Majini
Imeandaliwa Na 'Abdullaah Mu'aawiyah (Abu Baasim)
Alhidaaya.com
Majini
Alhidaaya.com [3]
01- Majini Ni Akina Nani
Neno "الجِنُّ" limenyambuliwa toka neno "الاجْتِنَانُ" lenye maana ya kufichika na kutoweza kuonekana. Na kwa vile wanadamu hawawezi kuwaona, ndio wakaitwa majini.
Majini hawa ni viumbe vyenye akili, vyenye utashi na vilivyokalifishwa na Allaah Ta’aalaa kutekeleza maamrisho Yake na kuacha makatazo Yake, na kesho akhera watahisabiwa matendo yao waliyoyafanya hapa duniani. Wameumbwa kutokana na moto, wana uwezo wa kujiweka katika maumbo tofauti, wanakula, wanakunywa, wanaoana na wanazaana kama sisi wanadamu. Kwa hiyo basi, wana familia, watoto, wajukuu na kadhalika.
Ibn Hazm amesema kuhusu majini: “Ni umma wenye akili na utambuzi, wanafanya ‘ibada, wameahidiwa kulipwa mema kama watafanya mema, na adhabu kama watakengeuka, wanazaana na wanakufa. Asili yao ni moto kama ilivyo asili yetu sisi udongo”.
Majini
Alhidaaya.com [3]
02- Dalili Za Uwepo Wa Majini Toka Kwenye Qur-aan:
Allaah Ta’aalaa Amewataja majini sehemu mbalimbali katika Kitabu Chake Kitukufu. Kati ya sehemu hizo ni:
1- Suwrat Al-Jinn:
"قُلْ أُوحِيَ إِلَيَّ أَنَّهُ اسْتَمَعَ نَفَرٌ مِّنَ الْجِنِّ فَقَالُوا إِنَّا سَمِعْنَا قُرْآنًا عَجَبًا"
“Sema (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم): Nimefunuliwa Wahy kwamba kundi miongoni mwa majini lilisikiliza, wakasema: Hakika sisi tumeisikia Qur-aan ya ajabu”. [Al-Jinn: 01]
As-Sa’adiyy amesema kuhusu suwrah hii: “Ndani ya suwrah hii kuna faida nyingi. Miongoni mwazo ni uwepo wa majini, na kwamba majini hawa wamekalifishwa mambo ya kufanya na mambo ya kuacha, na watakuja kulipwa matendo yao kama aya za suwrah hii zinavyoonyesha”.
2- Suwrat Adh-Dhaariyaat:
"وَمَا خَلَقْتُ الْجِنَّ وَالْإِنسَ إِلَّا لِيَعْبُدُونِ"
“Na Sikuumba majini na wanadamu isipokuwa wapate kuniabudu Mimi tu”. [Adh-Dhaariyaat: 56]
3- Suwrat Al-An’aam:
"يَا مَعْشَرَ الْجِنِّ وَالْإِنسِ أَلَمْ يَأْتِكُمْ رُسُلٌ مِّنكُمْ يَقُصُّونَ عَلَيْكُمْ آيَاتِي وَيُنذِرُونَكُمْ لِقَاءَ يَوْمِكُمْ هَـٰذَا"
“Enyi hadhara ya majini na wana Aadam! Je hawajakufikieni Rusuli miongoni mwenu wanakusimulieni Aayaat Zangu na wanakuonyeni kukutana na Siku yenu hii?” [Al-An’aam: 156]
4- Suwrat As Sajdah:
"وَلَوْ شِئْنَا لَآتَيْنَا كُلَّ نَفْسٍ هُدَاهَا وَلَـٰكِنْ حَقَّ الْقَوْلُ مِنِّي لَأَمْلَأَنَّ جَهَنَّمَ مِنَ الْجِنَّةِ وَالنَّاسِ أَجْمَعِينَ"
“Na Tungelitaka, Tungeliipa kila nafsi mwongozo wake, lakini imethibiti kauli kutoka Kwangu kwamba: Bila shaka Nitajaza Jahannam kwa majini na watu pamoja”. [As-Sajdah: 13]
Ibn Jariyr amesema: “Jahannam itajazwa majini na wanadamu waliomwasi Allaah”.
Kwa maana kwamba majini nao wataingia motoni kutokana na matendo yao mabaya kama ilivyo kwa wanadamu.
5- Suwrat Ar Rahmaan:
"فِيهِنَّ قَاصِرَاتُ الطَّرْفِ لَمْ يَطْمِثْهُنَّ إِنسٌ قَبْلَهُمْ وَلَا جَانٌّ"
“Mna humo wanawake wenye staha wanaoinamisha macho, hajawabikiri kabla yao binadamu yeyote wala jinni”. [Ar-Rahmaan: 56]
Al-Baghawiy kasema: “Hii ni dalili kwamba jini anajimai kama anavyojimai mwanadamu”.
6- Suwrat Al-Israa:
"قُل لَّئِنِ اجْتَمَعَتِ الْإِنسُ وَالْجِنُّ عَلَىٰ أَن يَأْتُوا بِمِثْلِ هَـٰذَا الْقُرْآنِ لَا يَأْتُونَ بِمِثْلِهِ وَلَوْ كَانَ بَعْضُهُمْ لِبَعْضٍ ظَهِيرًا"
“Sema: Ikiwa watajumuika wana Aadam na majini ili walete mfano wa hii Qur-aan; hawatoweza kuleta mfano wake na japokuwa watasaidiana wao kwa wao”. [Al-Israa: 88]
7- Suwrat Sabaa:
"فَلَمَّا خَرَّ تَبَيَّنَتِ الْجِنُّ أَن لَّوْ كَانُوا يَعْلَمُونَ الْغَيْبَ مَا لَبِثُوا فِي الْعَذَابِ الْمُهِينِ "
“Basi alipoanguka, ikawabainikia majini kwamba lau wangelikuwa wanajua ya ghayb, basi wasingelibakia katika adhabu ya kudhalilisha”. [Sabaa: 14]
Majini
Alhidaaya.com [3]
03- Dalili Za Uwepo Wa Majini Toka Kwenye Hadiyth:
Addamiyriyy amesema: “Jua kwamba Hadiyth za Rasuli zinazozungumzia uwepo wa majini na mashetani ni nyingi mno. Pia yapo mashairi ya Waarabu na simulizi zao zinazozungumzia uwepo huo”.
Kati ya Hadiyth hizo ni:
1- Toka kwa ‘Aaishah (Radhwiya Allaah ‘anhaa): Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
"خُلِقَتِ الْمَلاَئِكَةُ مِنْ نُورٍ، وَخُلِقَ الْجَانُّ مِنْ مَارِجٍ مِنْ نَارٍ، وَخُلِقَ آدَمُ مِمَّا وُصِفَ لَكُمْ"
“Malaika wameumbwa kutokana na nuru, na majini wameumbwa kutokana na mwako mchanganyiko wa moto, na Aadam ameumbwa kutokana na hicho mlichoelezewa (udongo)”. [Hadiyth Swahiyh. Muslim (2996)]
2- Toka kwa ‘Aamir, amesema:
"عن عامر، قال: سألتُ عَلْقَمةَ: هل كان ابنُ مسعود شَهِدَ مع رسول الله صلى الله عليه وسلم ليلةَ الجنِّ قال: فقال عَلْقَمةُ، أنا سألتُ ابنَ مسعود فقلتُ: هل شَهِدَ أحدٌ منكم مع رسول الله صلى الله عليه وسلم ليلةَ الجنِّ؟ قال لا، ولكنَّا كنَّا مع رسول الله ذاتَ ليلة ففَقَدْناه فالتمسناه في الأودية والشِّعاب. فقلنا استُطِير أو اغْتِيل قال: فبِتْنَا بِشَرِّ ليلة بات بها قومٌ، فلما أصبحْنا إذا هو جاء من قِبَل حِرَاء. قال: فقلنا يا رسول الله فقدْناك فطلبْناك فلم نجدْك، فبِتْنَا بِشَرِّ ليلة بات بها قوم. فقال: أتاني داعي الجِنِّ فذَهَبْتُ مَعَه فقَرَأتُ عليهمُ القُرآنَ، قال: فانطَلَقَ بنا فأرانا آثارَهم، وآثارَ نيرانِهم، وسَألوه الزَّادَ، فقال: لَكَم كُلُّ عَظمٍ ذُكِرَ اسمُ اللَّهِ عليهِ يَقَعُ في أيديكُم أوفَرَ ما يَكونُ لَحمًا، وكُلُّ بَعرةٍ عَلَفٌ لدَوابِّكُم. فقال رَسولُ اللَّهِ صلَّى اللهُ عليه وسلَّم: فلا تَستَنجوا بها؛ فإنَّها طَعامُ إخوانِكُم"
“Nilimuuliza ‘Alqamah kama Ibn Mas-‘uwd alihudhuria pamoja na Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) usiku wa kukutana na majini. ‘Alqamah akasema: Mimi nilimuuliza Ibn Mas-‘uwd kama kuna yeyote kati yao ambaye alihudhuria pamoja na Rasuli (Swalla nAllaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) usiku huo. Akasema: Hapana, lakini sisi usiku mmoja tulikuwa pamoja na Rasuli wa Allaah, kisha akatupotea. Tukaanza kumtafuta kwenye mabonde na njia za milimani tusimpate. Tukasema: Pengine majini wameruka naye, au pengine ameuawa. Hapo tukakesha usiku mbaya kabisa ambao watu hawajawahi kukesha. Kulipopambazuka, ghafla tukamwona anakuja kutokea pande za Hiraa. Tukamwambia: Ee Rasuli wa Allaah! Tumekukosa, tukakutafuta sana na wala hatukukupata, na tukakesha usiku mbaya mno ambao hatujawahi kuupitia. Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akatuambia: Alinijia mjumbe wa majini (kunialika) nami nikaongozana naye, kisha nikawasomea Qur-aan. Halafu (Rasuli) akaondoka nasi na akawa anatuonyesha athari zao na athari za mioto yao. Na majini hao walimwomba awaainishie kitu ambacho kitakuwa ni chakula kwao. Akawaambia: Ni haki yenu mifupa yote mnayoipata ambayo imetajiwa Jina la Allaah, mnapoipata itakuwa na nyama nyingi, na pia vinyesi vyote vya wanyama ni malisho kwa wanyama wenu. Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akasema: Basi msistanji kwavyo, kwani ni chakula cha ndugu zenu”. [Swahiyh Muslim: 450]
3- Toka kwa Abu Hurayrah: “Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
"إنَّ عِفْريتًا مِنَ الجِن ِّتَفَلَّتَ البارِحةَ ليَقطَعَ عَليَّ صَلاتي، فأمكَنَني اللَّهُ مِنه فأخَذْتُه، فأرَدتُ أن أربِطَه على ساريةٍ من سَوارَي المَسجِدِ حَتَّى تَنظُروا إليهِ كُلُّكُم، فذَكَرْتُ دَعوةَ أخي سُلَيمانَ: رَبِّ هَبْ لي مُلْكًا لا يَنبَغي لأحَدٍ من بَعْدي، فرَدَدتُه خاسِئًا"
“Hakika afriti mmoja katika majini alinitokezea ghafla ili anivurugie swalah yangu, lakini Allaah Alinipa nguvu nikaweza kumdhibiti. Nikataka kumfunga kwenye nguzo moja kati ya nguzo za Msikiti ili nyinyi nyote muweze kumwona. Na hapo nikakumbuka dua ya ndugu yangu Sulaymaan: Rabb wangu! Nitunukie ufalme asiupate mtu yeyote baada yangu, kisha nikamwachia aende zake akiwa amedhalilika”.. [Hadiyth Swahiyh. Al-Bukhaariy (461)]
An Nawawiy amesema: “Katika Hadiyth hii, kuna dalili kwamba majini wapo na kwamba baadhi ya wanadamu wanaweza kuwaona. Ama Kauli Yake Ta’aalaa: “Hakika yeye (Ibliys) anakuoneni yeye na kabila lake (la mashetani) na hali ya kuwa nyinyi hamuwaoni”, hii inachukulika juu ya walio wengi ambao hawawaoni katika sisi. Na kama kuwaona isingeliwezekana, basi Nabiy (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) asingelisema haya aliyoyasema ya afriti huyo kumtokezea, akamdhibiti na akataka kumfunga kwenye nguzo ya Msikiti”.
4- Abu Hurayrah (Radhwiya Allaah ‘anhu) amesema:
"وكَّلني رَسولُ اللَّهِ صلَّى اللهُ عليه وسلَّم بحِفظِ زَكاةِ رَمضانَ، فأتاني آتٍ فجَعَلَ يَحثو مِنَ الطَّعامِ فأخذْتُه، وقُلتُ: واللهِ لأرفَعَنَّك إلى رَسولِ اللَّهِ صلَّى اللهُ عليه وسلَّم، قال: إنِّي مُحتاجٌ، وعليَّ عيالٌ، ولي حاجةٌ شَديدةٌ، قال: فخَلَّيتُ عَنه، فأصبَحْتُ، فقال النَّبيُّ صلَّى اللهُ عليه وسلَّم: يا أبا هُريرةَ، ما فعل أسيرُكَ البارِحةَ؟، قال: قُلتُ: يا رَسولُ اللَّهِ، شَكا حاجةً شَديدةً وعِيالًا فرَحمْتُه، فخَلَّيتُ سَبيلَه، قال: أما إنَّه قد كذَبَكَ وسَيَعودُ، فعَرَفْتُ أنَّه سَيَعودُ؛ لقَولِ رَسولِ اللَّهِ صلَّى اللهُ عليه وسلَّم: إنَّه سَيَعودُ، فرَصدْتُه، فجاءَ يَحثو مِنَ الطَّعامِ، فأخَذْتُه، فقُلتُ: لأرفَعَنَّكَ إلى رَسولِ اللَّهِ صلَّى اللهُ عليه وسلَّم، قال: دَعْني فإنِّي مُحتاجٌ وعليَّ عيالٌ، لا أعودُ، فرَحِمْتُه، فخَلَّيتُ سَبيلَه، فأصبَحْتُ، فقال لي رَسولُ اللَّهِ صلَّى اللهُ عليه وسلَّم: يا أبا هُريرةَ، ما فعل أسيرُكَ؟، قُلتُ: يا رَسولَ اللَّهِ شَكا حاجةً شَديدةً وعيالًا، فرَحمْتُه، فخَلَّيتُ سَبيلَه، قال: أمَا إنَّه قد كذَبَكَ وسَيَعودُ، فرَصدَتُه الثَّالِثةَ، فجاءَ يَحثو مِنَ الطَّعامِ، فأخَذتُه، فقُلتُ: لأرفَعَنَّكَ إلى رَسولِ اللَّهِ، وهَذا آخِرُ ثَلاثِ مَرَّاتٍ، أنَّكَ تَزعُمُ لا تَعودَ، ثُمَّ تَعودُ، قال: دَعْني أعلِّمْكَ كَلِماتٍ يَنفَعُكَ اللهُ بها، قُلتُ: ما هوَ؟ قال: إذا أوَيتَ إلى فراشِكَ، فاقرَأْ آيةَ الكُرسيِّ: اللَّهُ لَا إِلَهَ إِلَّا هُوَ الْحَيُّ الْقَيُّومُ، حَتَّى تَختِمَ الآيةَ، فإنَّكَ لَن يَزالَ عليكَ مِنَ اللَّهِ حافِظٌ، ولا يَقْرَبَنَّكَ شَيطانٌ حَتَّى تُصبِحَ، فخَلَّيتُ سَبيلَه، فأصبَحْتُ، فقالَ لي رَسولُ اللَّهِ صلَّى اللهُ عليه وسلَّم: ما فعل أسيرُكَ البارِحةَ؟، قُلتُ: يا رَسولَ اللَّهِ، زَعَمَ أنَّه يُعَلِّمُني كَلِماتٍ يَنفَعُني اللَّهُ بها، فخَلَّيتُ سَبيلَه، قال: ما هيَ؟، قُلتُ: قال لي: إذا أويتَ إلى فراشِكَ فاقرَأْ آيةَ الكُرسيِّ مِن أوَّلِها حَتَّى تَختِمَ الآيةَ: اللَّهُ لَا إِلَهَ إِلَّا هُوَ الْحَيُّ الْقَيُّومُ، وقال لي: لَن يَزالَ عليكَ مِنَ اللَّهِ حافِظٌ، ولا يَقرَبُكَ شَيطانٌ حَتَّى تُصبِحَ ، فقال النَّبيُّ صلَّى اللهُ عليه وسلَّم: أمَا إنَّه قد صَدَقَكَ وهوَ كَذُوبٌ، تَعلَمُ من تُخاطِبُ مُنذُ ثَلاثِ ليالٍ يا أبا هُريرةَ؟، قال: لا، قال: ذاكَ شَيطانٌ"
“Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alinipa jukumu la kulinda zaka ya Ramadhani. Akanijia mtu, na akaanza kuteka chakula kwa mikono yake, nami nikamkamata. Nikamwambia: Wal-Laahi, nitakupeleka kwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam). Akasema: Mimi ni mhitaji, nina watoto, na nina dhiki sana. Nikamwachia. Nilipopambaukiwa, Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) aliniuliza: Ee Abu Hurayrah! Alifanya nini mateka wako usiku? Nikasema: Ee Rasuli wa Allaah! Alinililia dhiki na watoto, nami nikamhurumia halafu nikamwachilia aende zake. Akasema: Ahaa, basi jua kwamba amekudanganya na kesho atakuja tena, nami nikajua kwa hakika kuwa lazima atarudi tena kutokana na kauli hiyo ya Rasuli. Nikamvizia, na mara akaja tena na kuanza kuchota chakula, nikamkamata na kumwambia: Nitakupeleka kwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam). Akaniambia: Niachie, mimi ni mhitaji na nina mzigo wa watoto, sitorudi tena hapa. Nikamwonea huruma na kumwachia aende zake. Nilipokutana na Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) asubuhi aliniuliza: Ee Abu Hurayrah! Nini alifanya mateka wako? Nikasema: Ee Rasuli wa Allaah! Alinililia dhiki kubwa na watoto, nami nikamhurumia na kumwacha aende zake. Akasema: Basi ujue kwamba amekudanganya na atarudi tena. Nikamvizia tena mara ya tatu, naye akaja, akaanza kuchota chakula, nami nikamkamata. Nikamwambia: Lazima nikupeleke kwa Rasuli wa Allaah, na hii ni mara ya tatu na ya mwisho, unadai hutorudi kisha unarudi. Akasema: Niache nikufundishe maneno ambayo Allaah Atakunufaisha kwayo. Nikamuuliza: Ni yepi hayo? Akasema: Unapokwenda kitandani kwako kulala, basi soma Aayatul Kursiy اللَّهُ لَا إِلَهَ إِلَّا هُوَ الْحَيُّ الْقَيُّومُ mpaka mwisho wa Aayah, hapo wewe utabaki na mlinzi anayekulinda toka kwa Allaah. Na kamwe shetani hatokukurubia mpaka upambaukiwe, nami nikamwachia aende zake. Nilipokutana asubuhi na Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) aliniuliza: Mateka wako alifanya nini jana? Nikamwambia: Ee Rasuli wa Allaah! Alidai kwamba atanifundisha maneno ambayo Allaah Ataninufaisha kwayo, nami nikamwachia aende zake. Akaniuliza: Ni maneno gani hayo? Nikamwambia: Aliniambia: Ukienda kitandani kwako kulala, basi soma Aayatul Kursiy toka mwanzo wake hadi mwisho اللَّهُ لَا إِلَهَ إِلَّا هُوَ الْحَيُّ الْقَيُّومُ . Akasema: Mlinzi toka kwa Allaah ataendelea kukulinda, na shaytwaan hatokukurubia mpaka asubuhi. Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akaniambia: Basi ujue kwamba amekwambia ukweli lakini yeye ni mwongo kupindukia. Basi je, unamjua ni nani uliyekuwa unazungumza naye toka siku hizo tatu zilizopita ee Abu Hurayrah? Nikasema hapana. Akasema: Basi huyo ni shetani”. [Swahiyhul Bukhaariy (2311)]
Ibn Hajar amesema: “Katika Hadiyth hii kuna faida kadhaa. Kati yake ni:
- Kwamba shetani anaweza kuyajua mambo ambayo yanamnufaisha Muislamu.
- Mtu mwovu anaweza kuipata hikmah lakini asiweze kunufaika nayo, na mtu akaichukua kutoka kwake na kunufaika nayo.
- Mtu anaweza kulijua jambo la faida lakini akashindwa kulitumia.
- Ni tabia ya shetani kusema uongo.
- Shetani anaweza kujiweka katika umbile la mwanadamu akaweza kuonekana.
- Majini wanakula vyakula wanavyokula wanadamu, wanazungumza lugha za wanadamu, wanaiba vya wanadamu na wanahadaa.
Majini
Alhidaaya.com [3]
04- Dalili Za Kiakili Za Uwepo Wa Majini:
Kutojua uwepo wa kitu fulani hakulazimishi kitu hicho kwamba hakipo. Katika maisha ya mwanadamu, kuna vitu vingi sana vinavyomzunguka naye ana uhakika kwamba viko pamoja na kwamba havioni. Ni kama umeme ambao unapita kwenye nyaya lakini hauoni, au mawimbi ya sauti ambayo yanasafiri na kumfikia na kuhisi athari yake bila ya kuyaona mawimbi yenyewe.
Muhammad Rashiyd Riza amesema: “Lau ingelikuwa kutokiona kitu ndiyo dalili sahihi ya kutokuwepo kwake, wataalamu wasingelijishughulisha kupekua na kutafiti vitu visivyojulikana, na wasingeliweza kugundua viini, virusi na kadhalika vilivyoifanya nyanja ya tiba na upasuaji kufikia mapinduzi haya makubwa tunayoyaona na tutakayoendelea kuyashuhudia kwa miaka mingi ijayo. Katika tone moja tu la maji, vinaweza kuonekana viumbe hai vingi kwa kutumia darubini za nguvu. Na lau kama angelisema yeyote katika karne zilizopita kwamba kuna viumbe hai vidogo mno visivyoonekana kwa macho na vinaishi kwenye mwili wa mwanadamu, basi watu wangesema kwamba mtu huyo ni mwendawazimu”.
Na teknolojia ya mawasiliano ya hivi sasa ni katika mambo ambayo hakuna aliyeweza kudhania kwamba yanaweza kufikia hali hii miaka iliyopita nyuma, lakini yametokea na mengi zaidi ya maajabu yatagunduliwa.
Abu Bakr Al-Jazaairiy amesema: “Athari zinazoonyesha kuwepo kwa majini na mashetani ni nyingi sana. Zinatutosha hizi zifuatazo:
1- Kifafa ambacho kimekuweko kuanzia enzi na enzi. Hapa tunamaanisha kile kifafa ambacho kinasababishwa na marohani wabaya. Hata katika enzi yetu ya leo ambapo tiba imeshuhudia mapinduzi makubwa, bado madaktari hawajaweza kufanya lolote kuhusiana na tiba ya kifafa ambacho ni athari ya majini na mashetani na dalili isiyo na shaka kwamba wapo.
2- Majini wanazungumza kupitia kwa mwanadamu wanayemvaa, na mwanadamu huyu akapata kuzungumza mambo ambayo hakuwa akiyajua. Kadhalika, anaweza kuzungumza lugha ambayo haijui asilani.
3- Jini hutolewa ndani ya mwili wa mwanadamu aliyekuwa amemvaa kwa njia ya ruqya, na jinni akaeleza kwamba anatoka na hatorudi tena ndani ya mwili wa mtu aliyekuwa amemvaa.
4- Kudhihiri baadhi ya majini kwa baadhi ya watu na kuzungumza nao. Habari ya hili imetangaa kizazi baada ya kizazi.
Majini
Alhidaaya.com [3]
05- Mada Waliyoumbiwa Kwayo Majini:
Majini wameumbwa kutokana na moto. Allaah Ta’aalaa Anasema:
"وَالْجَانَّ خَلَقْنَاهُ مِن قَبْلُ مِن نَّارِ السَّمُومِ"
“Na majini Tuliwaumba kabla kutokana na moto ulio mkali mno”. [Al-Hijri: 27]
Ayah hii ni dalili pia kwamba majini waliumbwa kabla ya sisi wanadamu.
Allaah Anasema tena:
"وَخَلَقَ الْجَانَّ مِن مَّارِجٍ مِّن نَّارٍ"
“Na Akaumba majini kutokana na mwako wa moto”. [Ar-Rahmaan: 15]
Ash-Shawkaaniy amesema: “Allaah Amemuumba Al-Jaann kutokana na moto, na Al-Jaann ndiye baba wa majini. Na المارِجُ ni mwako safi wa moto usio na moshi.
Na Amesema tena Allaah Ta’aalaa:
"قَالَ أَنَا خَيْرٌ مِّنْهُ خَلَقْتَنِي مِن نَّارٍ وَخَلَقْتَهُ مِن طِينٍ"
“(Allaah) Akasema: Nini kilichokuzuia usisujudu Nilipokuamrisha? (Ibliys) Akasema: Mimi ni mbora zaidi kuliko yeye. Umeniumba kwa moto, na yeye Umemuumba kwa udongo”. [Al-A’araaf: 12]
Bibi ‘Aaishah (Radhwiya Allaah ‘anhaa) amesema:
"خُلِقَتِ الْمَلاَئِكَةُ مِنْ نُورٍ، وَخُلِقَ الْجَانُّ مِنْ مَارِجٍ مِنْ نَارٍ، وَخُلِقَ آدَمُ مِمَّا وُصِفَ لَكُمْ"
“Malaika wameumbwa kutokana na nuru, na majini wameumbwa kutokana na mwako mchanganyo wa moto, na Aadam ameumbwa kutokana na hicho mlichoelezewa (udongo)”. [Hadiyth Swahiyh. Muslim (2996)]
Majini
Alhidaaya.com [3]
06- Majini Wanaoana Na Wanazaana:
Majini wanaoana na wanazaana. Allaah Ta’aalaa Anatuambia:
"وَإِذْ قُلْنَا لِلْمَلَائِكَةِ اسْجُدُوا لِآدَمَ فَسَجَدُوا إِلَّا إِبْلِيسَ كَانَ مِنَ الْجِنِّ فَفَسَقَ عَنْ أَمْرِ رَبِّهِ ۗ أَفَتَتَّخِذُونَهُ وَذُرِّيَّتَهُ أَوْلِيَاءَ مِن دُونِي وَهُمْ لَكُمْ عَدُوٌّ ۚ بِئْسَ لِلظَّالِمِينَ بَدَلًا"
“Na pindi Tulipowaambia Malaika: Msujudieni Aadam. Wakasujudu isipokuwa Ibliys, alikuwa miongoni mwa majini, akaasi Amri ya Rabb wake. Je, basi mnamfanya yeye na kizazi chake walinzi pasi Nami, na hali wao kwenu ni maadui? Ubaya ulioje mbadala huu kwa madhalimu!” [Al-Kahf: 50]
Watoto hawapatikani bila mke na mume, na hii ni dalili kwamba wanaoana na kuzaana .
Ibn Al-Hajar Al-Haytamiy amesema: “Hii ni dalili kwamba wanaoana kwa ajili ya kupata watoto”.
Qataadah amesema: “Shetani anaoa na anazaa kama anavyooa mwanadamu na kuzaa”.
Na Allaah Ta’aalaa Amesema tena:
"لَمْ يَطْمِثْهُنَّ إِنسٌ قَبْلَهُمْ وَلَا جَانٌّ"
“Hajawabikiri kabla yao binadamu yeyote wala jinni”. [Ar-Rahmaan: 56]
Ibn Hajar Al-Haythamiy amesema: “Hii inaonyesha kwamba majini wana uwezo wa kuingilia na kuvunja bikira”.
Allaah Ta’aalaa Amesema tena:
"وَأَنَّهُ كَانَ رِجَالٌ مِّنَ الْإِنسِ يَعُوذُونَ بِرِجَالٍ مِّنَ الْجِنِّ فَزَادُوهُمْ رَهَقًا"
“Na kwamba walikuwa wanaume miongoni mwa wana Aadam wanajikinga na wanaume miongoni mwa majini, basi wakawazidishia madhambi, uvukaji mipaka ya kuasi na khofu”. [Al-Jinn: 06]
Kwa vile wako wanaume katika majini, ni lazima pia waweko wanawake katika majini. Na uwepo wa jinsia hizi mbili, unawajibisha kuoana na kuzaana.
Anas (Radhwiya Allaah ‘anhu) amesema: Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa anapoingia msalani husema:
"اللَّهُمُ إنِّي أعوذُ بكَ مِنَ الخُبثِ والخَبائِثِ"
“Ee Allaah! Hakika mimi ninajilinda kwako na majini wanaume na majini wanawake”. [Al-Bukhaariy (142) na Muslim (375)]
Majini
Alhidaaya.com [3]
07- Majini Wanakula Na Wanakunywa:
Malaika kama inavyojulikana hawali wala hawanywi, lakini majini na mashetani wanakula na wanakunywa. Na dalili ya hili ni haya yafuatayo:
1- Toka kwa ‘Aamir, amesema:
سألتُ عَلْقَمةَ: هل كان ابنُ مسعود شَهِدَ مع رسول الله صلى الله عليه وسلم ليلةَ الجنِّ قال: فقال عَلْقَمةُ، أنا سألتُ ابنَ مسعود فقلتُ: هل شَهِدَ أحدٌ منكم مع رسول الله صلى الله عليه وسلم ليلةَ الجنِّ؟ قال لا، ولكنَّا كنَّا مع رسول الله ذاتَ ليلة ففَقَدْناه فالتمسناه في الأودية والشِّعاب. فقلنا استُطِير أو اغْتِيل قال: فبِتْنَا بِشَرِّ ليلة بات بها قومٌ، فلما أصبحْنا إذا هو جاء من قِبَل حِرَاء. قال: فقلنا يا رسول الله فقدْناك فطلبْناك فلم نجدْك، فبِتْنَا بِشَرِّ ليلة بات بها قوم. فقال: أتاني داعي الجِنِّ فذَهَبْتُ مَعَه فقَرَأتُ عليهمُ القُرآنَ، قال: فانطَلَقَ بنا فأرانا آثارَهم، وآثارَ نيرانِهم، وسَألوه الزَّادَ، فقال: لَكَم كُلُّ عَظمٍ ذُكِرَ اسمُ اللَّهِ عليهِ يَقَعُ في أيديكُم أوفَرَ ما يَكونُ لَحمًا، وكُلُّ بَعرةٍ عَلَفٌ لدَوابِّكُم. فقال رَسولُ اللَّهِ صلَّى اللهُ عليه وسلَّم: فلا تَستَنجوا بها؛ فإنَّها طَعامُ إخوانِكُم"
“Nilimuuliza ‘Alqamah kama Ibn Mas-‘uwd alihudhuria pamoja na Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) usiku wa kukutana na majini. ‘Alqamah akasema: Mimi nilimuuliza Ibn Mas-‘uwd kama kuna yeyote kati yao ambaye alihudhuria pamoja na Rasuli (Swalla nAllaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) usiku huo. Akasema: Hapana, lakini sisi usiku mmoja tulikuwa pamoja na Rasuli wa Allaah, kisha akatupotea. Tukaanza kumtafuta kwenye mabonde na njia za milimani tusimpate. Tukasema: Pengine majini wameruka naye, au pengine ameuawa. Hapo tukakesha usiku mbaya kabisa ambao watu hawajawahi kukesha. Kulipopambazuka, ghafla tukamwona anakuja kutokea pande za Hiraa. Tukamwambia: Ee Rasuli wa Allaah! Tumekukosa, tukakutafuta sana na wala hatukukupata, na tukakesha usiku mbaya mno ambao hatujawahi kuupitia. Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akatuambia: Alinijia mjumbe wa majini (kunialika) nami nikaongozana naye, kisha nikawasomea Qur-aan. Halafu (Rasuli) akaondoka nasi na akawa anatuonyesha athari zao na athari za mioto yao. Na majini hao walimwomba awaainishie kitu ambacho kitakuwa ni chakula kwao. Akawaambia: Ni haki yenu mifupa yote mnayoipata ambayo imetajiwa Jina la Allaah, mnapoipata itakuwa na nyama nyingi, na pia vinyesi vyote vya wanyama ni malisho kwa wanyama wenu. Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akasema: Basi msistanji kwavyo, kwani ni chakula cha ndugu zenu”. [Swahiyh Muslim: 450]
Ibn Hubayrah amesema: “Katika Hadiyth hii, kuna mambo yanayoonyesha huruma na upole wa Allaah kwa sisi wanadamu. Ametuchagulia sisi vitu vyema na vizuri vya kuvila na Akavifanya baadhi ya tusivyoweza kuvila kama mifupa kuwa chakula kwa ndugu zetu majini. Kwa picha hii, inatakikana kwa Muislamu auhifadhi vizuri mfupa kisha autupe sehemu nzuri kwa niya ya kuwa ni swadaqah kwa majini, lakini pia alitaje Jina la Allaah ili Waumini wa kijini waupate wakiwa na hisia njema. Vile vile, asiuvunje ili waupate ukiwa katika hali bora zaidi ya inavyokuwa nyama”.
Kadhalika, Hadiyth hii inatuonyesha Huruma ya Allaah kwetu kwa kukifanya chakula chetu kitokane na nafaka halisi za mahindi, mpunga, ngano, na kadhalika, na chakula cha wanyama wetu kitokane na majani, ukoka, pumba, chuya na kadhalika. Kadhalika, Amekifanya kinyesi cha wanyama wetu kuwa pia ni chakula kwa majini ili Atufundishe sisi wanadamu kwamba hakuna chochote katika Alivyoviumba Allaah ambacho kinapotea bure, na kwamba vitu pamoja na wingi wake, vimeshakadiriwa kwa kila mmoja katika Viumbe Vyake kuweza kuvitumia.
Jaabir bin ‘Abdullaah (Radhwiya Allaah ‘anhu): Nimemsikia Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akisema:
"إذا دَخَلَ الرَّجُلُ بَيتَه، فذَكَرَ اللَّهَ عِندَ دُخولِهِ وعِندَ طَعامِهِ، قال الشَّيْطَانُ: لا مَبيتَ لَكُم، ولا عَشاءَ، وإذا دَخَلَ فلَم يَذكُرِ اللَّهَ عِندَ دُخولِهِ، قال الشَّيْطَانُ : أدرَكتُمُ المَبيتَ، وإذا لَم يَذكُرِ اللَّهَ عِندَ طَعامِهِ، قال: أدرَكتُمُ المَبيتَ والعَشاءَ"
“Mtu akiingia nyumbani kwake na akamdhukuru Allaah wakati wa kuingia na wakati wa kula, shetani husema (kuwaambia wasaidizi wake): Hamna pa kulala wala pa kula hapa. Na anapoingia bila ya kumdhukuru Allaah wakati anaingia, shetani huwaambia: Mmepata pa kulala hapa. Na kama hakumdhukuru wakati wa kula huwaambia: Mmepata malazi, na mmepata na chakula pia”. [Swahiyh Muslim (2018)]
Hadiyth hii inatufunza fadhla ya kumtaja Allaah ambayo pia ni sababu ya kumfukuza shetani. Shetani anaitumia vizuri nafasi kama mtu ataghafilika kumdhukuru Allaah, na kwamba shetani huyu anakula sambamba na mtu asiyemdhukuru Allaah.
Toka kwa Hudhayfah (Radhwiya Allaah ‘anhu):
"كُنَّا إذا حَضَرنا مَعَ النَّبيِّ صلَّى اللهُ عليه وسلَّم طَعامًا لَم نَضَع أيديَنا حَتَّى يَبدَأَ رَسولُ اللَّهِ صلَّى اللهُ عليه وسلَّم فيَضَعَ يَدَه، وإنَّا حَضَرنا مَعَه مَرَّةً طَعامًا، فجاءَت جاريةٌ كأنَّها تدفَعُ، فذَهَبَت لتَضَعَ يَدَها في الطَّعامِ، فأخذَ رَسولُ اللَّهِ صلَّى اللهُ عليه وسلَّم بَيدِها، ثُمَّ جاء أعرابيٌّ كأنَّما يُدفَعُ فأخذَ بيدِهِ، فقال رَسولُ اللَّهِ صلَّى اللهُ عليه وسلَّم: إنَّ الشَّيْطَان يَستَحِلُّ الطَّعامَ ألَّا يُذكَرَ اسمُ اللَّهِ عليهِ، وإنَّه جاءَ بهذه الجاريةِ ليَستَحِلَّ بها فأخَذْتُ بَيدِها، فجاءَ بهَذا الأعرابيِّ ليَستَحِلَّ بهِ فأخَذْتُ بيدِه، والَّذي نَفسي بيدِه، إنَّ يَدَه في يَدي مَعَ يَدِها"
“Tulikuwa tunapokula chakula pamoja na Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) hatunyooshi mikono yetu mpaka Rasuli aanze kuweka mkono wake. Na mara moja tulikula naye chakula, na ghafla akaja msichana mdogo haraka akiwa kama anasukumwa na kitu. Halafu akasogea ili amege chakula lakini, Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alimkamata mkono. Kisha akaja bedui kana kwamba anasukumwa na kitu, na Rasuli akaukamata mkono wake. Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akasema: Hakika shetani hukihalalisha chakula ambacho hakijatajiwa Jina la Allaah, na shetani amekuja pamoja na binti huyu ili ahalalishe chakula kupitia kwake, na mimi nimeuzuia mkono wake. Akaja pia na bedui huyu ili akihalalishe kupitia kwake, na mimi nimeuzuia mkono wake. Naapa kwa Yule Ambaye Nafsi Yangu iko Mkononi Mwake, hakika mkono wake (shetani) pamoja na wa bedui na wa binti, iko mkononi mwangu nimeikamata”. [Swahiyh Muslim: 2017]
Ibn Hubayrah amesema: “Hapa tunapata kutambua kwamba ni jambo lililokokotezwa kusema “Bismil Laahi” wakati wa kuanza kula, na kwamba Allaah Ta’aalaa Hukibarikia chakula ambacho mlaji anakianza kwa kutaja Jina Lake, kwa vile Anakilinda kutokana na shetani. Shetani anashiriki chakula cha mtu kama hakulitaja Jina la Allaah, kwa sababu Allaah ni nuru kama Alivyosema: “Allaah Ni Nuru ya mbingu na ardhi”. Linapotajwa Jina lake wakati wa kula, nuru hiyo hukifunika chakula hicho. Mwanadamu anaponyooosha mkono wake kwenye chakula bila kusema “Bismil Laah”, hapo humfungulia shetani njia ya kunyoosha mkono wake na kuwa sambamba na mkono wake”.
‘Abdullaah bin ‘Umar (Radhwiya Allaah ‘anhu): Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
"لا يَأكُلَنَّ أحَدٌ مِنكُم بشِمالِهِ، ولا يَشرَبَنَّ بها؛ فإنَّ الشَّيْطانَ يَأكُلُ بشِمالِهِ، ويَشرَبُ بها"
“Asithubutu mmoja wenu kula kwa mkono wake wa kushoto, na wala asinywe kwa mkono huo, kwa sababu shetani anakula kwa mkono wake wa kushoto na anakunywa nao pia”. [Swahiyh Al-Bukhaariy (2020)]
An Nawawiy amesema kuhusu Hadiyth hii: “Tunatakiwa kujiepusha na vitendo vinavyofanana na vya shetani, na tujue kwamba shetani ana mikono miwili”.
Ash-Shibliy amesema: “Wanaosema kwamba majini hawali wala hawanywi, ikiwa wanakusudia kwamba majini wote hawali wala hawanywi, basi kauli yao hiyo ni batili, kwa kuwa inakinzana na Hadiyth nyingi ambazo ni swahiyh zinazothibitisha hili. Lakini ikiwa wanakusudia aina miongoni mwao kwamba hawali wala hawanywi, basi hili lina uwezekano wa kuwa ndio au siyo, isipokuwa ujumla unaashiria kwamba wote wanakula na wanakunywa”.
Majini
Alhidaaya.com [3]
08- Majini Wanakufa Na Watafufuliwa Baada Ya Kufa:
Allaah Ta’aalaa Amesema:
"أُولَـٰئِكَ الَّذِينَ حَقَّ عَلَيْهِمُ الْقَوْلُ فِي أُمَمٍ قَدْ خَلَتْ مِن قَبْلِهِم مِّنَ الْجِنِّ وَالْإِنسِ ۖ إِنَّهُمْ كَانُوا خَاسِرِينَ"
“Hao ndio wale ambao imehakiki juu yao kauli (ya adhabu) kama katika umati nyingi zilizokwishapita kabla yao miongoni mwa majini na wanadamu. Hakika wao wamekuwa ni wenye kukhasirika”. [Al-Ahqaaf: 18]
Ibn ‘Atwiyya amesema: “Kauli Yake: “Umati nyingi zilizokwishapita kabla yao miongoni mwa majini na wanadamu”, inamaanisha kwamba majini wanakufa kama wanavyokufa wanadamu karne baada ya karne”.
Al-Hasan bin Abil Hasan alisema kwenye baadhi ya vikao vyake vya kusomesha ilmu kwamba majini hawafi, lakini Qataadah alimpinga kwa aayah hii, naye akanyamaza.
Lakini baadhi wamemtetea wakisema kwamba anamaanisha kuwa majini wamepewa muhula wa kuishi mpaka siku ya kufufuliwa pamoja na Ibliys. Atakapokufa, na wao pia watakufa pamoja naye kama zinavyoeleza aayaat za Suwrat Al-A’araaf:
"قَالَ أَنظِرْنِي إِلَىٰ يَوْمِ يُبْعَثُونَ ● قَالَ إِنَّكَ مِنَ الْمُنظَرِينَ"
“(Ibliys) akasema: Nipe muhula hadi Siku watakapofufuliwa ● (Allaah) Akasema: Hakika wewe ni miongoni mwa waliopewa muhula”. [Al-A’araaf: 14-15]
Aayah hii inaonyesha kwamba wako watakaopewa muhula wa kuishi mpaka siku hiyo pamoja na Ibliys. Inawezekana ni baadhi ya majini na si wote, kwani hakuna dalili ya kuwa ni wote katika Qur-aan au Sunnah.
Toka kwa ‘Abdullaah bin ‘Abbaas (Radhwiya Allaah ‘anhumaa kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa anasema:
"اللَّهُمُ لَكَ أسلَمتُ، وبِكَ آمَنتُ، وعليكَ تَوَكَّلتُ، وإليكَ أنبْتُ، وبِكَ خاصَمْتُ، اللَّهُمَّ إنّي أعوذُ بعِزَّتِكَ، لا إلَهَ إلَّا أنتَ، أنْ تُضِلَّني، أنتَ الحَيُّ الَّذي لا يَموتُ، والجِنُّ والإنسُ يَموتونَ"
“Ee Allaah! Ni Kwako tu nimejisalimisha, na Wewe tu Ndiye niliyekuamini, na Kwako tu nimetegemeza mambo yangu yote, na Kwako tu ndio nimerejea, na kwa Msaada Wako tu ndio nimeendelea kupambana. Ee Allaah! Ninajilinda kwa Nguvu na Utukufu Wako Ulio imara, hapana wa kuabudiwa kwa haki isipokuwa Wewe, Usije Kuniachia nikaja kupotea, Wewe Ndiye Uliye Hai Ambaye Hafi ilhali majini na watu ndio wanakufa”. [Muslim (2717) na Al-Bukhaariy (7383)]
Abul-‘Abbaas Al-Qurtubiy amesema: “Sababu ya aina hizi mbili (majini na wanadamu) kuhusishwa na umauti ingawa wanyama wote wanakufa, ni kuwa wao ndio waliokalifishwa, na ndio walengwa wa Risala za Mitume. Allaah Ndiye Ajuaye zaidi”.
Na Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
"إنَّ بالمَدِينَةِ نَفَرًا مِنَ الجِنِّ قدْ أسْلَمُوا، فمَن رَأَى شيئًا مِن هذِه العَوامِرِ فَلْيُؤْذِنْهُ ثَلاثًا، فإنْ بَدا له بَعْدُ فَلْيَقْتُلْهُ، فإنَّه شيطانٌ"
“Hakika Madiynah kuna kundi la majini waliosilimu, basi yeyote atakayemwona nyoka yoyote katika hawa ‘awaamir, basi ampe ilani kwamba asionekane tena hapo baada ya siku tatu. Na kama atajitokeza kwake tena baada ya ilani hiyo, basi amuue, kwani huyo ni shetani”. [Swahiyh Muslim (2236)]
"عَوَامِرٌ" (‘Awaamir) ni aina maalum ya nyoka waliokuwa wamezoeleka kuonekana kwenye nyumba za watu huko Madiynah. Na amri ya kumuua kama hakuondoka kwenye nyumba na kwamba atakuwa ni shetani, ni dalili kuwa shetani hufa.
Hivyo basi, majini baadhi ya nyakati huwa wanaishi majumbani mwa watu na wanajiweka katika umbo la nyoka hawa waitwao ‘awaamir.
Majini
Alhidaaya.com [3]
09- Majini Wana Uwezo Wa Kujibadilisha Maumbo Tofauti:
Jumhuwr ya ‘Ulamaa wamethibitisha kwamba majini wanaweza kujiweka katika maumbo tofauti ya kibinadamu, au wanyama na kadhalika. Ibn Taymiyah amesema:
“Majini wanaweza kujitengeneza katika umbo la binadamu, wanyama, nyoka, nge, ndege na kadhalika”.
Dalili zifuatazo zinathibitisha haya:
1- Toka kwa Abud Dardaai (Radhwiya Allaah ‘anhu):
"قامَ رَسولُ اللَّهِ صلَّى اللهُ عليه وسلَّم فسَمِعْناه يَقولُ: أعوذُ باللَّهِ مِنكَ، ثُمَّ قال ألعَنُكَ بلعَنةِ اللهِ ثَلاثًا، وبَسطَ يَدَه كأنَّه يَتَناوَلُ شَيئًا، فلَمَّا فرغَ مِنَ الصَّلاةِ قُلنا: يا رَسولَ اللَّهِ، قد سَمِعناكَ تَقولُ في الصَّلاةِ شَيئًا لَم نَسمَعْكَ تَقولُه قَبلَ ذلك، ورَأيناكَ بَسَطْتَ يَدَكَ، قال: إنَّ عَدوَّ اللَّهِ إبليسَ [12] جاءَ بشِهابٍ من نارِ ليَجعَلَه في وجهي، فقُلتُ: أعوذُ باللهِ مِنكَ، ثَلاثَ مَرَّاتٍ، ثُمَّ قُلتُ: ألعَنُكَ بلعَنةِ اللَّهِ التَّامَّةِ، فلَم يَستَأخِرْ، ثَلاثَ مَرَّاتٍ، ثُمَّ أرَدتُ أخْذَه، واللهِ لَولا دَعوةُ أخينا سُلَيمانَ لأصبَحَ مُوثَقًا يَلعَبُ بهِ وِلْدانُ أهلِ المَدينةِ
“Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alisimama halafu tukamsikia akisema: Najilinda kwa Allaah kutokana na wewe. Halafu akasema mara tatu: Ninakulaani kwa laana ya Allaah, halafu akaukunjua mkono wake kama vile anapokea kitu. Na baada ya kumaliza swalah, tulimwambia: Ee Rasuli wa Allaah! Tumekusikia unasema kitu ndani ya swalah hatujawahi kukusikia ukikisema kabla na tukakuona pia unanyoosha mkono wako. Akasema: “Hakika adui wa Allaah Ibliys alikuja na kijinga cha moto ili anitupie nacho usoni nami nikasema mara tatu: Najilinda kwa Allaah kutokana na wewe, kisha nikasema tena mara tatu: Nakulaani kwa laana iliyotimia ya Allaah, lakini hakuwa tayari kurudi nyuma, kisha nikataka kumkamata. Wa-Allaah, lau si du’aa ya ndugu yetu Sulaymaan, angekuwa amefungwa na kuchezewa na watoto wa watu wa Madiynah”. [Swahiyh kwa sharti ya Muslim]
2- Abu Hurayrah (Radhwiya Allaah ‘anhu) amesema:
"وكَّلني رَسولُ اللَّهِ صلَّى اللهُ عليه وسلَّم بحِفظِ زَكاةِ رَمضانَ، فأتاني آتٍ فجَعَلَ يَحثو مِنَ الطَّعامِ فأخذْتُه، وقُلتُ: واللهِ لأرفَعَنَّك إلى رَسولِ اللَّهِ صلَّى اللهُ عليه وسلَّم، قال: إنِّي مُحتاجٌ، وعليَّ عيالٌ، ولي حاجةٌ شَديدةٌ، قال: فخَلَّيتُ عَنه، فأصبَحْتُ، فقال النَّبيُّ صلَّى اللهُ عليه وسلَّم: يا أبا هُريرةَ، ما فعل أسيرُكَ البارِحةَ؟، قال: قُلتُ: يا رَسولُ اللَّهِ، شَكا حاجةً شَديدةً وعِيالًا فرَحمْتُه، فخَلَّيتُ سَبيلَه، قال: أما إنَّه قد كذَبَكَ وسَيَعودُ، فعَرَفْتُ أنَّه سَيَعودُ؛ لقَولِ رَسولِ اللَّهِ صلَّى اللهُ عليه وسلَّم: إنَّه سَيَعودُ، فرَصدْتُه، فجاءَ يَحثو مِنَ الطَّعامِ، فأخَذْتُه، فقُلتُ: لأرفَعَنَّكَ إلى رَسولِ اللَّهِ صلَّى اللهُ عليه وسلَّم، قال: دَعْني فإنِّي مُحتاجٌ وعليَّ عيالٌ، لا أعودُ، فرَحِمْتُه، فخَلَّيتُ سَبيلَه، فأصبَحْتُ، فقال لي رَسولُ اللَّهِ صلَّى اللهُ عليه وسلَّم: يا أبا هُريرةَ، ما فعل أسيرُكَ؟، قُلتُ: يا رَسولَ اللَّهِ شَكا حاجةً شَديدةً وعيالًا، فرَحمْتُه، فخَلَّيتُ سَبيلَه، قال: أمَا إنَّه قد كذَبَكَ وسَيَعودُ، فرَصدَتُه الثَّالِثةَ، فجاءَ يَحثو مِنَ الطَّعامِ، فأخَذتُه، فقُلتُ: لأرفَعَنَّكَ إلى رَسولِ اللَّهِ، وهَذا آخِرُ ثَلاثِ مَرَّاتٍ، أنَّكَ تَزعُمُ لا تَعودَ، ثُمَّ تَعودُ، قال: دَعْني أعلِّمْكَ كَلِماتٍ يَنفَعُكَ اللهُ بها، قُلتُ: ما هوَ؟ قال: إذا أوَيتَ إلى فراشِكَ، فاقرَأْ آيةَ الكُرسيِّ: اللَّهُ لَا إِلَهَ إِلَّا هُوَ الْحَيُّ الْقَيُّومُ، حَتَّى تَختِمَ الآيةَ، فإنَّكَ لَن يَزالَ عليكَ مِنَ اللَّهِ حافِظٌ، ولا يَقْرَبَنَّكَ شَيطانٌ حَتَّى تُصبِحَ، فخَلَّيتُ سَبيلَه، فأصبَحْتُ، فقالَ لي رَسولُ اللَّهِ صلَّى اللهُ عليه وسلَّم: ما فعل أسيرُكَ البارِحةَ؟، قُلتُ: يا رَسولَ اللَّهِ، زَعَمَ أنَّه يُعَلِّمُني كَلِماتٍ يَنفَعُني اللَّهُ بها، فخَلَّيتُ سَبيلَه، قال: ما هيَ؟، قُلتُ: قال لي: إذا أويتَ إلى فراشِكَ فاقرَأْ آيةَ الكُرسيِّ مِن أوَّلِها حَتَّى تَختِمَ الآيةَ اللَّهُ لَا إِلَهَ إِلَّا هُوَ الْحَيُّ الْقَيُّومُ، وقال لي: لَن يَزالَ عليكَ مِنَ اللَّهِ حافِظٌ، ولا يَقرَبُكَ شَيطانٌ حَتَّى تُصبِحَ ، فقال النَّبيُّ صلَّى اللهُ عليه وسلَّم: أمَا إنَّه قد صَدَقَكَ وهوَ كَذُوبٌ، تَعلَمُ من تُخاطِبُ مُنذُ ثَلاثِ ليالٍ يا أبا هُريرةَ؟، قال: لا، قال: ذاكَ شَيطانٌ"
“Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alinipa jukumu la kulinda zaka ya Ramadhani. Akanijia mtu, halafu akaanza kuteka chakula kwa mikono yake, nami nikamkamata. Nikamwambia: Wal-Laahi, nitakupeleka kwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam). Akasema: Mimi ni mhitaji, nina watoto, na nina dhiki sana. Nikamwachia. Nilipopambaukiwa, Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) aliniuliza: Ee Abu Hurayrah! Alifanya nini mateka wako usiku? Nikasema: Ee Rasuli wa Allaah! Alinililia dhiki na watoto nami nikamhurumia halafu nikamwachilia aende zake. Akasema: Ahaa, basi jua kwamba amekudanganya na kesho atakuja tena, nami nikajua kwa hakika kuwa lazima atarudi tena kutokana na kauli hiyo ya Rasuli. Nikamvizia, na mara akaja tena na kuanza kuchota chakula, na hapo hapo nikamkamata na kumwambia: Nitakupeleka kwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam). Akaniambia: Niachie, mimi ni mhitaji na nina mzigo wa watoto, sitorudi tena hapa. Nikamwonea huruma na kumwachia aende zake. Ilipoingia asubuhi, Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) aliniambia: Ee Abu Hurayrah! Nini alifanya mateka wako? Nikasema: Ee Rasuli wa Allaah! Alinililia dhiki kubwa na watoto, nami nikamhurumia na kumwacha aende zake. Akasema: Basi ujue kwamba amekudanganya na atarudi. Nikamvizia tena mara ya tatu, naye akaja, akaanza kuchota chakula, nami hapo hapo nikamkamata. Nikamwambia: Nitakupeleka kwa Rasuli wa Allaah, na hii ni mara ya tatu ya mwisho, unadai hutorudi kisha unarudi. Akasema: Niache nikufundishe maneno ambayo Allaah Atakunufaisha kwayo. Nikamuuliza: Ni yepi hayo? Akasema: Unapokwenda kitandani kwako kulala, basi soma Aayatul Kursiy اللَّهُ لَا إِلَهَ إِلَّا هُوَ الْحَيُّ الْقَيُّومُ mpaka mwisho wa Aayah, hapo wewe utabaki na mlinzi anayekulinda toka kwa Allaah. Na kamwe shaytwaan hatokukurubia mpaka upambaukiwe, nami nikamwachia aende zake. Ilipoingia asubuhi, Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) aliniambia: Mateka wako alifanya nini jana? Nikamwambia: Ee Rasuli wa Allaah! Alidai kwamba atanifundisha maneno ambayo Allaah Ataninufaisha kwayo, nami nikamwachia aende zake. Akaniuliza: Ni maneno gani hayo? Nikamwambia: Aliniambia: Ukienda kitandani kwako kulala, basi soma Aayatul Kursiy toka mwanzo wake hadi mwisho اللَّهُ لَا إِلَهَ إِلَّا هُوَ الْحَيُّ الْقَيُّومُ . Akasema: Mlinzi toka kwa Allaah ataendelea kukulinda, na shaytwaan hatokukurubia mpaka asubuhi. Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akaniambia: Basi ujue kwamba amekwambia ukweli lakini yeye ni mwongo kupindukia. Basi je, unamjua ni nani huyo uliyekuwa unazungumza naye toka siku hizo tatu zilizopita ee Abu Hurayrah? Nikasema hapana. Akasema: Huyo ni shetani”. [Swahiyhul Bukhaariy (2311)]
Akizungumzia faida tuzipatazo kutokana na Hadiyth hii, Ibn Hajar amesema: “Tunapata kujua kwamba shetani anaweza kujua mambo ambayo Muislamu anaweza kufaidika nayo, lakini pia anaweza kujiweka katika baadhi ya maumbo yatakayomfanya aonekane na mwanadamu, na kwamba Kauli Yake Ta’aalaa:
"إِنَّهُ يَرَاكُمْ هُوَ وَقَبِيلُهُ مِنْ حَيْثُ لَا تَرَوْنَهُمْ"
“Hakika yeye (Ibliys) anakuoneni, yeye na kabila lake (la mashaytwaan) na hali ya kuwa nyinyi hamuwaoni, linahusiana tu pale shetani anapokuwa katika umbile lake la asili aliloumbiwa kwalo, hapo haiwezekani, (lakini akijiweka katika umbile la binadamu au mnyama, hapo anaonekana kama alivyojiweka)”.
Ni kama alivyojiweka katika sura ya mwanadamu mwizi wa chakula kwa Abu Hurayrah kwa mujibu wa Hadiyth iliyotangulia.
3- Toka kwa Abu As -Saaib:
"أنَّه دَخَل على أبي سَعيدٍ الخُدْريِّ في بَيتِهِ، قال: فوَجَدتُه يُصَلِّي، فجَلَسْتُ أنتَظِرُه حَتَّى يَقضيَ صَلاتَه، فسَمِعتُ تَحريكًا في عَراجِينَ في ناحيةِ البَيتِ، فالتفَتُّ فإذا حَيَّةٌ، فوَثَبْتُ لأقتُلَها، فأشارَ إليَّ: أن اجلِسْ، فجَلَسْتُ، فلَمَّا انصَرَفَ أشارَ إلى بَيتٍ في الدَّارِ فقال: أترى هَذا البَيتَ؟ فقُلت: نَعَم. فقال: كانَ فيه فتًى مِنَّا حَديثُ عَهْدٍ بعُرسٍ. فخَرَجْنا مَعَ رَسولِ اللَّهِ صلَّى اللهُ عليه وسلَّم إلى الخَندَقِ، فكانَ ذلك الفَتى يَستَأذِنُ رَسولَ اللَّهِ صلَّى اللهُ عليه وسلَّم بأنصافِ النَّهارِ فيَرجِعُ إلى أهلِهِ، فاستَأذَنَه يَومًا فقال لَه رَسولُ اللَّهِ صلَّى اللهُ عليه وسلَّم: خُذْ عليكَ سِلاحَكَ، فإنِّي أخشى عليكَ قُرَيظةَ، فأخذَ الرَّجُلُ سِلاحَه، ثُمَّ رَجَعَ فإذا امرَأتُه بَينَ البابَين قائِمةً، فأهوى إليها الرُّمحَ ليَطعَنَها بهِ، وأصابَتْه غَيرةٌ، فقالت لَه: اكفُفْ عليكَ رُمحَكَ، وادخُلِ البَيتَ حَتَّى تَنظُرَ ما الَّذي أخرَجَني! فدَخلُ فإذا بحيَّةٍ عَظيمةٍ مُنْطَويةٍ على الفِراشِ، فأهوى إليها بالرُّمحِ فانتَظَمَها بهِ، ثُمَّ خَرجَ فرَكزَه في الدَّارِ، فاضطَرَبت عليهِ، فما يُدرى أيُّهُما كانَ أسرَعَ مَوتًا الحَيَّةُ أمِ الفَتى؟ قال: فجِئْنا إلى رَسولِ اللَّهِ صلَّى اللهُ عليه وسلَّم فذَكَرْنا لَه، وقُلنا: ادْعُ اللهَ يُحييهِ لَنا، فقال: استَغفِروا لصاحِبِكُم، ثُمَّ قال: إنَّ بالمَدينةِ جِنًّا قد أسلَموا، فإذا رَأيتُم مِنهم شَيئًا فآذِنوه ثَلاثةَ أيَّامٍ، فإنْ بَدا لَكُم بَعدَ ذلك فاقتُلوه، فإنَّما هوَ شَيطانٌ"
“Kwamba aliingia kwenye nyumba ya Abu Sa’iyd Al-Khudriy. Anasema: Nikamkuta anaswali. Nikakaa kumsubiri mpaka alipomaliza kuswali. Halafu nikasikia mchakato wa sauti toka kwenye mzigo wa kuni pembezoni mwa nyumba. Nikageuka, kushtuka, naona ni nyoka. Nikaruka ili nimuue, lakini yeye aliniashiria niketi, nami nikaketi. Alipomaliza, alinionyesha chumba kwenye nyumba yake na kuniambia: Unakiona chumba hiki? Nikamwambia naam. Akaniambia: Humu alikuwemo kijana ambaye alikuwa ndio bado bwana harusi, nasi tukatoka pamoja na Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kwenda kwenye Vita vya Khandaq. Kijana huyo alikuwa akiomba ruksa kwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) katikati ya mchana ili kwenda kwa mkewe. Na siku moja, alipomwomba ruksa, Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alimwambia: Chukua silaha yako, usiisahau, kwani mimi ninakuhofia na Quraydhwah (wanaweza kukudhuru). Kijana akachukua silaha yake na kuelekea nyumbani kwake. Alipofika, akashtuka kumwona mkewe amesimama kati ya milango miwili. Hapo hapo wivu ukamchemka, akainama na kuukamata vizuri mkuki wake ili ampige nao. Mkewe akamwambia: Weka chini mkuki wako, halafu ingia ndani uangalie nini kilichonitoa humo. Akaingia, mara kushtuka, akaona joka limejiviringisha kitandani, na hapo hapo alilidunga kwa mkuki likajisokota, kisha akaukita chini mkuki, akageuka ili atoke nje ya nyumba. Lakini bila kutarajia, joka lile lilijisukuma likamgonga, haijulikani nani alikufa kabla ya mwingine, ni joka au kijana. Tukaja kwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) tukamhadithia. Tukamwambia: Mwombe Allaah Atuhuishie. Akasema: Mwombeeni maghfira mwenzenu. Kisha akasema: Hakika Madiynah kuna majini ambao wamesilimu, hivyo basi, mkiona chochote kinachoashiria kwamba ni wao, basi wapeni ilani kwamba wasionekane tena baada ya siku tatu, na kama watajitokeza tena kwenu baada ya hapo, basi waueni, kwani hao ni mashetani”.
Neno lake Rasuli “Hakika Madiynah kuna majini ambao wamesilimu”, haimaanishi kwamba kwingineko kusiko Madiynah hakuna majini waliosilimu, bali wako kila mahali, hivyo basi katazo la kuwaua ni sehemu zote ila tu kama watadhihiri tena baada ya kuwahadharisha na kutoa onyo kwao. Kadhalika, hatuwezi kufahamu kutokana na Hadiyth hii kama jini huyo ambaye kijana alimuua, alikuwa ni Muislamu au la, na kama pia jini huyo naye alimuua kijana kulipiza kisasi. Vile vile, kijana huyu pia hakukusudia kuua nafsi ya Muislamu kwa kuwa hakuwa akijua, bali alikusudia kuua kile ambacho kisharia kimeruhusiwa kuuawa. Hivyo basi, tunaloweza kusema hapa ni kuwa majini makafiri au waovu wao ndio waliomuua kijana kiuadui na kulipizia kisasi.
4- Toka kwa ‘Abdullaah bin ‘Umar (Radhwiya Allaah ‘anhumaa):
"أنَّه كانَ يَقتُلُ الحَيَّاتِ ثُمَّ نَهى، قال: إنَّ النَّبيَّ صلَّى اللهُ عليه وسلَّم هَدمَ حائِطًا لَه، فوَجَدَ فيه سِلْخَ حَيَّةٍ، فقال: انظُروا أينَ هوَ؟ فنَظَروا، فقال: اقتُلوه. فكُنتُ أقتُلُها لذلك، فلَقِيتُ أبا لُبابةَ، فأخبَرَني أنَّ النَّبيَّ صلَّى اللهُ عليه وسلَّم قال: لا تَقتُلوا الجِنَّ [13]انَ إلَّا كُلَّ أبتَرَ ذي طُفْيَتَينِ؛ فإنَّه يُسقِطُ الوَلَدَ، ويُذهِبُ البَصَرَ، فاقتُلوه"
“Kwamba yeye alikuwa anaua nyoka, kisha akakataza akisema: “Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) aliwahi kubomoa ukuta wake, akakuta chini yake gamba la nyoka. Akasema: Mtafuteni alikojificha, wakamtafuta, wakamwona, akawaambia: Muueni. Nikawa nawaua kutokana na amri hiyo. Kisha ‘Abdullaah bin ‘Umar akasema: Nikaja kukutana na Abu Lubaabah, akanieleza kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: Msiwaue nyoka waliozoeleka kuonekana majumbani, isipokuwa kila mwenye mkia mfupi na mistari miwili mgongoni, huyo huangusha mimba na huleta upofu, muueni”. [Swahiyhul Bukhaariy (3310)]
Ibn Hajar Al-Haytamiy amesema: Kuwavua wenye sifa hizi mbili, kunamaanisha kwamba jini hawezi kujiweka katika umbo lao (la kasoro ya kimwili), hivyo hawa ni vyema kuwaua.
5- Jaabir bin ‘Abdullaah amesema:
"أَمَرَنَا رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ بِقَتْلِ الْكِلَابِ حَتَّى إِنَّ الْمَرْأَةَ تَقْدَمُ منَ الْبَادِيةِ بِكَلْبِهَا فَنَقْتُلَهُ، ثُمَّ نَهَى رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ عَنْ قَتْلِهَا وَقَالَ: عَلَيْكُمْ بِالْأَسْوَدِ الْبَهِيمِ ذِي النُّقْطَتَيْن فَإِنَّهُ شَيْطَان"
“Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alituamuru kuwaua mbwa, hata ikawa mwanamke anakuja tokea majangwani na mbwa wake nasi tunamuua. Kisha baadaye Rasuli akakataza kuwaua, na akasema: Muueni tu mweusi mwenye vitone viwili, kwa sababu huyo ni shaytwaan”. [Hadiyth Swahiyh. Imekharijiwa na Muslim (1572) na Abu Daawuwd (2846)].
6- Toka kwa Abu Dharr (Radhwiya Allaah ‘anhu): Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
"إذا قامَ أحَدُكُم يُصَلِّي، فإنَّه يَستُرُه إذا كانَ بَينَ يَدَيهِ مِثلُ آخِرةِ الرَّحلِ، فإذا لَم يَكُن بَينَ يَدَيهِ مِثلُ آخِرةِ الرَّحْلِ، فإنَّه يَقطَعُ صَلاتَهُ الحِمارُ والمَرأةُ والكَلبُ الأسوَدُ. قُلتُ: يا أبا ذر، ما بالُ الكَلبِ الأسوَدِ مِنَ الكَلبِ الأحمَرِ مِنَ الكَلبِ الأصفَرِ؟ قال: يا ابنَ أخي، سَألتُ رَسولَ اللَّهِ صلَّى اللهُ عليه وسلَّم كما سَألتَني فقال: الكَلبُ الأسوَدُ شَيطانٌ"
“Anaposimama mmoja wenu kuswali, basi na ajiwekee mbele yake kizuizi (sutrah) chenye urefu wa kwenda juu wa kiasi cha sogi ya ngamia. Na kama hana chenye urefu huo, basi kwa hakika swalah yake itakatwa na punda, au mwanamke au mbwa mweusi. Nikasema: Ee Abu Dharr! Mbwa mweusi ana nini hata awe tofauti na mbwa mwekundu au mbwa wa njano?! Akasema: Ee mtoto wa ndugu yangu, nilimuuliza Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) swali hilo hilo uliloniuliza, naye akasema: Mbwa mweusi ni shetani”. [Hadiyth Swahiyh. Swahiyh Muslim (510)]
Kuhusiana na kauli ya Rasuli “Mbwa mweusi ni shetani” Ulamaa wamesema yafuatayo:
- Kwamba kikawaida shetani hujiweka katika umbo la mbwa mweusi, na kwa ajili hiyo akasema: Waueni kila mweusi ti ti ti kati yao.”.
- Kwa vile mbwa mweusi ndiye mwenye madhara zaidi kuliko mwingine na mwenye kutisha zaidi, na mwenye kuswali anapomwona, basi hutetereka akapoteza khushuu, na swalah yake ikakatika.
- Anayekusudiwa ni mbwa mweusi kama alivyo, na si vinginevyo.
- Jini hujimathilisha katika sura ya mbwa mweusi na pia paka mweusi, kwa sababu weusi ni chanzo cha mkusanyo wa nguvu za kishetani, na ndani yake kuna nguvu ya joto.
Kuna Uwezekano Wa Kiasi Gani Wa Mwanadamu Kumwona Jini?
Kiujumla, mwanadamu anaweza kumwona jini katika umbo jingine lisilo umbo lake la asili.
Muhammad Rashiyd Ridhwaa amesema: “Malaika au jini akijiweka katika picha ya mwanadamu au kiumbe kingine, basi mwanadamu anaweza kumwona, lakini mwanadamu hawezi kuwaona hao katika umbo lao la asili”.
Ibn Baaz amesema: “Jini anaweza kujidhihirisha kwa baadhi ya watu, na baadhi ya watu wanaweza kuwasiliana nao, wanaweza kuwasemesha wakajibishana, baadhi ya watu wanaweza kuwaona, lakini kiuhalisia, majini hawaonekani kama Alivyosema Allaah Ta’aalaa:
"إِنَّهُ يَرَاكُمْ هُوَ وَقَبِيلُهُ مِنْ حَيْثُ لَا تَرَوْنَهُمْ"
“Hakika yeye (Ibliys) anakuoneni, yeye na kabila lake (la mashaytwaan) na hali ya kuwa nyinyi hamuwaoni”.
Na jini anaweza kujitokeza akaonekana na baadhi ya watu majangwani au katika nyumba, na anaweza akamsemesha mwanadamu. ‘Ulamaa wengi wametuhadithia matukio mengi kuhusiana na hili. Hata baadhi yao wameeleza kwamba baadhi ya majini wamewahi kuhudhuria majaalisi zao za kiilmu, na wakauliza baadhi ya maswali ya kiilmu wakiwa hawaonekani”.
Kiufupi, ‘Ulamaa wamekhitilafiana kuhusiana na uwezekano kwa binadamu kuwaona majini katika maumbile yao halisi. Baadhi yao wanasema kwamba uwezekano huo uko kwa Manabii basi, lakini wengine wanasema hilo pia linawezekana kwa yeyote ambaye Allaah Ametaka awaone katika Waja Wake.
Ibn Al-‘Arab amesema: “Hakuna kizuizi cha kumzuia Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kuwaona majini katika umbile lao asili kama anavyowaona Malaika. Ama kwa sisi, mara nyingi wanadhihiri katika umbo la nyoka”.
Na Hadiyth zinazogusia Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Maswahaba wake kuwaona majini, matamshi yake ni jumuishi. Ima yanabeba uwezekano wa kuwaona katika umbile lao halisi, au kuwaona katika umbo jinginelo. Allaah Ndiye Ajuaye zaidi”.
Kati ya Hadiyth hizo ni:
1- - Toka kwa Abu Hurayrah: “Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
"إنَّ عِفْريتًا مِنَ الجِن ِّتَفَلَّتَ البارِحةَ ليَقطَعَ عَليَّ صَلاتي، فأمكَنَني اللَّهُ مِنه فأخَذْتُه، فأرَدتُ أن أربِطَه على ساريةٍ من سَوارَي المَسجِدِ حَتَّى تَنظُروا إليهِ كُلُّكُم، فذَكَرْتُ دَعوةَ أخي سُلَيمانَ: رَبِّ هَبْ لي مُلْكًا لا يَنبَغي لأحَدٍ من بَعْدي، فرَدَدتُه خاسِئًا"
“Hakika afriti mmoja katika majini alinitokezea ghafla ili anivurugie swalah yangu, lakini Allaah Alinipa nguvu nikaweza kumdhibiti. Nikataka kumfunga kwenye nguzo moja kati ya nguzo za Msikiti ili nyinyi nyote muweze kumwona. Na hapo nikakumbuka dua ya ndugu yangu Sulaymaan: Rabb wangu! Nitunukie ufalme asiupate mtu yeyote baada yangu, kisha nikamwachia aende zake akiwa amedhalilika”.. [Hadiyth Swahiyh. Al-Bukhaariy (461)]
2- Hadiyth ya Abu Hurayrah inayohusiana na shetani aliyekuja kuiba chakula cha zaka, akmkamata akiwa katika umbo la binadamu.
Majini
Alhidaaya.com [3]
10- Uwezo Wa Baadhi Ya Wanyama Kuwaona Majini:
Baadhi ya wanyama wana uwezo wa kuwaona majini. Dalili zifuatazo zinathibitisha hili:
1- Abu Hurayrah (Radhwiya Allaah ‘anhu): Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
"إذا سَمِعتُم صياحَ الدِّيَكةِ فاسألوا اللهَ مِنْ فَضْلِه؛ فإنَّها رَأت مَلَكًا، وإذا سَمِعتُم نَهيقَ الحِمارِ فتَعوَّذوا باللَّهِ مِنَ الشيطان؛ فإنَّه رَأى شَيطانًا"
“Mkisikia jogoo wanawika, basi mwombeni Allaah Fadhla Zake, kwani wanakuwa wamemwona Malaika. Na mnaposikia sauti kali ya punda, basi jilindeni kwa Allaah na shetani, kwani anakuwa amemwona shetani”. [Al-Bukhaariy (3303) na Muslim (2729)]
Ibn Al-‘Abbaas Al-Qurtubiy amesema: “Hii inaonyesha kwamba Allaah Ta’aalaa Amemuumbia jogoo utambuzi wa kuweza kumwona Malaika kama Alivyomuumbia punda utambuzi wa kuweza kumwona shetani”.
2- Jaabir (Radhwiya Allaah ‘anhu): Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
"إذا سَمِعتُمْ نِباحَ الكِلابِ، ونَهِيقَ الحَمِيرِ بِالليلِ فتَعَوَّذُوا بِاللهِ من الشيطانِ، فإنَّهُنَّ يَرَيْنَ ما لا تَرَوْنَ، وأَقِلُّوا الخُروجَ إذا هَدَأَتِ الرِّجْلُ؛ فإِنَّ اللهَ عزَّ وجَلَّ يَبُثُّ في لَيْلِهِ من خَلْقِهِ ما يَشاءُ، وأَجِيفُوا الأبوابَ، واذْكُرُوا اسْمَ اللهِ علَيْهَا؛ فإِنَّ الشَّيطانَ لا يَفتَحُ بابًا أُجِيفَ وذُكِرَ اسْمُ اللهِ عليْهِ، وغَطُّوا الجِرارَ، وأوْكِئُوا القِرَبَ، وأكْفِئُوا الآنِيَةَ"
“Mkisikia mbweko wa mbwa au mlio wa punda usiku, basi jilindeni kwa Allaah na shetani, kwa kuwa wao wanaona msivyoviona. Na punguzeni kutoka (usiku) barabara zikiwa hazina watu, kwani Allaah ‘Azza wa Jalla Hueneza katika usiku Wake vyovyote Anavyovitaka katika Viumbe Vyake. Na fungeni milango, na litajeni Jina la Allaah wakati wa kuifunga, kwani shetani hawezi kufungua mlango uliotajiwa Jina la Allaah wakati wa kuufunga. Na funikeni vyombo, midomo ya vyungu itatieni kitambaa, na vyombo vitupu vipindueni”. [Hadiyth Swahiyh. Imechakatwa na Abu Daawuwd (5103) na Ahmad (14422)]
‘Umar Al-Ashqar amesema: “Wanyama kuweza kuona vile tusivyoviona si jambo geni. Wataalamu wamethibitisha kwamba baadhi ya viumbe vinaweza kuona vitu ambavyo sisi hatuwezi kuviona. Kwa mfano, buma anaweza kumwona panya ndani ya giza totoro”.
Majini
Alhidaaya.com [3]
11- Wana Spidi Ya Juu Na Uwezo Wa Kufanya Kazi Ngumu:
Kati ya majini hao, ni wale ambao Allaah Alimtiishia Nabiy Sulaymaan (‘alayhis salaam) wakawa wanamfanyia kazi kubwa za sulubu. Allaah Ta’aalaa Analielezea hili Akisema:
" وَمِنَ الْجِنِّ مَن يَعْمَلُ بَيْنَ يَدَيْهِ بِإِذْنِ رَبِّهِ ۖ وَمَن يَزِغْ مِنْهُمْ عَنْ أَمْرِنَا نُذِقْهُ مِنْ عَذَابِ السَّعِيرِ ● يَعْمَلُونَ لَهُ مَا يَشَاءُ مِن مَّحَارِيبَ وَتَمَاثِيلَ وَجِفَانٍ كَالْجَوَابِ وَقُدُورٍ رَّاسِيَاتٍ ۚ اعْمَلُوا آلَ دَاوُودَ شُكْرًا ۚ وَقَلِيلٌ مِّنْ عِبَادِيَ الشَّكُورُ"
“Na (Tulimtiishia pia) kati ya majini wanaofanya kazi mbele yake kwa Idhini ya Rabb wake. Na yeyote atakayezikengeuka Amri Zetu, Tunamuonjesha adhabu ya moto uliowashwa vikali mno ● Wanamfanyia kazi atakayo; (kujenga) ngome ndefu za fakhari na tasawiri, na madeste makubwa kama mahodhi na masufuria makubwa yaliyothibiti imara. (Tukasema): Tendeni enyi familia ya Daawuwd huku mkishukuru! Na wachache miongoni mwa Waja Wangu ndio wenye kushukuru”. [Sabaa: 13]
Na Anasema tena:
"فَسَخَّرْنَا لَهُ الرِّيحَ تَجْرِي بِأَمْرِهِ رُخَاءً حَيْثُ أَصَابَ ● وَالشَّيَاطِينَ كُلَّ بَنَّاءٍ وَغَوَّاصٍ"
“Basi Tukamtiishia upepo unaokwenda kwa amri yake polepole popote anapotaka kufika ● Na mashaytwaan, kila ajengaye na mpiga mbizi”. [Swaad: 36-37]
Na Nabiy Sulaymaan (‘alayhis salaam) alipotaka kukileta kiti cha enzi cha Malkia wa Sabaa, alisema kama inavyosema Qur-aan:
"قَالَ يَا أَيُّهَا الْمَلَأُ أَيُّكُمْ يَأْتِينِي بِعَرْشِهَا قَبْلَ أَن يَأْتُونِي مُسْلِمِينَ • قَالَ عِفْرِيتٌ مِّنَ الْجِنِّ أَنَا آتِيكَ بِهِ قَبْلَ أَن تَقُومَ مِن مَّقَامِكَ ۖ وَإِنِّي عَلَيْهِ لَقَوِيٌّ أَمِينٌ"
“Akasema: Enyi wakuu! Nani kati yenu ataniletea kiti chake cha enzi kabla hawakunijia wakiwa wamesilimu? ● Akasema ‘Ifriti miongoni mwa majini: Mimi nitakuletea kabla hujasimama kutoka mahali pako, na hakika mimi kwa hilo, bila shaka ni mwenye nguvu mwaminifu”. [Sabaa: 38-39]
Kadhalika, Qur-aan imegusia uwezo wao wa kuzifikia anga za juu kabisa na kuzivinjari ili kudukua habari za mbinguni. Allaah Anasema:
"وَأَنَّا لَمَسْنَا السَّمَاءَ فَوَجَدْنَاهَا مُلِئَتْ حَرَسًا شَدِيدًا وَشُهُبًا • وَأَنَّا كُنَّا نَقْعُدُ مِنْهَا مَقَاعِدَ لِلسَّمْعِ ۖ فَمَن يَسْتَمِعِ الْآنَ يَجِدْ لَهُ شِهَابًا رَّصَدًا"
“Na kwamba sisi tulitafuta kuzifikia mbingu, basi tukazikuta zimejaa walinzi wakali na vimondo • Na kwamba sisi tulikuwa tukikaa huko vikao kwa ajili ya kusikiliza, basi atakayetega sikio kusikiliza sasa atakuta kimondo kinamvizia”. [Al-Jinn: 8-9]
Vile vile, Nabiy Sulaymaan (‘alayhis salaam) alikuwa akitumikiwa na majini wapiga mbizi na wafanyao kazi nyinginezo. Allaah Ta’aalaa Anasema:
"وَمِنَ الشَّيَاطِينِ مَن يَغُوصُونَ لَهُ وَيَعْمَلُونَ عَمَلًا دُونَ ذَٰلِكَ ۖ وَكُنَّا لَهُمْ حَافِظِينَ"
“Na (Tukamtiishia) miongoni mwa mashaytwaan wakimpigia mbizi na wakimfanyia kazi nyinginezo zisizokuwa hizo. Nasi Tulikuwa Ni Wenye Kuwalinda”. [Al-Anbiyaa: 82]
Ash-Shinqiytwy amesema: “Walikuwa wakizamia kwenye vina vya bahari na kumtolea kutoka humo vito vya thamani kama lulu na marijani. Walikuwa pia wakimfanyia kazi nyingine kama kujenga miji, makasri, vyungu vikubwa na mengineyo katika kazi zenye ufanisi wa hali ya juu”.
Lakini majini haya pamoja na uwezo huo mkubwa waliopewa, hawawezi kufanya baadhi ya mambo . Kati yake ni:
1- Hawawezi kuleta muujiza wowote kama ile waliyokuja nayo Mitume (‘alayhimus Salaam). Allaah Ta’aalaa Amekanusha Qur-aan kuwa ni kazi ya mashetani, na Akabainisha kwamba hawawezi kuleta chochote katika Qur-aan, Akisema:
"وَمَا تَنَزَّلَتْ بِهِ الشَّيَاطِينُ • وَمَا يَنبَغِي لَهُمْ وَمَا يَسْتَطِيعُونَ • إِنَّهُمْ عَنِ السَّمْعِ لَمَعْزُولُونَ"
“Na wala hawakuteremka nayo (hii Qur-aan) mashaytwaan • Na wala haipasi kwao na wala hawawezi ● Hakika wao bila shaka wametengwa mbali kuisikiliza”. [Ash-Shu’araa: 210-212]
Na hata majini na wanadamu kwa pamoja, Allaah Amewapa changamoto kwamba hata kama wataungana, hawawezi kuleta mfano wa Qur-aan hii. Allaah Amesema:
"قُل لَّئِنِ اجْتَمَعَتِ الْإِنسُ وَالْجِنُّ عَلَىٰ أَن يَأْتُوا بِمِثْلِ هَـٰذَا الْقُرْآنِ لَا يَأْتُونَ بِمِثْلِهِ وَلَوْ كَانَ بَعْضُهُمْ لِبَعْضٍ ظَهِيرًا "
“Sema: Ikiwa watajumuika wana Aadam na majini ili walete mfano wa hii Qur-aan; hawatoweza kuleta mfano wake na japokuwa watasaidiana wao kwa wao”. [Al-Israa: 88]
2- Hawawezi kujimathilisha wakaja kwenye ndoto au njozi ya mtu katika sura ya Nabiy wetu Muhammad (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam).
Abu Hurayrah (Radhwiya Allaah ‘anhu): Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
"من رَآني في المَنامِ فقد رَآني؛ فإنَّ الشيطان لا يَتَمَثَّلُ بي"
“Atakayeniona usingizini basi atakuwa ameniona kikweli, kwa sababu shetani hawezi kujimathilisha katika sura yangu”. ”
Ibn Hajar amesema: “Hadiyth inaashiria kwamba pamoja na kwamba Allaah Ta’aalaa Amempa jini au shetani uwezo wa kujigeuza katika umbo lolote alitakalo, lakini Hakumpa uwezo wa kujiweka katika sura au umbo la Nabiy Muhammad (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam)”.
3- Hawawezi kuvuka mipaka maalum kwenye mbingu za juu.
Allaah Anasema:
"يَا مَعْشَرَ الْجِنِّ وَالْإِنسِ إِنِ اسْتَطَعْتُمْ أَن تَنفُذُوا مِنْ أَقْطَارِ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ فَانفُذُوا ۚ لَا تَنفُذُونَ إِلَّا بِسُلْطَانٍ"
“Enyi jamii ya majini na watu! Mkiweza kupenya kwenye zoni za mbingu na ardhi, basi penyeni. Hamtoweza kupenya isipokuwa kwa mamlaka (ya Allaah). [Ar-Rahmaan: 33]
4- Hawawezi kufungua mlango uliotajiwa Jina la Allaah wakati wa kuufunga
Toka kwa Jaabir (Radhwiya Allaah ‘anhu): Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
"فإنَّ الشَّيْطَانَ لا يَفتَحُ بابًا مُغلَقًا، وأوكُوا قِرَبَكُم، واذَكُروا اسمَ اللَّهِ، وخَمِّروا آنيَتَكُم، واذَكُروا اسمَ اللَّهِ، ولَو أن تَعرِضوا عليها شَيئًا، وأطفِؤوا مَصابيحَكُم"
“Kwani hakika shetani hawezi kufungua mlango uliofungwa, zibeni midomo ya vyungu vyenu, litajeni Jina la Allaah, funikeni vyombo vyenu na litajeni Jina la Allaah ijapokuwa kwa kuweka kitu juu yake, na zimeni taa zenu”. [Al-Bukhaariy (5623) na Muslim (2012)]
5- Hawakuweza kumdhuru ‘Iysaa na mama yake wakati walipozaliwa
Toka kwa Abu Hurayrah (Radhwiya Allaah ‘anhu): Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
"ما من مَولودٍ يُولَدُ إلَّا والشَّيْطَان َيمَسُّه حينَ يُولَدُ، فيَستَهِلُّ صارِخًا من مَسِّ الشّيْطَانِ إيَّاه، إلَّا مَريَم وابنَها، ثُمَّ يَقولُ أبو هُريرةَ: واقرَؤوا إنْ شِئتُم: وَإِنِّي أُعِيذُهَا بِكَ وَذُرِّيَّتَهَا مِنَ الشَّيْطَانِ [12] الرَّجِيمِ"
“Hakuna mtoto yeyote anayezaliwa isipokuwa shetani humgusa wakati anapozaliwa na mtoto huanza kulia kutokana na mguso huo wa shetani, isipokuwa Maryam na mwanaye (hawa hawakuguswa)”. Kisha Abu Hurayrah akasema: Someni mkitaka:
"وَإِنِّي أُعِيذُهَا بِكَ وَذُرِّيَّتَهَا مِنَ الشَّيْطَانِ الرَّجِيمِ"
“Nami namkinga Kwako na dhuria wake kutokana na shetani aliyetokomezwa mbali na kulaaniwa”. [Aal ‘Imraan: 36]
Ibn Hubayrah amesema: “Hadiyth hii inatuonyeha ni namna gani ulivyo uadui wa shetani kwa mwanadamu kiasi cha kwamba anapoona mtoto kazaliwa tu, hapo hapo humchokonoa mtoto apate kulia. Na kwa ajili hiyo, Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) anatutaka tuwe tunajilinda nyakati zote na adui huyu pamoja na watoto wetu”.
Pia Hadiyth inatufunza kwamba Allaah Ta’aalaa Alimlinda Bi Maryam pamoja na mwanaye kutokana na shetani baada ya Bi Maryam kuomba kinga hiyo kutoka Kwake.
Majini
Alhidaaya.com [3]
12- Mahala Wanakoishi Majini:
1- Majini kiujumla wanaishi ardhini. Allaah Ta’aalaa Amesema:
"قَالَ اهْبِطُوا بَعْضُكُمْ لِبَعْضٍ عَدُوٌّ ۖ وَلَكُمْ فِي الْأَرْضِ مُسْتَقَرٌّ وَمَتَاعٌ إِلَىٰ حِينٍ"
“Akasema: Shukeni! Nyinyi kwa nyinyi ni maadui. Na ardhi itakuwa ndio mastakimu yenu na starehe kwenu mpaka muda mahsusi”. [Al-A’araaf: 24]
Amesema Ibn ‘Aashuwr: Wanaosemeshwa hapa ni Aadam na mkewe pamoja na Ibliys. Na kwa amri hiyo, Aadam, mkewe na Ibliys wamekuwa ni katika wakazi wa ardhi”.
Allaah Amesema tena:
"وَالْأَرْضَ وَضَعَهَا لِلْأَنَامِ"
“Na ardhi Ameiweka chini kwa ajili ya viumbe”. [Ar-Rahmaan: 10]
Al-Hasan amesema viumbe hapa ni watu na majini.
Linalotilia nguvu kuwa wasemeshwa katika aayah hii ni majini na binadamu ni Kauli Yake Ta’alaa baada ya kutaja kila neema katika Neema Zake:
"فَبِأَيِّ آلَاءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ"
“Basi ni zipi Neema za Rabb wenu mnazikadhibisha?”
2- Majumbani mwa watu:
Kuna kundi la majini ambalo linaishi pamoja na watu majumbani mwao. Hawa ni wale wanaojiweka katika umbo la nyoka kisha wakaingia majumbani. Ni kama kisa kilichopita nyuma cha kijana aliyekuwa bado ni bwana harusi, akaliua joka lililokuwa nyumbani kwake, na joka nalo likamuua kijana.
Na kwa ajili hiyo, Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amekataza kuua nyoka wanaoonekana majumbani kabla ya kuwapa indhari, kwa kuwa wako majini Waislamu kati yao.
Toka kwa Naafi’i:
"أنَّ أبا لُبابةَ كُلَّمَ ابن عمر ليَفتَحَ لَه بابًا في دارِهِ، يَستَقرِبُ بهِ إلى المَسجِدِ. فوجَدَ الغِلْمةُ جِلْدَ جانٍّ. فقال عَبدُ اللهِ: التَمِسوه فاقتُلوه. فقال أبو لُبابةَ: لا تَقتُلوه؛ فإنَّ رَسولَ اللَّهِ صلَّى اللهُ عليه وسلَّم نَهى عَن قَتلِ الجِنَّانِ الَّتي في البُيوتِ"
“Kwamba Abu Lubaabah alizungumza na (‘Abdullaah) bin ‘Umar kumtaka amfungulie mlango wa nyumba yake ili Msikiti upate kuwa karibu yake. Kijana ‘Abdullaah bin ‘Umar akakuta ngozi ya nyoka (wakati anaufungua mlango) na hapo hapo akasema: Msakeni mumuue. Lakini Abu Lubaabah akasema: Msimuue, kwani Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amekataza kuua nyoka walioko majumbani”. [Al-Bukhaariy (3312, 3313) na Muslim (2233)]
3- Mwahala penye najisi nyingi kama vyooni, ndani ya mifumo ya maji taka na kadhalika.
Zayd bin Arqam: “Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
"إنَّ هذه الحُشوشَ مُحتَضَرةٌ، فإذا أتى أحَدُكُمُ الخَلاءَ فليَقُلْ: أعوذُ باللهِ مِنَ الخُبُثِ والخَبائِثِ"
“Hakika sehemu hizi za kufanyia haja zimekaliwa (na majini na mashetani). Hivyo basi, anapoingia mmoja wenu chooni aseme: Najilinda kwa Allaah kutokana na majini wabaya wanaume na majini wabaya wanawake”. [As-Silsilat As-Swahiyhah: 1070]
Kwa mujibu wa Hadiyth hii, vyooni, msalani, bafuni na kadhalika, ndio makazi ya majini na mashetani. Na kwa ajili hiyo, Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) anatuamuru tujikinge kwa Allaah wakati wa kuingia sehemu hizi kutokana shari za viumbe hawa ambao wanaweza kumdhuru mtu.
4- Sehemu wanakolala ngamia au kupumzikia.
Jaabir bin Samurah (Radhwiya Allaah ‘anhu amesema:
"فعَن جابِرِ بْنِ سَمُرةَ رَضِيَ اللهُ عَنه: أنَّ رَجُلًا سَألَ رَسولَ الله صلَّى اللهُ عليه وسلَّم: أأتَوضَّأُ من لُحومِ الغَنَمِ؟ قال: إنْ شِئْتَ فتوَضَّأْ، وإنْ شِئْتَ فلا توَضَّأْ، قال: أتَوَضَّأُ من لُحومِ الإبِلِ؟ قال: نَعَم فتَوَضَّأْ من لُحومِ الإبلِ قال: أصَلِّي في مَرابِضِ الغَنَمِ؟ قال: نَعَم، قال: أصَلِّي في مَبارِكِ الإبِلِ؟ قال: لا"
Toka kwa Jaabir bin Samurah (Radhwiya Allaah ‘anhu): Mtu mmoja alimuuliza Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akimwambia: Je, nitawadhe kama nimekula nyama ya mbuzi au kondoo? Akamwambia: Ukitaka unaweza kutawadha, na kama hutaki usitawadhe. Akamuuliza tena: Je, nitawadhe kwa kula nyama ya ngamia? Akamwambia: Naam, tawadha ukila nyama ya ngamia. Akauliza tena: Je, naweza kuswali kwenye zizi la mbuzi na kondoo? Akamwambia naam. Akauliza: Naweza kuswali wanakopumzikia ngamia? Akamwambia hapana”. [Swahiyh Muslim: 360]
Baadhi ya ‘Ulamaa wamesema sababu ya katazo ni kuwa mwahala hapo ni makazi ya mashetani.
Abu Hurayrah: “Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
"صَلُّوا في مَرابِضِ الغَنَمِ، ولا تُصَلُّوا في أعطانِ الإبِلِ"
“Swalini kwenye zizi la mbuzi na kondoo, lakini msiswali sehemu wanakolala na kupumzika ngamia”.
Ibn Taymiyah amesema: “Mahala ambapo pamekatazwa kuswali kama chooni na mapumzikio ya ngamia ni makazi ya mashetani. Kadhalika, mapango ambayo watu wanafunga safari kuyaendea kwa lengo la kuyatukuza pamoja na maeneo yake husika, kwa kuwa mahala popote ambapo watu wanapatukuza ambapo si Misikiti au maeneo ya kufanyiwa amali za hijja, basi mwahala hapo ni makazi ya mashetani. Mashetani hao hujiweka katika maumbo ya wanadamu ili watu waone kwamba wao ni katika wanadamu kama Anavyosema Allaah Ta’aalaa:
"وَأَنَّهُ كَانَ رِجَالٌ مِّنَ الْإِنسِ يَعُوذُونَ بِرِجَالٍ مِّنَ الْجِنِّ فَزَادُوهُمْ رَهَقًا"
“Na kwamba walikuwa wanaume miongoni mwa wanadamu wanajikinga na wanaume miongoni mwa majini, basi wakawazidishia madhambi, uvukaji mipaka ya kuasi na khofu”. [Al-Jinn: 06]
5- Kwenye mashimo.
Toka kwa Qataadah toka kwa ‘Abdullaah bin Sarjas (Radhwiya Allaah ‘anhu):
"أنَّ النَّبيَّ صلَّى اللهُ عليه وسلَّم نَهى أن يُبالَ في الجُحْرِ"
“Kwamba Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amekataza mtu kukojoa kwenye tundu (la shimo)”.
Qataadah aliulizwa: Kwa nini imekatazwa kukojoa kwenye tundu (la shimo)? Akasema: “Ilikuwa inasemwa kwamba shimo ni makazi ya majini”.
الجُحْر kama alivyosema Al-Minaawiy ni kila pahali ambapo wadudu na wanyama wanajichimbia wenyewe kwa ajili ya kukaa humo na kuishi.
6- Kwenye masoko ili kuwafitini watu.
Kwa ajili hiyo, Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amekataza mtu kukaa sana masokoni. Alisema akimuusia Salmaan Al-Faarisiy (Radhwiya Allaah ‘anhu):
"لا تَكونَنَّ إنِ استَطَعْتَ أوَّلَ مَن يَدخُلُ السُّوقَ، ولا آخِرَ مَن يَخرُجُ مِنها؛ فإنَّها مَعْرَكَةُ الشَّيْطَانِ وبِها يَنصِبُ رايَتَه"
“Ukiweza, usije kuwa mtu wa mwanzo kuingia sokoni wala wa mwisho kutoka humo, kwani soko ni medani ya vita ya shetani, na hapo ndipo anaposimika bendera yake”. [Swahiyh Muslim (2451)]
Majini
Alhidaaya.com [3]
13- Aina Za Majini Kutokana Na Maumbo Yao
Toka kwa Abu Tha’alabah Al-Khushaniy (Radhwiya Allaah ‘anhu): Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
"الجِنُّ [13] ثَلاثةُ أصنافٍ: صِنْفٌ لَهم أجنِحةٌ يَطيرونَ في الهَواءِ، وصِنفٌ حَيَّاتٌ وكِلابٌ، وصِنْفٌ يَحلُّونَ ويَظعَنونَ"
“Majini ni sampuli tatu: Sampuli ya wenye mbawa ambao wanaruka hewani, sampuli ya nyoka na mbwa, na sampuli ya wanaokaa sehemu na kusafiri”. [Ni swahiyh. Iko katika Mishkaat Al Maswaabiyh (4148)]
Majini
Alhidaaya.com [3]
14- Sampuli Za Majini Kwa Upande Wa Imani Zao
Na Ukafiri Wao Na Wema Wao Na Ufisadi Wao
Allaah Akilizungumzia hili Anasema:
"وَأَنَّا مِنَّا الصَّالِحُونَ وَمِنَّا دُونَ ذَٰلِكَ ۖ كُنَّا طَرَائِقَ قِدَدًا"
“Na kwamba miongoni mwetu ni wema, na miongoni mwetu wako chini ya hivyo; tumekuwa makundi ya njia mbali mbali”. [Al-Jinn: 11]
Ibn Jariyr amesema: “Tumekuwa makundi ya njia mbali mbali”, yaani tumekuwa wenye matamanio tofauti, makundi mbalimbali, na kati yetu yuko Muumini na yuko kafiri”.
Naye Al-Qurtubiy kasema: “Waliambiana wenyewe kwa wenyewe wakati walipowalingania wenzao wamuamini Muhammad (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam): Hakika sisi kabla ya kuisikiliza Qur-aan, tulikuwa baadhi yetu walio wema na baadhi yetu walio makafiri”.
Na Anasema tena Allaah Ta’aalaa:
"وَأَنَّا مِنَّا الْمُسْلِمُونَ وَمِنَّا الْقَاسِطُونَ ۖ فَمَنْ أَسْلَمَ فَأُولَـٰئِكَ تَحَرَّوْا رَشَدًا"
“Na kwamba miongoni mwetu ni Waislamu, na miongoni mwetu wako wakengeukaji haki; hivyo atakayesilimu, basi hao ndio waliofuata uongofu”. [Al-Jinn: 14]
Ibn Al-Qayyim amesema: “Aayaat hizi zinatuonyesha mgawanyiko wao wa matabaka matatu: Walio wema, walio chini ya walio wema na makafiri. Matabaka haya ndio yale yale waliyo nayo wanadamu ambao wako wema, walio kati na kati na makafiri. Vigawanyo hivi ndivyo vile vile ambavyo Allaah Ta’aalaa Aliwagawa Bani Israaiyl kama Anavyosema:
"وَقَطَّعْنَاهُمْ فِي الْأَرْضِ أُمَمًا ۖ مِّنْهُمُ الصَّالِحُونَ وَمِنْهُمْ دُونَ ذَٰلِكَ ۖ وَبَلَوْنَاهُم بِالْحَسَنَاتِ وَالسَّيِّئَاتِ لَعَلَّهُمْ يَرْجِعُونَ "
“Na Tuliwafarikisha katika ardhi mataifa mbalimbali. Miongoni mwao ni wako wema na miongoni mwao wako kinyume chake. Na Tukawajaribu kwa ya faraja na ya dhiki ili wapate kurejea (katika utiifu). [Al-A’araaf: 168]
.
Ibn Al-Baaz amesema: “Kuna majini wema, wazushaji (bid’a), makafiri na mafasiki kama walivyo wanadamu”.
Naye Ibn ‘Uthaymiyn kasema: “Majini wapo Waumini, makafiri, watiifu na waasi. Allaah Ta’aalaa Amesema:
"قَالَ ادْخُلُوا فِي أُمَمٍ قَدْ خَلَتْ مِن قَبْلِكُم مِّنَ الْجِنِّ وَالْإِنسِ فِي النَّارِ"
“(Allaah) Atasema: Ingieni motoni pamoja na ummah zilizokwishapita kabla yenu miongoni mwa majini na wana Aadam”. [Al-A’araaf: 38]
Na akasema tena: “Ulimwengu wa majini asili yake ni kutokana na moto, kwa kuwa baba yao ni shetani Ibliys. Huyu, Allaah Alimuumba kutokana na moto. Kisha katika ulimwengu wao, wako walio wema na wasio wema, wako Waislamu na wako makafiri, ijapokuwa asili yao ni Ibliys aliye kafiri. Wako pia wenye kutafuta elimu na wako waliobobea kwenye ibada”.
Majini
Alhidaaya.com [3]
15- Majina Ya Majini:
1- Ifriti "العِفْرِيتُ"
"قَالَ عِفْرِيتٌ مِّنَ الْجِنِّ أَنَا آتِيكَ بِهِ قَبْلَ أَن تَقُومَ مِن مَّقَامِكَ ۖ وَإِنِّي عَلَيْهِ لَقَوِيٌّ أَمِينٌ"
“Akasema ‘Ifriti miongoni mwa majini: Mimi nitakuletea kabla hujasimama kutoka mahali pako, na hakika mimi kwa hilo, bila shaka ni mwenye nguvu mwaminifu”. [An-Naml: 39]
Ibn Jariyr amesema: “Ifriti miongoni mwa majini ni mkuu wao, aliye shupavu zaidi na mwenye nguvu”.
Toka kwa Abu Hurayrah: “Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
"إنَّ عِفْريتًا مِنَ الجِن ِّتَفَلَّتَ البارِحةَ ليَقطَعَ عَليَّ صَلاتي، فأمكَنَني اللَّهُ مِنه فأخَذْتُه، فأرَدتُ أن أربِطَه على ساريةٍ من سَوارَي المَسجِدِ حَتَّى تَنظُروا إليهِ كُلُّكُم، فذَكَرْتُ دَعوةَ أخي سُلَيمانَ: رَبِّ هَبْ لي مُلْكًا لا يَنبَغي لأحَدٍ من بَعْدي، فرَدَدتُه خاسِئًا"
“Hakika ifriti mmoja katika majini alinitokezea ghafla ili anivurugie swalah yangu, lakini Allaah Alinipa nguvu nikaweza kumdhibiti. Nikataka kumfunga kwenye nguzo moja kati ya nguzo za Msikiti ili nyinyi nyote muweze kumwona. Na hapo nikakumbuka dua ya ndugu yangu Sulaymaan: Rabb wangu! Nitunukie ufalme asiupate mtu yeyote baada yangu, kisha nikamwachia aende zake akiwa amedhalilika”.. [Hadiyth Swahiyh. Al-Bukhaariy (461)]
2- Ghoul الغُولُ: (Mashetani wa majangwani)
Jaabir bin ‘Abdillaah (Radhwiya Allaah ‘anhu): Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
"لا عَدوَى ولا طِيَرةَ ولا غُولَ"
“Ugonjwa hauambukizi (ila kwa Idhni ya Allaah), wala hakuna mkosi (kwa kuona ndege anakwenda kushoto), wala mashetani wa majangwani hawadhuru kwa lolote (ila kwa Idhni ya Allaah)”. [Swahiyhul Jaami (7531)]
Ibn Hajar amesema: “Jopo la ‘Ulamaa wamesema: “Waarabu walikuwa wakidai kwamba maghoul ambao ni aina ya mashetani, wapo kwenye majangwa. Mashetani hawa huwatokezea watu wakiwa katika rangi tofauti tofauti, halafu huwapoteza njia, na hatimaye huwaua. Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akaja na kuiondosha itikadi hii”.
Na makusudio hapa si kukanusha uwepo wa maghoul, bali wapo, isipokuwa tu hayo waliyokuwa wakiyaamini Waarabu ndio ambayo hayapo.
Ibn ‘Uthaymiyn amesema: “Waarabu walipokuwa wanasafiri, au wanakwenda kulia au kushoto, mashetani walikuwa wakiwatokezea kwa rangi za kutisha na kuogopesha na nyoyo zao zikaingia hofu kubwa. Na hapo wanapatwa na majonzi na huzuni kubwa ya kutoweza kwenda kule walikokusudia. Na hili bila shaka linadhoofisha nguvu ya kumtegemea Allaah. Na shetani wakati wote ni mwenye pupa ya kuingiza wasiwasi na huzuni kwa Muislamu kiasi anavyoweza. Allaah Anasema:
"إِنَّمَا النَّجْوَىٰ مِنَ الشَّيْطَانِ لِيَحْزُنَ الَّذِينَ آمَنُوا وَلَيْسَ بِضَارِّهِمْ شَيْئًا إِلَّا بِإِذْنِ اللَّـهِ ۚ وَعَلَى اللَّـهِ فَلْيَتَوَكَّلِ الْمُؤْمِنُونَ"
“Hakika mnong’ono unatokana na shaytwaan ili awahuzunishe wale walioamini, na wala hawezi kuwadhuru kwa chochote isipokuwa kwa Idhini ya Allaah. Na kwa Allaah watawakali Waumini”. [Al-Mujaadalah: 10]
Na mtu mara nyingi hutahiniwa kwa mambo haya ikiwa moyo wake umefungamanika nayo. Ama ikiwa ni mwenye kumtegemea Allaah, basi hakuna lolote la kumdhuru.
Majini
Alhidaaya.com [3]
16- Nasaba Zao Na Nchi Zao:
Majini wana makabila na mataifa kama tulivyo sisi wanadamu. Allaah Akiwazungumzia majini walioisikiliza Qur-aan toka kwa Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) Anasema:
"يَا قَوْمَنَا أَجِيبُوا دَاعِيَ اللَّـهِ وَآمِنُوا بِهِ يَغْفِرْ لَكُم مِّن ذُنُوبِكُمْ وَيُجِرْكُم مِّنْ عَذَابٍ أَلِيمٍ"
“Enyi kaumu yetu! Mwitikieni Mlinganiaji wa Allaah, na mwaminini. (Allaah) Atakughufurieni madhambi yenu, na Atakukingeni na adhabu iumizayo”. [Al-Ahqaaf: 31]
Na Anasema tena Allaah ‘Azza wa Jalla:
"إِنَّهُ يَرَاكُمْ هُوَ وَقَبِيلُهُ مِنْ حَيْثُ لَا تَرَوْنَهُمْ"
“Hakika yeye (Ibliys) anakuoneni, yeye na kabila lake (la mashaytwaan) na hali ya kuwa nyinyi hamuwaoni”.
Na baadhi ya majini ni raia na wakazi wa maeneo na nchi tofauti kwa mujibu wa vipimo vyao wenyewe kama tulivyo sisi wanadamu. Kati ya hao, ni kundi la majini waliomjia Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) toka Nasibin.
Nasibin ulikuwa ni mji kati ya Sham na Iraki. Inasemekana pia ulikuwa Yemen.
Toka kwa Abu Hurayrah (Radhwiya Allaah ‘anhu) kwamba:
" كانَ يَحمِلُ مَعَ النَّبيِّ صلَّى اللهُ عليه وسلَّم إدواةً لوُضوئِهِ وحاجَتِهِ، فبَينَما هوَ يَتبَعُه بها فقال: من هَذا؟ فقال: أنا أبو هُريرةَ، فقال: أبغِني أحجارًا أستَنفِضُ بها، ولا تَأتِني بعَظمٍ ولا بِرَوْثةٍ، فأتَيتُه بأحجارٍ أحمِلُها في طَرَفِ ثَوبي حَتَّى وضعْتُها إلى جَنبِهِ، ثُمَّ انصَرَفْتُ، حَتَّى إذا فرَغَ مَشَيتُ فقُلتُ: ما بالُ العَظمِ والرَّوْثةِ؟! قال: هُما من طَعَامِ الجِنِّ، وإنَّه أتاني وفدُ جِنِّ نَصيبِينَ، ونِعْمَ الجِنِّ فسَألوني الزَّادَ، فدَعَوتُ اللهَ لَهم ألَّا يَمُرُّوا بعَظمٍ ولا بِرَوثةٍ إلَّا وجَدوا عليها طعمًا"
Abu Hurayrah (Radhwiya Allaah ‘anhu) ameeleza kwamba alikuwa pamoja na Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na alikuwa amembebea kiriba cha maji yake ya kutawadhia na kustanjia. Na wakati akiwa anamfuata nyuma akiwa na kiriba hicho, Rasuli aliuliza: Nani huyu? Akasema: Mimi Abu Hurayrah. Akamwambia: Niletee vijiwe nipate kustanjia kwavyo, lakini usiniletee mfupa wala kinyesi cha mnyama. Nikamletea vijiwe ambavyo nilivibeba kwenye ncha ya nguo yangu na kuviweka pembeni mwake halafu nikaondoka. Nikasubiri hadi alipomaliza halafu nikamwendea na kumuuliza: Imekuwaje nisikuletee mfupa au kinyesi cha mnyama? Akasema: Viwili hivi ni chakula cha majini. Na kwa hakika ulinijia ujumbe wa majini wa Nasibin, ni wema walioje majini hao! Wakaniomba chakula, nami nikawaombea kwa Allaah kwamba wasipite popote ulipo mfupa au kinyesi cha mnyama isipokuwa wapate humo chakula”. [Swahiyhul Bukhaariy: 3860]
Sababu ya Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kuwasifu majini hao kuwa ni wema wa majini, ni yale yaliyosimuliwa na At-Tirmidhiy toka kwa Jaabir aliyesema:
"خرَج رَسولُ اللهِ صلَّى اللهُ عليه وسلَّمَ على أصْحابِه، فقَرأَ عليهم سُورةَ الرَّحمَنِ مِن أوَّلِها إلى آخِرِها، فسَكَتوا، فقال: لقد قَرأْتُها على الجِنِّ ليلةَ الجِنِّ، فكانوا أحسَنَ مَرْدودًا منكم؛ كُنتُ كلَّما أتَيْتُ على قولِه: "فَبِأَيِّ آلَاءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ"، قالوا: لا بشَيءٍ مِن نِعَمِكَ ربَّنا نُكذِّبُ، فلكَ الحَمدُ"
“Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alitoka kwa Maswahaba wake akawasomea Suwrat Ar-Rahmaan kuanzia mwanzo hadi mwisho, nao wakanyamaza bila kujibu kitu. Akawaambia: Hakika niliwasomea majini usiku nilipokutana nao (suwrah hii), nao walijibisha vizuri sana kukushindeni nyinyi. Nilikuwa kila nikifika kwenye Kauli Yake Ta’aalaa:
"فَبِأَيِّ آلَاءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ"
“Basi ni ipi katika Neema za Rabb wenu mnaweza kuikanusha?”…wao walikuwa wakijibu: Hakuna neema yoyote kati ya neema Zako ee Rabbi wetu tunayoikanusha, na Himdi unastahiki Wewe tu”. [Hadiyth Hasan. Swahiyhul Jaami’i (5138)]
Majini
Alhidaaya.com [3]
17- Ibliys
Neno Ibliys "إِبْلِيْسُ" katika lugha ya kawaida limenyambulika kutokana na "الإبْلاسُ" lenye maana ya kuwekwa mbali na kheri, au kukata tamaa kutokana na Rahma za Allaah. Kwa maana hii, Ibliys kawekwa mbali na kheri zote, na hana tamaa kamwe ya kuzipata Rahma za Allaah, na kwa hivyo, ni kiumbe wa kuishia motoni milele.
Ama kiistilahi, Ibliys ni kiumbe aliyeumbwa kutokana na moto. Alikuwa pamoja na Malaika akifanya pamoja nao ibada, lakini hakuwa ni katika aina yao. Na wakati Allaah Alipowaamuru Malaika Wake wamsujudie Aadam, Ibliys alikataa kutii Amri ya Mola Wake kwa kujiona kwamba yeye ni bora zaidi kuliko Aadam kwa kuwa yeye ameumbwa kutokana na moto aliouona ni bora zaidi kuliko udongo alioumbiwa nao Aadam. Yakawa matokeo ya kukaidi kwake amri ni kufukuzwa toka kwenye Rahma ya Allaah na kuteremshwa toka mbinguni kuja ardhini.
Lakini Ibliys alimwomba Allaah Ampe muhula wa kuishi mpaka Siku ya kufufuliwa. Na hapo Allaah Ambaye Ni Mwingi wa Subira Akamkubalia ombi lake, na Ibliys akachukua ahadi ya kuwapoteza wanadamu mpaka wakati huo kama inavyosema Qur-aan:
"قَالَ فَبِعِزَّتِكَ لَأُغْوِيَنَّهُمْ أَجْمَعِينَ ● إِلَّا عِبَادَكَ مِنْهُمُ الْمُخْلَصِينَ"
(Ibliys) akasema: Naapa kwa Utukufu Wako, bila shaka nitawapotosha wote • Isipokuwa waja Wako miongoni mwao waliokhitariwa kwa ikhlasi zao. [Swaad: 82-83]
Majini
Alhidaaya.com [3]
18 Shaytwaan
Ama shaytwaan "الشَّيْطَانُ"katika lugha ya kawaida, ni kila aliye mwasi, mwovu, mshari, ni sawa akiwa katika majini, au wanadamu au wanyama. Asili yake ni kutokana na neno "شَطَنَ" (kitenzi cha wakati uliopita) chenye maana ya “amejiweka mbali”, na hii ni kwa vile shaytwaan amejiweka mbali na kheri zote au Rahma za Allaah
Qur-aan imemwita kwa jina la Shaytwaan katika aayah mbalimbali. Ni kama katika Kauli Yake Ta’alaa:
"فَوَسْوَسَ لَهُمَا الشَّيْطَانُ لِيُبْدِيَ لَهُمَا مَا وُورِيَ عَنْهُمَا مِن سَوْآتِهِمَا وَقَالَ مَا نَهَاكُمَا رَبُّكُمَا عَنْ هَـٰذِهِ الشَّجَرَةِ إِلَّا أَن تَكُونَا مَلَكَيْنِ أَوْ تَكُونَا مِنَ الْخَالِدِينَ "
“Basi shaytwaan (naye ni Ibliys) akawatia wasiwasi ili awafichulie sehemu zao za siri zilizositiriwa. Na akasema: Rabb wenu Hakukukatazeni huu mti isipokuwa msijekuwa Malaika wawili au kuwa miongoni mwa wenye kudumu milele”. [Al-A’araaf: 20]
Na Kauli Yake Ta’aalaa:
"يَا بَنِي آدَمَ لَا يَفْتِنَنَّكُمُ الشَّيْطَانُ كَمَا أَخْرَجَ أَبَوَيْكُم مِّنَ الْجَنَّةِ يَنزِعُ عَنْهُمَا لِبَاسَهُمَا لِيُرِيَهُمَا سَوْآتِهِمَا"
“Enyi wana wa Aadam! Asikufitinisheni kabisa shaytwaan kama alivyowatoa wazazi wenu katika Jannah, huku akiwavua nguo zao ili awaonyeshe sehemu zao za siri”. [Al-A’araaf: 27]
Ama kiistilahi, tamko la "الشَّيطانِ" linaweza kukusudiwa kwa maana ya Ibliys mwenyewe hasa kama katika kisa cha Aadam na Ibliys. Pia linaweza kukusudiwa kila mbaya, mharibifu, na mwenye kulingania upotevu katika majini au binadamu. Ni kama Kauli Yake Ta’aalaa:
"وَكَذَٰلِكَ جَعَلْنَا لِكُلِّ نَبِيٍّ عَدُوًّا شَيَاطِينَ الْإِنسِ وَالْجِنِّ يُوحِي بَعْضُهُمْ إِلَىٰ بَعْضٍ زُخْرُفَ الْقَوْلِ"
“Na hivyo ndivyo Tulivyojaalia kwa kila Nabiy maadui mashaytwaan wa kibinadamu na kijini, wanadokezana wenyewe kwa wenyewe maneno ya kupambapamba”. [Al-A’araaf: 112]
Majini
Alhidaaya.com [3]
19 Sifa Za Shaytwaan
Shaytwaan amesifiwa katika Qur-aan kwa sifa mbaya. Kati ya sifa hizo ni:
1- Rajiym "الرَّجِيْمُ" (Aliyelaaniwa, aliyewekwa mbali na Rahma za Allaah)
Sifa hii imetajwa katika aayah zifuatazo:
"قَالَ فَاخْرُجْ مِنْهَا فَإِنَّكَ رَجِيمٌ"
“(Allaah) Akasema: Basi toka humo, kwani hakika wewe umetokomezwa mbali na kulaaniwa”. [Al-Hijr: 34]
Hii ni baada ya Ibliys kukataa kumsujudia Aadam.
Anasema tena Allaah:
"فَإِذَا قَرَأْتَ الْقُرْآنَ فَاسْتَعِذْ بِاللَّـهِ مِنَ الشَّيْطَانِ الرَّجِيمِ"
“Unaposoma Qur-aan basi (kwanza) omba kinga kwa Allaah dhidi ya shaytwaan aliyetokomezwa mbali na kulaaniwa. [An-Nahl: 98]
Pia,
"فَلَمَّا وَضَعَتْهَا قَالَتْ رَبِّ إِنِّي وَضَعْتُهَا أُنثَىٰ وَاللَّـهُ أَعْلَمُ بِمَا وَضَعَتْ وَلَيْسَ الذَّكَرُ كَالْأُنثَىٰ ۖ وَإِنِّي سَمَّيْتُهَا مَرْيَمَ وَإِنِّي أُعِيذُهَا بِكَ وَذُرِّيَّتَهَا مِنَ الشَّيْطَانِ الرَّجِيمِ"
“Basi alipomzaa akasema: Rabb wangu! Hakika mimi nimezaa mwanamke, na Allaah Anajua zaidi alichokizaa. Na mwanamme si kama mwanamke. Nami nimemwita Mayram, nami namkinga Kwako na dhuria wake kutokana na shaytwaan aliyetokomezwa mbali na kulaaniwa”. [Aal-‘Imraan: 36]
2- Al-Maarid "المَارِدُ" (aliyeasi)
Hili ni katika aayaat zifuatazo:
"وَحِفْظًا مِّن كُلِّ شَيْطَانٍ مَّارِدٍ"
“Na hifadhi kutokana na kila shaytwaan asi”. [As-Swaaffaat: 07]
"وَمِنَ النَّاسِ مَن يُجَادِلُ فِي اللَّـهِ بِغَيْرِ عِلْمٍ وَيَتَّبِعُ كُلَّ شَيْطَانٍ مَّرِيدٍ "
“Na miongoni mwa watu kuna ambao wanaobishana kuhusu Allaah bila ya elimu, na wanafuata kila shaytwaan muasi”. [Al-Hajj: 03]
“إِن يَدْعُونَ مِن دُونِهِ إِلَّا إِنَاثًا وَإِن يَدْعُونَ إِلَّا شَيْطَانًا مَّرِيدًا “
“Hawaombi badala Yake isipokuwa miungu ya kike na hawaombi isipokuwa shaytwaan muasi”. [An-Nisaa: 117]
Majini
Alhidaaya.com [3]
20 Je, Ibliys Ni Katika Majini Au Malaika?
"وَإِذْ قُلْنَا لِلْمَلَائِكَةِ اسْجُدُوا لِآدَمَ فَسَجَدُوا إِلَّا إِبْلِيسَ أَبَىٰ وَاسْتَكْبَرَ وَكَانَ مِنَ الْكَافِرِينَ "
“Na pale Tulipowaambia Malaika: Msujudieni Aadam. Wakasujudu isipokuwa Ibliys alikataa na akatakabari na akawa miongoni mwa makafiri”. [Al-Baqarah: 34]
"وَلَقَدْ خَلَقْنَاكُمْ ثُمَّ صَوَّرْنَاكُمْ ثُمَّ قُلْنَا لِلْمَلَائِكَةِ اسْجُدُوا لِآدَمَ فَسَجَدُوا إِلَّا إِبْلِيسَ لَمْ يَكُن مِّنَ السَّاجِدِينَ"
“Na kwa yakini Tumekuumbeni kisha Tukakutieni sura; kisha Tukawaambia Malaika: Msujudieni Aadam. Wakasujudu isipokuwa Ibliys hakuwa miongoni mwa waliosujudu”. [Al-A’araaf: 11]
"فَسَجَدَ الْمَلَائِكَةُ كُلُّهُمْ أَجْمَعُونَ" ● إِلَّا إِبْلِيسَ اسْتَكْبَرَ وَكَانَ مِنَ الْكَافِرِينَ "
“Wakamsujudia Malaika wote pamoja ● Isipokuwa Ibliys, alitakabari na akawa miongoni mwa makafiri”. [Swaad: 73-74]
Kadhalika, imeelezwa kiwazi ndani ya Qur-aan kwamba Ibliys ni katika majini. Allaah Ta’aalaa Amesema:
"وَإِذْ قُلْنَا لِلْمَلَائِكَةِ اسْجُدُوا لِآدَمَ فَسَجَدُوا إِلَّا إِبْلِيسَ كَانَ مِنَ الْجِنِّ فَفَسَقَ عَنْ أَمْرِ رَبِّهِ ۗ أَفَتَتَّخِذُونَهُ وَذُرِّيَّتَهُ أَوْلِيَاءَ مِن دُونِي وَهُمْ لَكُمْ عَدُوٌّ ۚ بِئْسَ لِلظَّالِمِينَ بَدَلًا "
“Na pindi Tulipowaambia Malaika: Msujudieni Aadam. Wakasujudu isipokuwa Ibliys, alikuwa miongoni mwa majini, akaasi Amri ya Rabb wake. Je, basi mnamfanya yeye na kizazi chake walinzi pasi Nami; na hali wao kwenu ni maadui? Ubaya ulioje mbadala huu kwa madhalimu!”. [Al-Kahf: 50]
Ibliys hakuwa katika Malaika, bali yeye anatokana na majini.
Al-Hasan Al-Baswriy amesema: “Ibliys hakuwa kamwe katika Malaika, bali asili yake ni majini kama alivyo Aadam ambaye ni asili ya wanadamu”.
‘Abdulrahmaan bin Zayd bin Aslam amesema: “Ibliys ndiye baba wa majini kama alivyo Aadam ambaye ni baba wa wanadamu”.
Ibn Shihaab amesema: “Ibliys ni baba wa majini kama ilivyo kwa Aadam ambaye ni baba wa wanadamu. Ibliys ametokana na majini, naye ndiye baba yao. Na hili liko wazi kwa wote kutokana na Kauli Yake Ta’aalaa:
"وَإِذْ قُلْنَا لِلْمَلَائِكَةِ اسْجُدُوا لِآدَمَ فَسَجَدُوا إِلَّا إِبْلِيسَ كَانَ مِنَ الْجِنِّ فَفَسَقَ عَنْ أَمْرِ رَبِّهِ ۗ أَفَتَتَّخِذُونَهُ وَذُرِّيَّتَهُ أَوْلِيَاءَ مِن دُونِي وَهُمْ لَكُمْ عَدُوٌّ ۚ بِئْسَ لِلظَّالِمِينَ بَدَلًا "
“Na pindi Tulipowaambia Malaika: Msujudieni Aadam. Wakasujudu isipokuwa Ibliys, alikuwa miongoni mwa majini, akaasi Amri ya Rabb wake. Je, basi mnamfanya yeye na kizazi chake walinzi pasi Nami, na hali wao kwenu ni maadui?! Ubaya ulioje mbadala huu kwa madhalimu!”. [Al-Kahf: 50]
Az-Zajjaaj amesema: “Kundi la mabingwa wa lugha wamesema: “Ibliys hakuwa kamwe katika Malaika. Na dalili ya hilo ni Kauli Yake Ta’aalaa:
“Wakasujudu isipokuwa Ibliys, alikuwa miongoni mwa majini”. Wakaulizwa: Imewezekana vipi akatolewa nje ya kundi lao? Wakajibu kwamba Malaika pamoja na yeye waliamuriwa kusujudu, na dalili ya kwamba aliamuriwa pamoja nao kusujudu ni Kauli Yake Ta’aalaa:
"وَإِذْ قُلْنَا لِلْمَلَائِكَةِ اسْجُدُوا لِآدَمَ فَسَجَدُوا إِلَّا إِبْلِيسَ أَبَىٰ وَاسْتَكْبَرَ وَكَانَ مِنَ الْكَافِرِينَ "
“Na pale Tulipowaambia Malaika: Msujudieni Aadam. Wakasujudu isipokuwa Ibliys, alikataa na akatakabari na akawa miongoni mwa makafiri”. [Al-Baqarah: 34]
Hivyo basi, yeye hakukataa isipokuwa kwamba aliamrishwa, akagoma. Kauli hii sisi ndio tunaichagua”.
Ibn Hazm kasema: “Baadhi ya watu wanadai kwamba Ibliys alikuwa ni Malaika, kisha akaasi. Hili haliwezekani kwa Utakasifu wa Allaah Ambaye Amelikadhibisha hilo katika Kauli Yake:
إِلَّا إِبْلِيسَ كَانَ مِنَ الْجِنِّ
“Isipokuwa Ibliys, alikuwa miongoni mwa majini”.
Na Kauli Yake pia:
أَفَتَتَّخِذُونَهُ وَذُرِّيَّتَهُ أَوْلِيَاءَ مِن دُونِي
.”Je, basi mnamfanya yeye na kizazi chake walinzi pasi Nami”, na Malaika hawana kizazi. Kadhalika, Allaah Ameeleza kwamba Amemuumba Ibliys kutokana na moto wenye mwako mkali huku Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akitueleza kwamba Malaika wameumbwa kutokana na nuru aliposema:
"خُلِقَتِ المَلائِكةُ من نُور"
“Malaika wameumbwa kutokana na nuru”.
Na nuru bila shaka si moto, hivyo ni dhahiri kabisa kwamba majini si Malaika. Aidha, Malaika wote ni viumbe wema waliokirimiwa na Allaah kama inavyoeleza Qur-aan, wakati ambapo katika majini na wanadamu kuna waliolaumiwa na kuna waliosifiwa.
Links
[1] https://www.alhidaaya.com/sw/taxonomy/term/246
[2] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11890&title=Majini
[3] http://www.alhidaaya.com/
[4] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11891&title=01-Majini%3A%20Majini%20Ni%20Akina%20Nani
[5] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11892&title=02-Majini%3A%20Dalili%20Za%20Uwepo%20Wa%20Majini%20Toka%20Kwenye%20Qur-aan
[6] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11893&title=03-Majini%3A%20Dalili%20Za%20Uwepo%20Wa%20Majini%20Toka%20Kwenye%20Hadiyth
[7] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11894&title=04-Majini%3A%20Dalili%20Za%20Kiakili%20Za%20Uwepo%20Wa%20Majini
[8] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11895&title=05-Majini%3A%20Mada%20Waliyoumbiwa%20Kwayo%20Majini
[9] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11896&title=06-Majini%3A%20Majini%20Wanaoana%20Na%20Wanazaana
[10] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11897&title=07-Majini%3A%20Majini%20Wanakula%20Na%20Wanakunywa
[11] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11898&title=08-Majini%3A%20Majini%20Wanakufa%20Na%20Watafufuliwa%20Baada%20Ya%20Kufa
[12] https://dorar.net/aqeeda/1274
[13] https://dorar.net/aqeeda/1232
[14] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11899&title=09-Majini%3A%20Majini%20Wana%20Uwezo%20Wa%20Kujibadilisha%20Maumbo%20Tofauti
[15] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11900&title=10-Majini%3A%20Uwezo%20Wa%20Baadhi%20Ya%20Wanyama%20Kuwaona%20Majini
[16] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11901&title=11-Majini%3A%20Wana%20Spidi%20Ya%20Juu%20Na%20Uwezo%20Wa%20Kufanya%20Kazi%20Ngumu
[17] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11902&title=12-Majini%3A%20Mahala%20Wanakoishi%20Majini
[18] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11903&title=13-Majini%3A%20Aina%20Za%20Majini%20Kutokana%20Na%20Maumbo%20Yao
[19] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11904&title=14-Majini%3A%20Sampuli%20Za%20Majini%20Kwa%20Upande%20Wa%20Imani%20Zao%20Na%20Ukafiri%20Wao%20Na%20Wema%20Wao%20Na%20Ufisadi%20Wao
[20] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11905&title=15-Majini%3A%20Majina%20Ya%20Majini
[21] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11906&title=16-Majini%3A%20Nasaba%20Zao%20Na%20Nchi%20Zao
[22] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11907&title=17-Majini%3A%20Ibliys
[23] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11908&title=18-Majini%3A%20Shaytwaan
[24] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11909&title=19-Majini%3A%20Sifa%20Za%20Shaytwaan
[25] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11910&title=20-Majini%3A%20Je%2C%20Ibliys%20Ni%20Katika%20Majini%20Au%20Malaika%3F