Hairuhusiwi Kumpa Zakaatul-Fitwr Mtu Ambaye Umewajibika Kumuhudumia
SWALI
Mimi mwanamke nnayeishi nchi za nje. Nimeolewa nikiwa na watoto saba. Kila mwaka nampelekea mama yangu Zakaatul-Fitwr ambaye anaishi mbali namimi, nami ndiye nnayemhudumia kwa mahitajio yake (mwenye mas-uliya naye). Je, naruhusiwa kumpa Zakaah au haifai?
JIBU:
AlhamduliLlaah,
‘Ulamaa wamekubaliana bila ya kukhitilafiana kwamba hairuhusiwi kutuma Zakaah ya fardhi ambayo inajumuuisha Zakaatul-Fitwr kwa mtu ambaye inampasa kumhudumia (kuwa na mas-uliya nao) kama wazazi na watoto.
Inasema katika al-Mudawaanah (1/344):
Je, Vipi kuhusu Zakaah ya mali, kutokana na rai ya Maalik nimpe nani?
Akajibu:
"Usimpe yeyote katika jamaa zako ambaye unapaswa kumhudumia" [mwisho wa kunukuu]
Ash-Shaafi'iy kasema katika Al-Umm (2/87)
"Asimpe (Zakaah ya mali) baba yake, mama, babu au bibi" [mwisho wa kunukuu]
Ibn Qudaamah kasema katika Al-Mughniy (2/509):
“Zakaah yoyote ya fardhi isitolewe kwa wazazi hata mstari (wa ukoo) ukifikia vipi (yaani mababu na mabibi) au watoto hata mstari (wa ukoo) ukifikia vipi (yaani wajukuu).”
Ibn Mundhir kasema:
"’Ulamaa wamekubaliana bila ya kukhitilafiana kwamba hairuhusiwi kuwapa Zakaah wazazi ikiwa hali ya mtoaji ni mwenye kuwahudumia kwa sababu kuwapa Zakaah kutamaanisha kuwa hawahitaji tena awahudumie na manufaa yake yatamrudia yeye. Hivyo ni kama kujipa mwenyewe (hiyo Zakaah) nayo hairuhusiwi. Hali hiyo kadhalika ingelikuwa kama kujilipia deni lake mwenye" [mwisho wa kunukuu]
Imaam Ibn 'Uthaymiyn (Rahimahu Allaah) aliulizwa kuhusu hukmu ya kumpa Zakaatul-Fitwr jamaa ambaye ni masikini:
Akajibu:
"Inaruhusiwa kumpa Zakaatul-Fitwr na Zakaah ya mali ya mtu kwa jamaa ambao ni maskini. Bali kuwapa jamaa ni bora kuliko kuwapa watu wageni kwa sababu kuwapa jamaa ni sadaka na pia kuunga ukoo. Lakini sharti kwamba kuwapa sio kwa kuhifadhi mali yake mtu, yaani ikiwa huyo jamaa masikini ni ambaye anapasa kumhudumia. Katika hali hii, hairuhisiwi kumtimizia haja zake kwa kumpa Zakaah kwa sababu akifanya hivyo atakuwa amehifadhi pesa zake mwenyewe kwa kumpa yeye Zakaah na hivyo hairuhusiwi. Lakini ikiwa hana mas-uliya naye ya kumhudumia basi anaweza kumpa Zakaah yake, na kumpa Zakaah yake ni bora kuliko kumpa mtu mgeni kwa sababu Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Sadaka yenu kwa jamaa ni sadaka na pia kuunga ukoo)) [mwisho wa kunukuu]
Kwa hiyo, hairuhusiwi kwako kuitoa Zakaatul-Fitwr yako kumpa mama yako, bali umhudumie kutokana na mali yako nyingine isiyokuwa ya Zakaah. Na tunamuomba Allaah Akuruzuku rizki kwa wingi"
Na Allaah Anajua zaidi
Zakaatu-Fitwr Apewe Nani?
Al-Lajnah Ad-Daaimah
SWALI
Zakaatul-Fitwr apewe nani? Je, inaruhusiwa kuituma mfano kwa Mujaahidiyn waliko vitani? Au kuitoa katika vyama vinavyokusanya sadaka au kujengea msikiti?
JIBU:
AlhamduliLLaah
Zakaatul-Fitwr inapaswa kupewa maskini Waislamu katika nchi au mji ambao inatolewa kwa sababu ya usimulizi wa Abuu Daawuwd kutoka kwa Ibn 'Abbaas (Radhwiya Allaahu 'anhumaa) ambaye amesema: "Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ameamrisha Zakaatul-Fitwr ilipwe Ramadhwaan kuwalisha watu masikini…."
Inaruhusiwa kuituma kwa masikini wa nchi nyingine ambao watu wake wanahitaji zaidi. Hairuhusiwi kujengea msikiti au kuitoa katika miradi ya sadaka.
[Fataawaa Al-Lajnah Ad-Daaimah]
Mtoto Wa Kiume Ana Uwezo Mzuri Wa Kifedha Lakini Baba
Anashikilia Kumtolea Zakaatul-Fitwr
SWALI:
Baadhi ya baba wanashikilia kuwatolea Zakaatul-Fitwr watoto wao wakiume ambao wana uwezo mzuri wa kifedha. Afanyeje mtoto?
JIBU:
AlhamduliLLaah,
Madamu mtoto anao uwezo, inampasa atoe mwenyewe Zakaatul-Fitwr. Ikiwa baba atamlipia Zakaatul-Fitwr hakuna ubaya khaswa ikiwa ni mazoea ya baba kuwatolea watoto wake Zakaatul-Fitwr kila mwaka japokuwa wameshakuwa wakubwa na wafanyakazi. Huenda akapenda kuendelea kufanya hivyo alivyozoea kabla na huenda ikamkasirisha baba ikiwa mwanawe atamwambia: "Usinilipie Zakaah". Hivyo mtoto ampe fursa baba yake kumlipia Zakaatul-Fitwr na pia mwenyewe ajitolee. Baadhi ya watu wanachukulia kwamba kuendelea kuwatolea watoto wao Zakaah ni kuendeleza kuambatana na watoto wake na dalili ya kwamba wao bado wako chini ya hifadhi na mas-uliya yake. Hivyo mtoto ampe baba yake fursa afanye kinachomfurahisha.
Na Allaah Anajua zaidi
Zakaatul-Fitwr Ni Chakula, Si Pesa Na Itolewe Kwa Waislamu Wanaohitaji Pekee
SWALI:
Kitu gani unatoa kwa ajili ya Zakaatul-Fitwr? Ni pesa au chakula. Vipi ikiwa humjui mtu wa kumpa? Je, inaruhusiwa kuitoa katika miskitii au kwa kafiri asiye na mahali pa kuishi au kafiri kwa ujumla?
JIBU:
AlhamduliLLaah
Ibn 'Umar (Radhwiya Allaahu 'anhumaa) amesema: "Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) aliifanya kutoa swaa' (pishi) ya tende au swaa' ya shayiri kuwa ni Zakaatul-Fitwr iliyowajibika kwa Waislamu wote, mtumwa aliye huru, mwanamke na mwanamume, kijana na mzee, na akaamrisha kwamba itolewe kabla ya watu kwenda kuswali (Swalaatul-'Iyd). [Al-Bukhaariy]
Abuu Sa'iydil-Khudriyy (Radhwiya Allaahu 'anhu) amesema: "Tulikuwa tukilipa Zakaatul-Fitwr swaa' (pishi) moja ya chakula, au swaa' ya shayiri (ambacho ndicho kilichokuwa chakula chao zama hizo) au swaa' ya tende au swaa' ya aqitw (mtindi mkavu) au swaa' ya zabibu" [Al-Bukhaariy]
Kwa dalili hizo, ni dhahiri kwamba Zakaatul-Fitwr lazima iwe ni chakula, si pesa. Hivyo lazima tutekeleze ilivyoamrishwa katika Sunnah. Hivyo lipa swaa' moja ya chakula chochote kinachotumika na watu katika nchi yako mfano mchele au ngano kwa ajili yako na kila mtu katika nyumba yako. (swaa' (pishi) ni sawa na taqriban Kilo 2 1⁄2 au 3).
Na Allaah Anajua zaidi
Kuwakilisha Katika Kulipa Zakaatul-Fitwr
SWALI:
Baadhi ya miskiti wanaashiria kupokea kiwango cha Zakaatul-Fitwr kutoka kwa watu ili wagawe kwa wanaohitaji kwa ajili yao. Hugawa chakula kama mchele, unga n.k. Je, desturi hii ni sawa?
JIBU:
AlhamduliLLaah
Kwa vile imekusudiwa kununua na kugawa bidhaa kwa wanaohitaji (hizo bidhaa) kwa ajili yao, hivya ni sawa na watapa thawabu In Shaa Allaah.
Na Allaah Anajua zaidi
Wapi Itolewe Zakaatul-Fitwr?
SWALI:
Mimi ni kijana ninayeishi Zanzibar, lakini nimepeleka mtoto wangu wa kike Uingereza kwa ajili ya matibabu na nimefunga Ramadhaan Uingereza. Inanipasa nilipe Zakaatul-Fitwr Uingereza au niwakilishe familia yangu Zanzibar kunilipia? Nini hukmu ya kulipa Zakaatul-Fitwr kwa pesa? Tafadhali tanbihi kwamba Uingereza watu hutoa pesa badala ya chakula.
JIBU:
AlhamduliLLaah
‘Ulaamaa wamesema kwamba Zakaatul-Fitwr inaambatana na idadi ya watu, sio pesa hivyo ilipwe mahali ambapo mtu atakuweko usiku kabla ya 'Iyd.
Ibn Qudaamah amenukuu katika Al-Mughniy [4/134]
"Ama Zakaatul-Fitwr ilipwe katika nchi ambayo yule apasaye kulipa yuko, ikiwa ni mali yake iko hapo au haipo hapo" [mwisho wa kunukuu]
Ama kuhusu kulipa Zakaatul-Fitwr kwa pesa, imeelezewa katika Fatwa ya 'Kiwango Cha Zakatul-Fitwr' kwamba lazima ilipwe katika mfumo wa chakula na kwamba kulipa pesa haikubaliwi.
Hivyo lazima ujitahidi kulipa kwa mfumo wa chakula. Ikiwa masikini atakaata chakula na akataka pesa, basi hakuna ubaya kumpa pesa katika hali hiyo kwa sababu ya kuhitajika zaidi.
Na Allaah Anajua zaidi
Je, Inafaa Kutoa Zakaatul-Fitwr Kwa Familia Ya Mkewe Ambao Wanahitaji?
SWALI:
Inafaa kutoa Zakaatul-Fitwr kwa familia ya mke wangu ambao wanahitaji?
JIBU:
AlhamduliLLaah,
Zakaatul-Fitwr itolewe kwa masikini na wanaohitaji kwa sababu Ibn 'Abbaas (Radhwiya Allaahu 'anhumaa) amesema: "Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alifaradhisha Zakaatul-Fitwr kuwapa masikini iwe kama ni kutakasa Swawm ya mfungaji kutokana na maneno ya upuuzi na machafu" [Imesumiliwa na Abuu Daawuwd [1609] na ikapewa daraja ya Hasan na An-Nawawiy katika al-Majmuu' [6/126] na Imaam Al-Albaaniy katika Swahiyh Abi Daawuwd]
Ikiwa familia ya mke wako ni masikini na wenye kuhitaji, hakuna ubaya kuwapa Zakaatul-Fitwr, bali ni bora zaidi kuliko kuwapa wengine kwa sababu familia ya mke wako (wakwe, mashemeji, mawifi) wana haki kuwahudumia kama ni sehemu ya kumheshimu mke na kumtendea wema na upole.
Imaam Ibn 'Uthaymiyn (Rahimahu Allaah) amesema katika An-Nuwr 'alaa ad-Darb [682]:
"Hakuna shaka kwamba wakwe, mashemeji na mawifi wana haki ambazo ni zaidi ya mtu mwengine yeyote" [mwisho wa kunukuu]
Na Allaah Anajua zaidi
Zakaatul-Fitwr Igaiwe Kwa Mtu Mmoja Au Watu Mbali Mbali?
Al-Lajnah Ad-Daaimah
SWALI:
Je, Zakaatul-Fitwr ni kwa ajili ya mtu mmoja pekee au igaiwe kwa wengi?
JIBU:
AlhamduliLLaah
Inaruhusiwa kutoa Zakaatul-Fitwr kwa mtu mmoja kwa ajili ya mtu mmoja na inaruhusiwa pia kuigawa kwa watu zaidi ya mmoja.
Na Allaah ni Mweza wa yote.
[Fataawaa Al-Lajnah (1204)]
Je, Kuna Du'aa Ya Kusomwa Inapotolewa Zakaatul-Fitwr?
Al-Lajnah Ad-Daaimah
SWALI:
Je, kuna du'aa mahsusi iombwe wakati wa kutoa Zakaatul-Fitwr na ni du'aa gani?
JIBU:
AlhamduliLLaah
Hatujui du'aa yoyote mahsusi ipasayo kuombwa wakati wa kutoa (Zakaatul-Fitwr).
[Fataawaa Al-Lajnah Ad-Daaimah (1204)]
Zakaatul-Fitwr Ni Fardhi Kwa Masikini Pamoja Na Familia Yake?
Al-Lajnah Ad-Daaimah
SWALI:
Mtu masikini mwenye majukumu ya familia yake ambayo ni miongoni mwa mama, baba na watoto. 'Iydul-Fitwr inawadia naye ana swaa’ (pishi moja) tu ya chakula. Amlipie nani?
JIBU:
AlhamduliLLaah
Ikiwa hali ya masikini huyu ni kama ilivyoelezewa katika Swali, hivyo alipe swaa’ (pishi – kilo 1 ½ - 3) ya chakula kwa ajili yake kwani ni ziada ya mahitajio yake na mahitajio ya wale ambao ni wajibu wake kuwahudumia mchana na usiku wa 'Iyd, kwa sababu Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kasema: ((Anza kwa nafsi yako kisha kwa wanaokutegemea)) [Al-Bukhaariy 2/117, 6/190, Muslim 2.717, 718, 721, 1034, 1036, 1042]
Kuhusu wanaomtegemea ikiwa hawana chochote cha kujitolea katika Zakaah kwa nafsi zao wenyewe, basi hawakuwajibika kulipa kwa sababu Allaah Anasema:
((Allaah Haikalifishi nafsi yoyote ila kwa kadiri ya iwezavyo)) [2: 286]
Na Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Hakuna sadaka isipokuwa kwa yule mwenye uwezo)) [Al-Bukhaariy 2/117, 6/190, Muslim 2/717 Namba 1034. Naye (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Ninapokuamrisheni kufanya jambo, basi fanyeni kadiri muwezavyo))
Wa biLLaahi at-tawfiyq wa Swalla Allaahu ‘alaa Nabiyyina Muhammad wa aalihi wa Swahbihi wa sallam.
[Fataawaa Al-Lajnah Ad-Daaimah]
Hukmu Ya Asiyelipa Zakaatul-Fitwr Japokuwa Ana Uwezo
Al-Lajnah Ad-Daaimah
SWALI:
Nini hukmu ya mwenye uwezo wa kutoa Zakaatul-Fitwr lakini hatoi?
JIBU:
AlhamduliLLaah,
Asiyetoa Zakaatul-Fitwr lazima afanye Tawbah kwa Allaah na aombe maghfirah kwa sababu anapata dhambi kuizuia. Itambidi pia ailipe kwa wanaostahiki kuipokea, lakini ikiwa baada ya Swalaah ya 'Iyd itahesabika kama ni sadaka ya kawaida.
Wa biLLaahi at-tawfiyq wa Swalla Allaahu ‘alaa Nabiyyina Muhammad wa aalihi wa Swahbihi wa sallam.
[Fataawaa Al-Lajnah Ad-Daaimah]
Kutoa Kiwango Cha Zakaatul-Fitwr Katika Vyama Vya Misaada Mwanzo Wa Ramadhwaan
SWALI:
Vyama vya misaada vinaruhusiwa kupokea Zakaatul-Fitwr mwanzo wa Ramadhwaan ili waweze kuigawa kwa mpangilio mzuri kabisa?
JIBU:
Sifa Zote Ni Za Allaah
Ikiwa hakuna watu masikini katika eneo au wale watakaopokea hawaihitajii hasa, na hawatoila bali wataiuza kwa nusu ya thamani yake, na ikiwa ni tabu kupata maskini na wanaohitaji watakaoila, hivyo inaruhusiwa kuituma nje ya nchi. Inaruhusiwa kutoa thamani (ya Zakaatul-Fitwr) mwanzo wa mwezi kwa dalali ambaye atainunua (Zakaatul-Fitwr) na kuituma kwa watu wanaostahiki wakati huo unapotakiwa kulipwa, ambao ni usiku kabla ya 'Iyd au siku mbili kabla yake.
Na Allaah Anajua zaidi
[Al-Fataawa Al-Jibriyn fil A'maal Ad-Da'wiyyah li Fadhwiylat Ash-Shaykh 'Abdillaah bin Jibriyn Uk. 33]
Hukmu Ya Zakaatul-Fitwr, Na Ni Kiasi Gani Ilipwe?
Al-Lajnah Ad-Daaimah
SWALI:
Ikiwa Muislamu anayefunga ni muhitaji asiye miliki Niswaab (Kiwango chenye kuhitajika kutolewa Zakaah) ya Zakaah, je anawajibika kulipa Zakaatul-Fitwr kwa sababu ya usahihi wa Hadiyth hiyo au shariy’ah iliyo sahihi nyingine iliyothibitika katika Sunnah?
JIBU:
AlhamduliLLaah
Swadaqah ya Al-Fitwr (Zakaatul-Fitwr) ni wajibu kwa Muislamu mwenye uwezo wa kujitegemea mwenyewe ikiwa anayo swaa’ (pishi) moja au zaidi ya mahitajio yake ya chakula chake na familia yake mchana na usiku ya 'Iyd.
Hii ni kutokana na usimulizi uliosimuliwa na Ibn 'Umar (Radhwiya Allaahu 'anhumaa) amesema: "Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) aliwajibisha kutoa swaa’ (pishi) ya tende au swaa’ ya shayiri (ngano) kuwa ni Zakaatul-Fitwr iliyowajibika kwa Waislamu wote, mtumwa aliye huru, mwanamke na mwanamume, kijana na mzee, na akaamrisha kwamba itolewe kabla ya watu kwenda kuswali (Swalaatul-'Iyd) [Al-Bukhaariy 1503]
Abuu Sa'iydAl-Khudriyy (Radhwiya Allaahu 'anhu) amesema: "Tulikuwa tukilipa Zakaatul-Fitwr swaa’ (pishi) moja ya chakula, au swaa’ ya shayiri (ambacho ndicho kilichokuwa chakula chao zama hizo) au swaa’ ya tende au swaa’ ya zabibu au swaa’ ya aqit" (mtindi mkavu) [Al-Bukhaariy Na Muslim]
Inakubalika kutoa swaa’ ya chakula wanachotumia sana watu wa mji kama mchele n.k. Lililomaanishwa kwa swaa’ hapa ni swaa’ ya Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ambayo ni mara nne ya kipimo kitakachojaza vitanga viwili vya mikono vya mtu wa umbo la kawaida. (takriban ni kilo 2½ mpaka 3). Ikiwa mtu hatolipa Zakaatul-Fitwr atakuwa anafanya dhambi hivyo itabidi ailipe.
Na Allaah ni Mweza wa yote.
[Fataawaa Al-Lajnah Ad-Daaimah]
Zakaatul-Fitwr Kwa Aliyefariki Kabla Au Baada Ya Magharibi Siku Ya Mwisho Ramadhwaan
Al-Lajnah Ad-Daaimah
SWALI:
Nini hukmu ya mtu aliyefariki kabla ya Magharibi na mwengine baada ya Magharibi siku ya mwisho ya Ramadhwaan?
JIBU:
Zakaatul-Fitwr si waajib kwa yeyote aliyefariki kabla ya Magharibi siku inayofuatia ‘Iydul-Fitwr kwa sababu inawajibika baada ya Magharibi tu ya usiku wa mwisho wa Ramadhwan na aliyetajwa wa kwanza katika swali amefariki kabla ya Magharibi. Ama aliyefariki baada ya Magharibi imewajibika kwake Zakaatul Fitwr kwa sababu amefariki baada ya wakati uliowekewa shariy’ah Zakaatul-Fitwr kuwajibika.
Wa biLLaahi At-Tawfiyq wa Swalla Allaahu ‘alaa Nabiyyina Muhammad wa aalihi wa Swahbihi wa sallam.
[Fataawaa Al-Lajnah Ad-Daaimah (20514)]
Zakaatul-Fitwr Kwa Ajili Ya Mtoto Aliye Tumboni
Al-Lajnah Ad-Daaimah
SWALI:
Zakaatul-Fitwr ilipwe kwa ajili ya mtoto aliye bado tumboni mwa mama?
JIBU:
Inapendekezeka kulipa kwa sababu 'Uthmaan (Radhiya Allaahu 'anhu) alifanya. Lakini sio fardhi bali ni jambo linalopendezeka tu.
Wa biLLaahi At-Tawfiyq wa Swalla Allaahu ‘alaa Nabiyyina Muhammad wa aalihi wa Swahbihi wa sallam.
[Fataawaa Al-Lajnah Ad-Daaimah]
Inafaa Mtoto Wa Kike Kumlipa Baba Yake Zakaatul-Fitwr?
Imaam Ibn ‘Uthaymiyn (Rahimahu Allaah)
SWALI:
Mtoto wa kike anaweza kumlipia baba yake Zakaatul-Fitwr?
JIBU:
Imaam Ibn 'Uthaymiyn (Rahimahu- Allaah) amesema:
Yeyote anayelipa Zakaatul-Fitwr kwa mtu na ambaye hakuwajibika kumlipia lazima achukue ruhusa yake. Hivyo ikiwa Zayd anamlipia 'Amr bila ya ruhusa yake, itakuwa ni batili, kwa sababu Zayd hakuwajibika kumlipia 'Amr Zakaatul-Fitwr.
Ni muhimu kwamba niyyah sahihi itiwe ikiwa kwa ajili ya kujitolea mtu binafsi au kumlipia mtu mwignine. Hii ni kutokana na hukmu inayojulikana sana kwa Fuqahaa ambao wameiita 'taswarruf al-fudhwuwl' ikimaanishwa suala wakati mtu anamfanyia mwenziwe kitendo bila ya ruhusa yake, je huwa kitendo kinasihi kikamilifu au inategemea ruhusa na ridhaa ya mtu mwengine?
Kuna ikhtilaaf baina ya ‘Ulamaa katika mas-ala haya. Na rai iliyo sahihi kabisa ni kwamba inasihi ikiwa mtu mwengine ametoa ruhusa. Na Shaykh amenukuu Hadiyth ya Abu Hurayrah alipozungumza na Shaytwaan alipokuwa akiilinda Zakaah.
Hii inathibitisha suala kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amekubali kitendo cha Shaytwaan alichomfanyia Abuu Hurayarah na akakichukulia kuwa kimesihi japokuwa iliyochukuliwa ilikuwa ni kutoka katika Zakaah na Abu Hurayrah alipewa majukumu ya kuilinda na sio mtu mwengine.
[Ash-Sharh Al-Mumti' 6/165]
Na Allaah Anajua zaidi
Kugawa Zakaatul-Fitwr Kwa Wanaoomba Njiani Japokuwa Hawastahiki
Al-Lajnah Ad-Daaimah
SWALI:
Watu wanaomba Zakaatul-Fitwr njiani na hatujui kama ni wenye dini au watu waovu. Wengineo hali zao ni za kuridhisha, chochote wapatacho kutokana na Zakaatul-Fitwr huwatumilia kwa watoto wao. Wengine wanapokea mishahara lakini ni dhaifu katika msimamo wa dini. Je inaruhusiwa kuwapa Zakaatul-Fitwr au haifai?
JIBU
Zakaatul-Fitwr itolewe kwa Waislamu masikini japokuwa ni wenye kutenda madhambi madamu tu madhambi yao hayawatoi nje ya Uislamu. Iliyomaanishwa kuhusu masikini ni wale wanaoonekana kuwa ni masikini, hata kama ukweli ni matajri. Anayetoa Zakaatul-Fitwr atafute watu masikini wanaostahiki kwa kadiri awezavyo. Akijua baadaye kwamba aliyepokea ni tajiri, haitoathiri kwa aliyetoa bali amefanya wajibu wake.
Wa biLLaahi At-Tawfiyq wa Swalla Allaahu ‘alaa Nabiyyina Muhammad wa aalihi wa Swahbihi wa sallam.
[Fataawaa Al-Lajnah Ad-Daaimah]
Kuichelewesha Zakaatul-Fitwr
Al-Lajnah Ad-Daaimah
SWALI:
Nilikuwa katika safari na nikasahau kutoa Zakaatul-Fitwr. Nikuwa nasafiri usiku wa 27 Ramadhwaan na hatukutoa Zakaatul-Fitwr hadi leo.
JIBU:
Ikiwa mtu amechelewesha Zakaatul-Fitwr japokuwa alikumbukua kuitoa, basi atakuwa ni mtenda dhambi na itampasa atubie kwa Allaah na kuilipa kwa sababu ni kitendo cha ibada ambacho kinabakia kuwajibika japokuwa muda wa kutoa umepita kama mfano wa Swalaah. Lakini kama muulizaji huyu alivyotaja kuwa alisahau kuilipa kwa wakati wake, hivyo hakuna dhambi juu yake lakini lazima ailipe.
Kusema kuwa hakuna dhambi juu yake ni maana kwa ujumla kutokana na dalili inayoonyesha kuwa hakuna dhambi kwa mtu anayesahau lakini bado atakuwa amewajibika kuilipa kutokana na sababu zilizotolewa juu.
Wa biLLaahi At-Tawfiyq wa Swalla Allaahu ‘alaa Nabiyyina Muhammad wa aalihi wa Swahbihi wa sallam.
[Fataawaa Al-Lajnah Ad-Daaimah (2867)]
Kuongeza Kitu Ziada Katika Zakaatul-Fitwr
Al-Lajnah Ad-Daaimah
SWALI:
Je, Zakaatul-Fitwr imewekewa mipaka ya swaa’aa moja kwa kila mtu mmoja katika familia yangu bila ya kuongeza kitu zaidi? Nnachomaanisha ni kwamba kuiongezea sadaka ili nibakie katika usalama wa shaka kwamba saa' yangu imetosheleza. Kufanya hivyo bila ya kumwambia maskini nnayempa kwamba hiyo ziada ni sadaka. Mfano nnao watu kumi katika familia lakini nikanunua gunia la mchele ambalo lina kilo khamsiyn kisha nikalitoa lote kama ni Zakaatul-Fitwr kwa ajili ya watu kumi bila ya kuhesabu swaa’aa kwa kila mmoja kwa sababu najua kuwa huo mchele una zaidi ya kilo ishirini ziada nikizitilia nia kuwa ni sadaka na bila ya kuwaambia kuwa hiyo ziada ni sadaka bali niseme: "Pokeeni Zakaatul-Fitwr yetu" hivyo hatojua mtu kama gunia hilo lina zaidi ya kiwango cha Zakaah, hivyo achukue na afurahie. Nini hukmu yake?
JIBU:
Zakaatul-Fitwr ni swaa’aa moja ya ngano au tende, au mchele n.k. ambayo ni chakula kinachotumika na watu katika mji. Nayo ni kwa ajili ya mtu mmoja mwanamume au mwanamke, mkubwa au mdogo.
Hakuna ubaya kuzidisha Zakaatul-Fitwr kama ulivyofanya kwa nia ya kutoa ziaida kama ni sadaka japokuwa hutowaambia.
Wa biLLaahi At-Tawfiyq wa Swalla Allaahu ‘alaa Nabiyyina Muhammad wa aalihi wa Swahbihi wa sallam.
[Fataawaa Al-Lajnah Ad-Daaimah (9386)]
Kamlipia Zakaatul-Fitwr Mtoto Aliye Tumboni Akaja Kujua Kwamba Ni Mapacha
Al-Lajnah Ad-Daaimah
SWALI:
Mke wangu alikuwa mja mzito mwezi wa Ramadhwaan, nikalipa Zakaatul-Fitwr kwa ajili ya mtoto aliye tumboni. Alipokuja kujifungua siku chache baada ya 'Iyd kumbe walikuwa ni mapacha kwa uwezo wa Allaah. Je, napaswa kufanya nini sasa na hali nilitoa Zakaatul-Fitwr kwa ajili ya mtoto mmoja aliye tumboni na sio wa pili?
JIBU:
Huna haja ya kufanya lolote kwa kutokumlipia mtoto wa pili Zakaatul-Fitwr.
Wa biLLaahi At-Tawfiyq wa Swalla Allaahu ‘alaa Nabiyyina Muhammad wa aalihi wa Swahbihi wa sallam.
[Fataawaa Al-Lajnah Ad-Daaimah (9/366)]
Kuwalipia Zakaatul-Fitwr Wafanyakazi
Al-Lajnah Ad-Daaimah
SWALI:
Tuna kiwanda na shamba ambamo kuna wafanyakazi wanaolipwa mishahara. Je tuwalipe Zakaatul-Fitwr au wajilipe wenyewe?
JIBU:
Wafanyakazi ambao wanalipwa mishahara kwa kibarua chao katika kiwanda au shamba wanapaswa kujilipia wenyewe Zakaatul-Fitwr kwa sababu hukmu ya asili ni kwamba imewajibika kwako. (Hivyo hupasi wewe kuwalipia)
Wa biLLaahi At-Tawfiyq wa Swalla Allaahu ‘alaa Nabiyyina Muhammad wa aalihi wa Swahbihi wa sallam.
[Fataawaa Al-Lajnah Ad-Daaimah (9/372)]
Mume Na Mke Wamekhasimiana, Je Amlipie Mkewe Zakaatul-Fitwr?
Al-Lajnah Ad-Daaimah
SWALI:
Mume aliyekhasimiana na mkewe katika ukhasama mkubwa wa hatari amlipie mkewe Zakaatul-Fitwr?
JIBU:
Mwanamume anawajibika kujilipia Zakaatul-Fitwr pamoja na watu wote walio chini ya majukumu yake kuwahudumia akijumlishwa na mke kwa sababu amewajibika kumhudumia. Ikiwa kuna ukhasama mkubwa baina yao, hii inajulikana kama nushuwz (uasi baina ya mke na mume, kukawa na chuki baina yao na uadui) ambayo ina maana kwamba hana tena wajibu wa kumhudumia. Hivyo hawajibiki kumlipia Zakaatul-Fitwr kwa sababu inahusiana na kuwajibika kwake, na ikiwa hakuwajibika naye (kuwa katika hali hiyo ya nushuwz) basi hayuko tena katika kuwajibika kumlipia Zakaatul-Fitwr.
Wa biLLaahi At-Tawfiyq wa Swalla Allaahu ‘alaa Nabiyyina Muhammad wa aalihi wa Swahbihi wa sallam.
[Fataawaa Al-Lajnah Ad-Daaimah (9/367)]
Kuwalipia Watumishi Wa Nyumbani Wasio Waislamu Zakaatul-Fitwr
Al-Lajnah Ad-Daaimah
SWALI:
Watu wengi wana wafanyakazi wa nyumbani wasio Waislamu. Je, walipiwe Zakaatul-Fitwr au inafaa kuwapa chochote katika Zakaatul-Fitwr?
JIBU:
Hawalipiwi Zakaatul-Fitwr na haipasi wao kupewa Zakaatul-Fitwr. Ikiwa mtu atawapa baadhi ya Zakaah, haitoshi (kwa maana atakuwa hakutimiza wajibu wa kuilipia). Lakini anaweza kuwatendea wema na kuwapa chochote ambacho hakitokani na Zakaah inayowajibika (kama Zakaatul-Fitwr au Zakaah ya mali inayotimia mwaka).
Na Allaah Anjua zaidi
Wa biLLaahi At-Tawfiyq wa Swalla Allaahu ‘alaa Nabiyyina Muhammad wa aalihi wa Swahbihi wa sallam.
[Fataawaa Al-Lajnah Ad-Daaimah (9/375)]
Wakati Gani Zakaatul-Fitwr Itolewe? Na Muda Gani Mwisho Kutoa?
Al-Lajnah Ad-Daaimah
SWALI:
Je, wakati za kutoa Zakaatul-Fitwr ni kuanzia Swalah hadi siku inapomalizika? (Siku ya 'Iyd?)
JIBU:
Wakati wa kutoa Zakaatul-Fitwr sio inapoanza Swalaah ya 'Iyd bali inaanza kutoka jua linapozama siku ya mwisho ya Ramadhwaan ambayo ni usiku wa mwanzo wa mwezi wa Shawwaal na unamalizikia na Swalaah ya 'Iyd. Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ameamrisha kwamba itolewe kabla ya Swalaah. Ibn 'Abbaas (Radhwiya Allaahu 'anhuma) amesimulia kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Atakeyeitoa kabla ya Swalaah itakuwa ni Zakaah iliyokubaliwa (Zakaatul-Fitwr) na atakayeitoa baada ya Swalaah itakuwa ni sadaka ya kawaida)) [Abu Daawuwd 2/262-263, Namba 1609, Ibn Maajah 1/585, namba 1827, Ad-Daaraqutwniy 2/138, Al-Haakim 1/409]
Inaruhusiwa kuitoa siku moja au mbili kabla kutokana na dalili kutoka kwa Ibn 'Umar (Radhwiya Allahu anhumaa) ambaye amesema: "Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) aliamrisha Swadaqah ya Fitwr katika Ramadhaan)) na katika usimulizi mwengine walikuwa wakilipa siku moja au siku mbili kabla ya kumalizika Ramadhwaan.
Atakayechelewa kuitoa ukapita muda wake atakuwa amepata dhambi na itabidi afanye tawbah kwa kuchelewesha kuwapa masikini.
Wa biLLaahi At-Tawfiyq wa Swalla Allaahu ‘alaa Nabiyyina Muhammad wa aalihi wa Swahbihi wa sallam.
[Fataawaa Al-Lajnah Ad-Daaimah (2896)]
Markaz Za Kiislamu Kununua Chakula Cha Zakaatul-Fitwr Mapema Ili Kuwuazia Waislamu
Imaam Ibn ‘Uthaymiyn (Rahimahu Allaah)
SWALI:
Markazi za Kiislamu nchi za Magharibi inataka kununua vyakula kama mchele, mapema sana kabla ya 'Iyd tuseme siku kumi kabla. Kisha watatangaza kuwa wako tayari kupokea pesa za Zakaatul-Fitwr kutoka kwa Waislamu ili wazigawe kwa ajili yao. Hii ni kwa sababu haiwezekani kununua kiasi ya chakula wakipokea pesa siku mbli kabla ya 'Iyd. Nini Hukmu Yake?
JIBU:
Hakuna ubaya kwa Markazi kununua chakula mapema kisha kuwauzia wanaotaka kununua Zakaatul-Fitwr kisha kuigawa kabla ya wakati wake.
[Imaam Ibn ‘Uthaymiyn [Fataawaa (71475)]
Hukmu Ya Kukanusha Zakaatul-Fitwr
Imaam Ibn ‘Uthaymiyn (Rahimahu Allaah)
SWALI:
Nini hukmu ya kukanusha Zakaatul-Fitwr na vipi ahukumiwe mwenye kuikanusha?
JIBU:
Kuikanusha hairuhusiwi (haraam) kwa sababu itakuwa ni kupinga aliyoamrisha Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kama ilivyokwishatajwa katika Hadiyth ya 'Ibn 'Umar ambaye amesema: "Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alifaridhisha Zakaatul-Fitw…" Na inajulikana kwamba kuacha kutenda kilichofaridhishwa hairuhusiwi (ni haraam) na (kufanya hivyo) ni dhambi na kuasi (amri)
[Imaam Ibn ‘Uthaymiyn Fataawaa Ramadhwaan – Mjalada 2, Uk. 902, Fatwa Namba 887- Fiqhul-'Ibaadaati libni 'Uthaymiyn – Uk. 213]
Masikini Wanapendekeza Kupewa Pesa Badala Ya Chakula Cha Zakaatul-Fitwr
Imaam Ibn ‘Uthaymiyn (Rahimahu Allaah)
SWALI:
Masikini wengi siku hizi wanasema kuwa wanapendekezea kupokea Zakaatul-Fitwr katika mfumo wa pesa badala ya chakula kwa sababu zina manufaa zaidi kwao. Je, inaruhusiwa kutoa pesa kwa ajili ya Zakaatul-Fitwr?
JIBU:
Tunavyodhani ni kwamba hairuhusiwi kutoka Zakaatul-Fitwr katika mfumo wa pesa kwa hali yoyote bali lazima itolewe kama ni chakula. Ikiwa mtu masikini anataka kuuza chakula na kutumia thamani yake anaweza kufanya hivyo. Lakini yule anayetoa inampasa atoe chakula. Hakuna neno ikiwa ni chakula kilichokuwa kilichojulikana zama za Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa aalihi wa sallam) au ni aina ya chakula kinachotumika sasa. Mchele siku hizi huenda ukawa na manufuaa zaidi kuliko ngano, kwa sababu mchele hauhitaji mashaka ya kusagwa na kufanywa unga n.k. Kusudio ni kumnufaisha masikini.
Imesimuliwa katika Swahiyh al-Bukhaariy kwamba Sa'iyd (Radhwiya Allaahu 'anhu) amesema: "Zama za Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa aalihi wa sallam) tulikuwa tukitoa (kama Zakaatul-Fitwr) swaa’ ya chakula, na chakula chetu zama hizo kilikuwa ni tende, shayiri, zabibu na mtindi mkavu".
Hivyo ikiwa mtu atatoa kwa mfumo wa chakula, basi achague chakula ambacho kina manufaa zaidi kwa masikini. Hii itabadilika kulingana na zama na mahali (nchi unayotolea Zakaatul-Fitwr).
Kuhusu kutoa Zakaatul-Fitwr kwa pesa, nguo, fanicha au vifaa, hii haitoshi na haitimizi ilivyowajibika kwa sababu Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Atakayetenda ‘amali isiyokuwa yetu (katika dini yetu) basi kitarudishwa))"
[Imaam Ibn ‘Uthayiyn Majmuw' Fataawa (18/191)]
Kuwapa Zakaatul-Fitwr Jamaa
Imaam Ibn ‘Uthaymiyn (Rahimahu Allaah)
SWALI:
Nini hukmu ya Zakaatul-Fitwr kupewa jamaa walio masikini?
JIBU:
Inaruhusiwa kutoa Zakaatul-Fitwr na Zakaah ya mali kuwapa jamaa walio masikini. Na hakika kuwapa jamaa ni bora kuliko kuwapa watu wageni kwa sababu kuwapa jamaa huwa ni sadaka na pia kuunga ukoo. Lakini sharti isiwe kwa ajili ya kuhifadhi mali yake ambayo ndivyo itakavyokuwa hali ikiwa jamaa yenyewe aliye maskini ni ambaye mwenye jukumu naye kumhudumia. Kwa hali hiyo hairuhusiwi kumtimizia mtu haja kwa chochote katika Zakaah yake kwa sababu akifanya hivyo atakuwa anahifadhi mali yake kutokana na anachokitoa (kwa maana atakuwa anataoa Zakaah yake kwa kumpa mtu ambaye ni wajibu wake kumhudumia) Nayo haipasi wala kuruhusiwa.
Lakini ikiwa hana majukumu naye basi anaweza kumpa Zakaah bali kutoa Zakaah yake kwa jamaa ni bora kuliko kumpa mtu mgeni kwa sababu Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Swadaqah zenu kwa jamaa ni swadaqah na pia ni kuunga ukoo))
[Majmuw' Fataawaa Shaykh Ibn 'Uthaymiyn (18/301]
Inaruhusiwa kuhamisha Zakaatul-Fitwr Kutoka Nchi Kwenda Nchi Nyingine?
Je, inaruhusiwa kutoa Zakaah kupeleka nchi nyingine ikiwa hakuna maskini nchi yangu?
JIBU:
Sifa Zote Ni Za Allaah
Imesemwa katika Fataawa al-Lajnah ad-Daaimah 10/9:
"Zakaah itolewe kwa wale ambao Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) Amewataja
((Wa kupewa sadaka ni mafakiri, na masikini, na wanaozitumikia, na wa kutiwa nguvu nyoyo zao, na katika kukomboa watumwa, na wenye madeni, na katika Njia ya Allaah, na wasafiri. Huu ni waajibu ulio faridhiwa na Allaah. Na Allaah ni Mwenye kujua Mwenye hikima)) [At-Tawbah: 60].
Itolewe kwa Waislamu kwa sababu Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amemumbia Mu'aadh bin Jabal alipomtuma
Maskini na wanaohitaji walio na ucha Mungu na wema ndio wanaostahiki zaidi kupewa kuliko wengine.
Hukmu ya asili kuhusu Zakaah ni kwamba itolewe kwa masikini katika nchi ambayo
Na Allaah Anajua zaidi
Kuwatolea Zakaatul-Fitwr Familia Hata Kama Wameshajitolea
Imaam Ibn ‘Uthaymiyn (Rahimahu Allaah)
SWALI:
Anayeishi nchi za ki-Magharibi anaweza kutoa Zakaatul-Fitwr kwa ajili yake na familia yake ikiwa anajua kuwa wameshajitolea wenyewe?"
JIBU:
Zakaatul-Fitwr ambayo ni swaa’ ya chakula kama mchele, ngano, tende au aina yoyote ya chakula, ni kitu ambacho mtu inampasa atoe kwa ajili yake kama kwani ndivyo inavyowajibika kwa sababu Ibn 'Umar (Radhwiya allaahu 'anhuma) amesema: Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amefaridhisha Swadaqatul-Fitwr kwa Waislamu, aliye huru na mtumwa, mwanaume na mwanamke, mdogo na mkubwa, na ameamrisha itolewe kabla ya watu kwenda kuswali".
Ikiwa watu wa nyumba wameshajilipia, basi hakuna haja tena mtu ambaye yuko mbali na familia yake kuwatolea. Bali ajitolee mwenyewe pekee huko anakoishi na ikiwa wako Waislamu ambao wanastahiki kupewa Zakaah hii. Ikiwa hakuna wanaostahiki basi awakilishe familia yake imtolee katika nchi yake ya asili.
[Majmuw' Fataawa Ibn 'Uthaymiyn (18/771)]
Ni Kweli Swawm Inanin'ginia Baina Ya Mbingu na Ardhi Hadi Mtu Atoe Zakaatul-Fitwr?
SWALI:
Je, Hadiyth inayosema kuwa Swawm ya Ramadhaan inaning'inia baina ya mbinu na ardhi na haipandishwi juu hadi ilipwe Zakaatul-Fitwr ni Sahihi?
JIBU:
AlhamduliLLaah - Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aala) Rabb wa walimwengu, Swalaah na salamu zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho
Hadiyth hiyo ni dhaifu.
Katika Al-Jaami' as-Swaghiyr, as-Suyuwtwiy ameihusisha kwa Ibn Shaahiyn katika Targhiyb yake: "Imesimuliwa katika Adhw-Dhwiyaa' kutoka kwa Jariyr bin 'Abdillaah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: Mwezi wa Ramadhaan unaning'inia baina ya mbingu na ardhi na (Swawm) haipelekwi juu kwa Allaah isipokuwa kwa (kutolewa) Zakaatul-Fitwr"
Imechambuliwa kuwa ni dhaifu na as-Suyuwtwiy. Al-Manaawiy ameeleza sababu yake katika Faydhw Al-Qadiyr ambako amesema: "Imesimuliwa na Ibn Al-Jawziy katika Al-Waahiyaat na kasema: Sio Swahiyh, isnaad yake inajumuisha Muhammad bin 'Ubayd al-Baswriy ambaye ni majhuwl (asiyejulikana).
Imechambuliwa pia kuwa ni dhaifu na Imaam al-Albaaniy katika as-Silsilatul-Ahaadiyth ad-Dhwa'iyfah (43). Kasema: "Hata kama ingekuwa ni Hadiyth Swahiyh, basi maana iliyodhihiri ni kukubaliwa kwa Swawm ya Ramadhwaan inategemea baada ya kulipa Zakaatul-Fitwr tu, na ikiwa mtu hakulipa, basi Swawm yake haitokubaliwa. Lakini simjui Mwanachuoni yeyote aliyesema hivyo na Hadiyth sio Swahiyh" [mwisho wa kunukuu]
Kwa vile Hadiyth sio Swahiyh, hakuna atakayeweza kusema kwamba Swawm ya Ramadhwaan inakubalika tu baada ya kutoa Zakaatul-Fitwr kwa saabu hakuna atakayejua hivyo isipokuwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam).
Imethibitika katika Sunan Abi Daawuwd kwamba Ibn 'Abbaas (Radhwiya Allaahu 'anhumaa) amesema: Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amefaridhisha Zakaatul-Fitwr kuwalisha masikini kama ni kutakasa swiyaam za aliyefunga kutokana na maneno ya upuuzi na kauli chafu" [Imepewa daraja ya Hasan na Shaykh al-Albaaniy katika Swahiyh Sunan Abi Daawuwd]
Hadiyth hii inaelezea hikma ya Zakaatul-Fitwr ambayo kufidia kasoro yoyote iliyotokea katika Swawm. Haisemi kuwa Swawm haitokubaliwa ila tu baada ya kutoa Zakaatul-Fitwr.
Na Allaah Anajua zaidi
Kutoa Nyama Kwa Ajili Ya Zakaatul-Fitwr
SWALI:
Je, inaruhusiwa kutoa nyama kwa ajili ya Zakaatul-Fitwr?
JIBU:
Zakaatul-Fitwr lazima itolewe katika mfumo wa chakula kinachotumika na watu kwa sababu ya usimulizi uliosimuliwa na Al-Bukhaariy (151) kutoka kwa Abuu Sa'iyd al-Khudriyy (Radhwiya Allaahu 'anhu) ambaye amesema: "Zama za Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) tulikuwa tukitoa siku ya ('Iyd) al-Fitwr, swaa’ moja ya chakula" Na Abuu Sa'iyd kasema: "Chakula chetu kilikuwa ni shayiri, zabibu, mtindi mkavu na tende."
Ikiwa aina ya chakula cha watu wa mji wako ni nyama basi inaruhusiwa kutoa Zakaatul-Fitwr.
Shaykhul-Islaam (Rahimahu Allaah) katika Al-Majmuwu' Al-Fataawa (25/68): "Ikiwa aina ya chakula cha watu ni mojawapo wa aina hizi, basi hakuna shaka kuwa kinaruhusiwa kutoa aina yao ya chakula.”
Lakini je, wanaweza kutoa chakula kisichokuwa miongoni mwa hivyo? Mfano ikiwa chakula chao ni mchele au mahindi, je, watoe ngano au shayiri au inakubalika kwao kutoa mchele na mahindi?
Ikhtilaaf mashuhuri ya rai kuhusu (Swali) hilo lipo. Rai iliyo sahihi baina ya mbili ni kwamba chakula kinachotumika na watu kitolewe japokuwa sio miongoni mwa aina hizo. Hii ni rai ya wengi wa ‘Ulamaa, kama ash-Shaafi'y na wengineo. Hikma asasi kutoa sadaka ni kusaidia masikini kama Anavyosema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):
((chakula cha wastani mnachowalisha ahali zenu)) [Al-Maaidah 5:89]
Na Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ameamrisha Zakaatul-Fitwr iwe ni swaa’ ya tende au swaa’ ya shayiri, kwa sababu hivyo ndivyo vilivyokuwa vyakula vya watu wa Madiynah. Ingelikuwa chakula chao ni kitu kingine basi asingeliwaamrisha watoe chakula ambacho sio kinachotumika kama Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Alivyokuwa Hakuamrisha katika hali ya kafara" [mwisho wa kunukuu]
Ibnul-Qayyim (Rahimahu Allaah) amesema katika I'laam Al-Muwaqqi'iyn (3/12):
"Hicho ndicho kilichokuwa chakula cha Madiynah. Ama kwa watu wa nchi nyingine, watoe swaa’ ya chakula chao, ikiwa mfano chakula chao ni mahindi au mchele au tiyn au aina yoyote ya nafaka. Ikiwa chakula chao sio aina ya nafaka, kama maziwa, nyama, samaki, basi watoe Zakaatul-Fitwr yao katika mfumo wa chakula kinachotumika chochote kitakachokuwa. Hii ni rai ya ‘Ulamaa wengi wao na ndio rai iliyo sahihi na hakuna rai nyingine itakayoshauriwa. Nia ni kutimiza haja ya masikini siku ya 'Iyd na kuwasaidia kwa kuwapa chakula wanachotumia sana. Kutokana na hivi, inakubaliwa kutoa unga japokuwa haikutajwa katika Hadiyth Swahiyh" [mwisho wa kunukuu]
Imaam Ibn 'Uthaymiyn (Rahimahu Allaah) amesema katika Ash-Sharh Al-Mumti' (6/182):
"Lakini ikiwa chakula kinachotumika na watu sio mbegu (nafaka) au mazao bali ni chakula kama nyama, kama mfano wa watu wanaoishi Ncha Ya Kaskazini (North Pole), ambao chakula chao zaidi ni nyama, basi rai iliyo sahihi kabisa na kukubalika ni kuitoa nyama." [mwisho wa kunukuu]
Zakaatul-Fitwr Imewajibika Kwa Mtu Asiyefunga Ramadhaan Kwa Dharua?
SWALI:
Je, Zakaatul-Fitwr inawajibika kwa mtu aliyekuwa hakufunga Ramadhaan kwa sababu alikuwa katika safari au mgonjwa?
JIBU:
AlhamduliLLaah - Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aala) Rabb wa walimwengu, Swalaah na salamu zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho.
Rai za wengi miongoni mwa ‘Ulamaa pamoja na Maimaam wanne na wengineo ni kwamba Zakaatul-Fitwr inawajibika kwa Muislamu hata kama hakufunga Ramadhwaan. Hakuna mwingine aliyekhitilafiana isipokuwa Sa'iyd bin Muswayyab na Hasan Al-Baswriy ambao wamesema kuwa Zakaatul-Fitwr inawajibika kwa wale waliofunga pekee. Lakini rai iliyo sahihi ni rai ya wengi wao kwa kutokana na dalili zifuatazo:
1-Maana kwa ujumla ya Hadiyth ambayo asili yake ni kuwa Zakaatul-Fitwr ni fardhi.
Imesimuliwa kwamba Ibn 'Umar (Radhwiya Allaahu 'anhuma) amesema: "Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amefaridhisha Zakaatul-Fitwr kwa swaa’ ya tende, au swaa’ ya shayiri (ngano) kwa kila mtu, mtumwa au aliye huru, mwanamume au mwanamke, mdogo au mkubwa na ameamrisha kwamba ilipwe kabla ya watu kwenda kuswali" [Al-Bukhaariy (1503) na Muslim (9840]
Neno la 'mdogo' inajumuisha watoto wadogo ambao hawawezi kufunga.
2- Sadaka na Zakaah zinapoamrishwa kawaida ni kwa ajili ya kuwasaidia watu masikini na wanaohitaji na inakusudiwa kupatikana upeo fulani wa hifadhi ya jamii. Iliyo dhahiri kwa kusudio hili ni Zakaatul-Fitwr ambayo imeamrishwa kwa wadogo na wakubwa, aliye huru na mtumwa, mwanamume na mwanamke na mtoaji sheria hakubainisha thamani ya chini kabisa (Niswaab) au muda wa mwaka kuwa ni fardhi.
Hivyo kwa vile ni fardhi kwa wale ambao hawakufunga Ramadhwaan, ikiwa ni kutokana na sababu au bila ya sababu, inaonyesha sababu ya kuwekwa kwa sheria ya Zakaah.
3- Kuhusu mabishano ya wale walionukuu kama ni dalili ya maneno ya Ibn 'Abbaas (Radhwiya Allaahu 'anhumaa): "Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amefaridhisha Zakaatul-Fitwr kama ni kumtakasa mwenye kufunga kutokana na maneno ya upuuzi na machafu na kuwalisha masikini" [Abuu Daawuwd (1609)]
Wamesema: Maneno 'kama ni kumtwaharisha mtu aliyefunga' ina maana kwamba Zakaatul-Fitwr ni fardhi kwa wale waliofunga. Al-Haafidhw Ibn Hajar amejibu hivyo katika Al-Fat-h (3/369) ambako kasema:
"Jibu langu ni kwamba kutaja ‘kutakaswa’ kunamaanisha hali ya kawaida (kwa watu wengi ilivyo) kama vile inavyohitajika kwa wale ambao hawakutenda dhambi, mfano Wachaji Allaah au ambaye amekuwa Muislamu dakika kabla ya jua kuzama." [mwisho wa kunukuu].
Inayokusudiwa ni kwamba katika hali nyingi Zakaatul-Fitwr imefaridhishwa katika shariy'ah kwa sababu ni twahara ya aliyefunga, lakini kupatikana twahara si sharti inayoifanya kuwa ni fardhi. Mfano kama Zakaah ya mali ambayo pia imefaridhishwa kwa ajili ya kutwaharisha nafsi:
((Chukua swadaqa katika mali zao, uwasafishe na uwatakase kwazo, na uwaombee rahmah. Hakika maombi yako ni utulivu kwao. Na Allaah ni Mwenye kusikia Mjuzi)) [At-Tawbah: 103].
Juu ya kwamba Zakaah ni fardhi katika hali ya mali inayomilikiwa na mtoto mdogo ambaye hahitaji kutwaharisha nafsi, kwa sababu hakuna vitendo vibaya vinavyoandikwa kwa ajili yake.
Na Allaah Anajua zaidi
Inaruhusiwa Kumpa Zakaatul-Fitwr Mama Wakubwa Na Wadogo?
SWALI:
Je, inafaa kutoa Zakaatul-Fitwr kwa mama mkubwa na mama mdogo ambaye ameachwa, hana watoto wa kiume bali ana watoto wa kike ambao wameolewa na anamiliki 500 mita mraba ya ardhi. Hana chanzo cha kipato. Je inaruhusiwa kumpa Zakaah hii au wapewe maskini wengine?
JIBU:
Sifa Zote Ni Za Allaah
Kwanza:
‘Ulamaa wamekhitilafiana kuhusu watu wa kuwapa Zakaatul-Fitwr. Rai ya wengi wao ni kwamba wapewe aina nane ya watu ambao wametajwa kupewa (katika Suwrah At-Tawbah Aayah ya 60). Rai ya wengineo ni kwamba wapewe wote waliomo katika aina nane ya watu na wengineo wameona kwamba itolewe kwa masikini na wenye kuhitaji pekee.
Inasema katika al-Mawsu’ah al-Fiqhiyyah (23/344): “Mafuqahaa wamekhitilafiana kuhusu nani apewe Zakaatul-Fitwr na kuna rai tatu:
1- Rai ya wengi wao ni kwamba inaruhusiwa kuigawa baina ya aina nane ya watu ambao Zakaah ya mali inapasa kuwapa. – Rai ya Maalik.
2- Rai ya Imaam Ahmad ambayo imependekezwa na Ibn Taymiyyah kwamba wapewe masikini na wanaohitaji pekee.
3- Rai ya Shaafi'y igaiwe kwa aina nane ya watu au yeyote aliyekuweko. [mwisho wa kunukuu]
Shaykhul-Islaam Ibn Taymiyyah amekanusha rai ya kwanza na ya tatu katika Majmuw' al-Fataawa (25/73-78). Ameelezea kwamba Zakaatul-Fitwr inategemea idadi ya watu, sio mali. Baadhi ya aliyoyataja ni yafuatayo:
"Hivyo Allaah Ameamrisha itolewe kwa mfumo wa chakula kama Alivyoamrisha kafara iwe pia katika mfumo wa chakula.
Kutokana na rai hii, haipasi kuitoa Zakaatul-Fitwr ila wale wanostahiki kupokea chakula kama ni kafara. Nao ni wale wanaopokea kwa sababu wanakihitaji. Hivyo isitolewe kwa wale wa kutiwa nguvu nyoyo zao, au watumwa n.k. Hii ni rai iliyo na nguvu kabisa, kutokana na dalili.
Rai dhaifu kabisa ni ile wanaosema kwamba ni fardhi kwa kila Muislamu kutoa Zakaatul-Fitwr kwa (watu) kumi na mbili, au kumi na nane, au ishirini na nne, au ishirini na nane, au thelathini na mbili n.k. kwa sababu hii ni kinyume na desturi ya Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Makhalifa Waliongoka na Maswahaba wote.
Hakuna Muislamu aliyefanya hivi zama hizo bali Muislamu alijitolea Zakaatul-Fitwr na Zakaatul-Fitwr ya familia yake kwa Muislam mmoja. Walipomuona mtu anagawana swaa’ baina ya watu wakigawana kitanga cha mkono, walikataza kwa nguvu na ilionekana kama ni bid'ah na kitendo kisichokubaliwa. Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema kwamba kuamrishwa kwa swaa’ ya tende, au swaa’ ya shayiri, au nusu swaa’ au swaa’ ya ngano imepimwa kuwa inamtosheleza maskini mmoja. Pia ameelezea kwamba iwe katika mfumo wa chakula wapewe siku ya 'Iyd ili wawe wenye kujitegemea. Ikiwa mtu maskini atachukua kitanga cha chakula haitamnufaisha na haitamtosheleza. Hali kadhalika ni hali ya mwenye deni na msafiri. Wakichukua kitanga cha mkono cha ngano haitawatosheleza. Uislamu umezingatia kitendo hiki ambacho hakuna mtu mwenye busara angelikubali na ambacho hakuna Salaf au Maimaam wa Ummah walifanya"
Juu ya hivyo, maneno ya Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ((Kama ni chakula cha masikini)) inaonyesha kwamba hii ni haki ya maskini kama Anavyosema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) katika Aayah za Dhwihaar (kafara ya Dhwihaar):
((basi awalishe masikini sitini)) [Al-Mujaadilah: 58:4]
Hivyo ikiwa hairuhusiwi kuitoa kuwapa hao aina nane ya watu basi inahusu hapa pia" [mwisho wa kunukuu]
Kutokana na hii, rai iliyo sahihi kabisa miongoni mwa hizo rai tatu ni ya pili ambayo Zakaatul-Fitwr itolewe kwa masikini na wenye kuhitaji na sio mtu mwingine. Hivyo ndivyo iliyochukuliwa kuwa ni rai iliyo sahihi kabisa na Imaam Ibn 'Uthaymiyn (Rahimahu Allaah) kama inavyosema katika ash-Sharh al-Mumtii' (6/17)
Pili:
Ikiwa Zakaatul-Fitwr na Zakaah ya mali watapewa jamaa ambao wanastahiki, ni bora zaidi kuliko kuwapa wengineo wanaostahiki kwa sababu katika hali hii Zakaah zote mbili zinaunganisha ukoo. Lakini inategemea na hali ya huyo jamaa kama anastahiki kupewa (yaani kama ni maskini na mwenye kuhitaji)
Shaykh Muhammad Swaalih bin 'Uthaymiyn (Rahimahu Allaah) alipoulizwa kuhusu hukmu ya Zakaatul-Fitwr kupewa jamaa walio masikini.
Alijibu:
Inaruhusiwa kutoa Zakaatul-Fitwr na Zakaah ya mali kuwapa jamaa walio masikini. Na hakika kuwapa jamaa ni bora kuliko kuwapa watu wageni kwa sababu kuwapa jamaa huwa ni sadaka na pia kuunga ukoo. Lakini sharti isiwe kwa ajili ya kuhifadhi mali yake ambayo ndivyo itakavyokuwa hali ikiwa jamaa yenyewe aliye maskini ni ambaye mwenye jukumu naye kumhudumia. Kwa hali hiyo hairuhusiwi kumtimizia mtu haja kwa chochote katika Zakaah yake kwa sababu akifanya hivyo atakuwa anahifadhi mali yake kutokana na anachokitoa (kwa maana atakuwa anataoa Zakaah yake kwa kumpa mtu ambaye ni wajibu wake kumhudumia) Nayo haipasi wala kuruhusiwa.
Lakini ikiwa hana majukumu naye basi anaweza kumpa Zakaah bali kutoa Zakaah yake kwa jamaa ni bora kuliko kumpa mtu mgeni kwa sababu Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Swadaqah zenu kwa jamaa ni swadaqah na pia ni kuunga ukoo)) [mwisho wa kunukuu- Majmuu' Fataawa Shaykh Ibn 'Uthaymiyn (18/Swali Namba 301]
Hitimisho:
Ikiwa mama mkubwa na mama mdogo wako ni maskini anastahiki Zakaah, japo kuwa anamiliki mita mraba 500 ya ardhi. Lakini ni bora kwake aiuze ili awe ni mwenye kujitegemea mwenyewe ili asitegemee zawadi kutoka kwa watu.
Waislamu wasiwaache jamaa zao hadi mwezi wa Ramadhwaan unamalizika ndio waanze kuwafikiria na kuwapa swaa’ ya chakula, bali Waislamu wanapaswa daima kuwahudumia maskini na wanaohitaji na kukimbilia kuwapa wanayohitaji ya chakula, pesa na nguo na hivi inapaswa ifanyike zaidi na zaidi ili walio matajiri wawe wanawafikiria na kuwahudumia jamaa zao walio maskini.
Na Allaah Anajua zaidi
Hakuna Masikini Wanakoishi. Je Watume Zakaatul-Fitwr Nchi Nyingine?
SWALI:
Sisi tunaishi Uingereza na hatujui watu masikini wowote hapa. Tumepata mtu wa kuaminika In Shaa Allaah, ambaye amesema: "Nipeni pesa nitanunua mchele nusu yake na kugawa kwa masikini, na nusu yake nitawapa pesa". Sababu yake ni kwamba tuko zaidi ya watu 500 hivyo itakuwa shida kwake kununua kiasi kikubwa cha chakula na kukibeba. Pia kwa vile masikini pengine wasitake chochote ila pesa kwa sababu wataweza kuzitumia vizuri zaidi kuliko kupata mchele. Je tumpe pesa au tuwakilishe ndugu zetu huko Tanzania ili watutolee?
JIBU:
Rai ya ‘Ulamaa wengi (wakijumuuisha Maalik, ash-Shaafi'y na Ahmad) ni kwamba hairuhusiwi kutoa pesa kwa ajili ya Zakaatul-Fitwr, bali lazima itolewe kama chakula kama ilivyoamrishwa na Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) [Al-Bukhaariy (1504) na Muslim (984) iliyosimuliwa na Ibn 'Umar (Radhwiya Allaahu 'anhumaa) kwamba: "Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amefaridhisha Zakaatul-Fitwr swaa’ moja ya tende au swaa’ moja ya shayiri (ngano) kwa kila mtu, aliye huru au mtumwa, mwanamume au mwanamke, miongoni mwa Waislamu"
Kutokana na hivyo, ikiwa mtu huyo ni wa kuaminika basi unaweza kumsisitiza kuwa atoe kwa mfumo wa chakula. Ikiwa hatokubali hivyo basi ni bora utoe chochote uwezavyo kwa maskini wa nchi hiyo unayoishi. Kisha hakuna ubaya kutuma zilizizobakia nchi nyingine. Sio lazima utume nchi yako ya asili, bali nchi yoyote ambayo kunahitaji na umasikini ni mkubwa zaidi au kwa jamaa ambao ni masikini pia itakuwa bora.
Katika Swali la:
Inaruhusiwa kuhamisha Zakaatul-Fitwr Kutoka Nchi Kwenda Nchi Nyingine?
Tumesema kwamba hakuna ubaya kutuma Zakaah nchi nyingine ambayo inahitaji kama kutuma nchi ambayo ina jamaa wenye uhusiano wa damu au nchi ambayo inahitaji zaidi.
Shaykh Ibn 'Uthaymiyn aliulizwa: 'Anayeishi nchi za ki-Magharibi anaweza kutoa Zakaatul-Fitwr kwa ajili yake na familia yake ikiwa anajua kuwa wameshajitolea wenyewe?"
Akajibu:
"Zakaatul-Fitwr ambayo ni swaa’ ya chakula kama mchele, ngano, tende au aina yoyote ya chakula, ni kitu ambacho mtu inampasa atoe kwa ajili yake kama kwani ndivyo inavyowajibika kwa sababu Ibn 'Umar (Radhwiya allaahu 'anhumaa) amesema: "Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amefaridhisha Swadaqatul-Fitwr kwa Waislamu, aliye huru na mtumwa, mwanaume na mwanamke, mdogo na mkubwa, na ameamrisha itolewe kabla ya watu kwenda kuswali".
Ikiwa watu wa nyumba wameshajilipia, basi hakuna haja tena mtu ambaye yuko mbali na familia yake kuwatolea. Bali ajitolee mwenyewe pekee huko anakoishi na ikiwa wako Waislamu ambao wanastahiki kupewa Zakaah hii. Ikiwa hakuna wanaostahiki basi awakilishe familia yake imtolee katika nchi yake ya asili" [Mwisho wa kunukuu - Majmuw' Fataawa Ibn 'Uthaymiyn 18/ Swali Namba 771]
Aliulizwa pia kuhusu: Kutuma Zakaatul-Fitwr nchi za mbali kwa sababu ya kuweko huko maskini wengi?
Alijibu:
"Hakuna ubaya kutuma Zakaatul-Fitwr nchi nyingine kwa sababu ikiwa hakuna maskini nchi ya anayetoa. Lakini ikiwa itafanywa hivyo na hali nchi yake wako masikini basi hairuhusiwi" [mwisho wa kunukuu Fataawa Ibn 'Uthaymiyn 18/ Swali Namba 102]
Inafuatia pia Fatwa ya Al-Lajnah Ad-Daaimah –
Kiwango cha Zakaatul-Fitwr ni swaa’ moja ya tende, shayiri, zabibu, mtindi mkavu au chakula chochote na itolewe usiku kabla ya 'Iyd hadi kabla ya Swalaah ya 'Iyd. Inaruhusiwa pia kuitoa siku mbili au tatu mapema. Itolewe kwa maskini wa nchi ambayo inakotolewa. Lakini inaruhusiwa kuipeleka kwa maskini wa nchi ambayo mahitaji yake ni makubwa. Inaruhusiwa Imaam wa msikiti na watu wanaoaminika kukusanya na kuigawa kwa maskini madamu tu watahakikisha itawafikia kabla ya Swalaah ya 'Iyd. Haiungani na mfumuko (thamani) bali kiasi kimewekwa katika sheria kama ni swaa’ moja. Asiyekuwa na chochote isipokuwa chakula tu cha kula siku ya 'Iyd pamoja na walio chini ya jukumu lake, hawajibiki kutoa Zakaatul-Fitwr. Hairuhusiwi kuitumia kwa kujengea misikiti au miradi yoyote mingine. [Fataawa Al-Lajnah ad-Daaimah 9/369, 370]
Imeshanukuliwa kwamba Zakaatul-Fitwr ni fardhi na kiwango cha kutoa na kwamba hairuhusiwi kutoa kwa pesa, na kwamba inaruhusiwa kuituma katika nchi ambazo mahitaji yake ni makubwa zaidi.
Na Allaah Anajua zaidi
Links
[1] https://www.alhidaaya.com/sw/taxonomy/term/261
[2] http://www.alhidaaya.com/sw/node/8744
[3] http://www.alhidaaya.com/sw/
[4] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F1919&title=Fataawaa%3A%20Za%20Zakaatul-Fitwr
[5] http://www.alhidaaya.com
[6] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F1920&title=01-Fatwa%3A%20Hairuhusiwi%20Kumpa%20Zakaatul-Fitwr%20Mtu%20Ambaye%20Umewajibika%20Kumuhudumia
[7] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F1921&title=02-Al-Lajnah%20Ad-Daaimah%3A%20Zakaatul-Fitwr%20%20Apewe%20Nani%3F
[8] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F1922&title=03-Fatwa%3A%20Mtoto%20Ana%20Uwezo%20Mzuri%20Wa%20Kifedha%20Lakini%20Baba%20Anashikilia%20Kumtolea%20Zakaatul-Fitwr
[9] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F1924&title=04-Fatwa%3A%20Zakaatul-Fitwr%20Ni%20Chakula%2C%20Si%20Pesa%20Na%20Itolewe%20Kwa%20Waislamu%20Wanaohitaji%20Pekee
[10] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F1925&title=05-Fatwa%3A%20Kuwakilisha%20Katika%20Kulipa%20Zakaatul-Fitwr%20%20
[11] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F1926&title=06-Fatwa%3A%20Wapi%20Itolewe%20Zakaatul-Fitwr%3F
[12] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F1927&title=07-Fatwa%3A%20Inafaa%20Kutoa%20Zakaatul-Fitwr%20Kwa%20Familia%20Ya%20Mkewe%20Ambao%20Wanahitaji%3F
[13] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F1928&title=08-Al-Lajnah%20Ad-Daaimah%3A%20Zakaatul-Fitwr%20Igaiwe%20Kwa%20Mtu%20Mmoja%20Au%20Watu%20Mbali%20Mbali%3F
[14] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F1929&title=09-Al-Lajnah%20Ad-Daaimah%3A%20Kuna%20Du%27aa%20Ya%20Kusomwa%20Inapotolewa%20Zakaatul-Fitwr%3F
[15] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F1930&title=10-Al-Lajnah%20Ad-Daaimah%3A%20Zakaatul-Fitwr%20Ni%20Fardhi%20Kwa%20Masikini%20Pamoja%20Na%20Familia%20Yake%3F
[16] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F1931&title=11-Al-Lajnah%20Ad-Daaimah%3A%20Hukmu%20Ya%20Asiyelipa%20Zakaatul-Fitwr%20Japokuwa%20Ana%20Uwezo
[17] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F1933&title=12-Fatwa%3A%20Kutoa%20Kiwango%20Cha%20Zakaatul-Fitwr%20Katika%20Vyama%20Vya%20Misaada%20Mwanzo%20Wa%20Ramadhwaan
[18] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F1934&title=13-Al-Lajnah%20Ad-Daaimah%3A%20Hukmu%20Ya%20Zakaatul-Fitwr%2C%20Na%20Ni%20Kiasi%20Gani%20Ilipwe%3F
[19] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F1935&title=14-Al-Lajnah%20Ad-Daaimah%3A%20Zakaatul-Fitwr%20Kwa%20Aliyefariki%20Kabla%20Au%20Baada%20Ya%20Magharibi%20Siku%20Ya%20Mwisho%20Ramadhwaan
[20] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F1936&title=15-Al-Lajnah%20Ad-Daaimah%3A%20Zakaatul-Fitwr%20Kwa%20Ajili%20Ya%20Mtoto%20Aliye%20Tumboni
[21] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F1937&title=16-Imaam%20Ibn%20%E2%80%98Uthaymiyn%3A%20Inafaa%20Mtoto%20Wa%20Kike%20Kumlipa%20Baba%20Yake%20Zakaatul-Fitwr%3F
[22] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F1938&title=17-Al-Lajnah%20Ad-Daaimah%3A%20Kugawa%20Zakaatul-Fitwr%20Kwa%20Wanaoomba%20Njiani%20Japokuwa%20Hawastahiki
[23] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F1939&title=18-Al-Lajnah%20Ad-Daaimah%3A%20Kuichelewesha%20Zakaatul-Fitwr
[24] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F1940&title=19-Al-Lajnah%20Ad-Daaimah%3A%20Kuongeza%20Kitu%20Ziada%20Katika%20Zakaatul-Fitwr
[25] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F1942&title=20-Al-Lajnah%20Ad-Daaimah%3A%20Kamlipia%20Zakaatul-Fitwr%20Mtoto%20Aliye%20Tumboni%20Akaja%20Kujua%20Kwamba%20Ni%20Mapacha
[26] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F1941&title=21-Al-Lajnah%20Ad-Daaimah%3A%20Kuwalipia%20Zakaatul-Fitwr%20Wafanyakazi
[27] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F1943&title=22-Al-Lajnah%20Ad-Daaimah%3A%20Mume%20Na%20Mke%20Wamekhasimiana%20Je%2C%20Amlipie%20Mkewe%20Zakaatul-Fitwr%3F
[28] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F1944&title=23-Fatwa%3A%20Kuwalipia%20Watumishi%20Wa%20Nyumbani%20Wasio%20Waislamu%20Zakaatul-Fitwr
[29] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F1945&title=24-Al-Lajnah%20Ad-Daaimah%3A%20Wakati%20Gani%20Zakaatul-Fitwr%20Itolewe%3F%20Na%20Muda%20Gani%20Mwisho%20Kutoa%3F
[30] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F1946&title=25-Imaam%20Ibn%20%E2%80%98Uthaymiyn%3A%20Markaz%20Kununua%20Chakula%20Cha%20Zakaatul-Fitwr%20Mapema%20Ili%20Kuwuazia%20Waislamu
[31] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F1959&title=26-Imaam%20Ibn%20%E2%80%98Uthaymiyn%3A%20Hukmu%20Ya%20Kukanusha%20Zakaatul-Fitwr%20
[32] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F1949&title=27-Imaam%20Ibn%20%E2%80%98Uthaymiyn%3A%20Masikini%20Wanapendekeza%20Kupewa%20Pesa%20Badala%20Ya%20Chakula%20Cha%20Zakaatul-Fitwr
[33] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F8655&title=28-Imaam%20Ibn%20%E2%80%98Uthaymiyn%3A%20Kuwapa%20Zakaatul-Fitwr%20Jamaa%20
[34] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F1950&title=29-Fatwa%3A%20Inaruhusiwa%20kuhamisha%20Zakaatul-Fitwr%20Kutoka%20Nchi%20Kwenda%20Nchi%20Nyingine%3F
[35] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F8654&title=30-Imaam%20Ibn%20%E2%80%98Uthaymiyn%3A%20Kuwatolea%20Zakaatul-Fitwr%20Familia%20Hata%20Kama%20Wameshajitolea
[36] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F1957&title=31-Fatwa%3A%20Ni%20Kweli%20Swawm%20Inanin%27ginia%20Baina%20Ya%20Mbingu%20na%20Ardhi%20Hadi%20Mtu%20Atoe%20Zakaatul-Fitwr%3F
[37] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F1958&title=32-Fatwa%3A%20Kutoa%20Nyama%20Kwa%20Ajili%20Ya%20Zakaatul-Fitwr
[38] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F8656&title=33-Fatwa%3A%20Zakaatul-Fitwr%20Imewajibika%20Kwa%20Mtu%20Asiyefunga%20Ramadhaan%20Kwa%20Dharua
[39] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F8657&title=34-Fatwa%3A%20Inaruhusiwa%20Kumpa%20Zakaatul-Fitwr%20Mama%20Wakubwa%20Na%20Wadogo%3F
[40] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F8658&title=35-Fatwa%3A%20Hakuna%20Masikini%20Wanakoishi.%20Je%20Watume%20Zakaatul-Fitwr%20Nchi%20Nyingine%3F