Hakika ya khumusu ni kitu kingine kilichotumika vibaya na wanazuoni na mujtahidina(wakishia),ikawa ni njia ya kuwaingizia mabwana wakubwa ikawa inawaingizia mali nyingi sana.
Ingawa maelezo ya kisheria yanaonyesha kwa mashia wa kawaida hawalazimishwi khumusu. Bali ni nkhiari yao kufanya hivyo , ispokuwa wao wanaruhusiwa kuitumia khumsi kama wanavyo tumia mali zao, Bali anazingatiwa yule anayetoa khumus kuwapa mabwana wakubwa kuwa anapata madhambi kwa anapingana na maelezo ya Amiril muuminin na viongozi wa Ahlul Bayt (Alayhim Salaam).
Na ili aufahamu vizuri msomaji uhakika wa khumus na jinsi ya kutumika kwake tutaielezea maudhui ya khumus na kushamiri kwake katika historia, na tutayatia nguvu maneno yetu hayo kwa maelezo ya kisheria na maneni ya maimamu na fat’wa za wanazuoni wanaotegemewa na kukubalika maneno yao.
[8:41](واعلموا أنما غنمتم من شيئ فإن لله خمسه وللرسول ولذي القربى) الأنفال 41
{Na jueni ya kwamba chochote mnachokiteka( mnacho kipata ngawira) , basi sehemu yake ya tano ni kwa ajili ya Mwenyezi Mungu na Mtume na jamaa zake Mtume} (Al Anfal 41). Akasema Abuu Abdillah(Alayhis Salaam) kwa kueka mikono yake juu ya magoti yake,kisha akaashiria kwa mikono yake akasema {hivyo na apaa kwa Allah (Subhaanahu wa Ta’ala) nifaida inayopatikana siku hadi siku, isipokua baba yangu amejaalia shia wake kuwahalalishia ili wajitakase}(Al Kaafi 2/499)
Basi riwaya hizi na nyinginezo nyingi ziko wazi katika kuwasamehe mashia khumus kwani wao wameruhusiwa wasitowe basi anayetaka kuitumia yeye mwenyewe,au kuila wala asiwape Ahlul Bayt chochote basi hiyo ni halali yake kufanya atakavyo na wala hakuna dhambi juu yake, bali pia haiwapaswi wao kutoa mpaka atakapo kuja mahdi anaesuniriwa, kama ilivyopokewa katika riwaya ya tatu.
Na hatakama angekuwepo Imamu (kiongozi wa kishia) asingepewa mpaka asimame kiongozi wa Ahlu Bayt, basi itawezekana vipi kupewa wanazuoni na mafaqihi?
Fatwa za mafaqih na wanazuoni wanao tegemewa katika kuwazuia mashia kutowa khumusi.
Kufuatana na hoja zilizo tangulia na nyinginezo nyingi zilizoweka wazi kusamehewa mashia kutowa kuhums zilitolewa fatwa nyingi kutoka kwa wanazuoni wakubwa na mujtahidin miongoni mwa wale wenye upeo mkubwa wa elimu na ambao wana nafasi kubwa kati ya wanazuoni wetu, zinazo halalisha khumsi kwa mashia na kutompa mtu yoyote mpaka atakapo kuja kiongozi wa Ahlul Bayt:
Ninasema: neno
(واعلموا أنما غنمتم من شيئ)
{Na jueni ya kwamba chochote mlicho kipata kitika ngawira}Al anfal:41. kisha akabainisha kuwa kuna riwaya nyingine kutoka kwa Al-Mahdiy akisema mashia tumewahalalishia khumus.
Kama hivyo tunaona ya kwamba kauli ya kuhalalisha khumus kwa mashia,na kuwasamehe wao kutowa kauli hiyo ndio inayojulikana kwa wanazuoni wote wazamani na wa sasa na ndio kauli iliyofanyiwa kazi mpaka mwanzo wa karne ya kumi na nne, achilia mbali kuwa ndiyo yenye ushahidi wa uhalali wake, ,basi itawezekana vipi na ili hali ni hii kutowa khumsi na kuwapa wanazuoni? Pamoja na kuwa maimamu (Alayhis Salaam) waliikataa khumus na wakairudisha kwa wenyewe na wakawasamehe kutowa hiyo khumusi, je inawezekana kuwa wanazuoni ni bora kuliko maimamu (Alayhis Salaam)?
Hakika fat’wa za kuhalalisha khumus kuwapa mashia haiishii kwa hawa tulio wataja peke yao miongoni mwa wanazuoni bali pia kuna zaidi ya idadi hii tulio itaja na kwa kupita karne hizi, lakini tumechagua katika kila karne moja katika mafaqihi na wanaosema kwamba si halali kuwalazimisha watu kutowa khumsi, na kauli hii ndiyo waliyo isema wanazuoni wengi kwa nyakati tofauti kwani ndio kauli inayo tegemewa katika mas’ala haya,na kwa sababu ya kukubaliana kwake na maelezo ya kisheria na vitendo vya maimamu (Alayhis Salaam).
Na tutachukua fatwa mbili za wanazuoni wawili miongoni mwa wanazuoni wa kishia nao ni: sheikh Al mufidu na sheikh Al Tuusiy,amesema sheikh Al mufid: wamekhitalifiana watu miongoni mwetu kwa hilo yaani khumus wakati wa ghaibah kila kundi na msimamo wake ( kisha anataja idadi ya kauli hizo) miongoni mwa wanazuoni kuna wano iondosha kauli ya kutowa khumsi wakati wa ghaiba na kwa sababu ya hojjah zilizo tangulia , na wengine kuna wanaolazimisha izikwe na wanaitafsiri iliyo pokewa isemayo: ( hakika ardhi itatoa hazina zake wakati atapo dhihiri Al imamu na kua yeye (Alayhis Salaam) atapo simama, Mwenyezi Mungu atamjulisha hazina zake na atazichukua kutoka kila sehemu)
Kisha akachagua kauli moja katika hizo.
Kuindosha khumus kwa mwenye mamlaka yaani Al Mahdiy, ikiwa ana wasiwasi wa kufikwa na umauti kabla ya kuja kwake atamuusia anae muamini katika akili yake na dini yake,kwa sharti hili mpaka aje amkabidhi imamu, akikuwahi kuja kwake asipowahi atamuusia mtu atakaye isimamia mwenye sifa kama zake kwa uaminifu na dini kisha wataendelea kuusiana kwa kufuata sharti hili mpaka atakapo kuja imamu, na kauli hii kwangu iko wazi zaidi kuliko zote zilizotazngulia, kwa sababu khumusi ni haki ya imamu aliyejificha na hayakutuka maelekezo yoyote kabla ya kujificha kwake ambayo yanaweza kufuatwa.
Kisha akasema na khumsi inakwenda kama vile zakka ambayo hutolewa pale anapopatikana anaye stahiki kwa hiyo haipasi kuanguka wakati huo , kisha akasema atakapo fuata mtu msimamo huo tulio utaja wa kwamba nusu ya khumsi ni fungu la imamu kisha akaifanya nusu nyingine ni kwa ajili ya familia ya Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) wasafiri wao masikini wao kama ilivyo kuja katika Qur-an.
Amesema atakaye fanya hivi hayupo mbali na kuipata haki katika
Na amesema Al sheikh Al Tuusiy aliyefariki (460H) ambae ni muasisi wa chuo cha kishia
cha Al Najaf na ndiye kiongozi wake wa kwanza baada ya kutaja hukumu za khumus akasema: hii itakuwa katika muda atakao kuja imamu, kisha akasema: ama katika hali ya kutokuwepo wamewaruhusu mashia wao kufanya katika haki zao ndoa, biashara na makazi... ama isiyo kuwa hayo haifai mtu kujifanyia atakavyo kwa hali yoyote ama kile wanacho stahiki katika khumusi zilizo hifadhiwa wakati wa ghaiba, wamekhitalifiana watu wetu kwa hilo na hakuna hoja maalum isipokuwa kila mmoja kati yao mafaqihi wa shia amesema usemi wa kuondowa shaka .
Kisha Al Tuusiy akazidhibiti hoja hizi katika sehemu nne:
Na mafungu matatu mengine yatagawanywa kwa wanao stahiki miongoni mwa mayatima wa familia ya Mohammad na masikini wao na wakatikiwa na njia wao, na haya ni miongoni mwa yanayotakiwa kufanyiwa kazi, na kauli hii inalingana na fat’wa ya mufidu katika kuifananisha khumusi na zaka.
Kisha anasema (na lau wangekuwa watu ni mwenye kutumia njia ya kutoa wasiwasi kwa kuifanyia kazi njia mojawapo kati ya hizi zilizotajwa asinge pata madhambi).
Sheikh Al-Tuusiy ameyadhibiti matumizi ya khumusi katika kauli nne hizi zilizotangulia, na yeye mwenyewe amechaguwa kauli ya nne , lakini akaweka wazi kuwa mtu akichagua kauli yoyote kati ya hizi hana madhambi.
Nasi tunaziona kauli hizi nne, ingawa zimekhitalifiana katika baadhi ya maelezo lakini tunaziona zimekubaliana katika kitu kimoja, ambacho ndicho tunachokielezea , nacho ni kwamba
Na pamoja nakuwa kauli nne hizi zilizotangulia zimekhitalafiana katika namna ya ugawaji wa
Hakika kauli ya nne ambayo ndiyo aliyo ichagua Al shaikh al tuusiy ndiyo waliyokuwa nayo mashia wote , na Al Tuusiy. Kama inavyofahamika ndiye muasisi wa chuo cha kishia cha Annajaf nae ndie sheikh wa kikundi, je hivi unadhani sheikh huyu na mashia wote wa zama zake na wa nyuma yake walikuwa wanakosea .
Basi hii ndiyo fatwa ya kiongozi wa kwanza wa chuo cha Annajaf.
Basi sasa tuone fatwa nyingine ya kiongozi mwingine wa chuo hicho maulana al imamu aliyeaga dunia Abil- Qasim Al khuuiy ili itupambanukie tofauti iliyopo kati ya fatwa ya kiongozi wa kwanza wa chuo hiki na fat’wa ya kiongozi mwengine wa chuo hicho hicho.
Amesema al imamu al khuuiy katika kubainisha anayestahiki kupewa khumus.
Khumus katika zama zetu hugawanywa katika sehemu mbili: nusu ni kwajili ya imamu wa zama hizi Al Hujatu Al Muntadhir mwenyezimungu azifanye fidia roho zetu kwake . Na nusu ni kwa ajili ya banii Hashimu Mayatima wa na masikini wao na walio katikiwa na njia… mpaka aliposema: nusu ambayo inatolewa kwa imamu (Alayhis Salaam) inarejea katika zama za kujificha kwa naibu wake nae ni Al faqihi mwanazuoni mwenye kuaminika anae jua matumizi yake,ima kwa kumpa au kumuomba ruhusa… Angalia kitabu (Dhiyau Al Salihina Mas’ala 1259, Uk: 347) hakika fatwa ya imamu Al khuuiy ina khitalifiana na fatwa ya Al sheikh Al Tuusiy, sheikh Atuusiy hakusema khumus apewe mwanazuoni, na wamefuata maelezo ya fatwa yake mashia wote wa zama zake,ili hali tunaona fatwa ya maulana aliyefariki Al imamu Al khuuiy inatoa hoja ya kuitoa khumus au sehemu yake kupewa faqih na mujatahidin (wanazuoni)
.
Links
[1] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F482&title=05-Kwa%20Ajili%20Ya%20Allaah%20Kisha%20Historia%3A%20Khumus