Fataawaa Mas-ala 60 Kuhusu Hedhi Na Nifaas
01-Mwanamke Akitoharika Baada Ya Kuingia Alfajiri Afunge Au Itabidi Alipe Swawm?
Imaam Ibn 'Uthaymiyn (Rahimahu-Allaah)
Alhidaaya.com [3]
SWALI:
Mwanamke akitoharika mara tu baada ya kuingia Alfajiri je atajizuia na kufunga siku hii? Au itabidi aje kulipa?
JIBU:
Mwanamke akitohariki baada kuchomoza Alfajiri, ‘Ulamaa wana kauli mbili kuhusu kujizuia:
Kauli ya Kwanza:
Itabidi ajizuie siku ile nzima na asiihesabu siku ile bali itampasa ailipe, kauli hii ni mashuhuri kwa madhehebu ya Imaam Ahmad (Rahimahu-Allaah).
Kauli ya Pili:
Haimlazimu kujizuia siku ile nzima kwani ni siku ambayo hakuwajibika Swawm kwa kuwa kwake mwenye hedhi na sio katika wanaowajibishwa Swawm na kama ni hivyo basi hakuna faida kwake kujizuia. Na wakati huo sio wakati wa kuheshimika kwake kwani ni mwenye kuamrishwa kwa fitwrah mwanzo wa mchana na Swawm ya ki-Shariy’ah ni kujizuia na vyenye kufunguza Swawm kwa ajili ya kumwabudu Allaah ('Azza wa Jalla) tokea Alfajiri hadi kuzama kwa Jua.
Kauli hii ndio kauli iliyochukuliwa zaidi kuliko ile ya kulazimika kujizuia na kauli zote mbili atalazimika kulipa Swawm.
Fataawaa Mas-ala 60 Kuhusu Hedhi Na Nifaas
02-Mwenye Hedhi Akitoharika Kabla Ya Alfajiri
Lakini Akaoga Baada Ya Swalaah Swawm Yake Sahihi?
Imaam Ibn 'Uthaymiyn (Rahimahu-Allaah)
Alhidaaya.com [3]
SWALI:
Muulizaji huyu anasema: Pindi aliyekuwa na hedhi akitoharika na kukoga (ghuslu) baada ya Swalaah ya Alfajiri akaswali na kukamilisha Swawm ya siku ile, je yampasa kuilipa?
JIBU:
Pindi aliyekuwa na hedhi akitoharika kabla ya kuchomoza Alfajiri, hata kama ni kwa dakika moja lakini akathibitika kutoharika kwake ikiwa ni Ramadhwaan, itamlazimu afunge na Swawm yake siku hiyo itakuwa sahihi wala haimpasi kulipa; kwani alifunga akiwa ametoharika na kama hajakoga ila baada ya kuchomoza Alfajiri basi si neno kwake, kama vile ambavyo mtu atakuwa na janaba baada ya jimai au kuota na akakesha na hakukoga ila baada ya kuchomoza Alfajiri basi Swawm yake itakuwa sahihi.
Kwa mnasaba huu ningependa kuwatanabahisha katika jambo lingine kwa mwanamke inapomjia hedhi hali ya kuwa yuko kwenye Swawm siku ile kwani baadhi ya wanawake wanadhani kuwa hedhi inapowajia baada ya kufuturu kwake (Magharibi) na kabla ya Swalaah ya ‘Ishaa, hudhani kuwa Swawm yake imeharibika siku ile. Hii si kweli na haina asili yoyote ile bali ni kuwa hedhi inapomjia baada ya kuzama kwa jua (Magharibi) walau kwa muda mdogo, basi Swawm yake huwa ni sahihi.
Fataawaa Mas-ala 60 Kuhusu Hedhi Na Nifaas
03-Akitoharika Nifaas Kabla Ya Siku Arubaini Je Aswali Na Afunge?
Imaam Ibn 'Uthaymiyn (Rahimahu-Allaah)
Alhidaaya.com [3]
SWALI:
Je yapasa kwa mwanamke mwenye nifaas afunge na kuswali akitoharika kabla ya arubaini?
JIBU:
Naam. Pindi akitoharika mwenye nifaas kabla ya arubaini basi inawajibika kwake Swawm ikiwa katika Ramadhwaan na itampasa kuswali pia na inajuzu kwa mumewe kujamii naye kwani ametoharika hana kizuizi cha Swawm wala kinachomzuia Swalaah na kupasa kwake kufanya jimai.
Fataawaa Mas-ala 60 Kuhusu Hedhi Na Nifaas
04-Hedhi Yenye Kawaida Ya Siku Sita Au Saba Kisha Ikaendelea Siku Chache
Imaam Ibn 'Uthaymiyn (Rahimahu-Allaah)
Alhidaaya.com [3]
SWALI:
Ikiwa ada ya mwezi ya mwanamke ni siku nane au saba katika mwezi kisha ikaendelea mara moja au mara mbili au zaidi ya hapo hukumu ni ipi?
JIBU:
Ikiwa ada yake mwanamke huyu ni siku sita au saba kisha ikaongezeka muda na ikawa ni nane au tisa au kumi au kumi na moja basi atabaki kutoswali hadi atoharike na hiyo ni kwa sababu Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) hakuweka mpaka maalum katika hedhi na Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Anasema:
وَيَسْأَلُونَكَ عَنِ الْمَحِيضِ ۖ قُلْ هُوَ أَذًى
Na wanakuuliza kuhusu hedhi. Sema: “Hiyo ni dhara; [al-Baqarah: 222]
Madamu damu hii itaendelea kubaki, basi mwanamke ataendelea kubaki katika hali yake hadi atoharike kisha ataoga josho (ghuslu) na kuswali. Na akija katika mwezi mwengine akiwa imepunguka kuliko hivyo basii ataoga josho atakapotoharika hata kama sio katika muda ule uliopita. La muhimu ni kuwa madamu atakuwa bado ni mwenye hedhi hatosali ikiwa hedhi hiyo inawafikiana na muda uliotangulia au imeongezeka au kupungua basi akitoharika tu anawajibika kuswali.
Fataawaa Mas-ala 60 Kuhusu Hedhi Na Nifaas
05-Damu Ya Nifaas Lazima Ifikie Siku Arubaini Au Ikikatika Ametoharika?
Imaam Ibn 'Uthaymiyn (Rahimahu-Allaah)
Alhidaaya.com [3]
SWALI:
Mwanamke mwenye Nifasi atasubiri siku arubaini haswali wala hafungi au mazingatio ni kukatika kwa damu. Muda wa kuwa damu imekatika anaweza kujitoharisha na kuswali?
Na muda upi ni uchache wa kutoharika?
JIBU:
Mwenye Nifasi hana muda maalum lakini muda wa kuwa damu bado ipo atasubiri, hatoswali na hatofunga na hatoingiliana na mume wake. Na akiona ametoharika hata kabla ya arubaini hata kama hakukaa siku tano au kumi basi ataswali na kufunga na kuingiliana na mumewe wala hakuna ubaya hivyo.
La muhimu ni kwamba Nifaas ni jambo lenye kuhisiwa inahusiana hukumu yake kwa kuwepo kwake au kutokuwepo. Madamu (damu) ipo basi hukumu yake itathibitika, na muda wa kuwa ametoharika ataachana na hukumu yake.
Hata hivyo ikizidi zaidi ya siku sitini basi mtu mwenyewe atakuwa ni 'Mustahaadhwah' atakaa na kufuata ada ya hedhi yake tu kisha atakoga na kuswali.
06-Damu Inayotoka Puani Inabatilisha Swawm?
Fataawaa Mas-ala 60 Kuhusu Hedhi Na Nifaas
Imaam Ibn 'Uthaymiyn (Rahimahu-Allaah)
Alhidaaya.com [3]
SWALI:
Damu kidogo sana kama vile tone likitoka kwa mwanamke mchana wa Ramadhwaan na damu hii ikaendelea Ramadhwaan nzima ilhali anafunga, Je, Swawm yake itasihi?
JIBU:
Naam. Swawm yake itasihi. Ama tone hili au alama hii si kitu bali ni kama jasho tu, imepokewa kutoka kwa 'Aliy bin Abi Twaalib (Radhwiya Allaahu 'anhu) kuwa amesema: “Kwa hakika nukta au tone hili ni kama vile Riaaf al-anfu sio hedhi. Hivi imetajwa kutoka kwake (Radhwiya Allaahu 'anhu).
Maana ya Riaaf al-anf: Ni damu inayotoka puani.
07-Akitoharika Nifaas Au Hedhi Kabla Ya Alfajiri Lakini Akajitoharisha (Ghuslu)
Baada Ya Alfajiri Je, Swawm Yake Itasihi?
Fataawaa Mas-ala 60 Kuhusu Hedhi Na Nifaas
Imaam Ibn 'Uthaymiyn (Rahimahu-Allaah)
Alhidaaya.com [3]
SWALI:
Mwenye hedhi au mwenye Nifaas akitoharika kabla ya Alfajiri na hakukoga ila baada ya Alfajiri, je, Swawm yake itasihi au hapana?
JIBU:
Naam. Swawm ya mwanamke mwenye hedhi inasihi akitoharika kabla ya Alfajiri lakini hakujitoharisha (ghuslu) ila baada ya Alfajiri. Kadhalika mwenye Nifaas kwani wakati huo atakuwa ni miongoni mwa wenye Swawm na anafanana na mwenye janaba itakapopambazuka akiwa ana janaba basi Swawm yake inasihi kwa dalili ya kauli ya Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):
فَالْآنَ بَاشِرُوهُنَّ وَابْتَغُوا مَا كَتَبَ اللَّـهُ لَكُمْ ۚ وَكُلُوا وَاشْرَبُوا حَتَّىٰ يَتَبَيَّنَ لَكُمُ الْخَيْطُ الْأَبْيَضُ مِنَ الْخَيْطِ الْأَسْوَدِ مِنَ الْفَجْرِ ۖ
Basi sasa waingilieni na tafuteni Aliyokuandikieni Allaah kwenu. Na kuleni na kunyweni mpaka ubainike kwenu uzi mweupe (mapambazuko) wa Alfajiri kutokana na uzi mweusi (wa kiza cha usiku). [Al-Baqarah: 187]
Hivyo basi ikiwa Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Ameidhinisha kujamiiana mpaka ibainike Alfajiri, imelazimika kufanya ghuslu inapoingia tu Alfajiri.
Na Hadiyth ya ‘Aaishah (Radhwiya Allaahu ‘anhaa) amesema kuwa: “Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akiamka asubuhi akiwa na janaba ya kujamiiana na ahli wake naye akiwa katika Swawm. Yaani: Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa hajitoharishi (ghuslu) kutokana na janaba isipokuwa baada ya kuingia Alfajiri.
08-Akihisi Damu Au Maumivu Ya Hedhi Lakini Haikutoka Kabla Ya Magharibi
Je, Swawm Yake Itasihi?
Fataawaa Mas-ala 60 Kuhusu Hedhi Na Nifaas
Imaam Ibn 'Uthaymiyn (Rahimahu-Allaah)
Alhidaaya.com [3]
SWALI:
Mwanamke akihisi damu na haikutoka kabla ya Magharibi au maumivu ya ada yake je, Swawm yake itasihi au itampasa alipe siku hiyo?
JIBU:
Mwanamke mwenye tohara akihisi damu hali ya kuwa yuko katika Swawm lakini damu yenyewe haikutoka ila baada ya kuzama jua (Magharibi) basi Swawm yake ni sahihi na hawajibishwi kuirejea ikiwa ni Swawm ya fardhi. Kadhalika haibatilishi thawabu yake ikiwa ni Swawm ya Sunnah.
09-Akiona Damu Isiyothibitika Kuwa Ni Hedhi Nini Hukmu Ya Swawm Yake
Fataawaa Mas-ala 60 Kuhusu Hedhi Na Nifaas
Imaam Ibn 'Uthaymiyn (Rahimahu-Allaah)
Alhidaaya.com [3]
SWALI:
Mwanamke akiona damu lakini hakuthibitisha au kuwa na hakika kuwa ni damu ya hedhi. Ni nini hukumu ya Swawm yake siku ile?
JIBU:
Swawm yake siku ile ni sahihi kwani asili ya jambo ni kuwa hana hedhi hadi athibitishe kuwa ana hedhi.
10-Akipata Matone Ya Damu Usiku Ambayo Mara Huwa Ni Hedhi Na Mara Si Hedhi
Nini Hukmu Ya Swawm?
Fataawaa Mas-ala 60 Kuhusu Hedhi Na Nifaas
Imaam Ibn 'Uthaymiyn (Rahimahu-Allaah)
Alhidaaya.com [3]
SWALI:
Mara nyengine mwanamke anaona athari ndogo ya damu au nukta au tone katika nyakati za siku. Mara nyengine huonekana akiwa ada yake wakati huo kabla ya kushuka, na wakati mwingine sio wakati wa ada yake. Ni nini hukumu ya Swawm yake katika hali zote mbili?
JIBU:
Jibu la swali hili nilishalijibu mapema. Kilichobakia ni kuwa ikiwa kuna nukta katika siku zake za hedhi na inaonekana ni damu ya hedhi anayoijua basi itakuwa ni hedhi.
11-Wenye Hedhi Na Nifaas Wanaruhusiwa Kula Mchana Wa Ramadhwaan
Fataawaa Mas-ala 60 Kuhusu Hedhi Na Nifaas
Imaam Ibn 'Uthaymiyn (Rahimahu-Allaah)
Alhidaaya.com [3]
SWALI:
Je Mwenye hedhi na Nifasi wanaruhusiwa kula mchana wa Ramadhwaan?
JIBU:
Naam. Wanaruhusiwa kula mchana wa Ramadhwaan lakini ni vyema iwe kwa siri na haswa kama kuna kijana katika nyumba kwa sababu huenda likamtatiza (akataka kufungulia Swawm).
12-Mwenye Hedhi Au Nifaas Akitoharika Alasiri
Je Anawajibika Kuswali Swalaah Ya Adhuhuri Na Alasiri?
Fataawaa Mas-ala 60 Kuhusu Hedhi Na Nifaas
Imaam Ibn 'Uthaymiyn (Rahimahu-Allaah)
Alhidaaya.com [3]
SWALI:
Akitoharika mwenye hedhi na nifasi wakati wa Alasiri je, itamlazimu kuswali Swalaah ya Adhuhurii na Alasiri au ataswali Adhuhuri tu?
JIBU:
Kauli iliyokubaliwa zaidi katika masuala haya itampasa aswali Alasiri tu. Kwani hakuna dalili ya kupasa kuswali Adhuhuri na asili yake ni 'Baraatu Dhimma' kisha Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Atakayediriki rakaa moja ya Alasiri kabla ya kuzama jua atakuwa amediriki Alasiri.” wala hakutaja kudiriki Adhuhuri na kama Adhuhuri ingekuwa ni wajibu basi Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) angebainisha.
Na lau mwanamke angeanza hedhi yake baada ya kuingia Adhuhuri haitomlazimu isipokuwa kulipa Swalaah ya Adhuhuri bila ya Alasiri pamoja ya kuwa Adhuhuri inakusanywa pamoja na Alasiri.
Hii haitofautiani na hali ya swali la awali. Hivyo kauli inayochukuliwa ni kuwa haimlazimu isipokuwa Swalaah ya Alasiri pekee kwa dalili ya andiko na qiyaas juu yake.
Vivyo hivyo hali lau akitoharika kabla ya kutoka wakati wa ‘Ishaa basi haimlazimu isipokuwa Swalaah ya ‘Ishaa wala halazimikii Swalaah ya Magharibi.
13-Mimba Ikitoka Kabla Ya Kuumbika Kichanga Na Baada Ya Kuumbika
Nini Hukmu Ya Swawm?
Fataawaa Mas-ala 60 Kuhusu Hedhi Na Nifaas
Imaam Ibn 'Uthaymiyn (Rahimahu-Allaah)
Alhidaaya.com [3]
SWALI:
Baadhi ya wanawake waliotoa mimba hali yao ni kama hivyo: Ima mimba iwe imetoka kabla ya kuumbwa kichanga au imetoka baada ya kuumbwa kwake. Ni nini hukumu ya Swawm yake katika siku ile iliyotoka mimba na Swawm ya masiku ambayo ameona damu?
JIBU:
Ikiwa kichanga bado hakijaumbwa basi damu yake hii sio damu ya nifaas, na hivyo anawajibika Swawm na Swalaah na Swawm yake itakuwa ni sahihi. Na ikiwa kichanga kimeumbika basi damu hiyo ni damu ya nifaas na haimpasi kuswali wala Swawm.
Na Shariy’ah katika mas-ala haya ni kwamba ikiwa kichanga kimeshaumbwa basi ni damu ya nifaas, na ikiwa hakijaumbwa basi sio damu ya nifaas, na ikiwa ni damu ya nifaas basi inakuwa kwake haraam kile kilichoharamishwa kwa wenye nifaas na ikiwa sio damu ya nifaas, basi sio haraam kwake hilo.
14-Kutoka Damu Kwa Mwenye Mimba Mchana Wa Ramadhwaan Inaathiri Swawm Yake?
Fataawaa Mas-ala 60 Kuhusu Hedhi Na Nifaas
Imaam Ibn 'Uthaymiyn (Rahimahu-Allaah)
Alhidaaya.com [3]
SWALI:
Mwenye mimba anapotokwa na damu mchana wa Ramadhwaan je, Swawm yake inaathirika?
JIBU:
Damu ya hedhi ikitoka na akawa yuko katika Swawm basi Swawm yake itakuwa imeharibika kwa kauli ya Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam): “Je, kwani akiwa na hedhi si haswali na hafungi?”
Kwa hivyo tunachukuliwa kwa vinavyofunguza Swawm. Na kwa wenye nifaas ni vivyo hivyo, na kutoka damu ya hedhi na nifaas huharibu Swawm. Na kutoka damu kwa mwenye mimba mchana wa Ramadhwaan na ikiwa ni hedhi itakuwa ni hedhi kwa asiye na mimba yaani huathiri kwenye Swawm yake. Kama sio hedhi basi haiathiri.
Na hedhi ambayo inaweza kumpata mwenye mimba ni ile hedhi inakwenda ikirudi haijakatika tokea alipopata mimba bali ilikuwa ikimjia wakati wa ada yake. Hedhi hii kwa kauli iliyoungwa mkono zaidi ni huthibiti juu yake hukumu za hedhi. Ama damu ikikatika na baada ya muda akaona damu basi damu yenyewe sio damu ya ada yake basi hii haiathiri Swawm yake kwani sio damu ya hedhi.
15-Akipata Damu Siku Moja Lakini Ya Pili Yake Hakuona Damu Afanyeje?
Fataawaa Mas-ala 60 Kuhusu Hedhi Na Nifaas
Imaam Ibn 'Uthaymiyn (Rahimahu-Allaah)
Alhidaaya.com [3]
SWALI:
Pindi mwanamke akiona katika kipindi cha ada yake siku moja damu na siku nzima inayofuata haoni afanye nini?
JIBU:
Huu utohara au ukavu aliouona katika nyakati za hedhi yake haihesabiki kuwa ni utohara. Hapa yampata ajizuie kama anavyojizuia mwenye hedhi. Baadhi ya ‘Ulamaa wameserna: “Atakayeona damu na siku nyingine hakuna basi damu hiyo ni damu ya hedhi.”
Na huo usafi au utohara hadi ufikie siku kumi na tano na ikifika muda huo basi damu hiyo itakuwa ni Istihaadhwah na hili ndilo jambo mashuhuri kwa muono wa madhehebu ya Imaam Ahmad bin Hanbal (Rahimahu-Allaah).
16-Alipomalizia Hedhi Kabla Ya Adhuhuri Hakuona Damu Je Afunge Siku Hiyo?
Fataawaa Mas-ala 60 Kuhusu Hedhi Na Nifaas
Imaam Ibn 'Uthaymiyn (Rahimahu-Allaah)
Alhidaaya.com [3]
SWALI:
Katika siku za mwisho za hedhi na kabla ya Swalaah ya Adhuhuri mwanamke hakuona athari yoyote ya damu je afunge siku ya leo ihali hakuona Qiswat baydhwaa (maji maji meupe ambayo ni dalili ya utohara yanayokuja baada ya kukatika damu) au afanye nini?
JIBU:
Ikiwa ni katika ada yake sio kuona Qiswat baydhwaa kama ilivyo kwa baadhi ya wanawake basi na afunge. Na ikiwa ni miongoni mwa ada yake kuona Qiswat baydhwaa basi asifunge hadi aone Qiswat baydhwaa.
Kusoma Na Kuhifadhi Qur-aan Kwa Mwenye Hedhi Au Nifaas Akiangalia Mswahafuni
Fataawaa Mas-ala 60 Kuhusu Hedhi Na Nifaas
Imaam Ibn 'Uthaymiyn (Rahimahu-Allaah)
Alhidaaya.com [3]
SWALI:
Nini hukumu ya usomaji wa Qur-aan kwa mwenye hedhi na nifaas akiwa anaangalia Mswahafuni au anahifadhi na haswa tukizingatia katika hali ya dharura kuwa ni mwanafunzi au mwalimu?
JIBU:
Si vibaya kwa mwanamke mwenye hedhi na nifaas kusoma Qur-aan kwa haja kama vile yeye ni mwalimu au mwanafunzi ambaye anasoma uradi wake wa siku kama ni usiku au mchana. Ama usomaji wa Qur-aan kwa maana ya usomaji wa kupata ujira na thawabu asifanye kwa sababu ‘Ulaama wengi wanaona kuwa mwenye hedhi haimfali kusoma Qur-aan.
Anawajibika Kubadilisha Nguo Baada Ya Kumaliza Hedhi Japokuwa Hazikuingia Damu?
Fataawaa Mas-ala 60 Kuhusu Hedhi Na Nifaas
Imaam Ibn 'Uthaymiyn (Rahimahu-Allaah)
Alhidaaya.com [3]
SWALI:
Je inamlazimu kwa mwenye hedhi kubadilisha nguo zake baada ya kupata tohara pamoja na kujua kuwa nguo zenyewe hazijaingia damu wala najisi?
JIBU:
Haimpasi kufanya hivyo; kwa sababu hedhi hainajisi kiwili wili bali damu ya hedhi ndio ambayo hunajisi pale palipodondokea na ndio maana Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akaamrisha wanawake nguo zao zikipata damu ya hedhi wakoshe kisha waswali nazo.
Hakuweza Kulipa Deni La Swiyaam Mpaka Imefikia Ramadhwaan Ya Tatu
Kwa Sababu Ya Uzazi Kunyonyesha Na Ugonjwa Afanyeje?
Fataawaa Mas-ala 60 Kuhusu Hedhi Na Nifaas
Imaam Ibn 'Uthaymiyn (Rahimahu-Allaah)
Alhidaaya.com [3]
JIBU:
Anauliza muulizaji mmoja kuwa mwanamke amekula (hakufunga) siku saba katika Ramadhwaan akiwa ni mwenye nifaas, na hakulipa hata ikamjia Ramadhwaan nyingine na katika Ramadhwaan hii ya pili siku saba zikampita akiwa ananyonyesha na hakulipa kwa hoja kuwa ana maradhi, afanye nini na inakaribia Ramadhwaan ya tatu kufika. Tupeni faida juu ya hilo na Allaah Atawalipeni?
JIBU:
Ikiwa mwanamke huyu kama alivyotaja mwenyewe kuwa ana maradhi na hawezi kulipa basi pindipo atakapoweza atafunga kwa kuwa ni mwenye udhuru hata kama itakuja Ramadhwaan nyingine. Ama kama hatokuwa na udhuru bali anajifanya kuwa ni mgonjwa na kufanya uvivu na kuzembea basi haifai kwake kuakhirisha kulipa Ramadhwaan hadi Ramadhwaan nyingine. ‘Aaishah (Radhwiya-Allaahu ‘anhaa) amesema: “Ilikuwa kwangu Swiyaam ambazo ninadaiwa sikuwa naweza kuzilipa isipokuwa mwezi wa Sha’baan.”
Kwa hili, ni juu ya mwanamke huyu ajiangalie mwenyewe kama hana udhuru basi atakuwa ni mkosaji na juu yake kutubia kwa Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) na afanye haraka kulipa kilicho katika dhima yake katika Swiyaa,. Ama kama ni mwenye udhuru hapana neno hata kama akichelewa mwaka au miaka miwili.
Kuchelewa Kulipa Deni La Swiyaam Za Ramadhwaan
Fataawaa Mas-ala 60 Kuhusu Hedhi Na Nifaas
Imaam Ibn 'Uthaymiyn (Rahimahu-Allaah)
Alhidaaya.com [3]
SWALI:
Baadhi ya wanawake inawajia Ramadhwaan ya pili ilhali wanadaiwa baadhi za Swiyaam katika Ramadhwaan ya kwanza. Wajibu wao ni nini?
JIBU:
Wajibu wao ni kutubia kwa Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) kwa matendo haya kwani haifai kwa mwenye deni la Swiyaam za Ramadhwaan ya kwanza kuzichelewesha hadi Ramadhwaan ya pili bila ya udhuri kwa kauli ya ‘Aaishah “Nilikuwa nina deni la Swiyaam za Ramadhwaan na nilikuwa siwezi kuilipa hadi inapofika Sha’baan, ndipo nailipa.” Hii inathibitisha kwa dalili kuwa haiwezekani kuichelewesha hadi Ramadhwaan ya pili hivyo ni juu yake atubie kwa Allaah ('Azza wa Jalla) kwa alichokifanya na alipe siku alizowacha baada ya Ramadhwaan ya pili.
Fataawaa Mas-ala 60 Kuhusu Hedhi Na Nifaas
Imaam Ibn 'Uthaymiyn (Rahimahu-Allaah)
21-Alikuwa Na Hedhi Saa Saba Mchana Na Hakuswali Adhuhuri Je Alipe Swalaah Hiyo?
Alhidaaya.com [3]
SWALI:
Mwanamke akiwa kwenye hedhi saa saba mchana kwa mfano naye hakuwa ameswali sala ya adhuhuri je anatakiwa kuilipa swala hiyo?
JIBU:
Katika hili kuna tofauti miongoni mwa ‘Ulamaa.
Kuna miongoni mwao waliosema: Haimpasi kulipa Swalaah hii; kwani hakupetuka mipaka au hakufanya uovu kwani inampasa yeye kuchelewesha Swalaah hadi mwisho wa wakati wake.
Na kuna miongoni mwao waliosema: Inampasa kulipa , yaani kulipa Swalaah ile kwa Hadiyth Ya Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) “Atakayediriki rakaa moja basi ameidiriki Swalaah.”
Na jambo la akiba ni kuilipa kwani ni Swalaah moja tu haina mashaka kuilipa.
Fataawaa Mas-ala 60 Kuhusu Hedhi Na Nifaas
Imaam Ibn 'Uthaymiyn (Rahimahu-Allaah)
22-Akiona Damu Kabla Ya Kuzaa Siku Moja Au Mbili Je Aache Swawm Na Swalaah?
Alhidaaya.com [3]
SWALI:
Mwanamke mwenye mimba akiona damu kabla ya kuzaa kwa siku moja au mbili je kwa ajili hiyo ataacha kufunga na kuswali?
JIBU:
Pindi mwanamke mwenye mimba akiona damu kabla ya kujifungua kwa siku au siku mbili basi hayo ni maumivu ya kujifungua na hiyo ni damu ya Nifaas na aache Swalaah na Swawm.
Na kama akiwa hana maumivu hayo basi itakuwa ni damu chafu hakuna mazingatio ndani yake wala haimzuii na Swalaah na Swawm.
Fataawaa Mas-ala 60 Kuhusu Hedhi Na Nifaas
Imaam Ibn 'Uthaymiyn (Rahimahu-Allaah)
23-Kutumia Vidonge Kuzuia Hedhi Ili Aweze Swiyaam Inafaa?
Alhidaaya.com [3]
SWALI:
Vipi kama nitatumia vidonge vya kuzuia kwenda mwezini ili nipate kufunga na watu?
JIBU:
Mimi natahadharisha hili, vidonge hivi vina madhara makubwa, hili lilinithibitikia kutoka kwa madaktari. Tutamwambia mwanamke “Jambo hili limeandikwa na Allaah ('Azza wa Jalla) kwa banati wa wana Aadam, kwa hivyo kinai akichokuandikia Allaah ('Azza wa Jalla) na funga pale ambapo hapana kizuizi, na ikitokea kizuizi fungua kuridhika na lile Alilokukadiria Allaah ('Azza wa Jalla).
Fataawaa Mas-ala 60 Kuhusu Hedhi Na Nifaas
Imaam Ibn 'Uthaymiyn (Rahimahu-Allaah)
24-Baada Ya Miezi Miwili Ya Nifaas Akatoharika
Ameona Matone Ya Damu Aache Swalaah Na Swiyaam
Alhidaaya.com [3]
SWALI:
Anauliza muulizaji: Mwanamke baada ya miezi miwili ya Nifaas na baada ya kutoharika anaona matone madogo ya damu je atafungua na haswali? Au afanye nini?
JIBU:
Matatizo ya mwanamke kuhusu hedhi na nifaas ni bahari isiyo na pwani. Sababu mojawapo ni kutumia vidonge hivi vyenye kuzuia mimba na vyenye kuzuia hedhi na watu wengi hawayajui matatizo haya makubwa. Ni kweli matatizo haya yapo tokea kwa kutimilizwa Nabiy wetu Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) bali tokea kuwepo kwa mwanamke ulimwenguni, isipokuwa uwepo wake unaomfanya mtu kutatizika unaowapata watu wengi katika kufikia suluhisho lake ni jambo la kusikitisha sana.
Hata hivyo kawaida ya Shariy’ah ni kuwa mwanamke akitoharika na akiona tohara anayoiamini na yakini katika hedhi na nifaas; nakusudia tohara ya hedhi kutoka kwa maji meupe yanayojulikana na wanawake je baada ya tohara kuna maji machafu au manjano au umajimaji; zote hizi sio hedhi, hivyo haimzuii na Swalaah wala Swiyaam, wala jimai ya mtu kwa mke wake kwa sababu sio hedhi. Ummu ‘Atwiyyah amesema, ‘Tulikuwa hatuoni umanjano na umajimaji kuwa ni kitu’ [Al-Bukhari] na Abuu Daawuwd akazidisha: “Baada ya tohara.” Na Isnaad yake ni Swahiyh.
Kwa haya tunasema: Kila kinachotokea baada ya tohara yakini kwa mambo haya haimdhuru mwanamke na haimzuii na Swalaah yake wala Swiyaam zake wala kuingiliwa na mumewe, bali yapasa tusifanye haraka hadi tuone tohara, kwa sababu baadhi ya wanawake damu ikikauka anafanya haraka kukoga kabla ya kuona tohara. Hili liliwafanya wanawake Maswahaba wakienda kwa mama wa waumini ‘Aaishah (Radhwiya-Allaahu ‘anhaa) wakienda na pamba ikiwa na damu na ‘Aiashah akiwaambia: “Msifanye haraka hadi muone maji meupe.”.
Fataawaa Mas-ala 60 Kuhusu Hedhi Na Nifaas
Imaam Ibn 'Uthaymiyn (Rahimahu-Allaah)
25-Damu Inaendelea Na Inakatika Siku Moja Au Mbili Kisha Inarudi
Alhidaaya.com [3]
SWALI:
Baadhi ya wanawake damu inaendelea na wakati mwingine inakatika siku moja au mbili kisha inarudi. Nini hukumu ya hali hii kwa Swalaah na Swiyaam na ‘Ibaadah zingine?
JIBU:
Kinachojulikana kwa ‘Ulamaa ni kuwa mwanamke akiwa kwenye ada yake kisha ikakatika anakoga na kuswali na kufunga na anachokiona baada ya siku mbili au tatu sio hedhi, kwa sababu tohara chache kwa ‘Ulamaa hao ni siku kumi na tatu.
Wamesema baadhi ya ‘Ulamaa kuwa “Muda wowote akiona damu basi ni hedhi na muda akitoharika kwayo basi ni tohara na hata kama sio kati ya hedhi mbili siku kumi na tatu.”
Fataawaa Mas-ala 60 Kuhusu Hedhi Na Nifaas
26-Wanawake Bora Kuswali Nyumbani Au Miskitini
Katika Nyusiku Za Ramadhwaan Kufaidika Na Mawaidha?
Imaam Ibn 'Uthaymiyn (Rahimahu-Allaah)
Alhidaaya.com [3]
SWALI:
Lipi bora kwa mwanamke; kuswali usiku nyumbani kwake wakati wa Ramadhwaan au kuswali Msikitini na haswa ikiwa kuna mawaidha na kukumbushwa kuhusu Dini. Na nini maelekezo yako kwa wanawake wanaoswali Misikitini?
JIBU:
Bora zaidi ni kuswali nyumbani kwa ujumla wa kauli ya Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam):
وبيوتهن خير لهن
“Na nyumbani kwao ni bora zaidi.”
Na mwanamke kutoka nyumbani kwake wakati mwingine hasalimiki kwa fitnah. Hivyo mwanamke kubaki nyumbani mwake ni bora zaidi kwake kuliko kwenda Msikitini kuswali. Ama Hadiyth na mawaidha mbali mbali anaweza kuyapata kwa njia ya kanda mbali mbali.
Ama maelekezo yangu kwa wale wanaokwenda kuswali Misikitini ni kuwa watoke majumbani mwao bila ya kujipamba na wasipake uturi.
Fataawaa Mas-ala 60 Kuhusu Hedhi Na Nifaas
27-Kuonja Chakula Mchana Wa Ramadhwaan Kwa Mwenye Swawm Inafaa?
Imaam Ibn 'Uthaymiyn (Rahimahu-Allaah)
Alhidaaya.com [3]
SWALI:
Nini hukumu ya kuonja chakula katika mchana wa Ramadhwaan kwa mwanamke aliyefunga?
JIBU:
Si vibaya kulingana na haja iliyopo lakini ateme anachokionja baada ya kuonja.
Fataawaa Mas-ala 60 Kuhusu Hedhi Na Nifaas
28-Mwanamke Kapata Ajali Akiwa Na Mimba Changa
Akatokwa Damu Nyingi Je Afungulie Swawm
Imaam Ibn 'Uthaymiyn (Rahimahu-Allaah)
Alhidaaya.com [3]
SWALI:
Mwanamke kapata ajali na alikuwa na mimba katika miezi ya mwanzo na mimba ikatoka baada ya kutoka damu nyingi. Je yapasa afungulie Swawm yake au aendelee na Swawm? Na je akifungua atakuwa ana madhambi yoyote?
JIBU:
Tunajibu kwa kusema kuwa mwenye mimba hawi na hedhi kama alivyosema Imaam Ahmad: “Wanawake wenye mimba wanafahamika kwa kukatika kwa hedhi.” Na hedhi kama walivyosema ‘Ulamaa imeumbwa na Allaah (Tabaaraka wa Ta’aalaa) kwa hekima: Chakula cha kichanga katika tumbo la mamake, na mimba ikianza hedhi hukatika; lakini baadhi ya wanawake inaweza kuendelea hedhi yake kama ilivyokuwa kabla ya mimba, kwa hili inahukumiwa kuwa hedhi yake ni sahihi; kwa sababu kwani hedhi iliendelea na haikuathiriwa na mimba, kwa hali hiyo hedhi hii inakuwa ni kizuizi kwa kila chenye kuzuia hedhi isipokuwa mimba inapaswa kwa kila chenye kupaswa na hudondoka kwa kila chenye kudondoshwa. Matokeo yake ni kuwa damu inayotoka kwa mwenye mimba zipo aina mbili:
Aina ya kwanza: Aina ambayo inahukumiwa kuwa ni hedhi ambayo inaendelea kama vile ilivyokuwa kabla ya mimba. Kwa maana hiyo kuwa mimba haikuuathiri basi itakuwa ni hedhi.
Aina ya pili: Ni damu inayotoka kwa mwenye mimba na kuchuruzika ima ni kwa sababu ya ajali, au kubeba kitu, au kuangukia kitu na mfano wa hayo. Damu hii sio damu ya hedhi bali ni damu ya ‘Irq (damu ya Istihaadhwah). Kwa hili halimzuii na Swalaah wala Swawm bali yeye ataingia katika hukmu ya watu waliotoharika.
Ama ikitokea kwenye ajali mtoto akatoka au mimba tumboni ikidondoka basi ni kama walivyosema ‘Ulamaa akitoka na kubainika kuwa mwana Aadam keshaumbwa, basi damu yake baada ya kutoka itakuwa ni nifaas na hapo ataacha Swalaah na Swawm na atajitenga mbali na mumewe hadi atoharike. Na kama kichanga kitatoka kabla hajaumbwa basi haizingatiwi kuwa ni damu ya nifaas, bali ni damu chafu ambayo haimkatazi na Swalaah wala Swiyaam wala yasiyokuwa hayo.
‘Ulamaa wamesema: “Na muda mchache wa kuumbwa kichanga tumboni ni siku themanini na moja; kwani kichanga katika tumbo la mamake kama alivyosema ‘Abdullah bin Mas’uwd (Radhwiya Allaahu 'anhu) kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alituhadithia naye ni mkweli wa kusadikishwa kasema:
(إِنَّ أَحَدَكُمْ يُجْمَعُ خَلْقُهُ فِي بَطْنِ أُمِّهِ أَرْبَعِينَ يَوْمًا نُطْفَةً، ثُمَّ يَكُونُ عَلَقَةً مِثْلَ ذَلِكَ، ثُمَّ يَكُونُ مُضْغَةً مِثْلَ ذَلِكَ، ثُمَّ يُرْسَلُ إلَيْهِ الْمَلَكُ فَيَنْفُخُ فِيهِ الرُّوحَ، وَيُؤْمَرُ بِأَرْبَعِ كَلِمَاتٍ: بِكَتْبِ رِزْقِهِ، وَأَجَلِهِ، وَعَمَلِهِ، وَشَقِيٍّ أَمْ سَعِيدٍ رواه البخاري ومسلم
Kutoka kwa Abuu 'Abdir-Rahmaan 'Abdillaah bin Mas-‘uwd (Radhwiya Allaahu 'anhu) ambaye amesema: “Ametusimulia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ambaye ni mkweli mwenye kuaminiwa: “Hakika kila mmoja wenu hukusanywa umbo lake katika tumbo la mama yake siku arubaini akiwa ni mkusanyiko wa mbegu (za uzazi za mama na baba), kisha arubaini zifuatazo huwa ni donge la damu, kisha arubaini zijazo huwa pande la nyama, kisha Allaah Humtuma Malaika kwake na kumpulizia roho (yake). Na (Malaika huyo) anaamrishwa maneno manne; Kuandika rizki yake, ajali yake (umri atakaoishi duniani), amali zake, mtu muovu au mwema. [Al-Bukhaariy, Muslim]
Hawezi kuumbwa kabla ya hapo na mara nyingi uumbaji hauonekani kabla ya siku tisiini kama walivyosema baadhi ya ‘Ulamaa.
Fataawaa Mas-ala 60 Kuhusu Hedhi Na Nifaas
29-Ameharibu Mimba Mwaka Jana Akiwa Na Miezi Mitatu Hakuswali Mpaka Alipotoharika Je Alipaswa Kuswali Na Kama Hakujua Idadi Ya Siku Afanyeje?
Imaam Ibn 'Uthaymiyn (Rahimahu-Allaah)
Alhidaaya.com [3]
SWALI:
Mimi ni mwanamke ambaye nimetoa mimba katika mwezi wa tatu yapata mwaka hivi, na sikuanza kuswali hadi nilipotoharika na niliambiwa kuwa ilikuwa juu yako kuswali. Je nifanye nini nami sijui idadi za siku haswa?
JIBU:
Kinachojulika kwa ‘Ulamaa ni kuwa mwanamke akiangusha mimba baada ya miezi mitatu basi haswali; kwa kuwa mwanamke akidondosha mimba basi imeshabainika kuwa kichanga kimeshaumbwa kwani damu ambayo inatoka itakuwa ni damu ya nifaas, kwa hiyo hatakiwi kuswali. ‘Ulamaa wamesema: “Inayumkinika kubaini uumbwaji wa kichanga ikitimia siku themanini na moja.” Na hizi ni chini ya miezi mitatu. Kwa hiyo akiwa na yakini kuwa kichanga kimedondoka baada ya miezi mitatu, basi ambayo itakuwa imemsibu itakuwa ni damu chafu. Lakini ikiwa kabla ya siku themanini, basi damu itakuwa ni kwa ajili ya ugonjwa na haachi kuswali. Na huyu muulizaji akumbuke kuwa kama kichanga kimedondoka kabla ya siku themanini basi itabidi alipe Swalaah na kama hajui ni ngapi ameacha basi na akadirie na alipe anayodhania hakuswali ndani yake.
Fataawaa Mas-ala 60 Kuhusu Hedhi Na Nifaas
30-Hakulipa Deni La Swiyaam Kwa Kutokujua Siku Alizofungulia Afanyeje?
Imaam Ibn 'Uthaymiyn (Rahimahu-Allaah)
Alhidaaya.com [3]
SWALI:
Muulizaji anauliza: Tokea imuwajibikie Swiyaam, amekuwa akifunga Ramadhawaan lakini hakuwa akilipa siku alizoshindwa kufunga kwa sababu ya ada yake ya mwezi na vile kutokujua siku alizofungua. Anaomba maelekezo cha anachotakiwa kufanya?
JIBU:
Inatusikitisha kutokea mas-ala kama haya kwa wanawake Waislaam.
Kuacha huku, yaani kuacha kulipa deni (la Swiyaam) za kumuwajibikia, itakuwa ni ima kwa sababu ya ujahili au kwa sababu ya uzembe, na yote hayo yote ni msiba, kwa kuwa ujahili tiba yake ni elimu na kuuliza.
Ama uzembe tiba yake ni taqwa ya Allaah ('Azza wa Jalla) na kuchunga maamrisho Yake na kuogopa adhabu Yake na kukimbilia kufanya yale yenye kumridhisha.
Hivyo ni juu ya mwanamke huyu kutubia kwa Allaah kwa alichokifanya na aombe maghfirah na kujaribu kukumbuka siku alizoacha kwa kadiri ya uwezo wake na alipe. Kwa haya dhima yake itaondoka na tunataraji Allaah Ataqabali tawbah yake.
Fataawaa Mas-ala 60 Kuhusu Hedhi Na Nifaas
31-Akipata Hedhi Baada Ya Kuingia Wakati Wa Swalaah
Au Akitoharika Kabla Ya Kutoka Wakati
Imaam Ibn 'Uthaymiyn (Rahimahu-Allaah)
Alhidaaya.com [3]
SWALI:
Muulizaji anauliza: Ni nini hukumu ya mwanamke akiingia kwenye hedhi baada ya kuingia wakati wa Swalaah? Je yampasa ailipe akitoharika? Na vile vile akitoharika kabla ya kutoka wakati wa Swalaah?
JIBU:
Kwanza: Mwanamke akiingia katika hedhi baada ya kuingia wakati yaani baada ya kuingia wakati wa Swalaah inampasa kwake akitoharika kuilipa Swalaah ile kama hakuiswali kabla ya kumjia hedhi kwa kauli ya Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam):
من أدرك ركعة من الصلاة فقد أدرك الصلاة
“Atakayediriki rakaa katika Swalaah basi ameidiriki Swalaah yenyewe.”
Hivyo kama mwanamke ameidiriki Swalaah kiasi cha rakaa kisha ikamjia hedhi kabla ya kuswali basi akitoharika itamlazimu kuilipa.
Pili: Akitoharika na hedhi kabla ya kuondoka kwa wakati wa Swalaah itampasa ailipe Swalaah ile. Na akitoharika kabla ya kuchomoza kwa jua kwa kiasi cha rakaa basi inampasa kuilipa Swalaah ya Alfajiri. Na akitoharika kabla ya kuzama kwa jua kwa kiasi cha rakaa basi ni juu yake kulipa Swalaah ya Alasiri. Na akitoharika kabla ya kufikia nusu ya usiku kwa kadiri ya rakaa, basi inamwajibikia alipe Swalaah ya ‘Ishaa. Akitoharika baada ya kufikia nusu ya usiku, haimwajibikii kulipa Swalaah ya ‘Ishaa, bali aswali Alfajiri itakapofika wakati wake. Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Anasema:
فَإِذَا اطْمَأْنَنتُمْ فَأَقِيمُوا الصَّلَاةَ ۚ إِنَّ الصَّلَاةَ كَانَتْ عَلَى الْمُؤْمِنِينَ كِتَابًا مَّوْقُوتًا
Mtakapopata utulivu, simamisheni Swalaah (kama desturi), hakika Swalaah kwa Waumini ni fardhi iliyowekwa nyakati maalumu)). [An-Nisaa (4:103)]
Yaani faradhi yenye wakati maalum haimpasi mtu kuiacha Swalaah kutoka katika wakati wake hajaswali au kuianza kabla ya kuingia wakati wake.
Fataawaa Mas-ala 60 Kuhusu Hedhi Na Nifaas
31-Amepata Hedhi Wakati Anaswali Afanyeje
Na Je Alipe Swalaah Muda Wa Hedhi?
Imaam Ibn 'Uthaymiyn (Rahimahu-Allaah)
Alhidaaya.com [3]
SWALI:
Niliingia katika ada ya mwezi (hedhi) wakati wa Swalaah, Je, nifanye nini? Je nilipe Swalaah katika muda wote wa ada yangu
JIBU:
Ikitokezea umeingia katika hedhi baada ya kuingia wakati wa Swalaah kwa mfano kuingia mwezini baada ya kuzama (zawaal) kwa nusa saa, basi yeye baada ya kutoharika na hedhi atailipa Swalaah hii ambao umeingia wakati wake naye akiwa mwenye tohara kwa kauli yake Ta’aalaa:
إِنَّ الصَّلَاةَ كَانَتْ عَلَى الْمُؤْمِنِينَ كِتَابًا مَّوْقُوتًا
Hakika Swalaah kwa Waumini ni fardhi iliyowekwa nyakati maalumu. [An-Nisaa (4:103)]
Wala hatolipa Swalaah wakati wa hedhi kwa kauli yake Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) katika Hadiyth ndefu:
أليست إذا حاضت لم تصل ولم تصم
“Je si akiwa mwezini haswali na hafungi…”
‘Ulamaa wamekubaliana kuwa mwanamke halipi Swalaah iliyompita alipokuwa wakati wa hedhi. Ama akitoharika na ikabakia wakati kiasi cha rakaa moja na zaidi ya hapo basi huswali wakati ule aliotoharika kwa kauli yake Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam): “Atakayediriki rakaa katika Swalaah ya Alasiri kabla ya kuzama kwa jua basi huyu amediriki Swalaah ya Alasiri.”
Akitoharika wakati wa Alasiri au kabla ya kuchomoza kwa jua na akawa amebaki hadi kuzama kwa jua au kuchomoza kwake kiasi cha rakaa moja basi ataswali Alasiri katika masuala ya mwanzo na Alfajiri katika masuala ya pili.
Fataawaa Mas-ala 60 Kuhusu Hedhi Na Nifaas
33-Ana Umri Wa Sitini Na Tano Sasa Anapata Damu Inayoendelea Miaka Mitatu
Nini Hukmu Ya Swawm?
Imaam Ibn 'Uthaymiyn (Rahimahu-Allaah)
Alhidaaya.com [3]
SWALI:
Nina mama yangu mzazi mwenye umri wa miaka sitini na tano na ana muda wa miaka ipatayo kumi na tisa hajapata mtoto na sasa hivi damu inamtoka yapata muda wa miaka mitatu. Hivi inaelekea maradhi haya aliyapata wakati ule na hivi karibuni kuna Swiyaam je unamnasihi nini au tufanye nini?
JIBU:
Katika hali hii kwa mwanamke huyu ambaye amepatwa damu ya kuendelea, hukmu yake ni kuacha Swalaah na Swawm kwa muda wa ada yake ya zamani kabla ya kutokea kwa tukio hili. Kwa mfano, ikiwa hedhi yake ilikuwa inamjia mwanzo wa mwezi kwa muda wa siku sita, basi itabidi akae siku sita ya kila mwanzo wa mwezi asiswali na asifunge. Baada ya siku hizo kumalizika akoge na aswali na afunge.
Namna ya Swalaah kwa huyu na mfano wake ni: Kuosha sehemu zake za siri vizuri sana na atawadhe wakati ule inapoingia wakati wa Swalaah ya faradhi, na kwa hali hii ili kuondosha mashaka juu yake ni kujumuisha Swalaah ya Adhuhuri na Alasiri na Maghribi pamoja na ‘Ishaa, ili iwe kufanya kwake hivi, ni moja kwa Swalaah zake mbili; Swalaah ya Adhuhuri na Alasiri, na moja kwa ajili ya Swalaah ya Magharibi na ‘Ishaa na moja kwa ajili ya Swalaah ya Alfajiri; badala ya kufanya hivyo mara tano kwa siku, atafanya mara tatu tu.
Narejea kusema tena kwa mara ya pili: Anapotaka kujitoharisha atakosha sehemu zake za siri vizuri na kukausha kwa nje kwa kipande cha nguo au mfano wake hadi nje pakauke, kisha atatawadha na kuswali. Ataswali Adhuhuri rakaa nne, Alasiri rakaa nne, Maghrib tatu, ‘Ishaa nne na Alfajiri mbili, na hatopunguza Swalaah kwa kufupisha kama wanavyodhani baadhi ya watu. (Bali kuunganisha zikiwa kamilifu).
Hata hivyo inajuzu kukusanya Adhuhuri na Alasiri, Maghrib na ‘Ishaa. Adhuhuri na Alasiri ima iwe kutanguliza au kuchelewesha na kadhalika Maghrib na ‘Ishaa kwa kutanguliza au kuchelewesha na akitaka kuswali Sunnah kwa udhu huu hakuna neno.
Fataawaa Mas-ala 60 Kuhusu Hedhi Na Nifaas
34-Mwenye Hedhi Kuweko Msikitini Kwa Ajili Ya Kusikiliza Hadiyth Na Khutbah
Imaam Ibn 'Uthaymiyn (Rahimahu-Allaah)
Alhidaaya.com [3]
SWALI:
Nini hukumu ya kuwepo mwanamke katika Masjid Al-Harama naye ni mwenye hedhi kwa ajili ya kusikiliza khutbah au Hadiyth?
JIBU:
Haijuzu kwa mwanamke mwenye hedhi kukaa Masjid Al-Haraam au katika Msikiti mwingine wowote, bali inapasa kupita Msikitini na kuchukua haja yake na mfano wake kama alivyosema Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kumwambia ‘Aaishah alipomwambia alete kilemba naye ‘Aaishah akasema: “Kipo Msikitini nami ni mwenye hedhi.” Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akasema: “Hedhi yako haipo mikononi mwako.”
Ikiwa mwenye hedhi atapita Msikitini na akaaminisha kutokuteremka kwa damu ya hedhi pale Msikitini sio tatizo.
Ama akitaka kuingia na kukaa, basi hii haijuzu, na dalili juu ya hilo ni kauli yake Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alipowaamrisha wanawake watoke kwenda kwenye Mswalla wa ‘Iyd isipokuwa wenye hedhi waliambiwa wasikae kwenye Muswalla.
Hii ni dalili kuwa mwenye hedhi hatakiwa kukaa Msikitini kwa kusikiliza khutbah au darsa au Hadiyth.
Fataawaa Mas-ala 60 Kuhusu Hedhi Na Nifaas
35-Majimaji Yanayomtoka Mwanamke Mara Kwa Mara Ni Tohara Au Najisi
Je Afanye Achukue Wudhuu?
Imaam Ibn 'Uthaymiyn (Rahimahu-Allaah)
Alhidaaya.com [3]
SWALI:
Je majimaji yanayomtoka mwanamke yawe ni manjano au meupe ni tohara au yana najisi? Na je yampasa kuchukua wudhuu pamoja na kufahamu kuwa yanatoka mara kwa mara? Na ipi hukumu yake ikiwa yanakatika na haswa ya kuwa wanawake wengi zaidi wale wasomi wanaona ni majimaji ya kawaida hayahitaji wudhuu?
JIBU:
Kilichonidhihirikia mimi ni kuwa majimaji yanayotoka kwa mwanamke ikiwa hayatotoka katika kinena bali yanatoka katika fuko la uzazi basi ni tohara, lakini yanatengua wudhuu hata kama ni tohara kwa kuwa haishurutishi kwa kinachotengua wudhuu kuwa ni najisi. Kwa mfano upepo unaotoka katika duburi ambao ni lazima utoke pamoja na hayo unatengua wudhuu na kwa hiyo ikitoka kwa mwanamke mwenye wudhuu basi utatengua wudhuu wake na aufanye upya wudhuu wake.
Ikiwa yataendelea mara kwa mara basi hayatotengua wudhuu, lakini atatawadha kwa ajili ya Swalaah itakapoingia wakati wake na wakati huu ataswali Swalaah yake ya faradhi na za Sunnah na kusoma Qur-aan na yaliyoruhusiwa kama walivyosema ‘Ulamaa. Kwa mfano kama huu, kwa yule ambaye mkojo unamtoka mara kwa mara bila kuwa na uwezo wa kuuzuia. Hii ni hukmu ya muulizaji kwa njia ya utohara basi tohara. Na kwa upande wa wudhuu ni kuwa yanatengua wudhuu isipokuwa kama yataendelea. Kama yatakuwa yanaendelea basi hayatengui wudhuu wake isipokuwa kwa mwanamke atatakiwa achukue wudhuu wake pale tu inapoingia wakati wa kuswali au auhifadhi. Ama kama yatakuwa ni ya kukatika katika na ilikuwa ada yake kukatika tu wakati wa Swalaah, basi atachelewesha wakati wa Swalaah hadi katika wakati ambao yanakatika kama hatohofia kutoka kwa wakati, akihofia kutoka kwa wakati basi atatawadha na kuuhifadhi na kuswali. Wala hakuna tofauti yoyote kati ya kidogo na kingi kwa kuwa yote yanatoka katika njia (ya uchi) na yote yanatengua wudhuu yawe ni kidogo au kingi, tofauti na yanayotoka katika sehemu zingine katika kiwiliwili kama vile damu, matapishi; hizi hazitengui wudhuu wa mtu yawe mengi au kidogo.
Ama itikadi ya baadhi ya wanawake kuwa hayatengui wudhuu mimi sijui asili ya maneno haya isipokuwa kauli moja tu ya Ibn Hazm (Rahimahu-Allaah) yeye amesema, “Haya hayatengui udhu.” Lakini hakutaja dalili yake, na lau akiwa na dalili katika Kitabu na Sunnah au kauli za Maswahaba, ingekuwa ni hoja. Ni juu ya mwanamke kumcha Allaah na kujali sana tohara yake, kwa kuwa Swalaah haifai bila ya tohara na hata mtu akiswali mara mia moja, bali baadhi ya ‘Ulamaa wanasema: “Yule ambaye anaswali bila ya tohara hufanya mambo ya ukafiri.” kwani hii ni katika istihzai ya kwa Aayah za Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa).
Fataawaa Mas-ala 60 Kuhusu Hedhi Na Nifaas
36-Mwanamke Anayetokwa Majimaji Anafaa Kusoma Qur-aan
Na Kuswali Swalaah Za Sunnah?
Imaam Ibn 'Uthaymiyn (Rahimahu-Allaah)
Alhidaaya.com [3]
SWALI:
Mwanamke akitawadha ambae hutokwa na majimaji haya kwa ajili ya Swalaah ya faradhi je ni sahihi kwake aswali anachotaka kwa ajili ya Sunnah na kusoma Qur-aan kwa wudhu wa faradhi ile kwa ajili ya faradhi nyingine?
JIBU:
Akitawadha kwa ajili ya Swalaah ya faradhi kwa wakati wake wa mwanzo basi ni juu yake kuswali faradhi, Sunnah au kusoma Qur-aan hadi wakati mwingine wa Swalaah nyingine.
Fataawaa Mas-ala 60 Kuhusu Hedhi Na Nifaas
37-Mwanamke Anayetokwa Majimaji
Je, Inajuzu Aswali Swalaah Ya Adhw-Dhwuhaa Kwa Wudhuu Wa Alfajiri?
Imaam Ibn 'Uthaymiyn (Rahimahu-Allaah)
Alhidaaya.com [3]
SWALI:
Je, ni sahihi mwanamke (anayetokwa majimaji)
kuswali Swalaah ya Adhw-Dhwuhaa kwa udhuu wa (Swalaah ya) Alfajiri?
JIBU:
Haisihi kwa kuwa Swalaah ya Adhw-Dhwuhaa imewekwa muda maalum hivyo basi hapana budi kuchukuwa wudhuu unapoingia wakati wake kwa sababu mwanamke huyu ni kama vile mustahaadhah, na Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ameamrisha Mustahadhah achukue udhu katika kila Swalaah.
Wakati wa Adhuhuri ni: Pindi jua linapokuwa katikatika hadi wakati wa Alasiri.
Wakati wa Alasiri ni: Kutoka kwa wakati wa Adhuhuri hadi jua linapokuwa la njano au mpaka linapokaribia kuzama. Katika hali yake ya dharura ni kuzama kwa jua.
Wakati wa Magharibi ni: Kuzama kwa jua hadi kuondoka wekundu wa jua.
Wakati wa ‘Ishaa ni: Kupotea wekudu wa jua hadi katikati ya usiku.
Fataawaa Mas-ala 60 Kuhusu Hedhi Na Nifaas
38-Anayetokwa Majimaji Je Inasihi Aswali Qiyaamul-Layl Kwa Wudhuu Wa ‘Ishaa?
Imaam Ibn 'Uthaymiyn (Rahimahu-Allaah)
Alhidaaya.com [3]
SWALI:
Je inasihi kwa mwanamke huyu (anayetokwa majimaji) kuswali Qiyaamul-Layl itapokatika nusu ya pili ya usiku kwa wudhu wa ‘Ishaa?
JIBU:
Hapana, itakapokatika usiku wa nusu ya pili inapasa kuchukua wudhu mwingine. Na imesemwa pia halazimiki kurejea kuchukua wudhu, na hii ndiyo rai iliyokubaliwa.
Fataawaa Mas-ala 60 Kuhusu Hedhi Na Nifaas
39-Ni Upi Muda Wa Mwisho Wa Swalaah Ya ‘Ishaa Na Vipi Kuujua
Imaam Ibn 'Uthaymiyn (Rahimahu-Allaah)
Alhidaaya.com [3]
SWALI:
Ni upi muda wa mwisho wa Swalaah ya ‘Ishaa, na vipi kuujua muda wenyewe?
JIBU:
Mwisho wa wakati wa ‘Ishaa ni katikati ya usiku na wakati wenyewe unaweza kuujua kwa kuugawa kati ya muda wa Magharibi na muda wa Swalaah ya Alfajiri. Nusu ya kwanza inaisha wakati wa Swalaah ya ‘Ishaa. Na nusu ya pili inayobaki haikadiriwi kwa wakati bali kwa kitenganisho baina ya ‘Ishaa na Alfajiri.
Fataawaa Mas-ala 60 Kuhusu Hedhi Na Nifaas
40-Anayetokwa Majimaji Akatawadha Yakakatika Kisha Yakarudia Afanyeje?
Imaam Ibn 'Uthaymiyn (Rahimahu-Allaah)
Alhidaaya.com [3]
SWALI:
Mwenye kutoka na majimaji haya akitawadha hali ya kuwa yamekatika na baada ya kumaliza wudhu wake na kabla ya Swalaah yake ikateremka tena, je afanye nini?
JIBU:
Ikiwa ni yenye kukatikakatika basi na asuburi hadi yatakapokatika. Ama ikiwa hali yenyewe haipo wazi yaani muda inateremka na muda inaacha. Basi huyu anatakiwa atawadhe ule muda tu wa kuingia Swalaah.
Fataawaa Mas-ala 60 Kuhusu Hedhi Na Nifaas
41-Majimaji Yanayomtoka Mwanamke Anapaswa Afanyeje?
Imaam Ibn 'Uthaymiyn (Rahimahu-Allaah)
Alhidaaya.com [3]
SWALI:
Nini kinacholazimu pindi kiwiliwili au inapopatwa na majimaji hayo?
JIBU:
Akiwa ni tohara haimlazimu chochote, na ikiwa ni najisi ambayo inatoka katika kinena basi ni wajibu wake kusafisha.
Fataawaa Mas-ala 60 Kuhusu Hedhi Na Nifaas
42-Anapotokwa Na Majimaji Je Inatosha Aoshe Viungo Vya Wudhuu Pekee?
Imaam Ibn 'Uthaymiyn (Rahimahu-Allaah)
Alhidaaya.com [3]
SWALI:
Kuhusuana na udhu wa majimaji hayo je itatosheleza kukosha viungo vya udhu tu?
JIBU:
Naam, itatosheleza hilo pindi ikiwa ni tohara nayo ni ambayo inatoka kwenye nyumba ya kizazi na sio kwenye kinena.
Fataawaa Mas-ala 60 Kuhusu Hedhi Na Nifaas
43-Kuna Hadiyth Kuhusu Kutokwa Majimaji?
Imaam Ibn 'Uthaymiyn (Rahimahu-Allaah)
Alhidaaya.com [3]
SWALI:
Ni kwa nini haikunukuliwa kutoka kwa Nabiy Hadiyth inayothibitisha kutenguka kwa uwdhu kutokana na majimaji yale pamoja na kuwa Maswahaba walikuwa wakijali mno kutoa fatwa katika mambo ya Sini yao?
JIBU:
Ni kwa kuwa majimaji haya hayamtoki kila mwanamke.
Fataawaa Mas-ala 60 Kuhusu Hedhi Na Nifaas
44-Wanawake Wasiojua Kutawadha Nini Hukmu Yake
Imaam Ibn 'Uthaymiyn (Rahimahu-Allaah)
Alhidaaya.com [3]
SWALI:
Nini hukumu ya kutokujua hukumu ya kutawadha kwa baadhi ya wanawake?
JIBU:
Ni kutubia kwa Allaah na kuwauliza wenye elimu ya hilo.
Fataawaa Mas-ala 60 Kuhusu Hedhi Na Nifaas
45-Hawapaswi Kutawadha Kutokana Na Majimaji Yanayomtoka?
Imaam Ibn 'Uthaymiyn (Rahimahu-Allaah)
Alhidaaya.com [3]
SWALI:
Kuna wanaonasibisha kauli kwako kuwa hawapaswi kutawadha kutokana na majimaji yale (yanayomtoka mwanamke)?
JIBU:
Mwenye kunasibisha kauli hii kwangu hakusema kweli, (bali anapaswa kutawadha) kwani kilicho wazi ni kuwa amefahamu kutoka katika kauli yangu ni kuwa ni tohara hayatengui wudhuu (ikiwa ni majimaji yanayoendelea kutoka; Rejea Swali namba 35).
Fataawaa Mas-ala 60 Kuhusu Hedhi Na Nifaas
46-Yanayomtoka Kabla Ya Hedhi Kama Uzi Wa Rangi Nyeusi Au Buni
Imaam Ibn 'Uthaymiyn (Rahimahu-Allaah)
Alhidaaya.com [3]
SWALI:
Ni nini hukumu ya majimaji yale machafu (yanayoelekea kwenye wekundu au wanavyosema Fuqahaa maji yaliyochanganyika na udongo) yanayotoka kwa mwanamke kabla ya hedhi kwa siku au zaidi au chini ya hapo. Inaweza kuwa inateremka kwa njia ya uzi uzi mweusi au rangu ya buni mwembamba?
JIBU:
Hii ikiwa ni miongoni mwa vitangulizi vya hedhi basi hiyo ni sehemu ya hedhi na hilo huambatana na maumivu na tumbo kukatika katika na baada ya hapo ada yake inaanza. Ama yale majimaji machafu (yanayoelekea kwenye wekundu au wanavyosema Fuqahaa maji yaliyochanganyika na udongo) yanayotoka baada ya hedhi hiyo itasubiriwa hadi itakapoteremka; kwani majimaji hayo yaliyoambatana na hedhi ni hedhi kwa kauli ya ‘Aaishah (Radhwiya-Allaahu ‘anhaa):
لا تعجلن حتى ترين القصة البيضاء
“Wala usifanye haraka hadi utakapoona majimaji meupe.”
Allaah Ndiye mjuzi zaidi
Fataawaa Mas-ala 60 Kuhusu Hedhi Na Nifaas
47-Ihraam Haina Swalaah Na Hukmu Ya Mwenye Hedhi Kusoma Qur-aan
Imaam Ibn 'Uthaymiyn (Rahimahu-Allaah)
Alhidaaya.com [3]
SWALI:
Mwenye hedhi ataswali vipi rakaa mbili za Ihraam? Na je yampasa mwanamke mwenye hedhi kusomasoma Aayah katika hali ya siri (moyoni)?
JIBU:
Kwanza kabisa yapasa kujua kuwa Ihraam haina Swalaah, hivyo haikupokewa kutoka kwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kuwa amelazimisha kwa umma wake Swalaah ya Ihraam wala hakuonesha kwa matendo yake au kukiri.
Pili: Kuwa mwanamke huyu mwenye hedhi ambaye amekuwa na hedhi kabla ya kuhirimia anaweza kuhirimia akiwa ni mwenye hedhi kwani Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alimuamrisha Asmaa bint ‘Umays mke wa Abuu Bakar alipokuwa na nifaas katika Dhul-Hulayfah ni kuwa akoge na azungushe nguo na ahirimie. Vivyo hivyo kwa mwenye hedhi na ataendelea kubaki kwenye ihraam yake hadi atoharike, kisha baada ya hapo atatufu na kufanya Sa’yi.
Ama kauli yake katika swali: Je yafaa kwake kusoma Qur-aan? Naam, mwenye hedhi ana haki kusoma Qur-aan atakapokuwa na haja ya kufanya hivyo au maslahi fulani. Ama kama hakuna haja au maslahi fulani kusoma kwake kama ni kwa ajili ya kuabudu na kujikurubisha na Allaah ni bora asifanye hivyo.
Fataawaa Mas-ala 60 Kuhusu Hedhi Na Nifaas
48-Imemtokea Hedhi Akiwa Katika Twawaaf
Amekamilisha Kwa Ajili Ya Kusitahi Akarudi Nchini Kwake
Imaam Ibn 'Uthaymiyn (Rahimahu-Allaah)
Alhidaaya.com [3]
SWALI:
Mwanamke amesafiri kwenda Hajj ikamjia ada yake ya mwezi siku tano tokea aanze safari yake na baada ya kufika kwake Miyqaat alikoga na kuingia katika ihraam yake hali ya kua hajatwaharika na ada yake. Pindi alipofika Makkah alibaki nje ya Haram (Masjid Al-Haraam) na hakufanya chochote kwenye ‘ibaadah ya Hajj wala ya ‘Umrah. Alikaa siku mbili Minaa kisha akatoharika na kukoga na kufanya ‘ibaadah zote za ‘Umrah akiwa ametoharika kisha damu ikamrejea akiwa katika Twawaaf Al-Ifaadhwah ya Hajj. Akaendelea kwa sababu alistahi (kusema) hivyo akakamilisha ‘ibaadah zote za Hajj bila kumwambia kiongozi wake isipokuwa alimjulisha hayo baada ya kurudi nchini mwao nini hukumu yake?
JIBU:
Hukumu yake ilikuwa damu iliyomtokea katika Twawaaf Al-Ifaadhwah ikiwa damu hiyo ya hedhi ambayo unaijua kwa tabia yake na maumivu yake basi Twawaaf Al-Ifaadhwah itakuwa haijaswihi na itamlazimu kurudi Makkah kufanya Twawaaf Al-Ifaadhwah na atahirimia kwa ajili ya ‘Umrah katika Miyqaat na kufanya ‘Umrah kwa kutufu na kufanya Sa’y na kupunguza nywele kisha hapo atafanya Twawaaf Al-Ifaadhwah. Ama damu hii ikiwa siyo ya hedhi kwa wasifu ule tuliyoutaja mwanzoni (tabia yake na maumivu yake, rangi na kadhaalika) basi itakuwa ima imetokea kwa ajili ya msongamano au wasiwasi, khofu au unao fanana na hiyo, basi Twawaaf yake inaswihi kwa yule ambaye hashurutishwi kufanya tohara kwa ajili ya Twawaaf. Na kama hawezi kurudi kama tulivyozungumza awali kwa sababu anakaa nchi ya mbali basi Hijjah yake inaswihi.
Fataawaa Mas-ala 60 Kuhusu Hedhi Na Nifaas
49-Amehirimia ‘Umrah Akapatwa Hedhi Na Mahram Wake Ilibidi Asafari
Imaam Ibn 'Uthaymiyn (Rahimahu-Allaah)
Alhidaaya.com [3]
SWALI:
Mwanamke alipohirimia ‘Umrah alipofika Makkah akapatwa na hedhi na mahram wake akatakiwa asafiri haraka na hana mtu mwengine Makkah ni nini hukumu yake?
JIBU:
Anatakiwa asafiri naye akiwa pamoja na ihraam yake kisha atarejea akitwaharika ikiwa mtu huyu anaishi Saudi Arabia kwani kurudi kwake kutakua wepesi kwa sababu hahitajii passport au mfano wake. Ama akiwa ni mgeni na kurudi kwake ni kwa taabu basi itabidi atufu na kufanya Sa’y na kupunguza nywele na kumaliza ‘Umrah yake katika safari hiyo hiyo ya awali, kwani Twawaaf yake wakati huo itakuwa ni jambo la dharura na dharura huhalalisha yaliyokatazwa.
Fataawaa Mas-ala 60 Kuhusu Hedhi Na Nifaas
50-Hijjah Ya Mwenye Hedhi Inakubalika?
Imaam Ibn 'Uthaymiyn (Rahimahu-Allaah)
Alhidaaya.com [3]
SWALI:
Nini hukumu ya mwanamke ambaye amekuwa na hedhi katika siku za Hajj je, Hijjah ile itakubaliwa?
JIBU:
Hili haliwezekani kujibiwa hadi ijulikane ni wakati gani alipatwa na hedhi na hilo ni kwa sababu baadhi ya matendo ya hija Hajj hayamkatai zmwenye hedhi na mengine yanamkataza mwenye hedhi. Kwa mfano Twawaaf hawezi kuifanya mwenye hedhi ila isipokuwa akiwa ni mwenye tohara. Ama matendo mengine yanawezekana kwa mwenye hedhi.
Fataawaa Mas-ala 60 Kuhusu Hedhi Na Nifaas
51-Ametekeleza ‘Ibaadah Zote Za Hajj Isipokuwa Twawaaf Al-Ifaadhwah
Na Al-Widaa’ Akarudi Nyumbani Akajivua Katika Ihraam
Imaam Ibn 'Uthaymiyn (Rahimahu-Allaah)
Alhidaaya.com [3]
SWALI:
Muulizaji anauliza: Nilitekeleza ‘Ibaadah ya Hajj mwaka uliopita na nikatekeleza ‘ibaadah zote za Hijjah isipokuwa Twawaaf Al-Ifaadhwah na Twawaaf Al-Widaa’ na kilichonizuia ni udhuru wa ki-Shariy’ah na hivyo nikarejea nyumbani kwangu Madinah Al-Munawwarah ili baadae nirejee siku nyingine na nipate kufanya Twawaaf Al-Ifaadhwah na Twawaaf Al-Widaa’. Isipokuwa sijui baadhi ya mambo ya dini hivyo nilitahallal (kujivua Ihraam) na nikaacha kila kitu chenye kukatazwa wakati wa Ihraam na nikauliza kuhusu kurudi kwangu ili nifanye Twawaaf, nikaambiwa kuwa haisihi kwangu kutufu kwani nilishaharibu kila kitu na natakiwa nihiji tena kwa mara nyingine mwakani pamoja na kuchinja ng’ombe au ngamia. Je hii ni sahihi? Je kuna utatuzi mwingine zaidi ya huu? Ni kweli Hijjah yangu imeharibika? Na juu yangu kurejea upya? Nijulisheni ninachoweza kukifanya Baaraka Allaahu Fiykum.
JIBU:
Hili nalo ni balaa lingine kutoa Fatwa pasina kuwa na elimu. Katika hali yako hii inabidi urudi tena Makka na ufanye Twaaf Al-Ifaadhwah peke yake. Ama Twawaaf Al-Widaa’ sio juu yako kwani madamu ulikuwa na hedhi ulipokuwa unatoka Makkah na hilo ni kwa sababu mwenye hedhi haiwi lazima kwako Twawaaf Al-Widaa’ kwa Hadiyth ya Ibn ‘Abaas (Radhwiya-Allaahu ‘anhumaa): “Watu wameamrishwa ahadi yao katika nyumba isipokuwa imewepesishwa kwa mwenye hedhi.” Katika riwaya ya Abuu Daawuwd “Ili ahadi yao ya mwisho na kutufu nyumba.”
Kwa sababu Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alipoambiwa kuwa Swafiyyah ametufu Twawaaf Al-Ifaadhwah alisema, “Basi na achukie au aache basi.” Na imetoa dalili hili kuwa Twawaaf Al-Widaa’ huanguka kwa mwenye hedhi. Ama Twawaaf Al-Ifaadhwah huna budi nayo. Na kwa sababu ulishatahallal (uliondoka kwenye ihraam) kwa kila kitu ukiwa hufahamu basi hili halitokudhuru kitu katika yaliyokatazwa kwa aliyehirimia hakuna kitu juu yake kwa kauli yake Ta’aala:
رَبَّنَا لاَ تُؤَاخِذْنَا إِن نَّسِينَا أَوْ أَخْطَأْنَا
“Rabb wetu Usituchukulie tukisahau au tukikosea. [Al-Baqarah:286]
Na kauli Yake Ta’alaa vile vile:
وَلَيْسَ عَلَيْكُمْ جُنَاحٌ فِيمَا أَخْطَأْتُم بِهِ وَلَـٰكِن مَّا تَعَمَّدَتْ قُلُوبُكُمْ
Na walio katika ulinzi wenu, na wala hakuna dhambi juu yenu katika yale mliyoyakosea, lakini isipokuwa katika yale yaliyoyakusudia nyoyo zenu. [Al-Ahzaab : 5]
Hivyo makatazo yote ambayo Allsah Amekataza kwa aliyehirimia akifanya asiyefahamu au mtu aliyesahau au kulazimishwa hana kitu juu yake, lakini muda wowote utakapoondoka udhuru wake basi inampasa aache lililomchanganya.
Fataawaa Mas-ala 60 Kuhusu Hedhi Na Nifaas
51-Alikuwa Katika Nifaas Akatekeleza Nguzo Zote Isipokuwa Twawaaf Na Sa’y
Akahisi Ametoharika Akamilishe Twawaaf Al-Ifaadhwah?
Imaam Ibn 'Uthaymiyn (Rahimahu-Allaah)
Alhidaaya.com [3]
SWALI:
Mwanamke mwenye nifaas atakapoanza nifaas yake siku ya Tarwiyah na kukamilisha nguzo za Hajj isipokuwa Twawaaf na Sa’y ila akaona kuwa ‘kuna ishara za awali’ kuwa ametoharika baada ya kupita siku kumi. Je, atajitoharisha na na kuoga na kukamilisha nguzo iliyobakia ambayo ni Twawaaf Ya Hajj?
JIBU:
Hapana haijuzu kwake kukoga na kutufu hadi ahakikishe kwa yakini kabisa tohara yake. Kinachofahamika katika swali hili hapa ni kuwa ‘kuna ishara za awali’ ni kuwa bado hajaona utohara kwa ukamilifu wake, hivyo hapana budi kwanza aone tohara kwa ukamilifu wake na muda wa kuwa atakuwa ametoharika basi na akoge na atekeleze Twawaaf na Sa’yi. Akipata wasaa kabla ya Twawaaf basi hamna neno; kwa sababu Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) aliulizwa kuhusu Hijjah kwa Yule aliyefanya Sa’y kabla ya kutufu akasema: “Si vibaya.”
Fataawaa Mas-ala 60 Kuhusu Hedhi Na Nifaas
53-Amehirimia Hajj As-Sayl Akaenda Jeddah Akatoharika Huko
Akatekeleza Hajj Je Hajj Yake Sahihi?
Imaam Ibn 'Uthaymiyn (Rahimahu-Allaah)
Alhidaaya.com [3]
SWALI:
Mwanamke amehirimia Hajj kutokea (Miyqaat ya) As-Sayl nae akiwa ni mwenye hedhi na pindi alipofika Makkah alikwenda Jeddah kwa kwa haja zake na akapata tohara huko Jeddah na kuoga na kuchana nywele zake kisha akatimiza Hijjah yake je, Hijjah yake ni sahihi je itamuhitajia kitu?
JIBU:
Hijjah yake ni sahihi na haihitajii lolote baada ya hapo.
Fataawaa Mas-ala 60 Kuhusu Hedhi Na Nifaas
54-Alikuwa Na Hedhi Hakuhirimia Miyqaat Bali Ameharimia Makkah Je Inajuzu?
Imaam Ibn 'Uthaymiyn (Rahimahu-Allaah)
Alhidaaya.com [3]
SWALI:
Muulizaji anauliza: Mimi nakwenda ‘Umrah na nikapitia Miyiqaat nami nikiwa ni mwenye hedhi, hivyo sikuhirimia na nikabakia Makkah hadi nilipotoharika hivyo nikahirimia Makkah je hili linajuzu? Au nifanye nini au yanipasa nini?
JIBU:
Jambo hili halifai, mwanamke ambaye anataka kufanya ‘Umrah haimpasi kuwa karibu na Miyqaat isipokuwa ni baada ya kuhirimia hata kama akiwa ni mwenye hedhi. Dalili ya hilo ni kuwa Asmaa bint Khumays ambaye ni mke wa Abuu Bakr (Radhwiya-Allaahu ‘anhumaa) alizaa wakati huo Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akiwa Dhul-Hulayfa akikusudia kufanya Hajj Al-Wadaa’i hivyo Asmaa bint Khumays akatuma mjumbe kwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akiuliza afanye nini? Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akasema:
اغتسلي واستثفري بثوب وأحرمي
“Koga (ghuslu) na jifunge kwa nguo na uhirimie.”
Damu ya hedhi ni kama damu ya nifaas, hivyo mwanamke mwenye hedhi atasema kuwa akipita Miyqaad akiwa anakusudia kufanya ‘Umrah au kufanya Hajj, tunamwambia, Koga (ghuslu) na jifunge kwa nguo na uhirimie. Maana yake atafunga vizuri sehemu zake za siri kwa nguo na kufunga vizuri kisha atahirimia iwe ni kwa ajili ya Hajj au kwa ajili ya ‘Umrah lakini akihirimia na akafika Makkah haendi kwenye Nyumba (Al-Ka’bah) au kutufu hadi atoharike na kwa hilo Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema alipomwambia Mama ‘Aaishah alipokuwa na hedhi wakati wa ‘Umrah:
افعلي ما يفعل الحاج غير أن لا تطوفي في البيت حتى تطهري
“Fanya yote ayafanyayo hujaji isipokuwa usitufu katika nyumba hadi utoharike.” Hii ni riwaayah ya Al-Bukhariy na Muslim.
Katika Swahiyh Al-Bukhariy imetajwa kuwa alipotoharika Mama ‘Aaishah alitufu nyumba na akafanya Sa’yi kati ya Swafaa na Marwah na hii ikawa ni dalili kuwa mwanamke akihirimia Hajj au ‘Umrah ilhali ana hedhi au ikamjia hedhi kabla ya kutufu basi hatoweza kutufu wala hatofanya Sa’yi hadi atoharike na akoge. Ama lau akitufu nae akiwa ni mwenye tohara na baada ya kukamilisha Twawaaf ikamjia hedhi basi ataendelea na kufanya Sa’yi na hata akiwa ni mwenye hedhi na atapunguza nywele zake na hivyo atamaliza ‘Umrah yake kwa sababu Sa’yi kati ya Swafaa na Marwah haishurutishi tohara.
Fataawaa Mas-ala 60 Kuhusu Hedhi Na Nifaas
55-Ametoka Mji Mmoja Kukusudia ‘Umrah Mkewe Alikuwa Katika Hedhi
Akakamilisha ‘Umrah Bila Mkewe
Imaam Ibn 'Uthaymiyn (Rahimahu-Allaah)
Alhidaaya.com [3]
SWALI:
Muulizaji anauliza: Nimetokea Yanbu’ kwenda kwenye ‘Umrah mimi pamoja na familia yangu lakini nilipofika Jeddah mke wangu akaingia kwenye ada yake ya mwezi ama mimi nilikamilisha ‘Umrah peke yangu bila ya mke wangu, ni ipi hukumu inayomhusu mke wangu?
JIBU:
Hukumu inayomhusu mke wako ni kuwa abakie hadi atoharike kisha alipe ‘Umrah yake, kwa sababu wakati Mama wa Waumini Swafiyyah alipopatwa na hedhi Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alisema: “Yeye ametuzuia.” Wakasema kuwa Swafiyyah ameshafanya Twawaaf Al-Ifaadhwah. Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akasema: “Basi ajifunge funge.” Hivyo basi kauli yake Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) “Yeye ametuzuia.” Ni dalili ya kuwa ni waajbi kwa mwanamke kubaki akiwa na hedhi kabla ya kufanya Twawaaf Al-Ifaadhwah hadi atoharike kisha atufu na kadhalika Twawaaf ya ‘Umrah mfano wake ni Twawaaf Al-Ifaadhwah kwa sababu ni nguzo katika ‘Umrah. Hivyo basi akiwa na hedhi aliyekwenda kufanya ‘Umrah kabla ya Twawaaf atasubiri hadi atoharike kisha atatufu.
Fataawaa Mas-ala 60 Kuhusu Hedhi Na Nifaas
56-Swafaa Na Marwah Na Hukmu Ya Mwenye Hedhi Na Hukmu Ya Tahiyyatul-Masjid
Imaam Ibn 'Uthaymiyn (Rahimahu-Allaah)
Alhidaaya.com [3]
SWALI:
Je, Al-Mas’aa (sehemu ya Swafaa na Marwah) ni katika Msikiti (Al-Haram)? Je, mwenye hedhi anaruhisiwa kuikurubia? Na je anayeingia Msikitini kupitia eneo la Mas’aa aswali Tahiyyatul-Masjid? (Rakaa za kuamkia Msikiti)
JIBU:
Kinachodhihiri ni kuwa Al-Mas’aa sio katika Msikiti na ndio maana ikawekwa ukuta unaotenganisha lakini ni ukuta mfupi na hapana shaka kuwa hili ni jambo la kheri kwa watu, na lau ingeingia au kuingizwa Msikitini na kufanywa sehemu ya Msikiti basi ingekuwa mwanamke akipatwa na hedhi katikati ya Twawaaf na Sa’yi basi atazuiwa kufanya Sa’yi na lile ambalo nalifutu hapa ni kuwa mwanamke akipata hedhi baada ya Twawaaf na kabla ya kufanya Sa’yi huyo atafanya Sa’yi kwa sababu Al-Mas’aa haizingatiwi kuwa ni Msikiti.
Ama Tahiyyatul-Masjid inaweza kusemwa: Kuwa mtu akifanya Sa’yi kati ya Swafaa na Marwah baada ya Twawaaf kisha akarejea Msikitini basi ataiswali lau hata akiacha Tahiyyatul-Masjid si neno juu yake na bora zaidi atumie fursa hiyo kuswali rakaa mbili kwani kuswali sehemu hii ni bora zaidi.
Fataawaa Mas-ala 60 Kuhusu Hedhi Na Nifaas
57-Baada Ya Kuhiji Amepata Hedhi Akaona Hayaa
Akaswali Na Kutufu Al-Ka’bah Na Kutekeleza Sa’yi
Imaam Ibn 'Uthaymiyn (Rahimahu-Allaah)
Alhidaaya.com [3]
SWALI:
Anauliza muulizaji: Nilikuwa nimeshahiji ikanijia ada yangu ya mwezi nikaona haya kumwambia mtu nikaingia Al-Haram (Msikitii wa Makkah) nikaswali na kutufu na kufanya Sa’yi. Nifanye nini baada ya hapo na suala hili limenijia baada ya nifaas?
JIBU:
Haiwi halaal kwa mwanamke akiwa ni mwenye hedhi au mwenye nifaas kuswali iwe ni Makkah au katika mji wake au sehemu yoyote ile kwa kauli ya Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kwa mwanamke:
أليس إذا حاضت لم تصل ولم تصم
“Si unajua kuwa mwanamke akiwa na hedhi haswali wala hafungi.”
Na Waislamu wamekubaliana katika ‘Ijmaa kuwa si halaal kwa mwenye hedhi kufunga, wala haiwi halaal kwake kuswali. Na kwa ajili hii mwanamke ambaye amefanya hivyo juu yake ni kutubia kwa Allaah na kuomba maghfirah kwa yaliyotokea.
Ama kuhusu Twawaaf yake akiwa katika hali ya hedhi sio sahihi. Ama Sa’yi yake ni sahihi. Kwa sababu kauli inayokubalika ni kuruhusiwa kutanguliza Sa’yi kuliko Twawaaf katika Hajj, na kwa hili inampasa kwake arejee kufanya Twawaaf; kwa kuwa Twawaaf Al-Ifaadhwah ni nguzo katika nguzo za Hajj. Wala haitimii kutahallal (kujivua katika ihraam) ya pili isipokuwa kwayo na kwa ajili ya hilo, mwanamke huyu hawezi kuingiliwa na mumuwe akiwa ameolewa hadi afanye Twawaaf, wala haolewi akiwa bado hajaolewa hadi afanye Twawaaf. Na Allaah Mjuzi zaidi
Fataawaa Mas-ala 60 Kuhusu Hedhi Na Nifaas
58-Mwenye Hedhi Siku Ya ‘Arafah Afanye Nini?
Imaam Ibn 'Uthaymiyn (Rahimahu-Allaah)
Alhidaaya.com [3]
SWALI:
Mwanamke akiwa na hedhi siku ya ‘Arafah afanye nini?
JIBU:
Mwanamke akiwa na hedhi siku ya ‘Arafah basi ataendelea na Hijjah yake na kufanya wanaofanya watu wala haruhusiwi kutufu katika Nyumba (Al-K’abah) hadi atoharike.
Fataawaa Mas-ala 60 Kuhusu Hedhi Na Nifaas
59-Akiwa Katika Hedhi Baada Ya Jamarah Kabla Ya
Twawaaf Al-Ifaadhwah Na Hawezi Kurudi Baada Ya Safari
Imaam Ibn 'Uthaymiyn (Rahimahu-Allaah)
Alhidaaya.com [3]
SWALI:
Mwanamke akiwa na hedhi baada ya Jamarah (Kurushwa vijiwe) katika Al-‘Aqabah na kabla ya Twawaaf Al-Ifaadhwah, nae akiwa katika kundi pamoja na mumewe na marafiki wake, juu yake ni nini afanye pamoja na elimu ya kuwa hawezi kurejea baada ya safari yake?
JIBU:
Kama hawezi kurudi basi atajihifadhi vizuri kisha atatufu kwa hali ya dharura wala isiwe kitu juu yake, na kukamilisha baki ya ‘ibaadah za matendo ya Hijjah.
Fataawaa Mas-ala 60 Kuhusu Hedhi Na Nifaas
60-Mwenye Nifaas Akitoharika Nifaas Kabla Ya Siku Arubaini Hijjah Yake Sahihi?
Na Kama Hakupata Utohara?
Imaam Ibn 'Uthaymiyn (Rahimahu-Allaah)
Alhidaaya.com [3]
SWALI:
Mwenye nifaas akitoharika kabla ya siku arubaini je Hijjah yake inasihi? Na kama hakuona tohara basi afanye nini pamoja na elimu kuwa amenuia Hajj?
JIBU:
Akitoharika mwenye nifaas kabla ya arubaini basi atakoga (ghuslu) na kuswali na kufanya yale ayafanyayo waliokuwa na tohara hadi Twawaaf kwani nifaas haina ukomo wa uchache wake.
Ama kama hakuona tohara basi Hijjah yake ni sahihi vile vile lakini hatotufu katika Nyumba (Al-Ka’bah) hadi apate tohara kwani Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amemkataza mwenye hedhi kutufu Nyumba na nifaas ni kama vile mwenye hedhi.
Links
[1] https://www.alhidaaya.com/sw/taxonomy/term/206
[2] http://www.alhidaaya.com/sw/node/10069
[3] http://www.alhidaaya.com/sw/
[4] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F10069&title=Imaam%20Ibn%20%27Uthaymiyn%3A%20Fataawaa%3A%20Mas-ala%2060%20Kuhusu%20Hedhi%20Na%20Nifaas%20
[5] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F10070&title=01-Imaam%20Ibn%20%27Uthaymiyn%3A%20Mwanamke%20Akitoharika%20Baada%20Ya%20Kuingia%20Alfajiri%20Afunge%20Au%20Itabidi%20Alipe%20Swawm%3F%20
[6] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F10071&title=02-Imaam%20Ibn%20%27Uthaymiyn%3A%20Mwenye%20Hedhi%20Akitoharika%20Kabla%20Ya%20Alfajiri%20Lakini%20Akaoga%20Baada%20Ya%20Swalaah%20Swawm%20Yake%20Sahihi%3F
[7] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F10072&title=03-Imaam%20Ibn%20%27Uthaymiyn%3A%20Akitoharika%20Nifaas%20Kabla%20Ya%20Siku%20Arubaini%20Je%20Aswali%20Na%20Afunge%3F
[8] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F10073&title=04-Imaam%20Ibn%20%27Uthaymiyn%3A%20Hedhi%20Yenye%20Kawaida%20Ya%20Siku%20Sita%20Au%20Saba%20Kisha%20Ikaendelea%20Siku%20Chache
[9] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F10074&title=05-Imaam%20Ibn%20%27Uthaymiyn%3A%20Damu%20Ya%20Nifaas%20Lazima%20Ifikie%20Siku%20Arubaini%20Au%20Ikikatika%20Ametoharika%3F
[10] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F10075&title=06-Imaam%20Ibn%20%27Uthaymiyn%3A%20Damu%20Inayotoka%20Puani%20Inabatilisha%20Swawm%3F
[11] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F10076&title=07-Imaam%20Ibn%20%27Uthaymiyn%3A%20Akitoharika%20Nifaas%20Au%20Hedhi%20Kabla%20Ya%20Alfajiri%20Lakini%20Akajitoharisha%20%28Ghuslu%29%20Baada%20Ya%20Alfajiri%20Swawm%20Yake%20Itasihi%3F
[12] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F10077&title=08-Imaam%20Ibn%20%27Uthaymiyn%3A%20Akihisi%20Damu%20Au%20Maumivu%20Ya%20Hedhi%20Lakini%20Haikutoka%20Kabla%20Ya%20Magharibi%20Je%2C%20Swawm%20Itasihi%3F
[13] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F10078&title=09-Imaam%20Ibn%20%27Uthaymiyn%3A%20Akiona%20Damu%20Isiyothibitika%20Kuwa%20Ni%20Hedhi%20Nini%20Hukmu%20Ya%20Swawm%20Yake%3F
[14] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F10079&title=10-Imaam%20Ibn%20%27Uthaymiyn%3A%20Akipata%20Matone%20Ya%20Damu%20Usiku%20Ambayo%20Mara%20Huwa%20Ni%20Hedhi%20Na%20Mara%20Si%20Hedhi%20Nini%20Hukmu%20Ya%20Swawm%3F
[15] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F10080&title=11-Imaam%20Ibn%20%27Uthaymiyn%3A%20Wenye%20Hedhi%20Na%20Nifaas%20Wanaruhusiwa%20Kula%20Mchana%20Wa%20Ramadhwaan
[16] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F10081&title=12-Imaam%20Ibn%20%27Uthaymiyn%3A%20Mwenye%20Hedhi%20Au%20Nifaas%20Akitoharika%20Alasiri%20Je%20Anawajibika%20Kuswali%20Swalaah%20Ya%20Adhuhuri%20Na%20Alasiri%3F
[17] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F10082&title=13-Imaam%20Ibn%20%27Uthaymiyn%3A%20Mimba%20Ikitoka%20Kabla%20Ya%20Kuumbika%20Kichanga%20Na%20Baada%20Ya%20Kuumbika%20Nini%20Hukmu%20Ya%20Swawm%3F
[18] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F10083&title=14-Imaam%20Ibn%20%27Uthaymiyn%3A%20Kutoka%20Damu%20Kwa%20Mwenye%20Mimba%20Mchana%20Wa%20Ramadhwaan%20Inaathiri%20Swawm%20Yake%3F
[19] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F10084&title=15-Imaam%20Ibn%20%27Uthaymiyn%3A%20Akipata%20Damu%20Siku%20Moja%20Lakini%20Ya%20Pili%20Yake%20Hakuona%20Damu%20Afanyeje%3F
[20] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F10096&title=16-Imaam%20Ibn%20%27Uthaymiyn%3A%20Alipomalizia%20Hedhi%20Kabla%20Ya%20Adhuhuri%20Hakuona%20Damu%20Je%20Afunge%20Siku%20Hiyo%3F
[21] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F10097&title=17-Imaam%20Ibn%20%27Uthaymiyn%3A%20Kusoma%20Na%20Kuhifadhi%20Qur-aan%20Kwa%20Mwenye%20Hedhi%20Au%20Nifaas%20Akiangalia%20Mswahafuni%20
[22] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F10098&title=18-Imaam%20Ibn%20%27Uthaymiyn%3A%20Anawajibika%20Kubadilisha%20Nguo%20Baada%20Ya%20Kumaliza%20Hedhi%20Japokuwa%20Hazikuingia%20Damu%3F%20
[23] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F10099&title=19-Imaam%20Ibn%20%27Uthaymiyn%3A%20Hakuweza%20Kulipa%20Deni%20La%20Swiyaam%20Mpaka%20Imefikia%20Ramadhwaan%20Ya%20Tatu%20Kwa%20Sababu%20Ya%20%20Uzazi%20Kunyonyesha%20Na%20Ugonjwa%20Afanyeje%3F
[24] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F10100&title=20-Imaam%20Ibn%20%27Uthaymiyn%3A%20Kuchelewa%20Kulipa%20Deni%20La%20Swiyaam%20Za%20Ramadhwaan
[25] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F10116&title=21-Imaam%20Ibn%20%27Uthaymiyn%3A%20Alikuwa%20Na%20Hedhi%20Saa%20Saba%20Mchana%20Na%20Hakuswali%20Adhuhuri%20Je%20Alipe%20Swalaah%20Hiyo%3F
[26] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F10117&title=22-Imaam%20Ibn%20%27Uthaymiyn%3A%20Akiona%20Damu%20Kabla%20Ya%20Kuzaa%20Siku%20Moja%20Au%20Mbili%20Je%20Aache%20Swawm%20Na%20Swalaah%3F%20%20
[27] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F10118&title=23-imaam%20Ibn%20%27Uthaymiyn%3A%20Kutumia%20Vidonge%20Kuzuia%20Hedhi%20Ili%20Aweze%20Swiyaam%20Inafaa
[28] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F10119&title=24-Imaam%20Ibn%20%27Uthaymiyn%3A%20Baada%20Ya%20Miezi%20Miwili%20Ya%20Nifaas%20%20Akatoharika%20Ameona%20%20Matone%20Ya%20Damu%20Aache%20Swalaah%20Na%20Swiyaam
[29] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F10120&title=25-Imaam%20Ibn%20%27Uthaymiyn%3A%20Damu%20Inaendelea%20Na%20Inakatika%20Siku%20Moja%20Au%20Mbili%20Kisha%20Inarudi%20%20%20
[30] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F10125&title=26-Imaam%20Ibn%20%27Uthaymiyn%3A%20Wanawake%20Bora%20Kuswali%20Nyumbani%20Au%20Miskitini%20Katika%20Nyusiku%20Za%20Ramadhwaan%20Kufaidika%20Na%20Mawaidha%3F
[31] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F10126&title=27-Imaam%20Ibn%20%27Uthaymiyn%3A%20Kuonja%20Chakula%20Mchana%20Wa%20Ramadhwaan%20Kwa%20Mwenye%20Swawm%20Inafaa%3F%20%20
[32] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F10127&title=28-Imaam%20Ibn%20%27Uthaymiyn%3A%20Mwanamke%20Kapata%20Ajali%20Akiwa%20Na%20Mimba%20Changa%20Akatokwa%20Damu%20Nyingi%20Je%20Afungulie%20Swawm
[33] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F10128&title=29-Imaam%20Ibn%20%27Uthaymiyn%3A%20Ameharibu%20Mimba%20%20Mwaka%20Jana%20Akiwa%20Na%20Miezi%20Mitatu%20Hakuswali%20Mpaka%20Alipotoharika%20Je%20Alipaswa%20Kuswali%20Na%20Kama%20Hakujua%20Idadi%20Ya%20Siku%20Afanyeje%3F
[34] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F10129&title=30-Imaam%20Ibn%20%27Uthaymiyn%3A%20Hakulipa%20Deni%20La%20Swiyaam%20Kwa%20Kutokujua%20Siku%20Alizofungulia%20%20Afanyeje%3F
[35] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F10130&title=31-Imaam%20Ibn%20%27Uthaymiyn%3A%20Akipata%20Hedhi%20Baada%20Ya%20Kuingia%20Wakati%20Wa%20Swalaah%20Au%20Akitoharika%20Kabla%20Ya%20%20Kutoka%20Wakati%20
[36] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F10131&title=32-Imaam%20Ibn%20%27Uthaymiyn%3A%20Amepata%20Hedhi%20Wakati%20Anaswali%20Afanyeje%20Na%20Je%20Alipe%20Swalaah%20Muda%20Wa%20Hedhi%3F%20%20
[37] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F10132&title=33-Imaam%20Ibn%20%27Uthaymiyn%3A%20Ana%20Umri%20Wa%20Sitini%20Na%20Tano%20Sasa%20Anapata%20Damu%20Inayoendelea%20Miaka%20Mitatu%20Nini%20Hukmu%20Ya%20Swawm%3F
[38] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F10133&title=34-Imaam%20Ibn%20%27Uthaymiyn%3A%20Mwenye%20Hedhi%20Kuweko%20Msikitini%20Kwa%20Ajili%20Ya%20Kusikiliza%20Hadiyth%20Na%20Khutbah%20
[39] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F10134&title=35-Imaam%20Ibn%20%27Uthaymiyn%3A%20Majimaji%20Yanayomtoka%20Mwanamke%20Mara%20Kwa%20Mara%20Ni%20Tohara%20Au%20Najisi%20%20Je%20Afanye%20Achukue%20Wudhuu%3F
[40] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F10143&title=36-Imaam%20Ibn%20%27Uthaymiyn%3A%20Mwanamke%20Anayetokwa%20Majimaji%20Anafaa%20Kusoma%20Qur-aan%20Na%20Kuswali%20Swalaah%20Za%20Sunnah%3F
[41] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F10144&title=37-Imaam%20Ibn%20%27Uthaymiyn%3A%20Mwanamke%20Anayetokwa%20Majimaji%20Je%2C%20Inajuzu%20Aswali%20Swalaah%20Ya%20Adhw-Dhwuhaa%20Kwa%20Wudhuu%20Wa%20Alfajiri%3F%20%20
[42] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F10145&title=38-Imaam%20Ibn%20%27Uthaymiyn%3A%20Anayetokwa%20Majimaji%20Je%20Inasihi%20Aswali%20Qiyaamul-Layl%20Kwa%20Wudhuu%20Wa%20%E2%80%98Ishaa%3F%20
[43] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F10146&title=39-Imaam%20Ibn%20%27Uthaymiyn%3A%20Ni%20Upi%20Muda%20Wa%20Mwisho%20Wa%20Swalaah%20Ya%20%E2%80%98Ishaa%20Na%20Vipi%20Kuujua
[44] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F10147&title=40-Imaam%20Ibn%20%27Uthaymiyn%3A%20Anayetokwa%20Majimaji%20Akatawadha%20Yakakatika%20Kisha%20Yakarudia%20Afanyeje%3F%20
[45] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F10162&title=41-Imaam%20Ibn%20%27Uthaymiyn%3A%20Majimaji%20Yanayomtoka%20Mwanamke%20Anapaswa%20Afanyeje%3F
[46] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F10163&title=42-Imaam%20Ibn%20%27Uthaymiyn%3A%20Anapotokwa%20Na%20Majimaji%20Je%20Inatosha%20Aoshe%20Viungo%20Vya%20Wudhuu%20Pekee%3F
[47] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F10164&title=43-Imaam%20Ibn%20%27Uthaymiyn%3A%20Kuna%20Hadiyth%20Kuhusu%20Kutokwa%20Majimaji%3F
[48] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F10165&title=44-Imaam%20Ibn%20%27Uthaymiyn%3A%20Wanawake%20Wasiojua%20Kutawadha%20Nini%20Hukmu%20Yake
[49] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F10172&title=45-Imaam%20Ibn%20%27Uthaymiyn%3A%20Hawapaswi%20Kutawadha%20Kutokana%20Na%20Majimaji%20Yanayomtoka
[50] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F10173&title=46-Imaam%20Ibn%20%27Uthaymiyn%3A%20Yanayomtoka%20Kabla%20Ya%20Hedhi%20Kama%20Uzi%20Wa%20Rangi%20Nyeusi%20Au%20Buni%20%20
[51] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F10174&title=47-Imaam%20Ibn%20%27Uthaymiyn%3A%20Ihraam%20Haina%20Swalaah%20Na%20Hukmu%20Ya%20Mwenye%20Hedhi%20Kusoma%20Qur-aan
[52] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F10175&title=48-Imaam%20Ibn%20%27Uthaymiyn%3A%20Imemtokea%20Hedhi%20Akiwa%20Katika%20Twawaaf%20Amekamilisha%20Kwa%20Ajili%20Ya%20Kusitahi%20Akarudi%20Nchini%20Kwake
[53] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F10176&title=49-Imaam%20Ibn%20%27Uthaymiyn%3A%20Amehirimia%20%E2%80%98Umrah%20Akapatwa%20Hedhi%20Na%20Mahram%20Wake%20Ilibidi%20Asafari%20
[54] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F10177&title=50-Imaam%20Ibn%20%27Uthaymiyn%3A%20Hijjah%20Ya%20Mwenye%20Hedhi%20Inakubalika
[55] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F10178&title=51-Imaam%20Ibn%20%27Uthaymiyn%3A%20Ametekeleza%20%E2%80%98Ibaadah%20Zote%20Za%20Hajj%20Isipokuwa%20Twawaaf%20Al-Ifaadhwah%20Na%20Al-Widaa%E2%80%99%20Akarudi%20Nyumbani%20Akajivua%20Katika%20Ihraam%20%20
[56] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F10179&title=52-Imaam%20Ibn%20%27Uthaymiyn%3A%20Alikuwa%20Katika%20Nifaas%20Akatekeleza%20Nguzo%20Zote%20Isipokuwa%20Twawaaf%20Na%20Sa%E2%80%99y%20%20Akahisi%20Ametoharika%20Akamilishe%20Twawaaf%20Al-Ifaadhwah%3F
[57] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F10190&title=53-Imaam%20Ibn%20%27Uthaymiyn%3A%20Amehirimia%20Hajj%20As-Sayl%20Akaenda%20Jeddah%20Akatoharika%20Huko%20Akatekeleza%20Hajj%20Je%20Hajj%20Yake%20Sahihi%3F%20%20
[58] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F10191&title=54-Imaam%20Ibn%20%27Uthaymiyn%3A%20Alikuwa%20Na%20Hedhi%20Hakuhirimia%20Miyqaat%20Bali%20Ameharimia%20Makkah%20%20Je%20%20Inajuzu%3F
[59] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F10192&title=55-Imaam%20Ibn%20%27Uthaymiyn%3A%20Ametoka%20Mji%20Mmoja%20Kukusudia%20%E2%80%98Umrah%20Mkewe%20Alikuwa%20Katika%20Hedhi%20%20Akakamilisha%20%E2%80%98Umrah%20Bila%20Mkewe
[60] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F10193&title=56-Imaam%20Ibn%20%27Uthaymiyn%3A%20Swafaa%20Na%20Marwah%20Na%20Hukmu%20Ya%20Mwenye%20Hedhi%20Na%20Hukmu%20Ya%20Tahiyyatul-Masjid%20%20
[61] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F10194&title=57-Imaam%20Ibn%20%27Uthaymiyn%3A%20Baada%20Ya%20Kuhiji%20Amepata%20Hedhi%20Akaona%20Hayaa%20Akaswali%20Na%20Kutufu%20Al-Ka%E2%80%99bah%20%20Na%20Kutekeleza%20Sa%E2%80%99yi
[62] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F10195&title=58-Imaam%20Ibn%20%27Uthaymiyn%3A%20Mwenye%20Hedhi%20Siku%20Ya%20%E2%80%98Arafah%20Afanye%20Nini%3F
[63] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F10196&title=59-Imaam%20Ibn%20%27Uthaymiyn%3A%20Akiwa%20Katika%20Hedhi%20Baada%20Ya%20Jamarah%20Kabla%20Ya%20Twawaaf%20Al-Ifaadhwah%20Na%20Hawezi%20Kurudi%20Baada%20Ya%20Safari%20
[64] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F10197&title=60-Imaam%20Ibn%20%27Uthaymiyn%3A%20Mwenye%20Nifaas%20Akitoharika%20Nifaas%20Kabla%20Ya%20Siku%20Arubaini%20Hijjah%20Yake%20Sahihi%3F%20%20Na%20Kama%20Hakupata%20Utohara%3F