Sifa Na Akhlaaq Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Huruma Na Upole Wake:
01-Hakumtaka Jibriyl Awaangamize Makafiri Waliomfukuza Na Kumtesa
Alhidaaya.com [4]
Pindi Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alporudi kutoka Twaaif ambako wakaazi wake hawakumpokea kwa wema bali walimfukuza na kumtesa; waliwatuma watoto wadogo na wendawazimu na watumwa wao wamfukuze. Wakawa wanamuandama huku wakimtukana na kumpiga mawe mpaka damu ikaanza kumtoka Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na viatu vyake vikarowa damu. Alipokuwa anarudi kuelekea Makkah katika eneo la Qarn Al-Manaazil, Jibriyl pamoja na Malaika wa majabali wakamuuliza iwapo anataka yaangushwe majabali mawili na kuwaangamiza watu wa Makkah, lakini Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alikataa kutokana na huruma zake. Maelezo kama ilivyothibiti katika Hadiyth ifuatayo:
عن عَائِشَةَ ـ رضى الله عنها ـ زَوْجَ النَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم حَدَّثَتْهُ أَنَّهَا قَالَتْ لِلنَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم هَلْ أَتَى عَلَيْكَ يَوْمٌ كَانَ أَشَدَّ مِنْ يَوْمِ أُحُدٍ قَالَ " لَقَدْ لَقِيتُ مِنْ قَوْمِكِ مَا لَقِيتُ، وَكَانَ أَشَدُّ مَا لَقِيتُ مِنْهُمْ يَوْمَ الْعَقَبَةِ، إِذْ عَرَضْتُ نَفْسِي عَلَى ابْنِ عَبْدِ يَالِيلَ بْنِ عَبْدِ كُلاَلٍ، فَلَمْ يُجِبْنِي إِلَى مَا أَرَدْتُ، فَانْطَلَقْتُ وَأَنَا مَهْمُومٌ عَلَى وَجْهِي، فَلَمْ أَسْتَفِقْ إِلاَّ وَأَنَا بِقَرْنِ الثَّعَالِبِ، فَرَفَعْتُ رَأْسِي، فَإِذَا أَنَا بِسَحَابَةٍ قَدْ أَظَلَّتْنِي، فَنَظَرْتُ فَإِذَا فِيهَا جِبْرِيلُ فَنَادَانِي فَقَالَ إِنَّ اللَّهَ قَدْ سَمِعَ قَوْلَ قَوْمِكَ لَكَ وَمَا رَدُّوا عَلَيْكَ، وَقَدْ بَعَثَ إِلَيْكَ مَلَكَ الْجِبَالِ لِتَأْمُرَهُ بِمَا شِئْتَ فِيهِمْ، فَنَادَانِي مَلَكُ الْجِبَالِ، فَسَلَّمَ عَلَىَّ ثُمَّ قَالَ يَا مُحَمَّدُ، فَقَالَ ذَلِكَ فِيمَا شِئْتَ، إِنْ شِئْتَ أَنْ أُطْبِقَ عَلَيْهِمِ الأَخْشَبَيْنِ، فَقَالَ النَّبِيُّ صلى الله عليه وسلم بَلْ أَرْجُو أَنْ يُخْرِجَ اللَّهُ مِنْ أَصْلاَبِهِمْ مَنْ يَعْبُدُ اللَّهَ وَحْدَهُ لاَ يُشْرِكُ بِهِ شَيْئًا ".
Amesimulia ‘Aaishah Mke wa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kuwa alimuuliza Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam): Hivi imekupitia siku iliyo ngumu zaidi ya siku ya Uhud? Akasema: “Nimepata mateso niliyo yapata kutoka kwa jamaa zako, na mateso zaidi niliyoyapata kwao ni siku ya ‘Aqabah, pale nilipojipeleka mwenyewe kwa Ibn ‘Abd Yaaliyl ibn ‘Abd Kulaal. Hakunikubalia nilicho kitaka. Nikaondoka sielewi niendako, sikuzinduka isipokuwa nilipokaribia Qarn Ath-Tha‘alib, nikainua kichwa change nikaliona wingu limenifunika, nikaangalia nikamkuta humo Jibriyl, akaniita akasema: ‘Hakika Allaah Ameisikia kauli ya watu wako kwako na jibu walilokupa, na Amekuletea Malaika wa milima ili umuamuru unachotaka katika adhabu kuwafikia jamaa zako’. Akaniita Malaika wa milima, akanisalimia, kisha akasema: ‘Ee Muhammad!’ Akasema: ‘Ikiwa ni katika unachokitaka niwafunike kwa milima miwili’. Akasema Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam): “Bali nataraji Allaah atawatoa migongoni mwao watakao mwabudu Allaah Peke Yake, hawamshirikishi na chochote.” [Al-Bukhaariy, Muslim]
Sifa Na Akhlaaq Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Huruma Na Upole Wake:
02-Mwenye Moyo Laini Si Mkali Wala Si Mjeuri
Alhidaaya.com [4]
Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alikuwa mpole, mwenye moyo laini wa huruma na hakuwa mkali wala mjeuri kwa Swahaba zake. Amejaaliwa kuwa hivyo kutokana na Rahmah ya Allaah (سبحانه وتعالى) kama Anavyosema:
فَبِمَا رَحْمَةٍ مِّنَ اللَّـهِ لِنتَ لَهُمْ ۖ وَلَوْ كُنتَ فَظًّا غَلِيظَ الْقَلْبِ لَانفَضُّوا مِنْ حَوْلِكَ ۖ فَاعْفُ عَنْهُمْ وَاسْتَغْفِرْ لَهُمْ وَشَاوِرْهُمْ فِي الْأَمْرِ ۖ فَإِذَا عَزَمْتَ فَتَوَكَّلْ عَلَى اللَّـهِ ۚإِنَّ اللَّـهَ يُحِبُّ الْمُتَوكِّلِينَ ﴿١٥٩﴾
Basi ni kwa rahmah kutoka kwa Allaah umekuwa mpole kwao (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم). Na lau ungelikuwa mjeuri mwenye moyo mgumu wangelitawanyika mbali nawe. Basi wasamehe na waombee maghfirah na washauri katika mambo. Na unapoazimia basi tawakali kwa Allaah. Hakika Allaah Anapenda wanaotawakali. [Aal-‘Imraan: 159]
Imaam Ibn Kathiyr amesema kuhusu kauli hiyo: “Yaani ungelikuwa na maneno maovu ya ujeuri, na moyo mgumu kwao basi wangelikutenga na kukukimbia, lakini Allaah (سبحانه وتعالى) Amewaunganisha kwako na kukufanya uwe mwema na laini kwao ili mioyo yao iunganike nawe.” Na ‘Abdullaah bin ‘Amr amesema kuwa alisoma sifa za Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) katika Vitabu (Vya Mbinguni) vilivyotangulia kwamba: "Yeye si mjeuri, si mwenye moyo mgumu, si mfidhuli sokoni na halipizi maovu kwa maovu bali anasamehe na kupuuza.”
Na ndio maana alikuwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) anawafanyia Swahaba zake wepesi katika mambo yao ya Dini kama ilivyothibiti katika Hadiyth ifuatayo:
عَنْ عَائِشَةَ، قَالَتْ مَا خُيِّرَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم بَيْنَ أَمْرَيْنِ أَحَدُهُمَا أَيْسَرُ مِنَ الآخَرِ إِلاَّ اخْتَارَ أَيْسَرَهُمَا مَا لَمْ يَكُنْ إِثْمًا فَإِنْ كَانَ إِثْمًا كَانَ أَبْعَدَ النَّاسِ مِنْهُ .
‘Aaishah (رضي الله عنها) amesema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) hakupewa khiyari ya mambo mawili ila alichagua lilokuwa wepesi kati ya hayo mawili madamu si dhambi. Na kama (hilo la wepesi lilikuwa) ni dhambi, basi alikuwa mbali mno na jambo hilo kuliko watu watu. [Muslim]
Na sifa zake na huruma zake kwa Swahaba Anazitaja Allaah (سبحانه وتعالى) katika kauli Yake:
لَقَدْ جَاءَكُمْ رَسُولٌ مِّنْ أَنفُسِكُمْ عَزِيزٌ عَلَيْهِ مَا عَنِتُّمْ حَرِيصٌ عَلَيْكُم بِالْمُؤْمِنِينَ رَءُوفٌ رَّحِيمٌ﴿١٢٨﴾
Kwa yakini amekujieni Rasuli anayetokana na nyinyi wenyewe, yanamtia mashaka (na huzuni) yanayokutaabisheni, anakujalini, mwenye huruma kwa Waumini ni mwenye huruma mno, mwenye rahmah. [At-Tawbah: 128]
Sifa Na Akhlaaq Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Huruma Na Upole Wake:
03-Mpole Hata Kwa Adui Zake
Walipotoa Maamkizi Ya Maangamizi Kwa Waislaam
Alhidaaya.com [4]
Makafiri walipowaamkia Waislamu kwa maamkizi ya kuwakusudia maangamizi, ‘Aaishah (ضي الله عنها) aliwarudishia maamkizi ya maangamizi na laana juu yao, lakini Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) hakupendelea kuwarudishia waziwazi bali alitumia hikma kutokana na upole wake:
حَدَّثَنَا أَبُو الْيَمَانِ، أَخْبَرَنَا شُعَيْبٌ، عَنِ الزُّهْرِيِّ، قَالَ أَخْبَرَنِي عُرْوَةُ، أَنَّ عَائِشَةَ رضى الله عنها قَالَتْ دَخَلَ رَهْطٌ مِنَ الْيَهُودِ عَلَى رَسُولِ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم فَقَالُوا السَّامُ عَلَيْكَ. فَفَهِمْتُهَا فَقُلْتُ عَلَيْكُمُ السَّامُ وَاللَّعْنَةُ. فَقَالَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم " مَهْلاً يَا عَائِشَةُ، فَإِنَّ اللَّهَ يُحِبُّ الرِّفْقَ فِي الأَمْرِ كُلِّهِ ". فَقُلْتُ يَا رَسُولَ اللَّهِ أَوَلَمْ تَسْمَعْ مَا قَالُوا قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم " فَقَدْ قُلْتُ وَعَلَيْكُمْ ".
Amesimulia ‘Urwah kuwa ‘Aaishah (ضي الله عنها) amesema: Liliingia kundi la Mayahudi kwa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) wakasema:
السَّامُ عَلَيْكَ
“Assaamu ‘alayka (mauti yawe juu yake)”.
Nikafahamu wanakusudia nini, nami nikawajibu:
عَلَيْكُمُ السَّامُ وَاللَّعْنَةُ
“Alaykumus-saamu wa al-la‘nah (juu yenu kifo na laana)”.
Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akaniambia: “Taratibu ee ‘Aaishah! Hakika Allaah Anapenda upole katika kila jambo”. Nikasema: “Ee Rasuli wa Allaah! Kwani hukuwasikia walivyosema?” Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akasema: “Hakika tayari nishawaambia
وَعَلَيْكُمْ
‘Wa ‘Alaykum (iwe juu yenu)’”. [Al-Bukhaariy]
Sifa Na Akhlaaq Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Huruma Na Upole Wake:
04-Alikuwa Na Huruma Mno Kwa Watoto
Alisema Asiyekuwa Na Huruma Hatorehemewa
Alhidaaya.com [4]
Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alikuwa ni mwenye huruma mno khasa kwa Watoto:
عن أنس بن مالك رضي الله عنه أنّه قال: "ما رَأَيْتُ أَحَدًا كانَ أَرْحَمَ بالعِيَالِ مِن رَسولِ اللهِ صَلَّى اللَّهُ عليه وسلَّمَ" مسلم
Anas bin Maalik (رضي الله عنه) amesema: Sijapatapo kumwona mtu aliyekuwa na huruma zaidi kwa Watoto kama Rasuli wa Allaah صلى الله عليه وآله وسلم” [Muslim]
Hakupendezewa na mtu asiyekuwa na huruma kwa Watoto:
عن ابي سَلَمَةَ بْن عَبْدِ الرَّحْمَنِ، أَنَّ أَبَا هُرَيْرَةَ رضى الله عنه قَالَ قَبَّلَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم الْحَسَنَ بْنَ عَلِيٍّ وَعِنْدَهُ الأَقْرَعُ بْنُ حَابِسٍ التَّمِيمِيُّ جَالِسًا. فَقَالَ الأَقْرَعُ إِنَّ لِي عَشَرَةً مِنَ الْوَلَدِ مَا قَبَّلْتُ مِنْهُمْ أَحَدًا. فَنَظَرَ إِلَيْهِ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم ثُمَّ قَالَ " مَنْ لاَ يَرْحَمُ لاَ يُرْحَمُ ".
Imepokewa kwa Abu Salamah bin ‘Abdir-Rahmaan kuwa Abu Hurayrah (رضي الله عنه) amesema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alimbusu al-Hasan bin ‘Aliyy na mbele yake alikuwepo al-Aqra‘ bin Haabis at-Taymiymiy amekaa. Al-Aqra‘ akasema: Hakika mimi nina watoto kumi, katika hao hakuna hata mmoja niliyembusu. Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akamuangalia, kisha akasema: “Asiye na huruma kwa wengine hawezi kuhurumiwa.” [Al-Bukhaariy]
Na pia,
حَدَّثَنَا أَبُو بَكْرِ بْنُ أَبِي شَيْبَةَ، حَدَّثَنَا أَبُو أُسَامَةَ، عَنْ هِشَامِ بْنِ عُرْوَةَ، عَنْ أَبِيهِ، عَنْ عَائِشَةَ، قَالَتْ قَدِمَ نَاسٌ مِنَ الأَعْرَابِ عَلَى النَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم فَقَالُوا أَتُقَبِّلُونَ صِبْيَانَكُمْ قَالُوا نَعَمْ . فَقَالُوا لَكِنَّا وَاللَّهِ مَا نُقَبِّلُ . فَقَالَ النَّبِيُّ ـ صلى الله عليه وسلم ـ " وَأَمْلِكُ أَنْ كَانَ اللَّهُ قَدْ نَزَعَ مِنْكُمُ الرَّحْمَةَ " .
Imepokewa kwa ‘Urwah kuwa ‘Aaishah (رضي الله عنها) amesema: Alikuja Mbedui kwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akasema: Je, mnawabusu watoto! Sisi hatuwabusu.” Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akamwambia: “Sina cha kukupa ikiwa Allaah tayari Ameitoa huruma katika moyo wako.” [Al-Bukhaariy]
Sifa Na Akhlaaq Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Huruma Na Upole Wake:
05-Aliwaheshimu Watoto Na Kuwatimizia Haki Zao Na Mapendekezo Yao
Alhidaaya.com [4]
Kutokana na huruma na upole wake na mapenzi yake na uadilifu wake, Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) aliwaheshimu hata Watoto na Vijana kwa kuwatimizia haki zao na mapendekezo yao, akamtimizia kijana mmoja pendekezo lake la kutaka apewe yeye maziwa ambayo aliyabakisha Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) katika bilauri baada ya kunywa kama inavyoelezea Hadiyth ifuatayo:
حَدَّثَنَا سَعِيدُ بْنُ أَبِي مَرْيَمَ، حَدَّثَنَا أَبُو غَسَّانَ، قَالَ حَدَّثَنِي أَبُو حَازِمٍ، عَنْ سَهْلِ بْنِ سَعْدٍ ـ رضى الله عنه ـ قَالَ أُتِيَ النَّبِيُّ صلى الله عليه وسلم بِقَدَحٍ فَشَرِبَ مِنْهُ، وَعَنْ يَمِينِهِ غُلاَمٌ أَصْغَرُ الْقَوْمِ، وَالأَشْيَاخُ عَنْ يَسَارِهِ فَقَالَ " يَا غُلاَمُ أَتَأْذَنُ لِي أَنْ أُعْطِيَهُ الأَشْيَاخَ ". قَالَ مَا كُنْتُ لأُوثِرَ بِفَضْلِي مِنْكَ أَحَدًا يَا رَسُولَ اللَّهِ. فَأَعْطَاهُ إِيَّاهُ.
Ametuhadithia Sa’iyd bin Abiy Maryama, ametuhadithia Abuu Ghassaan amesema: Amenihadithia Abuu Haazim kutoka kwa Sahl bin Sa’iyd (رضي الله عنه) amesema: Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) aliletewa bilauri (iliyojaa maziwa), akanywa na kuumeni mwake kulikuwa na kijana aliyekuwa mdogo wa wote waliokuwepo na wazee walikuwa kushotoni mwake. Akasema (صلى الله عليه وآله وسلم): “Ee kijana! Utaniruhusu niwapatie (kinywaji) wazee?” Akajibu: Ee Rasuli wa Allaah! Sitapendelea kumtanguliza yeyote juu yangu kunywa kutokana na ulichokunywa. Hivyo, Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akampatia yeye (kijana kinywaji). [Al-Bukhaariy]
Sifa Na Akhlaaq Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)
06-Upole Wake: Hakuwa Akiwakaripia Watoto Wala Watumishi Wake
Alhidaaya.com [4]
Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alikuwa mwema kwa Watoto, akiwafahamu hisia zao, akiwahimiza kufanya mema na kuwafundisha maadili mema, akiwahimiza katika kuhudhuria Swalaah za jamaa na akiwanasihi na akisikiliza ushauri wao. Pia Watoto walipokosea hakuwakaripia wala kuwadharau au kuwatenga; mfano ni Anas bin Maalik (رضي الله عنه) ambaye alimhudumia Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) katika nyumba yake ambako aliishi naye kuanzia Hijrah mpaka kufariki kwake alisema:
خَدَمْتُ النَّبِيَّ صلى الله عليه وسلم عَشْرَ سِنِينَ، فَمَا قَالَ لِي أُفٍّ. وَلاَ لِمَ صَنَعْتَ وَلاَ أَلاَّ صَنَعْتَ.
Nimemtumikia Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) miaka kumi (10), hakuniambia hata Uff (ni sauti inayoonyesha kughsika) na wala kunikaripia kwa kuniambia, “Kwa nini ulifanya hivi? Au kwa nini usifanye hivi!?” [Al-Bukhaariy]
Sifa Na Akhlaaq Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Huruma Na Upole Wake:
07-Alikataza Na Kutahadharisha Kudanganywa Watoto
Alhidaaya.com [4]
Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) kutokana na huruma yake, na uadilifu wake kwa watoto, alionya na kutahadharisha kutokuwadanganya Watoto kwa lolote:
عَنْ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ عَامِرٍ أَنَّهُ قَالَ دَعَتْنِي أُمِّي يَوْمًا وَرَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم قَاعِدٌ فِي بَيْتِنَا فَقَالَتْ هَا تَعَالَ أُعْطِيكَ . فَقَالَ لَهَا رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم " وَمَا أَرَدْتِ أَنْ تُعْطِيهِ " . قَالَتْ أُعْطِيهِ تَمْرًا . فَقَالَ لَهَا رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم " أَمَا إِنَّكِ لَوْ لَمْ تُعْطِيهِ شَيْئًا كُتِبَتْ عَلَيْكِ كِذْبَةٌ "
Amesimulia ‘Abdullaah ibn ‘Aamir kwamba: Mama yangu aliniita siku moja pindi Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alikuwa ameketi nyumbani kwetu. Aksema: Njoo hapa nitakupa kitu! Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akamuuliza: “Je, ulidhamiria kumpa nini?” Akajibu: Nilidhamiria kumpa tende. Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akamwmabia. “Ingelikuwa hukumpa chochote, basi ungelirekodiwa uongo dhidi yako.” [Sunan Abiy Daawuwd na amepa daraja ya Hasan Imaam Al-Albaaniy]
Links
[1] https://www.alhidaaya.com/sw/taxonomy/term/285
[2] http://alhidaaya.com/sw/
[3] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F10311&title=Sifa%20Na%20Akhlaaq%20Za%20Nabiy%20%28%D8%B5%D9%84%D9%89%20%D8%A7%D9%84%D9%84%D9%87%20%D8%B9%D9%84%D9%8A%D9%87%20%D9%88%D8%A2%D9%84%D9%87%20%D9%88%D8%B3%D9%84%D9%85%29%3A%20Huruma%20Na%20Upole%20Wake%3A
[4] http://www.alhidaaya.com/sw/
[5] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F10746&title=01-Sifa%20Na%20Akhlaaq%20Za%20Nabiy%20%28%D8%B5%D9%84%D9%89%20%D8%A7%D9%84%D9%84%D9%87%20%D8%B9%D9%84%D9%8A%D9%87%20%D9%88%D8%A2%D9%84%D9%87%20%D9%88%D8%B3%D9%84%D9%85%29%3A%20Huruma%20Na%20Upole%20Wake%3A%20Hakumtaka%20Jibriyl%20Awaangamize%20Makafiri%20Waliomfukuza%20Na%20Kumtesa%20
[6] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F10755&title=02-Sifa%20Na%20Akhlaaq%20Za%20Nabiy%20%28%D8%B5%D9%84%D9%89%20%D8%A7%D9%84%D9%84%D9%87%20%D8%B9%D9%84%D9%8A%D9%87%20%D9%88%D8%A2%D9%84%D9%87%20%D9%88%D8%B3%D9%84%D9%85%29%3A%20Huruma%20Na%20Upole%20Wake%3A%20Mwenye%20Moyo%20Laini%20Si%20Mkali%20Wala%20Si%20Mjeuri
[7] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F10764&title=03-Sifa%20Na%20Akhlaaq%20Za%20Nabiy%20%28%D8%B5%D9%84%D9%89%20%D8%A7%D9%84%D9%84%D9%87%20%D8%B9%D9%84%D9%8A%D9%87%20%D9%88%D8%A2%D9%84%D9%87%20%D9%88%D8%B3%D9%84%D9%85%29%3A%20Huruma%20Na%20Upole%20Wake%3A%20Mpole%20Hata%20Kwa%20Adui%20Zake%20Walipotoa%20Maamkizi%20Ya%20Maangamizi%20Kwa%20Waislaam%20%20
[8] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F10793&title=04-Sifa%20Na%20Akhlaaq%20Za%20Nabiy%20%28%D8%B5%D9%84%D9%89%20%D8%A7%D9%84%D9%84%D9%87%20%D8%B9%D9%84%D9%8A%D9%87%20%D9%88%D8%A2%D9%84%D9%87%20%D9%88%D8%B3%D9%84%D9%85%29%3A%20Huruma%20Na%20Upole%20Wake%3A%20Alikuwa%20Na%20Huruma%20Mno%20Kwa%20Watoto%20Alisema%20Asiyekuwa%20Na%20Huruma%20Hatorehemewa%20
[9] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F10803&title=05-Sifa%20Na%20Akhlaaq%20Za%20Nabiy%20%28%D8%B5%D9%84%D9%89%20%D8%A7%D9%84%D9%84%D9%87%20%D8%B9%D9%84%D9%8A%D9%87%20%D9%88%D8%A2%D9%84%D9%87%20%D9%88%D8%B3%D9%84%D9%85%29%3A%20Huruma%20Na%20Upole%20Wake%3A%20Aliwaheshimu%20Watoto%20Na%20Kuwatimizia%20Haki%20Zao%20Na%20Mapendekezo%20Yao%20
[10] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F10807&title=06-Sifa%20Na%20Akhlaaq%20Za%20Nabiy%20%28%D8%B5%D9%84%D9%89%20%D8%A7%D9%84%D9%84%D9%87%20%D8%B9%D9%84%D9%8A%D9%87%20%D9%88%D8%A2%D9%84%D9%87%20%D9%88%D8%B3%D9%84%D9%85%29%3A%20Hakuwa%20Akiwakaripia%20Watoto%20Wala%20Watumishi%20Wake
[11] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F10823&title=07-Sifa%20Na%20Akhlaaq%20Za%20Nabiy%20%28%D8%B5%D9%84%D9%89%20%D8%A7%D9%84%D9%84%D9%87%20%D8%B9%D9%84%D9%8A%D9%87%20%D9%88%D8%A2%D9%84%D9%87%20%D9%88%D8%B3%D9%84%D9%85%29%3A%20Huruma%20Na%20Upole%20Wake%3A%20Alikataza%20Na%20Kutahadharisha%20Kudanganywa%20Watoto