeshwa mizigo safarini, kupatikana ngozi zao, maziwa na pambo. Pia neema ya maji yatokayo mbinguni yanayootesha mazao mbalimbali. Neema ya Allaah (سبحانه وتعالى) kuitisha usiku na mchana, kuitisha bahari na faida zinazopatikana humo za mapambo, nyama safi, na meli zinazopita humo kuwapatia watu rizki zao. Kujaalia milima thabiti ardhini. Kujaalia nyota za kuwaongoza watu njia na mengineyo. Kisha Allaah (سبحانه وتعالى) Anamalizia kuhusu Neema Zake kuwa haiwezekani kuziorodhesha hesabuni. Na hayo yote Allaah (سبحانه وتعالى) Anataja kuwa ni Aayaat (Ishara, Dalili, Mazingatio) kwa watu wenye kutafakari, wenye kutia akilini, wenye kukumbuka na wenye kushukuru.
4-Kuna matahadharisho kwa washirikina, ya yale yaliyowapata waliomshirikisha Allaah (سبحانه وتعالى) na kuwapinga Rusuli wa Allaah (عليهم السلام), ambayo ni maangamizi na adhabu za dunia na zinazowangojea Aakhirah.
5-Suwrah imebainisha tofauti ya kutolewa roho kwa kafiri na Muumin: Kafiri hutolewa kwa adhabu na kubashiriwa kuingizwa motoni huko Aakhirah. Ama Muumin, yeye hutolewa roho yake huku Malaika wakimtolea Salaam na bishara ya kuingizwa Jannah.
6-Imebainishwa jinsi washirikina na waabudiwa wao watakavyokanushana ibaada zao Siku ya Qiyaamah.
7-Imetajwa baadhi ya mila na desturi za kijaahiliyyah, za dhulma ya hali ya juu, kuwachukia watoto wa kike na kuwazika wakiwa hai.
8-Zimetajwa neema nyenginezo za Allaah (سبحانه وتعالى) nazo ni maziwa masafi yanayotoka matumboni mwa wanyama. Pia mazao mbalimbali. Na neema ya kupata asali kutokana na nyuki, ambayo ni shifaa ya magonjwa mbalimbali. Na Aayah (80-81) za zimeendelea kutaja Neema Zake Allaah (سبحانه وتعالى) za sufi, ngozi, vivuli na kadhaalika.
9-Kuna mifano ya wazi baina ya Muumini na kafiri. Muumini ni mwenye kushukuru. Ama kafiri ni aliyekosa shukurani na mwenye kukufuru. Na mifano ya tofauti ya Mwabudiwa wa haki ambaye ni Allaah (سبحانه وتعالى) na waabudiwa wasiokuwa wa haki.
10-Imetajwa baadhi ya tabia njema, ikiwemo uadilifu, ihsaan, kujitolea, kukemea uovu, kuhimiza watu kutekeleza ahadi, na kuwakemea watu juu ya kuvunja ahadi.
11-Ukumbusho wa Muumini kutenda mema ili apate maisha mazuri duniani na Aakhirah.
12-Kuna amri ya kuomba kinga dhidi ya shaytwaan katika kusoma Qur-aan, jambo ambalo ni miongoni mwa adabu za kuisoma Qur-aan.
13-Imetajwa baadhi ya shubha ambazo walizizusha washirikina dhidi ya Qur-aan, pamoja na kuzifanyia raddi.
14-Imetajwa hukmu ya mtu anayekufuru baada ya kuwa Muumini (mwenye kurtadd), na anayelazimishwa kukufuru, ilihali moyo wake umethibitika katika imaan.
15-Imetajwa amrisho la kula vizuri vya halali na haramisho la kula vya haramu kama nyama ya nguruwe. Na kubainisha kwamba kuhalalisha na kuharamisha ni kazi ya Allaah (سبحانه وتعالى).
16-Ametajwa Nabiy Ibraahiym (عليه السّلام) na baadhi ya sifa na fadhila zake, na ukumbusho kwa watu kuwa alikuwa haniyfah (mwenye kuelemea haki) wala hakuwa mshirikina, na sifa yake ya kuwa mwenye kushukuru. Rejea Aayah (120) kwenye uchambuzi wa fadhila na sifa za Nabiy Ibraahiym (عليه السّلام).
17-Imetajwa njia muhimu za kufanya daawah ya Allaah, na jinsi ya kuamiliana na watu, ambako ni kuwalingania kwa hekima, na mawaidha mazuri.
18-Suwrah imekhitimishwa kwa amri ya kuvuta subira katika mitihani na kwamba subra inatokana na tawfiyq ya Allaah (سبحانه وتعالى) baada kumuomba Yeye Amjaalie mja Wake kuvumilia.
Faida:
Suwrah ya An-Nahl ni Suwrah inayobainisha kwa wingi Neema za Allaah (سبحانه وتعالى) ambazo haiwezekani kuziorodhesha hesabuni kama Anavyosema Mwenyewe Allaah (سبحانه وتعالى) katika Aayah namba (18). Na mojawapo ya neema ni Kuumba An-Nahl (Nyuki) wanaotoa asali matumboni mwao ambayo ni shifaa, tiba na kinga ya magonjwa. Rejea Aayah namba (68-69).
017-Al-Israa: Utangulizi Wa Suwrah
Alhidaaya.com [2]
Imeteremka: Makkah kwa itifaki ya ‘Ulamaa.
Idadi Za Aayah: 111
Jina La Suwrah: Al-Israa
Suwrah imeitwa Al-Israa (Safari ya Usiku), na inayodalilisha ni kutajwa katika Hadiyth zilizonukuliwa chini katika Fadhila, na kutajwa katika Aayah namba (1). Rejea pia Faida.
Na imeitwa pia Suwrah Bani Israaiyl, kutokana na maelezo yaliyotajwa kuhusu Wana wa Israaiyl na ufisadi wao katika ardhi.
Miongoni Mwa Makusudio Ya Suwrah:
1-Allaah (سبحانه وتعالى) kumthibitisha Rasuli wake, (صلى الله عليه وآله وسلم) na kumtia nguvu kwa dalili za wazi, na kumpa bishara Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) ya ushindi na kuthibiti. [Al-Mukhtaswar Fiy Tafsiyr Al-Qur-aan Al-Kariym]
2-Kuithibitisha misingi ya ‘Aqiydah ya Uislamu, na kuisafisha na kila kinachotia dosari katika Uislamu.
3-Kubainisha kwamba, Qur-aan inaongoza katika yaliyonyooka na inawabashiria Waumini ujira mtukufu na mkubwa. Na kuthibitishwa adhabu kwa wasioamini. Na kwamba malipo ya hidaaya na dhambi za upotevu humjia mtu binafsi. Na pia hakuna atakayebeba dhambi za mtu mwengine. Na kwamba Siku ya Qiyaamah, kila mtu atashuhudia mwenyewe matendo yake.
4-Kuthibitisha Tawhiyd ya Allaah na kuwafanyia ihsaan wazazi wawili na kutokuwakemea hata kwa neno la uff! Rejea tanbihi ya Aayah namba (23). Pia kuwafanyia ihsaan arhaam (wenye uhusiano wa damu), walioharibikiwa safarini, kuwaonea huruma maskini na mafakiri.
5-Haramisho la kumshirikisha Allaah, na kufanya ubadhirifu wa mali, kukaribia zinaa, kuua na makatazo mengineyo.
6-Kuthibitisha Qur-aan na kwamba ni mustahili kwa yeyote yule kuleta mfano wa Qur-aan kwani ni muujiza wa Dini Tukufu ya Kiislamu. Na pia kubainishwa kwamba Qur-aan imeteremshwa kidogo kidogo kwa hikma.
7-Maelezo yanayomuhusu Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) na kubainisha misimamo ya washirikina kwa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم).
8-Kubainisha baadhi ya majukumu ya kisharia yanayoendana na tabia za kila mmoja na jamii kwa ujumla.
Miongoni Mwa Maudhui Ya Suwrah:
1-Suwrah imefunguliwa kwa kutajwa muujiza wa safari ya Al-Israa na Al-Mi’raaj, ambayo ni safari ya sehemu ya usiku mmoja kuanzia Masjid Al-Haraam hadi Masjid Al-Aqswaa kisha kupanda mbinguni hadi mbingu ya saba.
2-Imetajwa Kitabu ambacho Allaah alimpa Muwsaa (عليه السلام), ili kiwe mwongozo kwa watu wake, na kuwajulisha Bani Israaiyl kuwa watafanya uharibifu katika ardhi mara mbili.
3-Imebainisha fadhila za Qur-aan, na kwamba inaongoza kwenye jambo zuri zaidi, na inawabashiria Waumini kuwa watapata malipo makubwa.
4-Imethibitisha dalili ya kuwa Allaah Pekee Ndiye Anaepasa kuabudiwa. Imetaja dalili ya uwepo wa usiku na mchana na kwamba kuna faida nyingi kwa mwanaadam.
5-Imebainisha Desturi ya Allaah (سبحانه وتعالى) ya maangamizo kwa watu wa karne zilizopita. Na kwamba Allaah (سبحانه وتعالى) Haadhibu wala Haangamizi watu isipokuwa baada ya kuwatumia Rusuli wake kuwabashiria na kuwaonya ili kuwasimamishia hoja.
6-Imebainishwa kwamba maisha mazuri ya Aakhirah ni kwa matakwa Yake Allaah (سبحانه وتعالى), kukiambatana na matendo ya mja akiwa na imaan.
7-Kuna Makatazo na Maamrisho Ya Allaah (سبحانه وتعالى) ambayo yameanzia Aayah ya (22) hadi ya (39) yakiwemo: (i) Tahadharisho la kutokumshirikisha Yeye Allaah (سبحانه وتعالى) (ii) Amri ya kumwabudu Allaah (سبحانه وتعالى) Pekee (iii) Kuwafanyia wema wazazi wawili na kutokuwaudhi hata kwa neno la uff! Kuwanyenyekea, kuwahurumia na kuwaombea duaa. (iv) Kuwapa jamaa wa karibu haki zao na masaakini (v) Kutokufanya ubadhirifu na tahadharisho la shaytwaan anayepelekea ubadhirifu (vi) Kuwatamkia maneno mazuri jamaa wa karibu wanapoomba rizki (vii) Kutokufanya ubakhili na kutokutumia mali kwa israfu (viii) Kutokuwaua watoto kwa kukhofia ufuqara (ix) Kutokukaribia machafu ya zinaa (x) Kutokuua nafsi ambayo Allaah Ameiharamisha (kuiua) isipokuwa kwa haki ya kisharia (xi) Kutokukaribia kula mali ya yatima (xii) Kutimiza ahadi (xiii) Kutimiza kipimo kamilifu kinapopimwa mizanini (xiv) Kutokufuata (au kusema) asiyekuwa nayo mtu kwayo ilimu (xv) Kutokutembea katika ardhi kwa majivuno (xvi) Akamalizia Allaah (سبحانه وتعالى) kwa tahadharisho la kutokumshirikisha Yeye (سبحانه وتعالى).
8-Kuna Radd kuwapinga wanaomzulia Allaah (سبحانه وتعالى) kuwa Ana wana wa kike.
9-Imetajwa kuwa kila kilichopo mbinguni na ardhini kinamsabihi na Kumhimidi Allaah (سبحانه وتعالى).
10-Imetajwa sehemu ya kauli za washirikina kutokuamini kwao kufufuliwa.
11-Waumini wameamrishwa watamke maneno mazuri na wajitahadharishe na shaytwaan.
12-Imetajwa kisa cha kuumbwa Aadam na kumkirimu kwa kuamrisha Malaika wamsujudie, na msimamo wa Ibliys juu ya hilo.
13-Allaah (سبحانه وتعالى) Amemthibitisha Rasuli Wake (صلى الله عليه وآله وسلم) na Kumuamrisha kudumisha Swalaah za usiku na mchana na kusoma Qur-aan.
14-Imebainishwa kuwa Qur-aan ni shifaa na rehma kwa Waumini.
15-Imeelezewa madai ya washirikina kumtaka Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alete mambo ya ajabu yasiyokuwa ya kibinaadam; rejea Aayah (90-95).
16-Imetajwa kuhusu miujiza na ishara tisa alizopewa Nabiy Muwsaa (عليه السلام) kwa Firawni.
17-Imebainishwa kuwa Qur-aan imeteremshwa kidogo kidogo kwa hikma yake ya kuwasomea watu kwa kituo.
18-Suwrah imekhitimishwa kwa kuthibitisha Majina ya Allaah, kwamba yote ni Mazuri kwani madai ya washirikina walikuwa wakipinga sifa ya Ar-Rahmaan. Basi kwa Jina lolote lile atakavoombwa duaa ikiwa ni “Yaa Allaah” au “Yaa Rahmaan” basi yote ni sahihi.
Fadhila Za Suwrah:
Miongoni mwa Suwrah alizokuwa akizisoma Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) kabla ya kulala ni Suwrah Al-Israa:
عن عائشة رضي الله عنها قالت: كانَ النَّبيُّ صلَّى اللَّهُ عليهِ وسلَّمَ لا ينامُ علَى فِراشِه حتَّى يقرأ بَني إسرائيلَ ، والزُّمَرِ
Amesimulia ‘Aaishah (رضي الله عنها): Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alikuwa halali kitandani mwake ila akisoma kwanza (Suwrah) Bani Israaiyl na Az-Zumar. [At-Tirmidhiy na ameisahihisha Al-Albaaniy katika Swahiyh At-Tirmidhiy (2920), Swahiyh Al-Jaami’ (4874)]
Faida:
1-Suwrah imeitwa Al-Israa kutokana na tukio adhimu la safari ya Al-Israa Wal-Mi’raaj ambayo ilikuwa ni safari ya baadhi ya nyakati za usiku mmoja (Al-Israa) kuanzia Masjid-Al-Haraam Makkah hadi Masjid Al-Aqswaa (Mji wa Quds Jerusalem), kisha kupanda (Mi’raaj) kufika mbingu ya saba, (na kurudi usiku huo huo Makkah). Imetajwa mwanzo wa Suwrah, rejea Aayah namba (1) kwenye maelezo bayana.
2-Suwrah Al-Israa ni miongoni mwa Suwrah zilizotangulia kuteremshwa, na Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akazitaja kuwa ni pato lake la mwanzo:
حَدَّثَنَا آدَمُ، حَدَّثَنَا شُعْبَةُ، عَنْ أَبِي إِسْحَاقَ، قَالَ سَمِعْتُ عَبْدَ الرَّحْمَنِ بْنَ يَزِيدَ، سَمِعْتُ ابْنَ مَسْعُودٍ، يَقُولُ فِي بَنِي إِسْرَائِيلَ وَالْكَهْفِ وَمَرْيَمَ وَطَهَ وَالأَنْبِيَاءِ إِنَّهُنَّ مِنَ الْعِتَاقِ الأُوَلِ وَهُنَّ مِنْ تِلاَدِي.
Amesimulia ‘Abdur-Rahmaan bin Yaziyd (رضي الله عنه): Nimemsikia ‘Abdullaah bin Mas‘uwd (رضي الله عنه) akisema: Suwrah Bani Israaiyl, Al-Kahf, Maryam, Twaahaa na Al-Anbiyaa ndio miongoni mwa pato langu la kwanza na mali yangu kongwe, na (hakika ni) ndio mali yangu kongwe.” [Al-Bukhaariy]
018-Al-Kahf: Utangulizi Wa Suwrah
Alhidaaya.com [2]
Imeteremka: Makkah kwa itifaki ya ‘Ulamaa.
Idadi Za Aayah: 110
Jina La Suwrah: Al-Kahf
Suwrah imeitwa Al-Kahf (Pango), na inayodalilisha ni kutajwa katika Hadiyth zilizonukuliwa chini katika Fadhila. Na imeitwa Al-Kahf kutokana na kisa cha Aswhaabul-Kahf (watu wa pangoni) waliotaja kuanzia Aayah namba (9).
Miongoni Mwa Makusudio Ya Suwrah:
1-Kubainisha Manhaj (njia) ya kuamiliana na fitnah. [Al-Mukhtaswar Fiy Tafsiyr Al-Qur-aan Al-Kariym]
2-Kuwajibika Kumhimidi Allaah (سبحانه وتعالى) na kumshukuru kwa Neema Zake tele, kuwa na imaan na matendo mema, kuthibitisha Tawhiyd Yake (Kumpwekesha) na haramisho la kumshirikisha kwa ibaada na riyaa-a (kujionyesha).
3-Kuthibitisha kufufuliwa, na adhabu za wenye kukanusha.
4-Mwongozo wa ‘Aqiydah sahihi na tabia njema, na mwongozo juu ya fikra salama ambayo inamfanya mtu aishi maisha mazuri ya duniani na Aakhirah.
5-Kubainisha Hikma ya Allaah (سبحانه وتعالى) katika Ujuzi Wake, na kwamba wanaadam wanatofautiana ilimu na maarifa waliyojaaliwa na Allaah.
Miongoni Mwa Maudhui Ya Suwrah:
1-Suwrah imefunguliwa kwa Kumhimidi Allaah (سبحانه وتعالى) kwa kuteremsha Kitabu kwa Mja Wake Nabiy Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم), na kukisifu kuwa ni Kitabu kitukufu kisicho na dosari, na kwamba kinabashiria Waumini watendao mema kuwa watapata ujira mzuri, na kinawaonya wanaomsingizia Allaah (سبحانه وتعالى) kuwa ana mwana.
2-Imebainishwa kwamba vilivyopo juu ya ardhi ni pambo lake na kwamba limewekwa na Allaah (سبحانه وتعالى) ikiwa kama mtihani kwa waja.
3-Imetajwa kisa cha Aswhaabul-Kahf (Watu wa pangoni) ambao walithibitika katika Tawhiyd ya Allaah.
4-Imeamrishwa kusema In Shaa Allaah pindi mtu akitaka kufanya jambo kesho au hata baada ya muda fulani.
5-Imetahadharishwa fitnah ya mali kwa kutajwa kisa cha mwenye bustani mbili aliyemkufuru Rabb wake akakanusha Siku ya Qiyaamah, na adhabu yake.
6-Umepigwa mfano wa maisha ya dunia; mfano unaojulisha kumalizika kwake na kuondoka starehe zake.
7-Imetajwa baadhi ya adhabu za moto kwa madhalimu na makafiri Siku ya Qiyaamah na mateso yao na baadhi ya matukio ya Siku hiyo ya Mwisho.
8-Waumini wamekumbushwa kwamba, mali na watoto ni mapambo ya dunia, lakini al-baaqiyaatu asw-swaalihaatu ndio bora zaidi mtu kutarajia malipo mema kutoka kwa Allaah. Rejea Aayah (46).
9-Imebainishwa uadui wa Ibliys kwa Aadam na kizazi chake.
10-Imetajwa kisa cha Nabiy Muwsaa (عليه السلام) pamoja na kijana wake Yuwsha’ Bin Nuwn pamoja na kisa chake na mja aliyepewa ilimu zaidi naye ni Al-Khidhwr.
11-Imetajwa kisa cha Dhul-Qarnayni na kutajwa kwa Yaajuwj na Maajuwj ambao ni mmojawapo ya alama kubwa za Qiyaamah.
12-Suwrah imekhitimishwa kwa makemeo ya ushirikina na kubatilisha shirki, na kubainisha mazuri ya kudumu milele, Aliyoyaahidi Allaah (سبحانه وتعالى) kwa Waumini.
Fadhila Za Suwrah:
1-Kuhifadhi Aayah kumi za mwanzo wa Suwrah ni kinga ya Masiyh Dajjaal:
عن أَبي الدرداءِ رضي اللهُ عنه : أنَّ رسول الله صلى الله عليه وسلم ، قَالَ : مَنْ حَفِظَ عَشْرَ آيَاتٍ مِنْ أَوَّلِ سُورَةِ الكَهْفِ ، عُصِمَ مِنَ الدَّجَّالِ . رواه مسلم
Amesimulia Abuu Dardaa (رضي الله عنه): Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: "Mwenye kuhifadhi Aayah kumi mwanzo wa Suwrah Al-Kahf ataepushwa na (Masiyh) Dajjaal.” [Muslim]
Na katika riwaayah nyengine Hadiyth ndefu ambayo:
Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alimtaja Ad-Dajjaal siku moja…. Akasema:
فَمَنْ أَدْرَكَهُ مِنْكُمْ فَلْيَقْرَأْ عَلَيْهِ فَوَاتِحَ سُورَةِ الْكَهْفِ إِنَّهُ خَارِجٌ خَلَّةً بَيْنَ الشَّأْمِ وَالْعِرَاقِ فَعَاثَ يَمِينًا وَعَاثَ شِمَالاً
"Atakayesalia miongoni mwenu na kumwona, amsomee Aayah za mwanzo za Suwrah Al-Kahf kwani atatokea njia baina ya Sham na Iraq na atafanya ufisadi pande za kuliani na kushotoni.” [Muslim]
وفي رواية : مِنْ آخِرِ سُورَةِ الكَهْفِ رواه مسلم
Na riwaayah nyengine: “Mwisho wa Suwrah Al-Kahf.” [Muslim]
2-Kuisoma inateremsha sakiynah (Utulivu):
حَدَّثَنِي مُحَمَّدُ بْنُ بَشَّارٍ، حَدَّثَنَا غُنْدَرٌ، حَدَّثَنَا شُعْبَةُ، عَنْ أَبِي إِسْحَاقَ، سَمِعْتُ الْبَرَاءَ بْنَ عَازِبٍ ـ رضى الله عنهما ـ قَرَأَ رَجُلٌ الْكَهْفَ وَفِي الدَّارِ الدَّابَّةُ فَجَعَلَتْ تَنْفِرُ فَسَلَّمَ، فَإِذَا ضَبَابَةٌ ـ أَوْ سَحَابَةٌ ـ غَشِيَتْهُ، فَذَكَرَهُ لِلنَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم فَقَالَ " اقْرَأْ فُلاَنُ، فَإِنَّهَا السَّكِينَةُ نَزَلَتْ لِلْقُرْآنِ، أَوْ تَنَزَّلَتْ لِلْقُرْآنِ ".
Amesimulia Abuu Is-haaq (رضي الله عنه): Nimemsikia Al-Baraa Bin ‘Aazib (رضي الله عنهما) akisema: Mtu mmoja alisoma Suwrah Al-Kahf (katika Swalaah yake), na ndani ya nyumba yake mlikuwa na mnyama. (Mnyama) akawa anaogopa na huku anarukaruka. Akatoa Salaam (kumaliza Swalaah) basi ghafla ukamfinika ukungu au wingu. Akamwelezea kisa hicho Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) basi akasema: “Soma ee fulani, kwani hiyo ni as-sakiynah (utulivu) umeteremka kwa sababu ya Qur-aan.” Au “Unateremka kwa ajili ya Qur-aan.” [Al-Bukhaariy na Muslim]
3-Inamwangazia Nuru kati ya Ijumaa mbili, atakayeisoma siku ya Ijumaa:
عَنْ أَبِي سَعِيدٍ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ أَنَّ النَّبِيَّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: من قَرَأَ سُورَة الْكَهْف فِي يَوْم الْجُمُعَة أَضَاء لَهُ النُّور مَا بَيْنَ الْجُمْعَتَيْنِ
Amesimulia Abu Sa’iyd Al-Khudriyy (رضي الله عنه): Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Mwenye kusoma Suwrah Al-Kahf Siku ya Ijumaa, basi itamwangazia nuru ya kati ya Ijumaa mbili.” [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Haakim (2/368) na Al-Bayhaqiy (3/249) na ameisahihisha Al-Albaaniy katika Swahiyh Al-Jaami’ (6470)]
Tanbihi: Baadhi ya ‘Ulamaa wameona kuwa hii ni Hadiyth dhwaiyf ila kuna ambao wameona si vibaya kuisoma kama Imaam Ibn Baaz (رحمه الله) aliposema: “Ina udhaifu lakini mtu akiisoma kutaraji fadhila zake, basi ni vizuri kwani alifanya hivo Ibn ‘Umar (رضي الله عنهما).
Faida:
1-Suwrah Al-Kahf (18) ni miongoni mwa Suwrah tano zinazoanzia kwa AlhamduliLlaah. Nyenginezo ni Al-Faatihah (1), Al-An’aam (6), Saba-a (34) na Faatwir (35).
2-Rejea faida katika Aayah namba (23) kujua sababu ya kuteremshwa kisa cha Aswhaabul-Kahf.
3-Suwrah Al-Kahf ni miongoni mwa Suwrah zilizotangulia kuteremshwa, na Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akazitaja kuwa ni pato lake la mwanzo:
حَدَّثَنَا آدَمُ، حَدَّثَنَا شُعْبَةُ، عَنْ أَبِي إِسْحَاقَ، قَالَ سَمِعْتُ عَبْدَ الرَّحْمَنِ بْنَ يَزِيدَ، سَمِعْتُ ابْنَ مَسْعُودٍ، يَقُولُ فِي بَنِي إِسْرَائِيلَ وَالْكَهْفِ وَمَرْيَمَ وَطَهَ وَالأَنْبِيَاءِ إِنَّهُنَّ مِنَ الْعِتَاقِ الأُوَلِ وَهُنَّ مِنْ تِلاَدِي.
Amesimulia ‘Abdur-Rahmaan bin Yaziyd (رضي الله عنه): Nimemsikia ‘Abdullaah bin Mas‘uwd (رضي الله عنه) akisema: Suwrah Bani Israaiyl, Al-Kahf, Maryam, Twaahaa na Al-Anbiyaa ndio miongoni mwa pato langu la kwanza na mali yangu kongwe, na (hakika ni) ndio mali yangu kongwe.” [Al-Bukhaariy]
019-Maryam: Utangulizi Wa Suwrah
Alhidaaya.com [2]
Imeteremka: Makkah kwa itifaki ya ‘Ulamaa.
Idadi Za Aayah: 98
Jina La Suwrah: Maryam
Suwrah imeitwa Maryam, na inayodalilisha ni kutajwa katika Hadiyth iliyonukuliwa katika nukta (3) ya Fadhila. Na imeitwa Maryam kutokana na kisa chake Maryam mama wa Nabiy ‘Iysaa (عليه السّلام) kuanzia Aayah namba (16).
Miongoni Mwa Makusudio Ya Suwrah:
1-Kubatilisha ‘Aqiydah (itikadi) ya washirikina na Manaswara ya kumnasibishia Allaah (سبحانه وتعالى) kuwa na mtoto, na kubainisha ukunjufu (ukubwa) wa Rehma za Allaah (سبحانه وتعالى) kwa waja Wake. [Al-Mukhtaswar Fiy Tafsiyr Al-Qur-aan Al-Kariym]
2-Kubainisha Miujiza Ya Allaah (سبحانه وتعالى) na Uwezo Wake Mkubwa wa kuumba bila ya kuweko sababu.
3-Radd kwa Mayahudi waliomsingizia machafu Maryam mama wa Nabiy ‘Iysaa (عليه السّلام).
4-Kuthibitisha Tawhiyd ya Allaah kwamba Anayestahiki kuabudiwa ni Allaah (سبحانه وتعالى). Na haramisho la kumshirikisha Allaah, na kwamba hilo ni chukizo kubwa hata kwa vitu Alivyoviumba Allaah mbinguni na ardhini.
Miongoni Mwa Maudhui Ya Suwrah:
1-Suwrah imefunguliwa kwa herufi zinazojulikana kama الحروف المقطعة (Al-Huruwf Al-Muqatw-twa’ah), ambazo hakuna ajuaye maana zake isipokuwa Allaah (سبحانه وتعالى). Rejea Al-Baqarah (2:1). Kisha kimetajwa sehemu ya kisa cha Nabiy Zakariyyaa (عليه السلام) na kujaaliwa kwake kumzaa Nabiy Yahyaa (عليه السّلام) juu ya kuwa alifikia uzee wa kuvuka mipaka pamoja na mkewe kuwa tasa.
2-Imetajwa kuzaliwa kwa Nabiy Yahyaa (عليه السّلام) na sifa zake.
3-Imetajwa kisa cha Maryam na muujiza wa kuzaliwa kwa Nabiy ‘Iysaa (عليهما السلام).
4-Imetaja sehemu fulani ya kisa cha Nabiy Ibraahiym (عليه السلام) alivyojadiliana na baba yake aliyekuwa ni kafiri.
5-Wametajwa baadhi ya Manabii na ishara kuwa walikuwa wengi akiwemo: Is-haaq, Ya’quwb, Muwsaa, Haaruwn, Ismaa’iyl, Idriys, Nuwh, Aadam (عليهم السَّلام).
6-Suwrah imedhihirisha aina tatu za Tawhiyd; Rejea Aayah (65) kwa maelezo bayana.
7-Imetaja kuhusu moto ambao kila mtu lazima aupitie.
8-Suwrah imebainisha malipo ya wamchao Allaah, na adhabu za makafiri, na kufungua mlango wa tawbah kwa wanaomuasi.
9-Imetaja baadhi ya shubha za washirikina dhidi ya Qur-aan, na kufufuliwa, pamoja na kuziraddi.
10-Imebainisha baadhi ya mambo yatakayotokea Siku ya Qiyaamah.
11-Imebainisha jinsi gani mbingu zinavokaribia kupasuka, na ardhi kuraruka, na milima kuporomoka na kubomoka kwa kumsingizia Allaah (سبحانه وتعالى) kuwa Ana mwana!
12-Suwrah imekhitimishwa kwa kile kilichoanzwa nacho ambacho ni kubainisha mapenzi ya Allaah na Ikraam Yake kwa vipenzi Vyake, na kubainisha hikma ya kuteremshwa Qur-aan.
Fadhila Za Suwrah:
1-Ni Suwrah pekee iliyoitwa kwa jina la mwanamke naye ni Maryam mama wa Nabiy ‘Iysaa (عليه السّلام). Na Allaah (سبحانه وتعالى) Amemtakasa na kumsifia. Rejea Suwrah Aal-‘Imraan (3:42-43).
2-Na pia katika Hadiyth za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) amesifika kuwa ni katika wanawake bora kabisa:
عَنْ أَنَسٍ، رضى الله عنه أَنَّ النَّبِيَّ صلى الله عليه وسلم قَالَ " حَسْبُكَ مِنْ نِسَاءِ الْعَالَمِينَ مَرْيَمُ ابْنَةُ عِمْرَانَ وَخَدِيجَةُ بِنْتُ خُوَيْلِدٍ وَفَاطِمَةُ بِنْتُ مُحَمَّدٍ وَآسِيَةُ امْرَأَةُ فِرْعَوْنَ " . قَالَ أَبُو عِيسَى هَذَا حَدِيثٌ صَحِيحٌ .
Amesimulia Anas (رضي الله عنه): Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Wanakutosheleza katika wanawake wa ulimwengu: Maryam bint ‘Imraan, Khadiyjah bint Khuwaylid Faatwimah bint Muhammad na Aasiyah mke wa Firawni.” [At-Tirmidhiy na amesema: Hii ni Hadiyth Swahiyh na ameisahihisha Al-Albaaniy katika Swahiyh At-Tirmidhiy Uk au namba (3878)]
Na pia:
عَنْ أَبِي مُوسَى الأَشْعَرِيِّ رضى الله عنه قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم: كَمَلَ مِنَ الرِّجَالِ كَثِيرٌ، وَلَمْ يَكْمُلْ مِنَ النِّسَاءِ إِلاَّ مَرْيَمُ بِنْتُ عِمْرَانَ، وَآسِيَةُ امْرَأَةُ فِرْعَوْنَ، وَفَضْلُ عَائِشَةَ عَلَى النِّسَاءِ كَفَضْلِ الثَّرِيدِ عَلَى سَائِرِ الطَّعَامِ
Amesimulia Abuu Muwsaa Al-Ash’ariyy (رضي الله عنه): Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Wanaume wengi wamefikia daraja ya ukamilifu lakini hakuna mwanamke aliyefikia daraja hiyo isipokuwa Aasiyah mke wa Firawni, na Maryam bint 'Imraan. Na ubora wa 'Aaishah (رضي الله عنها) kwa wanawake wengine ni kama mfano wa ubora wa thariyd kwa vyakula vingine.” [Al-Bukhaariy na wengineo]
3-Suwrah Maryam ni miongoni mwa Suwrah zilizotangulia kuteremshwa, na Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akazitaja kuwa ni pato lake la mwanzo:
حَدَّثَنَا آدَمُ، حَدَّثَنَا شُعْبَةُ، عَنْ أَبِي إِسْحَاقَ، قَالَ سَمِعْتُ عَبْدَ الرَّحْمَنِ بْنَ يَزِيدَ، سَمِعْتُ ابْنَ مَسْعُودٍ، يَقُولُ فِي بَنِي إِسْرَائِيلَ وَالْكَهْفِ وَمَرْيَمَ وَطَهَ وَالأَنْبِيَاءِ إِنَّهُنَّ مِنَ الْعِتَاقِ الأُوَلِ وَهُنَّ مِنْ تِلاَدِي.
Amesimulia ‘Abdur-Rahmaan bin Yaziyd (رضي الله عنه): Nimemsikia ‘Abdullaah bin Mas‘uwd (رضي الله عنه) akisema: Suwrah Bani Israaiyl, Al-Kahf, Maryam, Twaahaa na Al-Anbiyaa ndio miongoni mwa pato langu la kwanza na mali yangu kongwe, na (hakika ni) ndio mali yangu kongwe.” [Al-Bukhaariy]
020-Twaahaa: Utangulizi Wa Suwrah
Alhidaaya.com [2]
Imeteremka: Makkah kwa itifaki ya ‘Ulamaa.
Idadi Za Aayah: 135
Jina La Suwrah: Twaahaa
Suwrah imeitwa Twaahaa, na inayodalilisha ni kutajwa katika Aayah namba (1), na herufi hizo ni ambazo zinajulikana kuwa ni Al-Huruwf Al-Muqatw-twa’ah zinazotokea katika mwanzo wa baadhi ya Suwrah. Na pia kutajwa katika Hadiyth iliyonukuliwa chini katika Fadhila za Suwrah.
Miongoni Mwa Makusudio Ya Suwrah:
1-Kuishi maisha mazuri kwa kufuata mwongozo wa Qur-aan, na kuubeba ujumbe wake, na kuishi maisha magumu kwa kwenda kinyume na mwongozo wa Qur-aan. [Al-Mukhtaswar Fiy Tafsiyr Al-Qur-aan Al-Kariym]
2-Utukufu na hadhi ya Qur-aan na kubainisha kwamba Qur-aan ni Risala ya kutoka mbinguni, na haikuteremshwa kwa ajili ya kuwatia watu mashakani, bali Allaah (سبحانه وتعالى) Ameiteremsha kuwa ni mwongozo na uwokovu wa watu, na ni sababu ya kufaulu katika maisha ya duniani na Aakhirah.
3-Ulinzi wa Allaah (سبحانه وتعالى) kwa Rusuli Wake Aliowachagua kubeba Risala Yake, wakiwemo wafuasi wao.
4-Maelezo kuhusu baadhi ya matukio ya Siku ya Qiyaamah, na jazaa ya makafiri kuwa ni adhabu, na jazaa ya Waumini kuwa ni Jannah yenye neema na starehe za kudumu.
Miongoni Mwa Maudhui Ya Suwrah:
1-Suwrah imefunguliwa kwa herufi zinazojulikana kama الحروف المقطعة (Al-Huruwf Al-Muqatw-twa’ah), ambazo hakuna ajuaye maana zake isipokuwa Allaah (سبحانه وتعالى). Rejea Al-Baqarah (2:1). Kisha imekumbusha Utukufu wa Qur-aan, na kwamba imeteremshwa kutoka kwa Allaah (سبحانه وتعالى), na kwamba haikuteremshwa kwa ajili kutia mashaka bali ni ukumbusho kwa wenye kukhofu.
2-Suwrah imethibitisha Al-Istiwaa ambayo inamaanisha Allaah Kuweko juu ya ‘Arsh Yake Tukufu kwa namna inayolingana na Uadhama na Ujalali Wake Yeye Mwenyewe Allaah (سبحانه وتعالى). Rejea Aayah namba (5) kwenye maelezo bayana.
3-Imeelezea sehemu kubwa ya kisa cha Nabiy Muwsaa (عليه السلام). Kisa kikianzia Nabiy Muwsaa (عليه السلام) alipoacha ahli wake akaenda katika bonde tukufu la Twuwaa akaongea na Rabb wake. Kisha Allaah (سبحانه وتعالى) Akamkumbusha Nabiy Muwsaa (عليه السلام), pindi alipozaliwa akatiwa katika sanduku na kutupwa katika mto wa Nile, na jinsi alivyofika nyumbani mwa adui yake Firawni na kulelewa humo. Kisha pale Allaah (سبحانه وتعالى) Alipomtuma Nabiy Muwsaa (عليه السلام) na nduguye Haaruwn (عليه السلام) kwenda kwa Firawni na mazungumzo yao huko. Kisha kusilimu kwa wachawi na chukizo la Firawni kuhusu wao. Kisha kuhusu Saamiriyyu kuwapotosha Bani Israaiyl kumwabudu ndama, wakati Nabiy Muwsaa (عليه السلام) alipoondoka kwenda Miyqaat (sehemu na muda maalumu wa miadi) ya Allaah.
4-Mwanaadam amekumbushwa kwamba ameumbwa kutokana na udongo (ardhini), na kwamba atarudishwa humo ardhini kuzikwa, na kwamba atafufuliwa kutoka humo pia.
5-Imetajwa malipo ya wanaoipuuza Qur-aan, na kutaja sehemu fulani ya matukio ya siku ya Qiyaamah.
6-Limetajwa Jina Tukufu kabisa la Allaah; Al-Hayyu Al-Qayyuwm, rejea Aayah (111) na Al-Baqarah (2:255), Aal-‘Imraan (3:2).
7-Imetaja daraja na utukufu wa Qur-aan, na kwamba imeteremshwa kwa lugha ya Kiarabu, lugha yenye ufasaha wa pekee.
8-Imetajwa kisa cha kuumbwa Aadam (عليه السلام).
9-Kuna maamrisho ya mambo mengi kwa Nabiy (صلى الله عليه وسلم) kama vile: Kuvuta subira, Kumdhukuru Allaah (سبحانه وتعالى) kwa wingi. Kutoangalia sana mapambo ya dunia. Kuwaamrisha watu wake Swalaah.
10-Suwrah imekhitimishwa kwa kuradd (kupinga) madai ya washirikina, na kuwatisha na mafikio mabaya endapo wataendelea na tabia yao ya kumpinga Rasuli wa Allaah (سبحانه وتعالى) na kudai kuletewa miujiza.
Fadhila Za Suwrah:
Suwrah Twaahaa ni miongoni mwa Suwrah zilizotangulia kuteremshwa, na Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akazitaja kuwa ni pato lake la mwanzo:
حَدَّثَنَا آدَمُ، حَدَّثَنَا شُعْبَةُ، عَنْ أَبِي إِسْحَاقَ، قَالَ سَمِعْتُ عَبْدَ الرَّحْمَنِ بْنَ يَزِيدَ، سَمِعْتُ ابْنَ مَسْعُودٍ، يَقُولُ فِي بَنِي إِسْرَائِيلَ وَالْكَهْفِ وَمَرْيَمَ وَطَهَ وَالأَنْبِيَاءِ إِنَّهُنَّ مِنَ الْعِتَاقِ الأُوَلِ وَهُنَّ مِنْ تِلاَدِي.
Amesimulia ‘Abdur-Rahmaan bin Yaziyd (رضي الله عنه): Nimemsikia ‘Abdullaah bin Mas‘uwd (رضي الله عنه) akisema: Suwrah Bani Israaiyl, Al-Kahf, Maryam, Twaahaa na Al-Anbiyaa ndio miongoni mwa pato langu la kwanza na mali yangu kongwe, na (hakika ni) ndio mali yangu kongwe.” [Al-Bukhaariy]
021-Al-Anbiyaa: Utangulizi Wa Suwrah
Alhidaaya.com [2]
Imeteremka: Makkah kwa itifaki ya ‘Ulamaa.
Idadi Za Aayah: 112
Jina La Suwrah: Al-Anbiyaa
Suwrah imeitwa Al-Anbiyaa (Manabii), na inayodalilisha ni kutajwa katika Hadiyth iliyonukuliwa chini katika Fadhila za Suwrah. Na pia kutokana na kutajwa kwa Manabii mbalimbali katika Suwrah.
Miongoni Mwa Makusudio Ya Suwrah:
1-Kuthibitisha Risala ya Allaah (سبحانه وتعالى) na kubainisha kuwa Manabii wote walikuwa na lengo moja, na ndio lengo la Allaah kwao. [Al-Mukhtaswar Fiy Tafsiyr Al-Qur-aan Al-Kariym]
2-Kubainisha haqq (ukweli) unavyoshinda baatwil, kwa kutaja mifano ya Rusuli na jinsi walivyowashinda watu wao. Na kuthibitisha kwamba Manabii na Rusuli wote walilingania Dini moja ya asili yake ambayo ni Tawhiyd ya Allaah, na kusimamisha dalili zake, kama kubainisha kwamba, ingelikuwa mbinguni na ardhini kulikuwa na waabudiwa wasiokuwa Allaah (سبحانه وتعالى) wenye kuyaendesha mambo yake, ungeliharibika mpango wa mbingu na ardhi.
3-Maonyo na kuthibitisha matokeo ya Siku ya Qiyaamah na kurejea viumbe kwa Allaah, na kuzibainisha dalili zake, kama kutokea baadhi ya alama zake kubwa, kama Yaajuwj na Maajuwj.
4-Kubainisha yale waliyokutana nayo Rusuli katika njia ya daawah (ulinganiaji), na kuwakumbusha makafiri yale yaliyowasibu nyumati za nyuma kwa sababu ya kuwakanusha Rusuli, na kwamba ahadi ya Allaah (سبحانه وتعالى) kuwaadhibu makafiri hao haibadiliki.
Miongoni Mwa Maudhui Ya Suwrah:
1-Suwrah imefunguliwa kwa kuwaonya watu kwa kuwathibitishia kwamba Qiyaamah kiko karibu.
2-Imetaja baadhi ya shubha ambazo walizizusha washirikina dhidi ya Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) katika kubalighisha Risala ya Allaah (سبحانه وتعالى).
3-Suwrah imemliwaza Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) juu ya yale aliyokuwa akiambiwa na washirikina.
4-Suwrah imethibitisha kwamba Rusuli wote walitumwa kwa ajili ya kulingania Tawhiyd ya Allaah; Laa ilaaha illa-Allaah.
5-Suwrah imetaja usingiziaji wa washirikina kwamba Allaah (سبحانه وتعالى) Ana mwana ilhali Yeye Ametukuka na hilo. Basi imewathibitishia jazaa yao ya Jahannam kwa usingiziaji huu wa kuvuka mipaka!
6-Suwrah inawakumbusha watu juu ya waliyoyapata nyumati zilizopita baada ya kuwakadhibisha Rusuli wao.
7-Suwrah imethibitisha Neema za Allaah (سبحانه وتعالى), Ishara na Dalili Zake za Tawhiyd kwamba: Yeye Ndiye Aliyezibandua mbingu na ardhi baada ya kuwa ziliambatana. Na Akajaalia uhai wa kila kitu kutokana na maji. Na Akajaalia milima kuwa thabiti isiyumbe yumbe. Akajaalia katika ardhi njia pana za kupitika ili watu wapate kujua waendako. Na Akajaalia mbingu kuwa ni paa lililohifadhiwa. Na kwamba Ameumba usiku na mchana. Na Ameumba jua na mwezi. Na kwamba Yeye Allaah (سبحانه وتعالى) Ndiye Mwenye kuhuisha na kufisha.
8-Suwrah imetaja khabari za baadhi ya Manabii ambao ni Muwsaa, Haaruwn, Ibraahiym, Is-haaq, Ya’quwb, Luutw, Nuwh, Daawuwd, Sulaymaan, Ayyuwb, Ismaa’iyl, Idriys, Dhul-Kifl, Yuwnus (Dhan-Nuwn) na Zakariyyaa (عليهم السلام).
9-Baada ya kutajwa Manabii Suwrah ikafuatilia kumtaja kwa kumsifia Maryam mama wa Nabiy ‘Iysaa (عليه السّلام).
10-Wametajwa Yaajuwj na Maajuwj kama ni miongoni mwa alama kubwa za Qiyaamah.
11-Imetahadharisha kuwa washirikina na waabudiwa wao wote wataingizwa moto wa Jahannam wadumu humo milele.
12-Kisha Suwrah imewabashiria Waja wema wa Allaah (سبحانه وتعالى) kwamba wao wataepushwa na moto, na wala hawatosikia mvumo wake, wala hautowahuzunisha mfazaiko mkubwa, bali watadumu katika Jannah ambamo humo watapata yale wanayotamani nafsi zao na kubashiriwa mema na Malaika.
13-Suwrah imekhitimishwa kwa kutajwa kwamba Nabiy Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم) ametumwa kuwa ni rehma kwa walimwengu wote na ikathibitisha tena Tawhiyd ya Allaah kwamba Yeye Allaah (سبحانه وتعالى) Pekee Anayestahiki kuabudiwa. Na maonyo kwa washirikina wakiendelea kukengeuka na kwamba Allaah (سبحانه وتعالى) Ndiye Mwenye Kuombwa msaada kwa yale wanayomvumishia.
Fadhila Za Suwrah:
Suwrah Al-Anbiyaa ni miongoni mwa Suwrah zilizotangulia kuteremshwa, na Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akazitaja kuwa ni pato lake la mwanzo:
حَدَّثَنَا آدَمُ، حَدَّثَنَا شُعْبَةُ، عَنْ أَبِي إِسْحَاقَ، قَالَ سَمِعْتُ عَبْدَ الرَّحْمَنِ بْنَ يَزِيدَ، سَمِعْتُ ابْنَ مَسْعُودٍ، يَقُولُ فِي بَنِي إِسْرَائِيلَ وَالْكَهْفِ وَمَرْيَمَ وَطَهَ وَالأَنْبِيَاءِ إِنَّهُنَّ مِنَ الْعِتَاقِ الأُوَلِ وَهُنَّ مِنْ تِلاَدِي.
Amesimulia ‘Abdur-Rahmaan bin Yaziyd (رضي الله عنه): Nimemsikia ‘Abdullaah bin Mas‘uwd (رضي الله عنه) akisema: Suwrah Bani Israaiyl, Al-Kahf, Maryam, Twaahaa na Al-Anbiyaa ndio miongoni mwa pato langu la kwanza na mali yangu kongwe, na (hakika ni) ndio mali yangu kongwe.” [Al-Bukhaariy]
022-Al-Hajj: Utangulizi Wa Suwrah
Alhidaaya.com [2]
Imeteremka: Makkah au Madiynah kwa kuwa ‘Ulamaa wamekhitilafiana kuteremshwa kwake. Wamesema kuwa, baadhi ya Aayah zimeteremka Makkah, na baadhi ya Aayah zimeteremka Madiynah.
Idadi Za Aayah: 78
Jina La Suwrah: Al-Hajj
Suwrah imeitwa Al-Hajj, na inayodalilisha ni kutajwa kuhusu Hajj na taratibu zake kuanzia Aayah namba (25) hadi (37).
Miongoni Mwa Makusudio Ya Suwrah:
1-Kumuadhimisha Allaah (سبحانه وتعالى), na kutukuza Ishara Zake. Na watu kuzikubali Amri zake. [Al-Mukhtaswar Fiy Tafsiyr Al-Qur-aan Al-Kariym]
2-Kuthibitisha kufufuliwa na hali za watu Siku ya Qiyaamah na jazaa njema za Waumini na jazaa mbaya za makafiri.
3-Kuibainisha Tawhiyd kwa Dalili Zake, na kukanusha ushirikina na kuradd mijadala yao.
4-Kubainisha Maajabu ya Uwezo Allaah (سبحانه وتعالى) ardhini.
5-Kubainisha manufaa ya Hajj ya duniani na Aakhirah, na kubainisha umuhimu wa kutukuza Ishara na Vitu Vitukufu vya Allaah (سبحانه وتعالى).
Miongoni Mwa Maudhui Ya Suwrah:
1-Suwrah imefunguliwa kwa kuamrisha kumcha Allaah (سبحانه وتعالى), na maelezo kuhusu uzito wa Siku ya Qiyaamah kama zilzala (tetemeko la ardhi) na kiwewe cha watu kitakavyokuwa Siku hiyo.
2-Imethibitishwa kufufuliwa kwa watu, kwa hoja na dalili ya uumbaji wa mwanaadamu, kuanzia udongo hadi tone la manii, na daraja za kuumbwa kwake tumboni hadi kuzaliwa kwake, na kuendelea hali yake hadi kufariki. Kisha ikapiga mfano wa ardhi kame inayomiminiwa maji ikahuika na kutoa mazao. Ikaendelea kuthibitisha kuwa Qiyaamah kitatokea tu na kwamba Allaah (سبحانه وتعالى) Atawafufua watu kutoka makaburini mwao.
3-Imetajwa mijadala ya washirikina na ibaada za wanafiki.
4-Imeabainisha Hukmu ya Allaah kati ya watu na dini zao na kwamba Allaah (سبحانه وتعالى) Atahukumu baina yao Siku ya Qiyaamah.
5-Imetajwa kuwa kila kitu hapa ulimwenguni kinamsujudia Allaah (سبحانه وتعالى) na wale wanaokana kumsujudia watastahiki adhabu.
6-Imebainishwa uwiano kati ya wawili waliogombana kwa ajili ya Rabb wao; Waumini na makafiri, pamoja na kubainisha mwisho wa kila mmoja kati yao.
7-Suwrah imetoa baadhi ya mwongozo wa Manaasik (taratibu na ibaada) ya Hajj, na manufaa yake ya duniani na Aakhirah, na amri ya kuwazuia washirikina wasiingie Masjidul-Haraam.
8-Wametahadharishwa watu na shirki na washirikina.
9-Imetolewa idhini kwa Waislamu ya kupigana Jihaad na kwamba Allaah (سبحانه وتعالى) Atawanusuru Waja Wake wanaonusuru Dini Yake.
10-Allaah (سبحانه وتعالى) Amemliwaza Rasuli Wake (صلى الله عليه وآله وسلم) kwa yale yaliyompata ya kukadhibishwa na kupingwa na watu wake, kwa kumkumbusha yaliyowapata nyumati za nyuma waliokadhibisha na kuwapinga Rusuli wao.
11-Wamebashiriwa rizki njema na Jannah wale waliohajiri na kufanya Jihaad.
12-Imethibitishwa Tawhiyd ya Allaah na Uwezo Wake wa: (i) Kuleta usiku na mchana (ii) Kuteremsha maji ardhini (iii) Kutiisha ardhi na bahari (iv) Kuzuia mbingu zisianguke. (v) Kuhuisha na kufisha. Kwa Neema zote hizo za Allaah na Uwezo Wake (سبحانه وتعالى), kuanzia Aayah (58) hadi (65), Aayah zikamalizia kwa kutajwa Majina Yake Mazuri mbalimbali na Sifa za Allaah (سبحانه وتعالى).
13-Umepigwa mfano wa kuthitisha Tawhiyd ya Allaah ya Ar-Rubuwbiyyah (Uola, Uumbaji n.k), kwamba wanaoabudiwa badala ya Allaah (سبحانه وتعالى), hawawezi kuumba nzi hata kama wote watajumuika kutaka kufanya! Na kwamba mfano wa hao wanaoabudiwa (walioshirikishwa) na wanaoabudu (washirikina) wote ni dhaifu! Na hakika Hawakumkadiria Allaah kama inavyostahiki kumkadiria.
14-Suwrah imekhitimishwa kwa amrisho la kufanya Jihaad, na kusimamisha Swalaah na kutoa Zakaa na kushikamana pamoja kwa ajili ya Allaah.
Fadhila Za Suwrah:
Suwrah hii ya Al-Hajj ni Suwrah pekee yenye Sajdatut-Tilaawah (Sijdah ya kisomo) mbili, ingawa Sijda ya pili wamekhitilafiana ‘Ulamaa kuhusu kuwajibika kwake.
023-Al-Muuminuwn: Utangulizi Wa Suwrah
Alhidaaya.com [2]
Imeteremka: Makkah kwa itifaki ya ‘Ulamaa.
Idadi Za Aayah: 118
Jina La Suwrah: Al-Muuminuwn
Suwrah imeitwa Al-Muuminuwn (Waumini), na inayodalilisha ni kutajwa katika Hadiyth iliyonukuliwa chini katika Faida. Na pia kutokana na neno hili kutajwa katika Aayah ya kwanza.
Miongoni Mwa Makusudio Ya Suwrah:
1-Kubainisha kufaulu kwa Waumini, na hasara kwa makafiri. [Al-Mukhtaswar Fiy Tafsiyr Al-Qur-aan Al-Kariym]
2-Kuthibitisha kufaulu kwa Waumini ambao sifa zao zimetajwa, na kwamba wao ndio wenye kufaulu duniani na Aakhirah.
3-Kueleza jinsi mwanaadam alivyoumbwa, na kubainisha hatua za maisha ya mwanaadam ambazo anazipitia hadi anaishia katika kifo kama hali ya wanaadamu wote.
4-Kuthibitisha Tawhiyd ya Allaah na kubatilisha ushirikina.
5-Kutajwa Neema nyingi za Allaah (سبحانه وتعالى) juu ya viumbe Vyake na kudhihirisha Uadhimu na Miujiza Yake.
6-Kuthibitisha Unabiy wa Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم) na kuwaraddi makafiri wanaopinga.
7-Tahadharisho la uchochezi wa shaytwaan na mwongozo wa kujikinga naye.
Miongoni Mwa Maudhui Ya Suwrah:
1-Suwrah imefunguliwa kwa kutajwa sifa za Waumini na ibaada zao, na waliyoandaliwa na Allaah (سبحانه وتعالى) ya Jannatul-Firdaws.
2-Imetajwa hatua za maumbile ya mwanaadam, zinazothibitisha uwezekano wa kufufuliwa kwake.
3-Imebainishwa baadhi ya Neema kadhaa za Allaah (سبحانه وتعالى) na baadhi ya mambo yanayoonyesha Uwezo wa Allaah (سبحانه وتعالى) hapa ulimwenguni.
4-Imetajwa sehemu fulani ya visa vya baadhi ya Rusuli, na misimamo yao pamoja na watu wao, na mwisho wao ulikuwaje.
5-Suwrah imewaelekeza Rusuli wale rizki za halali, na wadumishe kutenda mema, na kuoneysha kuwa Rusuli wote dini yao ilikuwa moja.
6-Imebainishwa misimamo ya washirikina dhidi ya daawah ya Kiislamu, na mafikio yao Siku ya Qiyaamah.
7-Imetajwa tena baadhi ya Neema za Allaah (سبحانه وتعالى) kwa Waja Wake kama kusikia, kuona na nyoyo za kutafakari.
8-Imebainishwa dalili zinazoonyesha kuwa Allaah (سبحانه وتعالى) ni Mmoja tu, na Muweza wa kila kitu kama kuhuisha na kufisha, na kuleta mabadiliko ya usiku na mchana.
9-Imetambulishwa kuwa washirikina waliamini Tawhiyd ya Ar-Rubuwbiyyah (Kumpwekesha Allaah katika Uola; yaani Yeye ni Rabb Anapaswa Kupwekeshwa katika Uumbaji, Ufalme, Uendeshaji, Utoaji Rizki, Uhuishaji, Ufishaji). Lakini walipinga Tawhiyd ya Al-Uluwhiyyah (Kumpwekesha Allaah (سبحانه وتعالى) katika ibaada). Basi Allaah (سبحانه وتعالى) Amekanusha kabisa waliyomshirikisha kwa kuthibitisha kwamba Hakujichukulia mwana wala Hana mshirika.
10-Imetolewa mwongozo kwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) juu ya kupuuza miamala mibaya ya washirikina na aizuie kwa kuwarudishia yaliyo bora, na ajilinde na shaytwaan.
11-Imetajwa majuto ya kafiri na mwenye kuasi, pindi atakapokuwa anatolewa roho, akitamani kurudi duniani atende mema, lakini hilo haliwezekani kabisa kwani baada ya hapo, kuna al-barzakh ambayo ni kipindi baina ya mtu kufariki hadi kufufuliwa.
12-Imetajwa hali ya washirikina na makafiri itakapokuwa Siku ya Qiyaamah, ya moto kuwababua nyuso zao, na sura zao kubadilika kabisa kuwa zina hali ya kutisha! Pia majuto yao ya kuwafanyia dhihaka Waumini walipokuwa duniani.
13-Suwrah imekhitimishwa kwa kutajwa lengo la kuumbwa binaadam, na Allaah (سبحانه وتعالى) Anajitukuza kwa Uluwa. Ikatajwa pia onyo la kumuomba asiyekuwa Allaah. Kisha amri kwa Rasuli Wake (صلى الله عليه وآله وسلم) (na Waumini) kuomba Rehma ya Allaah (سبحانه وتعالى) na Maghfirah.
Faida:
عَنْ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ السَّائِبِ، قَالَ صَلَّى بِنَا رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم الصُّبْحَ بِمَكَّةَ فَاسْتَفْتَحَ سُورَةَ الْمُؤْمِنِينَ حَتَّى إِذَا جَاءَ ذِكْرُ مُوسَى وَهَارُونَ - أَوْ ذِكْرُ مُوسَى وَعِيسَى ابْنُ عَبَّادٍ يَشُكُّ أَوِ اخْتَلَفُوا - أَخَذَتْ رَسُولَ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم سُعْلَةٌ فَحَذَفَ فَرَكَعَ وَعَبْدُ اللَّهِ بْنُ السَّائِبِ حَاضِرٌ لِذَلِكَ .
Amesimulia ‘Abdullaah Bin As-Saaib (رضي الله عنه): Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alituswalisha Swalaah ya Asubuhi Makkah akaanza kwa Suwrah Al-Muuminuwn (23), mpaka alipofikia kutajwa kwa Muwsaa na Haaruwn (Aayah 45) au kutajwa kwa Iysaa (Aayah 50). Ibn ‘Abbaad alitilia shaka au wasimulizi wengine wamekhitilafiana baina yao kwa neno hili la kikohozi kumshika Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akaacha (kisomo) akarukuu. ‘Abdullaah Bin Saaib alikuweko kushuhudia (tukio) hilo. [Sunan Abiy Daawuwd na riwaaya kama hiyo ya Muslim]
024-An-Nuwr: Utangulizi Wa Suwrah
Alhidaaya.com [2]
Imeteremka: Madiynah kwa itifaki ya ‘Ulamaa.
Idadi Za Aayah: 64
Jina La Suwrah: An-Nuwr
Suwrah imeitwa An-Nuwr (Mwanga), na inayodalilisha ni kutaja katika Hadiyth iliyonukuliwa chini katika Faida. Na pia kutokana na kutajwa katika Aayah namba (35):
اللَّـهُ نُورُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ ۚ
“Allaah Ni Nuru ya mbingu na ardhi.”
Miongoni Mwa Makusudio Ya Suwrah:
1-Kuwalingania watu juu ya kujizuia, na kuhifadhi heshima za watu. [Al-Mukhtaswar Fiy Tafsiyr Al-Qur-aan Al-Kariym]
2-Kumtakasa Mama wa Waumini ‘Aaishah (رضي الله عنها) kutokana na usingiziaji wa kashfa juu yake. Na hukmu za kuwasingizia machafu wanawake watwaharifu.
3-Kutajwa kwa hukmu ya kujizuia na maasi na yaliyoharamishwa.
4-Hukmu za Hijaab.
5-Kubainishwa maadili mema katika familia na katika jamii ya Kiislamu.
Miongoni Mwa Maudhui Ya Suwrah:
1-Suwrah imefunguliwa kwa kuthibitisha uwajibu wa kufuata Sharia Alizoziteremsha Allaah (سبحانه وتعالى), hukmu na adabu.
2-Kisha ikabainisha hukmu ya zinaa.
3-Imebainisha pia hukmu ya kuwasingizia (zinaa) wanawake wenye kujizuia na maachafu, na hukmu ya kusingiziana (zinaa) kwa wanandoa, na Sharia ya Liaan (kulaaniana).
4-Suwrah imemtakasa Mama wa Waumini ‘Aaishah (رضي الله عنها) kwa kuelezewa tukio la ifk (uzushi wa usingiziaji kashfa) na ikawafundisha Waumini adabu kwamba, wanaposikia jambo la uzushi wasiwe wenye pupa ya kuliamini mpaka wapatikane mashahidi wanne.
5-Imeongoza Waumini katika kuendelea kuwafanyia ihsaan wahitaji japokuwa jamaa hao wameingia makosani.
6-Suwrah imetoa mafunzo kwa waliojaaliwa uwezo, waendelee kuwasaidia wahitaji na kuwafanyia ihsaan, hata kama walimkosea mfadhili.
7-Imebainishwa kwamba kauli ovu inaendana na watu waovu, na watu waovu wanaendana na kauli ovu. Na kauli njema inaendana na watu wema, na watu wema wanaendana na kauli njema.
8-Suwrah imetoa maamrisho kwa Waumini wanaume na wanawake, kuwajibika kufumba macho na kuhifadhi tupu. Na pia kuna amri ya hijaab kwa Wanawake Waumini, kwa makatazo ya kuonyesha mapambo yao, isipokuwa kwa wale walioruhusiwa na Allaah (maharim wao).
9-Kuna maamrisho ya kuwaozesha wasio na uwezo wa kuoa na kuolewa.
10-Imeelezea Nuru ya Allaah (سبحانه وتعالى) ya mbingu na ardhi na imefafanua kwa mifano ya Nuru Yake. Na Nuru hiyo inapatikana Misikitini. Na imebainishwa kwamba Nuru ya Allaah Humfikia Muumin tu!
11-Imetoa mfano wa amali za makafiri kuwa kama ni sarabi (mazigazi), au kama giza ndani ya bahari yenye kina, na kwamba Aakhirah hatakuta malipo yoyote yale.
12-Imebainisha kwamba viumbe vilivyomo mbinguni na ardhini vinamsabbih Allaah (سبحانه وتعالى).
13-Imebainisha Uwezo wa Allaah (سبحانه وتعالى) wa kuumba viumbe, mbingu na ardhi na Neema Zake za kuteremsha mvua.
14-Imetaja kuzibughudhi hali za wanafiki.
15-Imetaja Ahadi ya Allaah (سبحانه وتعالى) kwa Waumini ya kuwapa utawala katika ardhi, na kuwaondosha katika khofu.
16-Suwrah imetajwa adabu kadhaa katika jamii na familia. Katika jamii kubisha hodi katika nyumba za watu. Na pia adabu za kula na kuingia majumbani. Adabu za kifamilia kama watoto kupiga hodi vyumbani mwa wazazi katika nyakati kadhaa.
17-Suwrah imekhitimishwa kwa kubainisha sifa za Waumini wa kweli na imewafunza Waumini adabu katika kumwita Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم).
Faida:
عَنِ الشَّيْبَانِيِّ، سَأَلْتُ عَبْدَ اللَّهِ بْنَ أَبِي أَوْفَى هَلْ رَجَمَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم قَالَ نَعَمْ. قُلْتُ قَبْلَ سُورَةِ النُّورِ أَمْ بَعْدُ قَالَ لاَ أَدْرِي.
Amesimulia Ash-Shaybaaniy (رضي الله عنه): Nilimuuliza Abdullaah bin Abiy Awfaa: Je, Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alitekeleza adhabu ya rajm (kupigwa mawe hadi kufa)? Akajibu: Naam. Nikasema: Kabla ya Suwrah An-Nuwr au baada yake? Akajibu: Sijui. [Al-Bukhaariy]
025-Al-Furqaan: Utangulizi Wa Suwrah
Alhidaaya.com [2]
Imeteremka: Makkah kwa itifaki ya ‘Ulamaa.
Idadi Za Aayah: 77
Jina La Suwrah: Al-Furqaan
Suwrah imeitwa Al-Furqaan (Pambanuo), na inayodalilisha ni kutajwa katika Hadiyth iliyonukuliwa chini katika Faida. Na pia kutajwa neno hilo la Al-Furqaan katika Aayah namba (1). Rejea Tanbihi yake yenye ufafanuzi wa maana ya Al-Furqaan.
Miongoni Mwa Makusudio Ya Suwrah:
1-Ushindi wa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) na Qur-an, na kuondosha shubha za washirikina. [Al-Mukhtaswar Fiy Tafsiyr Al-Qur-aan Al-Kariym]
2-Kupambanua baina ya haqq (haki) na baatwil na mwongozo wa kufuata haqq na kwamba mwenye kufuata atapata mafanikio ya duniani na neema za Jannah huko Aakhirah. Na maonyo ya adhabu ya moto wa Jahannam kwa wanaofuata baatwil.
3-Kuinua hadhi ya Quraan na kuthibitisha kuwa inatoka kwa Allaah (عزّ وجلّ), na kwamba imeteremshwa kwa ajili ya walimwengu wote. Na kuthibitisha Taadhima ya Aliyeiteremsha na kubainisha dalili za ukweli wake.
4-Kuthibitisha moyo wa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) na kumliwaza.
5-Kujulisha sifa za waja wa Ar-Rahmaan (Mwingi wa Rehma).
Miongoni Mwa Maudhui Ya Suwrah:
1-Suwrah imefunguliwa kwa Kumtukuza Allaah (تبارك وتعالى) na kumuelezea kwa Sifa zinazodalilisha Tawhiyd Yake ya Ar-Rubuwbiyyah (Uola, Uumbaji, Umiliki, Uendeshaji na kadhaalika) na Al-Uluwhiyyah (ibaada) kwamba Yeye Ndiye Mwabudiwa wa haki.
2-Suwrah imetaja simulizi za baadhi ya maneno ya washirikina, na shubha zao za kumpachika sifa ovu Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) pamoja na Qur-aan.
3-Imelinganisha kati ya mafikio mabaya ya washirikinana mafikio mazuri ya Waumini Siku ya Qiyaamah.
4-Imetaja sehemu ya visa vya baadhi ya Manabii pamoja na kaumu zao.
5-Imetaja baadhi ya matukio ya Siku ya Qiyaamah.
6-Suwrah imetaja kumliwaza Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) juu ya yale aliyoudhiwa na kudhikishwa kutoka kwa washirikina.
7-Imeelezea juu ya baadhi ya Neema za Allaah (سبحانه وتعالى) na Uwezo Wake katika kuendesha ulimwengu.
8-Imewaradd washirikina wasioamini Jina la Ar-Rahmaan.
9-Suwrah ikamalizia kwa kuelezea sifa za ‘Ibaadur-Rahmaan (Waja wa Mwingi wa Rehma); ibaada zao na wanayojiepusha nayo, na duaa zao, na ikataja mwishowe umuhimu wa kuomba duaa.
Faida:
حَدَّثَنَا عَبْدُ اللَّهِ بْنُ يُوسُفَ، أَخْبَرَنَا مَالِكٌ، عَنِ ابْنِ شِهَابٍ، عَنْ عُرْوَةَ بْنِ الزُّبَيْرِ، عَنْ عَبْدِ الرَّحْمَنِ بْنِ عَبْدٍ الْقَارِيِّ، أَنَّهُ قَالَ سَمِعْتُ عُمَرَ بْنَ الْخَطَّابِ ـ رضى الله عنه ـ يَقُولُ سَمِعْتُ هِشَامَ بْنَ حَكِيمِ بْنِ حِزَامٍ، يَقْرَأُ سُورَةَ الْفُرْقَانِ عَلَى غَيْرِ مَا أَقْرَؤُهَا، وَكَانَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم أَقْرَأَنِيهَا، وَكِدْتُ أَنْ أَعْجَلَ عَلَيْهِ، ثُمَّ أَمْهَلْتُهُ حَتَّى انْصَرَفَ، ثُمَّ لَبَّبْتُهُ بِرِدَائِهِ فَجِئْتُ بِهِ رَسُولَ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم فَقُلْتُ إِنِّي سَمِعْتُ هَذَا يَقْرَأُ عَلَى غَيْرِ مَا أَقْرَأْتَنِيهَا، فَقَالَ لِي " أَرْسِلْهُ ". ثُمَّ قَالَ لَهُ " اقْرَأْ ". فَقَرَأَ. قَالَ " هَكَذَا أُنْزِلَتْ ". ثُمَّ قَالَ لِي " اقْرَأْ ". فَقَرَأْتُ فَقَالَ " هَكَذَا أُنْزِلَتْ. إِنَّ الْقُرْآنَ أُنْزِلَ عَلَى سَبْعَةِ أَحْرُفٍ فَاقْرَءُوا مِنْهُ مَا تَيَسَّرَ ".
Amesimulia ‘Umar Bin Al-Khatwaab (رضي الله عنه): “Nilimsikia Hishaam ibn Hakiym akisoma Suwratul-Furqaan tofuati na vile ninavyoisoma na alivyonifundisha Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم). Nilikaribia kugombana naye juu ya hilo, lakini nikamvumilia mpaka akamaliza kisha nikamfunga nguo yake shingoni na kumvuta mpaka kwa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) nikasema: “Nimesikia huyu mtu akisoma (Suwratul-Furqaan) kinyume na ulivyonifundisha.” Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akasema: “Mwachie!” Akamwambia (Hishaam): “Soma. Akasoma. Akasema: “Hivi ndivyo ilivyoteremshwa.” Kisha akaniambia mimi: “Soma.” Nikasoma. Akasema: “Hivi ndivyo ilivyoteremshwa. Hakika Qur-aan imeteremshwa kwa Herufi saba, hivyo someni iliyokuwa sahali kwenu.” [Al-Bukhaariy, Muslim na wengineo]
026-Ash-Shu’araa: Utangulizi Wa Suwrah
Alhidaaya.com [2]
Imeteremka: Makkah kwa itifaki ya ‘Ulamaa.
Idadi Za Aayah: 227
Jina La Suwrah: Ash-Shu’araa
Suwrah imeitwa Ash-Shu’araa (Washairi), na inayodalilisha ni kutajwa katika Aayah namba (224).
Miongoni Mwa Makusudio Ya Suwrah:
1-Kubainisha dalili za uwepo wa Allaah (سبحانه وتعالى) katika kuwaunga mkono Rusuli, na kuwaangamiza wanaokadhibisha. [Al-Mukhtaswar Fiy Tafsiyr Al-Qur-aan Al-Kariym]
2-Kuipa heshima na kuitukuza Qur-aan, na kuonyesha kushindwa kwa washirikina juu ya kuipinga kwao.
3-Kuelezewa visa vya baadhi ya Rusuli pamoja na waliyofanyiwa na watu wao na maangamizi ya Allaah kwa watu hao.
4-Kumliwaza Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) kwa maudhi aliyokutana nayo kutoka kwa watu wake.
Miongoni Mwa Maudhui Ya Suwrah:
1-Suwrah imefunguliwa kwa herufi zinazojulikana kama الحروف المقطعة (Al-Huruwf Al-Muqatw-twa’ah), ambazo hakuna ajuaye maana zake isipokuwa Allaah (سبحانه وتعالى). Rejea Al-Baqarah (2:1). Kisha imebainishwa Utukufu wa Qur-aan, na kutaja misimamo ya washirikina kuhusu Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم), na kumliwaza (صلى الله عليه وآله وسلم) kutokana na maudhi waliyomfanyia watu wake.
2-Imeelezea kwa kiasi, kisa cha Nabiy Muwsaa na ndugu yake Haaruwn (عليهما السلام), na Firawni na kisa cha wachawi walioamini. Kisha ikaelezewa hatima ya Firawni ya kugharakishwa baharini na jeshi lake kwa namna ya muujiza mkubwa! Na kuokolewa Nabiy Muwsaa (عليه السلام) na kaumu yake.
3-Imeelezwa dawaah ya Nabiy Ibraahiym (عليه السلام) kumlingania baba yake.
4-Imetajwa kisa cha Nabiy Nuwh (عليه السلام) na daawah ya kuwalingania watu wake, na kilichotokea kwa kuangamizwa wale waliompinga na kuokolewa Waumini.
5-Vimetajwa visa vinginevyo vya baadhi ya Rusuli akiwemo: Huwd, Swaalih, Luutw, na Shu’ayb (عليهم السلام) na yale yaliyowapata kutoka kwa watu wao.
6-Imetajwa heshima ya Qur-aan, na ushuhuda wa Ahlul-Kitaab juu ya Qur-aan, na kwamba imetakasika na kuepukana kuwa kama mashairi na maneno ya mashaytwaan.
9-Imetajwa kuamrishwa kwa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) kutakiwa kuwaonya jamaa zake wa karibu, na kwamba adhabu ni mafikio ya madhalimu.
027-An-Naml: Utangulizi Wa Suwrah
Alhidaaya.com [2]
Imeteremka: Makkah kwa itifaki ya ‘Ulamaa.
Idadi Za Aayah: 93
Jina La Suwrah: An-Naml
Suwrah imeitwa An-Naml (Sisimizi), na inayodalilisha ni kutajwa katika Aayah namba (18).
Miongoni Mwa Makusudio Ya Suwrah:
1-Shukurani na fadhila kwa Nabiy (صلى الله عليه وسلم) kwa neema ya Qur-aan, kuishukuru (neema hiyo), na subra juu ya kuifikisha. [Al-Mukhtaswar Fiy Tafsiyr Al-Qur-aan Al-Kariym]
2-Kushukuru Neema za Allaah (سبحانه وتعالى) na kwamba mwenye kushukuru anashukuru kwa manufaa ya nafsi yake kwani Allaah ni Mkwasi.
3-Kumwamini Allaah (سبحانه وتعالى), kumwabudu bila kumshirikisha na kuamini Wahy na Aakhirah, kuamini mambo ya ghaibu, na kuamini kwamba Allaah Ndiye Mtoaji Rizki.
4-Kuthibitisha Tawhiyd ya Allaah (سبحانه وتعالى) na Ni Muweza wa kila kitu na jinsi gani Allaah (سبحانه وتعالى) Anaweza kumuongoza Mja Wake.
Miongoni Mwa Maudhui Ya Suwrah:
1-Suwrah imefunguliwa kwa herufi zinazojulikana kama الحروف المقطعة (Al-Huruwf Al-Muqatw-twa’ah), ambazo hakuna ajuaye maana zake isipokuwa Allaah (سبحانه وتعالى). Rejea Al-Baqarah (2:1). Kisha imethibitishwa kwamba Qur-aan ni Kitabu Kinachobainisha wazi, na ni mwongozo na bishara kwa Waumini, na zikatajwa sifa za Waumini hao. Kisha ikabainishwa kuhusu makafiri wasioamini, kwamba watapata adhabu ovu na watakuwa wenye kukhasirika.
2-Imethibitisha kuwa Qur-aan ndio tegemeo kwa Vitabu vilivyotangulia na kwamba Qur-aan inawaongoa watu na imehabarisha visa na matukio ya watu waliopita.
3-Imeelezewa kwa kifupi kisa cha Nabiy Muwsaa (عليه السّلام).
4-Kisha Suwrah ikataja kisa cha Nabiy Sulaymaan (عليه السّلام) na kisa cha sisimizi aliyewatanabahisha wenzake waingie haraka masikanini mwao wasije kupondwa na jeshi la Nabiy Sulaymaan (عليه السّلام).
5-Imetaja kisa cha ndege hud-hud na mfalme wa Saba-a na watu wake na alivyoifanyia daawah Tawhiyd ya Allaah (سبحانه وتعالى). Kisha pindi Nabiy Sulaymaan alimpompelekea barua mfalme wa Saba-a kumlingania Uislamu akaanza barua yake kwa:
بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ
6-Imetaja pia visa vya Nabiy Muwsa, Swaalih, na Luutw (عليهم السلام), na waliyoyapata kwa watu wao.
7-Imebainisha kwa dalili za wazi ya kwamba Allaah (سبحانه وتعالى) Ni Mmoja na Akabainisha Neema Zake kadhaa ikiwemo neema ya kuwa Allaah (سبحانه وتعالى) Anaitikia duaa ya mwenye dhiki mno.
8-Imetaja baadhi ya alama za Qiyaamah.
9-Suwrah imekhitimishwa kwa amri kumwabudu Allaah (سبحانه وتعالى) na kuisoma Qur-aan.
028-Al-Qaswasw: Utangulizi Wa Suwrah
Alhidaaya.com [2]
Imeteremka: Makkah kwa itifaki ya ‘Ulamaa.
Idadi Za Aayah: 88
Jina La Suwrah: Al-Qaswasw
Suwrah imeitwa Al-Qaswasw (Visa), na inayodalilisha ni kutajwa neno hili katika Aayah namba (25).
Miongoni Mwa Makusudio Ya Suwrah:
1-Desturi ya Allaah katika kuwamakinisha Waumini wanyonge, nakuwaangamiza waovu wenye kiburi. [Al-Mukhtaswar Fiy Tafsiyr Al-Qur-aan Al-Kariym]
2-Kubainisha Uwezo wa Allaah (سبحانه وتعالى) katika kuwaangamiza madhalimu na wadanganyifu, hata kama watazitegemea nguvu zote za ardhini.
3-Kuwapa thabati Waumini na kuwapa bishara ya kwamba mwisho mwema ni wa kwao.
4-Kunyenyekea kwa Allaah (سبحانه وتعالى) kwa kujisalimisha kwa kila jambo.
Miongoni Mwa Maudhui Ya Suwrah:
1-Suwrah imefunguliwa kwa herufi zinazojulikana kama الحروف المقطعة (Al-Huruwf Al-Muqatw-twa’ah), ambazo hakuna ajuaye maana zake isipokuwa Allaah (سبحانه وتعالى). Rejea Al-Baqarah (2:1). Kisha ikathibitishwa kwamba Qur-aan ni Kitabu kinachobainisha wazi.
2-Imetaja uovu na ufisadi wa Firawni, na Ahadi ya Allaah (سبحانه وتعالى) ya kuwaangamiza wanaofanya ufisadi.
3-Suwrah imetaja kisa cha kuzaliwa Nabiy Muwsaa (عليه السلام), Ulinzi wa Allaah (سبحانه وتعالى) kwake pindi alipotiwa sandukuni akatupwa katika mto wa Nile akafika kupelekwa kwenye qasri la Firawni na mkewe akampenda na kumtaka kumlea. Pia jinsi Allaah (سبحانه وتعالى) Alivyopanga kwa hikma Akajaalia Nabiy Muwsaa (عليه السّلام) kurudishwa kwa mama yake ili amnyonyeshe.
4-Imetajwa matukio ya wakazi wa Misri na Bani Israaiyl. Na kuhama kwa Nabiy Muwsaa (عليه السّلام) kutoka Misri kuelekea Madyan. Kisha kisa chake cha kuwasaidia wanawake wawili kunywesha mifugo yao, kumfikia mja mwema na kumhadithia Al-Qaswasw (Visa), na kuoa binti mmoja wa mja mwema huyo, kuwa ni malipo ya kufanya kazi kwake.
5-Imetaja Nabiy Muwsaa (عليه السّلام) alipofika katika sehemu iliyobarikiwa akaongea na Allaah (سبحانه وتعالى) na akaamrishwa kwenda kwa Firawni kumlingania.
6-Imetajwa kumliwaza Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) kwa yaliyomsibu kutoka kwa watu wake. Na ikabainisha kwamba hii Qur-aan inatoka kwa Allaah, na kwamba Rasuli kamwe hana uwezo wa kumhidi amtakae, na kwamba uongofu unatoka kwa Allaah.
7-Imetaja kisa cha Qaaruwn na uovu wake kwa watu wa Nabiy Muwsaa (عليه السلام), na kudanganyika kwake na mali zake, na ikataja adhabu yake ya kudidimizwa ardhini kuwa ndio mwisho wa uovu na kiburi.
8-Suwrah imekhitimishwa kwa kuamrishwa kufanya ibaada kwa ikhlaasw, na kukataza ushirikina.
029-Al-‘Ankabuwt: Utangulizi Wa Suwrah
Alhidaaya.com [2]
Imeteremka: Makkah kwa itifaki ya ‘Ulamaa.
Idadi Za Aayah: 69
Jina La Suwrah: Al-‘Ankabuwt
Suwrah imeitwa Al-‘Ankabuwt (Buibui), na inayodalilisha ni kutajwa katika ayah namba (41).
Miongoni Mwa Makusudio Ya Suwrah:
1-Maamrisho juu ya kuvuta subira na kuthibiti wakati wa mitihani na fitnah, na kubainisha mwisho wa hayo yote. [Al-Mukhtaswar Fiy Tafsiyr Al-Qur-aan Al-Kariym]
2-Kutajwa kwamba Muumini lazima apitie mitihani ili athibitishe imaan yake, na kubainisha hali zao duniani na Aakhirah, na kubainisha kati ya Waumini wa kweli na waongo na wanafiki
3-Kuamrisha mema na kukataza munkari (maovu), na kujadiliana na Ahlul-Kitaab kwa njia bora.
4-Kuwaahidi Waumini ushindi, na kuwaahidi washirikina adhabu na kuwadhalilisha na kuwatolea mfano washirikina kuchukua walinzi wasiokuwa Allaah, ambao ni utando wa buibui, na hapa kuna marejeo ya wale wanaotegemea juu ya nguvu za sanamu.
Miongoni Mwa Maudhui Ya Suwrah:
1-Suwrah imefunguliwa kwa herufi zinazojulikana kama الحروف المقطعة (Al-Huruwf Al-Muqatw-twa’ah), ambazo hakuna ajuaye maana zake isipokuwa Allaah (سبحانه وتعالى). Rejea Al-Baqarah (2:1). Kisha ikabainishwa uhakika wa imaan, na Desturi ya Allaah ya Kuwapa mitihani Waja Wake, na kubainisha mwisho mwema wa Waumini, na mwisho mbaya wa makafiri na wanafiki.
2-Imetaja sehemu fulani ya nyumati za nyuma na adhabu zao. Miongoni mwao ni kaumu ya Nuwh, Ibraahiym, Luutw, Shu’ayb, Huwd, Swaalih na Muwsaa (عليهم السلام). Kisha ikabainisha aina za adhabu za kila mmoja wao na mwisho wao mbaya kwa kuwakadhibisha Rusuli hawa.
3-Allaah (سبحانه وتعالى) Amewapigia mfano hali ya washirikina kuwa ni sawa na buibui ambae amejijengea nyumba ambayo ni dhalili mno kuliko zote, haimkingi kwa jua wala mvua. Basi ni sawa na hao wanaowaabudu pasi na Allaah.
4-Maamrisho ya kuisoma Qur-aan na kusimamisha Swalaah.
5-Makatazo ya kujadiliana na Ahlul-Kitaabi isipokuwa kwa njia nzuri.
6-Imesimamisha baadhi ya hoja na dalili ya kwamba Qur-aan imetoka kwa Allaah.
7-Imebainisha mapungufu ya washirikina, kwani wao wanakiri kuwa Allaah ndio Muumba wa mbingu na ardhi, lakini pamoja na hayo bado wanaendelea kumshirikisha.
8-Suwrah imekhitimishwa kwa kuwaahidi Waumini ambao wamepigana Jihaad kwa ajili ya Allaah, watapata uongofu na watakuwa na mwisho mwema.
030-Ar-Ruwm: Utangulizi Wa Suwrah
Alhidaaya.com [2]
Imeteremka: Makkah kwa itifaki ya ‘Ulamaa.
Idadi Za Aayah: 60
Jina La Suwrah: Ar-Ruwm
Suwrah imeitwa Ar-Ruwm (Nchi ya Roma), na inayodalilisha ni kutajwa Warumi katika Aayah namba (2).
Miongoni Mwa Makusudio Ya Suwrah:
1-Msisitizo kwamba Allaah (سبحانه وتعالى) Ni Mfanyaji wa kila jambo Peke Yake, na kubainisha Desturi ya Allaah kwa Viumbe Wake. [Al-Mukhtaswar Fiy Tafsiyr Al-Qur-aan Al-Kariym]
2-Allaah (سبحانه وتعالى) Kuwabashiria Waja Wake kwamba watawashinda Wamajusi wa Waajemi, na kuthibitisha kwamba ushindi hauji kwa idadi au vifaa, bali ni kutoka kwa Allaah (سبحانه وتعالى) Pekee, Humsaidia Amtakaye, na Humshinda Amtakaye.
3-Kuweka wazi dalili za Tawhiyd ya Allaah (سبحانه وتعالى) na kubatilisha ushirikina.
4-Kuthibitisha uwepo wa kufufuliwa na malipo ya Aakhirah.
Miongoni Mwa Maudhui Ya Suwrah:
1-Suwrah imefunguliwa kwa herufi zinazojulikana kama الحروف المقطعة (Al-Huruwf Al-Muqatw-twa’ah), ambazo hakuna ajuaye maana zake isipokuwa Allaah (سبحانه وتعالى). Rejea Al-Baqarah (2:1). Kisha imetoa khabari kuhusu vita vya Ruwm na Fursi, na Ahadi ya Allaah (سبحانه وتعالى) ya kumalizika vita kwa kushinda Wafursi, na kwamba, Warumi watawashinda Wafursi baada ya miaka michache. Na hii bila ya shaka ilihakiki.
2-Imewataka makafiri juu ya kufikiria vile Alivyoviumba Allaah; mbingu na ardhi na vilivyomo, na watembee ili wajionee jinsi watu wa mwanzo walivyoangamizwa.
3-Imetajwa baadhi ya yatakayojiri Siku ya Qiyaamah, na mafikio ya Waumini na makafiri.
4-Zimekariri Aayah za Allaah zinazobainisha Ishara na Dalili za Tawhiyd ya Allaah (سبحانه وتعالى) ya Uumbaji Wake na Ishara nyenginezo
5-Imetajwa Uwezo wa Allaah wa kuumba viumbe na kuwafufua nayo ni mepesi mno kwa Allaah (سبحانه وتعالى).
6-Imetajwa mahimizo ya kushikamana na Dini Haniyfah (iliyoelemea katika haki) na kuifata, na makatazo ya kufata njia ya washirikina.
7-Imebainisha hali ya washirikina wanapofikwa na shida humuomba Allaah kwa kurudi Kwake kisha wanapoondoshewa shida zao, wanarudi kumshirikisha Allaah.
8-Imetaja kuwa ufisadi unaodhihirika ardhini ni kutokana na makosa wanayoyachuma watu wenyewe na itawafuatilia adhabu.
9-Imebainishwa Rehma na Neema za Allaah (سبحانه وتعالى); miongoni mwazo ni Kuwaruzuku waja na Kuwapelekea pepo za rehma zenye kuteremsha mvua katika ardhi iliyokufa, kisha ikarudi kufufuka, basi hii ni Ishara na Dalili ya wazi ya Uwezo wa Allaah kuwafufua viumbe.
10-Imebainishwa ukaidi wa makafiri na kwamba Allaah Amewapigia mifano kila aina lakini bado wamekufuru.
11-Suwrah imekhitimishwa kwa Amri ya Allaah kumuamrisha Rasuli Wake (صلى الله عليه وآله وسلم) kuvuta subira na kuthibitika katika Dini.
031-Luqmaan: Utangulizi Wa Suwrah
Alhidaaya.com [2]
Imeteremka: Makkah kwa itifaki ya ‘Ulamaa.
Idadi Za Aayah: 34
Jina La Suwrah: Luqmaan
Suwrah imeitwa Luqmaan, na inayodalilisha ni kutajwa mja mwema huyo katika Aayah namba (12-13).
Miongoni Mwa Makusudio Ya Suwrah:
1-Amri juu ya kufata hikma iliyokuja kwenye Qur-aan, na tahadhari kwa atakaeipuuza. [Al-Mukhtaswar Fiy Tafsiyr Al-Qur-aan Al-Kariym]
2-Kuthibitisha na kuisifu Qur-aan Tukufu katika sifa mbali mbali ikiwemo sifa ya hikma, na ambayo inahitaji hikma ya Aliyeiteremsha (سبحانه وتعالى), katika Maneno na Matendo Yake. Na kisa cha Luqmaan aliyejaaliwa hikma na Allaah (سبحانه وتعالى), ambaye ndio jina la Suwrah hii, ni mojawapo ya ushahidi wa wazi wa hili.
3-Kuwasifia Waumini kwa sifa mbalimbali.
4-Kuisemesha nafsi ya mwanaadam kwa mambo yatayoifanya iishi vizuri na maisha ya raha.
Miongoni Mwa Maudhui Ya Suwrah:
1-Suwrah imefunguliwa kwa herufi zinazojulikana kama الحروف المقطعة (Al-Huruwf Al-Muqatw-twa’ah), ambazo hakuna ajuaye maana zake isipokuwa Allaah (سبحانه وتعالى). Rejea Al-Baqarah (2:1). Kisha imtukuzwa Qur-aan kuwa ni ya hikma, na kwamba Qur-aan ni mwongozo kwa watu, na ni rehma kwa Waumini, Wahisani pamoja na kutajwa sifa zao.
2-Ikataja baadhi ya sifa ya washirikina, ambao wanazifanyia mchezo Aayah za Allaah.
3-Imetaja dalili za Tawhiyd ya Allaah (سبحانه وتعالى) ya Uumbaji Wake na Uwezo Wake wa kuumba mbingu bila ya kuwa na nguzo, na kuumba ardhi na vilivyomo humo pamoja na Neema Zake humo kwa watu.
4-Imetajwa kisa cha Luqmaan na hikma alizojaaliwa nazo; miongoni mwazo ni wasia wake kwa mwanawe uliokusanya daawah ya Tawhiyd na kusimamisha Swalaah, na tabia njema, na kutokuwa na kiburi.
5-Imetajwa kuwa kuna Neema za Allaah (سبحانه وتعالى) zenye kuonekana na zisizoenekana.
6-Imetajwa kumliwaza Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) juu ya kutowaamini washirikina.
7-Imetajwa zingatio kubwa la kuwa Maneno ya Allaah (سبحانه وتعالى) ni mengi mno hayawezi kuhesabika wala kumalizika wala hayana mwisho!
8-Imewalingia watu wote kuwa na taqwa ya Allaah, na kutodanganyika na dunia.
9-Suwrah imekhitimishwa kwa kutaja mambo matano ya ghaibu ambayo hakuna ayajuae isipokuwa Mwenyewe Allaah (سبحانه وتعالى).
032-As-Sajdah: Utangulizi Wa Suwrah
Alhidaaya.com [2]
Imeteremka: Makkah kwa itifaki ya ‘Ulamaa.
Idadi Za Aayah: 30
Jina La Suwrah: As-Sajdah
Suwrah imeitwa As-Sajdah (Sijda), na inayodalilisha ni kutajwa katika Hadiyth iliyonukuliwa chini katika Fadhila.
Miongoni Mwa Makusudio Ya Suwrah:
1-Ubainisho wa uhakika wa viumbe, na hali za watu duniani na Aakhirah. [Al-Mukhtaswar Fiy Tafsiyr Al-Qur-aan Al-Kariym]
2-Kubainisha Utukufu wa Allaah (سبحانه وتعالى) na Sifa Zake Kamilifu, na Uwezo Wake katika Kuumba, Kudabiri mambo, Kufufua na malipo.
3-Kuinua utajo wa Qur-aan, kwani hiyo ndio iliyokusanya kila aina ya uongofu.
Miongoni Mwa Maudhui Ya Suwrah:
1-Suwrah imefunguliwa kwa herufi zinazojulikana kama الحروف المقطعة (Al-Huruwf Al-Muqatw-twa’ah), ambazo hakuna ajuaye maana zake isipokuwa Allaah (سبحانه وتعالى). Rejea Al-Baqarah (2:1). Kisha imetukuzwa Qur-aan kwamba haina shaka ndani yake, na kwamba imeteremshwa na Rabb wa ulimwengu, na kuwapinga washirikina wanaodai kuwa imetungwa.
2-Imetajwa kuwa Allaah (سبحانه وتعالى) Ndiye Aliyeumba mbingu na ardhi na kubainisha baadhi ya mambo yanayoonyesha Uwezo Wake.
3-Imeweka wazi baadhi ya hoja za makafiri katika kupinga kwao kufufuliwa pamoja na kuwaraddi kwenye hilo.
4-Imetajwa baadhi ya mambo ya Siku ya Qiyaamah hasa kwa watu waovu wakiwa mbele ya Allaah (سبحانه وتعالى) .
5-Imetajwa baadhi ya sifa za Waumini, na waliyoahidiwa na Allaah (سبحانه وتعالى) Peponi katika Neema Zake.
6-Imetajwa kuwa Waumini hawako sawa na mafasiki na ikatajwa malipo yao; Waumini watapata Jannaat na makazi mazuri na takrima humo. Mafasiki makazi yao yatakuwa ni motoni.
7-Imetajwa kuhusu Nabiy Muwsaa (عليه السلام), na Neema aliyopewa na Allaah (سبحانه وتعالى) ya kupewa Tawraat.
8-Da’wah kwa washirikina kutakiwa waizingatie na kutafakari Qur-aan.
9-Simulizi za baadhi ya ujinga wa washirikina.
10-Suwrah imekhitimishwa kwa kuamrishwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) kuwapuuza washirikina na kujitenga nao.
Fadhila Za Suwrah:
Ni Sunnah kuisoma Suwrah As-Sajdha katika Swalaah ya Alfajiri siku ya Ijumaa:
عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ ـ رضى الله عنه ـ قَالَ كَانَ النَّبِيُّ صلى الله عليه وسلم يَقْرَأُ فِي الْجُمُعَةِ فِي صَلاَةِ الْفَجْرِ الم * تَنْزِيلُ السَّجْدَةَ وَ هَلْ أَتَى عَلَى الإِنْسَانِ
Amesimulia Abuu Hurayrah (رضي الله عنه): Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alikuwa akisoma katika Swalaah ya Alfsjiri siku ya Ijumaa:
الم ﴿١﴾ تَنزِيلُ
As-Sajdah (32) na
هَلْ أَتَىٰ عَلَى الْإِنسَانِ
Suwrah Al-Insaan (76). [Al-Bukhaariy, Muslim na wengineo]
033-Al-Ahzaab: Utangulizi Wa Suwrah
Alhidaaya.com [2]
Imeteremka: Madiynah kwa itifaki ya ‘Ulamaa.
Idadi Za Aayah: 73
Jina La Suwrah: Al-Ahzaab
Suwrah imeitwa Al-Ahzaab (Makundi Yaliyoshirikiana), na inayodalilisha ni kutajwa katika Hadiyth iliyonukuliwa katika Faida, na pia kutajwa katika Aayah namba (20) makundi ya washirikina waliokusanyika kuzunguka mji wa Madiynah kutaka kuwapiga vita Waislamu.
Na pia Suwrah imeitwa Al-Khandaq (Shimo) kutokana na uchimbaji wa Khandaq kuizunguka Madiynah kwa ajili ya kuwazuia washirikina kutokuingia mjini kuwapiga vita.
Miongoni Mwa Makusudio Ya Suwrah:
1-Ubainisho juu ya Allaah (سبحانه وتعالى) kushughulikia jambo la Nabiy Wake (صلى الله عليه وآله وسلم) na kumhami yeye pamoja na watu wa nyumbani mwake. [Al-Mukhtaswar Fiy Tafsiyr Al-Qur-aan Al-Kariym]
2-Mahimizo juu ya kumuelekea Muumba, bila kuangalia nafasi ya Viumbe na heshima zao.
3-Kubainisha Ulinzi wa Allaah kwa Nabiy Wake (صلى الله عليه وآله وسلم).
4-Kuwekwa wazi hukmu nyingi za Sharia na adabu za kijamii, kwa mujibu wa Uislamu.
Miongoni Mwa Maudhui Ya Suwrah:
1-Suwrah imefunguliwa kwa wito kwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) juu ya kumcha Allaah na kutowatii makafiri na wanafiki.
2-Imeharamishwa baadhi ya mila na desturi ambazo zilikuwa zimetangaa kwenye jamii yao, kama vile dhwihaar (aina ya talaka ambapo mume anamwambia mkewe: “Wewe kwangu ni kama mgongo wa mama yangu” na hivyo kumfanya kuwa ni haraam kwake kujamiana naye), na at-tabanniy (mtoto wa kumlea ukamuunganisha na nasabu yako).
3-Imetajwa baadhi ya hukumu za Sharia, kama vile: kumtii Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم), na pia imeelezewa kwamba Wake zake ni Mama wa Waumini, na kubatilisha watu kurithiana kwa njia ya undugu (wa kuunganisha).
4-Imetajwa matukio ya Vita vya Ahzaab na pia kuhusu Bani Quraydhwah, na matokeo ya mwisho wa vita.
5-Imetajwa kuhusu kufadhilishwa wake wa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم), na kubainisha ubora wao, na kutolewa mwongozo kwao.
6-Imetajwa sifa kadhaa za Waumini ambazo mwishowe wameahidiwa maghfirah na ujira adhimu.
7-Imetajwa kisa cha kuozeshwa kwa Zaynab Bint Jahsh (رضيَ الله عنها), baada ya kuachwa na Zayd Bin Haarithah (رضي الله عنه), na hekima yake ni kubatilisha athari za at-tabanniy (watoto wa kuwalea wasiwe sawa na watoto wa kuwazaa).
8-Imethibitishwa kuwa Nabiy Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم) hakubakia kuwa ni baba wa yeyote na kuthibitishwa kuwa yeye ni Nabiy wa mwisho.
9-Amri ya kukithirisha kumdhukuru Allaah (سبحانه وتعالى) na kumsabbih na fadhila zake.
10-Imebainishwa hukmu ya talaka kwa mke asiye ingiliwa.
11-Amri ya kumswalia Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم).
12-Imetajwa laana ya Allaah kwa wanaomuudhi Allaah na Rasuli Wake (صلى الله عليه وآله وسلم), na wanaowaudhi Waumini, na tahadharisho kuwa wasipokoma hatima yao ni kama ilivyo Desturi ya Allaah.
13-Amri ya vazi la hijaab kwa Waumini wanawake.
14-Imetajwa majuto ya watu Siku ya Qiyaamah kuwafuata wakubwa wao waliowapoteza duniani.
15-Suwrah imekhitimishwa kwa kubainishwa mwanaadam kukubali kuibeba amana.
Faida:
عَنِ الزُّهْرِيِّ، قَالَ أَخْبَرَنِي خَارِجَةُ بْنُ زَيْدِ بْنِ ثَابِتٍ، أَنَّ زَيْدَ بْنَ ثَابِتٍ، قَالَ لَمَّا نَسَخْنَا الصُّحُفَ فِي الْمَصَاحِفِ فَقَدْتُ آيَةً مِنْ سُورَةِ الأَحْزَابِ، كُنْتُ أَسْمَعُ رَسُولَ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم يَقْرَؤُهَا، لَمْ أَجِدْهَا مَعَ أَحَدٍ إِلاَّ مَعَ خُزَيْمَةَ الأَنْصَارِيِّ، الَّذِي جَعَلَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم شَهَادَتَهُ شَهَادَةَ رَجُلَيْنِ مِنَ الْمُؤْمِنِينَ رِجَالٌ صَدَقُوا مَا عَاهَدُوا اللَّهَ عَلَيْهِ
Amesimulia Zayd Bin Thaabit (رضي الله عنه) amesema: Tulipokuwa tunakusanya nyaraka katika Mswahafu, niliikosa Aayah katika Suwrah Al-Ahzaab niliyokuwa nikimsikia Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akiisoma. Sikuipata Aayah hiyo kwa yeyote isipokuwa kwa Khuzaymah Al-Answaariy ambaye Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alijaalia kuwa ushahidi wake ni sawa na ushahidi wa watu wawili. (Na Aayah yenyewe ni):
مِّنَ الْمُؤْمِنِينَ رِجَالٌ صَدَقُوا مَا عَاهَدُوا اللَّـهَ عَلَيْهِ ۖ
“Miongoni mwa Waumini, wapo wanaume waliotimiza kikweli waliyoahidiana na Allaah.” [Al-Ahzaab (33:23) – Hadiyth ameipokea Imaam Al-Bukhaariy]
034-Saba-a: Utangulizi Wa Suwrah
Alhidaaya.com [2]
Imeteremka: Makkah kwa itifaki ya ‘Ulamaa.
Idadi Za Aayah: 54
Jina La Suwrah: Saba-a
Imeitwa Saba-a (Mji wa Yemen), na inayodalilisha ni kutajwa kisa cha watu wake katika Aayah namba (15).
Miongoni Mwa Makusudio Ya Suwrah:
1-Kubainisha hali za watu wanapopata neema (wakaikufuru), na Desturi za Allaah katika kuibadilisha hali hiyo (ya neema). [Al-Mukhtaswar Fiy Tafsiyr Al-Qur-aan Al-Kariym]
2-Kubatilisha ushirikina na kuwapinga washirikina.
3-Kubainisha Tawhiyd ya Allaah (سبحانه وتعالى) kwa dalili na ukweli wa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم).
Miongoni Mwa Maudhui Ya Suwrah:
1-Suwrah imefunguliwa kwa Kumhimidi Allaah (سبحانه وتعالى) Aliyetakasika na kila mapungufu, Mmiliki wa vilivyomo mbinguni na ardhini, na kubainisha upana (kuenea) wa Ilimu Yake.
2-Imebainisha kwamba washirikina wanapinga Siku ya Qiyaamah na kufufuliwa, na baadhi ya maneno yao ya yaliyokuwa ni baatwil.
3-Imetajwa sehemu fulani ya kisa cha Nabiy Daawuwd (عليه السّلام) na mwanawe Sulaymaan (عليه السّلام) na neema na fadhila zake za kutiishiwa majini.
4-Imetajwa kisa cha kabila la Saba-a waliokufuru Neema za Allaah (سبحانه وتعالى) na hatima yao.
5-Imebainishwa Tawhiyd ya Allaah (سبحانه وتعالى) na kwamba Yeye Ndiye Mwenye kuruzuku waja.
6-Imebainishwa kwamba Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) ametumwa kwa watu wote ulimwenguni na sio Waarabu pekee.
7-Imetajwa baadhi ya matukio ya Siku ya Qiyaamah, na mijadala itayokuwepo kati ya wafuasi na wanaofuatwa.
8-Radd kwa matajiri ambao walidai kuwa mali zao na watoto wao vitawanufaisha Siku ya Qiyaamah.
9-Imetajwa baadhi ya ada za washirikina kutokuamini Qur-aan na kutokumuamini Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم).
10-Daawah kwa makafiri ya kuwataka waifikirie sana Daawah ya Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم).
11-Suwrah imekhitimishwa kwa kuwatisha makafiri ya kwamba watakuwa na mwisho mbaya, kama wataendelea na misimamo yao ya ukafiri na ukaidi.
Faida:
Suwrah Saba-a (34), ni miongoni mwa Suwrah tano zinazoanzia kwa AlhamduliLlaah. Nyenginezo ni Al-Faatihah (1), Al-An’aam (6), Al-Kahf (18), na Faatwir (35).
035-Faatwir: Utangulizi Wa Suwrah
Alhidaaya.com [2]
Imeteremka: Makkah kwa itifaki ya ‘Ulamaa.
Idadi Za Aayah: 45
Jina La Suwrah: Faatwir
Suwrah imeitwa Faatwir (Mwanzilishi), na inayodalilisha ni kutajwa katika Aayah namba (1) kumkusudia Allaah (سبحانه وتعالى) kuwa ni Mwanzilishi au Muumbaji. Rejea chini kwenye Faida.
Miongoni Mwa Makusudio Ya Suwrah:
1-Kubainisha uhitaji wa waja kwa Allaah Mwanzilishi wa mbingu na ardhi (uhitaji) usio na mpaka, na Ukamilifu wa Ukwasi Wake kwao. [Al-Mukhtaswar Fiy Tafsiyr Al-Qur-aan Al-Kariym]
2-Kuthibitisha Tawhiyd ya Allaah kwa njia ya kuwakumbusha waja Neema Zake zilizoenea ulimwenguni.
3-Kubainisha Uwezo wa Allaah Uliokamilika, pamoja na Uwezo wa kufufua.
4-Kuthibitisha Ukweli wa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم).
Miongoni Mwa Maudhui Ya Suwrah:
1-Suwrah imefunguliwa kwa Kumhimidi Allaah (سبحانه وتعالى) Mwanzilishi wa mbingu na ardhi na kuwafanya Malaika kuwa ni Wajumbe wenye mbawa, na kwamba Uwezo Wake Allaah (سبحانه وتعالى) upo kwenye kila kitu.
2-Imetajwa baadhi ya mambo yanayodalilisha Uwezo wa Allaah kwa Viumbe, na Neema Zake kwa waja wake.
3-Imetajwa kumliwaza Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) na kumpa thabati kwa kumbainishia hali ya Manabii waliotangulia.
4-Imetoa tahadhari ya dunia na kutodanganyika na shaytwani.
5-Imetajwa kuwa neno zuri ambalo ni aina yoyote ya kumdhukuru Allaah (سبحانه وتعالى) hutukuzwa na kupandishwa juu kwa Allaah.
6-Imebainisha malipo ya Waumini na malipo ya makafiri.
7-Imetajwa Neema ya Allaah (سبحانه وتعالى) kwa kuupelekea upepo, na kuteremsha mvua, na kuhuisha ardhi iliyokufa, na hivyo ndivyo mfano wa kufufuliwa.
8-Imebainishwa Tawhiyd ya Allaah (سبحانه وتعالى) ya Uumbaji Wake viumbe na Neema Zake mbalimbali, na kwamba washirikina hawana uwezo wa kumiliki chochote kile hata kiwe kidogo vipi.
9-Imetajwa uhitaji wa viumbe kumuhitajia Allaah (سبحانه وتعالى) Naye ni Mkwasi Asiyehitaji lolote lile.
10-Imebainishwa kuwa hakuna mwanaadam atakaebeba madhambi ya mwenzie hata kama ni jamaa wa karibu.
11-Imepigwa mifano mbalimbali ya kulinganisha Muumini na kafiri, au aliyekuwa na ilimu na mjinga.
12-Imebainishwa kuwa wenye kumkhofu zaidi Allaah (سبحانه وتعالى) ni wenye ilimu na ikatajwa fadhila za kusoma Qur-aan na kusimamisha Swalaah na kutoa mali kwa njia ya Allaah.
13-Imetajwa hali za Waumini watakapokuwa Jannah (Peponi) na hali za makafiri watakapokuwa motoni.
14-Imetajwa ujinga wa washirikina kuabudia kwao masanamu ambayo hayamiliki kwao madhara wala manufaa.
15-Imetajwa zingatio kubwa la Uwezo wa Allaah (سبحانه وتعالى) Kuzuia mbingu na ardhi zisitoweke.
16-Suwrah imekhitimishwa kwa kutajwa Utukufu wa Allaah na Uwezo Wake kwamba hakuna linalomshinda na pia ikatajwa Rehma Yake ya kutokuwaadhibu pale pale viumbe wanapokosea lakini Anawaakhirishia mpaka muda maalumu.
Faida:
1-Faatwir (Mwanzilishi): Imetajwa Sifa ya Allaah kuwa Ni Mwanzilishi wa mbingu na ardhi, katika Suwrah nyenginezo. Rejea Al-An’aam (6:14), (6:79), Suwrah Yuwsuf (12:101), Ibraahiym (14:10), Al-Anbiyaa (21:56), Az-Zumar (39:46), Ash-shuwraa (42:11). Na imekuja katika Sifa ya Muumbaji katika Suwrah Huwd (11:51) Al-Israa (17:51), Twaahaa (20:72), Yaasiyn (36:22), Az-Zukhruf (43:27).
2-Suwrah Faatwir (35) ni miongoni mwa Suwrah tano zinazoanzia kwa AlhamduliLlaah. Nyenginezo ni Al-Faatihah (1), Al-An’aam (6), Al-Kahf (18), na Saba-a (34).
036-Yaasiyn: Utangulizi Wa Suwrah
Alhidaaya.com [2]
Imeteremka: Makkah kwa itifaki ya ‘Ulamaa.
Idadi Za Aayah: 83
Jina La Suwrah: Yaasiyn
Suwrah imeitwa Yaasiyn, na inayodalilisha ni kutajwa katika Aayah namba (1) na herufi hizo ni ambazo zinajulikana kuwa ni Al-Huruwf Al-Muqatw-twa’ah zinazotokea katika mwanzo wa baadhi ya Suwrah.
Miongoni Mwa Makusudio Ya Suwrah:
1-Kuthibitisha Risala na ufufuo, na dalili za vyote hivyo. [Al-Mukhtaswar Fiy Tafsiyr Al-Qur-aan Al-Kariym]
2-Kuithibitisha misingi mikubwa ya Dini, nayo ni Tawhiyd ya Allaah (سبحانه وتعالى) Rabb wa walimwengu, Risala ya Rasuli Wake (صلى الله عليه وآله وسلم), kuthibitisha kufa, kufufuliwa na kukusanywa, na malipo ya Jannah na moto.
3-Kubainisha Neema za Allaah (سبحانه وتعالى) na Hikma Zake, Uwezo Usimamizi Wake kuendesha ulimwengu huu, ikitaja dalili nyingi tofauti katika kuhuisha ardhi baada ya kufa kwake, mfuatano wa mchana na usiku, mwendo wa sayari, mzunguko wa dunia, jua na mwezi, na mambo ambayo yamo Mikononi mwa Muumba Pekee (سبحانه وتعالى).
Miongoni Mwa Maudhui Ya Suwrah:
1-Suwrah imefunguliwa kwa herufi zinazojulikana kama الحروف المقطعة (Al-Huruwf Al-Muqatw-twa’ah), ambazo hakuna ajuaye maana zake isipokuwa Allaah (سبحانه وتعالى). Rejea Al-Baqarah (2:1). Kisha imetukuzwa Qur-aan kuwa ni yenye hikma. Kisha imethibitishwa ukweli wa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم), na kuthibitishwa kuwa Qur-aan ni Uteremsho Wake (Wahy).
2-Imetajwa hali za makafiri kutokukubali haki na kwamba wanaoikubali haki ni wenye kumkhofu Rabb wao kwa ghaibu.
3-Imetajwa kwamba kila jambo limeandikwa katika Al-Lawh Al-Mahfuwdhw (Ubao Uliohifadhiwa na kwamba athari za mema na maovu yanaendelea kurekodiwa humo.
4-Imetajwa kisa watu wa kijiji, na yaliyotokea kati yao na Rusuli ambao Allaah (سبحانه وتعالى) Aliwatuma kwao.
5-Imebainishwa baadhi ya mambo yanayoonyesha Uwezo wa Allaah katika kuendesha ulimwengu na Neema Zake kwa Waja Wake.
6-Imetoa khabari za madai ya baatwil ya washirikina.
7-Imetajwa hali za watu watakapofufuliwa makaburini.
8-Imetajwa hali za Waumini watakapokuwa Jannah (Peponi) na watapata maamkizi ya Salaam kutoka kwa Rabb wao Mwenye Kurehemu. Kinyume chake ni wahalifu watakaoingizwa katika moto wa Jahannam ambao walimwabudu shaytwaan akawapoteza.
9-Imetajwa kuwa viungo vya mwanaadamu vitashuhudia matendo yao Siku ya Qiyaamah.
10-Imetajwa kumliwaza Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) kutokana na kukanushwa na washirikina.
11-Imetajwa ukanushaji wa mmoja wa washirikina, aliyepiga mfano wa mifupa kuoza na kusagika, ya kwamba haiwezekani kufufuliwa, lakini Allaah (سبحانه وتعالى) Akamradd kwa kuthibitisha wazi, Qudra Yake Adhimu na Uwezo Wake wa kuumba na kufufua.
12-Suwrah imekhitimishwa kwa Allaah (سبحانه وتعالى) Kujithibitishia Mwenyewe Tawhiyd Yake ya Ar-Rubuwbiyyah (Uola), na Kujitukuza Mwenyewe Allaah (عزّ وجلّ) na Kujitakasa (سبحانه وتعالى) kutokana na kila kosa na Akabainisha kwamba mambo yote yamo Mkononi Mwake na kwamba kwa Utukufu na Uwezo Wake, Anafanya Atakalo!
037-Asw-Swaaffaat: Utangulizi Wa Suwrah
Alhidaaya.com [2]
Imeteremka: Makkah kwa itifaki ya ‘Ulamaa.
Idadi Za Aayah: 182
Jina La Suwrah: Asw-Swaaffaat
Suwrah imeitwa Asw-Swaaffaat (Safusafu), na inayodalilisha ni kutajwa katika Aayah namba (1), na pia katika Hadiyth iliyonukuliwa katika Faida.
Miongoni Mwa Makusudio Ya Suwrah:
1-Kumuepusha Allaah (سبحانه وتعالى) na yale waliyomnasibishia washirikina, na kubatilisha madai yao dhidi ya Malaika na majini. [Al-Mukhtaswar Fiy Tafsiyr Al-Qur-aan Al-Kariym]
2-Kusimamisha dalili ya Tawhiyd ya Allaah na kwamba kufufuliwa ni haki, na kuelezea baadhi ya matukio ya Siku ya Qiyaamah.
3-Kuelezea kuhusu nyumati za nyuma na upotovu wa ‘Aqiydah zao na ushirikina na hali zao motoni kwa kuwapinga Rusuli wao.
4-Kuradd madai na usingiziaji mkubwa wa Maquraysh kumshirikisha Allaah (سبحانه وتعالى) na Viumbe Vyake na kuwataka Waislamu kubakia imara.
Miongoni Mwa Maudhui Ya Suwrah:
1-Suwrah imefunguliwa kwa Kuapia Kwake Allaah (سبحانه وتعالى) Malaika wanaojipanga safusafu, wanaosukumiza mbali mawingu, wanaosoma Maneno ya Allaah. Kisha ikathibitishwa Tawhiyd ya Allaah (سبحانه وتعالى).
2-Imetajwa tabia ya mashaytwaan ya kusikiliza na kuiba habari za mbinguni, na hali yao ya kupigwa na vimondo.
3-Imetajwa baadhi ya ada za washirikina ya kufanya istihzai na kutokuamini kufufuliwa.
4-Imetajwa baadhi ya matukio ya Siku ya Qiyaamah, na hali ya washirikina watakapokabiliana kulaumiana walivyofuatana katika upotofu duniani. Hivyo basi watashirikiana katika adhabu kutokana na kibri zao za kukataa haki na kumpachika sifa ovu Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) .
5-Imetajwa baadhi ya neema na raha za Jannah (Peponi) kwa Waumini. Na Kauli ya Allaah (سبحانه وتعالى) ya kuwasifu Waja Wake waliokhitariwa kwa ikhlasi zao, na kuwatakia Amani juu yao, na kwamba hivyo ndivyo Allaah (سبحانه وتعالى) Anavyowalipa wafanyao ihsaan, imekariri mara kadhaa katika Suwrah pindi anapowataja Waja Wake wema na Manabii Wake.
6-Imetajwa mja mwema aliyekuwa Janna (Peponi), akimsemesha rafiki muovu aliyekuwa motoni, akishukuru kwa Rehma ya Allaah kumjaalia kutokumfuata rafiki huyo muovu aliyekuwa haamini kufufuliwa.
7-Imetajwa hali za makafiri motoni na watakayoyapata humo kama mti mchungu wa az-zaquwm.
8-Ametajwa Nabiy Nuwh (عليه السّلام). Na imetajwa kisa cha Nabiy Ibraahiym (عليه السّلام) na watu wake waliomuingiza motoni, lakini Allaah (سبحانه وتعالى) Akumuokoa. Na pia kisa cha mwanawe Ismaa’iyl (عليه السّلام) na njozi aliyoiona usingizini kwamba anamchinja mwanawe. Ikawa ni jaribio kubwa kwake! Lakini akaiamini njozi hiyo, na wote wawili wakaridhia kuitekeleza. Lakini Allaah (سبحانه وتعالى) Akawateremshia fidia ya dhabihu (mnyama wa kuchinja), na hiyo ndio Sunnah inayotekelezwa siku ya ‘Iydul-Adhwhaa (‘Iyd ya kuchinja). Kisha wametajwa Nabiy wengineo ambao ni Is-haaq, Muwsaa, Haaruwn, Ilyaas, Luutw, na Yunus (عليهم السّلام).
9-Imebainisha ukafiri na dhulma kubwa mno za washirikina kumsingizia Allaah (سبحانه وتعالى) kwamba Malaika ni mabinti Wake ilhali wao wenyewe hawakupenda kuzaa watoto wa kike! Juu ya hayo, wakamsingizia kuwa Ana unasaba na majini! Subhaanahu wa Ta’aalaa! (Ametakasika na kila dosari na Ametukuka kwa Uluwa) Basi Allaah (سبحانه وتعالى) Akawaradd kwa hilo na Akawaahidi kuwaadhibu motoni!
10-Imetajwa Allaah (سبحانه وتعالى) kuwaunga mkono Rusuli Wake na kuwaahidi nusra, na kumtaka Rasuli Wake (صلى الله عليه وآله وسلم) kuwapuuza makafiri na kwamba watakuja kukutana na Adhabu Yake.
11-Suwrah imekhitimishwa kwa kuthibitisha Nguvu za Allaah (سبحانه وتعالى) Asiyeshindika, na kumtakasa Allaah (سبحانه وتعالى) kutokana na wanayoyavumisha washirikina. Kisha ikatolewa Salaamun (Amani) iwe juu ya Rusuli, na AlhamduliLLaah (Himidi Anastahiki Allaah) Rabb wa walimwengu.
Faida:
عَنْ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ عُمَرَ، قَالَ كَانَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم يَأْمُرُ بِالتَّخْفِيفِ وَيَؤُمُّنَا بِالصَّافَّاتِ
Amesimulia ‘Abdullaah Bin ‘Umar (رضي الله عنهما) : Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alikuwa akiamrisha kufupisha (Swalaah), na alikuwa akituamimisha (Swalaah) kwa (Suwrah) Asw-Swaaffaat (kwa kuwa ni makhsusi kwake). [Swahiyh An-Nasaaiy (825)]
038-Swaad: Utangulizi Wa Suwrah
Alhidaaya.com [2]
Imeteremka: Makkah kwa itifaki ya ‘Ulamaa.
Idadi Za Aayah: 88
Jina La Suwrah: Swaad
Suwrah imeitwa Swaad, na inayodalilisha ni kutajwa katika Aayah namba (1), na ambayo ni katika herufi zinazojulikana kuwa ni Al-Huruwf Al-Muqatw-twa’ah zinazotokea katika mwanzo wa baadhi ya Suwrah.
Miongoni Mwa Makusudio Ya Suwrah:
1-Mapambano dhidi ya baatwil na mwisho wake (kwa aliyejipamba na ubatilifu). [Al-Mukhtaswar Fiy Tafsiyr Al-Qur-aan Al-Kariym]
2-Kusimamisha Tawhiyd ya Allaah (سبحانه وتعالى) na Uwezo Wake.
3-Kuthibitisha ukweli wa Unabiy Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم).
4-Kuthibitisha kufufuliwa na kuziradd hoja za washirikina.
Miongoni Mwa Maudhui Ya Suwrah:
1-Suwrah imefunguliwa kwa herufi zinazojulikana kama الحروف المقطعة (Al-Huruwf Al-Muqatw-twa’ah), ambazo hakuna ajuaye maana zake isipokuwa Allaah (سبحانه وتعالى). Rejea Al-Baqarah (2:1). Kisha imetukuzuwa Qur-aan na kusifiwa kwamba ni yenye ukumbusho. Kisha imebainishwa misimamo ya washirikina na ada zao za kutokumuamini Nabiy Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم), na kumfanyia istihzai na dhihaka, na kumpachika sifa ovu. Hivyo basi ni kuikanusha Risala ya Allaah.
2-Imetajwa kumliwaza Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) kwa yaliyomsibu kutoka kwa watu wake, kwa kuwataja baadhi ya Manabii waliokadhibishwa na watu wao pia.
3-Allaah (سبحانه وتعالى) Amemtaja na kumsifia Mja Wake Daawuwd (عليه السّلام) na Neema Zake Alizomjaalia, zikiwemo kumtunukia mwanawe ambaye ni Nabiy Sulaymaan (عليه السّلام). Kisha ikatajwa kisa cha watu wawili walioingia kwa Nabiy Daawuwd (عليه السّلام) kumtaka awahukumu kuhusu kondoo wao, naye akatoa hukumu, lakini akahisi kwamba Allaah (سبحانه وتعالى) Amemtia mtihanini, akaporomoka kumuomba Rabb wake maghfirah.
4-Na pia Allaah (سبحانه وتعالى) Amemtaja na kumsifu Nabiy Sulaymaan (عليه السّلام) na Neema kadhaa Alizojaaliwa; miongoni mwazo ni kupewa ufalme ambao hatoupata tena mtu baada yake, na kutiishiwa (kudhalilishwa) upepo aweze kusafiri safari ndefu kwa muda mfupi tu, na pia kutiishiwa (kudhalilishiwa) majini.
5-Na pia Allaah (سبحانه وتعالى) Amemtaja na kumsifu Nabiy Ayyuwb (عليه السّلام) na kisa chake cha mitihani aliyopewa ya maradhi, na jinsi alivyovuta subira hadi Allaah (سبحانه وتعالى) Akamuondeshea maradhi na kumbadilishia kila lilobaya kwa zuri.
6-Na Allaah (سبحانه وتعالى) Amewataja na kuwasifu Nabii Wake wengineo nao ni Ibraahiym, Is-haaq, Ya’quwb, Ismaa’iyl, Al-Yasaa na Dhul-Kifl (عليهم السّلام).
7-Imetajwa baadhi ya neema na raha za kudumu milele, Alizoziandaa (سبحانه وتعالى) huko Jannah kwa wamchao Yeye ambayo ni neema za kudumu.
8-Ikafuatilia kutajwa yaliyoandaliwa motoni kwa watu waovu, na hali zao huko za kulaumiana na kuombeana adhabu humo.
9-Imetajwa sehemu ya kisa cha Nabiy Aadam (عليه السّلام) na Ibliys aliyefanya kiburi akakataa amri ya Rabb wake, Akalaaniwa na Allaah (سبحانه وتعالى) na kuepushwa na Rehma Zake. Ibliys akaahidi kuwapotosha watu isipokuwa waliokhitariwa kwa ikhlaas zao. Basi Allaah (سبحانه وتعالى) Akaapa kumuingiza katika moto wa Jahannam na kuijaza kwa watakaomfuata.
10-Suwrah imekhitimishwa kwa Allaah (سبحانه وتعالى) Kumuunga mkono Rasuli Wake (صلى الله عليه وآله وسلم) na kuthibitisha kuwa Qur-aan ni ukumbusho kwa walimwengu, na wanaoipinga watakuja kujua khabari za ukweli wa Qur-aan. Rejea Aayah (88) kupata faida.
039-Az-Zumar: Utangulizi Wa Suwrah
Alhidaaya.com [2]
Imeteremka: Makkah kwa itifaki ya ‘Ulamaa.
Idadi Za Aayah: 75
Jina La Suwrah: Az-Zumar
Suwrah imeitwa Az-Zumar (Makundi), na inayodalilisha ni kutajwa katika Hadiyth iliyonukuliwa chini katika Fadhila za Suwrah. na kutajwa katika Aayah namba (71-72).
Miongoni Mwa Makusudio Ya Suwrah:
1-Daawah ya Tawhiyd na ikhlaasw, na kuacha shirki. [Al-Mukhtaswar Fiy Tafsiyr Al-Qur-aan Al-Kariym]
2-Kuthibitisha kwamba Allaah (سبحانه وتعالى) Ndiye Muabudiwa Pekee, na Mweza wa Kuumba, Kuhuisha na Kufufua.
3-Kuwasimimishia hoja washirikina na kubatilisha shirki zao na malipo yao motoni.
4-Tofauti ya taathira ya Qur-aan kwa Waumini na makafiri, na kuelezea sababu za hidaaya na taqwa, imaan na uthabiti katika haki,
5-Kudhihirisha Uwezo wa Allaah mbinguni na ardhini na kujulisha baadhi ya matukio ya Siku ya Qiyaamah na hali za Waumini na makafiri.
Miongoni Mwa Maudhui Ya Suwrah:
1-Suwrah imefunguliwa kwa kuitukuza Qur-aan na kuthibitisha kwamba Allaah (سبحانه وتعالى) Ndiye Aliyeiteremsha kwa Rasuli Wake (صلى الله عليه وآله وسلم).
2-Waja wanaamrishwa kumwabudu Allaah (سبحانه وتعالى) kwa ikhlaas na kubainisha shubha za wale wanaoabudu asiyekuwa Allaah kwa kisingizio kuwa waabudiwa wao wanawakuribisha tu kwa Allaah.
3-Allaah (سبحانه وتعالى) Anajitakasa na usingiziaji wa makafiri kuwa Kajichukulia mwana!
4-Imetajwa baadhi ya dalili za Tawhiyd ya Allaah ya Ar-Rubuwbiyyah (Uola) ya uumbaji wa mbingu na ardhi, kugeuza usiku na mchana, na kutiisha jua na mwezi kwenda mpaka muda maalumu, na uumbaji wa mwanaadam katika tumbo la uzazi.
5-Imetajwa hali za makafiri na hali za Waumini, na kubainisha mwisho wa wenye kuvuta subira.
6-Imetajwa baadhi ya maelekezo kwa Waumini na kubainisha mwisho wao, na maonyo ya adhabu kwa asiyemwabudu Allaah.
7-Imetajwa onyo kwa wenye nyoyo zinazo susuwaa kwa sababu ya kutajwa Allaah. Na kisha ikatajwa namna ya uteremshaji wa Qur-aan, na jinsi inavyowaathiri Waumini ngozini na nyoyoni mwao. Na kwamba Qur-aan hiyo Adhimu ambayo ni ya lugha ya Kiarabu, haina kombo.
8-Allaah (سبحانه وتعالى) Anapiga mfano wa mtu (kafiri, mshirikina) aliye chini ya washirika wagombanao, na mtu mwengine (Muumini) aliye pweke na bwana mmoja tu, (anamwabudu Allaah Pekee) kwamba hawalingani sawa.
9-Imebainishwa dhalimu anayekadhibisha haqq (ukweli) ulipomjia na adhabu zake, na Muumini aliyekubali na akapokea haqq, na jazaa zao.
10-Imethitibishwa kuwa washirikina waliamini Tawhiyd ya Allaah (سبحانه وتعالى) ya Ar-Rubuwbiyyah (Uola, Uumbaji, Ufalme, Uendeshaji ulimwengu, Kuruzuku na kadhaalika), lakini hawakumpwekesha Allaah katika Tawhiyd ya Al-Uluwhiyyah (ibaada).
11-Imetajwa hali ya mwanaadam anapolala kuwa anafishwa usingizini, kisha Allaah (سبحانه وتعالى) Anazuia roho za Aliowaqadaria kufa, na Anarudisha roho za Aliowaqadaria kuendelea kuishi mpaka muda wao maalumu. Na kwamba hili ni zingatio kwa watu ili waweze kutafakari kwamba usingizi ni kama mauti madogo.
12-Imetajwa kuwa madhalimu watatamani kufidia mali zote walizonazo ili waepukane na Adhabu za Allaah za Siku ya Qiyaamah.
13-Imetajwa hali ya kafiri anapoguswa na dhara, na hali yake anapoondoshewa dhara, kuwa hana shukurani.
14-Imethibitishwa kwamba Allaah (سبحانه وتعالى) Anaghufuria madhambi yote pindi mtu akirudia kutubia Kwake kabla ya kufikia sakaraatul-mawt.
15-Imetajwa majuto ya nafsi ya mtu muovu pindi inapotolewa roho, au pindi inapomfikia adhabu. Na hatakuwa na hoja kwani zilimfikia Aayaat (Ishara na Dalili) za waziwazi lakini alizikadhibisha na kuzikufuru, basi makazi yake ni Jahannam. Ama Waumini, Allaah (سبحانه وتعالى) Atawaokoa na watakuwa hawana khofu wala huzuni.
16-Imetajwa baadhi ya matukio ya Siku ya Qiyaamah pindi litakapopulizwa baragumu na vitisho vyake. Na jinsi ardhi itakavong’ara kwa Nuru ya Allaah (سبحانه وتعالى), na kutakuweko mkusanyiko wa viumbe wote, na watahukumiwa kwa haki.
17-Imebainishwa hali ya waovu watakavyoingizwa makundi makundi katika moto wa Jahannam kudumu humo, na kulaumiwa kwa kuwakanusha Rusuli wa Allaah (سبحانه وتعالى) walipowajia duniani kuwalingania. Kisha ikafuatilia kutaja hali za Waumini watakapoingizwa katika Jannah makundi makundi kubashiriwa kheri zake; raha na neema za Jannah. Na kwa hayo, Wanamhimidi Rabb wao Aliyewatimizia Ahadi Yake.
18-Suwrah imekhitimishwa kwa kutajwa Malaika watakaozunguka ‘Arsh ya Allaah (سبحانه وتعالى) huku Wakimsabbih na Kumhimidi Allaah Rabb wa walimwengu.
Fadhila Za Suwrah Az-Zumar:
Miongoni mwa Suwrah alizokuwa akizisoma Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) kabla ya kulala ni Suwrah Az-Zumar:
عن عائشة رضي الله عنها قالت: كانَ النَّبيُّ صلَّى اللَّهُ عليهِ وسلَّمَ لا ينامُ علَى فِراشِه حتَّى يقرأ بَني إسرائيلَ ، والزُّمَرِ
Amesimulia ‘Aaishah (رضي الله عنها): Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alikuwa halali kitandani mwake ila akisoma kwanza (Suwrah) Bani Israaiyl na Az-Zumar. [At-Tirmidhiy na ameisahihisha Al-Albaaniy katika Swahiyh At-Tirmidhiy (2920), Swahiyh Al-Jaami’ (4874)]
040-Ghaafir: Utangulizi Wa Suwrah
Alhidaaya.com [2]
Imeteremka: Makkah kwa itifaki ya ‘Ulamaa.
Idadi Za Aayah: 85
Jina La Suwrah: Ghaafir
Suwrah imeitwa Ghaafir (Mwenye Kughufuria), na inayodalilisha ni kutajwa Sifa hii ya Allaah (سبحانه وتعالى) katika Aayah namba (2).
Na Suwrah imeitwa pia Al-Muumin kwa kutajwa katika Hadiyth:
عَنْ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ السَّائِبِ، قَالَ صَلَّى لَنَا النَّبِيُّ صلى الله عليه وسلم الصُّبْحَ بِمَكَّةَ فَاسْتَفْتَحَ سُورَةَ الْمُؤْمِنِينَ حَتَّى جَاءَ ذِكْرُ مُوسَى وَهَارُونَ أَوْ ذِكْرُ عِيسَى - مُحَمَّدُ بْنُ عَبَّادٍ يَشُكُّ أَوِ اخْتَلَفُوا عَلَيْهِ - أَخَذَتِ النَّبِيَّ صلى الله عليه وسلم سَعْلَةٌ فَرَكَعَ وَعَبْدُ اللَّهِ بْنُ السَّائِبِ حَاضِرٌ ذَلِكَ . وَفِي حَدِيثِ عَبْدِ الرَّزَّاقِ فَحَذَفَ فَرَكَعَ . وَفِي حَدِيثِهِ وَعَبْدُ اللَّهِ بْنُ عَمْرٍو . وَلَمْ يَقُلِ ابْنِ الْعَاصِ .
Amesimulia ‘Abdullaah Bin As-Saaib (رضي الله عنه): Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alituswalisha Swalaah ya Asubuhi Makkah, akafungua (Swalaah) kwa Suwrah Al-Muumin (akasoma) mpaka alipofikia kutajwa Muwsaa na Haaruwn au kutajwa ‘Iysaa (عليهم السّلام), kikohozi kikamshika akarukuu. ‘Abdullaah bin As-Saaib alikuwepo hapo. Na katika Hadiyth iliyosimuliwa na ‘Abdur-Razzaaq (maneno yalikuwa): Alikata (kisomo) akarukuu. [Muslim]
Miongoni Mwa Makusudio Ya Suwrah:
1-Kubainisha hali ya wanaobishana Aayah za Allaah (ili wazipinge na wazibatilishe), na kuwaradd juu ya madai yao. [Al-Mukhtaswar Fiy Tafsiyr Al-Qur-aan Al-Kariym]
2-Kubainisha haqq (haki) na baatwil na kubatilisha mijadala ya wale waliokuwa wakijadili juu ya Aayah za Allaah ili wazipinge na wazibatilishe.
3-Hali za makafiri wa nyumati zilotangulia, waliokadhibisha Rusuli wao na maangamizi yao.
4-Kuthibitisha Tawhiyd ya Allaah (سبحانه وتعالى) na Uwezo Wake wa Kuumba kwa dalili kadhaa, na Uwezo wa Kufufua.
5-Kutaja baadhi ya matukio ya Siku ya Qiyaamah na hali za watu, na Hukmu ya uadilifu ya Allaah Siku hiyo ya malipo ya kheri na shari.
Miongoni Mwa Maudhui Ya Suwrah:
1-Suwrah imefunguliwa kwa herufi zinazojulikana kama الحروف المقطعة (Al-Huruwf Al-Muqatw-twa’ah), ambazo hakuna ajuaye maana zake isipokuwa Allaah (سبحانه وتعالى). Rejea Al-Baqarah (2:1). Kisha imethibitishwa kuwa Qur-aan ni Uteremsho kutoka kwa Allaah (سبحانه وتعالى), na kumsifu Allaah (سبحانه وتعالى) kwa Sifa Zake za wingi wa Kughufuria na Kupokea tawbah za Waja Wake, kisha kuthibitishwa Tawhiyd Yake, na kwamba marejeo yatakuwa Kwake Siku ya Qiyaamah.
2-Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) ameliwazwa kutokana na yaliyomsibu kutoka kwa watu wake; washirikina wa Makkah, kwamba Rusuli wa kabla yake pia walikadhibishwa na kaumu zao, lakini Allaah Aliwaadhibu.
3-Daawah kwa wanaadam juu ya kufanya ibaada kwa ikhlas, na kuwakumbusha vitisho vya siku ya Qiyaamah.
4-Imewasifu Malaika wanaobeba ‘Arsh ya Allaah (سبحانه وتعالى), na kwamba miongoni mwa kazi zao, ni kuwaombea maghfirah Waumini, na kuwaombea duaa.
5-Imetajwa kwamba kuna mauti mawili na uhai miwili. Rejea Faida ya Aayah (namba 11).
6-Imetajwa Siku ya Qiyaamah ambayo hakuna kitakachofichika, wala hakutakuwa na dhulma, na hakutakuwa na mfalme, wala mwenye kutakabari, wala mwenye kujifanya jabari, bali Ufalme Utabakia wa Allaah (سبحانه وتعالى) Pekee. Na Siku hiyo, nyoyo zitafika kooni kwa kiwewe, huzuni na majuto, na hata rafiki wa dhati hataweza kumsaidia mwenziwe.
7-Imeelezewa sehemu ya kisa cha Nabiy Muwsaa (عليه السّلام), na Akatajwa Muumin mmoja kutoka watu wa Firawni aliyewaonya watu wake wasimuue Nabiy Muwsaa (عليه السّلام), na akawalingania waikubali Risala ya Allaah, na akawaonya Siku ya Qiyaamah ambayo ni Siku ya kuitana. Pia akawalingania Tawhiyd ya Allaah (سبحانه وتعالى) na akawaonya kuingizwa motoni. Na pia ikatajwa jeuri na kibri cha Firawni kutaka kupanda mbinguni ili amuone Allaah (سبحانه وتعالى), na kumkadhibisha Nabiy Muwsaa (عليه السّلام). Na imethibitishwa adhabu za maisha ya Barzakh kaburini, kwamba Firawni anaendelea kuadhibiwa asubuhi na jioni na atatendelea hivyo mpaka ifike Siku ya Qiyaamah.
8-Imetajwa mazungumzo kati ya watu walio wadhaifu na walio na nguvu uwezo na waliotakabari. Watu wadhaifu wanaomba msaada kwa waliotakabari lakini hakuna kusaidiana Siku hiyo, bali watakanushana. Na ikatajwa watu wa motoni wanavyowaomba Walinzi wa moto wawaombee kwa Allaah (سبحانه وتعالى) takhfifu ya adhabu lakini duaa yao haikubaliwi!
9-Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) ameliwazwa kwa kutakwa avute subira na aombe maghfirah na Kumsabbih Rabb wake asubuhi na jioni.
10-Imehimizwa kumuomba duaa Allaah (سبحانه وتعالى), na kwamba kutokumuomba, ni aina ya kibri. Na imetanabahishwa Kumpwekesha Allaah katika ibaada na kubatilisha viabudiwa vyote kinyume na Allaah.
11-Imetajwa aina kadhaa za Neema za Allaah kwa watu, ili waweze kushukuru.
12-Wameonywa makafiri waliokadhibisha Risala ya Allaah kwa baadhi ya vitisho na adhabu za Siku ya Qiyaamah.
13-Suwrah imekhitimishwa kwa kuwaonya washirikina wa Makkah ya kwamba watakuja kutaka kuamini baada ya kuiona adhabu, lakini kuamini kwao hakutawafaa, na kwamba Desturi ya Allaah itahakiki kama walivyoadhibiwa nyumati za nyuma, na hivyo watakuwa katika khasara.
Faida:
Suwrah hii ya Ghaafir (40) ni Suwrah ya mwanzo katika mfululizo wa Suwrah zinazoanzia na herufi za حم. Ya mwisho wake ni Suwrah Al-Ahqaaf (46).
041-Fusw-Swilat: Utangulizi Wa Suwrah
Alhidaaya.com [2]
Imeteremka: Makkah kwa itifaki ya ‘Ulamaa.
Idadi Za Aayah: 54
Jina La Suwrah: Fusw-Swilat
Suwrah imeitwa Fusw-Swilat (Tafsili Ya Wazi), na inayodalilisha ni kutajwa neno hili katika Aayah namba (3).
Miongoni Mwa Makusudio Ya Suwrah:
1-Kubainisha hali ya wanaompuuza Allaah (سبحانه وتعالى), na kutaja mwisho wao. [Al-Mukhtaswar Fiy Tafsiyr Al-Qur-aan Al-Kariym]
2-Kuthibitisha kwamba Qur-aan inatoka kwa Allaah (سبحانه وتعالى), na dalili, ushahidi usiokanushwa wa miujiza ya Qur-aan, na kuthibitisha Risala kwa Mjumbe Wake; Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) ambaye ni binaadam kuwafikshia wanaadam wenzake na kwamba Dini ya Kiislamu ni haqq.
3-Kusimamisha dalili ya Tawhiyd ya Allaah na Uwezo Wake wa kuumba mbingu na ardhi na Aayaat (Ishara na Dalili) Zake.
4-Kumliwaza Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) kwa kutajiwa khabari za nyumati zilotangulia waliowakanusha Rusuli wao na upotovu wao duniani na adhabu zao.
5-Kuwabashiria Waumini mema ya duniani na ya Aakhirah.
Miongoni Mwa Maudhui Ya Suwrah:
1-Suwrah imefunguliwa kwa herufi zinazojulikana kama الحروف المقطعة (Al-Huruwf Al-Muqatw-twa’ah), ambazo hakuna ajuaye maana zake isipokuwa Allaah (سبحانه وتعالى). Rejea Al-Baqarah (2:1). Kisha imebainishwa kwamba Qur-aan ni ya lugha ya Kiarabu, na kwamba ni Kitabu kinachofasili waziwazi Aayah zake, na kwamba zinabashiria na kuonya, lakini wengi ya watu wamekengeuka.
2-Imebainishwa msimamo wa makafiri kuhusu Qur-aan.
3-Imetajwa baadhi ya mambo yanayoonyesha uwezo wa Allaah (سبحانه وتعالى) katika Uumbaji Wake.
4-Imetajwa kaumu ya ‘Aad na Thamuwd kuhusu kibri zao na ukanushaji wao wa Risala ya Allaah na ikatajwa adhabu zao.
5-Imeonya washirikina wanaopinga kuisikiliza Qur-aan, ya kwamba yatawapata yaliyo wapata waliopita kabla yao.
6-Imebainishwa hali za Waumini wanapotolewa roho zao kubashiriwa kheri.
7-Imetajwa sifa za mwenye kulingania (daawah) awe mnyenyekevu na mwenye kulipiza uovu kwa wema na kuvuta subira.
8-Imetajwa Aayah (Ishara, dalili) kadhaa zinazoonyesha Tawhiyd ya Allaah na Uwezo Wake juu ya kuwafufua wafu. Na katika hizo ni usiku na mchana, jua na mwezi na ikaamrishwa kutokusujudia hivyo bali asujudiwe Allaah (سبحانه وتعالى) Ambaye Ameviumba hivyo. Na hapo inapaswa mtu asujudu kwa kuweko alama ya Sijdah ya tilaawah (kusoma).
9-Ameliwazwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) juu ya maudhi anayoyapata kutoka kwa watu wake.
10-Suwrah imekhitimishwa kwa kuahidiwa makafiri kuwa wataonyeshwa Aayaat (Ishara na Dalili) za wazi katika nafsi zao na angani mpaka iwabainikie kwamba hii (Qur-aan) ni haki, na kwamba makafiri wako katika shaka ya kufufuliwa na kuhesabiwa.
042-Ash-Shuwraa: Utangulizi Wa Suwrah
Alhidaaya.com [2]
Imeteremka: Makkah kwa itifaki ya ‘Ulamaa.
Idadi Za Aayah: 53
Jina La Suwrah: Ash-Shuwraa
Suwrah imeitwa Ash-Shuwraa (Ushauri), na inayodalilisha ni kutajwa neno hilo katika Aayah namba (38).
Miongoni Mwa Makusudio Ya Suwrah:
1-Kubainisha ukamilifu wa Sharia za Allaah, na uwajibu wa kuzifuata, na kutahadharisha juu ya kuzikhalifu. [Al-Mukhtaswar Fiy Tafsiyr Al-Qur-aan Al-Kariym]
2-Kutambulishwa kwamba, tofauti katika Sharia za Allaah hazionyeshi tofauti katika chanzo chake.
3-Kubainishwa Rehma ya Allaah (سبحانه وتعالى) ya Maghfirah na Msamaha Wake kwa kupokea tawbah za Waja Wake na kuwapa bishara Waumini juu ya malipo yanayowangoja katika maisha ya Aakhirah.
4-Dalili za kubainisha Tawhiyd ya Allaah na Uwezo Wake wa kuumba mbingu na ardhi na Rehma na Neema Zake, na kwamba Yeye Pekee Ndiye Anayestahiki kuabudiwa.
5-Kuhimiza maadili mazuri, ikiwa ni pamoja na uvumilivu na kusameheana
6-Kuthibitisha kuwa Qur-aan ni Wahy kutoka kwa Allaah (سبحانه وتعالى) kuja kwa Nabiy Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم).
Miongoni Mwa Maudhui Ya Suwrah:
1-Suwrah imefunguliwa kwa herufi zinazojulikana kama الحروف المقطعة (Al-Huruwf Al-Muqatw-twa’ah), ambazo hakuna ajuaye maana zake isipokuwa Allaah (سبحانه وتعالى). Rejea Al-Baqarah (2:1). Kisha imethibitishwa kwamba Qur-aan imetoka kwa Allaah, na kwamba Alimpa Wahy Rasuli Wake (صلى الله عليه وآله وسلم) kama Alivyowapa Wahy Rusuli wengineo, na kwamba kila kilicho mbinguni na ardhini ni Milki ya Allaah (سبحانه وتعالى).
2-Imebainishwa U’adhwama (Utukufu) wa Allaah (سبحانه وتعالى) kwamba mpaka mbingu na ardhi zinakaribia kupasuka, na kwamba Malaika wanamsabbih Allaah (سبحانه وتعالى), na kwamba wanaombea maghfirah Waumini walioko ardhini, na kwamba Allaah ni Mwingi wa Kughufuria, Mwenye Kurehemu.
3-Imethibitishwa kwamba Wahy wa Qur-aan Ameuteremsha Allaah kwa lugha ya Kiarabu, ili awaonye watu wa Ummul-Quraa [Rejea Suwrah Al-An’aam (6:92)] kuhusu Siku ya Mkusanyiko; Siku ya Qiyaamah, na kwamba huko kutakuwa na makundi mawili; moja litakuwa Jannah na jengine motoni.
4-Imetajwa kuwapinga washirikina na kuonyesha baadhi ya dalili za kubatilisha ushirikina wao.
5-Imetajwa amri ya kurudi katika Kitabu cha Allaah itakapotokea mizozo na kutofautiana.
6-Imethibitishwa kuwa Rusuli wote (عليهم السّلام) walitumwa na Risala (Ujumbe) mmoja tu, na kwamba tofauti zinazojitokeza kwa watu ni kutokana na uovu na kufuata matamanio tu.
7-Imetajwa kukaribia Qiyaamah, na msimamo wa Waumini na makafiri juu ya hilo, na kubainisha mafikio ya kila mmoja siku ya Qiyaamah.
8-Radd kwa washirikina waliomzushia Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) kwamba amemtungia Allaah uongo. Na Allaah (سبحانه وتعالى) Akawapinga hilo!
9-Zimetajwa Aayaat (Ishara, Dalili) mbalimbali za kudhihirisha Tawhiyd ya Allaah na Uwezo Wake.
10-Zimetajwa sifa kadhaa za Waumini na mojawapo ni kwamba jambo lao ni kushauriana na ndio jina la Suwrah hii tukufu.
11-Imetolewa mwongozo wa kuamiliana na dhulma, ima kulipiza au kusamehe na kusamehe ni katika mambo ya kuazimiwa.
12-Imebainishwa aina za kuteremshwa Wahy kwa Risuli Wake (عليهم السّلام).
13-Suwrah imekhitimishwa kwa kutajwa jinsi Allaah Alivyomneemesha Rasuli Wake (صلى الله عليه وآله وسلم) kwa kumpa Wahy wa Qur-aan ambayo ni Nuru Anayomwongoza Kwayo Allaah Amtakaye, na kwamba mambo yote yanaishia kwa Allaah.
043-Az-Zukhruf: Utangulizi Wa Suwrah
Alhidaaya.com [2]
Imeteremka: Makkah kwa itifaki ya ‘Ulamaa.
Idadi Za Aayah: 89
Jina La Suwrah: Az-Zukhruf
Suwrah imeitwa Az-Zukhruf (Mapambo ya Dhahabu), na inayodalilisha ni kutajwa neno hilo katika Aayah namba (35).
Miongoni Mwa Makusudio Ya Suwrah:
1-Tahadhari juu ya mtu kufitinishwa na mapambo ya uhai na dunia, ili yasiwe njia ya kuiendea shirki. [Al-Mukhtaswar Fiy Tafsiyr Al-Qur-aan Al-Kariym]
2-Kusimamisha hoja za wazi za Tawhiyd ya Allaah (سبحانه وتعالى) ardhini na mbinguni na kubatilisha na kuradd (i) madai ya washirikina ya kumshirikisha Allaah (سبحانه وتعالى) na kumsingizia kuwa Malaika ni mabinti Wake (iii) Visingizio vyao vya kuwafuata baba zao kwa upofu na kutoa mfano wa Nabiy Ibraahiym (عليه السّلام) kwani baba yake alikuwa mshirikina lakini yeye alithibitisha Tawhiyd ya Allaah. (iv) Wanaodai kuwa Nabiy ‘Iysaa (عليه السّلام) ni mwana wa Allaah na kwamba yeye ni mojawapo wa alama za Qiyaamah.
3-Kumliwaza Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) kwa maudhi aliyoyapata kutoka kwa washirikina na kubainisha kwamba mali zinazomfanya mtu kuwa mkubwa miongoni mwa watu hazimstahiki kuteremshiwa Qur-aan Tukufu.
4-Matahadharisho kuwa asiyeitafakari Qur-aan kwamba Allaah (سبحانه وتعالى) Atamwandalia shaytwaan awe rafiki mwandani kisha Siku ya Qiyaamah itakuwa ni majuto. Lakini Allaah (سبحانه وتعالى) Amemwamrisha Rasuli Wake (صلى الله عليه وآله وسلم) na Waumini kushikamana na Qur-aan kwani Qur-aan ni Tukufu mno na imeteremshwa kwa lugha ya Kiarabu ambayo ni lugha ya ufasaha kabisa.
5-Kuwabashiria Waumini neema za Jannah na kubainisha hali za makafiri na adhabu zao motoni.
Miongoni Mwa Maudhui Ya Suwrah:
1-Suwrah imefunguliwa kwa herufi zinazojulikana kama الحروف المقطعة (Al-Huruwf Al-Muqatw-twa’ah), ambazo hakuna ajuaye maana zake isipokuwa Allaah (سبحانه وتعالى). Rejea Al-Baqarah (2:1). Kisha imetukuzwa Qur-aan na kuwa imekuja kwa lugha ya Kiarabu ili watu wapate kuzingatia. (Ni maalumu kuwa lugha ya Kiarabu ni lugha pekee ya ufasaha, iliyo bayana kabisa hakuna mfano wake.) Na imethibitishwa kuwa Qur-aan iko katika daraja ya juu kabisa katika Al-Lawh Al-Mahfuwdhw (Ubao Uliohifadhiwa). Rejea Al-Buruwj (85:22).
2-Ameliwazwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) kwa yaliyomsibu kutoka kwa watu wake.
3-Imebainisha mambo yanayoonyesha Uwezo wa Allaah (سبحانه وتعالى) na Neema Zake kwa Waja Wake. Miongoni mwazo ni vipando, na imetajwa duaa ya kipando iliyothibiti pia katika Sunnah. Rejea Aayah namba (13-14).
4-Imetaja baadhi ya uzushi wa washirikina na kauli zao ovu za kumpachika Allaah (سبحانه وتعالى) kuwa Ana mabinti. Na Allaah (سبحانه وتعالى) Akawaradd kwa hoja nzito kuwa wao wenyewe hawakuwa wanapendelea watoto wa kike! Na kwa dhulma hii kubwa, watafika Kwake Siku ya Qiyaamah kuhesabiwa na kuadhibiwa!
5-Imetajwa ada ya washirikina kukhiari kufuata nyendo za baba zao. Na hii ni ada ya watu wa nyumati za nyuma kusema hayo hayo.
6-Imetajwa sehemu ya da’wah ya Nabiy Ibraahiym (عليه السلام) kwa watu wake na likathibiti neno la Tawhiyd (laa ilaaha illa Allaah) na kuendelea baada yake.
7-Imetajwa kuwa mapato ya dunia, anasa zake na mapambo kama fedha na Zukhruf (mapambo ya dhahabu), ni starehe ya muda mdogo tu, bali Aakhirah ndio bora kwa Waumini.
8-Imetahadharishwa kuwa mwenye kujiweka mbali na Ukumbusho wa Allaah, shaytwaan humuandama mtu awe rafiki yake mwandani, kisha Siku ya Qiyaamah mtu huyo atajuta na kutamani shaytwaan awe mbali naye, umbali wa Mashariki na Magharibi. Kisha wote wataingia katika adhabu.
9-Imetajwa sehemu ya kisa cha Nabiy Muwsaa (عليه السّلام) na dhulma ya Firawni kumwita mchawi, na kutakabari mno na kujifanya yeye ni bora kuliko Nabiy Muwsaa (عليه السّلام).
10-Ametajwa Nabiy ‘Iysaa (عليه السّلام) na kwamba atakuwa ni miongoni mwa alama kubwa za Qiyaamah (atakaporudi duniani).
11-Watu wa Jannah wamebashiriwa mazuri, na zikatajwa baadhi ya raha na neema za Jannah. Kisha wakatajwa wahalifu kuwa watakuwa motoni na watamuomba Mlinzi wa moto awaombee kwa Allaah Awafishe kuliko kuadhibika lakini watabakishwa kudumu motoni!
12-Imebainishwa kwamba Allaah (سبحانه وتعالى) Ndiye Muabudiwa wa haki mbinguni na ardhini. Kisha Allaah (سبحانه وتعالى) Akajitukuza Mwenyewe Mwenye Ufalme wa mbingu na ardhi, na kwamba viumbe wote watarudishwa Kwake.
13-Suwrah imekhitimishwa kwa kutajwa washirikina kuwa wanaowaomba badala ya Allaah, hawana uwezo wa kumiliki uombezi. Na kisha ikathibitisha kuwa washirikina waliamini Tawhiyd ya Ar-Rubuwbiyyah (Uola). Kisha akaliwazwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) na akaamrishwa awapuuze kwani karibuni watakuja kujua.
044-Ad-Dukhaan: Utangulizi Wa Suwrah
Alhidaaya.com [2]
Imeteremka: Makkah kwa itifaki ya ‘Ulamaa.
Idadi Za Aayah: 59
Jina La Suwrah: Ad-Dukhaan
Suwrah imeitwa Ad-Dukhaan (Moshi), na inayodalilisha ni kutajwa katika Aayah namba (10).
Miongoni Mwa Makusudio Ya Suwrah:
1-Vitisho kwa washirikina na kuwabainishia yanayowangojea ya adhabu kali duniani na Aakhirah. [Al-Mukhtaswar Fiy Tafsiyr Al-Qur-aan Al-Kariym]
2- Kuthibitisha kuteremshwa Qur-aan kutoka kwa Allaah (سبحانه وتعالى) katika Usiku Uliobarikiwa (Laylatul-Qadr).
3-Kuthibitisha Tawhiyd ya Allaah na kwamba Yeye Ndiye Mwenye kufufua na kuwakusanya waja.
4-Kubainisha Neema za Waumini Jannah na adhabu za makafiri motoni.
Miongoni Mwa Maudhui Ya Suwrah:
1-Suwrah imefunguliwa kwa herufi zinazojulikana kama الحروف المقطعة (Al-Huruwf Al-Muqatw-twa’ah), ambazo hakuna ajuaye maana zake isipokuwa Allaah (سبحانه وتعالى). Rejea Al-Baqarah (2:1). Kisha imesifiwa Qur-aan kwamba ni Kitabu kinachobainisha wazi kimatamshi na kimaana, na kwamba Qur-aan imeteremshwa Usiku wa Baraka ambao ni Laylatul-Qadr. Na kwamba Allaah (سبحانه وتعالى) Anawaonya watu kwa kile kinachowanufaisha na kuwadhuru, nako ni kule kuwapelekea Rusuli Wake Kuteremsha Vitabu, ili hoja ya Allaah (سبحانه وتعالى) iwasimamie Waja Wake. Na kwamba Usiku huo; Laylatul-Qadr, linaamuliwa na kupambanuliwa, kutoka kwenye Al-Lawh Al-Mahfuwdhw (Rejea Al-Buruwj (85:22), na kuletewa waandishi kati ya Malaika, kila jambo lililokadiriwa la muda wa kuishi na riziki katika mwaka huo na mambo mengine yatakayokuwa na kukadiriwa na Allaah (سبحانه وتعالى) mpaka mwisho wa mwaka, hayabadilishwi wala hayageuzwi.
2-Imetajwa Dukhaan (Jina la Suwrah), ni moshi utakaotoka ambao ni miongoni mwa alama kubwa Qiyaamah, na kwamba moshi huo utawafunika watu waovu iwe ni adhabu kwao na wataomba waondolewe adhabu. Lakini hawatondoshewa!
3-Imetajwa sehemu ya kisa cha Nabiy Muwsaa (عليه السّلام) na Firawni aliyetakabari akazamishwa baharini na jeshi lake.
4-Imetajwa ada ya washirikina kutokuamini kufufuliwa .
5-Imetajwa vitisho na adhabu za makafiri ukiwemo mti wa zaqquwm ambao utakuwa ndio chakula chao nao ni kama masazo ya zebaki nyeusi iliyoyeyushwa, itokote matumboni mwao.
6-Kisha wametajwa Waumini wakiwa Jannah (Peponi) kwenye kila aina ya raha na neema; zikiwemo mabustani na chemchemu, wanapata humo wanachokitamani na wataozeshwa hurulaini, na kwamba hawataonja tena umauti. Na hiyo ni Fadhila ya Allaah na ndio kufuzu kukubwa.
7-Suwrah imekhitimishwa kuambiwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) kwamba amewepesisha Qur-aan, na akaliwazwa kuwa angojee, yaani angojee ushindi wa Allaah (سبحانه وتعالى) na Adhabu Yake kwa washirikina, na wao washirikina wanangojea kwa hamu kumshinda Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم).
045-Al-Jaathiyah: Utangulizi Wa Suwrah
Alhidaaya.com [2]
Imeteremka: Makkah kwa itifaki ya ‘Ulamaa.
Idadi Za Aayah: 37
Jina La Suwrah: Al-Jaathiyah
Suwrah imeitwa Al-Jaathiyah (Kupiga magoti) na inayodalilisha ni kutajwa katika Aayah namba (28).
Miongoni Mwa Makusudio Ya Suwrah:
1-Kubainisha hali za viumbe, kutokana na dalili za kisharia na kiulimwengu, na kuzitengua hoja za wenye kupinga ufufuo, wanaofanya kiburi kwa Allaah, na kuwatisha. [Al-Mukhtaswar Fiy Tafsiyr Al-Qur-aan Al-Kariym]
2-Kuthibitisha Utukufu wa Qur-aan na miujiza yake, na uthibitisho kuwa ni kutoka kwa Allaah, na kuthibitisha Tawhiyd ya Allaah kwa Aayaat (Ishara, Dalili) za wazi..
3-Daawah (wito) wa Kiislamu na jinsi washirikina waliyopokea daawah hii kwa upinzani.
4-Bainisho kuwa Allaah (سبحانه وتعالى) Aliwapa Wana wa Israaiyl hekima, Unabii na neema nyingi ili waweze kubeba Risala ya Tawhiyd, lakini hawakufaa kubeba Risala hiyo, basi Allaah (سبحانه وتعالى) Akamchagua Nabiy Wake Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم) kubeba Risala kwa watu wote, na hili ni onyo kwa ummah wa Muhammad dhidi ya kufanya kama walivyofanya Wana wa Israaiyl.
5-Kuthibitisha ufufuo, na kuelezea baadhi ya hali zake (kufufuliwa), na kuelezea baadhi ya kauli za washirikina juu ya kufufuliwa.
Miongoni Mwa Maudhui Ya Suwrah:
1-Suwrah imefunguliwa kwa herufi zinazojulikana kama الحروف المقطعة (Al-Huruwf Al-Muqatw-twa’ah), ambazo hakuna ajuaye maana zake isipokuwa Allaah (سبحانه وتعالى). Rejea Al-Baqarah (2:1). Kisha imetukuzwa Qur-aan na imethibitishwa Aayaat (Ishara, Dalili,) za Allaah duniani kote.
2-Imetajwa adhabu kali iumizayo na inayodhalilisha kwa wazushi na waongo, kutokana na kung’ang’ania kwao ukafiri, na kuzifanyia istihzai Aayah za Allaah.
3-Imebainisha baadhi ya Neema za Allaah (سبحانه وتعالى) kwa Waja Wake.
4-Imebainisha msimamo wa Bani Israaiyl baada ya kupewa neema za Allaah (سبحانه وتعالى) ambapo walikhalifu.
5-Imetajwa ada za washirikina kutokuamini kufufuliwa. Lakini Allaah (سبحانه وتعالى) Amewabainishia kwamba halina shaka hilo!
6-Imetajwa kuwa kila ummah utapiga magoti kwa unyenyekevu na khofu. Na kila ummah utaitwa pamoja kitabu chao ambacho kimerikodi kila tendo. Na watu watahesabiwa na kulipwa matendo yao; mema na maovu.
7-Imerudi kutaja ada ya washirikina kutokuamini Qiyaamah, basi watasahauliwa motoni kama walivyosahau Siku hii kubwa mno ya kukutana na Allaah (سبحانه وتعالى), na watadumu humo motoni bila kuachiliwa kujitetea.
8-Suwrah imekhitimishwa kwa Kumhimidi Allaah (سبحانه وتعالى), Kumtukuza na kwamba Ukubwa, Uadhama, Ujalali ni Wake Pekee mbinguni na ardhini. Naye Ndiye Mwenye Enzi ya Nguvu Asiyeshindika, Mwenye Hikmah wa yote.
Faida:
Maana ya Al-Jaathiyah ni kupiga magoti kwa unyenyekevu na khofu kwa kungojea kuhesabiwa.
046-Al-Ahqaaf: Utangulizi Wa Suwrah
Alhidaaya.com [2]
Imeteremka: Makkah kwa itifaki ya ‘Ulamaa.
Idadi Za Aayah: 35
Jina La Suwrah: Al-Ahqaaf
Suwrah imeitwa Al-Ahqaaf (Ardhi ya machuguu ya mchanga), na inayodalilisha ni kutajwa katika Aayah namba (21).
Miongoni Mwa Makusudio Ya Suwrah:
1-Kubainisha kuwa wanaadam wanahitaji zaidi Risala ya Allaah (سبحانه وتعالى) na kuwaonya wanaopuuza. [Al-Mukhtaswar Fiy Tafsiyr Al-Qur-aan Al-Kariym]
2-Kuwalingania watu kusahihisha imaan zao kwa kumpwekesha Allaah (سبحانه وتعالى) na kumwamini Rasuli Wake Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم) huku wakiamini Risala ya Rusuli waliotangulia, na kuamini Siku ya Mwisho na Aliyoyatayarisha Allaah (سبحانه وتعالى) kwa malipo ya Waumini na adhabu kwa makafiri.
3-Kuthibitisha Tawhiyd ya Allaah na Uwezo Wake wa kuumba mbingu na ardhi na vilivyomo baina yake bila ya kushikwa na uchovu. Na kwamba ana Uwezo wa kuwahuisha watu baada ya kufa na kuhesabiwa.
4-Radd kwa madai ya makafiri na washirikina kuhusu Qur-aan kuwa sio sihri bali Qur-aan inatoka kwa Allaah (سبحانه وتعالى), na kwamba ni Risala ya wanaadam na majini.
5-Kuwasifu Waumini kwa imaan zao juu ya Qur-aan Tukufu, huku ukibainisha baadhi ya sifa za Waumini na sifa zao zilizo kinyume na sifa za makafiri.
Miongoni Mwa Maudhui Ya Suwrah:
1-Suwrah imefunguliwa kwa herufi zinazojulikana kama الحروف المقطعة (Al-Huruwf Al-Muqatw-twa’ah), ambazo hakuna ajuaye maana zake isipokuwa Allaah (سبحانه وتعالى). Rejea Al-Baqarah (2:1). Kisha imetukuzwa Qur-aan na kuthibitishwa kwamba ni Uteremsho kutoka kwa Allaah (سبحانه وتعالى).
2-Imethibitishwa Tawhiyd ya Allaah ya Ar-Rubuwbiyyah (Uola, Uumbaji) na kubainishwa Uwezo Wake (سبحانه وتعالى) wa kuumba mbingu na ardhi. Kisha imewaradd washirikina na kuwataka walete vile walivyoumba waabudiwa wao, au walete dalili ya ushirikiano wao na Allaah (سبحانه وتعالى) mbinguni, ikiwa ni wakweli. Kisha Allaah (سبحانه وتعالى) Akawatolea hoja kwamba wanaoombwa pasi Naye, hawawaitikii duaa zao wala hawatambui maombi yao! Kisha Siku ya Qiyaamah watakapokusanywa wote, waabudiwa wao watakuwa maadui wao, na watakanusha ibaada zao!
3-Imetajwa ada za makafiri kupachika sifa ovu Qur-aan kama sihri (uchawi), na pia kumzushia Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) kwamba ameitunga Qur-aan, ilhali kuna ushahidi wa wazi wa Allaah (سبحانه وتعالى) kwamba ni Wahy kutoka Kwake.
4-Imebainisha mwisho mwema kwa Waumini wa kuingizwa Jannah na kudumu milele kwa sababu ya kumwamini Rabb wao na wakathibitika katika Dini.
5-Imetolewa wasia wa kuwatendea ihsaan wazazi wawili, na mwanaadam kukumbushwa shida na tabu anazozipata mama za kubeba mimba mpaka kujifungua na mpaka kumaliza kunyonyesha mwana. Kisha wenye kutii hayo, wamebashiriwa kupokelewa amali zao na kuingizwa Jannah, pindi wakiomba duaa na kushukuru Neema za Allaah na kutubia Kwake wanapofikia umri mkubwa.
6-Kisha imebainishwa mwisho mbaya kwa makafiri wa kuingiziwa motoni na kuadhibiwa, kwa kukanusha kwao Risala ya haki, na kuifanyia istihzai kwa kudai kuwa ni hekaya za watu wa kale.
7-Imetajwa sehemu ya kisa cha Nabiy Huwd (عليه السّلام) na kaumu yake ambao ni kina ‘Aad, wakaazi wa Ahqaaf (ardhi ya machuguu ya mchanga), na ukanushaji wao wa Risala na Rasuli wao, na kuhimiza kwao adhabu. Basi wakateremshiwa wingu lilotanda upeoni mwao likielekea mabonde yao, wakidhani kuwa ni wingu la mvua ya kawaida, kumbe ulikuwa ni upepo wa dhoruba, wenye adhabu kali uliowaangamiza!
8-Ameliwazwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) kwa kumkumbusha kuwa, kundi la majini lilihudhuria kusikiliza Qur-aan kwa makini, wakaiamini, na wakamwamini Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم), kisha wakawaendea majini wenzao kuwalingania, wakubali Ujumbe wa Allaah (سبحانه وتعالى) kuwa ni wa haki na kuwahamasisha kwamba wataghufuriwa madhambi yao, na wataepushwa na adhabu. Na pindi wasipoitikia Risala hiyo, basi hawataweza kukwepa adhabu ya Allaah.
9-Imethibitishwa Tawhiyd ya Allaah ya Ar-Rubuwbiyyah (Uola, Uumbaji n.k), na Uwezo wa Allaah (سبحانه وتعالى) wa kufufua wafu. Kisha ikatajwa hali ya makafiri watakapohudhurishwa motoni na kuonjeshwa adhabu kwa kufru zao.
10-Suwrah imekhitimishwa kwa kuamrishwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) avute subira, kama walivyovuta subira Rusuli wenzake waliokuwa na azimio madhubuti, na kwamba asitake kuwaharakizia makafiri adhabu, kwani itakapofika Qiyaamah, watahisi kuwa kama waliishi saa moja tu duniani! Kisha itahakiki maangamizo yao.
Faida:
Al-Ahqaaf ni ardhi ya machuguu ya mchanga ambayo ni Yemen, nayo ni ya kina ‘Aad kaumu ya Huwd (عليه السّلام).
047-Muhammad: Utangulizi Wa Suwrah
Alhidaaya.com [2]
Imeteremka: Madiynah kwa itifaki ya ‘Ulamaa.
Idadi Za Aayah: 38
Jina La Suwrah: Muhammad
Suwrah imeitwa Muhammad (Jina la Nabiy صلى الله عليه وآله وسلم), na inayodalilisha ni Jina lake katika Aayah namba (2).
Miongoni Mwa Makusudio Ya Suwrah:
1-Kuwahimiza Waumini juu ya suala la kupigana vita, kwa kuwatia nguvu, na kwa kuwadhoofisha makafiri. [Al-Mukhtaswar Fiy Tafsiyr Al-Qur-aan Al-Kariym]
2-Kuwatangazia watu kwamba Allaah (سبحانه وتعالى) Anabatilisha matendo ya makafiri kwa sababu wanang'ang'ania kufuata batili, wanapinga wito wa haqq (ukweli) na kuwaweka mbali na Dini ya Allaah.
3-Kuvutia kwenye Jihaad katika Njia ya Allaah, na kuunga mkono haqq (ukweli) na kushikamana na yale ambayo Allaah (سبحانه وتعالى) Ameyateremsha kwa Nabiy Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم) na hili ndilo linalowahakikishia Waumini ushindi dhidi ya maadui zao.
4-Kubashiriwa Waumini kuwa wao ni vipenzi vya Allaah na kubashiriwa Jannah na neema zake na makafiri kubainishwa adhabu zao motoni.
5-Kudhihirisha hali za wanafiki na sifa zao, sura zao na Waislamu kutahadharishwa nao.
Miongoni Mwa Maudhui Ya Suwrah:
1-Suwrah imefunguliwa kwa kubainisha mwisho mbaya wa makafiri, na mwisho mzuri wa Waumini walioamini aliyoteremshiwa Nabiy Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم).
2-Imewahimiza Waumini kufanya ugumu katika kupambana na makafiri, na kuwachukua mateka.
3-Waumini wameahidiwa ushindi pale watakapomnusuru Allaah (سبحانه وتعالى) na Rasuli Wake (صلى الله عليه وآله وسلم), na kuwabashiria Jannah na neema ambazo wameshajulishwa nazo. Kisha makafiri wakatishiwa maangamizi na kuharibikiwa amali zao, na kuwakemea juu kuchukia kwao waliyoteremshiwa. Basi Allaah (سبحانه وتعالى) ni Mlinzi wa Waumini na makafiri hawana yeyote wa kuwalinda.
4-Waumini wamebashiriwa Jannah na neema zake humo za mabustani yenye kupitia mito chini yake, na mito yenye vinywaji aina nne safi venye kuburudisha. Juu ya hivyo watapata matunda na maghfirah. Basi hao si sawa na watu wa motoni ambao wao, vinywaji vyao ni maji yachemkayo yatakayowakatakata machango yao!
5-Imetajwa baadhi ya misimamo ya wanafiki kwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) na da’wah yake na kutaja baadhi ya sifa zao mbaya, kama vile udanganyifu wao na adabu mbaya, na uwoga wao pindi wanapoitwa katika vita vya Jihaad.
6-Imebainishwa kuwa unafiki wa wanafiki ulikua kwa sababu ya shaytwaan kuwatawala, na kuwatisha kwa mafikio mabaya katika maisha yao na baada ya mauti yao.
7-Imetaja vitisho kwa makafiri ya kuharibika matendo yao, na kwamba wana maradhi nyoyoni mwao na Allaah (سبحانه وتعالى) Atafichua chuki na niyya zao ovu.
8-Waumini wameamrishwa kumtii Allaah na Rasuli Wake (صلى الله عليه وآله وسلم) na kuwakataza kukata tamaa, na kuwabashiria nusra na ushindi. Na wameamrishwa wasinyong’onyee kutaka suluhu na makafiri, kwani Allaah Yu pamoja nao.
9-Imetanabahishwa kuwa uhai wa dunia ni mchezo na pumbao tu lakini kwa Allaah ndiko kwenye ujira mzuri.
10-Suwrah imekhitimishwa kwa kuwatahadharisha Waumini kutokana na ubakhili, na kuwalingania katika kutoa kwenye njia ya Allaah, na pindi wakikengeuka, basi Allaah (سبحانه وتعالى) ni Mkwasi na Mweza wa kuwabadilisha watu bora kuliko wao.
048-Al-Fat-h: Utangulizi Wa Suwrah
Alhidaaya.com [2]
Imeteremka: Madiynah kwa itifaki ya ‘Ulamaa.
Idadi Za Aayah: 29
Jina La Suwrah: Al-Fat-h
Suwrah imeitwa Al-Fat-h (Ushindi) yaani Ushindi wa Makkah, na inayodalilisha ni kutajwa katika Hadiyth zilizonukuliwa chini katika Fadhila na Faida na kwa kutajwa neno hili katika Aayah namba (1).
Miongoni Mwa Makusudio Ya Suwrah:
1-Kupewa bishara Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) na Waumini juu ya Al-Fat-h (Ushindi wa Makkah) na kumakinishwa (kuwa imara) katika ardhi. [Al-Mukhtaswar Fiy Tafsiyr Al-Qur-aan Al-Kariym]
2-Kumbashiria Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) na Swahaba wake (رضي الله عنهم) kwa aina mbali mbali za bishara.
3-Kuwatambulisha wanafiki na makafiri, na kubainisha uhalisia wao.
4-Kubainisha mengi katika Fadhila na Rehma za Allaah kwa Waumini.
Miongoni Mwa Maudhui Ya Suwrah:
1-Suwrah imefunguliwa kwa kumbashiria Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) na Swahaba wake (رضي الله عنهم) Al-Fat-h (Ushindi wa Makkah), na kwamba Allaah (سبحانه وتعالى) Amemghufuria Rasuli Wake (صلى الله عليه وآله وسلم) madhambi yake yaliyotangulia na yanayofuatia, na Amemtimizia Neema Zake, na kwamba Atamuongoza katika njia iliyonyooka, na Atamjaalia nusra ya nguvu.
2-Kisha Waumini wakabashiriwa kwa kuteremshiwa utulivu, na kuingizwa Jannaat, na kufutiwa maovu yao. Na wanafiki na washirikina wakaahidiwa ghadhabu za Allaah na Laana Yake juu yao, na mwishowe kuingizwa moto wa Jahannam.
3-Imetajwa bay’ah (fungamano la ahadi ya utiifu) baina ya Swahaba na Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) na Allaah (سبحانه وتعالى) Kuwaunga mkono kwa Kuwa pamoja nao kwa Ujuzi Wake, Anawasikia na Anawaona na Anajua niya zao. Na hiyo ilikuwa chini ya mti. Na hiyo ni bay’ah inayojulikana Bay’atur-Ridhwaan (fungamano la ahadi liloridhiwa na Allaah) kama ilivyotajwa katika Aayah namba (18), kuwa Allaah Amewaridhia Waumini waliofungamana ahadi ya utiifu chini ya mti, Akawateremshia utulivu na Akawaahidi ushindi, na kuwajaalia ghanima za vita nyingi.
4-Imebainishwa hali halisi ya wanafiki na washirikina kama vile kubakia nyuma wasiende kupigana Jihaad, kisha watake kuombewa maghfira. Kisha pindi Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) na Swahaba wake (رضي الله عنهم) walipoondoka kwenda Khaybar, wanafiki wakataka kwenda nao ili wapate kupewa ghanima (ngawira za vita).
5-Imebainishwa fadhila za Allaah na Rehma Zake kwa Waja Wake Waumini kama, kuwazuia wasiingie Makkah kwanza kupigana vita na washirikina, juu ya kuwa Allaah (سبحانه وتعالى) Aliwajaalia ushindi, na washirikina wakawa chini ya udhibiti wa Waumini. Basi Kuwazuia Kwake, ni kutokana na Hikma Zake (سبحانه وتعالى) kwamba, wasije kuwakanyaga na kuwaua Waumini waliolazimika kubakia Makkah. Na pia, kwa kuwa Allaah (سبحانه وتعالى) ni Mjuzi wa ghaibu, basi Allaah (سبحانه وتعالى) Alijua kuwa watakuweko washirikina watakaokuja kuingia Uislamu baada ya Fat-h Makkah (Ushindi wa Makkah), kwani Allaah (سبحانه وتعالى) Anamhidi Amtakaye kwa Rehma Zake. Na washirikina wengi wakaja kuingia Uislamu baada ya Fat-h Makkah.
6-Allaah (سبحانه وتعالى) Amemsadikisha Rasuli Wake (صلى الله عليه وآله وسلم) ndoto Aliyomuotesha, kwamba wataingia Al-Masjidul-Haraam kwa amani, hali ya kuwa wamenyoa vichwa vyao na wengine wamepunguza nywele. Na Akajaalia kabla ya kuingia Makkah ushindi, na ufunguzi wa Khaybar.
7-Imethibitishwa kwa dalili za wazi, kwamba Dini ya Kiislamu itakuja kushinda dini zote ulimwenguni.
8-Suwrah imekhitimishwa kwa kuelezwa sifa za Waumini juu ya makafiri, kuwa Waumini ni wakali zaidi dhidi ya makafiri, lakini wanahurumiana baina yao. Na ni wenye kusimamisha Swalaah na kutafuta Fadhila na Radhi za Allaah. Na kwamba alama zao zinadhihirika katika nyuso zao kutokana na athari za kusujudu, basi Allaah Amewaahidi Waumini watendao mema, maghfira na ujira adhimu ambao ni kuwaingiza Peponi.
Fadhila Za Suwrah:
Suwrah Al-Fat-h ni Suwrah kipenzi kabisa kwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم):
عَنْ زَيْدِ بْنِ أَسْلَمَ، عَنْ أَبِيهِ، أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم كَانَ يَسِيرُ فِي بَعْضِ أَسْفَارِهِ وَعُمَرُ بْنُ الْخَطَّابِ يَسِيرُ مَعَهُ لَيْلاً، فَسَأَلَهُ عُمَرُ بْنُ الْخَطَّابِ عَنْ شَىْءٍ، فَلَمْ يُجِبْهُ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم ثُمَّ سَأَلَهُ فَلَمْ يُجِبْهُ، ثُمَّ سَأَلَهُ فُلَمْ يُجِبْهُ، فَقَالَ عُمَرُ بْنُ الْخَطَّابِ ثَكِلَتْ أُمُّ عُمَرَ، نَزَرْتَ رَسُولَ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم ثَلاَثَ مَرَّاتٍ، كُلَّ ذَلِكَ لاَ يُجِيبُكَ. قَالَ عُمَرُ فَحَرَّكْتُ بَعِيرِي، ثُمَّ تَقَدَّمْتُ أَمَامَ النَّاسِ، وَخَشِيتُ أَنْ يُنْزَلَ فِيَّ الْقُرْآنُ، فَمَا نَشِبْتُ أَنْ سَمِعْتُ صَارِخًا يَصْرُخُ بِي فَقُلْتُ لَقَدْ خَشِيتُ أَنْ يَكُونَ نَزَلَ فِيَّ قُرْآنٌ. فَجِئْتُ رَسُولَ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم فَسَلَّمْتُ عَلَيْهِ فَقَالَ " لَقَدْ أُنْزِلَتْ عَلَىَّ اللَّيْلَةَ سُورَةٌ لَهِيَ أَحَبُّ إِلَىَّ مِمَّا طَلَعَتْ عَلَيْهِ الشَّمْسُ ". ثُمَّ قَرَأَ " إِنَّا فَتَحْنَا لَكَ فَتْحًا مُبِينًا
Amesimulia Zayd Bin Aslam (رضي الله عنه): Baba yangu amesema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alikua akitembea katika baadhi ya safari zake, na ‘Umar Bin Al-Khatw-twaab (رضي الله عنه) akitembea pamoja nae wakati wa usiku. ‘Umar akamuuliza Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) kitu, ikawa hakumjibu. Kisha akamuuliza tena lakini hakumjibu. Kisha akamuuliza tena lakini hakumjibu. ‘Umar akasema: Amekukosa mama yako ee ‘Umar! Umemsisitiza Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) mara tatu na mara zote hakujibu! ‘Umar (رضي الله عنه) akasema: Nikamuondoa mnyama wangu, kisha nikatangulia mbele ya Waislamu. Nikaogopa isijeteremka kwangu mimi Qur-aan, basi sikuingia katika jambo jengine. Haujapita muda hata kidogo mara nikasikia mpiga ukelele akiniita. Nikasema: Niliogopa isijekua imeteremka Qur-aan kunihusu mimi! Nikaenda kwa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) nikamsalimia, akasema: “Nimeteremshiwa usiku huu, Suwrah ambayo ni kipenzi zaidi kwangu kuliko chochote kilicho chomozewa na jua (ulimwenguni).” Kisha akasoma:
إِنَّا فَتَحْنَا لَكَ فَتْحًا مُّبِينًا﴿١﴾
“Hakika Tumekupa ushindi (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم), ushindi bayana.” [Al-Fat-h (48:1) – Al-Bukhaariy]
Faida:
حَدَّثَنَا عَبْدُ اللَّهِ بْنُ مُحَمَّدٍ، حَدَّثَنَا يَحْيَى بْنُ آدَمَ، حَدَّثَنَا يَزِيدُ بْنُ عَبْدِ الْعَزِيزِ، عَنْ أَبِيهِ، حَدَّثَنَا حَبِيبُ بْنُ أَبِي ثَابِتٍ، قَالَ حَدَّثَنِي أَبُو عَنْ وَائِلٍ، قَالَ كُنَّا بِصِفِّينَ فَقَامَ سَهْلُ بْنُ حُنَيْفٍ فَقَالَ أَيُّهَا النَّاسُ اتَّهِمُوا أَنْفُسَكُمْ فَإِنَّا كُنَّا مَعَ رَسُولِ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم يَوْمَ الْحُدَيْبِيَةِ، وَلَوْ نَرَى قِتَالاً لَقَاتَلْنَا، فَجَاءَ عُمَرُ بْنُ الْخَطَّابِ فَقَالَ يَا رَسُولَ اللَّهِ، أَلَسْنَا عَلَى الْحَقِّ وَهُمْ عَلَى الْبَاطِلِ فَقَالَ " بَلَى ". فَقَالَ أَلَيْسَ قَتْلاَنَا فِي الْجَنَّةِ وَقَتْلاَهُمْ فِي النَّارِ قَالَ " بَلَى ". قَالَ فَعَلَى مَا نُعْطِي الدَّنِيَّةَ فِي دِينِنَا أَنَرْجِعُ وَلَمَّا يَحْكُمِ اللَّهُ بَيْنَنَا وَبَيْنَهُمْ فَقَالَ " ابْنَ الْخَطَّابِ، إِنِّي رَسُولُ اللَّهِ، وَلَنْ يُضَيِّعَنِي اللَّهُ أَبَدًا ". فَانْطَلَقَ عُمَرُ إِلَى أَبِي بَكْرٍ فَقَالَ لَهُ مِثْلَ مَا قَالَ لِلنَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم فَقَالَ إِنَّهُ رَسُولُ اللَّهِ، وَلَنْ يُضَيِّعَهُ اللَّهُ أَبَدًا. فَنَزَلَتْ سُورَةُ الْفَتْحِ، فَقَرَأَهَا رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم عَلَى عُمَرَ إِلَى آخِرِهَا. فَقَالَ عُمَرُ يَا رَسُولَ اللَّهِ، أَوَفَتْحٌ هُوَ قَالَ " نَعَمْ ".
Amesimulia Abuu Waail (رضي الله عنه): Tulikuwa Swiffiyn, Sahl bin Hunayf (رضي الله عنه) akasimama na kusema: Enyi watu! Tuhumuni nafsi zenu, kwani sisi tulikuwa pamoja na Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) siku ya Hudaybiyah na lau kama tungeambiwa tupigane tungelipigana. ‘Umar Bin Al-Khatw-twaab (رضي الله عنه) akaja na akasema: Ee Rasuli wa Allaah! Hivi hatukuwa katika haki na wao katika baatwil? Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akasema: “Ndiyo (tuko katika haki).” Akasema: Hivi hawatakuwa Peponi waliouawa miongoni mwetu na watu wao waliouawa wao kuwa motoni? Akasema: “Ndiyo.” ‘Umar akasema: Je, ni kwa misingi ipi basi tunaitia udhalili Dini yetu? Hivi turudi kabla Allaah Hajahukumu kati yetu na wao? Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akasema: “Ibn Al-Khatw-twaab! Mimi ni Rasuli wa Allaah, na Allaah Hanitupi abadani!” ‘Umar akaenda kwa Abubakar, akamwambia kama alivyomuambia Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akasema: Yule ni Rasuli wa Allaah, na Allaah Hampotezi abadani!” Basi ikateremka Suwrah Al-Fat-h (48), Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akamsomea ‘Umar mpaka mwisho wa Suwrah. ‘Umar akasema: Ushindi ndio huo? Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akasema: “Naam.” [Al-Bukhaariy]
049-Al-Hujuraat: Utangulizi Wa Suwrah
Alhidaaya.com [2]
Imeteremka: Madiynah kwa itifaki ya ‘Ulamaa.
Idadi Za Aayah: 18
Jina La Suwrah: Al-Hujuraat
Suwrah imeitwa Al-Hujuraat (Vyumba), na inayodalilisha ni kutajwa neno katika Aayah namba (4).
Miongoni Mwa Makusudio Ya Suwrah:
1-Kuutibu ulimi, na kubainisha athari yake katika imaan ya mtu mmoja mmoja na katika jamii. [Al-Mukhtaswar Fiy Tafsiyr Al-Qur-aan Al-Kariym]
2-Kuwaongoza Waumini katika tabia njema mbele ya Allaah (سبحانه وتعالى) na Rasuli Wake (صلى الله عليه وآله وسلم) na Waumini wao kwa wao, na kuiweka jamii katika usalama na amani.
3-Kubainisha kwamba ukabila hauna thamani mbele ya Allaah (سبحانه وتعالى) bila ya kuwa na taqwa.
4-Kubainisha imaan ya uhakika.
Miongoni Mwa Maudhui Ya Suwrah:
1-Suwrah imefunguliwa kwa kuwaelimisha Waumini miongoni mwa akhlaaq na adabu zinazowajibika kwao kwa Muumba wao na Rasuli Wake (صلى الله عليه وآله وسلم). Nazo ni kutokuamua jambo la Sharia ya Dini kinyume na Allaah na Rasuli Wake (صلى الله عليه وآله وسلم). Kutokumpandishia sauti Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) wanapoongea wenyewe, au wanapoongea naye. Kutokumuingilia nyumbani kwake bila ya idhini.
2-Waumini wameamrishwa kuchunguza kwanza na kuthibitisha usahihi wa khabari zinazowafikia kabla ya kuhukumu na kuchukua hatua ya jambo.
3-Imebainisha baadhi ya Fadhila za Allaah kwa Waumini.
4-Imeongoza Waumini lipasalo kufanywa pindi yanapotokea mapigano kati ya makundi mawili ya Kiislamu, na katika kusuluhisha baina yao, na kulipiga vita kundi linalochupa mipaka pindi linapoendelea katika uovu wake na kukataa suluhu, mpaka lirudi katika Amri ya Allaah (سبحانه وتعالى).
5-Imewakataza Waumini kufanyiana kejeli, na kuitana majina maovu, na kuwaamrisha kujiepusha kuwadhania wengine dhana mbaya, na kuwakataza kuchunguzana, na ghiybah (kusengenya).
6-Imetoa wito kwa watu kwamba, wao wote wameumbwa kutokana na mume na mke, na kwamba mbora wao na mtukufu zaidi mbele ya Allaah ni yule mwenye taqwa.
7-Imewajibu mabedui waliodai kuwa wameamini pasi na kutulizana imaan katika nyoyo zao, na kuziweka wazi sifa za Waumini wa kweli.
8-Imekatazwa kujifakharisha mbele ya Allaah na Rasuli Wake (صلى الله عليه وآله وسلم) kwa imaan, na kwamba Neema ni za Allaah (سبحانه وتعالى), na fadhila katika kuongoza (watu) kwenye imaan.
9-Suwrah imekhitimishwa kwa kutajwa Ilimu ya Allaah iliyozunguka yaliyofichika mbinguni na aridhini, na kwamba Allaah ni Mwenye kuona yote yatendwayo.
050-Qaaf: Utangulizi Wa Suwrah
Alhidaaya.com [2]
Imeteremka: Makkah kwa itifaki ya ‘Ulamaa.
Idadi Za Aayah: 45
Jina La Suwrah: Qaaf
Suwrah imeitwa Qaaf, na inayodalilisha ni kutajwa katika katika Hadiyth zilizonukuliwa chini katika Fadhila, katika Aayah namba (1).
Miongoni Mwa Makusudio Ya Suwrah:
1-Mawaidha ya nyoyo juu ya kifo na ufufuo. [Al-Mukhtaswar Fiy Tafsiyr Al-Qur-aan Al-Kariym]
2-Kuwakumbusha watu Utukufu wa Qur-aan.
3-Kuelezea misingi ya imaan ambayo makafiri waliikanusha nayo ni kufufuliwa Siku ya Qiyaamah, kukusanywa, kuhesabiwa matendo. Na pia msingi wa Risala (Ujumbe) na Rusuli wa Allaah.
4-Wasifu Waumini Siku ya Qiyaamah na jinsi Allaah (سبحانه وتعالى) Alivyowaandalia malipo mema.
Miongoni Mwa Maudhui Ya Suwrah:
1-Suwrah imefunguliwa kwa herufi zinazojulikana kama الحروف المقطعة (Al-Huruwf Al-Muqatw-twa’ah), ambazo hakuna ajuaye maana zake isipokuwa Allaah (سبحانه وتعالى). Rejea Al-Baqarah (2:1). Kisha imeitukuza na kuisifu Qur-aan kwa sifa ya Al-Majiyd.
2-Imetaja madai ya washirikina na kupinga kwao Unabii pamoja na kufufuliwa, na radd juu ya hayo.
3-Imehimizwa kutazama uumbwaji wa mbingu na vilivyomo ndani yake, na uumbwaji wa ardhi na vilivyopo juu yake, na kuota mimea na mazao, na kuteremshwa maji mbinguni yenye baraka yanayohuisha ardhi baada ya kufa kwake, na hii ni dalili ya wazi ya kuhuishwa baada ya mauti.
4-Imetajwa kukadhibisha kwa (i) Kaumu ya Nabiy Nuwh (عليه السّلام) (ii) Watu wa Ar-Rass (kisima) (iii) Kaumu ya Thamuwd wa Nabiy Swaalih (عليه السّلام) (iv) Kaumu ya ‘Aad watu wa Nabiy Huwd (عليه السّلام) (v) Watu wa Nabiy Luutw (عليه السّلام) (vi) Watu wa Al-Aykah (kichakani) wa Nabiy Shu’ayb (عليه السّلام) (vii) Kaumu ya Tubba’ (mfalme wa Yemen) basi tishio Alilowaahidi Allaah kwa ukafiri wao, likathibiti.
5-Imekumbushwa kuwa Allaah ni Mjuzi wa yanayowazwa katika nafsi, na kwamba kuna Malaika wa kuliani na kushotoni wanaoandika kila jambo hata kauli iwe ndogo vipi inaandikwa katika kitabu kinachorekodi matendo.
6–Imetajwa sakaraatul-mawt na Malaika watakaosukuma watu katika ardhi ya mkusanyiko na wengineo watakaoshuhudia matendo Qiyaamah. Kisha kila kafiri, mshirikina na mvukaji mipaka ataingizwa Jahannam. Waliopotoshwa watalaumiana na mashaytwaan waliowapotosha, na Jahannam itajazwa kwa watu na majini.
7-Kisha Waumini wameahidiwa kuingizwa Jannah kwa utiifu wao na kumkhofu Rabb wao kwa ghaibu. Basi watapokelewa kwa Salaam na watapata wanayoyatamani humo na watadumu milele.
8-Ameliwazwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) kwa yaliyomsibu kutoka kwa watu wake. Akaelekezwa katika yatakayomsaidia kuvuta subira; miongoni mwayo ni Kumsabbih Allaah usiku na jioni na kila baada ya Swalaah.
9-Imeelezwa baadhi ya matukio ya Siku ya Qiyaamah kama kupulizwa baragumu na watu watoke makaburini mwao, wafike katika mkusanyiko.
10-Suwrah imekhitimishwa kwa kuliwazwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) na kuamrishwa akumbushe kwa Qur-aan mwenye kukhofu maonyo ya Allaah na Adhabu Zake.
Fadhila Za Suwrah:
1-Suwrah Qaaf inapendekezwa kuisoma katika minbari, Swalaah ya Ijumaa.
عَنْ أُمِّ هِشَامٍ بِنْتِ حَارِثَةَ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهَا قَالَتْ: مَا أَخَذْتُ: "ق وَالْقُرْآنِ اَلْمَجِيدِ", إِلَّا عَنْ لِسَانِ رَسُولِ اَللَّهِ - صلى الله عليه وسلم -يَقْرَؤُهَا كُلَّ جُمُعَةٍ عَلَى اَلْمِنْبَرِ إِذَا خَطَبَ اَلنَّاسَ رَوَاهُ مُسْلِمٌ
Amesimulia Ummu Hishaam Bint wa Haarithah (رضي الله عنها): Sikuichukua
ق ۚ وَالْقُرْآنِ الْمَجِيدِ﴿١﴾
“Qaaf. Naapa kwa Qur-aan Al-Majiyd”
Isipokua kutoka kwenye ulimi wa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akiisoma kila Siku ya Ijumaa juu ya mimbari pindi anapo wakhutubia watu. [Muslim]
2-Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alikuwa akiisoma Suwrah Qaaf katika Swalaah za ‘Iyd:
عَنْ أَبِي وَاقِدٍ اللَّيْثِيِّ قَالَ: { كَانَ اَلنَّبِيُّ - صلى الله عليه وسلم -يَقْرَأُ فِي اَلْأَضْحَى وَالْفِطْرِ بِـ (ق), وَ (اقْتَرَبَتْ). أَخْرَجَهُ مُسْلِمٌ
Amesimulia Waaqid Al-Laythiyy (رضي الله عنه): Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alikuwa akisoma katika (‘Iyd) Alfitwri na Al-Adhwhaa ق (Suwrah 50) na اقْتَرَبَتْ (Suwrah 54). [Muslim]
3-Suwrah ya Qaaf ndio ya kwanza katika Suwrah za Mufasw-swal (yaani zinazokithiri kutenganishwa kwa BismiLLaah kutokana na ufupi wake) kwa kauli iliyotiwa nguvu na ‘Ulamaa.
051-Adh-Dhaariyaat: Utangulizi Wa Suwrah
Alhidaaya.com [2]
Imeteremka: Makkah kwa itifaki ya ‘Ulamaa.
Idadi Za Aayah: 60
Jina La Suwrah: Adh-Dhaariyaat
Suwrah imeitwa Adh-Dhaariyaat (Pepo zinazopeperusha vumbi kuzitawanya), na inayodalilisha ni kutajwa mwanzo kabisa katika Aayah namba (1)
Miongoni Mwa Makusudio Ya Suwrah:
1-Kuwafahamisha majini na wanaadam kuwa rizki yao inatoka kwa Allaah (سبحانه وتعالى) Pekee ili watekeleze ibaada kwa ikhlaasw. [Al-Mukhtaswar Fiy Tafsiyr Al-Qur-aan Al-Kariym]
2-Kusimamisha dalili ya kwamba ibaada haiwi isipokua kwa Allaah (سبحانه وتعالى) Pekee na kwamba kufufuliwa ni kweli.
Miongoni Mwa Maudhui Ya Suwrah:
1-Suwrah imefunguliwa kwa Kiapo cha Allaah (سبحانه وتعالى) kuapia baadhi ya vitu Alivyoviumba kama vile Adh-Dhaariyaat (pepo zinazopeperusha vumbi kuzitawanya), mawingu, na vinginevyo. Kisha ikafuatilia jibu la kiapo ambalo, kuthibitisha kuwa kufufuliwa na kulipwa yote ni kweli.
2-Kisha Allaah (سبحانه وتعالى) Akaendelea kuapia kwa mbingu zilizojaa njia madhubuti na kwa kufuatilia madai ya wenye kukadhibisha, na Kuwaahidi adhabu ya moto.
3-Imetajwa Aliyoyaanda Allaah (سبحانه وتعالى) Peponi kwa wenye kumcha Yeye Allaah (عزّ وجلّ), na zikatajwa sifa zao kuwa ni wenye kuamka usiku kwa ajili ya ibaadah, na wenye kuomba maghfira kabla ya Alfajiri, na wenye kutoa baadhi ya mali zao kwa wahitaji.
4-Imetajwa baadhi ya Ishara na Dalili za Allaah ambazo wenye yaqini wanaziamini.
5-Imethibitishwa kuwa rizki za wanaadam zinatoka kwa Allaah (سبحانه وتعالى) Pekee na ikaapiwa jambo hili kwa Rabb wa mbingu na ardhi ya kwamba ni haqq (kweli)!
6-Imetajwa baadhi ya visa vya Manabii akianziwa Nabiy Ibraahiym (عليه السّلام) pindi Malaika walimwendea kwake na ikabainishwa ukarimu wake kwa wageni. Kisha akabashiriwa yeye na mkewe kujaaliwa mwana ambaye ni Is-haaq, juu ya kuwa wamefikia umri wa uzee.
7-Kisha Malaika hao wakaelezea kusudio lao la kutumwa kuwa waelekee kwa kaumu ya Nabiy Luutw (عليه السّلام) kuwaangamiza kwa kufru na uasi wao wa matendo yao machafu yanayokwenda kinyume na maadili sahihi.
8-Ikatajwa pia Nabiy Muwsaa (عليه السّلام) alipotumwa kwa Firawni na miujiza bayana, lakini Firawni akafanya kibri na kumpachika Nabiy Muwsaa kwa sifa ovu ya uchawi au majnuni. Basi akaangamizwa kwa gharka pamoja na jeshi lake.
9-Kisha kaumu nyenginezo; kaumu ya ‘Aad na maangamizo yao ya upepo mkali wa dhoruba ulioangamiza kila kitu. Kisha kaumu ya Thamuwd na maangamizi yao ya radi na umeme. Kisha kaumu ya Nabiy Nuwh (عليه السّلام).
10-Yametajwa yanadalilisha Uwezo na Ukamilifu wa Allaah (سبحانه وتعالى), Muumbaji wa mbingu na ardhi na kwamba Ameumba kila kitu kwa jozi mbili.
11-Imetajwa onyo la kutokuabudu asiyekuwa Allaah.
12-Ameamrishwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) ajitenge mbali na washirikina aepukane na maudhi yao.
13-Imebainishwa lengo na sababu ya kuwaumba majini na wanaadam kwa ajili ya kumwabudu Allaah (سبحانه وتعالى) Pekee.
14-Imetajwa kuwa umuhimu wa daawah na kwamba ukumbusho na mawaidha yananufaisha Waumini.
16-Suwrah imekhitimishwa kwa kuwatishia washirikina ya kuwa itawapata sehemu katika adhabu kama ile itakayowapata wale wanaofanana nao miongoni mwa wenye kukadhibisha, na kuwatishia makafiri kutokana na Siku watakayorejeshwa kwa Allaah kuhesabiwa na kuadhibiwa.
052-Atw-Twuur: Utangulizi Wa Suwrah
Alhidaaya.com [2]
Imeteremka: Makkah kwa itifaki ya ‘Ulamaa.
Idadi Za Aayah: 49
Jina La Suwrah: Atw-Twuur
Suwrah imeitwa Atw-Twuur (Mlima), na yanayodalilisha ni kutajwa katika Hadiyth zilizonukuliwa chini katika Faida. Na pia kwa kutajwa mwanzo kabisa Aayah namba (1). Na Mlima huo ni ambao Allaah (سبحانه وتعالى) Aliongea na Nabiy Muwsaa (عليه السّلام).
Miongoni Mwa Makusudio Ya Suwrah:
1-Hoja na dalili zinazopinga shubha za wanaomkadhibisha Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) [Al-Mukhtaswar Fiy Tafsiyr Al-Qur-aan Al-Kariym]
2-Kuthibitisha kufufuliwa, na kubainisha mwisho mbaya wa wenye kukadhibisha, na mwisho mzuri wa Waumini.
3-Majibu juu ya uzushi wa washirikina na uongo wao.
Miongoni Mwa Maudhui Ya Suwrah:
1- Suwrah imefunguliwa kwa Kiapo cha Allaah (سبحانه وتعالى) kuapia baadhi ya vitu Alivyoviumba kama vile Atw-Twuur (Mlima) na Kitabu kilichoandikwa (katika Lawh Al-Mahfuwdhw au Qur-aan), na vinginevyo vinavyodalilisha Uwezo Wake Allaah (سبحانه وتعالى) wa Uumbaji. Kisha ikafuatia jawabu la kiapo kuthibitisha kutokea Adhabu ya Allaah (سبحانه وتعالى) na kwamba hakuna wa kuizuia.
2-Zimetajwa baadhi ya matukio ya Siku ya Qiyaamah, na Ahadi ya Allaah kwa wanaokadhibisha, na kubainisha mwisho wao mbaya wa kuingizwa katika moto wa Jahannam.
3-Zimetajwa Neema kadhaa Alizoziandaa Allaah (سبحانه وتعالى) Peponi kwa wenye kumcha Yeye Allaah (سبحانه وتعالى), na Waumini kuahidiwa kukutana na dhuriya wao pindi wote wakiendelea kuthibitika katika imaan zao. Na Allaah (سبحانه وتعالى) Akaendelea kutaja neema za humo Peponi na kwamba Waumini watakabiliana kukumbushana mema yao ya duniani na kumshukuru Allaah kwa kuwafadhilisha na kuokolewa na moto.
4-Zikafuatilia Aayah kadhaa zinazotaja Ishara na Dalili mbalimbali za Tawhiyd ya Allaah (سبحانه وتعالى) na kuwaradd washirikina shubha zao, shirki na kufru zao, na uovu wao wa kumpachika Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) sifa ovu, pamoja na kumsingizia Allaah kuwa Ana mabinti. Na hayo ni katika kumliwaza Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) na kumtaka awapuuze, nao wangojee adhabu na maangamizi.
5-Suwrah imekhitimishwa kwa kumliwaza tena Nabiya avute subira kwa ibaada na Dhikru-Allaah nyakati zote na katika Dhikru-Allaah hizo ni Kumsabbih na Kumhimidi Rabb.
Faida:
Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alisoma Suwrah Atw-Twuur katika Swalaah ya Maghrib:
حَدَّثَنِي إِسْحَاقُ بْنُ مَنْصُورٍ، حَدَّثَنَا عَبْدُ الرَّزَّاقِ، أَخْبَرَنَا مَعْمَرٌ، عَنِ الزُّهْرِيِّ، عَنْ مُحَمَّدِ بْنِ جُبَيْرٍ، عَنْ أَبِيهِ، قَالَ سَمِعْتُ النَّبِيَّ صلى الله عليه وسلم يَقْرَأُ فِي الْمَغْرِبِ بِالطُّورِ، وَذَلِكَ أَوَّلَ مَا وَقَرَ الإِيمَانُ فِي قَلْبِي.
Amesimulia Jubayr Bin Mutw’im (رضي الله عنه): Nilimsikia Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akisoma Suwrah Atw-Twuur katika Swalaah ya Magharibi, na hicho ndicho cha kwanza kilichopandikiza imaan moyoni mwangu. [Al-Bukhaariy]
Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alisoma Suwrah Atw-Twuur alipokuwa akiswali pembeni ya Al-Ka’bah.
حَدَّثَنَا إِسْمَاعِيلُ، حَدَّثَنَا مَالِكٌ، عَنْ مُحَمَّدِ بْنِ عَبْدِ الرَّحْمَنِ بْنِ نَوْفَلٍ، عَنْ عُرْوَةَ بْنِ الزُّبَيْرِ، عَنْ زَيْنَبَ بِنْتِ أَبِي سَلَمَةَ، عَنْ أُمِّ سَلَمَةَ ـ رضى الله عنها ـ زَوْجِ النَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم قَالَتْ شَكَوْتُ إِلَى رَسُولِ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم أَنِّي أَشْتَكِي. فَقَالَ " طُوفِي مِنْ وَرَاءِ النَّاسِ، وَأَنْتِ رَاكِبَةٌ ". فَطُفْتُ وَرَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم حِينَئِذٍ يُصَلِّي إِلَى جَنْبِ الْبَيْتِ، وَهْوَ يَقْرَأُ وَالطُّورِ * وَكِتَابٍ مَسْطُورٍ
Amesimulia Ummu Salamah mke wa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Nilimshtakia Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) kuhusu maradhi yangu, akasema, "Fanya Twawaaf huku ukiwa juu ya mnyama nyuma ya watu." Nikafanya hivyo, na kwa wakati huo Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alikuwa akiswali pembeni ya Ka’bah na kusoma Suwrah Atw-Twuur. [Al-Bukhaariy]
053-An-Najm: Utangulizi Wa Suwrah
Alhidaaya.com [2]
Imeteremka: Makkah kwa itifaki ya ‘Ulamaa.
Idadi Za Aayah: 62
Jina La Suwrah: An-Najm
Suwrah imeitwa An-Najm (Nyota), na yanayodalilisha ni kutajwa kwake katika Hadiyth zilizonukuliwa chini katika Fadhila. Na pia kwa kutajwa mwanzo kabisa Suwrah, Aayah namba (1).
Miongoni Mwa Makusudio Ya Suwrah:
1-Kuthibitisha kuwa Wahy ni kweli, na kwamba Unatoka kwa Allaah (عزّ وجلّ). [Al-Mukhtaswar Fiy Tafsiyr Al-Qur-aan Al-Kariym]
2-Kuthibitisha dalili ya Tawhiyd ya Allaah (سبحانه وتعالى).
3-Kuthibitisha ya kwamba Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) ni mkweli katika kile anachokifikisha kutoka kwa Allaah (سبحانه وتعالى).
Miongoni Mwa Maudhui Ya Suwrah:
1-Suwrah imefunguliwa kwa kiapo cha Allaah (عزّ وجلّ) kuapia An-Najm (Nyota). Kisha likaja jibu la kiapo ambalo ni yaliyotajwa kuthibitisha ukweli wa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) kutimiza amri za Wahy kutoka kwa Rabb wake, na kwamba hasemi kwa matamanio yake bali ni Wahy aliofunuliwa. Na katika hayo, ni yale yaliyotokea katika Safari ya Al-Israa Wal-Mi’raaj.
2-Imetajwa wasifu wa Jibriyl (عليه السّلام) kama vile kuwa ni mwaminifu wa Wahy, na wasifu wa nguvu zake na ukomavu wake, na muonekano wake ulio jamili, na umbile lake Alilomuumba Allaah (عزّ وجلّ) ambalo Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alimuona.
3-Katika yaliyotajwa ya safari ya Al-Israa wal-Mi’raaj, ni Radd ya Allaah (سبحانه وتعالى) kwa washirikina kwa kumtilia shaka Rasuli Wake (صلى الله عليه وآله وسلم) kuhusu safari hiyo, na shaka yao ya kumuona Jibriyl (عليه السّلام).
4-Allaah (سبحانه وتعالى) Anawaradd washirikina kwa dhulma yao kubwa, ya kumsingizia Allaah (سبحانه وتعالى) kwamba Ana mabinti, na kubainisha kuwa majina ya waabudiwa wao ni majina waliyowaita wao tu, na kwamba wana dhana za hisia tu, zisizo na ukweli.
5-Imethibitishwa kwamba hakuna atakaeruhusika kutoa ash-shafaa’ah (uombezi) isipokuwa ambaye Allaah (سبحانه وتعالى) Atamtolea idhini na kumridhia.
6-Imebainishwa uadilifu wa Allaah (سبحانه وتعالى) wa kuwalipa waovu kwa uovu, na kuwalipa watendaji mema kwa mema. Kisha ikabainishwa Rehma Yake Allaah (سبحانه وتعالى) ya kuwaghufuria waja. Na ikabainishwa upana wa Ilimu Yake (سبحانه وتعالى) na Kuyajua ya ghaibu; Anamjua anayepotoka na anayehidika, Anajua yanayojiri katika fuko la uzazi la mama, na Anajua yaliyomo nyoyoni mwa wanaadam. Akakataza mtu kujitukuza mwenyewe.
7-Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) analiwazwa kuwapuuza na kujitenga na wanaokengeuka na kujiweka mbali na Ukumbusho wa Allaah na badala yake akajishughulisha na dunia na anasa zake.
8-Imetajwa baadhi ya radd na hoja kwa washirikina. Na ikatajwa kuwa hakuna atakayebeba dhambi za mwenziwe, na kwamba hakuna amali atakayolipwa mtu isipokuwa tu ile aliyoifanyia juhudi duniani na kuifanyia kazi, na kwamba mwisho wa mambo yote yanaishia kwa Allaah.
9-Ukumbusho kwa Rasuli Wake (صلى الله عليه وآله وسلم) kuhusu nyumati zilizotangulia kabla yake, kwamba waliwakadhibisha Rusuli wao kama vile alivyokadhibishwa yeye na watu wake. Na yakatajwa maangamizi yao. Nao ni kina ‘Aad kaumu ya Nabiy Huwd (عليه السّلام), kina Thamuwd kaumu ya Nabiy Swaalih (عليه السّلام), kaumu ya Nuwh (عليه السّلام), na waliopinduliwa miji yao chini juu ambao ni watu wa Nabiy Luutw (عليه السّلام).
10-Imetajwa mshangao kuhusu washirikina wanavyoghafilika na Qur-aan na kuidharau na kuipuuza wanapoisikia na badala yake kushughulika na anasa za dunia.
11-Suwrah imekhitimishwa kwa amri ya kumnyenyekea Allaah (سبحانه وتعالى) na kumwabudu na kumsujudia.
Fadhila Za Suwrah:
1-Suwrah An-Najm ni Suwrah ya kwanza kuteremshwa ndani yake Sijdah ya Tilaawah (Sijda inaposomwa Qur-aan).
عَنْ عَبْدِ اللَّهِ ـ رضى الله عنه ـ قَالَ أَوَّلُ سُورَةٍ أُنْزِلَتْ فِيهَا سَجْدَةٌ {وَالنَّجْمِ}. قَالَ فَسَجَدَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم وَسَجَدَ مَنْ خَلْفَهُ، إِلاَّ رَجُلاً رَأَيْتُهُ أَخَذَ كَفًّا مِنْ تُرَابٍ فَسَجَدَ عَلَيْهِ، فَرَأَيْتُهُ بَعْدَ ذَلِكَ قُتِلَ كَافِرًا، وَهْوَ أُمَيَّةُ بْنُ خَلَفٍ.
Amesimulia ‘Abdullaah (رضي الله عنه): Suwrah ya kwanza kuteremshwa ndani yake Sijdah, ni (Suwrah) An-Najm. Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alisujudu (alipoisoma), na wakasujudu waliokuwa nyuma yake, isipokuwa mtu mmoja ambaye nilimuona akichukua mchanga mkononi mwake na kusujudu juu yake. Baadaye nilimuona mtu huyo akiwa ameuliwa hali ya kuwa kafiri. Naye ni Umayyah bin Khalaf. [Al-Bukhaariy]
2-Watu wote walisujudu; Waislamu, washirikina na majini:
حَدَّثَنَا مُسَدَّدٌ، قَالَ حَدَّثَنَا عَبْدُ الْوَارِثِ، قَالَ حَدَّثَنَا أَيُّوبُ، عَنْ عِكْرِمَةَ، عَنِ ابْنِ عَبَّاسٍ ـ رضى الله عنهما أَنَّ النَّبِيَّ صلى الله عليه وسلم سَجَدَ بِالنَّجْمِ وَسَجَدَ مَعَهُ الْمُسْلِمُونَ وَالْمُشْرِكُونَ وَالْجِنُّ وَالإِنْسُ. وَرَوَاهُ ابْنُ طَهْمَانَ عَنْ أَيُّوبَ.
Amesimulia Ibn ‘Abbaas (رضي الله عنهما): Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alisujudu alipoisoma Suwrah An-Najm (53) wakasujudu pamoja naye Waislamu, washirikina, majini na watu wote. [Al-Bukhaariy]
054-Al-Qamar: Utangulizi Wa Suwrah
Alhidaaya.com [2]
Imeteremka: Makkah kwa itifaki ya ‘Ulamaa.
Idadi Za Aayah: 55
Jina La Suwrah: Al-Qamar
Suwrah imeitwa Al-Qamar (Mwezi), na yanayodalilisha, ni kutajwa kwake katika Hadiyth zilizonukuliwa chini katika Fadhila na Faida. Na pia kwa kutajwa mwanzo kabisa Suwrah, Aayah namba (1).
Miongoni Mwa Makusudio Ya Suwrah:
1-Ukumbusho wa neema ya Qur-aan kuwa ni nyepesi, na yaliyomo (kwenye Qur-aan) ambayo ni Aayaat (Ishara, Dalili, Miujiza, Hoja) na maonyo. [Al-Mukhtaswar Fiy Tafsiyr Al-Qur-aan Al-Kariym]
2-Mazungumzo kuhusu Desturi ya Allaah (سبحانه وتعالى) kwa Viumbe Vyake, ambao katika madhwhari yake ya wazi kabisa, ni kuwapa ushindi Waumini, na kuwafedhehesha na kuwaangamiza makafiri.
Miongoni Mwa Maudhui Ya Suwrah:
1-Suwrah imefunguliwa kwa tanabahisho na uhakikisho wa kukaribia Qiyaamah, na ishara yake ni kupasuka kwa mwezi.
2-Imetajwa upingaji wa washirikina kuhusu Aayaat (Ishara, Miujiza, Dalili) za Allaah zinapowajia, kwa kukengeuka na kupuuza na kuipachika sifa ovu Qur-aan kama vile kusema ni sihri (uchawi) ambayo wamezoea kuisikia.
3-Amri na liwazo kwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) kuwapuuza washirikina mpaka iwajie hukumu ya Allaah (سبحانه وتعالى) ya Siku ya Qiyaamah, na matukio yake watakapotoka makaburini mwao, wajute na waione siku hiyo ni ngumu mno!
4-Imetajwa visa vya Rusuli akianziwa Nabiy Nuwh (عليه السّلام) na kaumu yake waliomkadhibisha na kumpachika sifa ovu kumwita majnuni. Kisha Allaah (سبحانه وتعالى) Akateremsha Muujiza Wake wa kufungua mbingu na ardhi, yakamiminika maji wakagharakishwa makafiri wote. Na Akamwamrisha Rasuli Wake aunde jahazi apande yeye na walioamini, wakaokolewa na gharka.
5-Kisha kila mwisho wa kisa cha Rasuli, Allaah (سبحانه وتعالى) Amekumbusha maonyo Yake, na Ameahidi kuiwepesisha Qur-aan kwa mwenye kutaka kuisoma na kuihifadhi na kuifahamu.
6-Kisha wametajwa kina ‘Aad, kaumu ya Nabiy Huwd (عليه السّلام) na kukadhibisha kwao Risala ya Allaah, na ikatajwa maangamizi yao ya upepo mkali wa dhoruba, na sauti kali iliyoendelea mfululizo hadi wakafilia mbali!
7-Kisha wametajwa kina Thamuwd, kaumu ya Nabiy Swaalih (عليه السّلام), na kukadhibisha kwao Risala ya Allaah, kumpachika sifa ovu Rasuli wao kuwa ni muongo mkubwa, mfidhuli na mwenye kutakabari! Juu ya hayo, walipoletewa muujiza wa ngamia jike, ambaye walitaka wenyewe wateremshiwe iwe ni Ishara ya Allaah, waliamrishwa wasimguse kwa uovu, na wafanye zamu kunywa maji ya hodhi; siku moja wao, siku moja ngamia, lakini walikataa hayo na wakamchinja ngamia wa Allaah! Basi Allaah (سبحانه وتعالى) Akawaangamiza kwa ukelele angamizi. (na tetemeko la ardhi kama ilivyotajwa katika Suwrah nyenginezo. Rejea Al-‘Ankabuwt (29:40) kwenye uchambuzi kuhusu nyumati za awali na aina za maangamizi yao.
8-Kisha wametajwa kaumu ya Nabiy Luutw (عليه السّلام) waliokadhibisha Risala ya Allaah, na kutenda machafu. Ikatajwa maangamizi yao ya kupelekewa tufani ya mawe siku moja asubuhi mapema.
9-Kisha ametajwa Firawni na watu wake, na kukadhibisha kwao Risala ya Allaah, na maangamizi yao (ya kugharakishwa baharini).
10-Imewakemea na kuwaonya washirikina kwa kutozingatia haya maonyo, na kuahidiwa adhabu dhalilifu ya kuburutwa motoni kifudifudi.
11-Imebainishwa Uwezo wa Allaah (سبحانه وتعالى) na Hikma Yake iliyokamilika, na kwamba kila kitu ni kwa Hukmu na Qadr Yake.
12-Imebainisha Qudra Adhimu ya Allaah (سبحانه وتعالى) na Uwezo Wake wa kusimamisha Qiyaamah kwa muda wa upepeso wa jicho tu!
13-Imewakumbusha washirikina maangamizi ya nyumati za nyuma, na kwamba kila jambo linarekodiwa katika Kitabu cha matendo; kubwa na dogo.
14-Suwrah imekhitimishwa kwa kuwabashiria Waumini wenye taqwa, kuwa wataingizwa katika Jannaat za mito, ambako Yuko Mfalme Adhimu, Mwenye Nguvu na Uwezo mkubwa kabisa; Allaah (عزّ وجلّ).
Fadhila Za Suwrah:
Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alikuwa akiisoma katika Swalaah za ‘Iyd:
عَنْ أَبِي وَاقِدٍ اللَّيْثِيِّ قَالَ: { كَانَ اَلنَّبِيُّ - صلى الله عليه وسلم -يَقْرَأُ فِي اَلْأَضْحَى وَالْفِطْرِ بِـ (ق), وَ (اقْتَرَبَتْ). أَخْرَجَهُ مُسْلِمٌ
Amesimulia Waaqid Al-Laythiyy (رضي الله عنه): Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alikuwa akisoma katika (‘Iyd) Alfitwri na Al-Adhwhaa ق (Suwrah 50) na اقْتَرَبَتْ (Suwrah 54). [Muslim]
Faida:
عَنْ أَنَسٍ، قَالَ سَأَلَ أَهْلُ مَكَّةَ النَّبِيَّ صلى الله عليه وسلم آيَةً فَانْشَقَّ الْقَمَرُ بِمَكَّةَ مَرَّتَيْنِ فَنَزَلَت: ((اقتَرَبَتِ السَّاعَةُ وَانْشَقَّ الْقَمَرُ)) إِلَى قَوْلِهِ : ((سحْرٌ مُسْتَمِرٌّ)) يَقُولُ ذَاهِبٌ . قَالَ أَبُو عِيسَى هَذَا حَدِيثٌ حَسَنٌ صَحِيحٌ .
Amesimulia Anas (رضي الله عنه): Watu wa Makkah walimuomba Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) awaletee Aayah (Ishara, Muujiza), basi mwezi ukapasuka Makkah mara mbili (yaani sehemu mbili), kisha ikateremka:
اقْتَرَبَتِ السَّاعَةُ وَانشَقَّ الْقَمَرُ ﴿١﴾
“Saa imekaribia na mwezi umepasuka.”
Mpaka Kauli Yake:
سِحْرٌ مُّسْتَمِرٌّ ﴿٢﴾
“Sihiri ya siku zote, tumeizoea.”
[Atw-Twabaraniy na Al-Haafidhw Ibn Kathiyr amesema katika Al-Bidaayah Wan-Nihaayah: Isnaad yake ni Jayyid]
055-Ar-Rahmaan: Utangulizi Wa Suwrah
Alhidaaya.com [2]
Imeteremka: Makkah
Idadi Za Aayah: 78
Jina La Suwrah: Ar-Rahmaan
Suwrah imeitwa Ar-Rahmaan (Jina la Allaah), na yanayodalilisha, ni kutajwa mwanzo kabisa Suwrah, Aayah namba (1).
Miongoni Mwa Makusudio Ya Suwrah:
1-Kuwakumbusha majini na waanadam Neema za Allaah (سبحانه وتعالى) zilizojificha na zilizodhahiri, na athari za Rehma Zake (Allaah) duniani na Aakhirah. [Al-Mukhtaswar Fiy Tafsiyr Al-Qur-aan Al-Kariym]
2-Kukumbusha Uadhimu wa Allaah (عزّ وجلّ) na kubainisha wazi Neema Zake kwa Viumbe Vyake duniani na Aakhirah na kuwapinga wenye kukosa shukurani nazo.
Miongoni Mwa Maudhui Ya Suwrah:
1-Suwrah imefunguliwa kwa kumtukuza Allaah (سبحانه وتعالى) na ihsaan Yake kwa viumbe kwa kuwaelimisha Qur-aan, Uwezo Wake wa kuwaumba na kuwafunza ufasaha.
2-Imebainisha Uwezo wa Allaah (سبحانه وتعالى) na baadhi ya Neema Zake kwa Viumbe Vyake.
3-Suwrah imekariri baada ya kila Aayah au Aayah chache Kauli Yake Allaah (سبحانه وتعالى) inayowahusu majini na wanaadam:
فَبِأَيِّ آلَاءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ ﴿١٣﴾
“Basi ni zipi katika Neema za Rabb wenu mnazikadhibisha.”
Hivyo basi imekariri mara 31 katika Suwrah hii tukufu.
4-Imekumbusha kutoweka kwa kila kilichopo juu ya mgongo wa ardhi, na kwamba Atakayebakia ni Allaah (سبحانه وتعالى) Pekee. Na kwamba Anayepaswa kuombwa ni Yeye Pekee.
5-Imebainishwa udhalili na udhaifu wa majini na wanaadam kwamba hawataweza kupenya katika zoni za mbingu na ardhi. Na pindi wakijaribu kutaka kupenya, wataangamizwa kwa mwako wa moto!
6-Imetaja baadhi ya matukio na vitisho vya Siku ya Qiyaamah na mwisho mbaya wa makafiri, kuingizwa katika moto wa Jahannam.
7-Imetajwa aina mbili za mabustani ya Jannah na kila moja zimebainishwa raha na neema zake mbalimbali: (i) bustani mbili ambazo matawi yake yametanda (ii) bustani mbili nyenginezo ambazo rangi yake ni kijani iliyokoza.
8-Suwrah imekhitimishwa kwa kumtukuza Allaah (سبحانه وتعالى) Mwenye Ujalali na Ukarimu na Jina Lake Ambalo Limebarikika.
056-Al-Waaqi’ah: Utangulizi Wa Suwrah
Alhidaaya.com [2]
Imeteremka: Makkah kwa itifaki ya ‘Ulamaa,
Idadi Za Aayah: 96
Jina La Suwrah: Al-Waaqi’ah
Suwrah imeitwa Al-Waaqi’ah (Tukio) la Qiyaamah, na inayodalilisha ni kutajwa kwake mwanzo kabisa, Aayah namba (1).
Miongoni Mwa Makusudio Ya Suwrah:
1-Kubainisha hali za waja Siku ya Ufufuo. [Al-Mukhtaswar Fiy Tafsiyr Al-Qur-aan Al-Kariym]
2-Kukiri kufufuliwa na kulipwa, na kukumbusha Siku ya Qiyaamah, na kubainisha vigawanyo vya watu ndani yake.
Miongoni Mwa Maudhui Ya Suwrah:
1-Suwrah imefunguliwa kwa kukumbusha Tukio la Siku ya Qiyaamah, ambayo haiepukiki. Na ikatajwa yatakayotokea ya vitisho vya ardhi kutikisika, milima kupondwapondwa hadi iwe chembechembe za vumbi.
2-Kisha ikabainishwa aina tatu za watu: (i) Wa kuliani (ii) Kushotoni (iii) Waliotangulia (katika khayraat ambao ni katika ummah huu na wengineo).
3-Kisha zikatajwa neema kadhaa za Jannah za hawa waliotangulia, nao ni: Kuwa juu ya makochi ya kifakhari, kukabIliana na wenzao kwa furaha, kuhudumiwa kwa vyombo vya mvinyo na chemchemu, kupata matunda wayapendayo na nyama za ndege watakazozitamani, na kujaaliwa hurulaini (wanawake weupe wazuri kwa umbo na macho). Pia humo hawatasikia ya upuuzi ila maamkizi ya Salaam tu!
4-Kisha wakatajwa watu wa kuliani na neema zao kadhaaa za Jannah, nazo ni: Kuwekwa kwenye mikunazi isiyo na miba, na migomba ya ndizi iliyopangwa matabaka, kuwekwa katika vivuli vilotandazwa, kupewa maji ya kumiminwa, kuruzukiwa matunda mbalimbali, kuwekwa katika matandiko mazuri, kuozeshwa hurulaini.
5-Kisha wakatajwa watu wa kushotoni na jazaa zao za kuingizwa katika moto unaobabu vikali na maji yachemkayo. Na ikatajwa baadhi ya sababu ya adhabu zao, kuwa wameshughulika na anasa za dunia na kutenda maasi, na kutokuamini kufufuliwa. Zikatajwa hoja za nguvu kubainishiwa kwamba, bila shaka watakusanywa wa mwanzo wao na mwisho wao, na kikatajwa chakula chao cha mti wa zaqquwm, na kinywaji chao cha maji yachemkayo.
6-Kisha Allaah (سبحانه وتعالى) Akabainisha Uwezo Wake wa Kuumba wanaadam na kuumba vitu vinginevyo huku Akiwauliza makafiri kama wao ndio walivyoviumba hivyo.
7-Kisha Allaah (سبحانه وتعالى) Akaapia kwa jambo muhimu, nalo ni maanguko ya nyota, na jibu la kuapia ni kuthibitisha kwamba Qur-aan ni Tukufu mno na kwamba Imeteremshwa na Allaah (سبحانه وتعالى), na kwamba ni Neema ambayo Allaah Amewaneemesha watu lakini hawakushukuru, na wakakadhibisha yaliyo ndani yake.
8-Imetajwa aina tatu za watu wanapotolewa roho. (i) Waliokurubishwa ambao hubashiriwa raha, manukato na Jannaat za neema. (ii) Watu wa kuliani ambao hubashiriwa kwa maamkizi ya Salaam (iii) Waliokadhibisha ambao wanapokelewa kwa maji ya moto yachemkayo na kuingizwa motoni.
9-Suwrah imekhitimishwa kwa kuthibitishwa kwamba Qur-aan ni haki na yenye yaqini, kisha Allaah (سبحانه وتعالى) Anaamuamrisha Rasuli Wake (صلى الله عليه وآله وسلم) Kumsabbih Allaah Mwenye U’adhwama.
057-Al-Hadiyd: Utangulizi Wa Suwrah
Alhidaaya.com [2]
Imeteremka: Makkah kwa itifaki ya baadhi ya ‘Ulamaa
Idadi Za Aayah: 29
Jina La Suwrah: Al-Hadiyd
Suwrah imeitwa Al-Hadiyd (Chuma), na inayodalilisha ni kutajwa kwake katika Aayah namba (25).
Miongoni Mwa Makusudio Ya Suwrah:
1-Kukuza imaan kwenye nafsi, na kutoa katika Njia ya Allaah. [Al-Mukhtaswar Fiy Tafsiyr Al-Qur-aan Al-Kariym]
2-Ishara zinazodalilisha Qudra na Uwezo wa Allaah (سبحانه وتعالى) na Sifa Zake Jalili (Tukufu).
2-Wito kwa Waumini kushikamana na mafundisho ya Dini yao.
Miongoni Mwa Maudhui Ya Suwrah:
1-Suwrah imefunguliwa kwa kumtukuza Allaah (سبحانه وتعالى) kwamba, vyote vilivyopo mbinguni na aridhini vinamsabbih Yeye, Mwenye Enzi ya Nguvu Asiyeshindika, Mwenye Hikmah wa yote.
2-Zimetajwa Sifa Zake Allaah (سبحانه وتعالى) nyenginezo Kamilifu, na Uwezo wa kila kitu katika Ufalme Wake na kuenea Ilimu Yake.
3-Waumini wamehimizwa kuthibitika katika imaan na kutoa mali zao katika Njia ya Allaah, na Ahadi ya Allaah (سبحانه وتعالى) Kuwalipa maradufu ya wanayotoa.
4-Imebainishwa mwisho mwema wa Waumini wa kiume na wa kike Siku ya Qiyaamah, na Nuru itakayowaongoza katika Asw-Swiraatw (Njia) inayoelekea Jannah. Kisha ikabainishwa mwisho mbaya wa wanafiki na mazungumzo baina yao na Waumini; wakiwaomba Waumini wafuatane nao katika Asw-Swiraat ili wapate Nuru yao, lakini hilo hawatakubaliwa, kwa sababu wao walipokuwa duniani, walifuata matamanio na wakafitini nafsi zao. Na unafiki wao ulidhihirika wa kutilia shaka Risala ya Allaah, na kuwatamania Waislamu iwasibu misiba. Na Ibliys akawaghururi kumuasi Allaah.
5-Waumini wanahimizwa kumnyenyekea Allaah (سبحانه وتعالى) na kumkhofu, na wamdhukuru Allaah (سبحانه وتعالى), na kuwatahadharisha wasijekuwa kama waliopewa Kitabu ambao zama ziliwarefukia, na nyoyo zao zikawa ngumu wakatoka katika utiifu wa Allaah.
6-Wamebashiriwa Waumini wanaotoa swadaqa zao kuwa, hizo swadaqa ni mkopo mzuri wanaomkopesha Allaah, Naye Anawaahidi kuwalipa maradufu na ujira mtukufu. Na pia wamebashiriwa malipo mema wale waliosadikisha Risala ya Allaah, na kumwamini Rasuli wao (صلى الله عليه وآله وسلم). Ama makafiri waliokadhibisha Risala ya Allaah, wao watakuwa watu wa motoni.
7-Kisha Allaah (سبحانه وتعالى) Amepiga mfano wa uhai wa dunia na anasa zake kuwa ni kama mfano wa mvua inayohuisha mimea iliyokufa, kisha baada ya kusitawi inakufilia mbali. Hivyo basi ni zingatio kwa watu kwamba, uhai wa dunia si chochote isipokuwa ni starehe fupi za udanganyifu. Ikatajwa ukumbusho kwamba Aakhirah kuna adhabu kali kwa makafiri. Ama Waumini, wao watapata maghfirah na radhi za Allaah. Kisha Waumini wakaamrishwa kukimbilia kuomba maghfirah na wakatambulishwa upana wa Jannah ambayo Allaah (سبحانه وتعالى) Amewaandalia huko Aakhirah.
8-Kuthibitisha kwamba misiba inayowasibu wanaadam ni kutokana na Qadhwaa na Qadar ya Allaah (Yaliyohukumiwa na Yaliyokadiriwa).
9-Imebainishwa kwamba Risala ya Allaah ni moja tu, nayo ni kulingania Tawhiyd ya Allaah. Ikatajwa hikma ya kutumwa Rusuli wa Allaah (عليهم السّلام) pamoja na Vitabu.
10-Imeelezewa hali za Manaswara waliofuata Injiyl, kwamba walikuwa wenye nyoyo laini na huruma, na kwamba walizusha maisha ya utawa waliojilazimisha nayo ili kutafuta Radhi za Allaah. Lakini wengi wao hawakufuata ipasavyo, basi walioko walioamini na wengineo walitoka nje ya utiiifu wa Allaah, wakamkanusha Nabiy Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم).
11-Suwrah imekhitimishwa kwa kuamrishwa Waumini wamche Allaah kwa kufuata Amri Zake, na kujiepusha na makatazo Yake, na kumwamini Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم), na wakabashiriwa Rehma ya Allaah na Nuru itakayowaongoza, na kwamba wataghufuriwa madhambi yao. Na kwamba hayo yote, Allaah (سبحانه وتعالى) Amewajaalia ili watu wa Kitabu ambao hawakumuamini Nabiy Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم), watambue kwamba, hawawezi kupata chochote katika Fadhila za Allaah, na kwamba Allaah Ni Mwenye Fadhila adhimu na hiba tele kwa Viumbe Vyake.
058-Al-Mujaadalah: Utangulizi Wa Suwrah
Alhidaaya.com [2]
Imeteremka: Madiynah kwa itifaki ya ‘Ulamaa wengi.
Idadi Za Aayah: 22
Jina La Suwrah: Al-Mujaadalah
Suwrah imeitwa Al-Mujaadalah (Mjadala), na inayodalilisha ni kutajwa kwake katika Aayah namba (1); mwanamke aliyejadiliana na Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) kuhusu mumewe.
Miongoni Mwa Makusudio Ya Suwrah:
1-Kudhihirisha Ujuzi jumuishi wa Allaah uliokizunguka kila kitu kwa mapana yake na marefu yake, ili kuwalea watu wawe wanamchunga Allaah wakati wote, na kuwahadharisha wasije kwenda kinyume na Maamrisho Yake. [Al-Mukhtaswar Fiy Tafsiyr Al-Qur-aan Al-Kariym]
2-Kubainisha hukumu ya dhwihaar (aina ya talaka ambapo mume anamwambia mkewe: “Wewe kwangu ni kama mgongo wa mama yangu” na hivyo kumfanya kuwa ni haraam kwake kujamiana naye), na kubatilisha yale yaliyokua katika zama za jaahiliyyah (zama za ujinga kabla ya Uislamu).
3-Kuweka wazi siri za wanafiki, na kubainisha upotevu wao, na kauli zao za baatwil, na vitendo vyao viovu.
4-Kutaja baadhi ya adabu ambazo Waumini wanapaswa kujipamba nazo.
Miongoni Mwa Maudhui Ya Suwrah:
1-Suwrah imefunguliwa kuhusu mashitaka ya mwanamke aliyejadiliana na Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) kuhusu mumewe aliyemtamkia dhwihaar, na kwamba Allaah Amewaona na Amesikia majibizano yao.
2-Imetolewa hukmu ya dhwihaar na kafara yake.
3-Imetajwa kufedheheshwa na mwisho mbaya wa waliopinzana na kumpinga Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم).
4-Kuthibitisha upana wa Ilimu ya Allaah (سبحانه وتعالى) na kwamba hakuna kinachofichika Kwake; ya dhahiri au ya siri.
5-Imedhihirishwa minong’ono waliyokuwa wakinong’ona maadui wa Uislamu na kumsalimia kwao Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) kwa maneno yaliyomaanisha kumtakia maangamizi, na adhabu yao ya kuingizwa moto wa Jahannam.
6-Waumini wameamrishwa kutokunong’ona mambo ya dhambi na kumuasi Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) na wamche Allaah.
7-Waumini wanaongozwa baadhi ya adabu za vikao, na zimetajwa baadhi ya fadhila za ilimu.
8-Waumini waliwekewa sharia ya kutoa swadaqa walipotaka kunong’onezana katika kushauriana na Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم). Lakini hukmu ya Aayah hiyo namba (12) ilifutwa, wakabadilishiwa kwa Aayah inayofuatia. Rejea Alhidaaya.com kwenye Makala ya An-Naasikh Wal-Mansuwkh (Kinachofuta Na Kinachofutwa)
9-Zimetajwa baadhi ya sifa za wanafiki, na kuwafanya kwao vipenzi Mayahudi, na kuapa kwao juu ya uongo, na kusahau kwao kumdhukuru Allaah, na kubainisha mwisho wao mbaya.
10-Suwrah imekhitimishwa kwa kuwasifu Waumini kwa al-walaa (kupendana kwa ajili ya Allaah) na kuwafanya rafiki wa ndani na vipenzi wanaompenda Allaah na Rasuli Wake (صلى الله عليه وآله وسلم), na al-baraa (kuwachukia na kujitenga) na wanaompinga Allaah na Rasuli Wake (صلى الله عليه وآله وسلم) japokuwa ni watu wenye uhusiano wa damu nao. Na wakabashiriwa kwa Radhi za Allaah na kuingiziwa Jannah wadumu milele.
059-Al-Hashr: Utangulizi Wa Suwrah
Alhidaaya.com [2]
Imeteremka: Madiynah kwa itifaki ya ‘Ulamaa wengi.
Idadi Za Aayah: 24
Jina La Suwrah: Al-Hashr
Suwrah imeitwa Al-Hashr (Mkusanyiko), na inayodalilisha ni kutajwa kwake katika Aayah namba (2). Na pia imeitwa Suwrah Bani An-Nadhwiyr kwa kutajwa katika Hadiyth ifuatayo:
عَنْ سَعِيدٍ، قَالَ قُلْتُ لاِبْنِ عَبَّاسٍ ـ رضى الله عنهما ـ سُورَةُ الْحَشْرِ قَالَ قُلْ سُورَةُ النَّضِيرِ.
Amesimulia Sa’iyd Bin Jubayr: Nilimuuliza Ibn ‘Abbaas kuhusu Suwrah Al-Hashr, Akajibu: Sema Suwrah (Bani) An-Nadhwiyr. [Al-Bukhaariy]
Miongoni Mwa Makusudio Ya Suwrah:
1-Kudhihirisha Nguvu na Utukufu wa Allaah katika kuwadhoofisha Mayahudi na wanafiki, na kudhihirisha utengano wao unaokuja baada ya kudhihiri mshikamano kwa Waumini. [Al-Mukhtaswar Fiy Tafsiyr Al-Qur-aan Al-Kariym]
2-Mazungumzo kuhusu vita ya Bani Nadhwiyr, na Nusra ya Allaah kwa Waja Wake Waumini na kuwafedhehesha madhalimu.
3-Kutaja baadhi ya Majina Mazuri kabisa ya Allaah na Sifa Zake Tukufu.
Miongoni Mwa Maudhui Ya Suwrah:
1-Suwrah imefunguliwa kwa kutajwa kuwa viliomo mbinguni na ardhini vyote Vinamsabbih (Vinamtakasa) Allaah (سبحانه وتعالى) kutokana na yale yasiyoendana Naye, na kumalizia kwa Sifa Zake Tukufu.
2-Imeelezwa kuhusu vita ya Bani Nadhwiyr, na jinsi Allaah (سبحانه وتعالى) Alivyowepesisha kuwaondosha Madiynah kwa namna wasiyoitegemea, na akawatia khofu kubwa.
3-Imetajwa hukmu ya al-fay-u (ngawira inayopatikana bila kupigana vita) na Mwongozo wa Allaah (سبحانه وتعالى) kwa Rasuli Wake (صلى الله عليه وآله وسلم) katika mgawanyo huo.
4-Wamesifiwa Answaariy (wa Madiynah) walionusuru Dini ya Allaah, kwa kuwapokea vizuri kabisa Muhaajiruna (wa Makkah) na kuwakirimu kwa wingi hadi kwamba walijinyima wenyewe walivyovitoa kwao.
5-Wamesifiwa waliokuja baada yao, na duaa yao kwa ndugu zao waliotangulia ya kuondoshewa mafundo na chuki nyoyoni mwao.
6-Imebainishwa undani wa wanafiki wa kuungana na Mayahudi dhidi ya Waislamu, na kutaja baadhi ya kauli zao za uongo, na ahadi zao za hadaa.
7-Imefichuliwa sifa ya wanafiki ya uongo kuwaahidi Bani Nadhiwyr kuwa watawaunga mkono kuwa pamoja nao watakapotolewa Madiynah, lakini wakawatenga kutokana na kuwaogopa kwao Waumini, na kwamba wao wenyewe kwa wenyewe wana uadui nyoyoni mwao. Na umepigwa mfano wao ni kama mfano wa shaytwaan anapomshawishi mwanaadam akufuru kisha anamkanusha na kujitenga naye!
8-Waumini wameamrishwa kumcha Allaah, kujitayarisha na Aakhirah, na kuwakataza kujifananisha na wanaopinga Amri za Allaah, na kukumbusha utofauti wa hali za makundi mawili; ya motoni na watakaoingizwa Jannah
9-Watu wamepigiwa mfano wa kubainisha Utukufu wa Qur-aan, na kuwataka watu watafakari, kwamba Qur-aan ingeteremshwa juu ya mlima, ungepasukapasuka kwa khofu na kunyenyekea kwa Allaah kutokana na taathira yake. Basi wanaadam wanapaswa wazingatie Qur-aan na wafanyie kazi maamrisho yake na wajiepushe makatazo yake.
10-Suwrah imekhitimishwa kwa kutajwa baadhi ya Majina Mazuri kabisa ya Allaah na Sifa Zake na kwamba vyote viliomo mbinguni na ardhini Vinamsabbih Allaah.
060-Al-Mumtahinah: Utangulizi Wa Suwrah
Alhidaaya.com [2]
Imeteremka: Madiynah kwa itifaki ya ‘Ulamaa wengi.
Idadi Za Aayah: 13
Jina La Suwrah: Al-Mumtahinah
Suwrah imeitwa Al-Mumtahinah (Majaribio), na inayodalilisha ni kutajwa katika Aayah namba (10), pindi Waumini walipoamrishwa wawajaribu Waumini wa kike waliohajiri, imaan zao kama kweli wamemwamini Allaah na Rasuli Wake (صلى الله عليه وآله وسلم).
Miongoni Mwa Makusudio Ya Suwrah:
1-Kuwatahadharisha Waumini juu ya kuwafanya makafiri kuwa marafiki wa ndani na walinzi wao. [Al-Mukhtaswar Fiy Tafsiyr Al-Qur-aan Al-Kariym]
2-Amrisho la kusawazisha baina ya kutokuwafanya vipenzi maadui wa Allaah, na kufanya uadilifu kwa kuwatendea wema wale ambao hawakupigana vita na Waislamu.
Miongoni Mwa Maudhui Ya Suwrah:
1-Suwrah imefunguliwa kwa kuwakataza na kuwatahadharisha Waumini, kuwafanya vipenzi maadui wa Allaah na maadui wao, yaani: Maadui wa Waumini katika washirikina waliokuweko Makkah. Hii ni kwa sababu mmoja wa Swahaba alituma barua ya siri kwa mwanamke mmoja aliyekuwa baina ya Madiynah na Makkah, ili aipeleke barua hiyo kwa washirikina kuwajulisha khabari za Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم). Ikabainisha namna maadui wa Allaah wanavyoichukia haki, na mwisho mbaya wa wale wanaowafanya maadui kuwa vipenzi vyao. Na tahadharisho la kwamba Siku ya Qiyaamah, hata wenye uhusiano wa damu hawataweza kusaidiana.
2-Wito kwa Waumini, kufuata kigezo kizuri cha Nabiy Ibraahiym (عليه السّلام) kujiweka mbali na baba yake na watu wake, baada ya kumbainikia kuwa wao ni maadui wa Allaah kutokana na kumshirikisha na kukataa kupokea haki.
3-Kuweka wazi ruhusa ya kuwafanyia makafiri muamala mzuri wale ambao hawakuwapiga vita Waislamu na wala hawakuwatoa katika majumba yao.
4-Imepambanua hukumu za wanawake ambao wamehajiri hali ya kua ni Waumini, kutokuwarejesha kwa makafiri, na ruhusa ya kuwaoa baada ya kuwaacha waume zao makafiri.
5-Allaah Amemuamrisha Rasuli Wake (صلى الله عليه وآله وسلم) kuwafanyia bay’ah (fungamano la utiifu) wanawake Waumini, na kuchukua ahadi juu yao ya kumtii Allaah, na kujiweka mbali na yaliyoharamishwa.
6-Suwrah imekhitimishwa kwa kuwakataza Waumini kuwafanya maadui wa Allaah na maadui zao kuwa vipenzi.
061-Asw-Swaff: Utangulizi Wa Suwrah
Alhidaaya.com [2]
Imeteremka: Madiynah kwa itifaki ya ‘Ulamaa wengi.
Idadi Za Aayah: 11
Jina La Suwrah: Asw-Swaff
Suwrah imeitwa Asw-Swaff (Safu), na inayodalilisha ni kutajwa katika Aayah namba (4).
Miongoni Mwa Makusudio Ya Suwrah:
1-Mahimizo kwa Waumini juu ya kuinusuru Dini. [Al-Mukhtaswar Fiy Tafsiyr Al-Qur-aan Al-Kariym]
2-Mahimizo juu ya Jihaad katika Njia ya Allaah kwa mali na nafsi, na kumuitikia Allaah na Rasuli Wake (صلى الله عليه وآله وسلم).
Miongoni Mwa Maudhui Ya Suwrah:
1-Suwrah imefunguliwa kwa kubainishwa kwamba, kila kilichomo mbinguni na ardhini Kinamsabbih (Kumtakasa) Allaah (سبحانه وتعالى).
2-Waumini wametahadharishwa kutokuvunja ahadi kwa kusema maneno kisha wasitekeleze wayasemayo, na kwamba hivyo ni chukizo kubwa mbele ya Allaah.
3-Imetajwa aliyoyasema Nabiy Muwsaa (عليه السّلام) kuwalaumu watu wake kwa maudhi waliyomfanyia, na watu wake kujiingiza katika upotofu.
4-Imetajwa da’wah ya Nabiy ‘Iysaa (عليه السّلام) kwa wana wa Israaiyl, na kushuhudia yaliyotajwa katika Tawraat ya kuja kwa Rasuli aitwaye Ahmad ambaye ndiye Nabiy Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم). Lakini alipowajia kwa Ishara za wazi walikanusha Risala ya Allaah na kudai ni sihri ya wazi.
5-Imebainishwa kwamba, madhalimu wametaka kuikanusha Qur-aan aliyoteremshiwa Nabiy Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم), lakini Allaah Ameipa nguvu haki japokuwa makafiri wamechukia.
6-Waumini wameongozwa kutenda yatakayowaepusha na adhabu za Allaah, na kutenda yaliyo bora kwao, ambayo yatawapatia makazi mazuri ya Jannah yenye kudumu milele, nayo ni kumwamini Allaah na Rasuli Wake (صلى الله عليه وآله وسلم), na kufanya Jihaad katika Njia ya Allaah kwa mali na nafsi zao.
7-Suwrah imekhitimishwa kwa kuwahimiza Waumini kuwaiga wafuasi wa Nabiy Iysaa (عليه السّلام).
062-Al-Jumu’ah: Utangulizi Wa Suwrah
Alhidaaya.com [2]
Imeteremka: Madiynah kwa itifaki ya ‘Ulamaa.
Idadi Za Aayah: 11
Jina La Suwrah: Al-Jumu’ah
Suwrah imeitwa Al-Jumu’ah (Ijumaa), na yanayodalilisha ni kutajwa katika Hadiyth ifuatayo:
عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ، رضى الله عنه قَالَ كُنَّا جُلُوسًا عِنْدَ النَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم فَأُنْزِلَتْ عَلَيْهِ سُورَةُ الْجُمُعَةِ
Amesimulia Abuu Hurayrah (رضي الله عنه): Tulikuwa tumekaa pamoja na Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akateremshiwa Suwrah Al-Jumu’ah. [Al-Bukhaariy]
Na pia Hadiyth iliyonukuliwa katika Fadhila. Na pia kutajwa katika Aayah namba (9).
Miongoni Mwa Makusudio Ya Suwrah:
1-Neema na Fadhila walioyojaaliwa Ummah (wa Kiislamu kutumiwa) Rasuli wao (صلى الله عليه وآله وسلم) na kubainisha fadhila ya siku ya Ijumaa. [Al-Mukhtaswar Fiy Tafsiyr Al-Qur-aan Al-Kariym]
2-Kutaja vile ambavyo Allaah (سبحانه وتعالى) Ameuchagulia Ummah huu, na katika hivyo ni Swalaah ya Ijumaa, pamoja na kibainisha baadhi ya hukumu zake.
Miongoni Mwa Maudhui Ya Suwrah:
1-Suwrah imefunguliwa kwa kuthibitishwa kwamba kila kilichomo mbinguni na ardhini Kinamsabbih Allaah Mwenye Sifa Tukufu.
2-Imetajwa madhwhari ya Neema za Allaah kwa Ummah wa Kiislamu kwa Kuwatumia Rasuli ili awasomee Aayah Zake, awatakase na awaelimishe Qur-aan na Sunnah.
3-Mayahudi wamekemewa kwa kutokukifanyia kazi Kitabu chao (Tawraat), ambacho wameteremshiwa na Allaah (سبحانه وتعالى) kwa ajili ya kuwaongoza, na kubatilisha madai yao ya kwamba wao ni vipenzi vya Allaah.
4-Imetanabahishwa kwamba hakuna atakayeweza kuyakimbia mauti!
5-Suwrah imekhitimishwa kwa kuamrishwa Waumini kuhifadhi Swalaah ya Ijumaa, na kuikimbilia inaponadiwa, na amri ya kuacha yote yanayomshughulisha mtu wakati wa kuitekeleza. Kisha amri ya Kumdhukuru Allaah kwa wingi baada ya kumalizika Swalaah. Na tahadhari ya kuiacha, na kuwakemea watu walioiacha kwa kukimbilia biashara zao.
Fadhila Za Suwrah:
Ni Sunnah Kuisoma Katika Rakaa Ya Kwanza Ya Swalaah Ya Ijumaa:
عَنِ ابْنِ أَبِي رَافِعٍ، قَالَ اسْتَخْلَفَ مَرْوَانُ أَبَا هُرَيْرَةَ عَلَى الْمَدِينَةِ وَخَرَجَ إِلَى مَكَّةَ فَصَلَّى لَنَا أَبُو هُرَيْرَةَ الْجُمُعَةَ فَقَرَأَ بَعْدَ سُورَةِ الْجُمُعَةِ فِي الرَّكْعَةِ الآخِرَةِ إِذَا جَاءَكَ الْمُنَافِقُونَ - قَالَ - فَأَدْرَكْتُ أَبَا هُرَيْرَةَ حِينَ انْصَرَفَ فَقُلْتُ لَهُ إِنَّكَ قَرَأْتَ بِسُورَتَيْنِ كَانَ عَلِيُّ بْنُ أَبِي طَالِبٍ يَقْرَأُ بِهِمَا بِالْكُوفَةِ . فَقَالَ أَبُو هُرَيْرَةَ إِنِّي سَمِعْتُ رَسُولَ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم يَقْرَأُ بِهِمَا يَوْمَ الْجُمُعَةِ .
Amesimulia Ibn Abiy Raafi’i (رضي الله عنه): Marwaam alimteua Abuu Hurayrah (رضي الله عنه) kama naibu wake katika mji wa Madiynah, na yeye mwenyewe akaondoka kuelekea Makkah. Basi Abuu Hurayrah (رضي الله عنه) alituswalisha Swalaah ya Ijumaa akasoma baada ya Suwratul-Jumu’ah katika Rakaa ya pili:
إِذَا جَاءَكَ الْمُنَافِقُونَ
“Wanapokujia wanafiki.” [Al-Munaafiquwn (63:1)
Kisha nikamdiriki Abuu Hurayrah wakati alipoondoka nikamwambia: Umesoma Suwrah mbili ambazo ‘Aliy Bin Abiy Twaalib alikuwa akizisoma katika mji wa Kuwfah. Abu Hurayrah akasema: Nimemsikia Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akizisoma siku ya Ijumaa (katika Swalaah). [Muslim]
063-Al-Munaafiquwn: Utangulizi Wa Suwrah
Alhidaaya.com [2]
Imeteremka: Madiynah kwa itifaki ya ‘Ulamaa
Idadi Za Aayah: 11
Jina La Suwrah: Al-Munaafiquwn (Wanafiki)
Suwrah imeitwa Al-Munaafiquwn (Wanafiki), na inayodalilisha ni Hadiyth ifuatayo:
عن زَيدِ بنِ أَرْقَمَ رَضِيَ اللهُ عنه، قال ... فلمَّا أصبَحْنا قرأ رَسولُ اللهِ صلَّى اللهُ عليه وسلَّم سورةَ المُنافِقينَ
Amesimulia Zayd Bin Arqam (رضي الله عنه): “...... Tulipopambazukiwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akasoma Suwrah Al-Munaafiquwn.” [At-Tirmidhiy na ameisahihisha Al-Albaaniy katika Swahiyh At-Tirmidhiy (3313)]
Na katika Hadiyth iliyotajwa katika Fadhila. Na pia kutajwa katika Aayah namba (1).
Miongoni Mwa Makusudio Ya Suwrah:
1-Kuubainisha uhakika wa wanafiki na kutahadharisha (Ummah) juu yao. [Al-Mukhtaswar Fiy Tafsiyr Al-Qur-aan Al-Kariym]
2-Makatazo ya kughafilika na Kumdhukuru Allaah (سبحانه وتعالى) kwa kushughulishwa na mali na watoto, na amrisho la kutoa mali katika Njia ya Allaah.
Miongoni Mwa Maudhui Ya Suwrah:
1-Suwrah imefunguliwa kwa kuwaelezea wanafiki na kubainisha tabia zao mbaya, miongoni mwa uongo, na viapo vya uovu, uoga, na kuwazuia watu kutoa mali kuwasaidia Swahaba wa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) waliohajiri.
2-Waumini waliamrishwa kutokuwaombea maghfirah wanafiki kwani Allaah Hakupenda kuwaghufuria.
3-Waumini wameamrishwa kutokushughulishwa na mali na watoto kutokana na Kumdhukuru Allaah na tahadharisho la kula khasara.
4-Suwrah imekhitimishwa kwa kuhimizwa Waumini kutoa mali kwa ajili ya Allaah na tahadharisho kuwa nafsi itakuja kutamani kurudi duniani ili mtu atoe mali yake aliyoiacha, lakini muda wa kufariki mtu haurudishwi nyuma!
Fadhila Za Suwrah:
Ni Sunnah Kuisoma Katika Rakaa Ya Pili Kwenye Swalaah Ya Ijumaa:
عَنِ ابْنِ عَبَّاسٍ أَنَّ اَلنَّبِيَّ - صلى الله عليه وسلم -كَانَ يَقْرَأُ فِي صَلَاةِ الْجُمُعَةِ سُورَةَ الْجُمُعَةِ وَالْمُنَافِقِينَ رَوَاهُ مُسْلِم
Amesimulia Ibn ‘Abbaas (رضي الله عنهما): Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alikuwa akisoma katika Swalaah ya Ijumaa, Suwrah Al-Jumu’ah na Al-Munaafiquwn. [Muslim]
064-At-Taghaabun: Utangulizi Wa Suwrah
Alhidaaya.com [2]
Imeteremka: Makkah au Madiynah kwani ‘Ulamaa wamekhitilafiana kuhusu wapi imeteremshwa.
Idadi Za Aayah: 18
Jina La Suwrah: At-Taghaabun
Suwrah imeitwa At-Taghaabun (Kupata na Kukosa), na inayodalilisha ni kutajwa kwake katika Aayah namba (9).
Miongoni Mwa Makusudio Ya Suwrah:
1-Kutahadharisha mambo yanayosababisha watu kupata majuto na kunyimwa kheri Siku ya Qiyaamah. [Al-Mukhtaswar Fiy Tafsiyr Al-Qur-aan Al-Kariym]
2-Kubainisha uhalisia wa kupunjana na sababu zake pamoja na mwisho wake, kama inavyoongoza Suwrah hii katika njia ya kupata na kukosa au kufuzu na kufaulu.
3-Kutahadharishwa yanayomzuia mtu kutoa mali katika Njia ya Allaah.
Miongoni Mwa Maudhui Ya Suwrah:
1-Suwrah imefunguliwa kwa kuthibitishwa kwamba vyote vilivyomo mbinguni na ardhini vinamsabbih Allaah, na kwamba Yeye Pekee Mwenye Kustahiki kuhimidiwa na Mweza wa kila kitu.
2-Imebainishwa aina mbali mbali za Uwezo wa Allaah (سبحانه وتعالى) na upana wa Ilimu Yake, na imethibitisha Tawhiyd Yake ya Ar-Rubuwbiyyah (Uola; Uumbaji, Uongozaji, Utoaji Rizki, Uendeshaji na kadhaalika)
3-Imewaonya washirikina kwa kuwakumbusha yale yaliyowapata nyumati zilizopita kabla yao, pamoja na kubainisha ada zao za kuwakanusha Rusuli na kuwafanyia istihzai.
4-Imewaradd washirikina kwa madai yao ya kutokuamini kufufuliwa na Allaah Akawathibitishia kwa kiapo kuwa, bila shaka watafufuliwa na kwamba Siku hiyo Allaah Atawakusanya viumbe vyote na itakuwa ni Siku ya At-Taghaabun (kupata na kukosa, kufaulu na kukhasirika).
5-Imeainisha kati ya Waumini na mwisho wao mwema, na makafiri na mwisho wao mbaya.
6-Imebainishwa kwamba misiba yoyote ile inayowasibu watu ni kwa Qadar ya Allaah.
7-Waumini wamehimizwa kumtii Allaah na Rasuli Wake (صلى الله عليه وآله وسلم).
8-Imethibitishwa Tawhiyd Al-Uwuluwhiyyah (Kumwabudu Allaah Pekee).
9-Imeelezwa kwamba miongoni mwa wake na watoto ni maadui kwa mtu, na kwamba mali na watoto ni mitihani, hivyo basi wamehimizwa Waumini kumcha Allaah na kumtii, na kutoa mali katika Njia ya Allaah.
10-Suwrah imekhitimishwa kwa kukumbushwa Waumini, kwamba mali yoyote waitoayo ni mkopo mzuri kwa Allaah, na kwamba Atawazidishia malipo maradufu, na Atawaghufuria, na Yeye ni Mwenye Kupokea Shukurani zao, na zikatajwa Sifa Zake Allaah (سبحانه وتعالى) nyenginezo ikiwemo Sifa ya Mjuzi wa yaliyo ghaibu na yaliyo dhahiri.
065-Atw-Twalaaq: Utangulizi Wa Suwrah
Alhidaaya.com [2]
Imeteremka: Madiynah kwa itifaki ya ‘Ulamaa.
Idadi Za Aayah: 12
Jina La Suwrah: Atw-Twalaaq
Suwrah imeitwa Atw-Twalaaq (Talaka), na inayodalilisha ni kutajwa kwake katika Aayah namba (5).
Miongoni Mwa Makusudio Ya Suwrah:
1-Kubainisha hukmu za Talaka na kuiheshimu mipaka (sharia) yake. [Al-Mukhtaswar Fiy Tafsiyr Al-Qur-aan Al-Kariym]
2-Kubainisha hukumu zinazofungamana na talaka, na yanayoambatana juu yake; eda ya talaka, kunyonyesha, matumizi na makazi ya mtaliki na mwana.
Miongoni Mwa Maudhui Ya Suwrah:
1-Suwrah imefunguliwa kwa kuelezewa talaka ya kisharia katika kubainishwa muda unaopaswa kumtaliki mke, na amrisho la kutokuwatoa majumbani mwao, na kutokuvuka mipaka ya Sharia za Allaah.
2-Imetolewa amri ya kuwafanyia wema wataliki na kushuhudisha mashahidi katika talaka, na katika kurejea.
3-Allaah (سبحانه وتعالى) Ameahidi kuwafanyia wepesi Waumini mambo yao, na kuwaruzuku ikiwa watamcha Yeye, na watatawakali Kwake na Amewaahidi kuwafutia madhambi yao.
4-Imeendelea kubainisha baadhi ya hukmu za talaka za kuwahudumia wataliki mpaka kumaliza kunyonyesha.
5-Imetajwa mwisho mbaya wa nyumati za nyuma waliopinga Amri za Rabb wao kuwakanusha Rusuli Wake.
6-Waumini wamekumbushwa Fadhila ya Allaah ya kuwatumia Rasuli Wake (صلى الله عليه وآله وسلم), ambaye amewasomea Aayaat za Allaah zinazofafanua haki na kutenga ubatilifu, wakaongoka na wakatolewa kutoka kizani na kuingizwa katika nuru, na wakamuamini Allaah na Rasuli Wake (صلى الله عليه وآله وسلم). Kisha yakatajwa malipo mazuri ya kuingizwa Jannaat na kuruzukiwa humo neema.
7-Suwrah imekhitimishwa kwa kuthibitisha Tawhiyd ya Ar-Rubuwbiyyah (Uola; Uumbaji, Uendeshaji na kadhaalika) na kubainisha Uwezo wa Allaah (سبحانه وتعالى) na upana wa Ilimu Yake.
066-At-Tahriym: Utangulizi Wa Suwrah
Alhidaaya.com [2]
Imeteremka: Madiynah kwa itifaki ya ‘Ulamaa.
Idadi Za Aayah: 12
Jina La Suwrah: At-Tahriym
Suwrah imeitwa At-Tahriym (Haramisho), na inayodalilisha ni kutajwa kwake katika Aayah namba (1).
Miongoni Mwa Makusudio Ya Suwrah:
1-Kulingania juu ya kusimamisha na kuheshimu mipaka ya Allaah ndani ya majumba (yetu), kwa kutanguliza kumridhisha Allaah Pekee. [Al-Mukhtaswar Fiy Tafsiyr Al-Qur-aan Al-Kariym]
2-Kubainisha mafundisho na miongozo inayofungamana na familia.
Miongoni Mwa Maudhui Ya Suwrah:
1-Suwrah imefunguliwa kwa kumwongoza Nabiy Wake (صلى الله عليه وآله وسلم) aache kujiharamishia yale ambayo Allaah Amemhalalishia, kwa kuwa alipendelea kuwaridhia wake zake.
2-Imeelezea sehemu ya yaliyotokea kati ya Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) na wake zake wawili. Mmoja wao aliitoa siri ya Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akampasha mwenzake. Allaah (سبحانه وتعالى) Akamfichulia Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) maongezi hayo ya siri. Kisha Allaah (سبحانه وتعالى) Akawaonya wake hao wawili wa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم), kuwa pindi watakaposaidiana katika kufanya yanayomuudhi Rasuli Wake (صلى الله عليه وآله وسلم), basi Allaah Anamtosheleza kumhifadhi, pamoja na Jibriyl na Waumini wengineo. Kisha wakanasihiwa watubie kwa kosa lao hilo la kibinaadam, na kuwatishia kwamba wasipofanya hivyo, basi Allaah Atambadilishia Nabiy Wake (صلى الله عليه وآله وسلم), wake waliobora wenye sifa nzuri kadhaa.
3-Waumini wameamrishwa wajikinge na moto pamoja na ahli zao, na wamekumbushwa moto wa Jahannam, na walinzi wake ambao ni Malaika wakali na washupavu wasiokwenda kinyume na Amri za Allaah.
4-Waumini wameamrishwa kutubia tawbah ya nasuha (ya kweli) na kubainisha athari zake nzuri za kufutiwa madhambi na kuingizwa Jannah.
5-Wameamrishwa pia Waumini kuhusu Jihaad dhidi ya makafiri na wanafiki.
6-Suwrah imekhitimishwa kwa kupiga mifano miwili: (i) Mfano wa waliokufuru ambao wamefananishwa na mke wa Nabiy Nuwh na mke wa Nabiy Luutw, ambao walikuwa chini ya hifadhi ya ndoa ya waja wawili hawa. Wake hao wawili walimkufuru Allaah (سبحانه وتعالى) na wakawafanyia khiyana Rusuli hao. Basi uhusiano wao kama wake wa Rasuli wa Allaah, haukuwafaa kitu kwa sababu ya kufru zao, wakaingizwa motoni kuwa ni jazaa yao waliyostahiki. (ii) Mfano wa walioamini ambao wamefananishwa na (Aasiyah) mke wa Firawni, ambaye alikuwa kwenye hifadhi ya ndoa na kafiri huyo, lakini hakumtii katika kufru zake, na matokeo yake yakawa ni kuadhibiwa na mumewe Firawni. Basi pindi alipokuwa anaadhibiwa, aliomba duaa Allaah Amjengee nyumba Peponi, na Amuokoe na ukafiri wa Firawni na maasi yake, na Amuokoe na madhalimu. Wakafananishwa tena walioamini, kwa mfano wa Maryam Bint ‘Imraan ambaye ni mama yake Nabiy ‘Iysaa (عليه السّلام), aliyejihifadhi na akajilinda na uzinifu, basi Allaah (سبحانه وتعالى) Akamuamrisha Jibriyl (عليه السّلام) apulize kwenye mfuko wa nguo yake, na mpulizo huo ukafika katika uzao wake akabeba mimba ya ‘Iysaa (عليه السّلام). Akayaamini Maneno ya Rabb wake, akafuata Sharia Zake, na akawa miongoni mwa wenye kumtii Allaah (سبحانه وتعالى).
067-Al-Mulk: Utangulizi Wa Suwrah
Alhidaaya.com [2]
Imeteremka: Makkah kwa itifaki ya ‘Ulamaa.
Idadi Za Aayah: 30
Jina La Suwrah: Al-Mulk
Suwrah imeitwa Al-Mulk (Ufalme), na pia imeitwa Suwrah Tabaarak, na yanayodalilisha ni kutajwa kwake katika Hadiyth zilizonukuliwa chini katika Fadhila. Na pia kwa kutajwa kwake katika Aayah namba (1).
Miongoni Mwa Makusudio Ya Suwrah:
1-Kudhihirisha ukamilifu wa Ufalme wa Allaah (سبحانه وتعالى) na Nguvu Zake, jambo ambalo linapelekea kumkhofu na kuchukua tahadhari na Adhabu zake. [Al-Mukhtaswar Fiy Tafsiyr Al-Qur-aan Al-Kariym]
2-Kubainisha Uwezo Wake Mkubwa Allaah (سبحانه وتعالى) na ukamilifu wa Ufalme Wake unaojulisha Tawhiyd Yake.
3-Kubainisha adhabu Alizoziandaa Allaah (سبحانه وتعالى) kwa wale wanaojizuia kutafakari ulimwengu. Basi hawa ndio wapotofu. Ama waliomcha Rabb wao, basi wao jazaa yao ni maghfirah, na thawabu na takrima na kuokoka na adhabu Siku ya Qiyaamah.
Miongoni Mwa Maudhui Ya Suwrah:
1-Suwrah imefunguliwa kwa kubainishwa Utukufu wa Allaah (تبارك وتعالى) na Tawhiyd Yake ya Ar-Rubuwbiyyah (Uola: Uumbaji, Uhuishaji na Ufishaji, Uendeshaji ulimwengu na kadhaalika) na pia kubainishwa baadhi ya Sifa Zake Tukufu za Uwezo Wake juu ya kila kitu, Nguvu Zake na Wingi Wake wa Kughufuria.
2-Imebainishwa hikma ya kuumbwa mauti na uhai, kwamba ni kwa ajili ya kuwajaribu waja, watambulike wepi watakaotenda amali njema.
3-Ametakwa mwanaadam atazame uonekano wa Uwezo wa Allaah (سبحانه وتعالى) na Tawhiyd Yake ya Kuumba ulimwengu uliofikia upeo wa juu kabisa, Uumbaji usiokuwa na dosari yoyote ile.
4-Imebainishwa mwisho mbaya wa makafiri na adhabu kali walizoandaliwa za moto uwakao vikali mno na vitisho vyake, na hali itakavyokuwa huko motoni watakapokuwa wanahojiana na Walinzi wa moto. Na kukiri kwa makafiri hao ukanushaji wao duniani walipowajia Rusuli kuwaonya, na kukiri kwao madhambi yao na kudhihirisha majuto yao Siku hiyo.
5-Imebainishwa upana wa Ilimu ya Allaah (سبحانه وتعالى), kwamba hakifichiki Kwake kitu chochote, ni sawa iwe siri au dhahiri, na kwamba wanaotambua hayo wanamkhofu Rabb wao na watapata maghfirah na ujira mkubwa.
6-Imekumbushwa neema ya kuumbwa ardhi hii, na kuifanya ni yenye kuendana na maisha ya watu, na kuwaamrisha watu kuhangaika ndani yake, na kunufaika na vile vilivyomo ndani yake katika upande wa neema.
7-Imetahadharishwa mateso na Adhabu za Allaah na ukumbusho wa yaliyowapata makafiri wa nyumati zilizotangulia.
8-Wanaadam wametakiwa wazingatie na kutafakari tukio la ndege wanaokunjua mbawa zao angani, na katika hali za nafsi zao, na kwamba hakuna mwenye kunusuru isipokuwa Allaah, na kwamba Allaah (سبحانه وتعالى) Akiizuia Rizki Yake, basi hakuna mwengine wa kuwaruzuku.
9-Imepigwa mfano kwa watu wa imaan na watu wa kufru, na watu wa haki na watu wa baatwil.
10-Imetajwa ada mojawapo ya makafiri kuwahimiza Rusuli wao wateremshiwe adhabu, na kwamba Siku ya adhabu itakapofika wakaiona, watadhikika mno makafiri.
11-Imewakemea washirikina juu ya kukufuru kwao neema za Allaah, na kudharau kwao makemeo Yake, na kumuamrisha Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) awakumbushe Neema za Allaah juu yao, na kuziradd shubha zao (kauli zao zenye utata) na uongo wao kwa hoja zitakazozibatilisha Shubha zao.
12-Allaah (سبحانه وتعالى) Amemwongoza Nabiy Wake (صلى الله عليه وآله وسلم) pamoja na Waumini kutawakali Kwake Yeye Allaah Pekee.
13-Suwrah imekhitimishwa kwa kukumbushwa wanaadam Neema za Allaah na kwamba hakuna awezaye kuwapatia neema hizo pindi zikitoweka isipokuwa Allaah (سبحانه وتعالى).
Fadhila Za Suwrah:
1-Inazuia Adhabu Za Kaburi:
عن ابنِ مَسعودٍ رَضِيَ اللهُ عنه، قال: قال رَسولُ اللهِ صلَّى اللهُ عليه وسلَّم: ((سورةُ تَبَارَكَ هي المانِعةُ مِن عذابِ القَبْرِ))
Amesimulia Ibn Mas’uwd (رضي الله عنه): Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Suwrah ya Tabaarak inazuia adhabu za kaburi.” [Ameisahihisha Al-Albaaniy katika Swahiyh Al-Jaami’ (3643), Swahiyh Ibn Hibbaan (3/68)]
2-Inamuombea Maghfirah Anayedumisha Kuisoma:
عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: " إِنَّ سُورَةً فِي الْقُرْآنِ ثَلَاثُونَ آيَةً شَفَعَتْ لِرَجُلٍ حَتَّى غُفِرَ لَهُ وَهِيَ: ((تَبَارَكَ الَّذِي بِيَدِهِ الْمُلْكُ)) رَوَاهُ أَحْمَدُ وَالتِّرْمِذِيُّ وَأَبُو دَاوُدَ وَالنَّسَائِيُّ وَابْنُ مَاجَه
Amesimulia Abuu Hurayrah (رضي الله عنه): Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Hakika Suwrah katika Qur-aan yenye Aayah thelathini, zilimuombea mtu mpaka akaghufuriwa, nayo ni Suwrah:
تَبَارَكَ الَّذِي بِيَدِهِ الْمُلْكُ وَهُوَ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ﴿١﴾
“Amebarikika Ambaye Mkononi Mwake umo Ufalme.”
[Imaam Ahmad, At-Tirmidhiy amesema Hadiyth Hasan, na ameipokea pia Abuu Daawuwd, An-Nasaaiy, Ibn Maajah na ameisahihisha Al-Albaaniy katika Swahiyh At-Targhiyb (1474)]
068-Al-Qalam: Utangulizi Wa Suwrah
Alhidaaya.com [2]
Imeteremka: Makkah kwa itifaki ya ‘Ulamaa.
Idadi Za Aayah: 52
Jina La Suwrah: Al-Qalam
Suwrah imeitwa Al-Qalam (Kalamu), na inayodalilisha ni kutajwa kwake katika Aayah namba (1)
Miongoni Mwa Makusudio Ya Suwrah:
1-Ushuhuda wa Allaah kwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) juu ya tabia njema, na kumtetea na kumthibitisha. [Al-Mukhtaswar Fiy Tafsiyr Al-Qur-aan Al-Kariym]
2-Kubatilisha shutuma za washirikina kwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) na kubainisha upotevu wao.
3-Kuthibitisha utimamu wa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) duniani na Aakhirah, na kumthibitisha.
Miongoni Mwa Maudhui Ya Suwrah:
1-Suwrah imefunguliwa kwa herufi zinazojulikana kama Al-Huruwf Al-Muqatw-twa’ah ambazo, hakuna ajuaye maana zake isipokuwa Allaah. Rejea Al-Baqarah (2:1). Na ikafuatia kiapo cha Allaah (سبحانه وتعالى) kwa Al-Qalam (Kalamu) inayoandikwa na Malaika na watu, mambo wanayoyaandika ya kheri na manufaa.
2-Kisha ikafuatia jibu la kiapo nalo ni kumsifia Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) kwa sifa bora kabisa za khulqa na tabia zake, na kwamba atapata ujira usiokatika, na kumliwaza kwa Kuradd shubha za washirikina waliokuwa wakimpachika sifa ovu Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم).
3-Allaah (سبحانه وتعالى) Amemkataza Nabiy Wake (صلى الله عليه وآله وسلم) kutokuwatii waliokadhibisha, na kwamba wametamani lau angeliwalegezea na kulainisha baadhi ya misimamo yao, nao wawe laini kwake. Amemkataza pia kutokumtii mtu anayeapa kwa wingi. Kisha zikatajwa sifa kadhaa ovu za mtu huyo aliyejaaliwa utajiri akatakabari kuikubali haki.
4-Washirikina wa Makkah wametahiniwa kwa njaa na ukame kama walivyotahiniwa watu waliomiliki shamba. Ikaelezewa kisa chao walivyoapa kutilia niya kuwazuia maskini wasipate rizki ya mavuno ya shamba hilo. Wakapania kuliendea shamba asubuhi mapema bila ya kusema In Shaa Allaah, wapate kuvuna mazao ya shamba kabla ya kuingia maskini na mafuqaraa. Lakini Allaah (سبحانه وتعالى) Akaliangamiza shamba hilo kwa kulipelekea moto nyakati za usiku hali wao wakiwa wamelala. Walipoamka asubuhi na kuliendea, walidhania wamepotea, kisha wakatanabahi kuwa wameharamishwa nalo. Na mwishowe watu hao wa shamba wakabakia kujuta na wakajirudi kwa Rabb wao. Na hiyo ni adhabu ndogo ya dunia ambayo ni afadhali kuliko adhabu ya Aakhirah.
5-Waumini wanaomcha Allaah (سبحانه وتعالى) wamebashiriwa Jannaat za neema.
6-Imetofautishwa kati ya wanaomnyenyekea Allaah (سبحانه وتعالى) na wahalifu. Kisha Allaah (سبحانه وتعالى) Akawaradd hao wahalifu kwa kutoa hukmu ya dhulma kulinganisha baina yao na Waumini katika malipo, na kuwahoji walete dalili zao kama wana haki ya hayo wanayojihukumia.
7-Imetajwa baadhi ya matukio ya Siku ya Qiyaamah ambayo mambo yatakuwa magumu mno! Na ikatajwa Kufika kwa Allaah Awahukumu viumbe vyote, Afunue Muundi Wake usiofanana na kitu chochote, kisha hapo Waumini waliokuwa wakimsujudia Allaah (سبحانه وتعالى) duniani kwa khiari na kupenda kwao, wataweza kumsujudia Allaah Siku hiyo. Ama makafiri, wanafiki na wahalifu ambao walikanusha duniani kumsujudia Allaah ilhali walikuwa wazima, watataka kusujudu Siku hiyo, lakini hawataweza kusujudu kamwe! Uti wa mgongo wao utakuwa kama mfupa mmoja usioweza kupinda!
8-Allaah (سبحانه وتعالى) Amemliwaza Nabiy Wake (صلى الله عليه وآله وسلم) kwamba Amwachie Yeye mambo yote ya makafiri wanaokanusha Qur-aan, na kwamba Atawavuta pole pole kwenye adhabu kwa namna wasiyoijua, na hakuna atakayeweza kuikwepa.
9-Kisha Allaah (سبحانه وتعالى) Akamliwaza tena Rasuli Wake (صلى الله عليه وآله وسلم) kwa kumtaka avute subira, na kumkataza asije kuwa mwenye kukosa kuvuta subira, kama alivyokosa subira Nabiy Yuwnus (عليه السّلام) aliyemezwa na samaki alipoghadhibika na watu wake, akamuomba Allaah (سبحانه وتعالى) Awaharakizie adhabu kwa kukanusha Risala ya Allaah. Na lau kama si Neema ya Allaah kumwafikia kutubia, basi angelitupwa ufukoni kutoka tumboni mwa chewa, akitesekea na akiwa mwenye kulaumiwa kwa kuteleza kwake. Lakini Allaah (سبحانه وتعالى) Akamjaalia kuwa miongoni mwa Swalihina.
10-Suwrah imekhitimishwa kwa kutahadharishwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) na jicho baya la uhasidi wa washirikina wanapoisikia Qur-aan, na kwamba Allaah Amemhami na hayo. Na ikatajwa mojawapo wa ada zao za kumpachika sifa ovu Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) kama kumwita majnuni. Kisha Allaah (سبحانه وتعالى) Anamthibitishia Nabiy Wake (صلى الله عليه وآله وسلم) kwamba Qur-aan ni Ukumbusho na mawaidha kwa walimwengu wote miongoni mwa wanaadam na majini.
069-Al-Haaqqah: Utangulizi Wa Suwrah
Alhidaaya.com [2]
Imeteremka: Makkah kwa itifaki ya ‘Ulamaa.
Idadi Za Aayah: 52
Jina La Suwrah: Al-Haaqqah
Suwrah imeitwa Al-Haaqqah (Tukio la haki lisiloepukika), na inayodalilisha ni kutajwa kwake mwanzo wa Suwrah Aayah namba (1-3)
Miongoni Mwa Makusudio Ya Suwrah:
1-Kuthibitisha kutokea Qiyaamah na malipo ni kweli. [Al-Mukhtaswar Fiy Tafsiyr Al-Qur-aan Al-Kariym]
2-Maelezo kuhusu Siku ya Qiyaamah na hali za watu Siku hiyo.
2-Kusimamisha dalili juu ya ukweli wa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) uthibitisho wa Qur-aan kutoka kwa Allaah (سبحانه وتعالى).
Miongoni Mwa Maudhui Ya Suwrah:
1-Suwrah imefunguliwa kwa kuthibitisha tukio la Qiyaamah ambalo haliepukiki!
2-Wametajwa kina Thamuwd ambao ni kaumu ya Nabiy Swaalih (عليه السّلام), na kina ‘Aad ambao ni kaumu ya Nabiy Huwd (عليه السّلام) na kwamba wote hawa walikanusha Risala ya Allaah kupitia Rusuli wao hao na wakakanusha Qiyaamah, na zikatajwa baadhi ya adhabu zao za maangamizi. Kisha wakafuatilia kutajwa Firawni na walio kabla yake, na watu waliopinduliwa chini juu kuadhibiwa, ambao ni watu Nabiy Luutw (عليه السّلام), na wote waliwaasi Rusuli wao basi Allaah (سبحانه وتعالى) Akawaangamiza. Kisha ikatajwa kuokolewa kwa Nabiy Nuwh (عليه السّلام) kwa kupandishwa katika jahazi na kuangamizwa makafiri kwa gharka ili iwe mawaidha na mazingatio kwa watu wenye kusikia na kutia akilini. Rejea Al-‘Ankabuwt (29:40) kwenye maelezo kuhusu aina za kufru za nyumati za awali na aina zao za adhabu na maangamizi.
3-Imeelezwa matukio ya Siku ya Qiyaamah kuanziwa kupulizwa baragumu, na ardhi na milima kupondwapondwa, na mbingu kuraruka. Kisha kuteremka Malaika wanane wakiwa wamebeba ‘Arsh ya Allaah (عزّ وجلّ), na mkusanyiko wa watu ili kuhesabiwa matendo yao.
4-Imeelezewa watu watakaopokea Kitabu chao kuliani na furaha zao za kufaulu Siku hiyo tukufu, na jazaa zao za kuingizwa Jannah watakapodumu milele humo wakistareheshwa kwa kila aina za neema.
5-Kisha wakatajwa watakaopokea Kitabu chao kushotoni na majuto yao, na jinsi watakavyofungwa pingu na minyororo kuingizwa motoni na kimetajwa chakula chao humo cha usaha.
6-Allaah (سبحانه وتعالى) Ameapia kwa vinavyoonekana na visivyoonekana, na jibu la kiapo ni kuthibitisha ukweli wa Rasuli Wake (صلى الله عليه وآله وسلم) na aliyoyabalighisha kutoka katika Qur-aan Tukufu, na Allaah Kuziradd sifa ovu za kuisingizia Qur-aan kuwa ni mashairi au kauli za kahini na kuthibitishwa kuwa ni Uteremsho wa Rabb wa ulimwengu.
7-Imebainishwa kwamba Qur-aan ni Ukumbusho kwa Waumini na majuto kwa makafiri.
8-Suwrah imekhitimishwa kwa amri ya Kumsabbih (Kumtakasa) Allaah (عزّ وجلّ).
070-Al-Ma’aarij: Utangulizi Wa Suwrah
Alhidaaya.com [2]
Imeteremka: Makkah kwa itifaki ya ‘Ulamaa.
Idadi Za Aayah: 44
Jina La Suwrah: Al-Ma’aarij
Suwrah imeitwa Al-Ma’aarij (Njia Za Kupanda), na inayodalilisha ni kutajwa kwake katika Aayah namba (3), na rejea Tanbihi ya Aayah namba (3) ya Suwrah hii ya Al-Ma’aarij kupata maana nyenginezo.
Miongoni Mwa Makusudio Ya Suwrah:
1-Kubainisha hali ya malipo ya waja Siku ya Qiyaamah. [Al-Mukhtaswar Fiy Tafsiyr Al-Qur-aan Al-Kariym]
2-Kukumbusha Siku ya Qiyaamah na hali zake ngumu, na yatakayotokea pamoja na kuhesabiwa na kulipwa, na thawabu (malipo mema) na adhabu.
Miongoni Mwa Maudhui Ya Suwrah:
1-Suwrah imefunguliwa kwa kubainishwa ada mojawapo ya makafiri kuharakiza adhabu, nayo itawashukia tu hakuna wa kuizuia isipokuwa Allaah (سبحانه وتعالى), Mwenye Uluwa na fadhila tele.
2-Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) ameliwazwa kwa kutakwa avute subira kwa istihzai za makafiri wanaomkadhibisha na kuharakiza adhabu na kudhania kuwa iko mbali kabisa wala haitatokea, ilhali ipo karibu na hakuna shaka ya kutokea kwake.
3-Kisha yakatajwa baadhi ya matukio ya Siku ya Qiyaamah na majuto ya wahalifu Siku hiyo, watamani kujitolea fidia kwa ahli zake wote kutokana na adhabu.
4-Zimetajwa baadhi ya sifa za moto wenye mwako mkali kwamba unaonyofoa na ngozi za mwili na kuunguza viungo vya mwili.
5-Imetajwa hali ya baadhi ya wanaadam wenye kukosa kuvuta subira na hali yake anapopatwa shari kuwa hupapatika na kuhuzunika. Anapopatwa kheri hufanya uchoyo. Kisha ikafuatilia kuwasifu Waumini wasiokuwa na sifa za mwanaadam huyo aliye na pupa na kukosa subira.
6-Zikatajwa sifa za Waumini hao zikianza kuwasifia kuwa ni wenye kusimamisha na kudumisha Swalaah, na sifa nyenginezo kisha kumalizikia pia wenye kuhifadhi Swalaah zao. Na sifa hizi takriban, ni kama zile zilizotajwa mwanzoni mwa Suwrah Al-Muuminuwn (23), na zinamalizikia kwa kuahidiwa Jannah (Pepo).
7-Suwrah imekhitimishwa kwa kukemewa makafiri na kutajwa hali zao zitakavokuwa Siku ya Qiyaamah watakapotolewa makaburini kufufuliwa wakiwa madhalili na duni.
071-Nuwh: Utangulizi Wa Suwrah
Alhidaaya.com [2]
Imeteremka: Makkah kwa itifaki ya ‘Ulamaa.
Idadi Za Aayah: 28
Jina La Suwrah: Nuwh
Suwrah imeitwa Nuwh (عليه السّلام) na inayodalilisha ni kutajwa kwake katika Aayah namba (1).
Miongoni Mwa Makusudio Ya Suwrah:
1-Kubainisha njia ya kufanya da’wah kwa maduaati (walinganiaji). [Al-Mukhtaswar Fiy Tafsiyr Al-Qur-aan Al-Kariym]
2-Kupiga mfano kwa washirikina kupitia watu wa Nuwh, na wao ndio washirikina wa mwanzo ardhini.
Miongoni Mwa Maudhui Ya Suwrah:
1-Suwrah imefunguliwa kwa kuthibitishwa kutumwa Nuwh (عليه السّلام) kwa watu wake awaonye Adhabu za Allaah.
2-Ikafuatia uslubu ya Rusuli katika da’wah; kuanza kuwalingania watu katika Tawhiyd ya Allaah. Zikatajwa baadhi ya ada za washirikina kukanusha Risala ya Allaah, na ikatajwa jinsi Nuwh (عليه السّلام) alivomlalamikia Rabb wake kuhusu watu wake.
3-Akaendelea Nuwh (عليه السّلام) kuwanasihi watu wake kwa kuwapa matarajio na kuwakhofisha, na kuwatajia Rehma za Allaah Kuwaghufuria madhambi yao, na kuwatajia fadhila za istighfaar (kuomba maghfirah), na kuwakumbusha kuumbwa kwao, na kuwataka wazingatie Neema za Allaah juu yao za uanzilishi wa Uumbaji wa Allaah (سبحانه وتعالى) wa mbingu na ardhi na yaliyomo, na kuwakumbusha Siku ya kufufuliwa.
4-Imetajwa msimamo wa watu wa Nuwh (عليه السّلام) na inadi zao za kuwahimiza makafiri wenzao waendelee kuyaabudu masanamu yao kwa kuwatajia majina yao. Wakaendelea katika maasi na ushirikina, na ikatajwa adhabu zao duniani kwa kugharikishwa na Aakhirah kuingizwa motoni.
5-Yametajwa maombi ya Nuwh (عليه السلام) kwa Allaah (سبحانه وتعالى) Awang’oe makafiri ardhini asibakie kafiri yoyote.
6-Suwrah imekhitimishwa kwa Nuwh (عليه السلام) kuomba maghfirah yeye na wazazi wake na Waumini, na kuwaombea madhalimu wateketezwe.
072-Al-Jinn: Utangulizi Wa Suwrah
Alhidaaya.com [2]
Imeteremka: Makkah kwa itifaki ya ‘Ulamaa.
Idadi Za Aayah: 28
Jina La Suwrah: Al-Jinn
Suwrah imeitwa Al-Jinn (Majini), na inayodalilisha ni kutajwa kwake katika Aayah namba (1).
Miongoni Mwa Makusudio Ya Suwrah:
1-Kubatilisha dini ya washirikina, kwa kubainisha hali ya majini na imaan zao baada ya kuisikia Qur-aan. [Al-Mukhtaswar Fiy Tafsiyr Al-Qur-aan Al-Kariym]
2-Kutaja yanayofungamana na khabari za majini, na kusikiliza kwao Qur-aan, na mrejesho wao katika hilo, na kwa wale wenye kuitikia Amri za Allaah na wenye kuzipuuza.
Miongoni Mwa Maudhui Ya Suwrah:
1-Suwrah imefunguliwa kwa kutajwa majini walivoisifia Qur-aan kuwa ni ya ajabu, na inaongoza katika uongofu na wakaiamini.
2-Kisha wakamsifia Allaah (سبحانه وتعالى) kwa Ujalali Wake, na wakaahidi kutokumshirikisha Allaah (سبحانه وتعالى) na wakampwekesha na kumtakasa kwamba Yeye Allaah (سبحانه وتعالى) ni Pekee, Hahitaji kuwa na mke wala mwana!
3-Ikaendelea kutajwa mazungumzo ya majini kukiri makosa na madhambi yao, na kuwatahadharisha majini wenzao kwa adhabu itakayowapata pindi wakipanda juu kusikiliza siri za mbinguni, na wakadhihirisha unyenyekevu wao.
4-Imetajwa vigawanyo vya majini kati ya wema na waovu, na kati ya Waislamu na makafiri.
5-Ikatajwa makatazo ya kumshirikisha Allaah (سبحانه وتعالى) na yeyote bali inapaswa Kumpwekesha katika ibaada zote zikiwemo za kuomba duaa.
6-Yametajwa mas-ala kadhaa kwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) ayabalighishe kwa watu na wakaonywa wale watakaomuasi Allaah (سبحانه وتعالى) na kuahidiwa makazi mabaya ya motoni wadumu humo.
7-Suwrah imekhitimishwa kwa kubainishwa Sifa Tukufu za Allaah za Ujuzi wa ghaibu na yaliyofichika na sifa hii hakuna yeyote mwenye kuimiliki isipokuwa Yeye Pekee (عزّ وجلّ).
073-Al-Muzzammil: Utangulizi Wa Suwrah
Alhidaaya.com [2]
Imeteremka: Makkah kwa itifaki ya ‘Ulamaa.
Idadi Za Aayah: 20
Jina La Suwrah: Al-Muzzammil.
Suwrah imeitwa Al-Muzzammil (Mwenye Kujifunika), na yanayodalilisha ni kutajwa kwake katika Aayah namba (1).
Miongoni Mwa Makusudio Ya Suwrah:
1-Kuzibainisha sababu zitakazosaidia kuzisimamia tabu za da’wah. [Al-Mukhtaswar Fiy Tafsiyr Al-Qur-aan Al-Kariym]
2-Maelekezo katika kile kinachopasa kujiandaa nacho, ili kubeba (kuvumilia) uzito wa mizigo ya da’wah.
Miongoni Mwa Maudhui Ya Suwrah:
1-Suwrah imefunguliwa kwa kuamrishwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) aliyenadiwa kwa Al-Muzzammil (Aliyejifunika nguo), aamke kwa ajili ya Qiyaamul-Layl (Kisimamo cha usiku kutekeleza ibaada) kwa muda mwingi.
2-Allaah (سبحانه وتعالى) Amemthibitishia Rasuli Wake (صلى الله عليه وآله وسلم) katika kubalighisha Wahy, kwa kumwamrisha avute subira nzuri kutokana na maudhi ya makafiri.
3-Allaah (سبحانه وتعالى) Amewabainishia makafiri baadhi ya vitisho vya Siku ya Qiyaamah na adhabu Alizowaandalia.
4-Kisha Allaah (سبحانه وتعالى) Akawakumbusha makafiri maangamizi ya Firawni alipomkadhibisha Rasuli wa Allaah; Muwsaa (عليه السّلام).
5-Ikafuatilia kutajwa baadhi ya vitisho vya Siku ya Qiyaamah, Siku ambayo itawafanya watoto wawe na mvi, na mifupa yao kunyong’onyea kabisa.
6-Suwrah imekhitimishwa kwa kumsahilishia Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) na Waumini katika Qiyaamul-Layl (Kisimamo cha usiku, Tahajjud) kutekeleza ibaada katika hali ya safari, ugonjwa na pindi wanapokuwa wametoka kupigana Jihaad. Na wakawepesishiwa kuisoma Qur-aan katika hali hizo. Kisha wakaamrishwa kutekeleza faradhi za Swalaah na Zakaah, na kutoa swadaqa, na wakabashiriwa malipo makubwa na maghfirah kutoka kwa Allaah (سبحانه وتعالى).
074-Al-Muddath-thir: Utangulizi Wa Suwrah
Alhidaaya.com [2]
Imeteremka: Makkah kwa itifaki ya ‘Ulamaa.
Idadi Za Aayah: 56
Jina La Suwrah: Al-Muddath-thir
Suwrah imeitwa Al-Muddath-thir (Mwenye Kujigubika), na inayodalilisha ni kutajwa kwake katika Aayah namba (1).
Miongoni Mwa Makusudio Ya Suwrah:
1-Kuamrisha watu kujitahidi katika kuwalingania wanaokadhibisha (Risala ya Allaah), na kuwaonya kwa Aakhirah na Qur-aan. [Al-Mukhtaswar Fiy Tafsiyr Al-Qur-aan Al-Kariym]
2-Kumliwaza Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) kwa kuwaradd washirikina wa Makkah na kuwaahidi adhabu kwa kukanusha Risala ya Allaah.
3-Kubainishwa sababu za kuingizwa motoni.
Miongoni Mwa Maudhui Ya Suwrah:
1-Suwrah imefunguliwa kwa kuamrishwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) aliyenadiwa kwa Al-Muddath-thir (Aliyejigubika nguo) ainuke kwa ajili ya kubalighisha Risala ya Allaah (سبحانه وتعالى) na kuwaonya watu wake, na Amtukuze Rabb wake, na atoharishe nguo zake. Na akaamrishwa kuendelea kujiepusha na ushirikina.
2-Kisha akaongozwa katika misimamo ya da’wah ambayo ni kuwa na ikhlaasw katika da’wah kwa kutokutaraji malipo kutoka kwa watu, na kuvuta subira kwani lazima kuweko maudhi na mateso katika da’wah.
3-Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) ameliwazwa kutokana na kukadhibishwa na watu wake wa Makkah, kwa kuwatishia maadui zake kwa aina kali za adhabu. Na ikaelezwa kisa cha mmoja wa Quraysh aliyekuwa tajiri na hadhi kubwa katika Maquraysh, aliyeisikiliza Qur-aan kutoka kwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم), ambayo ilimuathiri kutaka kuiamini, lakini akatafakari na kutafakari, mwishowe akatakabari na kuipachika sifa ovu Qur-aan kuwa ni sihri inayonukuliwa tu! Basi Allaah (سبحانه وتعالى) Akamuahidi kafiri huyo adhabu kali ya moto wa saqar usiobakisha nyama wala mifupa ila kuvichoma, na unaounguza ngozi hadi iwe nyeusi.
4-Kisha ikatajwa idadi ya Malaika kumi na tisa (19) ambao ni walinzi wa moto, walio wakali na washupavu, na idadi hiyo ikawa ni jaribio kwa makafiri ili iwe yakini kwa Mayahudi na Manaswara kutambua yanayoafikiana na yale yaliyoandikwa katika Vitabu vyao kuhusu Malaika wa hazina ya moto, na iwazidishie imaan Waumini. Na wale wanafiki wenye maradhi nyoyoni mwao na makafiri waseme: “Ni lipi Alokusudia Allaah kwa idadi hii ya ajabu?” Lakini mfano kama huu, Allaah Humpotoa Amtakaye na Humhidi Amtakaye kwa sababu Ana Ujuzi wa ghaibu wa kujua yalimo nyoyoni mwa watu.
5-Kisha ikafuatilia Kiapo cha Allaah (سبحانه وتعالى) kuapia mwezi na usiku unapogeuka kutoweka, na asubuhi inapopambazuka. Na jibu la kiapo ni kuthibitishwa moto kwamba, ni katika mambo makuu na kwa ajili ya kuwatishia watu.
6-Imebainishwa mwisho mzuri wa Waumini kuingizwa Jannah. Na ikabainishwa mwisho mbaya kwa wahalifu, na zikatajwa sababu zao kuwa walikuwa hawaswali, wala kulisha masikini, na kunena ya ubatilifu pamoja na wapotevu.
7-Makafiri wamekemewa kwa kujiepusha kwao na Qur-aan, na kutaka wateremshiwe kitabu chao kutoka mbinguni, na kutokuiogopa Aakhirah.
8-Suwrah imekhitimishwa kwa kuthibitishwa kuwa Qur-aan ni mawaidha ya ufasaha, na kwamba hawaidhiki nayo isipokuwa ambaye Allaah (سبحانه وتعالى) Ameshamjua anayetaka kuwaidhika, hivyo basi Humhidi kwayo Amtakaye, na kwamba Allaah (سبحانه وتعالى) Ndiye Anayestahiki kuogopwa na Mwenye Kustahiki kughufuria madhambi ya waja.
075-Al-Qiyaamah: Utangulizi Wa Suwrah
Alhidaaya.com [2]
Imeteremka: Makkah kwa itifaki ya ‘Ulamaa
Idadi Za Aayah: 40
Jina La Suwrah: Al-Qiyaamah
Suwrah imeitwa Al-Qiyaamah (Ufufuo), na inayodalilisha ni kutajwa kwake katika Aayah namba (1).
Miongoni Mwa Makusudio Ya Suwrah:
1-Kudhihirisha Uwezo wa Allaah (سبحانه وتعالى) wa kuwafufua viumbe, na kuwakusanya Siku ya Qiyaamah. [Al-Mukhtaswar Fiy Tafsiyr Al-Qur-aan Al-Kariym]
2-Kuielezea Siku ya Qiyaamah na maelezo ya baadhi ya vitisho vyake, na hali za watu Siku hiyo.
Miongoni Mwa Maudhui Ya Suwrah:
1-Suwrah imefunguliwa kwa kiapo cha Allaah (سبحانه وتعالى) Kuapia Siku ya Qiyaamah, na nafsi inayojilaumu kwa kufanya maovu na kuacha kutenda mema. Na jibu lake limefuatia la kuwaradd wasioamini kufufuliwa, kwa kutolewa dalili ya nguvu kabisa, nayo ni kusawazisha sawasawa ncha za vidole vyao.
2-Imethibitishwa tena kufufuliwa kwa viumbe na kutajwa ada za makafiri kukanusha Qiyaamah kwa kuulizia lini kitatokea.
3-Kisha ikathibitishwa baadhi ya matukio ya Qiyaamah kama kutokea kwa khusuwf (kupatwa mwezi) na kusuwf (kupatwa jua). Na hapo mtu hatakuwa na pa kukimbilia, na atasimamishwa atambulishwe yote aliyoyatenda na kuhesabiwa. Na Siku hiyo mtu atajishuhudia mwenyewe wala hatoweza kutoa nyudhuru zozote zile.
4-Allaah (سبحانه وتعالى) Amemuongoza Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) adabu za kupokea Wahy.
5-Zimetajwa hali za watu kutofautiana; wema na waovu. Wema wataneemeshwa kwa kung’arishwa nyuso zao pindi watakapomwangalia Rabb wao huko Jannah.
6-Imekumbushwa mauti na kwamba (hayo mauti) ndio hatua ya mwanzo ya Aakhirah.
7-Suwrah imekhitimishwa kwa kuwathibitishia makafiri waliojigamba na kutakabari na kukanusha kufufuliwa, dalili za wazi kabisa za Uwezo wa Allaah (سبحانه وتعالى) kwamba Yeye Aliyewaumba kutokana na tone la manii, kisha Akaziunda sura na maumbo yao vizuri kabisa, kisha Akajaalie jinsia mbili; ya kiume na kike, kwamba yeye Allaah (سبحانه وتعالى) ni Mweza wa Kuwahuisha baada ya kufa kwao!
076-Al-Insaan: Utangulizi Wa Suwrah
Alhidaaya.com [2]
Imeteremka: Makkah au Madiynah kwani ‘Ulamaa wamekhitilafiana kuhusu wapi imeteremshwa.
Idadi Za Aayah: 31
Jina La Suwrah: Al-Insaan
Suwrah imeitwa Al-Insaan (Binaadam) kwa kutajwa kwake katika Aayah namba (1). Na pia kutajwa kwa jina lake jengine katika Hadiyth iliyonukuliwa chini katika Fadhila.
Miongoni Mwa Makusudio Ya Suwrah:
1-Kumkumbusha binaadam asili ya kuumbwa kwake na mafikio yake, na kubainisha Aliyoyaahidi Allaah (سبحانه وتعالى) kwa Vipenzi Vyake. [Al-Mukhtaswar Fiy Tafsiyr Al-Qur-aan Al-Kariym]
2-Kutajwa kuumbwa kwa binaadam, na kugawanyika kwao na marejeo yao Siku ya Qiyaamah.
3-Kuwafanya wanaadam wawe na At-Targhiyb (Yanayoshajiisha nafsi kuikubali haki na kutenda mema kutokana na fadhila zake) na At-Tarhiyb (yanayotishia na kutahadharisha kutenda maasi kutokana na malipo yake).
Miongoni Mwa Maudhui Ya Suwrah:
1-Suwrah imefunguliwa kwa kumkumbusha mwanaadam Neema za Allaah (سبحانه وتعالى) juu yake, pale alipoumbwa kutokana na tone la manii yaliyochanganyika, na akamfanya mwenye kusikia, mwenye kuona, na akamuongoza njia, basi kuna anayeshukuru na anayekufuru.
2-Makafiri wameahidiwa maandalizi ya motoni huku wamefungwa minyororo na pingu.
3-Al-Abraar (wenye kutenda mema mengi) wameahidiwa mazuri ya mto wenye kinywaji kizuri cha kafuri. Na zikatajwa sifa zao kadhaa kama kutimiza nadhiri zao, na kukhofu adhabu za Allaah, kulisha kwa mapenzi yao masikini, yatima na matekwa ya vita bila kutaka shukurani au kusifiwa, kuvuta kwao subira duniani. Kisha ikafuatia kutajwa mazuri na Neema kadhaa za Allaah Alizowaandalia Al-Abraar hao katika Jannah vikiwemo vyakula wanavyovitamani, vinywaji safi visivyo na madhara, mavazi na mengineyo kadhaa.
4-Imethibitishwa kwamba Qur-aan imetoka kwa Allaah (سبحانه وتعالى) na kumliwaza Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) avute subira kutokana na maudhi ya makafiri, na kumwamrisha amdhukuru Rabb wake asubuhi na jioni, na Kumsujudia na Kumsabbih (Kumtakasa) nyakati nyingi za usiku.
5-Suwrah imekhitimishwa kwa kubainishwa kwamba hakuna awezaye kutaka jambo lolote lile isipokuwa liwe kwa Matakwa ya Allaah (سبحانه وتعالى), na kwamba Anamuingiza Amtakaye katika Rehma Yake, na Amewaandalia adhabu kali madhalimu.
Fadhila Za Suwrah:
Inapendekezwa kuisoma katika Swalaah ya Asubuhi Siku ya Ijumaa katika Rakaa ya pili kwa dalili ifuatayo:
عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ ـ رضى الله عنه ـ قَالَ كَانَ النَّبِيُّ صلى الله عليه وسلم يَقْرَأُ فِي الْجُمُعَةِ فِي صَلاَةِ الْفَجْرِ الم * تَنْزِيلُ السَّجْدَةَ وَ هَلْ أَتَى عَلَى الإِنْسَانِ
Amesimulia Abuu Hurayrah (رضي الله عنه): Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alikuwa akisoma katika Swalaah ya Alfajiri siku ya Ijumaa:
الم ﴿١﴾ تَنزِيلُ
As-Sajdah (32) na
هَلْ أَتَىٰ عَلَى الْإِنسَانِ
Suwrah Al-Insaan (76). [Al-Bukhaariy, Muslim na wengineo]
077-Al-Mursalaat: Utangulizi Wa Suwrah
Alhidaaya.com [2]
Imeteremka: Makkah kwa itifaki ya ‘Ulamaa.
Idadi Za Aayah: 50
Jina La Suwrah: Al-Mursalaat
Suwrah imeitwa Al-Mursalaat (Vinavyotumwa), na yanayodalilisha ni kutajwa kwake katika Hadiyth zilizonukuliwa chini katika Fadhila na Faida. Na pia kutajwa kwake katika Aayah namba (1).
Miongoni Mwa Makusudio Muhimu Ya Suwrah:
1-Ahadi ya adhabu kali siku ya Qiyaamah kwa wanaokadhibisha. [Al-Mukhtaswar Fiy Tafsiyr Al-Qur-aan Al-Kariym]
2-Kuwaogopesha makafiri na kuwatahadharisha kutokana na ukafiri.
Miongoni Mwa Maudhui Ya Suwrah:
1-Suwrah imefunguliwa kwa Kiapo cha Allaah (سبحانه وتعالى) Kuapia Pepo zinazotumwa mfululizo. Na kwa pepo za dhoruba. Na kwa pepo zinazotawanya mawingu ya mvua. Kisha Allaah (سبحانه وتعالى) Akaendelea Kuapia Malaika wanaopambanua haki na baatwil, halali na haraam, na Malaika wanaopokea Wahy kutoka Kwake kupeleka kwa Rusuli Wake, Wahy ambao unawapa viumbe nyudhuru na maonyo ili wasiwe na hoja Siku ya Qiyaamah kwamba hawajaletewa Rusuli na Risala ya Allaah. Kisha likaja jibu la Kiapo cha Allaah, nalo ni kuthibitisha kutokea yote waliyoahidiwa viumbe ya kutokea Siku ya Qiyaamah kama kupulizwa baragumu, kufufuliwa, kukusanywa katika Ardhw Al-Mahshar (Ardhi ya Mkusanyiko), na kuhesabiwa matendo; mema jazaa yake kuingizwa Jannah, na maovu jazaa yake kuingizwa motoni.
2-Kisha ikafuatia kutajwa baadhi ya matukio ya Siku ya Qiyaamah kama nyota kutoweka mwangaza wake, mbingu kupasukapasuka, majabali kupondekapondeka yawe kama mavumbi yanayopeperushwa, na Rusuli kutoa ushahidi wao wa kubalighisha Risala ya Allaah (سبحانه وتعالى). Kisha ikakariri Kauli ya Allaah kila baada ya Aayah kadhaa:
وَيْلٌ يَوْمَئِذٍ لِّلْمُكَذِّبِينَ﴿١٥﴾
“Ole (wao) Siku hiyo kwa wenye kukadhibisha.”
3-Yakatajwa maangamizi ya nyumati zilizopita kwa kukadhibisha Risala ya Allaah.
4-Zikatajwa hoja za mionekano ya baadhi ya Uwezo wa Allaah (سبحانه وتعالى) kama kuumba viumbe, kuumba ardhi, kuthibitisha milima ardhini, kuteremshiwa mvua, kuhuisha na kufisha.
5-Ikatajwa baadhi ya vitisho kwa waliokadhibisha kama kuwekwa kwenye vivuli vyenye mwako wa moto, wasiweze kunena lolote la kuwanufaisha wala kupewa idhini ya kutoa nyudhuru. Wataambiwa kuwa hiyo ni Siku waliyoikadhibisha, ambayo ni Siku itakayokusanya viumbe wote tokea mwanzo hadi mwisho, Siku ambayo Allaah Atatoa Hukmu Yake na ukweli na ubatilifu utapambanuka.
6-Waumini wenye taqwa ambao waliogopa Adhabu za Allaah (سبحانه وتعالى), wamebashiriwa jazaa ya matendo yao mazuri kwa kuwekwa kwenye vivuli na chemchemu wastarehe, na wapate matunda wanayoyatamani na vinywaji safi vya ladha nzuri, wale na wanywe kwa furaha.
7-Ikatajwa jazaa ya makafiri kwa kuambiwa wale aina ya vyakula walivyokuwa wakila duniani ambayo ni starehe ya muda mfupi tu! Hiyo ni jazaa yao kwa kukanusha Amri za Allaah kukataa kumnyenyekea Allaah na kuswali.
8-Suwrah imemalizikia kwa onyo kwamba, ikiwa makafiri hawataiamini Qur-aan hii ambayo Aaayat Zake ziko wazi katika Hikma Zake, yenye mwongozo na Rehma, basi wataamini kitabu gani baada yake?
Fadhila Za Suwrah:
1-Suwrah Ya Mwisho Ambayo Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) ameisoma katika Swalaah ya Magharibi:
عَنِ ابْنِ عَبَّاسٍ ـ رضى الله عنهما ـ أَنَّهُ قَالَ إِنَّ أُمَّ الْفَضْلِ سَمِعَتْهُ وَهُوَ يَقْرَأُ - وَالْمُرْسَلاَتِ عُرْفًا - فَقَالَتْ يَا بُنَىَّ وَاللَّهِ لَقَدْ ذَكَّرْتَنِي بِقِرَاءَتِكَ هَذِهِ السُّورَةَ، إِنَّهَا لآخِرُ مَا سَمِعْتُ مِنْ رَسُولِ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم يَقْرَأُ بِهَا فِي الْمَغْرِبِ.
Amesimulia Ibn ‘Abbaas (رضي الله عنهما): (Mama yangu) Umul-fadhwl alinisikia nikisoma:
وَالْمُرْسَلَاتِ عُرْفًا﴿١﴾
Akasema: “Ee mwanangu! Wa-Allaahi umenifanya nikumbuke kuwa ilikuwa Suwrah ya mwisho niliyoisikia kutoka kwa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akiisoma katika Swalaah ya Maghrib.” [Al-Bukhaariy]
2-Nyoka Alikimbia Alipokuwa Akiisooma Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم):
عَنِ الأَسْوَدِ، قَالَ قَالَ عَبْدُ اللَّهِ بَيْنَا نَحْنُ مَعَ رَسُولِ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم فِي غَارٍ إِذْ نَزَلَتْ عَلَيْهِ وَالْمُرْسَلاَتِ فَتَلَقَّيْنَاهَا مِنْ فِيهِ وَإِنَّ فَاهُ لَرَطْبٌ بِهَا إِذْ خَرَجَتْ حَيَّةٌ فَقَالَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم " عَلَيْكُمُ اقْتُلُوهَا ". قَالَ فَابْتَدَرْنَاهَا فَسَبَقَتْنَا ـ قَالَ ـ فَقَالَ " وُقِيَتْ شَرَّكُمْ، كَمَا وُقِيتُمْ شَرَّهَا ".
Amesimulia Al-Aswad (رضي الله عنه): ‘Abdullaah [Bin Mas’uwd] (رضي الله عنه) amesema: Tulipokuwa pamoja na Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) katika pango ikateremka
وَالْمُرْسَلَاتِ
Naye anaisoma, nami naipokea kutoka kinywani mwake, na hakika kinywa chake kina rutuba (sio kikavu kwa kuisoma Suwrah hiyo). Ghafla akatoka nyoka, Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akasema: “Lazima mumuuwe!” ‘Abdillaah akasema: Tukamfukuza akatukimbia. Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akasema: “Amesalimishwa na shari yenu kama mlivyosalimishwa na shari yake.” [Al-Bukhaariy]
078-An-Nabaa: Utangulizi Wa Suwrah
Alhidaaya.com [2]
Imeteremka: Makkah kwa itifaki ya ‘Ulamaa.
Idadi Za Aayah: 40
Jina La Suwrah: An-Nabaa
Suwrah imeitwa An-Nabaa (Habari Muhimu), na inayodalilisha ni kutajwa kwake katika Aayah namba (2).
Miongoni Mwa Makusudio Ya Suwrah:
1-Kubainisha dalili za Uwezo wa Allaah (سبحانه وتعالى) wa Kufufua (viumbe), na kuwahofisha juu ya mwisho (mbaya). [Al-Mukhtaswar Fiy Tafsiyr Al-Qur-aan Al-Kariym]
2-Kuthibisha kufufuliwa na vitisho vyake, na kuwaonya wenye kuipinga.
Miongoni Mwa Maudhui Ya Suwrah:
1-Suwrah imefunguliwa kwa kuwauliza washirikina ni jambo gani wanaulizana? Na kwamba wanaulizana kuhusu habari muhimu iliyo kubwa mno nayo ni Qur-aan ambayo inatoa habari za Tawhiyd ya Allaah na mengineyo yaliyomo humo na kuhusu kufufuliwa, jambo ambalo washirikina hawakuamini. Na kisha kuwatishia kwa mafikio mabaya pindi watakapoendelea katika kufru zao za kupinga kwao yale aliyokuja nayo Nabiy Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم).
2-Kisha Allaah (سبحانه وتعالى) Akawabainishia Ishara Zake, na Dalili zenye kudhihirisha Tawhiyd Yake, na Uwezo Wake Mkubwa wa kuumba viumbe na vinginevyo, kama kuumba ardhi na mbingu na yaliyomo, pamoja na Neema Zake kadhaa Alizowajaalia viumbe waweze kuishi katika ardhi hii.
3-Kisha ikatajwa Siku ya Qiyaamah, Siku ambayo ni Siku ya Uamuzi kati ya viumbe, na kutajwa baadhi ya matukio yake kama kupulizwa baragumu na watu kufufuliwa makaburini, na mbingu kufunguliwa milango yake ili wateremke Malaika, na majabali kulipuliwa yakawa kama mangati.
4-Kisha ikatajwa Jahannam kuwa ni marejeo ya makafiri, na ikatajwa yale Aliyoyaandaa Allaah (سبحانه وتعالى) humo ya vyakula na vinywaji vya moto na usaha, kuwa ni jazaa yao humo kwa kukutoamini Siku hiyo ya kuhesabiwa, na kukadhibisha kwao Risala ya Allaah. Basi hakuna watakachopata isipokuwa kuongezewa adhabu.
5-Waumini wenye taqwa wamebashiriwa kufaulu na kuingizwa mabustani ya zabibu na mengineyo Aliyowaandalia Allaah humo ya Neema Zake, kama Hurulaini (wanawake wazuri wenye macho makubwa ya kupendeza), na vinywaji safi vizuri, na mengineyo, kuwa ni jazaa yao kwa kuamini kwao na matendo mema duniani.
6-Imebainishwa wazi kwamba Siku ya Qiyaamah ni kweli na haina shaka, na kwamba inapasa kutanguliza matendo mema kabla ya kutokea Siku hiyo.
7-Suwrah imekhitimishwa kwa kuonywa adhabu iliyo karibu, na kudhihirishwa matendo ya waja, ya kheri na ya shari, na kutamani kafiri Siku hiyo lau angekua mchanga.
079-An-Naazi’aat: Utangulizi Wa Suwrah
Alhidaaya.com [2]
Imeteremka: Makkah kwa itifaki ya ‘Ulamaa.
Idadi Za Aayah: 46
Jina La Suwrah: An-Naazi’aat
Suwrah imeitwa An-Naazi’aat (Wanaong’oa Kwa Nguvu), na inayodalilisha ni kutajwa kwake katika Aayah namba (1).
Miongoni Mwa Makusudio Ya Suwrah:
1-Kuwakumbusha watu kumjua Allaah (عزّ وجلّ), na (kuijua) Siku ya Mwisho. [Al-Mukhtaswar Fiy Tafsiyr Al-Qur-aan Al-Kariym]
2-Kuweka wazi kwamba kufufuliwa ni kweli, na kutaja baadhi ya vitisho vya Qiyaamah, na kuwaradd washirikina wenye kupinga kufufuliwa, na kuwatishia na kuwaogopesha.
Miongoni Mwa Maudhui Ya Suwrah:
1-Suwrah imefunguliwa kwa Kiapo cha Allaah (سبحانه وتعالى) Kuapia Malaika wanaotoa roho za makafiri kwa mng’oo mkali kabisa. Na kwa Malaika wanaotoa roho za Waumini kwa upole kabisa. Na kwa Malaika wanaoogelea katika kuteremka kwao kutoka mbinguni na kupaa kwenda mbinguni. Na kwa Malaika wanokimbilia kutekeleza Amri za Allaah. Na kwa Malaika wanaopitisha Amri za Allaah.
2-Kisha ikafuatia jibu la Kiapo, nalo ni kuthibitisha Qiyaamah, kwa kutajwa baadhi ya matukio yake, kama ardhi kutetemeka kwa mpulizo wa kwanza wa baragumu, ambao watu wote watakufa isipokuwa Awatakao Allaah. Kisha utafuatilia mpulizo wa pili wa baragumu, ambao watu watafufuliwa kutoka makaburini wakiwa katika umbo jipya. Siku hiyo nyoyo zitapapatika, na macho yatakuwa dhalili kwa vitisho watakavyoviona.
3-Kisha ikabainishwa kauli za washirikina waliokuwa wakiuliza duniani, kama kweli watafufuliwa waumbwe upya, ilhali mifupa imeshasagika na kuoza makaburini. Lakini Allaah (سبحانه وتعالى) Akawaradd kwa kuthibitisha kuwa, tukio hilo litatokea kwa mlio mmoja tu wa kuwafisha, kisha baada ya baragumu la pili, watatahamaki wako juu ya ardhi baada ya kuwa makaburini.
4-Imetajwa sehemu ya kisa cha Nabiy Muwsaa (عليه السّلام) alipoitwa na Allaah katika bonde lilobarikiwa la Twuwaa, na kutumwa kwa Firawni. Nabiy Muwsaa (عليه السّلام) akamwonyesha Firawni Ishara na Dalili za Allaah za miujiza, lakini alimkadhibisha na akaasi, na akawanadia watu wake wamwabudu yeye badala ya Allaah. Basi Allaah (سبحانه وتعالى) Akamwangamiza kwa adhabu ya duniani kwa kumgharikisha, na anaendelea kuadhibiwa mpaka Siku ya Qiyaamah, ambako atapata adhabu kali zaidi! Basi hayo yawe mazingatio kwa wenye kumkhofu Allaah.
5-Ikathibitishwa tena kufufuliwa kwa muonekano wa dalili kadhaa za Uwezo wa Allaah, wa uumbaji wa mbingu na ardhi na yaliyomo.
6-Yakatajwa baadhi ya matukio ya kutisha Siku ya Qiyaamah, Siku ambayo moto wa Jahannam utaonekana wazi, waingizwe humo waliopinduka mipaka na wakapendelea maisha ya dunia. Ama ambao walijizuia nafsi zao na matamanio, wakakhofu kusimamishwa mbele ya Rabb wao, basi hao makazi yao yatakuwa ni kuingizwa Jannah.
7-Suwrah imekhitimishwa kwa kujibu maswali ya washirikina kuhusu Qiyaamah, na kubainisha kwamba ahadi ya kutokea Siku hii, ujuzi wake uko kwa Allaah Pekee, na lilokuwa wajibu kwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم), ni kuwakumbusha tu hicho Qiyaamah, na kwamba pindi kitakapowajia na wakakiona, basi kana kwamba wao hawakuishi duniani isipokua sehemu tu katika mchana.
080-‘Abasa: Utangulizi Wa Suwrah
Alhidaaya.com [2]
Imeteremka: Makkah kwa itifaki ya ‘Ulamaa.
Idadi Za Aayah: 42
Jina La Suwrah: ‘Abasa
Suwrah imeitwa ‘Abasa (Alikunja Kipaji) cha uso. Na inayodalilisha ni kutajwa kwake katika Aayah namba (1).
Miongoni Mwa Makusudio Ya Suwrah:
1-Kuwakumbusha dalili za kufufuliwa makafiri walioghafilika na Rabb wao. [Al-Mukhtaswar Fiy Tafsiyr Al-Qur-aan Al-Kariym]
2-Uhalisia wa da’wah ya Qur-aan na utukufu wa yule mwenye kunufaika nayo, na udhalili wa yule mwenye kuipuuza.
Miongoni Mwa Maudhui Ya Suwrah:
1-Suwrah imefunguliwa kwa kudhihirika ukunjaji uso wa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) na kumgeukia kwake Swahaba Mtukufu, Ibn Ummi Maktuwm (رضي الله عنه) aliyemwendea kutaka kujifunza kwake, lakini Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akawa ameshughulika kumlingania Quraysh mmoja aliyekuwa tajiri, naye Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alikuwa ana himma ya kuongoza watu, akataraji ahidike tajiri huyo. Basi Allaah (سبحانه وتعالى) Akamuwaidhi Rasuli Wake Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم), mawaidha mazuri ya upole.
2-Ikabainishwa kwamba mawaidha hayo ya Allaah (سبحانه وتعالى) Alimyomuwaidhi Rasuli Wake (صلى الله عليه وآله وسلم), Anawakumbusha Waja Wake pia kwamba, ni mawaidha kwa mwenye kutaka kuwaidhika kwa Qur-aan. Na Anawabainishia usawa baina ya watu katika da’wah na kubalighisha ilimu kwa wenye hadhi na walio wanyonge.
3-Imebainishwa Utukufu wa Qur-aan iliyomo katika Sahifa zenye kutakaswa na kuadhimiwa, na zimo katika Mikono ya Malaika waandishi walio watukufu na watiifu.
4-Imethibitishwa Tawhiyd ya Allaah kwa kutajwa asili ya chimbuko la mwanaadam na Neema za Allaah kwao za kuwawepesishia njia, na hifadhi na takrima zao za kuzikwa makaburini, na Kuwateremshia mvua inayokuza mimea ikatoka humo kila aina ya mazao, yawanufaishe katika uhai wao, wao pamoja na wanyawa wao.
5-Suwrah imekhitimishwa kwa kukumbushwa vitisho vya Siku ya Qiyaamah, na hali za watu itakavokuwa kwamba, kila mtu atamkimbia mwenzake hata kuwakimbia wazazi wake, na wengineo wa uhusiano wa damu. Na kwamba watu watakuwa aina mbili; ambao watakaofaulu kwa kudhihirika nyuso zao kunawiri na kuwa na furaha. Na watakaokhasirika kwa kudhihirika nyuso zao kufunikwa na vumbi na kubadilika kuwa nyeusi, na hawa ndio makafiri wapotofu wavukao mipaka katika kufru na shirki zao, na matendo yao.
081-At-Takwiyr: Utangulizi Wa Suwrah
Alhidaaya.com [2]
Imeteremka: Makkah kwa itifaki ya ‘Ulamaa.
Idadi Za Aayah: 29
Jina La Suwrah: At-Takwiyr
Suwrah imeitwa At-Takwiyr (Kukunjikakunjika), na yanayodalilisha ni kutajwa katika Hadiyth iliyonukuliwa katika Faida, na kutajwa katika Aayah namba (1).
Miongoni Mwa Makusudio Ya Suwrah:
1-Ukamilifu wa Qur-aani katika kuikumbusha nafsi juu ya kuharibika ulimwengu wakati wa kufufuliwa waja. [Al-Mukhtaswar Fiy Tafsiyr Al-Qur-aan Al-Kariym]
2-Kubainisha hali za Qiyaamah, na vitisho vyake.
Miongoni Mwa Maudhui Ya Suwrah:
1-Suwrah imefunguliwa kwa kutajwa yatakayotokea Siku ya Qiyaamah, yenye kushtua nyoyo, kama jua kukunjwa na kupotea mwanga wake, nyota kuanguka, milima kupondwapondwa, ngamia kutelekezwa, wanyama mwitu kukusanywa, bahari zitakapowashwa moto, watu watakapounganishwa wema kwa wema, waovu kwa waovu, mtoto wa kike aliyezikwa hai kutokana na kudhalilishwa, atakapoulizwa ni dhambi ipi aliyofanya hata astahiki kudhulumiwa hivo! Sahifa za matendo zitakapokunjuliwa, mbingu zitakapobanduliwa.
2-Kisha ikafuatia kutajwa kuwa Jannah itakurubishwa, na moto kuwa utahudhurishwa; vyote hivi viwe mbele ya viumbe.
3-Kisha Allaah (سبحانه وتعالى) Akaapia kwa sayari zinazotoweka mchana na kudhihirika usiku, na kuingia kwa usiku, na kupambazuka kwa asubuhi.
4-Ikafuatia jibu la Kiapo ni kuthibitishwa kwamba Quraan inatoka kwa Allaah (سبحانه وتعالى) na akatajwa anayeipokea ambaye ni Jibriyl (عليه السّلام) na zikatajwa sifa zake tukufu, na akathibitishwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) kwa sifa nzuri, ambaye anaipokea Qur-aan na kuibalighisha. Na Allaah (سبحانه وتعالى) Akamliwaza Rasuli Wake (صلى الله عليه وآله وسلم) na kuwaradd washirikina waliompachika sifa ovu ya umajnuni.
4-Imebainishwa kwamba Qur-aan ni mawaidha na ukumbusho kwa mwenye kutaka kuhidika.
5-Suwrah imekhitimishwa kwa kuwekwa wazi ya kwamba, matakwa ya mja ni yenye kufuata Matakwa ya Allaah, Rabb wa walimwengu wote.
Faida:
Anayetaka Kuitazama Siku Ya Qiyaamah, Asome Suwrah hii:
عَنْ عَبْدِ الرَّحْمَنِ، وَهُوَ ابْنُ يَزِيدَ الصَّنْعَانِيُّ قَالَ سَمِعْتُ ابْنَ عُمَرَ، يَقُولُ قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم " مَنْ سَرَّهُ أَنْ يَنْظُرَ إِلَى يَوْمِ الْقِيَامَةِ كَأَنَّهُ رَأْىُ عَيْنٍ فَلْيَقْرَأْ إِذَا الشَّمْسُ كُوِّرَتْ ) و (إِذَا السَّمَاءُ انْفَطَرَتْ ) وَ (إذَا السَّمَاءُ انْشَقَّتْ " . هَذَا حَدِيثٌ حَسَنٌ غَرِيبٌ
Amesimulia ‘Abdur-Rahmaan naye ni Ibn Yaziyd Asw-Swan’aaniyy (رضي الله عنه): Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Mwenye kutaka kuitazama Siku ya Qiyaamah, kana kwamba anaiona kwa jicho hili, basi na asome:
إِذَا الشَّمْسُ كُوِّرَتْ ﴿١﴾
“Jua litakapokunjwa kunjwa na kupotea mwanga wake.” [At-Takwiyr (81)]
إِذَا السَّمَاءُ انفَطَرَتْ ﴿١﴾
“Mbingu itakapopasuka.” [Al-Infitwaar (82)]
إِذَا السَّمَاءُ انشَقَّتْ ﴿١﴾
“Mbingu itakaporaruka.” [Al-Inshiqaaq (84)]
[Ahmad (4806), At-Tirmidhiy (3333), amesema ni Hadiyth Hasan Ghariyb. Ameisahihisha Al-Albaaniy katika Swahiyh At-Tirmidhy]
082-Al-Infitwaar: Utangulizi Wa Suwrah
Alhidaaya.com [2]
Imeteremka: Makkah kwa itifaki ya ‘Ulamaa.
Idadi Za Aayah: 19
Jina La Suwrah: Al-Infitwaar
Suwrah imeitwa Al-Infitwaar (Kupasukapasuka), na yanayodalilisha ni kutajwa Hadiyth iliyonukuliwa katika Faida, na kutajwa katika Aayah namba (1).
Miongoni Mwa Makusudio Ya Suwrah:
1-Kumtahadharisha mwanaadam kutodanganyika, na kuisahau Siku ya Qiyaamah. [Al-Mukhtaswar Fiy Tafsiyr Al-Qur-aan Al-Kariym]
2-Kuthibitisha kufufuliwa, na kubainisha vitisho vya Siku ya Qiyaamah, na kuwazindua watu kujiandaa nayo.
Miongoni Mwa Maudhui Ya Suwrah:
1-Suwrah imefunguliwa kwa kutajwa yatakayotokea Siku ya Qiyaamah, yenye kushtua nyoyo, kama mbingu kupasukapasuka, sayari kuanguka na kutawanyika, bahari kupasuliwa, makaburi kupinduliwa chini juu. Kisha ikafuatia kubainishwa kwamba kila mtu atajua siku hiyo aliyoyatanguliza na aliyoyachelewesha.
2-Kisha kafiri anayekanusha kufufuliwa na kuhesabiwa, anaulizwa ni kipi kilichomfanya ahadaike na aghurike kuhusu Rabb wake, Mpaji, Mwenye Kheri nyingi na Anayestahiki kushukuriwa na kutiiwa? Rabb Ambaye Amemuumba Akamsawazisha umbo, sura na viungo na Akamrekebisha ili aweza kutekeleza nyadhifa zake.?
3-Imebainishwa kwamba matendo ya mwanaadam yamewakilishwa kwa Malaika watukufu wenye kuyaandika.
4-Imebainishwa wema na waovu na malipo yao; wema wataingizwa Jannah waneemeke humo kwa kila aina za neema. Waovu wataingizwa motoni kuadhibiwa.
5-Suwrah imekhitimishwa kwa kujulishwa kwamba Siku ya Qiyaamah, hakuna kusaidiana au kunufaishana, na Amri zote Siku hiyo ni za Allaah Pekee na hakuna wa kushindana Naye.
Faida:
Anayetaka Kuitazama Siku Ya Qiyaamah, Asome Suwrah hii:
عَنْ عَبْدِ الرَّحْمَنِ، وَهُوَ ابْنُ يَزِيدَ الصَّنْعَانِيُّ قَالَ سَمِعْتُ ابْنَ عُمَرَ، يَقُولُ قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم " مَنْ سَرَّهُ أَنْ يَنْظُرَ إِلَى يَوْمِ الْقِيَامَةِ كَأَنَّهُ رَأْىُ عَيْنٍ فَلْيَقْرَأْ إِذَا الشَّمْسُ كُوِّرَتْ ) و (إِذَا السَّمَاءُ انْفَطَرَتْ ) وَ (إذَا السَّمَاءُ انْشَقَّتْ " . هَذَا حَدِيثٌ حَسَنٌ غَرِيبٌ
Amesimulia ‘Abdur-Rahmaan naye ni Ibn Yaziyd Asw-Swan’aaniyy (رضي الله عنه): Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Mwenye kutaka kuitazama Siku ya Qiyaamah, kana kwamba anaiona kwa jicho hili, basi na asome:
إِذَا الشَّمْسُ كُوِّرَتْ ﴿١﴾
“Jua litakapokunjwa kunjwa na kupotea mwanga wake.” [At-Takwiyr (81)]
إِذَا السَّمَاءُ انفَطَرَتْ ﴿١﴾
“Mbingu itakapopasuka.” [Al-Infitwaar (82)]
إِذَا السَّمَاءُ انشَقَّتْ ﴿١﴾
“Mbingu itakaporaruka.” [Al-Inshiqaaq (84)]
[Ahmad (4806), At-Tirmidhiy (3333), amesema ni Hadiyth Hasan Ghariyb. Ameisahihisha Al-Albaaniy katika Swahiyh At-Tirmidhy]
083-Al-Mutwaffifiyn: Utangulizi Wa Suwrah
Alhidaaya.com [2]
Imeteremka: Makkah au Madiynah kwani ‘Ulamaa wamekhitilafiana kuhusu wapi imeteremshwa.
Idadi Za Aayah: 36
Jina La Suwrah: Al-Mutwaffifiyn
Suwrah imeitwa Al-Mutwaffifiyn (Wanaopunja), na inayodalilisha ni kutajwa kwake katika Aayah namba (1).
Miongoni Mwa Makusudio Ya Suwrah:
1-Kuwatahadharisha wanaokadhibisha, wanaodhulumu (katika kipimo) na (yatakayowapata) Siku ya Qiyaamah, na kuwapa bishara Waumini juu hilo. [Al-Mukhtaswar Fiy Tafsiyr Al-Qur-aan Al-Kariym]
2-Kutahadharisha kupunja vipimo.
3-Kuelezea kuhusu watu waovu na watu wema na kulinganisha mafikio ya kila mmoja wao.
Miongoni Mwa Maudhui Ya Suwrah:
1-Suwrah imefunguliwa kwa onyo na ahadi ya adhabu, kwa wenye kupunja vipimo vya ujazo mezani, na kuwathibitishia Siku Tukufu ya kufufuliwa na kusimamishwa mbele ya Allaah kuhesabiwa.
2-Kimetajwa kitabu cha waovu, mafasiki, wanafiki kuwa kiko Sijjiyn, ambako ni mahali pa dhiki mno! Na imesemwa kuwa Sijjiyn ni chini ya ardhi saba ambapo ni makazi mabaya ya kudumu, waadhibiwe humo madhalimu na waovu hao kwa kukadhibisha Siku ya Malipo, na kukanusha Aayah za Allaah, kwa kudai kuwa ni hekaya za kale. Na humo ndipo walipoandikiwa wafike, na humo ndipo yalipoandikwa na kurekodiwa barabara matendo yao, na hapana kitakachozidishwa wala kupunguzwa.
3-Ikaelezewa kuwa nyoyo za hao madhalimu na wakadhibishaji zimezibwa na kufunikwa madhambi, hivyo basi hawatamuona Allaah (سبحانه وتعالى).
4-Kisha kikatajwa Kitabu cha Al-Abraar (Waumini watendao mema kwa wingi), kwamba kipo ‘Illiyyiyn (daraja za juu). Na kwamba hakizidishwi kitu humo wala hakipunguzwi. Wanayatazama yaliyomo ndani yake, Malaika waliokurubishwa. Na wakasifiwa Al-Abraar kwamba watakuwa katika Jannah yenye neema za kila aina. Nyuso zao zina mng’aro, na watanyweshwa kinywaji safi, mchanganyo wake unatokana na chemchemu iliyoko Peponi. Kinywaji hicho kinajulikana kwa ubora wake kwa jina la Tasniym. Na kinywaji hicho kimetengezewa katika vyombo kwa ustadi na mwishowe kuna harufu ya misk.
5-Imeelezewa jinsi walivyokuwa wakiwadharau Waumini na kuwafanyia dhihaka, shere na istihzai na kuwaudhi.
6-Suwrah imekhitimishwa kwa kuwabashiria Waumini ya kwamba, wao Siku ya Qiyaamah watakuwa katika hali ya juu ya taadhima. Na watawacheka makafiri kama walivyokuwa wao wakiwacheka na kuwafanyia shere walipokuwa duniani. Basi makafiri na wanafiki watalipwa malipo muwafaka na yale waliyoyafanya duniani.
084-Al-Inshiqaaq: Utangulizi Wa Suwrah
Alhidaaya.com [2]
Imeteremka: Makkah kwa itifaki ya ‘Ulamaa.
Idadi Za Aayah: 25
Jina La Suwrah: Al-Inshiqaaq
Suwrah imeitwa Al-Inshiqaaq (Kuraruka), na yanayodalilisha ni kutajwa kwake katika Hadiyth iliyonukuliwa katika Faida, na kutajwa kwake katika Aayah namba (1).
Miongoni Mwa Makusudio Ya Suwrah:
1-Kumkumbusha mwanaadam kurejea kwake kwa Rabb wake, na kubainisha udhaifu wake na kubadilika kwa hali zake. [Al-Mukhtaswar Fiy Tafsiyr Al-Qur-aan Al-Kariym]
2-Wasifu wa Siku ya Qiyaamah na hali za watu ndani yake.
Miongoni Mwa Maudhui Ya Suwrah:
1-Suwrah imefunguliwa kwa kutajwa yatakayotokea Siku ya Qiyaamah, yenye kushtua nyoyo, Siku ambayo kila kitu kitatii Amri za Allaah Atakapoamrisha mbingu kuchanika, ardhi kutandazwa na kutolewa watu makaburini. Kisha akajulishwa binaadam kwamba, bila shaka atakutana na Rabb wake alipwe malipo yanayolingana na amali zake; njema au mbaya.
2-Imeelezewa watu watakaopokea Kitabu chao mkono wa kulia, ambao ni Waumini waliomcha Allaah na wakatenda mema, kwamba watahesabiwa hesabu nyepesi, kisha watawageukia ahli zao kwa furaha. Ama watu watakaopewa kitabu chao nyuma ya migongo yao ambao ni makafiri, hawa watapata maangamizi na wataingizwa motoni kwa kufru na kukadhibisha kwao Risala ya Allaah, na kutokuamini kufufuliwa.
3-Kisha kikatajwa Kiapo cha Allaah (سبحانه وتعالى) Kuapia wekundu wa mbingu baada ya Magharibi, na Kuapia mwezi unapokamilika ukatoa mwangaza wake. Kisha jibu la kiapo ni kuwatambulisha wanaadam kwamba, bila shaka watapitia hali tofauti za maisha yao, ikianzia kuumbwa kwao kwa tone la manii mpaka kuzaliwa, kuishi kwao duniani mpaka kufa na mpaka kufufuliwa.
4-Wakaulizwa makafiri ni kitu gani kinachowazuia kumwamini Allaah (سبحانه وتعالى) baada ya Aayah Zake kufafanuliwa kwao? Na kwamba wanaposomewa Qur-aan hawanyenyekei na hawajisalimishi kwa Allaah (سبحانه وتعالى) kutii amri Zake na Makatazo Yake, na kumsujudia. Na kwamba Allaah ni Mjuzi zaidi wa ukaidi wao wanaouficha kwenye nyoyo zao, hali wao wanajua kuwa yaliyoletwa na Qur-aan ni haqq (kweli).
5-Suwrah imekhitimishwa kwa kubashiriwa makafiri adhabu kali, na Waumini waliotenda mema wamebashiriwa kwa ujira usiokatika wala kupunguka.
Fadhila Za Suwrah:
Kuweko Sajdah At-Tilaawah (Sijda ya Kisomo) Ndani Ya Suwrah:
عَنْ أَبِي سَلَمَةَ، قَالَ رَأَيْتُ أَبَا هُرَيْرَةَ ـ رضى الله عنه ـ قَرَأَ إِذَا السَّمَاءُ انْشَقَّتْ فَسَجَدَ بِهَا فَقُلْتُ يَا أَبَا هُرَيْرَةَ، أَلَمْ أَرَكَ تَسْجُدُ قَالَ لَوْ لَمْ أَرَ النَّبِيَّ صلى الله عليه وسلم يَسْجُدُ لَمْ أَسْجُدْ.
Amesimulia Abu Salamah (رضي الله عنه): Nilimuona Abu Hurayrah (رضي الله عنه) akiisoma
إِذَا السَّمَاءُ انشَقَّتْ ﴿١﴾
“Mbingu zitakaporaruka.” [Al-Inshiqaaq (84)]
Akasujudu wakati alipokuwa akiisoma. Nikamuuliza Abu Hurayrah: Je, Sijakuona ukisujudu? Abu Hurayrah akajibu: “Ningekuwa sikumuona Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) anasujudu, nami nisingesujudu.” [Al-Bukhaariy]
Faida:
Anayetaka Kuitazama Siku Ya Qiyaamah, Asome Suwrah hii:
عَنْ عَبْدِ الرَّحْمَنِ، وَهُوَ ابْنُ يَزِيدَ الصَّنْعَانِيُّ قَالَ سَمِعْتُ ابْنَ عُمَرَ، يَقُولُ قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم " مَنْ سَرَّهُ أَنْ يَنْظُرَ إِلَى يَوْمِ الْقِيَامَةِ كَأَنَّهُ رَأْىُ عَيْنٍ فَلْيَقْرَأْ إِذَا الشَّمْسُ كُوِّرَتْ ) و (إِذَا السَّمَاءُ انْفَطَرَتْ ) وَ (إذَا السَّمَاءُ انْشَقَّتْ " . هَذَا حَدِيثٌ حَسَنٌ غَرِيبٌ
Amesimulia ‘Abdur-Rahmaan naye ni Ibn Yaziya Asw-Swan’aaniyy (رضي الله عنه): Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Mwenye kutaka kuitazama Siku ya Qiyaamah, kana kwamba anaiona kwa jicho hili, basi na asome:
إِذَا الشَّمْسُ كُوِّرَتْ ﴿١﴾
“Jua litakapokunjwa kunjwa na kupotea mwanga wake.” [At-Takwiyr (81)]
إِذَا السَّمَاءُ انفَطَرَتْ ﴿١﴾
“Mbingu itakapopasuka.” [Al-Infitwaar (82)]
إِذَا السَّمَاءُ انشَقَّتْ ﴿١﴾
“Mbingu itakaporaruka.” [Al-Inshiqaaq (84)]
[Ahmad (4806), At-Tirmidhiy (3333), amesema ni Hadiyth Hasan Ghariyb. Ameisahihisha Al-Albaaniy katika Swahiyh At-Tirmidhy]
085-Al-Buruwj: Utangulizi Wa Suwrah
Alhidaaya.com [2]
Imeteremka: Makkah kwa itifaki ya ‘Ulamaa.
Idadi Za Aayah: 22
Jina La Suwrah: Al-Buruwj (Buruji), na inayodalilisha ni kutajwa katika Aayah namba (1).
Miongoni Mwa Makusudio Ya Suwrah:
1-Kubainisha Nguvu za Allaah (سبحانه وتعالى) Zilizozunguka kila kitu, na Nusra Yake kwa Vipenzi Vyake na Mkamato Wake wa kuwaadhibu maadui Wake. [Al-Mukhtaswar Fiy Tafsiyr Al-Qur-aan Al-Kariym]
2-Kumliwaza Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) na Swahaba wake kwa yale yaliyawapata kutoka kwa maadui zao, na kuwafanya Waumini wathibitike katika haqq.
Miongoni Mwa Maudhui Ya Suwrah:
1-Suwrah imefunguliwa kwa Kiapo cha Allaah (سبحانه وتعالى) Kuapia mbingu na buruji. Na kwa Siku ya Qiyaamah Aliyoahidi kuwafufua na kuwakusanya viumbe wahesabiwe. Na kwa kila mwenye kushuhudia na anayeshuhudiwa. Ikafuatia jambo linalohakikishwa kiapo kwamba, wamelaaniwa na wameangamia watu wa mahandaki waliowatesa Waumini kwa kuwaingiza katika shimo kubwa lilowashwa moto kwa kuni nyingi, huku wakiwatazama wanavyoadhibika. Na mateso hayo waliyoteswa Waumini ni kwa sababu washirikina hao wa mahandaki, waliwalazimisha warudi katika dini yao wamshirikishe Allaah, lakini Waumini walikataa kabisa kwa kuwa walithibitika katika Tawhiyd ya Allaah (سبحانه وتعالى) wakamwamini.
3-Wameahidiwa wenye kuchupa mipaka ambao wanawafitini Waumini, kwamba watapata adhabu ya Jahannam.
4-Waumini wenye kutenda mema, wamebashiriwa kuingizwa Jannah zenye neema, na hawa ndio waliofaulu.
5-Imeashiriwa Adhabu kali ya Allaah (سبحانه وتعالى), na ikathibitishwa Tawhiyd Yake ya Ar-Rubuwbiyyah (Uola, Uumbaji, Uhuishaji na Ufishaji) na Sifa Zake nyenginezo Kamilifu, na Umiliki Wake wa ‘Arsh Tukufu, na Uwezo Wake wa Kufanya Atakalo, wala hakuna anayeweza kuzuia jambo Alitakalo Allaah (سبحانه وتعالى), bali Anaposema Kun! (Kuwa), basi jambo linakuwa!
6-Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) ameliwazwa kwa kupigiwa mfano wa watu wa Firawni na Thamuwd, ambao waliokufuru na kukanusha Risala ya Allaah (سبحانه وتعالى) kupitia Rusuli Wake ya kwamba, Allaah (سبحانه وتعالى) Aliwazunguka kwa Ujuzi Wake na Uwezo Wake Kuwaadhibu na kuwaangamiza.
7-Suwrah imekhitimishwa kwa kuendelea kumliwaza Nabiy Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم) kwa kuitukuza na kuisifu Qur-aan aliyoteremshiwa, kwamba Qur-aan hii si kama wanavyodai washirikina kuwa ni mashairi na uchawi hivyo wakaikanusha, na kwamba Qur-aan hii iko katika Al-Lawh Al-Mahfuwdhw (Ubao Uliohifadhiwa) haiwezi kubadilishwa au kupotoshwa.
Faida:
عَنْ جَابِرِ بْنِ سَمُرَةَ، أَنَّ النَّبِيَّ صلى الله عليه وسلم كَانَ يَقْرَأُ فِي الظُّهْرِ وَالْعَصْرِ بِالسَّمَاءِ ذَاتِ الْبُرُوجِ وَالسَّمَاءِ وَالطَّارِقِ وَنَحْوِهِمَا .
Amesimulia Jaabir Bin Samrah (رضي الله عنه): Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alikuwa akisoma katika Swalaah ya Adhuhuri na Alasiri:
وَالسَّمَاءِ ذَاتِ الْبُرُوجِ ﴿١﴾
“Naapa kwa mbingu yenye buruji.” [Al-Buruwj (85)]
Na
وَالسَّمَاءِ وَالطَّارِقِ ﴿١﴾
“Naapa kwa mbingu na kinachogonga kinapotoka usiku.” [Atw-Twaariq (86)]
Na Suwrah zinazofanana kama hizo. [Hadiyth Hasan Swahiyh - At-Tirmidhiy, An-Nasaaiy, Swahiyh Abiy Daawuwd (805)]
086-Atw-Twaariq: Utangulizi Wa Suwrah
Alhidaaya.com [2]
Imeteremka: Makkah kwa itifaki ya ‘Ulamaa.
Idadi Za Aayah: 17
Jina La Suwrah: Atw-Twaariq
Suwrah imeitwa Atw-Twaariq (Kinachokuja Na Kugonga Usiku), na inayodalilisha ni kutajwa kwake katika Aayah namba (1).
Miongoni Mwa Makusudio Ya Suwrah:
1-Kubainisha Uwezo wa Allaah (سبحانه وتعالى) na kwamba Anawafahamu wanaadam wote, na Yeye Ndiye Atakayewarejesha (Kwake Siku ya Qiyaamah). [Al-Mukhtaswar Fiy Tafsiyr Al-Qur-aan Al-Kariym]
2-Kusimamisha dalili ya Uwezo wa Allaah (سبحانه وتعالى) na kuthibitisha kwamba Qur-aan inatoka Kwake na Desturi ya Allaah Kulipiza vitimbi vya makafiri na kuwaangamiza.
Miongoni Mwa Maudhui Ya Suwrah:
1-Suwrah imefunguliwa kwa Kiapo cha Allaah (سبحانه وتعالى) Kuapia mbingu na nyota inayogonga inapotoka usiku. Ikafuatia jambo linalohakikishwa kiapo, kwamba kila mtu amewakilishwa Malaika mwenye kuchunguza na kusajili amali zake njema na ovu ili ahesabiwe Siku ya Qiyaamah.
2-Wamekumbushwa wanaokanusha kufufuliwa wajitazame na wazingatie wameumbwa na nini, ili wajue kwamba Aliyewaumba kwa manii, ni Mweza wa kuwarudisha katika umbo lao mara ya pili, Siku ya Qiyaamah, Siku ambayo siri zote zitafichuliwa wazi.
3-Kisha Allaah (سبحانه وتعالى) Akaapia kwa mbingu yenye mvua ya kurudiarudia kunyesha. Na kwa ardhi yenye mpasuko za kufanya mimea ichipuke. Kisha Allaah Akahakikisha jambo Analoapia ambalo ni kuthitibisha kuwa Qur-aan ni kauli zinazopambanua haki na baatwil, na kwamba wala si upuuzi.
4-Suwrah imekhitimishwa kwa kuwatishia washirikina wanaofanya vitimbi vya kupinga haqq (haki) na kutilia nguvu baatwil, kwamba Allaah (سبحانه وتعالى) Analipiza vitimbi vyao, basi Anamliwaza Rasuli Wake (صلى الله عليه وآله وسلم) awape muhula washirikina, kwani atakuja kuona adhabu na maangamizi watakayoyapata.
Faida:
عَنْ جَابِرِ بْنِ سَمُرَةَ، أَنَّ النَّبِيَّ صلى الله عليه وسلم كَانَ يَقْرَأُ فِي الظُّهْرِ وَالْعَصْرِ بِالسَّمَاءِ ذَاتِ الْبُرُوجِ وَالسَّمَاءِ وَالطَّارِقِ وَنَحْوِهِمَا .
Amesimulia Jaabir Bin Samrah (رضي الله عنه): Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alikuwa akisoma katika Swalaah ya Adhuhuri na Alasiri:
وَالسَّمَاءِ ذَاتِ الْبُرُوجِ ﴿١﴾
“Naapa kwa mbingu yenye buruji.” [Al-Buruwj (85)]
Na
وَالسَّمَاءِ وَالطَّارِقِ ﴿١﴾
“Naapa kwa mbingu na kinachogonga kinapotoka usiku.” [Atw-Twaariq (86)]
Na Suwrah zinazofanana kama hizo. [Hadiyth Hasan Swahiyh - At-Tirmidhiy, An-Nasaaiy, Swahiyh Abiy Daawuwd (805)]
087-Al-A’laa: Utangulizi Wa Suwrah
Alhidaaya.com [2]
Imeteremka: Makkah kwa itifaki ya ‘Ulamaa.
Idadi Za Aayah: 19
Jina La Suwrah: Al-A’laa
Suwrah imeitwa Al-A’laa (Mwenye ‘Uluwa Aliyetukuka), na yanayodalilisha ni kutajwa kwake katika Hadiyth zilizonukuliwa kwenye Fadhila, na kutajwa kwake katika Aayah namba (1).
Miongoni Mwa Makusudio Ya Suwrah:
1-Kuikumbusha nafsi (hali ya) maisha ya Aakhirah na kule kukatika kwake na kila jambo la kidunia. [Al-Mukhtaswar Fiy Tafsiyr Al-Qur-aan Al-Kariym]
2-Kudhihirisha wingi wa Neema za Allaah (سبحانه وتعالى) ambazo haiwezekani kuziorodhesha hesabuni.
Miongoni Mwa Maudhui Ya Suwrah:
1-Suwrah imefunguliwa kwa kutakasa Jina la Allaah Mwenye ‘Uluwa na ‘Uadhwama, Yuko juu kabisa ya viumbe Vyake na kila kitu, Yu Pekee Hana mshirika na Ametakasika na kila sifa pungufu (سبحانه وتعالى).
2-Imethibitishwa Tawhiyd ya Allaah ya Ar-Rubuwbiyyah (Uola, Uumbaji, Uendeshaji, Uongozaji na kadhaalika) .
3-Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) amebashiriwa bishara kubwa kutoka kwa Allaah (سبحانه وتعالى), kwamba pindi Atakapoteremshiwa Qur-aan na akafanywa aisome, basi Allaah (سبحانه وتعالى) Ataihifadhisha moyoni mwake ili ithibitike vizuri, basi hatoweza kusahau chochote. Na amebashiriwa pia kusahilishiwa mambo yake yote, yakiwemo majukumu ya Urasuli. Na pia amebashiriwa kusahilishiwa Sharia za Dini hii Tukufu.
4-Allaah (سبحانه وتعالى) Anamuamrisha Rasuli Wake (صلى الله عليه وآله وسلم) awakumbushe watu mawaidha. Na kwamba aendelee kuwakumbusha madhali watayasikiliza na kunufaika nayo. Basi hawa ni Waumini wenye kumtii na kumcha Allaah. Na hawa ndio watakaojaaliwa kuhidika, na ndio watakaofaulu kutokana na kuzitakasa nafsi zao. Na kuna watakapoupinga kwa kutokumkhofu Allaah. Basi hawa ni wapotofu, na hatima yao itakuwa ni kuingizwa motoni.
5-Wamekemewa watu wanaokhiyari na kupendelea maisha ya dunia kutokana na starehe zake. Lakini starehe za dunia hazidumu milele, bali ni za muda mfupi tu. Ama maisha ya Aakhirah ndiyo yenye starehe na neema tele. Na maisha haya, ndio yenye kudumu milele.
5-Suwrah imekhitimishwa kwa kukumbushwa kwamba waliyokumbushwa katika Suwrah hii tukufu, yametajwa pia katika Suhuf (Maandiko Matukufu) zilizotangulia kabla ya Qur-aan na Suhuf za Ibraahiym na Muwsaa (عليهما السلام).
Fadhila Za Suwrah:
1-Ni Sunnah Kuisoma Suwrah Hii Katika Swalaah Ya Ijumaa Na ‘Iyd Mbili:
عَن النُّعْمَانِ بْنِ بَشِيرٍ، قَالَ كَانَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم يَقْرَأُ فِي الْجُمُعَةِ وَالْعِيدِ بِـ { سَبِّحِ اسْمَ رَبِّكَ الأَعْلَى } وَ { هَلْ أَتَاكَ حَدِيثُ الْغَاشِيَةِ } وَإِذَا اجْتَمَعَ الْجُمُعَةُ وَالْعِيدُ فِي يَوْمٍ قَرَأَ بِهِمَا .
Amesimulia Nu’maan Bin Bashiyr (رضي الله عنه): Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alikuwa akisoma
سَبِّحِ اسْمَ رَبِّكَ الأَعْلَى
[Al-A’laa (87)]
Na
هَلْ أَتَاكَ حَدِيثُ الْغَاشِيَةِ
[Al-Ghaashiyah (88)]
Katika Rakaa ya kwanza ya Swalaah ya Ijuma. Na inapojumuika Ijumaa na ‘Iyd katika siku moja, alizisoma pia (Suwrah hizo). [Muslim, An- Nasaaiy, Abuu Daawuwd]
2-Ni Sunnah Kuisoma Katika Swalaah Ya Witr:
عَنْ سَعِيدِ بْنِ عَبْدِ الرَّحْمَنِ بْنِ أَبْزَى، عَنْ أَبِيهِ، عَنْ أُبَىِّ بْنِ كَعْبٍ، قَالَ كَانَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم يَقْرَأُ فِي الرَّكْعَةِ الأُولَى مِنَ الْوَتْرِ بِـ { سَبِّحِ اسْمَ رَبِّكَ الأَعْلَى } وَفِي الثَّانِيَةِ بِـ { قُلْ يَا أَيُّهَا الْكَافِرُونَ } وَفِي الثَّالِثَةِ بِـ { قُلْ هُوَ اللَّهُ أَحَدٌ }
Amesimulia Ubayy Bin Ka’ba (رضي الله عنه): Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alikuwa akisoma katika Rakaah ya kwanza ya Swalaah ya Witr:
سَبِّحِ اسْمَ رَبِّكَ الأَعْلَى
[Al-A’laa (87)]
Na katika ya pili:
قُلْ يَا أَيُّهَا الْكَافِرُونَ
[Al-Kaafiruwn (109)]
Na katika ya tatu:
قُلْ هُوَ اللَّهُ أَحَدٌ
[Al-Ikhlaasw (112)]
[At-Tirmidhiy, An-Nasaaiy, na ameisahihisha Al-Albaaniy katika Swahiyh An-Nasaaiy]
088-Al-Ghaashiyah: Utangulizi Wa Suwrah
Alhidaaya.com [2]
Imeteremka: Makkah kwa itifaki ya ‘Ulamaa
Idadi Za Aayah: 26
Jina La Suwrah: Al-Ghaashiyah.
Suwrah imeitwa Al-Ghaashiyah (Kufunikiza Na Kutoa Fahamu), na inayodalilisha ni kutajwa kwake katika Hadiyth iliyonukuliwa kwenye Fadhila, na kutajwa kwake katika Aayah namba (1).
Miongoni Mwa Makusudio Ya Suwrah:
1-Kuwakumbusha wanaadam kuhusu Aakhirah na mambo yaliyopo huko ya thawabu na adhabu, na kuangalia dalili zinazoonyesha Uwezo wa Allaah. [Al-Mukhtaswar Fiy Tafsiyr Al-Qur-aan Al-Kariym]
2-Kubainisha hali za makafiri na Waumini Siku ya Qiyaamah.
Miongoni Mwa Maudhui Ya Suwrah:
1-Suwrah imefunguliwa kwa kuelezea habari za Siku ya Qiyaamah, Siku ambayo itawafunikiza watu, fahamu ziwatoke.
2-Kisha ikafuatia kuelezea hali za makafiri kwamba, nyuso zao zitadhalilika, watakuwa wametaabika na kuchoka, na wataingizwa motoni ambako watanyweshwa maji ya moto yatokotayo. Hawatakuwa na chakula isipokuwa kinachotokana na miba, kichungu mno! Chakula hicho hakimnoneshi mwenye kukila wala hakimuondolei mtu njaa.
3-Kisha ikaelezewa hali za Waumini kwamba, Siku hiyo nyuso zao zitakuwa zenye kuneemeka, zitafarijika kwa kutokana na kuamini kwao Aakhirah na kuridhika, wakafanya juhudi duniani na kutenda mema. Basi watakuwa katika Jannah za daraja ya juu ambako hawatasikia upuuzi, na wataneemeshwa kwa kila aina za neema na starehe.
4-Imethibitishwa Tawhyid ya Allaah ya Ar-Rubuwbiyyah (Uola, Uumbaji na kadhalika) na Uwezo Wake Allaah (سبحانه وتعالى) wa Kuumba na Kuunda kwa hikma viumbe, kama vile jinsi Alivyomuumba ngamia kwa muujiza, mnyama ambaye ana faida na hadhi kubwa kwa wanaadam. Basi washirikina wakatanabahishwa wamwangalie na wazingatie kwa kina mwili wake wote, ambao kila sehemu ya mwili wake una muujiza. Na kwamba mnyama huyu wa ajabu, ana manufaa makubwa kwa wanaadam katika maisha yao, kama vile katika biashara zao, na safari zao. Hivyo basi kuna ishara na dalili za wazi kabisa zenye kuthibitisha Tawhiyd ya Allaah, kwamba ni Yeye Pekee Muumbaji wa viumbe na ulimwengu na yaliyomo ndani yake. Basi na watanabahi pia mengineyo ya Uumbaji wa Allaah kama mbingu, majabali na ardhi.
5-Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) anaamrishwa akumbushe watu awawaidhi, na wanaokengeuka na kukufuru, wametishiwa adhabu kubwa ya Allaah.
6-Suwrah imekhitimishwa kwa kuthibitishwa kufufuliwa viumbe na kuhesabiwa matendo.
Fadhila Za Suwrah:
Ni Sunnah Kuisoma Suwrah Hii Katika Swalaah Ya Ijumaa Na ‘Iyd Mbili:
عَن النُّعْمَانِ بْنِ بَشِيرٍ، قَالَ كَانَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم يَقْرَأُ فِي الْجُمُعَةِ وَالْعِيدِ بِـ { سَبِّحِ اسْمَ رَبِّكَ الأَعْلَى } وَ { هَلْ أَتَاكَ حَدِيثُ الْغَاشِيَةِ } وَإِذَا اجْتَمَعَ الْجُمُعَةُ وَالْعِيدُ فِي يَوْمٍ قَرَأَ بِهِمَا .
Amesimulia Nu’maan Bin Bashiyr (رضي الله عنه): Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alikuwa akisoma
سَبِّحِ اسْمَ رَبِّكَ الأَعْلَى
Na
هَلْ أَتَاكَ حَدِيثُ الْغَاشِيَةِ
Katika Rakaa ya kwanza ya Swalaah ya Ijuma. Na inapojumuika Ijumaa na ‘Iyd katika siku moja, alizisoma pia (Suwrah hizo). [Muslim, An- Nasaaiy, Abuu Daawuwd]
089-Al-Fajr: Utangulizi Wa Suwrah
Alhidaaya.com [2]
Imeteremka: Makkah kwa itifaki ya ‘Ulamaa.
Idadi Za Aayah: 30
Jina La Suwrah: Al-Fajr
Suwrah imeitwa Al-Fajr (Alfajiri), na inayodalilisha ni kutajwa kwake katika Aayah namba (1)
Miongoni Mwa Makusudio Ya Suwrah:
1-Kubainisha mwisho wa waovu, na hikma ya kuletwa mitihani, na kuwakumbusha Aakhirah. [Al-Mukhtaswar Fiy Tafsiyr Al-Qur-aan Al-Kariym]
2-Kumthibitisha na kumtia nguvu Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم).
2-Kuthibitisha Al-Aakhirah (Siku ya Mwisho) na kuhesabiwa kwa malipo ya motoni au kuingizwa Jannah.
Miongoni Mwa Maudhui Ya Suwrah:
1-Suwrah imefunguliwa kwa Kiapo cha Allaah (سبحانه وتعالى) Kuapia Alfajiri, na masiku kumi ya mwanzo wa mwezi wa Dhul-Hijjah, ambayo ni masiku bora kabisa ya Allaah. Akaendelea Allaah (سبحانه وتعالى) Kuapia kwa shufwa (idadi inayogawanyika kama mbili, nne, sita n.k). Na witr (idadi pweke isiyogawanyika kama moja, tatu, tano n.k). Na kwa usiku unapopita na giza lake. Ikafuatia uhakikisho wa kiapo ambao ni adhabu na maangamizo yaliyowapata kina ‘Aad ambao ni kaumu ya Nabiy Huwd (عليه السّلام). Hawa waliumbwa kwa umbo kubwa la nguvu, na hawakuumbwa mfano wao katika ardhi. Na wakatajwa kina Thamwud ambao ni kaumu ya Nabiy Swaalih (عليه السّلام) waliojaaliwa uwezo wa kuchonga jabali na kufanya nyumba ndani yake. Na Firawni aliyekuwa na askari waliouhami ufalme wake na kuutilia nguvu. Basi hao wote waliotajwa, walivuka mipaka wakawakanusha Rusuli wao na wakafanya ufisadi katika ardhi, basi Allaah (سبحانه وتعالى) Akawaangamiza kwa adhabu kali kabisa.
2-Imebainishwa hali ya binaadam asiye na shukurani kwamba, pindi Allaah (سبحانه وتعالى) Anapomkunjuliwa riziki hujivuna. Na Anapomjaribu kwa kumdhikisha rizki, basi hughalifika na kulalamika kuwa kadhalilishwa.
3-Wamekemewa wanaadam kama hao, kwa kutokuwakirimu mayatima na kutowatendea wema, wala hawafanyi hima kulisha masikini, na kula kwao mali za kurithi bila ya haki, na kupenda kwao mali kupita kiasi.
4-Wamekumbushwa watu vitisho vya Siku ya Qiyaamah, na matukio yake kama kuteremka Malaika na Kuteremka Allaah (سبحانه وتعالى), Mteremko unaolingana na Utukufu Wake, ili Awahesabie viumbe matendo yao na kuwalipa; ima waingizwe motoni au Jannah. Na watu wa motoni siku hiyo watadhihirisha majuto yao ya kutaka kutubia na kutamani kurudi duniani!
5-Suwrah imekhitimishwa kuwabashiria wenye nafsi zilizotulia kwamba wataridhika na Allaah, na Allaah Atawaradhia, na wataambiwa waingie katika Jannah ya Allaah (سبحانه وتعالى).
090-Al-Balad: Utangulizi Wa Suwrah
Alhidaaya.com [2]
Imeteremka: Makkah kwa itifaki ya ‘Ulamaa.
Idadi Za Aayah: 20
Jina La Suwrah: Al-Balad
Suwrah imeitwa Al-Balad (Mji), na inayodalilisha ni kutajwa kwake katika Aayah namba (1).
Miongoni Mwa Makusudio Ya Suwrah:
1-Kubainisha kuhitajia kwa mwanaadam, na kubainisha vitimbi vyake, na njia za kuokoka kwake. [Al-Mukhtaswar Fiy Tafsiyr Al-Qur-aan Al-Kariym]
2-Kutaja maumbile ya dunia na kile anachosumbuka nacho mwanaadam ndani yake katika kuvumilia kubeba shida, na kile kinachompeleka katika furaha.
Miongoni Mwa Maudhui Ya Suwrah:
1-Suwrah imefunguliwa kwa Kiapo cha Allaah (سبحانه وتعالى) Kuapia Al-Balad (Mji) ukikusudiwa mji Mtukufu wa Makkah na kuishi kwake Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) humo akiuzidisha Utukufu wake. Na kuapia kwa mzazi wa wanaadam (Aadam) na kilichozalikana naye (wanaadam). Kisha ikahakikishwa jambo linaloapiwa, nalo ni kuumbwa binaadam katika mashaka na tabu za kilimwengu, tokea mwanzo wa kuzaliwa kwake, kuishi kwake duniani, katika maisha yake ya Al-Barzakh baada ya kufariki, na atakapofufuliwa Siku ya Qiyaamah.
2-Imetajwa ubaya wa binaadam kudanganyika kwa nguvu alizonazo na mali, akafanya kiburi na kujivuna na kuvuka mipaka kuitumia mali kwa matamanio yake, akadhania kwamba hakuna awezaye kumdhalilisha, na akadhania kwa matendo yake hayo, kwamba Allaah (سبحانه وتعالى) Hamuoni wala Hatamhesabu juu ya matendo makubwa na madogo. Bali Allaah (سبحانه وتعالى) Anamuona na Amewawakilisha Malaika wanaoandika matendo yote; mema na maovu.
3-Binaadam huyo anakumbushwa Neema za Allaah (سبحانه وتعالى) Alizomjaalia aonekane mwenye sura nzuri yenye macho mawili ya kuonea, na midomo miwili ya kusemea, na kumbainishia njia mbili; ya kheri na shari itakayomwongoza ima katika hidaaya au upotovu, na ajichagulie mwenyewe aitakayo. Neema hizo kubwa zinamtaka mja azitimize haki za Allaah kwa kumshukuru na kutoa katika yanayomridhisha na sio kuzitumia kwa dhambi zake. Lakini mtu huyu hakufanya hivyo kujiepusha na janga la Aakhirah kwa kutoa mali yake kwa sababu ya kufuata matamanio yake, kama vile kukomboa Waumini kutokana na utumwa, au kulisha watu siku za njaa, na kumhudumia yatima aliye jamaa, au maskini aliye fakiri kabisa.
4-Suwrah imekhitimishwa kwa kubainisha mwisho mwema wa Waumini na makafiri. (i) Aliyekuwa miongoni mwa walioamini akatekeleza amali njema zilizotajwa juu, akaijenga imaan yake, akamtii Allaah na kufuata Amri Zake, akausiana na wenziwe katika kuvuta subira na kuusiana kuwahurumia viumbe na kuwatimizia haki zao. Hawa ndio watu wa kheri watakaopelekewa upande wa kulia kuelekea Peponi. (ii) Makafiri ambao hawakumwamini Allaah wala hawakutenda mema, wala hawakuwahurumia na kuwapa haki zao waja wa Allaah, bali walikanusha Aayaat, Ishara na Dalili za Allaah. Basi hawa watapelekwa upande kwa kushoto kuelekezwa katika Jahannam itakayowafunika na kuwaziba.
091-Ash-Shams: Utangulizi Wa Suwrah
Alhidaaya.com [2]
Imeteremka: Makkah kwa itifaki ya ‘Ulamaa.
Idadi Za Aayah: 15
Jina La Suwrah: Ash-Shams
Suwrah imeitwa Ash-Shams (Jua), na inayodalilisha ni kutajwa kwake katika Aayah namba (1).
Miongoni Mwa Makusudio Ya Suwrah:
1-Msisitizo juu ya sehemu ndefu zaidi ya Qur-aan inayozungumzia juu ya kuadhimisha na kuitakasa nafsi na hasara ya kuifisidi kwa kutenda maasi. [Al-Mukhtaswar Fiy Tafsiyr Al-Qur-aan Al-Kariym]
1-Kuhamasisha utiifu na kutahadharisha maasi.
2-Kuwatishia washirikina adhabu kama zilizowapata walio kabla yao.
Miongoni Mwa Maudhui Ya Suwrah:
1-Suwrah imefunguliwa kwa Kiapo cha Allaah (سبحانه وتعالى) Kuapia jua na mwangaza wake baada ya kuchomoza kwake asubuhi. Na Kuapia kwa mwezi unapolifuata jua likawa nyuma yake na kutoa mwangaza baada ya kuchwa jua. Na Kuapia kwa mchana unapodhihirisha jua waziwazi bila kufichikana. Na Kuapia kwa usiku unapofunika jua, ardhi ikawa giza. Na Kuapia kwa mbingu na kujengeka kwake imara. Na Kuapia kwa ardhi na kutandikika kwake ikawa kama tandiko wakaweza kuishi viumbe humo. Na Kuapia kwa nafsi Aliyoikamilisha umbo lake ili itekeleze kazi iliyoumbiwa nayo. Kisha Akaibanishia njia ya shari na njia ya kheri. Kisha yakatajwa yanayohakikishiwa kiapo, nayo ni kubainisha kufaulu kwa nafsi na kula khasara. Aliyefaulu ni mwenye kuitakasa nafsi kwa utiifu na matendo mema. Na aliyekula khasara ni mwenye kuitia nafsi katika maasi na kutokufanya matendo mema
2-Suwrah imekhitimishwa kuwatishia washirikina ya kwamba, itawapata adhabu na maangamizi kama ilivyowapata kina Thamuwd, pindi watakapoendelea katika ukafiri wao. Ikatajwa sehemu ya kisa cha kina Thamuwd waliokadhibisha Risala ya Allaah (سبحانه وتعالى) kupitia Rasuli wao Swaalih (عليه السّلام), na jinsi walivyovuka mipaka kuasi amri za Allaah, kwani pindi walipotaka waletewe muujiza ambao utawaonyesha ukweli wa Rasuli wao, Allaah Akawatolea ngamia jike kutoka katika jabali. Wakaamrishwa na Rasuli wao kwamba, huyo ni ngamia wa Allaah wasimguse kwa uovu, na wafanye zamu katika kinywaji; siku moja anywe ngamia, na siku moja wateke maji na wanywe wao. Lakini hilo lilikuwa zito kwao. Wakamkanusha Rasuli wao, na wakapuuza amri hizo, na mwishowe wakamchinja ngamia wa Allaah. Basi Allaah (سبحانه وتعالى) Akawaadhibu na kuwaangamiza kwa kuwatumia ukelele mkali, na tetemeko la ardhi, wakafariki wa kuanguka kifudifudi majumbani mwao. Na Akazibomoa nyumba zao na Kuzisawazisha na ardhi.
092-Al-Layl: Utangulizi Wa Suwrah
Alhidaaya.com [2]
Imeteremka: Makkah kwa itifaki ya ‘Ulamaa.
Idadi Za Aayah: 21
Jina La Suwrah: Al-Layl
Suwrah imeitwa Al-Layl (Usiku), na inayodalilisha ni kutajwa kwake katika Aayah namba (1).
Miongoni Mwa Makusudio Ya Suwrah:
1-Kubainisha hali ya viumbe katika imaan na kutoa (mali kwa ajili ya Allaah) na hali ya kila kundi. [Al-Mukhtaswar Fiy Tafsiyr Al-Qur-aan Al-Kariym]
2-Kubainisha umbali kati ya hali ya Waumini na makafiri katika dunia na Aakhirah.
Miongoni Mwa Maudhui Ya Suwrah:
1-Suwrah imefunguliwa kwa Kiapo cha Allaah (سبحانه وتعالى) Kuapia usiku unapofunika ardhi kwa giza lake pamoja na vilivyomo ardhini. Na giza hilo ni manufaa kwa wanaadam kupata utulivu na kupumzika baada ya tabu za mihangaiko ya mchana. Na Kuapia mchana unapodhihiri mwangaza wake ili watu waangazwe na nuru yake, waweze kutoka nje na kutafuta wanayoyahitajia katika maisha yao. Na Kuapia kuumbwa kila kinachozaliwa kuwa viwili viwili; dume na jike katika wanaadam na wanyama. Hivi ni kutokana na Hikma Yake ili watamaniane na wanufaishane katika uhai wa dunia. Na hali kadhalika kuumbwa dume na jike katika mimea na vinginevyo. Kisha ikatajwa jambo linaloapiwa, kwamba kwa matendo ya wanaadam yametofautiana. Kuna wanaotenda ya kheri kwa ajili ya Aakhirah, na wako wanaotenda ya shari.
2-Imebainishwa Utukufu wa Muumini na fadhila za kutoa mali katika Anayoyaamrisha Allaah (سبحانه وتعالى) kama kutoa Zakaah, swadaqa, kuwapa jamaa wenye uhusiano wa damu na wahitaji wengineo. Na pia imebainishwa fadhila za kumcha Allaah, kwa kutekeleza aliyokatazwa na kujiepusha na makatazo, na kutimiza ibaada za fardhi na za Sunnah, na kuamini neno la Tawhiyd; laa ilaaha illa-Allaah. Huyu fadhila zake itakuwa ni kufanyiwa sahali mambo yake katika kumwongoza kutenda ya kheri na kumwepusha na maovu. Ama anayefanyia ubakhili mali yake asitoe katika Aliyoamrisha Allaah, na akawa hana haja na malipo Yake, na akakanusha laa ilaaha illa-Allaah, basi huyo atafanyiwa njia za kutenda maovu apate mashaka ya kudumu.
3-Wanaadam wameonywa moto wa Jahannam wenye kuwaka vikali, ambao wataingia waliokataa kumwamini na kumtii Allaah na Rasuli Wake (صلى الله عليه وآله وسلم). Na ataepushwa na moto wa Jahannam aliyemwamini na kumtii pamoja na Rasuli Wake (صلى الله عليه وآله وسلم).
4-Suwrah imekhitimishwa kwa kusifiwa Muumini anayejitakasa kwa kutoa mali yake kutaja Wajihi wa Allaah. Basi huyu atapata malipo ya kumridhisha.
093-Adhw-Dhwuhaa: Utangulizi Wa Suwrah
Alhidaaya.com [2]
Imeteremka: Makkah kwa itifaki ya ‘Ulamaa.
Idadi Za Aayah: 11
Jina La Suwrah: Adhw-Dhwuhaa
Suwrah imeitwa Adhw-Dhwuhaa (Dhuha), na inayodalilisha ni kutajwa kwake katika Aayah namba (1).
Miongoni Mwa Makusudio Ya Suwrah:
1-Kubainisha kuwa Allaah Alimlinda Nabiy Wake (صلى الله عليه وآله وسلم) kutoka mwanzo wa jambo lake hadi mwisho. [Al-Mukhtaswar Fiy Tafsiyr Al-Qur-aan Al-Kariym]
2-Kubainisha kuwa maisha ya Aakhirah ni bora kuliko ya dunia hii. Na jinsi alivyoishi Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) kama yatima na Allaah Akamtunza.
Miongoni Mwa Maudhui Ya Suwrah:
1-Suwrah imefunguliwa kwa Kiapo cha Allaah (سبحانه وتعالى) Kuapia wakati mchana jua linapopanda na kuenea mwanga wake. Na kuapia usiku unapotulia na giza lake likatanda. Ikatajwa jambo la kuhakikisha kiapo kumwambia Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) kwamba Allaah Hakumchukia kwa kuchelewesha kumteremshia Wahy.
2-Akaliwazwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) kwa kujulishwa kwamba Aakhirah kwake ni bora kuliko dunia, na kwamba Allaah Atampa yatakayomridhisha, kwani alikuwa yatima Akamtunza, na alikuwa hajui Kitabu wala imaan Akamfundisha na akaweza kufanya mema. Na Alipokuwa masikini Allaah (سبحانه وتعالى) Alimjaalia rizki na Akamfanya atosheke na awe mwenye kuvuta subira.
3-Suwrah imekhitimishwa kwa amri ya kutokumkaripia yatima, bali kumtimizia haja zake. Na pia kuhadithia Neema za Allaah (سبحانه وتعالى).
094-Ash-Sharh: Utangulizi Wa Suwrah
Alhidaaya.com [2]
Imeteremka: Makkah kwa itifaki ya ‘Ulamaa.
Idadi Za Aayah: 8
Jina La Suwrah: Ash-Sharh
Suwrah imeitwa Ash-Sharh (Kukunjua), na inayodalilisha ni kutajwa kwake katika Aayah namba (1).
Miongoni Mwa Makusudio Ya Suwrah:
1-Kuelezea neema ya Allaah (سبحانه وتعالى) kwa Nabiy (صلى الله عليه وسلم) kwa kutimiza Kwake Neema za kimaana. [Al-Mukhtaswar Fiy Tafsiyr Al-Qur-aan Al-Kariym]
2-Kubainisha Utukufu wa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) mbele ya Rabb Wake.
Miongoni Mwa Maudhui Ya Suwrah:
1-Suwrah imefunguliwa kwa kuliwazwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) kwamba Allaah (سبحانه وتعالى) Amemkunjulia kifua chake kumtia utulivu na Nuru ya Allaah ili aweze kulingania watu Sharia za Dini, na aweze kujipamba kwa khulqa njema. Na kwamba Allaah (سبحانه وتعالى) Amemuodoshea mazito yaliyoelemea mgongoni mwake Akamsahilishia mambo yake. Akalitukuza jina lake awe anasifiwa na kutajwa Jina lake katika hali nyingi: (i) Katika kutamkwa Shahada watu wanaposilimu kuingia katika Dini hii tukufu. (ii) Katika Adhana na Iqaamah na katika Khutba. (iii) Ndani ya Swalaah (iv) Na kila anapotajwa (صلى الله عليه وآله وسلم), anaombewa Rehma na amani
2-Suwrah imekhitimishwa kwa kuendelea kumliwaza Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) aimarike katika kubalighisha Risala ya Allaah, wala asirudi nyuma kwa maudhi ya maadui wake, kwani kwenye dhiki kuna faraja. Na akaamrishwa ajitahidi katika ibaada na duaa anapomaliza mambo yake ya kidunia.
095-At-Tiyn: Utangulizi Wa Suwrah
Alhidaaya.com [2]
Imeteremka: Makkah kwa itifaki ya ‘Ulamaa.
Idadi Za Aayah: 8
Jina La Suwrah: At-Tiyn
Suwrah imeitwa At-Tiyn (Tini), na inayodalilisha ni kutajwa kwake katika Hadiyth iliyonukuliwa katika Fadhila na Faida, na kutajwa katika Aayah namba (1).
Miongoni Mwa Makusudio Ya Suwrah:
1-Allaah (سبحانه وتعالى) Kuwaneemesha wanaadam kwa kuwafanya wawe na tabia na maumbile yaliyonyooka, na kwa kukamilisha Risala ya mwisho. [Al-Mukhtaswar Fiy Tafsiyr Al-Qur-aan Al-Kariym]
2-Kuthibitisha Unabii na Tawhiyd ya Allaah ya Ar-Rubuwbiyyah (Uola, Uumbaji, Uendeshaji na kadhaalika) na marejeo ya viumbe Kwake.
Miongoni Mwa Maudhui Ya Suwrah:
1-Suwrah imefunguliwa kwa Kiapo cha Allaah (سبحانه وتعالى) Kuapia matunda yenye faida tele kwa mwanaadam nayo ni tini na zaytuni. Na kuapia kwa mlima wa Twuur ambao Allaah (سبحانه وتعالى) Alimsemesha Nabiy Muwsaa (عليه السلام). Na kuapia kwa mji mtukufu wa Makkah ambao ni mji aliozaliwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akajaaliwa kuwa Nabiy wa mwisho, na ukawa Makkah ni mji wa chimbuko la Uislamu. Kisha ikatajwa uhakikisho wa kiapo kwamba Allaah (سبحانه وتعالى) Amemuumba binaadam umbo zuri kabisa lenye viungo vinavyoonekana na vilivyofichika, na kila kiungo kimeumbwa na kuwekwa sehemu ya mwili wa mwanaadam kwa hikma. Basi inampasa binaadam amshukuru Muumba Wake kwa neema hii. Lakini wengi wamemkufuru na hawakumwamini Rasuli Wake (صلى الله عليه وآله وسلم). Hivyo basi, yeyote yule aliyekufuru Allaah (سبحانه وتعالى) Atamteremsha cheo afikie moto wa chini kabisa ambako ni mahali pa makafiri na wanafiki waliomuasi Rabb wao. Ama walioamini na wakatenda mema, wakajipamba na khulqa njema, hawa watapata ujira usiokatika, nao ni kuingizwa mahali wanapostahiki, napo ni Jannah, ambako kuna neema tele za raha na starehe za kudumu milele.
2-Suwrah imekhitimishwa kwa swali la mshangao kwa makafiri wanaokanusha kufufuliwa kwamba kwani Allaah Hawezi Kuwafufua? Bali Naam! Anaweza kuwafufua kwa sahali kabisa. Na Allaah (سبحانه وتعالى) Hakuumba wanaadam bila ya makusudio, au bila ya kuwekwa amri au makatazo. Au bila ya kuweko malipo mema na mabaya. Basi Allaah (سبحانه وتعالى) Ameiweka Siku hiyo tukufu ya Qiyaama Atoe uamuzi kati ya watu, Naye ni Muadilifu zaidi kuliko mahakimu wote wale.
Fadhila Za Suwrah:
عَنْ عَدِيِّ بْنِ ثَابِتٍ، قَالَ سَمِعْتُ الْبَرَاءَ بْنَ عَازِبٍ، قَالَ سَمِعْتُ النَّبِيَّ صلى الله عليه وسلم قَرَأَ فِي الْعِشَاءِ بِالتِّينِ وَالزَّيْتُونِ . فَمَا سَمِعْتُ أَحَدًا أَحْسَنَ صَوْتًا مِنْهُ .
Amesimulia ‘Adiyy Bin Thaabit (رضي الله عنه): Nimemsikia Al-Baraa (رضي الله عنه) akisema: Nimemsikia Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akisoma katika Swalaah ya ‘Ishaa:
وَالتِّينِ وَالزَّيْتُونِ ﴿١﴾
“Naapa kwa tini na zaytuni.” [At-Tiyn (95)]
Na sijapatapo kumsikia mtu yeyote yule mwenye sauti nzuri kama yeye. [Al-Bukhaariy na Muslim]
Faida:
Pindi mara moja, Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alipokuwa safarini, aliisoma Suwrah hii tukufu:
عَنْ عَدِيٍّ، قَالَ سَمِعْتُ الْبَرَاءَ، أَنَّ النَّبِيَّ صلى الله عليه وسلم كَانَ فِي سَفَرٍ فَقَرَأَ فِي الْعِشَاءِ فِي إِحْدَى الرَّكْعَتَيْنِ بِالتِّينِ وَالزَّيْتُونِ.
Amesimulia ‘Adiyy (رضي الله عنه): Nimemsikia Al-Baraa (رضي الله عنه) akisema: Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alikuwa safarini akaisoma Suwrah:
وَالتِّينِ وَالزَّيْتُونِ ﴿١﴾
“Naapa kwa tini na zaytuni.” [At-Tiyn (95)]
katika Rakaa mojawapo ya Swalaah ya ‘Ishaa. [Al-Bukhaariy na wengineo]
096-Al-‘Alaq: Utangulizi Wa Suwrah
Alhidaaya.com [2]
Imeteremka: Makkah kwa itifaki ya ‘Ulamaa.
Idadi Za Aayah: 19
Jina La Suwrah: Al-‘Alaq
Suwrah imeitwa Al-‘Alaq (Pande La Damu Linaloning’inia), na yanodalilisha ni kutajwa kwake katika Hadiyth zilizonukuliwa katika Fadhila, na pia kutajwa kwake pia katika Aayah namba (2).
Miongoni Mwa Makusudio Ya Suwrah:
1-Kumuelezea mwanaadam kati ya kuongoka kwake kupitia Wahy, na kupotoka kwake kupitia kiburi na ujahili. [Al-Mukhtaswar Fiy Tafsiyr Al-Qur-aan Al-Kariym]
2-Kumthibitisha Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) na kumtishia kila mwenye kuipinga Risala ya Allaah na kumfanyia uadui Rasuli Wake (صلى الله عليه وآله وسلم).
Miongoni Mwa Maudhui Ya Suwrah:
1-Suwrah imefunguliwa kwa kuamrishwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) asome Qur-aan ilipoanza kuteremshwa mara ya kwanza kwake, pindi alipojitenga mbali na watu akawa katika pango la Hiraa akimwabudu Allaah. Akaamrishwa asome. Naye akajibu: “Mimi sijui kusoma.” Akaamrishwa asome kwa Jina la Rabb wake Aliyemuumba, na Aliyemuumba binaadam kwa pande la damu linaloning’inia, na kwamba Rabb wake ni Mwingi wa Ukarimu, Ihsaan na Wema, na Ambaye Amefundisha wanaadam kwa kalamu, Akawafundisha mambo ambayo hawakuwa wanayajua, kwani wamezaliwa kutoka matumbo ya mama zao hawakuwa wana ujuzi wa lolote, kisha Akawajaaliwa Nuru za ilimu.
2-Akaonywa binaadam aliyedhania kuwa ametosheka kwa utajiri wake, akavuka mipaka kumkanusha Muumba wake kwamba, mwisho wake ni kurudia kwa Rabb wake aliyemuumba.
3-Allaah (سبحانه وتعالى) Amemliwaza Rasuli Wake Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) kwamba, Yeye ni Mwenye kujua yale wanayompangia njama maadui zake. Na hii amekusudiwa Abu Jahl, laana ya Allaah iwe juu yake, kwani aliazimia kwa kuapia masanamu yao kuwa atausigina uso wa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) atakaposwali mbele ya Al-Ka’bah. Lakini Allaah (سبحانه وتعالى) Alimtisha kwa kumfanya aone mbele yake kuna khandaqi (shimo) la moto na Malaika waliokuwa wamekaa kidete kumwangamiza Abu Jahl. Basi Allaah (سبحانه وتعالى) Akamdhalilisha Abu Jahl na Akamnusuru Nabiy Wake (صلى الله عليه وآله وسلم), na Akaahidi kumuingiza Abu Jahl motoni kwa paji lake la uso lenye sifa ya uongo, kukadhibisha na madhambi ikiwa ataendelea kumfanyia uadui Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم). Na Akamtishia awaite wasaidizi wake wamsaidie, na Allaah Ataita Malaika Wake wenye kuadhibu vikali. Basi kwa vile Abu Jahl aliendelea kumfanyia uaudi Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم), aliuwawa katika Vita vya Badr kwa namna ya kudhalilishwa kabisa, kwani baada ya kujeruhiwa, Ibn Mas’uwd (رضي الله عنه) alimwendea na kumkata kichwa chake na kukipeleka kwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم). Basi akastahiki kuingizwa motoni.
4-Suwrah imekhitimishwa kwa Amri ya Allaah (سبحانه وتعالى) kwa Nabiy Wake (صلى الله عليه وآله وسلم) asimtii kafiri yeyote, na aendelee katika kubalighisha Risala ya Allaah, na aswali na ajikurubishe kwa Rabb wake.
Fadhila Za Suwrah:
1-Aayah Tano Za Mwanzo Ni Za Kwanza Kuteremshiwa Wahy Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم):
عَنْ عَائِشَةَ أُمِّ الْمُؤْمِنِينَ، أَنَّهَا قَالَتْ أَوَّلُ مَا بُدِئَ بِهِ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم مِنَ الْوَحْىِ الرُّؤْيَا الصَّالِحَةُ فِي النَّوْمِ، فَكَانَ لاَ يَرَى رُؤْيَا إِلاَّ جَاءَتْ مِثْلَ فَلَقِ الصُّبْحِ، ثُمَّ حُبِّبَ إِلَيْهِ الْخَلاَءُ، وَكَانَ يَخْلُو بِغَارِ حِرَاءٍ فَيَتَحَنَّثُ فِيهِ ـ وَهُوَ التَّعَبُّدُ اللَّيَالِيَ ذَوَاتِ الْعَدَدِ قَبْلَ أَنْ يَنْزِعَ إِلَى أَهْلِهِ، وَيَتَزَوَّدُ لِذَلِكَ، ثُمَّ يَرْجِعُ إِلَى خَدِيجَةَ، فَيَتَزَوَّدُ لِمِثْلِهَا، حَتَّى جَاءَهُ الْحَقُّ وَهُوَ فِي غَارِ حِرَاءٍ، فَجَاءَهُ الْمَلَكُ فَقَالَ اقْرَأْ. قَالَ " مَا أَنَا بِقَارِئٍ". قَالَ " فَأَخَذَنِي فَغَطَّنِي حَتَّى بَلَغَ مِنِّي الْجَهْدَ، ثُمَّ أَرْسَلَنِي فَقَالَ اقْرَأْ. قُلْتُ مَا أَنَا بِقَارِئٍ. فَأَخَذَنِي فَغَطَّنِي الثَّانِيَةَ حَتَّى بَلَغَ مِنِّي الْجَهْدَ، ثُمَّ أَرْسَلَنِي فَقَالَ اقْرَأْ. فَقُلْتُ مَا أَنَا بِقَارِئٍ. فَأَخَذَنِي فَغَطَّنِي الثَّالِثَةَ، ثُمَّ أَرْسَلَنِي فَقَالَ اقْرَأْ بِاسْمِ رَبِّكَ الَّذِي خَلَقَ * خَلَقَ الإِنْسَانَ مِنْ عَلَقٍ * اقْرَأْ وَرَبُّكَ الأَكْرَمُ ". فَرَجَعَ بِهَا رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم يَرْجُفُ فُؤَادُهُ، فَدَخَلَ عَلَى خَدِيجَةَ بِنْتِ خُوَيْلِدٍ رضى الله عنها فَقَالَ " زَمِّلُونِي زَمِّلُونِي ". فَزَمَّلُوهُ حَتَّى ذَهَبَ عَنْهُ الرَّوْعُ...
Amesimulia ‘Aaishah Mama wa Waumini (رضي الله عنها): Wahyi kwa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) ulianza kwa ndoto njema usingizini na alikuwa haoni ndoto isipokuwa ni kweli kama ulivyo mwanga wa mchana, na alipendezeshwa kujitenga. Alikuwa akijitenga ndani ya pango la Hiraa akimwabudu (Allaah Pekee) mfululizo kwa siku nyingi kabla ya kwenda kwa familia yake. Na anachukua chakula cha safari cha kutosha, na kisha alirejea kwa (mkewe) Khadiyjah (رضي الله عنها) kuchukua chakula tena mpaka ukweli ulishukia alipokuwa ndani ya pango la Hiraa. Malaika alimjia na alimtaka asome. Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) Akajibu: “Mimi sio msomaji.” Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akaendelea kusema: “Malaika akanishika kwa nguvu na akaniminya kwa nguvu mpaka nikapata tabu. Kisha aliniachia, na tena akanitaka nisome na nikamjibu: Mimi si msomaji. Baada ya hapo akanishika tena akaniminya kwa mara ya pili mpaka nikapata taabu. Kisha akaniachia akasema:
اقْرَأْ بِاسْمِ رَبِّكَ الَّذِي خَلَقَ ﴿١﴾ خَلَقَ الْإِنسَانَ مِنْ عَلَقٍ ﴿٢﴾ اقْرَأْ وَرَبُّكَ الْأَكْرَمُ ﴿٣﴾
“Soma kwa Jina la Rabb wako Aliyeumba. Amemuumba mwana Aadam kutokana na pande la damu linaloning’inia. Soma na Rabb wako ni Mkarimu kushinda wote.” [Al-‘Alaq: (1-3)] Na kuendelea hadi Aayah namba (5).
Kisha Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alirejea na Wahy, na huku moyo ukidunda kwa nguvu. Kisha alikwenda kwa Khadiyjah bint Khuwaylid (رضي الله عنها) akasema: “Nifunikeni! Nifunikeni!” Wakamfunika mpaka khofu ikatoweka…[Al-Bukhaariy]
2-Swahaba Walisujudu Pamoja Na Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) Pindi Aliposoma Suwrah Hii:
عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ، قَالَ سَجَدْنَا مَعَ النَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم فِي إِذَا السَّمَاءُ انْشَقَّتْ وَ اقْرَأْ بِاسْمِ رَبِّكَ
Amesimulia Abuu Hurayrah (رضي الله عنه): Tulisujudu pamoja na Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) pindi aliposoma:
إِذَا السَّمَاءُ انشَقَّتْ ﴿١﴾
“Mbingu itakaporaruka.” [Al-Inshiqaaq (84)]
Na
اقْرَأْ بِاسْمِ رَبِّكَ
“Soma kwa Jina la Rabb wako,” [Al-‘Alaq (96)]
[Al-Bukhaariy, Muslim na wengineo]
097-Al-Qadr: Utangulizi Wa Suwrah
Alhidaaya.com [2]
Imeteremka: Makkah au Madiynah kwani ‘Ulamaa wamekhitilafiana kuhusu wapi imeteremshwa.
Idadi Za Aayah: 5
Jina La Suwrah: Al-Qadr
Suwrah imeitwa Al-Qadr (Qadar), na yanayodalilisha ni kutajwa kwake katika Fadhila, na pia kutajwa katika namba (1). Rejea kwenye Faida ya Aayah namba (1) ambako kuna maelezo kuhusu ‘Ulamaa kukhitilafiana maana ya Qadr.
Miongoni Mwa Makusudio Ya Suwrah:
1-Kubainisha fadhila za Laylatul-Qadr. [Al-Mukhtaswar Fiy Tafsiyr Al-Qur-aan Al-Kariym]
2-Kutaja fadhila za usiku mtukufu kabisa, Laylatul-Qadr, na kuashiria kuteremshwa Qur-aan Usiku huo.
Miongoni Mwa Maudhui Ya Suwrah:
1-Suwrah imeanza kuelezewa kuteremshwa Qur-aan katika Layalatul-Qadr (Usiku wa Qadar), na kwamba usiku huo ni mtukufu mno, nao umo katika kumi la mwisho la mwezi wa Ramadhwaan.
2-Ikaendelea kuelezwa na kukhitimishwa kwa kubainishwa kwamba usiku huo ni mbora kuliko miezi elfu moja, na kwamba Malaika wengi pamoja na Jibriyl (عليهم السّلام) wanateremka kwa Idhini ya Rabb wao kwa kila jambo Alilolikadaria mwaka huo, na kwamba usiku wote huo hakuna shari, bali kuna amani mpaka kutokea Alfajiri.
098-Al-Bayyinah: Utangulizi Wa Suwrah
Alhidaaya.com [2]
Imeteremka: Makkah au Madiynah kwani ‘Ulamaa wamekhitilafiana kuhusu wapi imeteremshwa.
Idadi Za Aayah: 8
Jina La Suwrah: Al-Bayyinah
Suwrah imeitwa Al-Bayyinah (Hoja Bayana), na yanayodalilisha ni kutajwa katika Hadiyth iliyonukuliwa katika Faida, na pia kutajwa kwake katika Aayah namba (1).
Miongoni Mwa Makusudio Ya Suwrah:
1-Kubainisha ukamilifu wa Risala ya Muhammad Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم), na ule uwazi wake. [Al-Mukhtaswar Fiy Tafsiyr Al-Qur-aan Al-Kariym]
2-Kuwakemea washirikina na watu waliopewa Kitabu juu ya kuikadhibisha kwao Qur-aan na kumpinga Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم), na kubainisha marejeo yao na marejeo ya Waumini.
Miongoni Mwa Maudhui Ya Suwrah:
1-Suwrah imefunguliwa kwa kuwalaumu watu waliopewa Kitabu ambao ni Mayahudi na Manaswara na pia kuwalamu washirikina wa aina zote katika nyumati, kwamba, hawakuwa wenye kuacha ukafiri wao mpaka iwajie hoja walioahidiwa katika Vitabu vilivyopita. Yaani wangeendelea na kuendelea katika upotevu wao, na kupita kwa zama ungewaongezea tu ukafiri wao mpaka iwafikie hoja na ushahidi wa wazi. Na ushahidi huo ni kutumiwa Nabiy Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم) akawasomea Qur-aan iliyo kwenye kurasa zilizotakasika, haziguswi isipokuwa kwa waliokuwa katika twahara. Na kwamba ndani ya Qur-aan, khabari za kweli na amri za uadilifu zenye kuongoza kwenye haki na njia iliyonyooka. Na pia hawakufarikiana wale waliopewa Kitabu, miongoni mwa Mayahudi na Manaswara, juu ya kuwa Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم) ni Rasuli wa kweli, kwa sifa zake walizokuwa wakiziona katika vitabu vyao, isipokuwa baada ya kuwathibitikia kuwa yeye ndiye Nabiy waliyoahidiwa katika Tawraat na Injiyl. Walikuwa wanakubali kwa umoja wao, kuwa Unabii wake ni wa kweli. Lakini alipotumwa, waliukanusha na wakatofautiana.
2-Imetajwa kukinzana (kutofautiana) hali zao, na kubainisha kwa ukafiri wao ulikua ni kwa sababu ya kupinga kwao na jeuri yao na husda yao kwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم). Ilhali hawakuamrishwa katika sharia zao zilizopita isipokuwa, wamwabudu Allaah Pekee na kumtakasia ibaada kwa kuepukana na ushirikina na wasimamishe Swalaah na watoe Zakaah na waifanye Dini iliyonyooka. Na hiyo ndio Tawhiyd na ikhlaasw katika Dini, na ndio Dini iliyonyooka ya Kiislamu. Ikabainishwa kwamba hao washirikina, na Mayahudi na Manaswara, hatima yao ni kuingizwa moto wa Jahannam wadumu, na wao ni viumbe waovu kabisa.
3-Suwrah ikakhitimishwa kwa kuwabashiriwa Waumini watendao mema, kwamba wao ni viumbe bora kabisa, na Rabb wao Atawaingiza Peponi kuwa ni jazaa yao, wadumu humo milele, Allaah Awaridhie nao pia wamridhie Allaah. Na hii ndio fadhila ya mwenye kumkhofu Rabb wake.
Faida:
Allaah (سبحانه وتعالى) Amemumarisha Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) amsomee ‘Ubayy Bin Ka’ab (رضي الله عنه) Suwrah hii ya Al-Bayyinah:
عَنْ أَنَسِ بْنِ مَالِكٍ ـ رضى الله عنه ـ قَالَ النَّبِيُّ صلى الله عليه وسلم لأُبَىٍّ " إِنَّ اللَّهَ أَمَرَنِي أَنْ أَقْرَأَ عَلَيْكَ لَمْ يَكُنِ الَّذِينَ كَفَرُوا قَالَ وَسَمَّانِي قَالَ " نَعَمْ " فَبَكَى.
Amesimulia Anas Bin Maalik (رضي الله عنه): Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alimwambia ‘Ubayy Bin Ka’ab (رضي الله عنه): “Allaah Ameniamrisha nikusomee:
لَمْ يَكُنِ الَّذِينَ كَفَرُوا مِنْ أَهْلِ الْكِتَابِ وَالْمُشْرِكِينَ مُنفَكِّينَ حَتَّىٰ تَأْتِيَهُمُ الْبَيِّنَةُ ﴿١﴾
“Hawakuwa wale waliokufuru.” [Al-Bayyinah (98)]
Basi ‘Ubayy (رضي الله عنه) akauliza: Allaah Ametaja jina langu? Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) Akajibu: “Naam.” Ubay Bin Ka’ab akalia. [Al-Bukhaariy, Muslim, na wengineo]
099-Az-Zalzalah: Utangulizi Wa Suwrah
Alhidaaya.com [2]
Imeteremka: Makkah au Madiynah kwani ‘Ulamaa wamekhitilafiana kuhusu wapi imeteremshwa.
Idadi Za Aayah: 8
Jina La Suwrah: Az-Zalzalah
Suwrah imeitwa Az-Zalzalah (Zilizali: Tetemeko La Ardhi), na inayodalilisha ni kutajwa kwake katika Aayah namba (1).
Miongoni Mwa Makusudio Ya Suwrah:
1-Ukumbusho wa hali ya Siku ya Qiyaamah, na kuhesabiwa matendo ya waja kwa umakini Siku hiyo. [Al-Mukhtaswar Fiy Tafsiyr Al-Qur-aan Al-Kariym]
2-Kuthibitisha kufufuliwa na yatakayotokea Siku ya Qiyaamah, na kulipwa matendo katika kheri au shari.
Miongoni Mwa Maudhui Ya Suwrah:
1-Suwrah imefunguliwa kwa kutajwa yatakayotokea Siku ya Qiyaamah; Zilzala ambayo itatikisa mno ardhi hadi kila kilichokuweko juu yake kibomoke, kama milima, majumba, na watu kutolewa makaburini. Kisha binaadam atashangaa na kuulizwa: “Kumezuka nini?” Na Siku hiyo ardhi itatoa habari ya mambo yote iliyotendwa juu yake; mazuri na mabaya, kwani ardhi ni katika vitakavyoshuhudia matendo ya waja Siku hiyo tukufu.
2-Ikakhitimishwa Suwrah kwa kuthibitishwa kwamba kila mtu atalipwa kulingana na matendo yake aliyoyatenda duniani, matendo ya kheri au shari, hata yawe madogo kiasi cha uzito wa sisimizi au atomi, binaadam atayaona katika daftari lake la hesabu, na atalipwa malipo yake mema au maovu, na wala Allaah (سبحانه وتعالى) Hatomdhulumu mtu kwa chochote, hata kwa chembe ya hardali au atomi.
100-Al-‘Aadiyaat: Utangulizi Wa Suwrah
Alhidaaya.com [2]
Imeteremka: Makkah kwa itifaki ya ‘Ulamaa.
Idadi Za Aayah: 11
Jina La Suwrah: Al-‘Aadiyaat
Suwrah imeitwa Al-‘Aadiyaat (Waendao Mbio Za Kasi), na inayodalilisha ni kutajwa kwake katika Aayah namba (1).
Miongoni Mwa Makusudio Ya Suwrah:
1-Kumpa tahadhari mwanaadam ya kutokuwa na tamaa na ukaidi, kwa kumkumbusha Aakhirah. [Al-Mukhtaswar Fiy Tafsiyr Al-Qur-aan Al-Kariym]
2-Kutahadhrishwa mwanaadam kutoa haki za mali anayoruzukiwa na kukumbuka kwamba Allaah (سبحانه وتعالى) Ni Mjuzi wa matendo yote na yatahesabiwa Siku ya Qiyaamah.
Miongoni Mwa Maudhui Ya Suwrah:
1-Suwrah imefunguliwa kwa Kiapo cha Allaah (سبحانه وتعالى) Kuapia farasi, ambao ni neema mojawapo kwa wanaadam, kwa sababu ya kutumika na kufaa mno katika kupigana Jihaad. Farasi hao wanakimbia kwa mwendo kasi katika kumkabili adui wakitoa sauti kutokana na kasi ya kukimbia. Na kuapia kwa farasi wanaotoa cheche za moto kwa kwato zao ngumu wanapokimbia kwa kasi, wenye kushambulia maadui kipindi cha asubuhi, na wakarusha vumbi kutokana na mbio za kasi. Likawa vumbi limewagubika maadui kwa vipando vyao, hata wakaingiwa kiwewe na kufazaika. Kisha ikafuatia uthibitisho wa kiapo kwamba, hakika binaadam ni mkanushaji mno wa Neema za Rabb wake, kwa kutokutoa haki anazopaswa kama Zakaah na swadaqa. Na kwamba Allaah Anashuhudia hayo. Au huyo binaadam bakhili atakuja kushudia hayo mwenyewe Siku ya Qiyaamah. Na kwamba binaadam huyo ni mpenda mno wa mali na ni mwenye kuipupia, hadi aache kutoa haki apasazo kuzitoa, kwa sababu ya kughafilika kwake na Aakhirah.
2-Kisha anaulizwa huyo binaadam aliyekosa shukurani kwa Neema za Allaah kwamba, kwani hajui linalomngojea mbele yake, pindi Allaah (سبحانه وتعالى) Atakapowatoa wafu makaburini waende kuhesabiwa na kulipwa? Na kwamba yatafichuliwa yaliyomo vifuani, mema na maovu?
3-Suwrah imekhitimishwa kwa uthibitisho kwamba Allaah (سبحانه وتعالى) Ni Mjuzi wa dhahiri na siri kwa kila wanachokifanya waanaadam, na kwamba Atawafanyia hesabu ya matendo yao Siku ya kufufuliwa.
101-Al-Qaari’ah: Utangulizi Wa Suwrah
Alhidaaya.com [2]
Imeteremka: Makkah
Idadi Za Aayah: 11
Jina La Suwrah: Al-Qaari’ah
Suwrah imeitwa Al-Qaari’ah (Janga Kuu Linalogonga), na inayodalilisha ni kutajwa kwake katika Aayah namba (1-3).
Miongoni Mwa Makusudio Ya Suwrah:
1-Kuzishtua nyoyo kwa kuzielezea vitisho vya Siku ya Qiyaamha, na hali za watu katika mizani zao (wakati wa kupimwa matendo yao). [Al-Mukhtaswar Fiy Tafsiyr Al-Qur-aan Al-Kariym]
2-Kutanabahisha tisho la tukio kubwa mno la Siku ya Qiyaamah, na amali za aina mbili katika mizani; za watakaofaulu na za watakaokula khasara.
Miongoni Mwa Maudhui Ya Suwrah:
1-Suwrah imefunguliwa kwa kutajwa mojawapo wa Jina la Siku ya Qiyaamah, nalo ni Al-Qaari’ah ambalo ni tukio linalogongagonga hadi likawafazaisha watu kutokana na tishio lake. Na ikafuatilia swali la kuulizia nini Al-Qaari’ah? Kisha ikaja jibu lake la kuelezea hali za watu na milima itakavyokuwa. Kwa vile kutakuwa na halaiki kubwa ya watu, basi kugawanyika kwao na kuzunguka kwao, ni kama panzi walioenea. Nao ni wale wanaojitupa motoni. Na milima itakuwa kama pamba yenye rangi tofauti inayochambuliwa.
2-Suwrah ikakhitimishwa kwa kubainisha hali mbili za mizani za watu; mizani za watu ambao mema yao yamekuwa mazito katika mizani. Hawa ndio watakaopata maisha ya kuridhika Peponi. Mizani ya pili ni za watu ambao maovu yao ni mengi mno katika mizani. Basi hawa makazi yao yatakuwa ni katika moto unaoitwa Haawiyah ambao unawaka mno kwa kuni zilizomo ndani yake.
102-At-Takaathur: Utangulizi Wa Suwrah
Alhidaaya.com [2]
Imeteremka: Makkah kwa itifaki ya ‘Ulamaa.
Idadi Za Aayah: 8
Jina La Suwrah: At-Takaathur
Suwrah imeitwa At-Takaathur (Kushindana Kukithirisha), na inayodalilisha ni kutajwa kwake katika Aayah namba (1).
Miongoni Mwa Makusudio Ya Suwrah:
1-Kuwakumbusha wale wanaotaka kuwa na mali nyingi, na wanaofanya upuuzi hapa duniani, (kuwakumbusha) makaburi na kuhesabiwa (matendo). [Al-Mukhtaswar Fiy Tafsiyr Al-Qur-aan Al-Kariym]
2-Tahadharisho la kutokushindana kutafuta mali kwa wingi huku wakighafilika na Aakhirah, na ukumbusho wa kuulizwa Siku ya Qiyaamah.
Miongoni Mwa Maudhui Ya Suwrah:
Suwrah imefunguliwa kwa kutahadharishwa watu wanaoghafilika na kutenda yanayowawajibikia ya utiifu kwa Allaah (سبحانه وتعالى), kwa kushindana kutafuta wingi wa mali na watoto na mengineyo yenye kuwasterehesha na kuwanufaisha duniani na wakajifakharisha nayo. Kushughulika kwao huko, kunaendelea mpaka yanapowafika mauti, wakazikwa makaburini. Basi humo ndimo kutakapohakiki mambo wakajuta kushughulika kushindana kwa mali na mengineyo, jambo ambalo limewafanya wasahau Aakhirah. Na watakapokuwa wanaadhibika humo kaburini, basi watatamani warudi duniani ili wajiandaalie mema ili waepukana na adhabu humo kaburini. Lakini wapi! Hakuna uwezekano wa kurudi duniani, na Allaah (سبحانه وتعالى) Anahakikisha kwamba humo kaburini, kwa yakini watauona moto wa Jahiym ambao una waka vikali mno! Kisha Allaah (سبحانه وتعالى) Amesisitiza tena kuwa watauona waziwazi na kwa yakini kabisa. Kisha wataulizwa kuhusu kila neema walizojaaliwa duniani, ambazo walinufaika nazo, kama walishukuru au walikufuru. Basi wataulizwa: Je, wamezipata vipi? Je, wamezitumia vipi? Je, walitimiza haki za Allaah na haki za jamaa, masikini na mafuqaraa?
103-Al-‘Aswr: Utangulizi Wa Suwrah
Alhidaaya.com [2]
Imeteremka: Makkah kwa itifaki ya ‘Ulamaa.
Idadi Za Aayah: 3
Jina La Suwrah: Al-‘Aswr
Suwrah imeitwa Al-‘Aswr (Zama), na inayodalilisha ni kutajwa kwake katika Aayah namba (1).
Miongoni Mwa Makusudio Ya Suwrah:
1-Kuelezea sababu za kuokoka na za kupata khasara. [Al-Mukhtaswar Fiy Tafsiyr Al-Qur-aan Al-Kariym]
2-Kubainisha ni watu wepi watakaopata khasara, na ni wepi watu watakaofaulu.
Miongoni Mwa Maudhui Ya Suwrah:
Suwrah imefunguliwa kwa Kiapo cha Allaah (سبحانه وتعالى) Kuapia zama, kwa sababu ya matukio mengi yaliyojiri kwa watu waliotangulia, yakiwemo ya maajabu; waliotenda ya kheri na malipo yao, na waliotenda ya shari na adhabu zao. Kisha ikahakikishwa kiapo kwamba, binaadam yuko katika khasara na maangamizi kwa kughafilika kutii Amri za Allaah (سبحانه وتعالى). Lakini waliokhasirika si wanaadam wote, kuna watakaofaulu. Hawa ni ambao wana imaan nyoyoni mwao, wakaamini nguzo za imaan, na wakamwamini Allaah (سبحانه وتعالى) kwa kutii Amri Zake, na kujiepusha makatazo Yake, na wakamwamini Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) na kutii amri zake na kujiepusha makatazo yake. Kisha wakatenda amali njema za kila aina; amali za kudhihirika na amali za kufichika. Na pia wakalingania (da’wah), jambo ambalo limesisitizwa mno katika Qur-aan na Sunnah; kuamrishana mema na kukatazana munkari. Kisha wakavuta subira kutokana na tabu na mashaka watakazozipata katika da’wah, wakathibitika katika Dini. Basi hawa ndio watakaosalimika na khasara na ndio watakaofaulu duniani na Aakhirah.
Faida:
Imaam Ibn Kathiyr (رحمه الله) amenukuu katika Tafsiyr yake kwamba, Al-Shaafi’iyy (رحمه الله) amesema: “Lau watu wangeitafakari Suwrah Al-‘Aswr, ingewatosheleza.” Na lilokusudiwa katika kauli yake hiyo kwamba, ingawa Suwrah hii ni fupi, lakini ina maana ya kina, ambayo inaongoza njia kamili ya maisha ya mwanaadam, na hivyo basi Suwrah inawaongoza wanaadam katika kuhimizana kushikamana na Dini ya Allaah kwa imaan, matendo mema, da’wah (kulingania Dini), na kuvuta subira katika hayo. Na hivyo basi, inamtosheleza mtu kupata mafaniko ya maisha ya dunia na Aakhirah.
104-Al-Humazah: Utangulizi Wa Suwrah
Alhidaaya.com [2]
Imeteremka: Makkah kwa itifaki ya ‘Ulamaa.
Idadi Za Aayah: 9
Jina La Suwrah: Al-Humazah
Suwrah imeitwa Al-Humazah (Kufedhehesha, Kukashifu Kwa Ishara Na Vitendo), na inayodalilisha ni kutajwa kwake katika Aayah namba (1).
Miongoni Mwa Makusudio Ya Suwrah:
1-Kuwatahadharisha wanaadam juu ya kuwafanyia istihzai Waumini kwa kudanganyika kwao na uwingi wa mali. [Al-Mukhtaswar Fiy Tafsiyr Al-Qur-aan Al-Kariym]
2-Kutaja sifa za wenye kuangamia.
Miongoni Mwa Maudhui Ya Suwrah:
Suwrah imefunguliwa kwa ahadi ya kuadhibiwa kila mwenye kuwavunjia watu heshima zao kwa kuwakashifu, kuwadharau, kuwakebehi kwa ishara na vitendo. Na pia kila mwenye kusengenya, kukashifu kwa ulimi. Na sifa ya mtu huyo ni yule anayerundika mali na kupenda kuhesabu, wala hana raghba ya kuitolea mali katika Aliyoyaamrisha Allaah (سبحانه وتعالى) kama Zakaah na Swadaqah, au kuwagawia arhaam (wenye uhusiano wa damu), na mengineyo ya khayraat. Basi anadhania kwamba mali yake ambayo ameikusanya, inampa dhamana ya kuishi milele duniani na itamfanya akwepe kuhesabiwa. Lakini anayoyadhania siyo kabisa! Kwani bila shaka ataingiziwa katika moto ulio na sifa ya Hutwamah, yaani moto unavunjavunja kila kinachotupwa humo. Na kwa ukali wa moto huo, unapenya miilini ukafika nyoyoni. Na umefunga milango yake baada ya kutumbukizwa watu humo kwenye nguzo ndefu ili wasiweze kutoka kamwe!
105-Al-Fiyl: Utangulizi Wa Suwrah
Alhidaaya.com [2]
Imeteremka: Makkah kwa itifaki ya ‘Ulamaa.
Idadi Za Aayah: 5
Jina La Suwrah: Al-Fiyl
Suwrah imeitwa Al-Fiyl (Tembo), na inayodalilisha ni kutajwa kwake katika Aayah namba (1).
Miongoni Mwa Makusudio Ya Suwrah:
1-Kubainisha Uwezo wa Allaah (سبحانه وتعالى) na Nguvu Zake juu ya wale wanaoifanyia vitimbi Nyumba Yake Tukufu (Al-Ka’bah). [Al-Mukhtaswar Fiy Tafsiyr Al-Qur-aan Al-Kariym]
2-Kubainisha uovu watu wa tembo na maangamizi yao.
Miongoni Mwa Maudhui Ya Suwrah:
Suwrah imefunguliwa kwa swali kumwelekea Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) kumuuliza: Hivi hukuona jinsi Allaah Alivyowafanya watu wa tembo, Abraha Mhabeshi na jeshi lake kubwa kutoka Habasha na Yemen, kukusudia kuishambulia Nyumba ya Allaah (Al-Ka’bah)? Na Allaah Hakujaalia njama zao zifeli na zipite patupu? Jeshi hilo kubwa lilipofika karibu na Makkah, Waarabu hawakuwa na nguvu na ulinzi wa kujihami, basi wakakimbia kwa kuhofia maisha yao. Kisha Allaah Akawasalitisha watu wa tembo, kwa ndege waliofuatana makundi kwa makundi yakawazunguka kila upande, wakiwatupia vijiwe vya udongo mkavu mgumu uliookwa motoni, Akawapondaponda wakawa kama majani makavu yaliyoliwa na wanyama kisha kutupwa.
Na hiki ni kisa maarufu cha tembo, kilichotokea mwaka aliozaliwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم), ukajulikana mwaka humo kama 'Aamul-Fiyl (Mwaka wa Tembo).
106-Quraysh: Utangulizi Wa Suwrah
Alhidaaya.com [2]
Imeteremka: Makkah kwa itifaki ya ‘Ulamaa.
Idadi Za Aayah: 4
Jina La Suwrah: Quraysh
Suwrah imeitwa Quraysh (Kabila La Quraysh), na inayodalilisha ni kutajwa katika Aayah namba (1).
Miongoni Mwa Makusudio Ya Suwrah:
1-Kubainisha Neema za Allaah kwa Maquraysh, na haki Yake Allaah kwao. [Al-Mukhtaswar Fiy Tafsiyr Al-Qur-aan Al-Kariym]
2-Kuwakumbusha watu wa Makkah Neema za Allaah (سبحانه وتعالى) kwao.
Miongoni Mwa Maudhui Ya Suwrah:
Suwrah imefunguliwa kwa kustaajabu mazowea ya Maquraysh, kuhusu amani waliyonayo, na kupangika kwa sahali na vizuri kabisa safari zao za kwenda Yemen katika msimu wa baridi, na safari za kwenda Sham katika msimu wa joto, kwa ajili ya biashara zao. Basi wamshukuru Rabb wao na wampwekeshe katika ibaada kwani Yeye Allaah (سبحانه وتعالى), Ndiye Aliyewaezesha hayo, na Yeye Ndiye Aliyewajaalia wawe na hadhi na heshima kubwa kwa kuwajaalia wawe wakaazi wa Makkah, mji ambao ni mtukufu kabisa, uliomo ndani yake Al-Ka’bah (Nyumba ya Allaah). Na pia wamshukuru na wampwekesha Allaah (سبحانه وتعالى) kwani Yeye Ndiye Aliyewaruzuku chakula kipindi cha njaa, na Akawajaalia amani na utulivu kutokana na khofu, kwa vile Allaah Aliwaangamiza wale waliowakusudia mabaya. Basi kujaaliwa rizki na amani, ni katika neema kubwa za kidunia.
107-Al-Maa’uwn: Utangulizi Wa Suwrah
Alhidaaya.com [2]
Imeteremka: Makkah kwa itifaki ya ‘Ulamaa
Idadi Za Aayah: 7
Jina La Suwrah: Al-Maa’uwn
Suwrah imeitwa Al-Maa’uwn (Misaada Ya Matumizi Madogodogo Ya Kawaida), na inayodalilisha ni kutajwa kwake katika Aayah namba (1).
Miongoni Mwa Makusudio Ya Suwrah:
1-Kubainisha sifa za wanaoikadhibisha Dini. [Al-Mukhtaswar Fiy Tafsiyr Al-Qur-aan Al-Kariym]
2-Kushangazwa na hali ya wenye kukadhibisha kufufuliwa na kuhesabiwa matendo, na ubaya wa matendo yao.
Miongoni Mwa Maudhui Ya Suwrah:
Suwrah imefunguliwa kwa mshangao kuhusu makafiri wasioamini kufufuliwa na kuhesabiwa matendo. Ikafuatia sifa zao ambazo, ni wenye kuacha kutoa haki za waja; kumdhulumu yatima kwa kumyima haki yake na kumkaripia, wala hamhurumii kutokana na ususuavu wa moyo wake, wala hakhofu kuhesabiwa kwa hili. Pia hawahimizi wengine kulisha maskini. Kisha Allaah (سبحانه وتعالى) Akaahidi adhabu kali ya moto kwa wenye sifa za unafiki, ambao huswali lakini wanaghafilika na Swalaah zao; hawazisimamishi kama ipasavyo, wala hawaziswali kwa nyakati zake, bali huswali kwa riyaa-a (kujionyesha kwa watu) ili wasifike kuwa ni waswalihina. Na wanakataa kuwafanyia watu ihsaan, kwa kuwanyima msaada wa aina yoyote ule unaokidhi haja zao za dharura, kama kutokuwaazima au kutokuwagaia vitu, ambavyo havina gharama kubwa pamoja na kuwa hawapungukiwi kitu kuviazimisha au kuvigawa, kama vile kumyima jirani vitu alivyopungukiwa katika matumizi ya jikoni, au kutokumuazima mtu vyombo au vitendea kazi, atumie kwa ajili ya vitu vilivyomharibikia nyumbani kwake.
108-Al-Kawthar: Utangulizi Wa Suwrah
Alhidaaya.com [2]
Imeteremka: Makkah au Madiynah kwani ‘Ulamaa wamekhitilafiana kuhusu wapi imeteremshwa.
Idadi Za Aayah: 3
Jina La Suwrah: Al-Kawthar
Suwrah imeitwa Al-Kawthar (Mto Wenye Kheri Nyingi), na inayodalilisha ni kutajwa kwake katika Hadiyth iliyonukuliwa katika Fadhila na pia kutajwa kwake katika Aayah namba (1).
Miongoni Mwa Makusudio Ya Suwrah:
1-Kubainisha Neema za Allaah kwa Nabiy Wake (صلى الله عليه وآله وسلم) ambazo ni kheri nyingi na kumtetea. [Al-Mukhtaswar Fiy Tafsiyr Al-Qur-aan Al-Kariym]
2-Kumbashiria Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) Neema ya Mto wa Al-Kawthar Siku ya Qiyaamah na kumliwaza.
Miongoni Mwa Maudhui Ya Suwrah:
Suwrah imefunguliwa kwa kumkumbusha Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) kheri nyingi alizojaaliwa duniani na Aakhirah. Miongoni mwa kheri za Aakhirah ni kumjaalia mto (Al-Kawthar) ambao pambizo zake ni mahema ya lulu na mchanga wake ni miski. Kisha Allaah (سبحانه وتعالى) Akamwamrisha Nabiy Wake (صلى الله عليه وآله وسلم) Amtakase kwa ibaada na achinje mnyama kwa ajili Yake Pekee pamoja na kutaja Jina la Allaah. Suwrah ikakhitimishwa kwa kumliwaza Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) kumbainishia kwamba, mgomvi wake anayemchukia kwa sababu ya kubalighisha Risala ya Allaah, ndiye atakayekatiwa kila kheri. Rejea Sababun-Nuzuwl (Sababu ya Kuteremka) Suwrah hii tukufu.
Fadhila Za Suwrah:
Bishara Kwa Waumini Watakaoshikamana Na Sunnah Wataruhusiwa Kunywa Kinywaji Katika Hodhi Lenye Maji Kutoka Mto Wa Al-Kawthar:
‘Ulamaa wametaja kuwa Al-Kawthar ni mto katika Jannah, nao ni katika kheri na fadhila nyingi mno atakazopewa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) Siku ya Qiyaamah. Mto huo una tawi lake ambalo ni hodhi litakalozungukwa na Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم), Swahaba na Waumini waliothibitika katika Manhaj sahihi, nao watakunywa hapo na hawatapata kiu tena milele. Ama waliozua mambo katika Dini (bidaa), hao watatengwa wasibakie hapo katika Al-Hawdhw. Simulizi kadhaa zimethibiti na miongoni mwazo ni Hadiyth hii:
عَنْ أَنَسٍ، قَالَ: بَيْنَا رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم ذَاتَ يَوْمٍ بَيْنَ أَظْهُرِنَا إِذْ أَغْفَى إِغْفَاءَةً ثُمَّ رَفَعَ رَأْسَهُ مُتَبَسِّمًا فَقُلْنَا: مَا أَضْحَكَكَ يَا رَسُولَ اللَّهِ؟ قَالَ: ((أُنْزِلَتْ عَلَىَّ آنِفًا سُورَةٌ )). فَقَرَأَ: (( بِسْمِ اللَّهِ الرَّحْمَنِ الرَّحِيمِ * إِنَّا أَعْطَيْنَاكَ الْكَوْثَرَ * فَصَلِّ لِرَبِّكَ وَانْحَرْ * إِنَّ شَانِئَكَ هُوَ الأَبْتَرُ)). ثُمَّ قَالَ: ((أَتَدْرُونَ مَا الْكَوْثَرُ؟)). فَقُلْنَا اللَّهُ وَرَسُولُهُ أَعْلَمُ. قَالَ: ((فَإِنَّهُ نَهْرٌ وَعَدَنِيهِ رَبِّي عَزَّ وَجَلَّ عَلَيْهِ خَيْرٌ كَثِيرٌ هُوَ حَوْضٌ تَرِدُ عَلَيْهِ أُمَّتِي يَوْمَ الْقِيَامَةِ آنِيَتُهُ عَدَدُ النُّجُومِ فَيُخْتَلَجُ الْعَبْدُ مِنْهُمْ فَأَقُولُ رَبِّ إِنَّهُ مِنْ أُمَّتِي. فَيَقُولُ مَا تَدْرِي مَا أَحْدَثَتْ بَعْدَكَ)). زَادَ ابْنُ حُجْرٍ فِي حَدِيثِهِ بَيْنَ أَظْهُرِنَا فِي الْمَسْجِدِ. وَقَالَ: ((مَا أَحْدَثَ بَعْدَكَ)).
Amesimulia Anas (رضي الله عنه): Siku moja Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alikuwa pamoja nasi akawa amepitiwa na lepe la usingizi kisha akanyanyua kichwa chake juu huku akitabasamu, tukasema: Ni kitu gani kimekufurahisha ee Rasuli wa Allaah? Akasema: “Imeniteremkia sasa hivi Suwrah: (Akaisoma Suwrah Al-Kawthar).
بِسْمِ اللَّهِ الرَّحْمَنِ الرَّحِيمِ * إِنَّا أَعْطَيْنَاكَ الْكَوْثَرَ * فَصَلِّ لِرَبِّكَ وَانْحَرْ * إِنَّ شَانِئَكَ هُوَ الأَبْتَرُ *
“Hakika Sisi Tumekupa (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) Al-Kawthar (Mto katika Jannah). Basi swali kwa ajili ya Rabb wako na chinja. Hakika mbaya wako, yeye ndiye atakayekatiliwa mbali (kizazi na kila kheri).” [Al-Kawthar: (108)]
Kisha akasema: “Je, mnajua ni nini Al-Kawthar?” Tukajibu: Allaah na Rasuli Wake Ndio Wajuao zaidi. Akasema: “Huo ni mto ambao Allaah (عزّ وجلّ) Ameniahidi. Una kheri nyingi sana, nao una hodhi lake ambalo Ummah wangu watakusudia kulifikia Siku ya Qiyaamah. Vyombo vyake (au bilauri) ni idadi ya nyota. Mja miongoni mwao atatolewa mbali atengwe. Nitasema: Ee Rabb! Hakika yeye ni katika Ummah wangu! Allaah Atasema: Hujui nini alizusha baada yako!”
Ibn Hujri amezidisha katika Hadiyth yake: Alikuwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) amekaa kitako pamoja nasi Msikitini. Na (Allaah) Atasema: “Hujui walichokizusha baada yako!” [Muslim – Kitaab Asw-Swalaah - Mlango wa hoja anayesema kuwa Al-Basmalah ni Aayah katika kila mwanzo wa Suwrah isipokuwa Suwrah Al-Baraa (At-Tawbah)]
109-Al-Kaafiruwn: Utangulizi Wa Suwrah
Alhidaaya.com [2]
Imeteremka: Makkah kwa itifaki ya ‘Ulamaa.
Idadi Za Aayah: 6
Jina La Suwrah: Al-Kaafiruwn
Suwrah imeitwa Al-Kaafiruwn (Makafiri), na inayodalilisha ni kutajwa katika Hadiyth zilizonukuliwa katika Fadhila, na kutajwa kwake katika Aayah namba (1).
Miongoni Mwa Makusudio Muhimu Ya Suwrah:
1-Utakaso kutokana na ukafiri na watu wake. [Al-Mukhtaswar Fiy Tafsiyr Al-Qur-aan Al-Kariym]
2-Kujiweka mbali kabisa kati ya wanaompwekesha Allaah na makafiri.
Miongoni Mwa Maudhui Ya Suwrah:
Amri ya Allaah (سبحانه وتعالى) kwa Rasuli Wake (صلى الله عليه وآله وسلم) awatangazie makafiri kwamba yeye haabudu wanavyoviabudu miongoni mwa masanamu na waungu wa urongo. Na kwamba wao hawamwabudu Mwabudiwa Mmoja Anayestahiki kuabudiwa. Na akasisitizwa tena awaambie makafiri hayo hayo. Na kwamba wao dini yao ni ya kuabudu masanamu yasiyoweza kuwanufaisha wala kuwadhuru, na yeye Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) ana Dini Tukufu ya Uislamu ambayo ni Dini ya haki, ya kumwabudu Ilaah Mmoja Pekee, Mwenye Kusikia na Kuona, Mwenye Uwezo wa Kunufaisha na kudhuru, na Mwenye Majina Mazuri Kabisa na Sifa Tukufu ambazo hakuna anayezimiliki isipokuwa Yeye Allaah (سبحانه وتعالى). Kuwatangazia hivyo makafiri, ni kwa sababu Allaah (سبحانه وتعالى) Ni Mjuzi wa kutambua kwamba miongoni mwa hao makafiri, wako ambao hawataamini kamwe!
Fadhila Za Suwrah.
1-Ni Sunnah Kuisoma Katika Swalaah Ya Sunnah Ya Alfajiri Na Magharibi:
عن أبي هريرة رضي الله عنه : أنَّ رَسُولَ اللهِ صلى الله عليه وسلم قرأ في رَكْعَتَي الفَجْرِ: قُلْ يَا أَيُّهَا الكَافِرُونَ وَ قُلْ هُوَ اللهُ أَحَدٌ . رَوَاهُ مُسلِمٌ .
Amesimulia Abuu Hurayrah (رضي الله عنه): Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alisoma katika Rakaa mbili za Sunnah ya Alfajiri:
قُلْ يَا أَيُّهَا الْكَافِرُونَ
[Al-Kaafiruwn (109)]
Na
قُلْ هُوَ اللَّهُ أَحَدٌ
[Al-Ikhlaasw (112)]
[Muslim na wengineo]
2-Ni Sunnah Kuisoma Katika Rakaa Ya Pili Ya Swalaatul-Witr:
عَنْ سَعِيدِ بْنِ عَبْدِ الرَّحْمَنِ بْنِ أَبْزَى، عَنْ أَبِيهِ، عَنْ أُبَىِّ بْنِ كَعْبٍ، قَالَ كَانَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم يَقْرَأُ فِي الرَّكْعَةِ الأُولَى مِنَ الْوَتْرِ بِـ سَبِّحِ اسْمَ رَبِّكَ الأَعْلَى وَفِي الثَّانِيَةِ بِـ قُلْ يَا أَيُّهَا الْكَافِرُونَ وَفِي الثَّالِثَةِ بِـ قُلْ هُوَ اللَّهُ أَحَدٌ
Amesimulia Ubayy Bin Ka’b (رضي الله عنه): Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alikuwa akisoma katika Rakaah ya kwanza ya Swalaah ya Witr:
سَبِّحِ اسْمَ رَبِّكَ الأَعْلَى
[Al-A’laa (87)]
Na katika ya pili:
قُلْ يَا أَيُّهَا الْكَافِرُونَ
[Al-Kaafiruwn (109)]
Na katika ya tatu:
قُلْ هُوَ اللَّهُ أَحَدٌ
[Al-Ikhlaasw (112)]
[At-Tirmidhiy, An-Nasaaiy, na ameisahihisha Al-Albaaniy katika Swahiyh An-Nasaaiy]
3-Ni Sunnah Kuisoma Katika Maqaam Ibraahiym (Kisimamo Cha Ibraahiym) Baada Ya Kumaliza Twawaaf Ya ‘Umrah:
عَنْ جَابِرِ بْنِ عَبْدِ اللَّهِ، أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم قَرَأَ فِي رَكْعَتَىِ الطَّوَافِ بِسُورَتَىِ الإِخْلاَصِ : قُلْ يَا أَيُّهَا الْكَافِرُونَ وَ قُلْ هُوَ اللَّهُ أَحَدٌ
Amesimulia Jaabir Bin ‘Abdillaah (رضي الله عنه): Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amezisoma Suwrah zinazojulikana za ikhlaasw katika Rakaa mbili baada ya Twawaaf. Nazo ni:
قُلْ يَا أَيُّهَا الْكَافِرُونَ
Na
قُلْ هُوَ اللَّهُ أَحَدٌ
[At-Tirmidhiy]
4-Thawabu Za Kuisoma Ni Kama Thawabu Za Kusoma Robo Ya Qur-aan:
قال رسول الله صلى الله عليه وسلم :((قُلْ هو اللَّهُ أحَدٌ تعدلُ ثلثَ القرآنِ. و قُلْ يَا أيُّهَا الْكَافِرُونَ تعدلُ ربعَ القرآنِ))
Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema:
قُلْ هو اللَّهُ أحَدٌ
ni sawa na thuluthi ya Qur-aan na
قُلْ يَا أيُّهَا الْكَافِرُونَ
ni sawa na robo ya Qur-aan.” [Hadiyth ya ‘Abdullaah bin ‘Umar, ameisahihisha Al-Albaaniy Taz. Swahiyh Al-Jaami’ (4405), As-Silsilah Asw-Swahiyhah (586)]
110-An-Naswr: Utangulizi Wa Suwrah
Alhidaaya.com [2]
Imeteremka: Madiynah kwa itifaki ya ‘Ulamaa.
Idadi Za Aayah: 3
Jina La Suwrah: An-Naswr
Suwrah imeitwa An-Naswr (Nusura), na inayodalilisha ni kutajwa kwake katika Aayah namba (1).
Miongoni Mwa Makusudio Ya Suwrah:
1-Bishara kwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) juu ya ushindi unaokuja na mwisho wa Unabiy. [Al-Mukhtaswar Fiy Tafsiyr Al-Qur-aan Al-Kariym]
2-Kufahamisha kukamilika kwa Dini ya Kiislamu kwa kubashiriwa nusura na ushindi wa Makkah.
Miongoni Mwa Maudhui Ya Suwrah:
Suwrah imefunguliwa kwa bishara na Ahadi ya Allaah (سبحانه وتعالى) kwa Rasuli Wake (صلى الله عليه وآله وسلم) ya ushindi juu ya ukafiri wa Maquraysh na Fat-h (Ufunguzi wa) Makkah. Na bishara ya makundi kwa makundi ya watu kuingia katika Dini ya Uislamu. Na Suwrah ikakhitimishwa kwa kumuamrisha Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) ashikamane na Tasbiyh (Kumtakasa Allaah) na Tahmiyd (Kumhimidi Allaah), na Istighfaar (Kuomba Maghfirah).
Fadhila Za Suwrah:
Ni Suwrah Ya Mwisho Iliyoteremshwa Kamili:
عَنْ عُبَيْدِ اللَّهِ بْنِ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ عُتْبَةَ، قَالَ قَالَ لِيَ ابْنُ عَبَّاسٍ تَعْلَمُ - وَقَالَ هَارُونُ تَدْرِي - آخِرَ سُورَةٍ نَزَلَتْ مِنَ الْقُرْآنِ نَزَلَتْ جَمِيعًا قُلْتُ نَعَمْ . إِذَا جَاءَ نَصْرُ اللَّهِ وَالْفَتْحُ قَالَ صَدَقْتَ . وَفِي رِوَايَةِ ابْنِ أَبِي شَيْبَةَ تَعْلَمُ أَىُّ سُورَةٍ . وَلَمْ يَقُلْ آخِرَ .
Amesimulia ‘Ubaydullaah Bin ‘Abdillaah Bin ‘Utbah (رضي الله عنه): Ibn ‘Abbaas (رضي الله عنهما) ameniambia: Je unajua- na katika maneno ya Haaruwn (msimulizi mwengine): “Unajua Suwrah ya mwisho ya Qur-aan kuteremka ikiwa kamili?” Nikajibu: Naam.
إِذَا جَاءَ نَصْرُ اللَّـهِ وَالْفَتْحُ ﴿١﴾
“Itakapokuja Nusura ya Allaah na ushindi.”
Akasema: Umesema kweli. Na katika usimulilzi wa Abu Shaybha (maneno yalikuwa): “Je unajua Suwrah gani.” Lakini hakutaja “Ya mwisho.” [Muslim]
111-Al-Masad: Utangulizi Wa Suwrah
Alhidaaya.com [2]
Imeteremka: Makkah kwa itifaki ya ‘Ulamaa.
Idadi Za Aayah: 5
Jina La Suwrah: Al-Masad
Suwrah imeitwa Al-Masad (Msokoto Madhubuti), na inayodalilisha ni kutajwa kwake katika Aayah namba (1).
Miongoni Mwa Makusudio Ya Suwrah:
1-Kubainisha khasara aliyoipata Abuu Lahb pamoja na mkewe. [Al-Mukhtaswar Fiy Tafsiyr Al-Qur-aan Al-Kariym]
2-Kutaja dhulma ya Abuu Lahab na mkewe waliomfanyia Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) na kubainishwa adhabu zao.
Miongoni Mwa Maudhui Ya Suwrah:
Suwrah imeelezea khasara ya Abuu Lahab na kuangamia kwake pamoja na mkewe na kupata khasara, kwa sababu ya kumfanyia maudhi Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم). Ikatajwa kwamba mali ya Abuu Lahab haikuweza kumnufaisha katika kumkinga na Adhabu ya Allaah. Basi ameahidiwa yeye kuingizwa moto uwakao vikali mno! Na mkewe, ambaye alikuwa akibeba miba na kuiweka katika njia anayopita Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) ili imchome na kumjeruhi, ameahidiwa kuingia motoni akiwa amefungwa shingoni mwake, kuti kavu la mtende lililo madhubuti, abebwe nalo kwenye moto wa Jahannam, kisha arushwe nalo mpaka chini humo.
112-Al-Ikhlaasw: Utangulizi Wa Suwrah
Alhidaaya.com [2]
Imeteremka: Makkah au Madiynah kwani ‘Ulamaa wamekhitilafiana kuhusu wapi imeteremshwa.
Idadi Za Aayah: 4
Jina La Suwrah: Al-Ikhlaasw
Suwrah imeitwa Al-Ikhlaasw (Ikhlasi), na inayodalilisha ni kutajwa katika Hadiyth zilizonukuliwa katika Fadhila na kutajwa kwake katika Aayah namba (1).
Miongoni Mwa Makusudio Ya Suwrah:
1-Kumpwekesha Allaah (سبحانه وتعالى) kwa ibaada na ukamilifu, na Kumtakasa kutokana kuzaa au kuwa na mwana, na kufanana na yeyote. [Al-Mukhtaswar Fiy Tafsiyr Al-Qur-aan Al-Kariym]
2-Kuthibitisha Tawhiyd ya Allaah (سبحانه وتعالى) na kwamba Yeye Ni Mkusudiwa wa kila kitu.
Miongoni Mwa Maudhui Ya Suwrah:
Suwrah imethibitisha Tawhiyd ya Allaah (سبحانه وتعالى) kwamba Yeye Ni Mmoja Pekee, Mwenye kustahiki kuabudiwa kwa haki. Naye Ndiye Asw-Swamad; Mweza na Mkusudiwa Pekee wa kukidhi haja za waja. Wala Hana Mwana wala mzazi wala mke; Ametakasika na kuhitaji hayo. Wala hakuna yeyote katika viumbe Vyake (سبحانه وتعالى) mwenye kufanana wala kushabihiyana na Yeye katika Majina Yake, Sifa Zake wala Vitendo Vyake.
Fadhila Za Suwrah:
Suwrah hii ina fadhila nyingi mno. Miongoni mwa fadhila zake ni:
1-Sunnah Kuisoma Katika Swalaah Za Sunnah Kama Sunnah Ya Alfajiri na Magharibi, Swalaah Ya Witr, Swalaah Katika Maqaam Ibraahiym Baada Ya Twawaaf: Rejea Suwrah Al-Kaafiruwn (109) kulikotajwa fadhila hizi.
2- Thawabu Za Kuisoma Ni Kama Thawabu Za Kusoma Thuluthi Ya Qur-aan:
عَنْ أَبِي سَعِيدٍ أَنَّ رَجُلًا سَمِعَ رَجُلًا يَقْرَأُ قُلْ هُوَ اللَّهُ أَحَدٌ يُرَدِّدُهَا، فَلَمَّا أَصْبَحَ جَاءَ إِلَى رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ فَذَكَرَ ذَلِكَ لَهُ ، وَكَأَنَّ الرَّجُلَ يَتَقَالُّهَا أي يراها قليلة فَقَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ : ((وَالَّذِي نَفْسِي بِيَدِهِ إِنَّهَا لَتَعْدِلُ ثُلُثَ الْقُرْآن))
Amesimulia Abuu Sa’iyd Al-Khudriyy (رضي الله عنه): Mtu mmoja alimsikia mtu akisoma
قُلْ هُوَ اللَّهُ أَحَدٌ
na akiikariri. Asubuhi yake akamwendea Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akamtajia hilo na alidhania kuwa ni kisomo kidogo tu. Lakini Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akasema: “Naapa kwa Ambaye nafsi yangu imo Mikononi Mwake, hiyo ni sawa na thuluthi ya Qur-aan.” [Al-Bukhaariy]
na pia:
عَنْ أَبِي الدَّرْدَاءِ، عَنِ النَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم قَالَ " أَيَعْجِزُ أَحَدُكُمْ أَنْ يَقْرَأَ فِي لَيْلَةٍ ثُلُثَ الْقُرْآنِ " قَالُوا : وَكَيْفَ يَقْرَأْ ثُلُثَ الْقُرْآنِ ؟ قَالَ : " قُلْ هُوَ اللَّهُ أَحَدٌ تَعْدِلُ ثُلُثَ الْقُرْآنِ "
Amesimulia Abuu Ad-Dardaa (رضي الله عنه) : Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema:
“Kuna yeyote kati yenu anayeishindwa kusoma thuluthi ya Qur-aan usiku?” Swahaba wakauliza: Vipi mtu aweze kusoma thuluthi ya Qur-aan? Akasema:
قُلْ هُوَ اللَّهُ أَحَدٌ
Ni sawa na thuluthi ya Qur-aan. [Al-Bukhaariy na Muslim]
3-Kuisoma Katika Adhkaar Za Asubuhi Na Jioni Na Adhkaar Za Kulala Kumkinga Mtu Na Kila Shari.
عَنْ عَائِشَةَ، أَنَّ النَّبِيَّ صلى الله عليه وسلم كَانَ إِذَا أَوَى إِلَى فِرَاشِهِ كُلَّ لَيْلَةٍ جَمَعَ كَفَّيْهِ ثُمَّ نَفَثَ فِيهِمَا فَقَرَأَ فِيهِمَا قُلْ هُوَ اللَّهُ أَحَدٌ وَ قُلْ أَعُوذُ بِرَبِّ الْفَلَقِ وَ قُلْ أَعُوذُ بِرَبِّ النَّاسِ ثُمَّ يَمْسَحُ بِهِمَا مَا اسْتَطَاعَ مِنْ جَسَدِهِ يَبْدَأُ بِهِمَا عَلَى رَأْسِهِ وَوَجْهِهِ وَمَا أَقْبَلَ مِنْ جَسَدِهِ يَفْعَلُ ذَلِكَ ثَلاَثَ مَرَّاتٍ.
Amesimulia ‘Aaishah (رضي الله عنها): Pindi Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alipoingia kitandani kila usiku, alikuwa akikusanya vitanga vyake vya mikono na kupuliza juu yake baada ya kusoma:
قُلْ هُوَ اللَّـهُ أَحَدٌ ﴿١﴾
na
قُلْ أَعُوذُ بِرَبِّ الْفَلَقِ ﴿١﴾
na
قُلْ أَعُوذُ بِرَبِّ النَّاسِ ﴿١﴾
Kisha akipangusa kwa mikono yake sehemu za mwili wake ambazo alikuwa anaweza kuzipangusa, akianza na kichwa chake, uso wake na sehemu yake ya mbele ya mwili. Alikuwa akifanya hivyo mara tatu. [Al-Bukhaariy]
Na pia
عَنْ مُعَاذِ بْنِ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ خُبَيْبٍ، عَنْ أَبِيهِ، أَنَّهُ قَالَ خَرَجْنَا فِي لَيْلَةِ مَطَرٍ وَظُلْمَةٍ شَدِيدَةٍ نَطْلُبُ رَسُولَ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم لِيُصَلِّيَ لَنَا فَأَدْرَكْنَاهُ فَقَالَ " أَصَلَّيْتُمْ " . فَلَمْ أَقُلْ شَيْئًا فَقَالَ " قُلْ " . فَلَمْ أَقُلْ شَيْئًا ثُمَّ قَالَ " قُلْ " . فَلَمْ أَقُلْ شَيْئًا ثُمَّ قَالَ " قُلْ " . فَقُلْتُ يَا رَسُولَ اللَّهِ مَا أَقُولُ قَالَ قُلْ هُوَ اللَّهُ أَحَدٌ وَالْمُعَوِّذَتَيْنِ حِينَ تُمْسِي وَحِينَ تُصْبِحُ ثَلاَثَ مَرَّاتٍ تَكْفِيكَ مِنْ كُلِّ شَىْءٍ " .
Amesimulia Mu’aadh Bin ‘Abdillaah Bin Khubayb kutoka kwa baba yake (رضي الله عنهما): Tulitoka usiku mmoja wenye mvua nyingi na kiza kilichotanda, kwenda kumtafuta Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) ili atuongoze katika Swalaah. Tulipomkuta aliuliza: “Je, mmeswali?” Lakini mimi sikusema chochote. Akasema: “Sema.” Lakini mimi sikusema chochote. Akasema tena: “Sema.” Lakini mimi sikusema lolote. Kisha akasema: “Sema.” Basi nikasema: Ee Rasuli wa Allaah, niseme nini? Akasema:
قُلْ هُوَ اللَّهُ أَحَدٌ
Na Al-Mu’awwidhatayn, mara tatu asubuhi na jioni, zitakutosheleza na kila kitu. [At-Tirmidhiy, Abuu Daawuwd na ameisahihisha Al-Albaaniy katika Swahiyh At-Tirmidhiy (3575), Swahiyh Abiy Daawuwd (5082)]
Al-Mu’awwidhatayn ni Suwrah Al-Falaq (113) na An-Naas (114).
4-Kupenda Kuisoma Ni Sababu Mojawapo Ya Kupata Mapenzi Ya Allaah:
عَنْ عَائِشَةَ أَنَّ النَّبِيَّ صلى الله عليه وسلم بَعَثَ رَجُلاً عَلَى سَرِيَّةٍ، وَكَانَ يَقْرَأُ لأَصْحَابِهِ فِي صَلاَتِهِ فَيَخْتِمُ بِ ـ قُلْ هُوَ اللَّهُ أَحَدٌ فَلَمَّا رَجَعُوا ذَكَرُوا ذَلِكَ لِلنَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم فَقَالَ " سَلُوهُ لأَىِّ شَىْءٍ يَصْنَعُ ذَلِكَ ". فَسَأَلُوهُ فَقَالَ لأَنَّهَا صِفَةُ الرَّحْمَنِ، وَأَنَا أُحِبُّ أَنْ أَقْرَأَ بِهَا. فَقَالَ النَّبِيُّ صلى الله عليه وسلم " أَخْبِرُوهُ أَنَّ اللَّهَ يُحِبُّهُ "
Amesimulia ‘Aaishah (رضي الله عنها): Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alituma kikosi cha jeshi chini ya uongozi wa mtu aliyekuwa akiwaongoza Swahaba zake katika Swalaah. Akawa katika Swalaah zake zote alizokuwa akiswalisha wenzake, akikhitimisha kwa kusoma:
قُل هُوَ الله أَحَدٌ
Waliporudi (Madiynah), Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alitajiwa hilo, naye akawaambia: "Muulizeni ni kwa sababu gani anafanya hivyo?" Wakamuuliza, naye akasema: Kwa sababu humo ndani zipo Sifa za Ar-Rahmaan (Mwingi wa Rehma), nami napenda kuzisoma. Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akasema: "Mpeni khabari kwamba Allaah (سبحانه وتعالى) Anampenda." [Al-Bukhaariy na Muslim]
5-Kuisoma Katika Duaa Ni Sababu Ya Kutaqabaliwa Duaa:
عن عَبْدِ اللَّهِ بن بُرَيْدَةَ الأسْلَمِيِّ عن أبِيهِ (رضي الله عنهما) قال: سَمِعَ النَّبِيُّ (صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ) رَجُلاً يَدْعُو وَهُوَ يَقُولُ: "اللَّهُمَّ إنِّي أسْأَلُكَ بِأنِّي أشْهَدُ أنَّكَ أنْتَ اللَّهُ لا إِلَهَ إِلاَّ أنْتَ الأحَدُ الصَّمَدُ الَّذِي لَمْ يَلِدْ وَلَمْ يُولَدْ وَلَمْ يَكُنْ لَهُ كُفُوًا أحَدٌ" فقال: ((وَالَّذِي نَفْسِي بِيَدِهِ لَقَدْ سَألَ اللَّهَ بِاسْمِهِ الأعْظَمِ الَّذِي إذَا دُعِيَ بِهِ أجَابَ وَإذَا سُئِلَ بِهِ أعْطَى))
Amesimulia ‘Abdullaah bin Buraydah Al-Aslamiyy, kutoka kwa baba yake (رضي الله عنهما): Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alimsikia mtu akiomba:
"اللَّهُمَّ إنِّي أسْأَلُكَ بِأنِّي أشْهَدُ أنَّكَ أنْتَ اللَّهُ لا إِلَهَ إِلاَّ أنْتَ الأحَدُ الصَّمَدُ الَّذِي لَمْ يَلِدْ وَلَمْ يُولَدْ وَلَمْ يَكُنْ لَهُ كُفُوًا أحَدٌ"
Ee Allaah, hakika mimi nakuomba kwa kushuhudia kwamba hakika Wewe ni Allaah, hapana mwabudiwa wa haki isipokuwa Wewe, Mmoja Pekee, Aliyekamilika Sifa za Utukufu Wake, Mkusudiwa haja zote, Ambaye Hakuzaa wala Hakuzaliwa, na wala haiwi Awe na yeyote anayefanana na kulingana Naye. Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akasema: “Naapa kwa Ambaye nafsi yangu imo Mikononi Mwake, amemuomba Allaah kwa Jina Lake Adhimu kabisa Ambalo Anapoombwa kwalo (duaa) Anaitikia na Anapotakwa kwalo (jambo) Hutoa)) [Swahiyh Ibn Maajah (3125) Swahiyh At-Tirmidhy (3475), Swahiyh Abi Daawuwd (1493), Swahiyh At-Targhiyb (1640)]
6-Kupenda Kuisoma Ni Sababu Ya Kuingizwa Jannah:
Rejea Hadiyth Za Al-Bukhaariy Namba (774B) katika Mlango Wa Kusoma Suwrah Mbili Katika Rakaa Moja Katika
7-Ni Sunnah Kuisoma Kila Baada Ya Kumaliza Swalaah Za Fardhi Pamoja Na Al-Mu’awwidhatayn [Suwrah Al-Falaq (113) na An-Naas (114)]
113-Al-Falaq: Utangulizi Wa Suwrah
Alhidaaya.com [2]
Imeteremka: Makkah au Madiynah kwani ‘Ulamaa wamekhitilafiana kuhusu wapi imeteremshwa.
Idadi Za Aayah: 5
Jina La Suwrah: Al-Falaq
Suwrah imeitwa Al-Falaq (Mapambazuko), na inayodalilisha ni kutajwa kwake katika Hadiyth zilizonukuliwa katika Fadhila na kutajwa kwake katika Aayah namba (1).
Miongoni Mwa Makusudio Ya Suwrah:
1-Mahimizo juu ya kushikamana na Allaah kutokana na shari zote. [Al-Mukhtaswar Fiy Tafsiyr Al-Qur-aan Al-Kariym]
2-Kujilinda na aina zote za shari, kwa ujumla, na khasa kutokana na shari za usiku, sihri na uhasidi.
Miongoni Mwa Maudhui Ya Suwrah:
Suwrah imefunguliwa kwa amri ya kujilinda kwa Rabb wa mapambazuko ya asubuhi na usiku kutokana na shari za viumbe vyote; wanaadamu, majini na wanyama. Na kuomba kinga ya shari zilioko usiku kutokana na viumbe vinavyofichika, na shari za wachawi wenye kupuliza kwenye mafundo wanayoyafunga kwa lengo la kuroga. Na kinga kutokana na shari za hasidi mwenye kuhusudu watu, kwa kutaka Neema za Allaah (سبحانه وتعالى) Alizomneemesha mtu zimuondoke.
Fadhila Za Suwrah:
Suwrah hii ina fadhila nyingi mno. Miongoni mwa fadhila zake ni:
1-Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) Alikuwa Anajisomea Kila Alipoumwa:
حَدَّثَنَا عَبْدُ اللَّهِ بْنُ يُوسُفَ، أَخْبَرَنَا مَالِكٌ، عَنِ ابْنِ شِهَابٍ، عَنْ عُرْوَةَ، عَنْ عَائِشَةَ، رضى الله عنها أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم كَانَ إِذَا اشْتَكَى يَقْرَأُ عَلَى نَفْسِهِ بِالْمُعَوِّذَاتِ وَيَنْفُثُ، فَلَمَّا اشْتَدَّ وَجَعُهُ كُنْتُ أَقْرَأُ عَلَيْهِ وَأَمْسَحُ بِيَدِهِ رَجَاءَ بَرَكَتِهَا.
Amesimulia ‘Urwah (رضي الله عنه): ‘Aaishah (رضي الله عنها) amesema: Pindi Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alipokuwa anaumwa, anajisomea mwenyewe Al-Mu‘awwidhaat na anapuliza katika vitanga vyake vya mikono na anajifuta kwavyo mwili wake. Ugonjwa ulipomzidi nilikuwa ninamsomea, na ninafuta kwa mkono wake nikitaraji baraka zake (mkono). [Al-Bukhaariy na Muslim]
Al-Mu‘awwidhaat ni Al-Falaq (113) na An-Naas (114).
2-Ni Sunnah Kuisoma Katika Swalaah Ya Witr:
عَنْ عَبْدِ الْعَزِيزِ بْنِ جُرَيْجٍ، قَالَ سَأَلْنَا عَائِشَةَ بِأَىِّ شَىْءٍ كَانَ يُوتِرُ رَسُولُ اللَّهِ ـ صلى الله عليه وسلم ـ قَالَتْ كَانَ يَقْرَأُ فِي الرَّكْعَةِ الأُولَى بِـ سَبِّحِ اسْمَ رَبِّكَ الأَعْلَى وَفِي الثَّانِيَةِ قُلْ يَا أَيُّهَا الْكَافِرُون وَفِي الثَّالِثَةِ قُلْ هُوَ اللَّهُ أَحَدٌ وَالْمُعَوِّذَتَيْنِ .
Amesimulia ‘Abdul-‘Aziyz Bin Jurayj (رضي الله عنه): Tulimuuliza ‘Aaishah (رضي الله عنها); Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alikuwa akisoma nini katika Swalaah ya Witr? Akasema: Alikuwa akisoma katika Rakaa ya kwanza:
سَبِّحِ اسْمَ رَبِّكَ الأَعْلَى
Na katika ya pili:
قُلْ يَا أَيُّهَا الْكَافِرُونَ
Na katika ya tatu:
قُلْ هُوَ اللَّهُ أَحَدٌ
Na Al-Mu’awwidhatayni. [Ibn Maajah, At-Tirmidhiy na ameisahihisha Al-Albaaniy katika Swahiyh At-Tirmidhiy (463)]
3-Kuisoma Katika Adhkaar Za Asubuhi Na Jioni Na Adhkaar Za Kulala Kumkinga Mtu Na Kila Shari.
عَنْ عَائِشَةَ، أَنَّ النَّبِيَّ صلى الله عليه وسلم كَانَ إِذَا أَوَى إِلَى فِرَاشِهِ كُلَّ لَيْلَةٍ جَمَعَ كَفَّيْهِ ثُمَّ نَفَثَ فِيهِمَا فَقَرَأَ فِيهِمَا قُلْ هُوَ اللَّهُ أَحَدٌ وَ قُلْ أَعُوذُ بِرَبِّ الْفَلَقِ وَ قُلْ أَعُوذُ بِرَبِّ النَّاسِ ثُمَّ يَمْسَحُ بِهِمَا مَا اسْتَطَاعَ مِنْ جَسَدِهِ يَبْدَأُ بِهِمَا عَلَى رَأْسِهِ وَوَجْهِهِ وَمَا أَقْبَلَ مِنْ جَسَدِهِ يَفْعَلُ ذَلِكَ ثَلاَثَ مَرَّاتٍ.
Amesimulia ‘Aaishah (رضي الله عنها): Pindi Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alipoingia kitandani kila usiku, alikuwa akikusanya vitanga vyake vya mikono na kupuliza juu yake baada ya kusoma:
قُلْ هُوَ اللَّـهُ أَحَدٌ ﴿١﴾
na
قُلْ أَعُوذُ بِرَبِّ الْفَلَقِ ﴿١﴾
na
قُلْ أَعُوذُ بِرَبِّ النَّاسِ ﴿١﴾
Kisha akipangusa kwa mikono yake sehemu za mwili wake ambazo alikuwa anaweza kuzipangusa, akianza na kichwa chake, uso wake na sehemu yake ya mbele ya mwili. Alikuwa akifanya hivyo mara tatu. [Al-Bukhaariy]
4-Haijapata Kuteremshwa Kabla Katika Tawraat Wala Injiyl:
عَنْ عُقْبَةَ بْنِ عَامِرٍ، قَالَ قَالَ لِي رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم " أُنْزِلَ - أَوْ أُنْزِلَتْ - عَلَىَّ آيَاتٌ لَمْ يُرَ مِثْلُهُنَّ قَطُّ الْمُعَوِّذَتَيْنِ "
Amesimulia ‘Uqbah Bin ‘Aamir (رضي الله عنه): Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: zimeteremshwa -au nimeteremshiwa Aayaat ambazo hazijapata kuteremshwa kabla. Nazo ni Al-Mu’awwidhatayni [Muslim] Na katika Riwaaya: “Nimeteremshiwa usiku.”
Al-Mu’awwidhatayni ni Al-Falaq (113) na An-Naas (114)
5-Ni Sunnah Kuisoma Kila Baada Ya Kumaliza Swalaah Za Fardhi Pamoja na Al-Ikhlaasw (112) na An-Naas (114).
عَنْ عُقْبَةَ بْنِ عَامِرٍ، قَالَ أَمَرَنِي رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم أَنْ أَقْرَأَ الْمُعَوِّذَاتِ دُبُرَ كُلِّ صَلاَةٍ .
Amesimulia ‘Uqbah Bin ‘Aamir (رضي الله عنه): Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) ameniamrisha nisome Al-Mu’awwidhaat kila baada ya Swalaah. [At-Tirmidhiy, An-Nasaaiy, Abuu Daawuwd na ameisahihisha Al-Albaaniy katika Swahiyh Abiy Daawuwd (1523)]
114-An-Naas: Utangulizi Wa Suwrah
Alhidaaya.com [2]
Imeteremka: Makkah au Madiynah kwani ‘Ulamaa wamekhitilafiana kuhusu wapi imeteremshwa.
Idadi Za Aayah: 6
Jina La Suwrah: An-Naas
Suwrah imeitwa An-Naas (Watu), na inayodalilisha ni kutajwa kwake katika Hadiyth zilizonukuliwa katika Fadhila na kutajwa kwake katika Aayah namba (1).
Miongoni Mwa Makusudio Muhimu Ya Suwrah:
Mahimizo juu ya kujilinda (kutaka hifadhi) kwa Allah kutokana na shari za Mashetani na wasiwasi wao. [Al-Mukhtaswar Fiy Tafsiyr Al-Qur-aan Al-Kariym]
Miongoni Mwa Maudhui Ya Suwrah:
Suwrah imefunguliwa kwa amri ya kujilinda na shari, kwa Rabb wa wanaadam, Ambaye ni Mfalme wa wanaadam Mwenye Kumiliki kila kitu ulimwenguni na Mwenye Kuyaendesha mambo ya walimwengu Anavyotaka. Kunapasa kujilinda Naye (سبحانه وتعالى) kwa sababu, Yeye Pekee Ndiye Mweza wa kurudisha shari hizo. Na Yeye Allaah (سبحانه وتعالى) Ndiye Ambaye hakuna apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Yeye. Na pia kujilinda kutokana na shari ya shaytwaan ambae katika sifa zake, hujificha na kuchochea watu, na kutia wasiwasi katika nyoyo za wanaadam. Na kwamba yeye (shaytwaan) anaweza kuwa katika majini na anaweza kua katika watu.
Fadhila Za Suwrah:
Suwrah hii ina fadhila nyingi mno. Miongoni mwa fadhila zake ni:
1-Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) Alikuwa Anajisomea Kila Alipoumwa:
حَدَّثَنَا عَبْدُ اللَّهِ بْنُ يُوسُفَ، أَخْبَرَنَا مَالِكٌ، عَنِ ابْنِ شِهَابٍ، عَنْ عُرْوَةَ، عَنْ عَائِشَةَ، رضى الله عنها أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم كَانَ إِذَا اشْتَكَى يَقْرَأُ عَلَى نَفْسِهِ بِالْمُعَوِّذَاتِ وَيَنْفُثُ، فَلَمَّا اشْتَدَّ وَجَعُهُ كُنْتُ أَقْرَأُ عَلَيْهِ وَأَمْسَحُ بِيَدِهِ رَجَاءَ بَرَكَتِهَا.
Amesimulia ‘Urwah (رضي الله عنه): ‘Aaishah (رضي الله عنها) amesema: Pindi Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alipokuwa anaumwa, anajisomea mwenyewe Al-Mu‘awwidhaat na anapuliza katika vitanga vyake vya mikono na anajifuta kwavyo mwili wake. Ugonjwa ulipomzidi nilikuwa ninamsomea, na ninafuta kwa mkono wake nikitaraji baraka zake (mkono). [Al-Bukhaariy na Muslim]
Al-Mu‘awwidhaat ni Al-Falaq (113) na An-Naas (114).
2-Ni Sunnah Kuisoma Katika Swalaah Ya Witr:
عَنْ عَبْدِ الْعَزِيزِ بْنِ جُرَيْجٍ، قَالَ سَأَلْنَا عَائِشَةَ بِأَىِّ شَىْءٍ كَانَ يُوتِرُ رَسُولُ اللَّهِ ـ صلى الله عليه وسلم ـ قَالَتْ كَانَ يَقْرَأُ فِي الرَّكْعَةِ الأُولَى بِـ سَبِّحِ اسْمَ رَبِّكَ الأَعْلَى وَفِي الثَّانِيَةِ قُلْ يَا أَيُّهَا الْكَافِرُون وَفِي الثَّالِثَةِ قُلْ هُوَ اللَّهُ أَحَدٌ وَالْمُعَوِّذَتَيْنِ .
Amesimulia ‘Abdul-‘Aziyz Bin Jurayj (رضي الله عنه): Tulimuuliza ‘Aaishah (رضي الله عنها); Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alikuwa akisoma nini katika Swalaah ya Witr? Akasema: Alikuwa akisoma katika Rakaa ya kwanza:
سَبِّحِ اسْمَ رَبِّكَ الأَعْلَى
Na katika ya pili:
قُلْ يَا أَيُّهَا الْكَافِرُونَ
Na katika ya tatu:
قُلْ هُوَ اللَّهُ أَحَدٌ
Na Al-Mu’awwidhatayni. [Ibn Maajah, At-Tirmidhiy na ameisahihisha Al-Albaaniy katika Swahiyh At-Tirmidhiy (463)]
3-Kuisoma Katika Adhkaar Za Asubuhi Na Jioni Na Adhkaar Za Kulala Kumkinga Mtu Na Kila Shari.
عَنْ عَائِشَةَ، أَنَّ النَّبِيَّ صلى الله عليه وسلم كَانَ إِذَا أَوَى إِلَى فِرَاشِهِ كُلَّ لَيْلَةٍ جَمَعَ كَفَّيْهِ ثُمَّ نَفَثَ فِيهِمَا فَقَرَأَ فِيهِمَا قُلْ هُوَ اللَّهُ أَحَدٌ وَ قُلْ أَعُوذُ بِرَبِّ الْفَلَقِ وَ قُلْ أَعُوذُ بِرَبِّ النَّاسِ ثُمَّ يَمْسَحُ بِهِمَا مَا اسْتَطَاعَ مِنْ جَسَدِهِ يَبْدَأُ بِهِمَا عَلَى رَأْسِهِ وَوَجْهِهِ وَمَا أَقْبَلَ مِنْ جَسَدِهِ يَفْعَلُ ذَلِكَ ثَلاَثَ مَرَّاتٍ.
Amesimulia ‘Aaishah (رضي الله عنها): Pindi Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alipoingia kitandani kila usiku, alikuwa akikusanya vitanga vyake vya mikono na kupuliza juu yake baada ya kusoma:
قُلْ هُوَ اللَّـهُ أَحَدٌ ﴿١﴾
na
قُلْ أَعُوذُ بِرَبِّ الْفَلَقِ ﴿١﴾
na
قُلْ أَعُوذُ بِرَبِّ النَّاسِ ﴿١﴾
Kisha akipangusa kwa mikono yake sehemu za mwili wake ambazo alikuwa anaweza kuzipangusa, akianza na kichwa chake, uso wake na sehemu yake ya mbele ya mwili. Alikuwa akifanya hivyo mara tatu. [Al-Bukhaariy]
4-Haijapata Kuteremshwa Kabla Katika Tawraat Wala Injiyl:
عَنْ عُقْبَةَ بْنِ عَامِرٍ، قَالَ قَالَ لِي رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم " أُنْزِلَ - أَوْ أُنْزِلَتْ - عَلَىَّ آيَاتٌ لَمْ يُرَ مِثْلُهُنَّ قَطُّ الْمُعَوِّذَتَيْنِ "
Amesimulia ‘Uqbah Bin ‘Aamir (رضي الله عنه): Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: zimeteremshwa -au nimeteremshiwa Aayaat ambazo hazijapata kuteremshwa kabla. Nazo ni Al-Mu’awwidhatayni [Muslim] Na katika Riwaaya: Nimeteremshiwa usiku..
Al-Mu’awwidhatayni ni Al-Falaq (113) na An-Naas (114)
5-Ni Sunnah Kuisoma Kila Baada Ya Kumaliza Swalaah Za Fardhi Pamoja na Al-Ikhlaasw (112) na An-Naas (114).
عَنْ عُقْبَةَ بْنِ عَامِرٍ، قَالَ أَمَرَنِي رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم أَنْ أَقْرَأَ الْمُعَوِّذَاتِ دُبُرَ كُلِّ صَلاَةٍ .
Amesimulia ‘Uqbah Bin ‘Aamir (رضي الله عنه): Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) ameniamrisha nisome Al-Mu’awwidhaat kila baada ya Swalaah. [At-Tirmidhiy, An-Nasaaiy, Abuu Daawuwd na ameisahihisha Al-Albaaniy katika Swahiyh Abiy Daawuwd (1523)]
114-An-Naas: Utangulizi Wa Suwrah
Alhidaaya.com [2]
Imeteremka: Makkah au Madiynah kwani ‘Ulamaa wamekhitilafiana kuhusu wapi imeteremshwa.
Idadi Za Aayah: 6
Jina La Suwrah: An-Naas
Suwrah imeitwa An-Naas (Watu), na inayodalilisha ni kutajwa kwake katika Hadiyth zilizonukuliwa katika Fadhila na kutajwa kwake katika Aayah namba (1).
Miongoni Mwa Makusudio Ya Suwrah:
Mahimizo juu ya kujilinda (kutaka hifadhi) kwa Allah kutokana na shari za Mashetani na wasiwasi wao. [Al-Mukhtaswar Fiy Tafsiyr Al-Qur-aan Al-Kariym]
Miongoni Mwa Maudhui Ya Suwrah:
Suwrah imefunguliwa kwa amri ya kujilinda na shari, kwa Rabb wa wanaadam, Ambaye ni Mfalme wa wanaadam Mwenye Kumiliki kila kitu ulimwenguni na Mwenye Kuyaendesha mambo ya walimwengu Anavyotaka. Kunapasa kujilinda Naye (سبحانه وتعالى) kwa sababu, Yeye Pekee Ndiye Mweza wa kurudisha shari hizo. Na Yeye Allaah (سبحانه وتعالى) Ndiye Ambaye hakuna apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Yeye. Na pia kujilinda kutokana na shari ya shaytwaan ambae katika sifa zake, hujificha na kuchochea watu, na kutia wasiwasi katika nyoyo za wanaadam. Na kwamba yeye (shaytwaan) anaweza kuwa katika majini na anaweza kua katika watu.
Fadhila Za Suwrah:
Suwrah hii ina fadhila nyingi mno. Miongoni mwa fadhila zake ni:
1-Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) Alikuwa Anajisomea Kila Alipoumwa:
حَدَّثَنَا عَبْدُ اللَّهِ بْنُ يُوسُفَ، أَخْبَرَنَا مَالِكٌ، عَنِ ابْنِ شِهَابٍ، عَنْ عُرْوَةَ، عَنْ عَائِشَةَ، رضى الله عنها أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم كَانَ إِذَا اشْتَكَى يَقْرَأُ عَلَى نَفْسِهِ بِالْمُعَوِّذَاتِ وَيَنْفُثُ، فَلَمَّا اشْتَدَّ وَجَعُهُ كُنْتُ أَقْرَأُ عَلَيْهِ وَأَمْسَحُ بِيَدِهِ رَجَاءَ بَرَكَتِهَا.
Amesimulia ‘Urwah (رضي الله عنه): ‘Aaishah (رضي الله عنها) amesema: Pindi Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alipokuwa anaumwa, anajisomea mwenyewe Al-Mu‘awwidhaat na anapuliza katika vitanga vyake vya mikono na anajifuta kwavyo mwili wake. Ugonjwa ulipomzidi nilikuwa ninamsomea, na ninafuta kwa mkono wake nikitaraji baraka zake (mkono). [Al-Bukhaariy na Muslim]
Al-Mu‘awwidhaat ni Al-Falaq (113) na An-Naas (114).
2-Ni Sunnah Kuisoma Katika Swalaah Ya Witr:
عَنْ عَبْدِ الْعَزِيزِ بْنِ جُرَيْجٍ، قَالَ سَأَلْنَا عَائِشَةَ بِأَىِّ شَىْءٍ كَانَ يُوتِرُ رَسُولُ اللَّهِ ـ صلى الله عليه وسلم ـ قَالَتْ كَانَ يَقْرَأُ فِي الرَّكْعَةِ الأُولَى بِـ سَبِّحِ اسْمَ رَبِّكَ الأَعْلَى وَفِي الثَّانِيَةِ قُلْ يَا أَيُّهَا الْكَافِرُون وَفِي الثَّالِثَةِ قُلْ هُوَ اللَّهُ أَحَدٌ وَالْمُعَوِّذَتَيْنِ .
Amesimulia ‘Abdul-‘Aziyz Bin Jurayj (رضي الله عنه): Tulimuuliza ‘Aaishah (رضي الله عنها); Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alikuwa akisoma nini katika Swalaah ya Witr? Akasema: Alikuwa akisoma katika Rakaa ya kwanza:
سَبِّحِ اسْمَ رَبِّكَ الأَعْلَى
Na katika ya pili:
قُلْ يَا أَيُّهَا الْكَافِرُونَ
Na katika ya tatu:
قُلْ هُوَ اللَّهُ أَحَدٌ
Na Al-Mu’awwidhatayni. [Ibn Maajah, At-Tirmidhiy na ameisahihisha Al-Albaaniy katika Swahiyh At-Tirmidhiy (463)]
3-Kuisoma Katika Adhkaar Za Asubuhi Na Jioni Na Adhkaar Za Kulala Kumkinga Mtu Na Kila Shari.
عَنْ عَائِشَةَ، أَنَّ النَّبِيَّ صلى الله عليه وسلم كَانَ إِذَا أَوَى إِلَى فِرَاشِهِ كُلَّ لَيْلَةٍ جَمَعَ كَفَّيْهِ ثُمَّ نَفَثَ فِيهِمَا فَقَرَأَ فِيهِمَا قُلْ هُوَ اللَّهُ أَحَدٌ وَ قُلْ أَعُوذُ بِرَبِّ الْفَلَقِ وَ قُلْ أَعُوذُ بِرَبِّ النَّاسِ ثُمَّ يَمْسَحُ بِهِمَا مَا اسْتَطَاعَ مِنْ جَسَدِهِ يَبْدَأُ بِهِمَا عَلَى رَأْسِهِ وَوَجْهِهِ وَمَا أَقْبَلَ مِنْ جَسَدِهِ يَفْعَلُ ذَلِكَ ثَلاَثَ مَرَّاتٍ.
Amesimulia ‘Aaishah (رضي الله عنها): Pindi Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alipoingia kitandani kila usiku, alikuwa akikusanya vitanga vyake vya mikono na kupuliza juu yake baada ya kusoma:
قُلْ هُوَ اللَّـهُ أَحَدٌ ﴿١﴾
na
قُلْ أَعُوذُ بِرَبِّ الْفَلَقِ ﴿١﴾
na
قُلْ أَعُوذُ بِرَبِّ النَّاسِ ﴿١﴾
Kisha akipangusa kwa mikono yake sehemu za mwili wake ambazo alikuwa anaweza kuzipangusa, akianza na kichwa chake, uso wake na sehemu yake ya mbele ya mwili. Alikuwa akifanya hivyo mara tatu. [Al-Bukhaariy]
4-Haijapata Kuteremshwa Kabla Katika Tawraat Wala Injiyl:
عَنْ عُقْبَةَ بْنِ عَامِرٍ، قَالَ قَالَ لِي رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم " أُنْزِلَ - أَوْ أُنْزِلَتْ - عَلَىَّ آيَاتٌ لَمْ يُرَ مِثْلُهُنَّ قَطُّ الْمُعَوِّذَتَيْنِ "
Amesimulia ‘Uqbah Bin ‘Aamir (رضي الله عنه): Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: zimeteremshwa -au nimeteremshiwa Aayaat ambazo hazijapata kuteremshwa kabla. Nazo ni Al-Mu’awwidhatayni [Muslim] Na katika Riwaaya: Nimeteremshiwa usiku..
Al-Mu’awwidhatayni ni Al-Falaq (113) na An-Naas (114)
5-Ni Sunnah Kuisoma Kila Baada Ya Kumaliza Swalaah Za Fardhi Pamoja na Al-Ikhlaasw (112) na An-Naas (114).
عَنْ عُقْبَةَ بْنِ عَامِرٍ، قَالَ أَمَرَنِي رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم أَنْ أَقْرَأَ الْمُعَوِّذَاتِ دُبُرَ كُلِّ صَلاَةٍ .
Amesimulia ‘Uqbah Bin ‘Aamir (رضي الله عنه): Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) ameniamrisha nisome Al-Mu’awwidhaat kila baada ya Swalaah. [At-Tirmidhiy, An-Nasaaiy, Abuu Daawuwd na ameisahihisha Al-Albaaniy katika Swahiyh Abiy Daawuwd (1523)]
Links
[1] https://www.alhidaaya.com/sw/taxonomy/term/1
[2] http://www.alhidaaya.com/sw/
[3] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11444&title=Tangulizi%20Za%20Suwrah%20Za%20Qur-aan
[4] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11448&title=001-Al-Faatihah%3A%20Utangulizi%20Wa%20Suwrah
[5] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11449&title=002-Al-Baqarah%3A%20Utangulizi%20Wa%20Suwrah
[6] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11450&title=003-Aal-%27Imraan%3A%20Utangulizi%20Wa%20Suwrah
[7] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11466&title=004-An-Nisaa%3A%20Utangulizi%20Wa%20Suwrah
[8] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11487&title=005-Al-Maaidah%3A%20Utangulizi%20Wa%20Suwrah
[9] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11498&title=006-Al-An%27aam%3A%20Utangulizi%20Wa%20Suwrah
[10] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11488&title=007-Al-A%27raaf%3A%20Utangulizi%20Wa%20Suwrah
[11] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11489&title=008-Al-Anfaal%3A%20Utangulizi%20Wa%20Suwrah
[12] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11490&title=009-At-Tawbah%3A%20Utangulizi%20Wa%20Suwrah
[13] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11491&title=010-Yuwnus%3A%20Utangulizi%20Wa%20Suwrah
[14] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11492&title=011-Huwd%3A%20Utangulizi%20Wa%20Suwrah
[15] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11493&title=012-Yuwsuf%3A%20Utangulizi%20Wa%20Suwrah
[16] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11494&title=013-Ar-Ra%27d%3A%20Utangulizi%20Wa%20Suwrah
[17] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11495&title=014-Ibraahiym%3A%20Utangulizi%20Wa%20Suwrah
[18] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11496&title=015-Al-Hijr%3A%20Utangulizi%20Wa%20Suwrah
[19] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11497&title=016-An-Nahl%3A%20Utangulizi%20Wa%20Suwrah
[20] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11499&title=017-Al-Israa%3A%20Utangulizi%20Wa%20Suwrah
[21] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11500&title=018-Al-Kahf%3A%20Utangulizi%20Wa%20Suwrah
[22] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11501&title=019-Maryam%3A%20Utangulizi%20Wa%20Suwrah
[23] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11502&title=020-Twaahaa%3A%20Utangulizi%20Wa%20Suwrah
[24] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11503&title=021-Al-Anbiyaa%3A%20Utangulizi%20Wa%20Suwrah
[25] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11504&title=022-Al-Hajj%3AUtangulizi%20Wa%20Suwrah
[26] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11505&title=023-Al-Muuminuwn%3A%20Utangulizi%20Wa%20Suwrah
[27] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11511&title=024-An-Nuwr%3A%20Utangulizi%20Wa%20Suwrah
[28] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11508&title=025-Al-Furqaan%3A%20Utangulizi%20Wa%20Suwrah
[29] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11533&title=026-Ash-Shu%E2%80%99araa%3A%20Utangulizi%20Wa%20Suwrah
[30] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11534&title=027-An-Naml%3A%20Utangulizi%20Wa%20Suwrah
[31] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11535&title=028-Al-Qaswasw%3A%20Utangulizi%20Wa%20Suwrah
[32] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11537&title=029-Al-%E2%80%98Ankabuwt%3A%20Utangulizi%20Wa%20Suwrah
[33] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11536&title=030-Ar-Ruwm%3A%20Utangulizi%20Wa%20Suwrah
[34] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11538&title=031-Luqmaan%3A%20Utangulizi%20Wa%20Suwrah
[35] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11539&title=032-As-Sajdah%3A%20Utangulizi%20Wa%20Suwrah
[36] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11540&title=033-Al-Ahzaab%3A%20Utangulizi%20Wa%20Suwrah
[37] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11541&title=034-Saba-a%3A%20Utangulizi%20Wa%20Suwrah
[38] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11542&title=035-Faatwir%3A%20Utangulizi%20Wa%20Suwrah
[39] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11543&title=036-Yaasiyn%3A%20Utangulizi%20Wa%20Suwrah
[40] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11544&title=037-Asw-Swaaffaat%3A%20Utangulizi%20Wa%20Suwrah
[41] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11555&title=038-Swaad%3A%20Utangulizi%20Wa%20Suwrah
[42] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11556&title=039-Az-Zumar%3A%20Utangulizi%20Wa%20Suwrah
[43] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11547&title=040-Ghaafir%3A%20Utangulizi%20Wa%20Suwrah
[44] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11545&title=041-Fusw-Swilat%3A%20Utangulizi%20Wa%20Suwrah
[45] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11546&title=042-Ash-Shuwraa%3A%20Utangulizi%20Wa%20Suwrah
[46] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11548&title=043-Az-Zukhruf%3A%20Utangulizi%20Wa%20Suwrah
[47] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11549&title=044-Ad-Dukhaan%3A%20Utangulizi%20Wa%20Suwrah
[48] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11550&title=045-Al-Jaathiyah%3A%20Utangulizi%20Wa%20Suwrah
[49] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11551&title=046-Al-Ahqaaf%3A%20Utangulizi%20Wa%20Suwrah
[50] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11552&title=047-Muhammad%3A%20Utangulizi%20Wa%20Suwrah
[51] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11553&title=048-Al-Fat-h%3A%20Utangulizi%20Wa%20Suwrah
[52] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11554&title=049-Al-Hujuraat%3A%20Utangulizi%20Wa%20Suwrah
[53] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11557&title=050-Qaaf%3A%20Utangulizi%20Wa%20Suwrah
[54] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11559&title=051-Adh-Dhaariyaat%3A%20Utangulizi%20Wa%20Suwrah
[55] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11558&title=052-Atw-Twuur%3A%20Utangulizi%20Wa%20Suwrah
[56] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11560&title=053-An-Najm%3A%20Utangulizi%20Wa%20Suwrah
[57] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11561&title=054-Al-Qamar%3A%20Utangulizi%20Wa%20Suwrah
[58] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11562&title=055-Ar-Rahmaan%3A%20Utangulizi%20Wa%20Suwrah
[59] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11565&title=056-Al-Waaqi%E2%80%99ah%3A%20Utangulizi%20Wa%20Suwrah
[60] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11563&title=057-Al-Hadiyd%3A%20Utangulizi%20Wa%20Suwrah
[61] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11564&title=058-Al-Mujaadalah%3A%20Utangulizi%20Wa%20Suwrah
[62] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11566&title=059-Al-Hashr%3A%20Utangulizi%20Wa%20Suwrah
[63] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11567&title=060-Al-Mumtahinah%3A%20Utangulizi%20Wa%20Suwrah
[64] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11568&title=061-Asw-Swaff%3A%20Utangulizi%20Wa%20Suwrah
[65] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11569&title=062-Al-Jumu%E2%80%99ah%3A%20Utangulizi%20Wa%20Suwrah
[66] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11570&title=063-Al-Munaafiquwn%3A%20Utangulizi%20Wa%20Suwrah
[67] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11571&title=064-At-Taghaabun%3A%20Utangulizi%20Wa%20Suwrah
[68] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11577&title=065-Atw-Twalaaq%3A%20Utangulizi%20Wa%20Suwrah
[69] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11579&title=066-At-Tahriym%3A%20Utangulizi%20Wa%20Suwrah
[70] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11580&title=067-Al-Mulk%3A%20Utangulizi%20Wa%20Suwrah
[71] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11581&title=068-Al-Qalam%3A%20Utangulizi%20Wa%20Suwrah
[72] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11572&title=069-Al-Haaqqah%3A%20Utangulizi%20Wa%20Suwrah
[73] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11573&title=070-Al-Ma%E2%80%99aarij%3A%20Utangulizi%20Wa%20Suwrah
[74] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11574&title=071-Nuwh%3A%20Utangulizi%20Wa%20Suwrah
[75] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11575&title=072-Al-Jinn%3A%20Utangulizi%20Wa%20Suwrah
[76] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11576&title=073-Al-Muzzammil%3A%20Utangulizi%20Wa%20Suwrah
[77] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11578&title=074-Al-Muddath-thir%3A%20Utangulizi%20Wa%20Suwrah
[78] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11586&title=075-Al-Qiyaamah%3A%20Utangulizi%20Wa%20Suwrah
[79] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11582&title=076-Al-Insaan%3A%20Utangulizi%20Wa%20Suwrah
[80] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11583&title=077-Al-Mursalaat%3A%20Utangulizi%20Wa%20Suwrah
[81] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11585&title=078-An-Nabaa%3A%20Utangulizi%20Wa%20Suwrah
[82] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11584&title=079-An-Naazi%E2%80%99aat%3A%20Utangulizi%20Wa%20Suwrah
[83] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11593&title=080-%E2%80%98Abasa%3A%20Utangulizi%20Wa%20Suwrah
[84] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11587&title=081-At-Takwiyr%3A%20Utangulizi%20Wa%20Suwrah
[85] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11588&title=082-Al-Infitwaar%3A%20Utangulizi%20Wa%20Suwrah
[86] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11589&title=083-Al-Mutwaffifiyn%3A%20Utangulizi%20Wa%20Suwrah
[87] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11590&title=084-Al-Inshiqaaq%3A%20Utangulizi%20Wa%20Suwrah
[88] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11591&title=085-Al-Buruwj%3A%20Utangulizi%20Wa%20Suwrah
[89] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11592&title=086-Atw-Twaariq%3A%20Utangulizi%20Wa%20Suwrah
[90] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11595&title=087-Al-A%E2%80%99laa%3A%20Utangulizi%20Wa%20Suwrah
[91] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11594&title=088-Al-Ghaashiyah%3A%20Utangulizi%20Wa%20Suwrah
[92] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11596&title=089-Al-Fajr%3A%20Utangulizi%20Wa%20Suwrah
[93] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11597&title=090-Al-Balad%3A%20Utangulizi%20Wa%20Suwrah
[94] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11598&title=091-Ash-Shams%3A%20Utangulizi%20Wa%20Suwrah
[95] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11615&title=092-Al-Layl%3A%20Utangulizi%20Wa%20Suwrah
[96] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11599&title=093-Adhw-Dhwuhaa%3A%20Utangulizi%20Wa%20Suwrah
[97] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11600&title=094-Ash-Sharh%3A%20Utangulizi%20Wa%20Suwrah
[98] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11601&title=095-At-Tiyn%3A%20Utangulizi%20Wa%20Suwrah
[99] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11602&title=096-Al-%E2%80%98Alaq%3A%20Utangulizi%20Wa%20Suwrah
[100] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11603&title=097-Al-Qadr%3A%20Utangulizi%20Wa%20Suwrah
[101] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11605&title=098-Al-Bayyinah%3A%20Utangulizi%20Wa%20Suwrah
[102] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11604&title=099-Az-Zalzalah%3A%20Utangulizi%20Wa%20Suwrah
[103] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11606&title=100-Al-%E2%80%98Aadiyaat%3A%20Utangulizi%20Wa%20Suwrah
[104] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11608&title=101-Al-Qaari%E2%80%99ah%3A%20Utangulizi%20Wa%20Suwrah
[105] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11607&title=102-At-Takaathur%3A%20Utangulizi%20Wa%20Suwrah
[106] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11609&title=103-Al-%E2%80%98Aswr%3A%20Utangulizi%20Wa%20Suwrah
[107] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11610&title=104-Al-Humazah%3A%20Utangulizi%20Wa%20Suwrah
[108] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11611&title=105-Al-Fiyl%3A%20Utangulizi%20Wa%20Suwrah
[109] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11616&title=106-Quraysh%3A%20Utangulizi%20Wa%20Suwrah
[110] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11617&title=107-Al-Maa%E2%80%99uwn%3A%20Utangulizi%20Wa%20Suwrah
[111] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11618&title=108-Al-Kawthar%3A%20Utangulizi%20Wa%20Suwrah
[112] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11619&title=109-Al-Kaafiruwn%3A%20Utangulizi%20Wa%20Suwrah
[113] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11612&title=110-An-Naswr%3A%20Utangulizi%20Wa%20Suwrah
[114] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11613&title=111-Al-Masad%3A%20Utangulizi%20Wa%20Suwrah
[115] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11620&title=112-Al-Ikhlaasw%3A%20Utangulizi%20Wa%20Suwrah
[116] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11621&title=113-Al-Falaq%3A%20Utangulizi%20Wa%20Suwrah
[117] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11622&title=114-An-Naas%3A%20Utangulizi%20Wa%20Suwrah
[118] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11639&title=114-An-Naas%3A%20Utangulizi%20Wa%20Suwrah