Mkwe Anashiriki Mambo Ya Uchawi, Mume
Anaogopa Kumnasihi Mama Yake -
Vipi Mke Awakinge Wanawe?
Alhidaaya.com [2]
SWALI:
Assalam alaykum warahmatullah wabarakatuh.
Napenda kumshukuru Allaah mwingi wa rehma zisizohesabika. In shaa Allaah Ijumaa ya leo iwe njema kwa sote Amin.
Mkwe wangu ana mambo ya ushirikina anataka kuwakabidhi watoto wangu mzimuni. Naomba Mnipe Kinga Yangu Na Watoto Wangu. Hasara mume wangu anaogopa kumwambia kitu mama yake.
JIBU:
AlhamduliLLaah - Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aala) Rabb wa walimwengu, Swalaah na Salaam zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho
Hili ni tatizo sugu katika jamii yetu – ushirikina. Ushirikina ambao unampeleka mtu katika dhulma kubwa na kuishia kwenye Moto wa Jahannam. Inatakiwa dada yetu usimama kidete, imara kuhakikisha kuwa mkwe wako hafaulu katika hayo, na In shaa Allaah hatofaulu.
Mwanzo kabisa kabla ya kutaka kinga ya watoto wako una wajibu wa kuona kuwa mama mkwe wako ametoka katika ushirikina ili asipate kipigo na kichapo cha hapa duniani na Kesho Aakhirah. Ikiwa mumeo hawezi kuzungumza naye basi itabidi utafute watu wengine unaoelewana nao wanaoweza kumnasihi arudi katika Dini sahihi.
Pili, Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ametupatia kinga nyingi kwetu sisi na watoto wetu. Miongoni mwa hizo ni:
In shaa Allaah watoto wako watakuwa salama na hawatodhurika.
Vipi Kuwakinga Watoto Na Mashaytwaan? [4]
Kuhusu Mashaytwaan Na Vipi Kujikinga Nao [5]
Na Allaah Anajua zaidi
Links
[1] https://www.alhidaaya.com/sw/taxonomy/term/213
[2] http://www.alhidaaya.com/sw
[3] http://www.alhidaaya.com/sw/node/1125
[4] http://www.alhidaaya.com/sw/node/312
[5] http://www.alhidaaya.com/sw/node/301
[6] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F4752&title=Mkwe%20Anashiriki%20Mambo%20Ya%20Uchawi%2C%20Mume%20Anaogopa%20Kumnasihi%20Mama%20Yake%20-%20Vipi%20Mke%20Awakinge%20Wanawe%3F