SWALI:
Nini hukmu ya mwanamke anaye mtamkia mme wake talaka;tangia leo mimi sio mke wako baada ya muda anaolewa na bwana mwingine.
JIBU:
Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘Alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.
Shukrani zetu za dhati kwa swali lako kuhusu mke kutamka talaka kwa mumewe. Kiislamu haki ya talaka anayo mume, ambaye anapoitoa hata kwa mzaha talaka inakuwa imepita.
Mke ikiwa hataki kubakia na mume kwa sababu moja au nyingine ni lazima aende kwa Qadhi ili kuchukua talaka yake. Mke anaweza kupata talaka kupitia kwa Qadhi kwa njia mbili:
Mke wa Thaabit bin Qyasi (Radhiya-Allaahu ‘anhu) alikwenda kushitaki kuwa hamtaki mume ambaye hana kosa lolote isipokuwa kwa maumbile yake. Akamwambia Mtume (Swalla Allaahu ‘Alayhi wa aalihi wa sallam):
“Ewe Mtume wa Allaah; Thaabit bin Qays, simsimangii tabia wala dini, lakini nachukia kukufuru katika Uislamu. Mtume akamwambia utamrejeshea shamba (bustani) yake? Akasema: ndiyo. Mtume akasema kumwambia Thaabit, ‘kubali shamba na umtaliki talaka moja’”. Hadithi hii imepokelewa na Imam Al-Bukhaariy. Na katika Riwaya nyingine ya Hadithi hii Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) alisema: “Utamrejeshea shamba lake (ambalo alikupa kama mahari?) akasema: ndiyo, akarejeshewa shamba lake kisha Mtume akamuamrisha atengane naye”.
Ikiwa mke ndiye aliyemtamkia mumewe kuwa amemtaliki bado talaka haijapita baina
Na Allaah Anajua zaidi.
Links
[1] https://www.alhidaaya.com/sw/taxonomy/term/57
[2] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F4603&title=Mke%20Anayo%20Haki%20Kisheria%20Kutamka%20Talaka%20Kwa%20Mume%3F%20%20Amefanya%20Hivyo%20%20Kisha%20Baada%20Ya%20Muda%20Ameolewa%20Na%20Mwengine%20