Riyaadhw Asw-Swaalihiyn
باب فضل الدعاء
01-Mlango Wa Fadhila za Duaa
Alhidaaya.com [4]
قال الله تَعَالَى :
وَقَالَ رَبُّكُمُ ادْعُونِي أَسْتَجِبْ لَكُمْ ۚ ﴿٦٠﴾
Na Rabb wenu Amesema: Niombeni, Nitakuitikieni. [Gaafir: 60]
ادْعُوا رَبَّكُمْ تَضَرُّعًا وَخُفْيَةً ۚ إِنَّهُ لَا يُحِبُّ الْمُعْتَدِينَ ﴿٥٥﴾
Muombeni Rabb wenu kwa unyenyekevu na kwa siri, hakika Yeye Hapendi wenye kupindukia mipaka. [Al-A'raaf: 55]
وَإِذَا سَأَلَكَ عِبَادِي عَنِّي فَإِنِّي قَرِيبٌ ۖ أُجِيبُ دَعْوَةَ الدَّاعِ إِذَا دَعَانِ ۖ ﴿١٨٦﴾
Na watakapokuuliza Waja Wangu kuhusu Mimi, basi (waambie) Mimi Niko Karibu (kwa ujuzi). Naitikia du’aa ya muombaji anaponiomba. [Al-Baqarah: 186]
أَمَّن يُجِيبُ الْمُضْطَرَّ إِذَا دَعَاهُ وَيَكْشِفُ السُّوءَ ﴿٦٢﴾
Au nani Anayemuitika mwenye dhiki mno anapomwomba, na Akamuondoshea uovu. [An-Naml: 62]
Hadiyth – 1
وعن النعمان بن بشيرٍ رضي الله عنهما ، عن النبيّ صلى الله عليه وسلم ، قَالَ : (( الدُّعَاءُ هُوَ العِبَادَةُ )) . رواه أَبُو داود والترمذي ، وقال : (( حديث حسن صحيح )) .
Imepokewa kutoka kwa An-Nu'maan bin Bashiyr (Radhwiya Allaahu 'ahumaa) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Duaa ni Ibaadah." [Abu Daawuwd na At-Tirmidhiy, na akasema ni Hadiyth Hasan Swahiyh]
Hadiyth – 2
وعن عائشة رَضِيَ اللهُ عنها ، قالت : كَانَ رسُولُ الله صلى الله عليه وسلم يَسْتَحِبُّ الجَوَامِعَ مِنَ الدُّعَاءِ ، وَيَدَعُ مَا سِوَى ذَلِكَ . رواه أَبُو داود بإسناد جيدٍ .
'Aaishah (Radhwiya Allaahu 'anhaa) amesema: Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) Alikuwa akipenda sana duaa zilizokamilika na kuacha nyinginezo. [Abu Daawuwd kwa Isnaad nzuri]
Hadiyth – 3
وعن أنس رَضِيَ اللهُ عنه قَالَ : كَانَ أكثرُ دعاءِ النبيّ صلى الله عليه وسلم : (( اللَّهُمَّ آتِنَا في الدُّنْيَا حَسَنَةً ، وَفِي الآخِرَةِ حَسَنَةً ، وَقِنَا عَذَابَ النَّارِ )) متفقٌ عَلَيْهِ .
زاد مسلم في روايتهِ قَالَ : وَكَانَ أَنَسٌ إِذَا أرادَ أنْ يَدْعُوَ بِدَعْوَةٍ دَعَا بِهَا ، وَإِذَا أرادَ أنْ يَدْعُوَ بِدُعَاءٍ دَعَا بِهَا فِيهِ .
Amesema Anas (Radhwiya Allaahu 'anhu): Duaa aliyokuwa akiiomba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) sana ni: "(Rabb Wetu! Tupe katika dunia mazuri na katika Aakhirah mazuri na Tukunge na adhabu ya moto) [Al-Baqarah: 201]." [Al-Bukhaariy na Muslim]
Ameongeza Muslim katika riwaayah yake, akasema: "Na Anas (Radhwiya Allaahu 'anhu) alikuwa anapotaka kuomba dua hutumia dua hiyo. Na akitaka kuomba dua yoyote hujumlisha dua hii ndani yake."
Hadiyth – 4
وعن ابن مسعودٍ رَضِيَ اللهُ عنه : أنَّ النبيَّ صلى الله عليه وسلم كَانَ يقول : (( اللَّهُمَّ إنِّي أسْألُكَ الهُدَى ، والتُّقَى ، والعَفَافَ ، والغِنَى )) . رواه مسلم .
Imepokewa kutoka kwa Ibn Mas'uwd (Radhwiya Allaahu 'anhu) kuwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akisema: "Allaahumma inniy as'alukal hudaa wat tuqaa wal 'afaafa wal ghinaa (Ee Rabb Wangu! Hakika mimi nakuomba unipatie uongofu, na uchaji Mungu (taqwa), na utohara na utajiri (kwa kuupa nyongo ulimwengu)." [Muslim]
Hadiyth – 5
وعن طارق بن أَشْيَمَ رَضِيَ اللهُ عنه قَالَ : كَانَ الرَّجُلُ إِذَا أسْلَمَ عَلَّمَهُ النَّبيُّ صلى الله عليه وسلم الصَّلاَةَ ثُمَّ أمَرَهُ أنْ يَدْعُوَ بِهؤلاَءِ الكَلِمَاتِ : (( اللَّهُمَّ اغْفِرْ لِي ، وَارْحَمْنِي ، وَاهْدِني ، وَعَافِني ، وَارْزُقْنِي )) . رواه مسلم .
وفي روايةٍ له عن طارق: أنَّه سمع النبيَّ صلى الله عليه وسلم ، وأتاهُ رَجُلٌ فَقَالَ : يَا رسول اللهِ ، كَيْفَ أقُولُ حِيْنَ أسْأَلُ رَبِّي ؟ قَالَ : (( قُلْ : اللَّهُمَّ اغْفِرْ لِي ، وَارْحَمْنِي ، وَعَافِني ، وارْزُقْنِي ، فإنَّ هؤلاَءِ تَجْمَعُ لَكَ دُنْيَاكَ وَآخِرَتَكَ )) .
Amesema Twariq bin Ashyam: Ilikuwa mtu anaposilimu, Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) humfundisha Swalaah, kisha humuamuru aombe kwa maneno haya: "Allaahumma Ghfirliy warhamniy wahdiniy wa 'aafiniy warzuqniy (Rabb Wangu! Nisamehe, na Unirehemu, na Uniruzuku)." [Muslim]
Na katika riwaayah yake nyingine kutoka kwa Twaariq: kuwa alimsikia Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alipomjia mtu na kumuuliza: "Ee Rasuli wa Allaah! Niseme vipi ninapomuomba Rabb wangu." Akaniambia: "Sema Allaahumma Ghfirliy warhamniy wa 'aafiniy warzuqniy (Mola Wangu! Nisamehe, na Unirehemu, na Uniponyeshe na Uniruzuku), kwani maombi haya yanajumlisha mabo yako ya dunia na Aakherah."
Hadiyth – 6
وعن عبد الله بن عمرو بن العاص رضي الله عنهما ، قَالَ : قَالَ رسُولُ الله صلى الله عليه وسلم : (( اللَّهُمَّ مُصَرِّفَ القُلُوبِ صَرِّفْ قُلُوبنَا عَلَى طَاعَتِكَ )) . رواه مسلم .
Imepokewa kutoka kwa 'Abdillaah bin 'Amruw bin Al-'Aas (Radhwiya Allaahu 'anhumaa) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Allaahumma muswarrifal quluwbi swarrif quluwbanaa 'alaa twaa'atika (Rabb Wangu! Mwenye kuongoza mioyo, Iongoze mioyo yetu katika twaa Yakoo)." [Muslim]
Hadiyth – 7
وعن أَبي هريرة رضي الله عنه ، عن النبيِّ صلى الله عليه وسلم ، قَالَ : (( تَعَوَّذُوا بِاللهِ مِنْ جَهْدِ البَلاَءِ ، وَدَرَكِ الشَّقَاءِ ، وَسُوءِ القَضَاءِ ، وَشَمَاتَةِ الأَعْدَاءِ )) متفق عَلَيْهِ .
وفي روايةٍ قَالَ سفيان : أَشُكُّ أنِّي زِدْتُ واحدةً مِنْهَا .
Imepokewa kutoka kwa Abu Huraiyrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Takeni ulinzi kutoka kwa Allaah na balaa la mtihani, na kupatwa na maisha mabaya (Aahkerah), na hukumu mbaya na furaha ya maadui." [Al-Bukhaariy na Muslim]
Na katika riwaayah: Sufyaan Amesema: "Nina shaka kuwa mimi nimezidisha moja kati ya hayo mambo."
Hadiyth – 8
وعن أَبي هريرة رضي الله عنه ، قَالَ : كَانَ رسُولُ الله صلى الله عليه وسلم يقول : (( اللَّهُمَّ أصْلِحْ لِي دِيني الَّذِي هُوَ عِصْمَةُ أمْرِي ، وأصْلِحْ لِي دُنْيَايَ الَّتي فِيهَا مَعَاشِي ، وأصْلِحْ لِي آخِرتِي الَّتي فِيهَا مَعَادي ، وَاجْعَلِ الحَيَاةَ زِيَادَةً لِي في كُلِّ خَيْرٍ ، وَاجْعَلِ المَوتَ رَاحَةً لِي مِنْ كُلِّ شَرٍّ )) . رواه مسلم .
Amesema Abu Huraiyrah (Radhwiya Allaahu 'anhu): Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akisema: "Allaahumma aswlih liy Diyniy ladhiy huwa 'iswmatiu amriy wa aswlih liy dunyaayal latiy fiyhaa ma'ashiy wa aswlih liy aakhiratiyl latiy fiyhaa ma'aadiy waj'alil hayaata ziyaadatan liy fiy kuli khayr waj'alil mawta raahatan liy min kuli sharr (Rabb Wangu! Nitengenezee Dini yangu ambayo ndiyo yenye kulinda mambo yangu, na Nitengenezee mimi dunia yangu ambayo ndiyomsingi wa maisha yangu, na Nitengenezee Aakherah yangu ambayo ndiyo marejeo yangu. Na yajaalie maisha yangu yawe marefu katika kufanya mambo mema na umauti wangu Ujaalie ni raha kwangu dhidi ya kila maovu." [Muslim]
Hadiyth – 9
وعن علي رضي الله عنه قَالَ: قَالَ لي رسولُ الله صلى الله عليه وسلم : (( قُلْ : اللَّهُمَّ اهْدِني ، وسَدِّدْنِي )) .
وفي رواية : (( اللَّهمَّ إنِّي أسْألُكَ الهُدَى والسَّدَادَ )) . رواه مسلم .
Imepokewa kutoka kwa'Aliy (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alimwambia: "Sema: Allaahumma ihdiniy wa saddidniy (Rabb Wangu! Niongoze na Unifanye mimi kusimama wima)."
Na katika riwaayah nyingine: "Allaahumma inniy as'alukal hudaa wa sadaad (Rabb Wangu! Hakika mimi nakuomba uongofu na kuwa wima)." [Muslim]
Hadiyth – 10
وعن أنس رضي الله عنه قَالَ : كَانَ رسولُ الله صلى الله عليه وسلم يقولُ : (( اللَّهُمَّ إنِّي أَعُوذُ بِكَ مِنَ العَجْزِ ، وَالكَسَلِ ، وَالجُبْنِ ، والهَرَمِ ، والبُخْلِ ، وأعُوذُ بِكَ مِنْ عَذَابِ القَبْرِ ، وأعوذُ بِكَ مِنْ فِتْنَةِ المَحْيَا وَالمَمَاتِ )) .
وفي رواية : (( وَضَلَعِ الدَّيْنِ ، وَغَلَبَةِ الرِّجَالِ )) . رواه مسلم .
Amesema Anas (Radhwiya Allaahu 'anhu): Alikuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akisema: "Allaahumma inniy a'uwdhu Bika minal 'ajzi wal kasali wal jubni wal harami wal bukhli wa a'uwdhu Bika min 'adhaabil qabri wa a'uwdhu Bika min fitnatil mahyaa wal mamaat (Rabb Wangu! Hakika ninajilinda Kwako na unyonge na uvivu, na uzembe na uzee na ubakhili. Na ninajilinda Kwako na adhabu ya kaburini, na ninajilinda Kwako na fitna ya uhai na kifo)."
Na katika riwaayah yake nyingine: "Wa dhala'id dayni wa ghalabatir rijaal (Na najilinda Kwako kutokana na uzito wa deni na kushindwa na watu)." [Muslim]
Hadiyth – 11
وعن أَبي بكر الصديق رضي الله عنه : أنَّه قَالَ لرسُولِ الله صلى الله عليه وسلم : عَلِّمْنِي دُعَاءً أَدْعُو بِهِ في صَلاَتِي ، قَالَ : (( قُلْ : اللَّهُمَّ إِنِّي ظَلَمتُ نَفْسِي ظُلْماً كَثِيراً ، وَلاَ يَغْفِرُ الذُّنُوبَ إِلاَّ أنْتَ ، فَاغْفِرْ لي مَغْفِرَةً مِنْ عِنْدِكَ ، وارْحَمْنِي ، إنَّكَ أنْتَ الغَفُورُ الرَّحِيمُ )) متفق عَلَيْهِ .
وفي روايةٍ : (( وفي بيتي )) وَرُوِيَ : (( ظلماً كثيراً )) ورُوِي : (( كبيراً )) بالثاء المثلثة وبالباء الموحدة ؛ فينبغي أنْ يجمع بينهما فيقال : كثيراً كبيراً .
Imepokewa kutoka kwa Abu Bakar As-Swiddiyq kuwa alimwambia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam): "Nifundishe duaa ntakayoomba katika Swalaah yangu." Akasema: "Sema: Allaahumma inniy dhalamtu nafsiy dhulman kathiyrannwalaa yaghfirudh dhunuba illaa Anta Faghfirliy Maghfiratan min 'Indika warhamniy Innaka Antal Ghafuurur Rahiym (Rabb Wangu! Hakika nimejidhulumu dhulma nyingi, na hakuna anayesamehe dhambi isipokuwa Wewe. Nisamehe msamaha wa kutoka Kwako tu, na unirehemu, hakika Yako ni Mwingi wa Kusamehe na Kuhurumia)." [Al-Bukhaariy, Muslim. At-Tirmidhiy na An-Nasaaiy]
Na katika riwaayah: "Na katika nyumba yangu." Na imepokewa: "Dhulman kathiyran (dhulma nyingi)." Na imepokewa: "Kabiyran (kubwa), kwa tha na kwa ba, hivyo zinatakiwa zijumlishe kwa kusema: "Kathiyran kabiyran."
Hadiyth – 12
وعن أَبي موسى رضي الله عنه ، عن النَّبيِّ صلى الله عليه وسلم : أنَّه كَانَ يدْعُو بِهذا الدُّعَاءِ : (( اللَّهُمَّ اغْفِرْ لِي خَطِيئَتِي وَجَهْلِي ، وإسرافِي في أمْرِي ، وَمَا أنْتَ أَعْلَمُ بِهِ مِنّي ، اللَّهُمَّ اغْفِرْ لِي جِدِّي وَهَزْلِي ؛ وَخَطَئِي وَعَمْدِي ؛ وَكُلُّ ذَلِكَ عِنْدِي ، اللَّهُمَّ اغْفِرْ لي مَا قَدَّمْتُ وَمَا أخَّرْتُ ، وَمَا أسْرَرْتُ وَمَا أعْلَنْتُ ، وَمَا أنتَ أعْلَمُ بِهِ مِنِّي ، أنْتَ المُقَدِّمُ ، وأنْتَ المُؤَخِّرُ ، وأنْتَ عَلَى كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ )) متفق عَلَيْهِ .
Imepokewa kutoka kwake Abu Muwsaa (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akiomba kwa duaa hii: "Allaahumma Ghfirliy khatwiyatiy wa jahliy wa israafiy fiy amriy wa maa Anta a'alamu bihi miniiy, Allaahumma Ghfirliy jiddiy wa hazliy wa khata'iy wa 'amdiy wa kullu dhaalika 'indiy. Allaahumma Ghfirliy maa qaddamtu wa maa akhkhartu wa maa asrartu wa maa a'lantu wa maa Anta a'alamu miniy Antal Muqaddimu wa Antal Muakhkhiru wa Anta 'alaa kulli Shaiyin Qadiyr (Rabb Wangu! Nighufurie makosa yangu na ujinga wangu. Na israfu yangu kwangu katika mambo yangu yote na lile ambalo Wewe Unalijua zaidi kuliko mimi. Rabb Wangu! Nighufirie makosa yangu niliyoyafanya kwa makusudi, kwa ujinga na kwa mzaha wangu na yote hayo niliyonayo. Ee Rabb Wangu! Nighufurie nilichokichelewesha, nilicho kifanya kwa siri na nilicho kifanya kwa bayana. Wewe Ndiye Unayetanguliza, na Wewe Ndiye Unayechelewesha na Wewe ni Muweza wa kila kitu)." [Al-Bukhaariy na Muslim]
Hadiyth – 13
وعن عائشة رَضِيَ اللهُ عنها : أنَّ النبيَّ صلى الله عليه وسلم كَانَ يقول في دُعَائِهِ : (( اللَّهُمَّ إنِّي أعُوذُ بِكَ مِنْ شَرِّ مَا عَمِلْتُ ومنْ شَرِّ مَا لَمْ أعْمَلْ )) . رواه مسلم .
Imepokewa kutoka kwake 'Aaishah (Radhwiya Allaahu 'anhaa) kuwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akisema katika duaa yake: "Allaahumma inniy a'uwdhubika min sharri maa 'amiltu wa min sharri maa lam a'amal (Rabb Wangu! Hakika ninajilinda Kwako na shari ya niliyoyafanya na kwa shari ya yale ambayo sijayatenda)." [Muslim]
Hadiyth – 14
وعن ابن عمر رضي الله عنهما ، قَالَ : كَانَ مِن دعاءِ رسُولِ الله صلى الله عليه وسلم : (( اللَّهُمَّ إنِّي أَعُوذُ بِكَ مِنْ زَوالِ نِعْمَتِكَ، وتَحَوُّلِ عَافِيَتِكَ، وفُجَاءةِ نِقْمَتِكَ ، وَجَميعِ سَخَطِكَ )) . رواه مسلم .
Amesema Ibn 'Umar (Radhwiya Allaahu 'anhumaa): Ni miongoni mwa duaa za Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam): "Allaahumma inniy a'uwdhu bika min zawaali ni'matika wa tahawwuli 'aafiyatika wa fujaati niqmatika wa jamiy'i sakhatwika (Rabb Wangu! Hakika ninajilinda Kwako na kukoma kwa neema Zako na kubadilika kwa usalamaWako na kuja haraka kwa ghadhabu Yako na hasira Yako yote)." [Muslim]
Hadiyth – 15
وعن زيد بن أرقم رضي الله عنه ، قَالَ : كَانَ رسُولُ الله صلى الله عليه وسلم ، يقول : (( اللَّهُمَّ إنِّي أَعُوذُ بِكَ مِنَ العَجْزِ وَالكَسَلِ ، والبُخْلِ والهَرَمِ ، وَعَذابِ القَبْرِ ، اللَّهُمَّ آتِ نَفْسِي تَقْوَاهَا ، وَزَكِّها أنْتَ خَيْرُ مَنْ زَكَّاهَا ، أنْتَ وَلِيُّهَا وَمَوْلاَهَا ، اللَّهُمَّ إنِّي أَعُوذُ بِكَ مِنْ عِلْمٍ لا يَنْفَعُ؛ وَمِنْ قَلْبٍ لا يَخْشَعُ ، وَمِنْ نَفْسٍ لاَ تَشْبَعُ ؛ وَمِنْ دَعْوَةٍ لا يُسْتَجابُ لَهَا )) .رواه مسلم .
Amesema Zayd bin Arqam (Radhwiya Allaahu 'anhu): Alikuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akisema: "Allaahumma inniy a'uwdhu bika minal 'ajzi wal kasal wal bukhli wal harami wa 'Adhaabil qabr. Allaahumma aati nafsiy taqwaahaa wa zakkihaa Anta khayra man zakkaahaa Anta waliyyuhaa wa mawlaahaa. Allaahumma inniy a'uwdhu bika min 'ilmin laa yanfa'u wa min qalbin laa yakhsha'u wa min nafsin laa tashba'u wa min da'watin laa yustajaabu lahaa (Rabb Wangu! Hakika ninajilinda Kwako na unyonge na uvivu, na ubakhili na uzee na adhabu ya kaburini. Rabb Wangu! Ipatie nafsi yangu Taqwa na Uitakase kwani Wewe ni mbora wa kuitakasa, Wewe Ndiye Mlinzi na Bwana (Mola) Wake. Rabb Wangu! Hakika ninajilinda na elimu isiyo na manufaa na kwa moyo usioogopa na nafsi isiyo shiba na duaa isiyojibiwa)." [Muslim]
Hadiyth – 16
وعن ابن عباس رضي الله عنهما : أنَّ رسُولَ الله صلى الله عليه وسلم كَانَ يقول : (( اللَّهُمَّ لَكَ أسْلَمْتُ ، وَبِكَ آمَنْتُ ، وَعَلَيْكَ تَوَكَّلْتُ ، وإلَيْكَ أنَبْتُ ، وَبِكَ خَاصَمْتُ ، وإلَيْكَ حَاكَمْتُ . فَاغْفِرْ لِي مَا قَدَّمْتُ ، وَمَا أَخَّرْتُ ، وَمَا أَسْرَرْتُ ، وَمَا أعْلَنْتُ ، أنتَ المُقَدِّمُ ، وأَنْتَ المُؤَخِّرُ ، لا إلهَ إِلاَّ أنْتَ )) .
زَادَ بَعْضُ الرُّوَاةِ : (( وَلاَ حَوْلَ وَلاَ قُوَّةَ إِلاَّ باللهِ )) متفق عَلَيْهِ .
Imepokewa kutoka kwa Ibn 'Abbaas (Radhwiya Allaahu 'anhumaa) kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akisema: "Allaahumma laka aslamtu wa bika aamantu wa 'alayka tawakkaltu wa ilayka haakamtu faghfirliy maa qaddamtu wa maa akhkhartu wa maa asrartu wa maa a'lantu Antal Muqaddim wa Antal Muakhkhiru Laa ilaaha illaa Anta (Rabb Wangu! Kwako nimenyenyekea, na nimekutegemea Wewe, na nimerudi Kwako na Kwako nataka usaidizi na Kwako ninataka hukumu. Hivyo, nisamehe madhambi yangu niliyoyatanguliza na nitakayo yafanya (baadae), na yale niliyo yafanya kwa siri na kwa dhahiri. Wewe Ndiye wa Mwanzo na Wewe Ndiye wa Mwisho. Hapana muabudiwa wa haki ila Wewe)."
Wameongeza baadhi ya wapokezi: "Walaa Hawla walaa Quwwata illaa BiLLaah." [Al-Bukhaariy na Muslim]
Hadiyth – 17
وعن عائشة رَضِيَ اللهُ عنها : أنَّ النبيّ صلى الله عليه وسلم كَانَ يدعو بِهؤُلاءِ الكَلِمَاتِ : (( اللَّهُمَّ إنِّي أَعُوذُ بِكَ مِنْ فِتْنَةِ النَّارِ ، وَعَذَابِ النَّارِ ، وَمِنْ شَرِّ الغِنَى وَالفَقْرِ )) . رواه أَبُو داود والترمذي ، وقال : (( حديث حسن صحيح )) ؛ وهذا لفظ أَبي داود .
Imepokewa kutoka kwa 'Aaishah (Radhwiya Allaahu 'anhaa) kuwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akiomba kwa maneno haya: "Allaahumma inniy a'uwdhu bika min fitnatin naari wa 'adhaabin naari wa min sharril ghinaa wal faqr (Rabb Wangu! Hakika ninajilinda Kwako na fitna ya Moto na adhabu ya Moto na shari ya utajiri na ufakiri)." [Abu Daawuwd na At-Tirmidhiy, na akasema ni Hadiyth Hasan Swahiyh, na hii ni lafdhi ya Abu Daawuwd]
Hadiyth – 18
وعن زياد بن عِلاَقَةَ عن عمه ، وَهُوَ قُطْبَةُ بنُ مالِكٍ رَضِيَ اللهُ عنه ، قَالَ : كَانَ النبيّ صلى الله عليه وسلم يقول : (( اللَّهُمَّ إنِّي أعُوذُ بِكَ مِنْ مُنْكَرَاتِ الأخْلاَقِ ، وَالأعْمَالِ ، والأهْواءِ )) . رواه الترمذي ، وقال : (( حديث حسن )) .
Imepokewa kutoka kwake Ziyaad bin 'Ilaaqah kutoka kwa ami yake, naye Qutbah bin Maalik (Radhwiya Allaahu 'anhu) kuwa alisema: Alikuwa Nabiy (Swalla Allaahu a'alyhi wa aalihi wa sallam) akisema: "Allaahumma a'uwdhu bika min munkaraatil akhlaaq wal a'maal wal ahwaai (Rabb Wangu! Hakika ninajilinda Kwako na utovu wa tabia na amali mbaya na hawaa (matamanio)." [At-Tirmidhiy, na akasema ni Hadiyth Hasan]
Hadiyth – 19
وعن شَكَلِ بن حُمَيدٍ رَضِيَ اللهُ عنه قَالَ : قلتُ : يَا رسولَ الله ، علِّمْنِي دعاءً ، قَالَ : (( قُلْ : اللَّهُمَّ إنِّي أعُوذُ بِكَ مِنْ شَرِّ سَمْعِي ، وَمِنْ شَرِّ بَصَرِي ، وَمِنْ شَرِّ لِسَانِي ، وَمِنْ شَرِّ قَلْبِي ، وَمِنْ شَرِّ مَنِيِّي )) . رواه أَبُو داود والترمذي ، وقال : (( حديث حسن )) .
Shakal bin Humayd (Radhwiya Allaahu 'anhu) amesema: Ee Rasuli wa Allaah: "Nifundishe duaa." Akasema: Sema: "Allaahumma inniy a'uwdhu Bika min sharri sam'iy wa min sharri baswariy wa min sharri lisaaniy wa min sharri qalbiy wa sharri manniyyiy (Rabb Wangu! Hakika ninajilinda Kwako na uovu wa masikizi yangu, na uovu wa uoni wangu na uovu wa ulimi wangu, na uovu wa moyo wangu na uovu wa sehemu zangu za siri (utupu))." [Abu Daawud na At-Timidhiy, na akasema ni Hadiyth Hasan]
Hadiyth – 20
وعن أنس رَضِيَ اللهُ عنه : أنَّ النبيَّ صلى الله عليه وسلم كَانَ يقول : (( اللَّهُمَّ إنِّي أَعُوذُ بِكَ مِنَ البَرَصِ ، والجُنُونِ ، والجُذَامِ ، وَسَيِّيءِ الأسْقَامِ )) . رواه أَبُو داود بإسناد صحيحٍ .
Imepokewa kutoka kwake Anas (Radhwiya Allaahu 'anhu) kuwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akisema: "Allaahumma inniy a'uwdhu Bika minal barasw wal junuwn wal jidhaam wa sayyiil asqaam (Rabb Wangu! Hakika ninajilinda Kwako na ukoma, na umajununi, na ugonjwa wa ngozi na maradhi mengine mabaya)." [Abu Daawuwd kwa isnaad Swahiyh]
Hadiyth – 21
وعن أَبي هريرة رَضِيَ اللهُ عنه قَالَ : كَانَ رسولُ الله صلى الله عليه وسلم يقول : (( اللَّهُمَّ إنِّي أعُوذُ بِكَ مِنَ الجُوعِ ، فَإنَّهُ بِئْسَ الضَّجِيعُ ، وأعوذُ بِكَ منَ الخِيَانَةِ ، فَإنَّهَا بِئْسَتِ البِطَانَةُ )) . رواه أَبُو داود بإسناد صحيح .
Imepokewa kutoka kwa Abu Huraiyrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akiomba: "Allaahumma inniy a'uwdhu Bika minal juw'i fainnahu bisal dhajiy'u wa a'uwdhu Bika minal khiyaanati fainnahaa bisatil bitwaanah (Rabb Wangu! Hakika ninajilinda Kwako na njaa, kwani huyo ni rafiki mbaya na ninajilinda Kwako na hiyana, kwani ni tabia mbaya ya ndani ya mwili)." [Abu Daawuwd kwa Isnaad Swahiyh]
Hadiyth – 22
وعن عليّ رَضِيَ اللهُ عنه : أنَّ مُكَاتباً جاءهُ فَقَالَ : إنِّي عَجِزْتُ عَنْ كِتَابَتِي فَأعِنِّي ، قَالَ : ألا أُعَلِّمُكَ كَلِماتٍ عَلَّمَنِيهنَّ رسُولُ الله صلى الله عليه وسلم ، لَوْ كَانَ عَلَيْكَ مِثْلُ جَبَلٍ دَيْناً أدَّاهُ اللهُ عَنْكَ ؟ قُلْ : (( اللَّهُمَّ اكْفِني بِحَلاَلِكَ عَنْ حَرَامِكَ ، وَأغْنِنِي بِفَضْلِكَ عَمَّنْ سِواكَ )) . رواه الترمذي ، وقال : (( حديث حسن )) .
Imepokewa kutoka kwa 'Aliy (Radhwiya Allaahu 'anhu) kuwa mtumwa (aliyeandikiana na bwana wake kuununua uhuru wake kwa kuandikiana mkataba wa hela atakazo toa) alikuja kwake na kumwambia: "Hakika nimeshindwa kulipa sehemu ya hela za mkataba tulizo kubaliana, hivyo nisaidie." Alimwambia: "Je, sikufundishi maneno ambayo alinifundisha Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam)? lau una deni mfano wa jabali Allaah Atakuondoshea. Sema: Allaahumma kfiniy bihalaalika 'an haraamika wa ghniniy bifadhlika 'amman siwaaka (Rabb Wangu! Nitosheleze mimi na halali kutoka Kwako kutokana na haramu (usinifanye kutegemea haramu) na Nipatie utajiri (na kinai) kwa fadhila Zako ambayo itanifanya nisimtegemee mwengine yeyote mbali na Wewe)." [At-Tirmidhiy, na akasema ni Hadiyth Hasan]
Hadiyth – 23
وعن عِمْرَانَ بن الحُصَينِ رضي الله عنهما : أنَّ النبيّ صلى الله عليه وسلم عَلَّمَ أبَاهُ حُصَيْناً كَلِمَتَيْنِ يَدْعُو بهما : (( اللَّهُمَّ ألْهِمْني رُشْدِي ، وأعِذْنِي مِنْ شَرِّ نَفْسي )) . رواه الترمذي ، وقال : (( حديث حسن )) .
Imepokewa kutoka kwa 'Imraan bin Al-Huswayn (Radhwiya Allaahu 'anhu) kuwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alimfundisha baba yao, Huswayn maneno mawili ambayo alikuwa akiomba kwa kuyatumia: "Allaahumma alhimniy rushdiy wa a'idhniy min sharri nafsi (Rabb Wangu! Nipatie uongofu na Unilinde na shari ya nafsi yangu)." [At-Tirmidhiy, na akasema ni Hadiyth Hasan]
Hadiyth – 24
وعن أَبي الفضل العباس بن عبد المطلب رضي الله عنه قَالَ : قُلْتُ : يَا رسول الله عَلِّمْني شَيْئاً أسْألُهُ الله تَعَالَى، قَالَ : (( سَلوا الله العَافِيَةَ )) فَمَكَثْتُ أَيَّاماً، ثُمَّ جِئْتُ فَقُلتُ : يَا رسولَ الله عَلِّمْنِي شَيْئاً أسْألُهُ الله تَعَالَى ، قَالَ لي : (( يَا عَبَّاسُ ، يَا عَمَّ رسول اللهِ ، سَلُوا الله العَافِيَةَ في الدُّنيَا والآخِرَةِ )) . رواه الترمذي ، وقال : (( حديث حسن صحيح )) .
Amesema Abil Fadhl Al-'Abbaas bin 'Abdil-Muttwalib (Radhwiya Allaahu 'anhu): Nilisema: "Ee Rasuli wa Allaah! Nifundishe duaa ambayo nitamuomba nayo Allaah Ta'aalaa." Akasema: "Mtake Allaah siha nzuri." Nikakaa kwa siku kadhaa, kisha nikaja na kumwambia: "Ee Rasuli wa Allaah! Nifundishe duaa ambayo nitamuomba nayo Allaah Ta'aalaa." Akaniambia: "Ee 'Abbaas, ee ami ya Rasuli wa Allaah! Muombe Allaah afya nzuri duniani na Aakhirah." [At-Tirmidhiy, na akasema ni Hadiyth Hasan Swahiyh]
Hadiyth – 25
وعن شَهْرِ بن حَوشَبٍ ، قَالَ : قُلْتُ لأُمِّ سَلَمة رَضِيَ اللهُ عنها ، يَا أمَّ المؤمِنينَ ، مَا كَانَ أكثْرُ دعاءِ رَسُولِ الله صلى الله عليه وسلم ، إِذَا كَانَ عِنْدَكِ ؟ قالت : كَانَ أكْثَرُ دُعائِهِ : (( يَا مُقَلِّبَ القُلُوبِ ثَبِّتْ قَلْبِي عَلَى دِينِكَ )) . رواه الترمذي ، وقال : (( حديث حسن )) .
Amesema Shahr bin Hawshab: Nilimuuliza Umm Salamah (Radhwiya Allaahu 'anhaa): "Ee Mama wa Waumini! Ni duaa gani aliyokuwa akiomba sana Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alipokuwa kwako?" Akasema: "Miongoni mwa duaa aliyokuwa akiomba sana ni Yaa muqallibal quluwbi thabbit qalbiy 'alaa Diynik (Ee Mwenye kugeuza mioyo uthibitishe moyo wangu katika Dini Yako)." [At-Tirmidhiy, na akasema ni Hadiyth Hasan]
Hadiyth – 26
وعن أَبي الدرداءِ رَضِيَ اللهُ عنه قَالَ : قَالَ رسُولُ الله صلى الله عليه وسلم : (( كَانَ مِنْ دُعاءِ دَاوُدَ : اللَّهُمَّ إنِّي أسْألُكَ حُبَّكَ ، وَحُبَّ مَنْ يُحِبُّكَ ، وَالعَمَلَ الَّذِي يُبَلِّغُنِي حُبَّكَ ، اللَّهُمَّ اجْعَلْ حُبَّكَ أحَبَّ إلَيَّ مِنْ نَفْسِي ، وأهْلِي ، وَمِنَ الماءِ البارِدِ )) . رواه الترمذي ، وقال : (( حديث حسن )) .
Imepokewa kutoka kwa Abid Dardaa (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Ilikuwa miongoni mwa duaa za Daawuwd: Allaahumma inniy asalika hubbaka wa hubba man yuhibbuka wal 'amalal ladhiy yuballighuniy hubbaka. Allaahumma j'al hubbaka ahabba ilayya min nafsiy wa ahliy wa minal maail baarid (Rabb Wangu! Hakika mimi nakuomba mapenzi Yako, na mapenzi ya wale Unao wapenda na amali ambayo itanifikisha kwa mapenzi Yako. Rabb Wangu! Yafanye mapenzi yangu Kwako ni mahububu zaidi kwangu kuliko nafsi yangu, na familia yangu na maji baridi)." [At-Tirmidhiy, na akasema ni Hadiyth Hasan]
Hadiyth – 27
وعن أنس رَضِيَ اللهُ عنه قَالَ : قَالَ رسُولُ الله صلى الله عليه وسلم : (( ألِظُّوا بـ ( يَاذا الجَلاَلِ والإكْرامِ ) )) . رواه الترمذي ، ورواه النسائي من رواية ربيعة بن عامِرٍ الصحابي ، قَالَ الحاكم : (( حديث صحيح الإسناد )) .
Imepokewa kutoka kwa Anas (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Jilazimisheni na mukariri sana maneno ya Yaadhal Jalaali wal Ikraam (Umetukuka Ee Mwenye Enzi na Mwenye Kustahiki Kuheshimika)." [At-Tirmidhiy na An-Nasaaiy kwa riwaayaah ya Rabi'ah bin 'Aamir, ambaye ni Swahaaba. Amesema Al-Haakim: Isnaad yake ni Swahiyh]
Hadiyth – 28
وعن أَبي أُمَامَةَ رَضِيَ اللهُ عنه قَالَ : دعا رسُولُ الله صلى الله عليه وسلم ، بدُعاءٍ كَثيرٍ ، لَمْ نَحْفَظْ مِنْهُ شَيْئاً ؛ قُلْنَا : يَا رسول الله ، دَعَوْتَ بِدُعاءٍ كَثِيرٍ لَمْ نَحْفَظْ مِنْهُ شَيْئاً ، فَقَالَ : (( ألا أدُلُّكُمْ عَلَى مَا يَجْمَعُ ذَلِكَ كُلَّهُ ؟ تقول : اللَّهُمَّ إنِّي أسَألُكَ مِنْ خَيْر مَا سَأَلَكَ مِنْهُ نَبِيُّكَ محمَّدٌ صلى الله عليه وسلم ؛ وأعوذُ بِكَ مِنْ شَرِّ مَا استَعَاذَ مِنْهُ نَبِيُّكَ مُحَمَّدٌ صلى الله عليه وسلم، وأنتَ المُسْتَعانُ ، وَعَليْكَ البَلاَغُ ، وَلاَ حَولَ وَلاَ قُوَّةَ إِلاَّ باللهِ )) . رواه الترمذي ، وقال : (( حديث حسن )) .
Amesema abu Umamah (Radhwiya Allaahu 'anhu): Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) aliomba duaa nyingi sana ambazo hatukuweza kuzihifadhi, hivyo tukamwambia: "Ee Rasuli wa Allaah! Umeomba duaa nyingi ambazo hatukuhifadhi humo chochote." Akasema: "Siwaonyeshi nyinyi duaa ambayo itajumlisha hizo zote? Semeni: Allaahumma inniy asaluka min khayri maa saalaka minhu Nabiyyuka Muhammadun (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) wa a'uwdhu bika min sharri masta'adha minhu Nabiyyuka Muhammadun (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) wa Antal Musta'aanu wa 'alaykal balaaghu walaa hawla walaa quwwata illaa BiLLaahi (Rabb Wangu! Hakika mimi nakuomba alicho kuomba Nabiy Wako Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) na ninajilinda Kwako na uovu alioomba ulinzi kwayo Nabiy Wako Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam). Na Wewe tu Ndiye Msaidizi wa pekee wa kuombwa msaada na Kwako ndio tunatarajia kuitikiwa maombi yetu. Na hapana hila wala nguvu isipokuwa kupitia kwa Allaah)." [At-Tirmidhiy, na akasema ni Hadiyth Hasan]
Hadiyth – 29
وعن ابن مسعود رَضِيَ اللهُ عنه قَالَ : كَانَ من دعاءِ رسُولِ الله صلى الله عليه وسلم : (( اللَّهُمَّ إنِّي أسْألُكَ مُوجِبَاتِ رَحْمَتِكَ، وَعَزَائِمَ مَغْفِرَتِكَ، والسَّلامَةَ مِنْ كُلِّ إثْمٍ، والغَنِيمَةَ مِنْ كُلِّ بِرٍّ ، والفَوْزَ بالجَنَّةِ ، والنَّجَاةَ مِنَ النَّارِ )) . رواه الحاكم أَبُو عبد الله ، وقال : (( حديث صحيح عَلَى شرط مسلمٍ )) .
Amesema Ibn Mas'uwd (Radhwiya Allaahu 'anhu): Miongoni mwa duaa za Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ni: Allaahumma inniy asaluka muujibaati Rahmatika wa 'azaaima Maghfiratika was Salaamata min kulli birrin wal fawza bil jannati wan najaata minan naar (Rabb Wangu! Hakika mimi nakuomba unipatie Rehema Zako Maghfira Yako na Unipatie ngawira kwa kukutii kwa kila jambo na kufuzu kupata pepo na Kuniokoa na Moto)." [Al-Haakim Abu 'Abdillaah, na akasema hii ni Hadiyth Swahiyh kulingana na mashartiyaliyowekwa na Muslim]
Riyaadhw Asw-Swaalihiyn
باب فضل الدعاء بظهر الغيب
02-Mlango Wa Fadhila za Kuwaombea Wasio Kuwepo
Alhidaaya.com [4]
قال الله تَعَالَى :
وَالَّذِينَ جَاءُوا مِن بَعْدِهِمْ يَقُولُونَ رَبَّنَا اغْفِرْ لَنَا وَلِإِخْوَانِنَا الَّذِينَ سَبَقُونَا بِالْإِيمَانِ ﴿١٠﴾
Na wale waliokuja baada yao wanasema: Rabb wetu! Tughufurie pamoja na ndugu zetu ambao wametutangulia kwa iymaan. [Al-Hashr: 10]
وَاسْتَغْفِرْ لِذَنبِكَ وَلِلْمُؤْمِنِينَ وَالْمُؤْمِنَاتِ ۗ ﴿١٩﴾
Na omba Maghfirah kwa dhambi zako na kwa ajili ya Waumini wa kiume na Waumini wa kike. [Muhammad: 19]
رَبَّنَا اغْفِرْ لِي وَلِوَالِدَيَّ وَلِلْمُؤْمِنِينَ يَوْمَ يَقُومُ الْحِسَابُ ﴿٤١﴾
Rabb wetu! Nighufurie mimi na wazazi wangu wawili na Waumini Siku itakayosimama hesabu. [Ibraahiym: 41]
Hadiyth – 1
وعن أَبي الدرداء رضي اللهُ عنه : أنَّه سَمِعَ رسولَ الله صلى الله عليه وسلم يقول : (( مَا مِنْ عَبْدٍ مُسْلمٍ يدعُو لأَخِيهِ بِظَهْرِ الغَيْبِ إِلاَّ قَالَ المَلَكُ : وَلَكَ بِمِثْلٍ )) . رواه مسلم .
Imepokewa kutoka kwa Abu Dardaa (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba amemsikia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akisema: "Hakuna mja yeyote Muislamu anamuombea ndugu yake asiye kuwepo isipokuwa Malaaikah anasema, nawe ana mfano wa hayo." [Muslim]
Hadiyth – 2
وعن أَبي الدرداء رضي اللهُ عنه : أنَّ رسُولَ الله صلى الله عليه وسلم كَانَ يقول : (( دَعْوَةُ المَرْءِ المُسْلِمِ لأَخيهِ بِظَهْرِ الغَيْبِ مُسْتَجَابَةٌ ، عِنْدَ رَأسِهِ مَلَكٌ مُوَكَّلٌ كُلَّمَا دَعَا لأَخِيهِ بِخَيْرٍ قَالَ المَلَكُ المُوَكَّلُ بِهِ : آمِينَ ، وَلَكَ بِمِثْلٍ )) . رواه مسلم .
Imepokewa kutoka kwa Abu Dardaa (Radhwiya Allaahu 'anhu) kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akisema: "Duaa ya mtu Muislamu kwa nduguye asiye kuwepo inakubaliwa kwani Malaaikah anawakilishwa kuwa naye, kila anapomuombea ndugu yake kwa kheri husema yule Malaaikah aliyewakilishwa kwake: Aamiyn (iwe hivyo), nawe upate mfano wa hayo (unayomuombea ndugu yako)." [Muslim]
Riyaadhw Asw-Swaalihiyn
باب في مسائل من الدعاء
03-Mlango Wa Katika Mas-ala ya Duaa
Alhidaaya.com [4]
Hadiyth – 1
وعن أسَامة بن زيد رضي الله عنهما ، قَالَ : قَالَ رسُولُ الله صلى الله عليه وسلم : (( مَنْ صُنِعَ إِلَيْهِ مَعْرُوفٌ، فَقَالَ لِفاعِلهِ : جَزَاكَ اللهُ خَيراً ، فَقَدْ أبْلَغَ فِي الثَّنَاءِ )) . رواه الترمذي ، وقال : (( حديث حسن صحيح )) .
Imepokewa kutoka kwa Usaamah bin Zayd (Radhwiya Allaahu 'anhumaa) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Mwenye kufanyiwa wema akamwambia kwa aliyefanyia: 'Jazaaka Allaahu Khayran (Allaah akijazi kila la kheri)', hakika amefika kilele cha kumsifu na kumshukuru muhisani wake." [At-Tirmidhiy, na akasema ni Hadiyth Hasan Swahiyh]
Hadiyth – 2
وعن جابر رضي الله عنه قَالَ : قَالَ رسُولُ الله صلى الله عليه وسلم : (( لا تَدْعُوا عَلَى أَنْفُسِكُمْ ؛ وَلاَ تَدعُوا عَلَى أوْلادِكُمْ ، وَلاَ تَدْعُوا عَلَى أموَالِكُمْ ، لا تُوافِقُوا مِنَ اللهِ سَاعَةً يُسألُ فِيهَا عَطَاءً فَيَسْتَجِيبَ لَكُمْ )) . رواه مسلم .
Imepokewa kutoka kwa Jaabir (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Msijiombee dhidi ya nafsi zenu wala dhidi ya watoto wenu wala dhidi ya mali zenu, kwani inaweza kuafiki saa ambayo duaa hukubaliwa na Allaah, hivyo mkawa ni wenye kujibiwa." [Muslim]
Hadiyth – 3
وعن أَبي هريرة رضي الله عنه : أنَّ رسولَ اللهِ صلى الله عليه وسلم قَالَ : (( أقْرَبُ مَا يكونُ العَبْدُ مِنْ رَبِّهِ وَهُوَ سَاجِدٌ ، فَأكْثِرُوا الدُّعَاءَ )) رواه مسلم .
Imepokewa kutoka kwa Abu Huraiyrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Mja anakuwa karibu sana na Rabb wake akiwa katika sijdah, hivyo jitahidini na ongezeni duaa (katika hali hiyo ya sijdah)." [Muslim]
Hadiyth – 4
وعن أَبي هريرة رضي الله عنه : أنَّ رسُولَ الله صلى الله عليه وسلم قَالَ : (( يُسْتَجَابُ لأَحَدِكُمْ مَا لَمْ يَعْجَلْ : يقُولُ : قَدْ دَعْوتُ رَبِّي ، فَلَمْ يسْتَجب لِي )) متفق عَلَيْهِ .
وفي روايةٍ لمسلمٍ : (( لا يَزالُ يُسْتَجَابُ لِلعَبْدِ مَا لَمْ يَدْعُ بإثْمٍ ، أَوْ قَطيعَةِ رحِمٍ ، مَا لَمْ يَسْتَعْجِلْ )) قيل : يَا رسولَ اللهِ مَا الاستعجال ؟ قَالَ : (( يقول : قَدْ دَعوْتُ ، وَقَدْ دَعَوْتُ ، فَلَمْ أرَ يسْتَجِبُ لي ، فَيَسْتحْسِرُ عِنْدَ ذَلِكَ وَيَدَعُ الدُّعَاءَ))
Imepokewa kutoka kwa Abu Huraiyrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Atajibiwa mmoja wenu kwa muda wa kutokuwa na haraka, kwa kusema: 'Nimemuomba Rabb wangu wala sikujibiwa." [Al-Bukhaariy, Muslim, Abu Daawuwd na At-Tirmidhiy]
Na ktika riwaayah ya Muslim: "Huendelea kujibiwa mja maadamu hataomba jambo la madhambi au kukata uhusiano wa kindugu na maadamu hatafanya haraka." Akaulizwa: "Ee Rasuli wa Allaah! Ni nini maana ya kufanya haraka?" Akasema: "Ni kusema: Hakika nimeomba, hakika nimeomba, wala sioni kujibiwa. Hivyo, anakufa moyo na kuacha wakati huo kuomba duaa."
Hadiyth – 5
وعن أَبي أمامة رضي الله عنه قَالَ : قيل لِرسولِ اللهِ صلى الله عليه وسلم : أيُّ الدُّعاءِ أَسْمَعُ ؟ قَالَ : (( جَوْفَ اللَّيْلِ الآخِرِ ، وَدُبُرَ الصَّلَواتِ المَكْتُوباتِ )) . رواه الترمذي ،وقال : (( حديث حسن )) .
Amesema Abu Umamah (Radhwiya Allaahu 'anhu): Aliulizwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam): "Ni duaa gani inayo sikilizwa (na kujibiwa)?" Akasema: "Ni ile inayoombwa usiku wa manane na baada ya kila Swalaah ya faradhi." [At-Tirmidhiy, na akasema ni Hadiyth Hasan]
Hadiyth – 6
وعن عُبَادَةَ بنِ الصامت رضي الله عنه : أنَّ رسولَ اللهِ صلى الله عليه وسلم قَالَ : (( مَا عَلَى الأرْضِ مُسْلِمٌ يَدْعُو الله تَعَالَى بِدَعْوَةٍ إِلاَّ آتَاهُ اللهُ إيَّاها ، أَوْ صَرفَ عَنْهُ مِنَ السُّوءِ مِثْلَهَا ، مَا لَمْ يَدْعُ بإثْمٍ ، أَوْ قَطِيعَةِ رَحِمٍ )) ، فَقَالَ رَجُلٌ مِنَ القَومِ : إِذاً نُكْثِرُ قَالَ : (( اللهُ أكْثَرُ )) . رواه الترمذي ، وقال : (( حديث حسن صحيح )) .
ورواه الحاكم من روايةِ أَبي سعيدٍ وزاد فِيهِ : (( أَوْ يَدخِرَ لَهُ مِن الأَجْرِ مثْلَها )) .
Imepokewa kutoka kwa 'Ubadah bin Swaamit (Radhwiya Allaahu 'anhu) kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Hapana katika ardhi Muislamu ambaye anamuomba Allaah Ta'aalaa kwa ombi isipokuwa Allaah Humpatia au Humuondoshea jambo baya mfano wake maadamu hataomba jambo la madhambi au kukata undugu." Akasema mtu miongoni mwa waliokuwa katika kikao: "Basi, tuombe zaidi." Akasema: "Allaah, ni Mkarimu zaidi." [At-Tirmidhiy, na akasema ni Hadiyth Hasan Swahiyh]
Na pia ameipokea Al-Haakim kutoka kwa riwaayah ya Abu Sa'iyd, na akaongeza ndani yake: "Au humukea malipo sawa na duaa yake mpaka Siku ya Malipo."
Hadiyth – 7
وعن ابنِ عباس رضي الله عنهما : أنَّ رسولَ الله صلى الله عليه وسلم كَانَ يقولُ عِنْدَ الكَرْبِ : (( لا إلهَ إِلاَّ اللهُ العَظِيمُ الحَليمُ ، لا إلهَ إِلاَّ اللهُ رَبُّ العَرْشِ العَظيمِ ، لاَ إلهَ إِلاَّ اللهُ رَبُّ السَّمَاواتِ، وَرَبُّ الأَرْضِ، وَرَبُّ العَرْشِ الكَرِيمِ )) متفق عَلَيْهِ .
Imepokewa kutoka kwa Ibn 'Abbaas (Radhwiya Allaahu 'anhumaa) kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) wakati wa matatizo alikuwa anasema: "Laa ilaaha illaa Allaahul 'Adhwiymul Haliym. Laa ilaaha illaa Allaahu Rabbul 'Arshil 'Adhwiym. Laa ilaaha illaa Allaahu Rabbus Samaawaati wa Rabbul ardhi wa Rabbul 'Arshil Kariym (Hapana Mola wa kuabudiwa isipokuwa Allaah Aliye Mtukufu Mpole sana. Hapana Mola wa kuabudiwa isipokuwa Allaah Rabb wa kiti cha enzi kitukufu. Hapana Mola wa kuabudiwa isipokuwa Allaah Rabb wa mbingu na Rabb wa kiti cha enzi cha heshima)." [Al-Bukhaariy na Muslim]
Riyaadhw Asw-Swaalihiyn
باب كرامات الأولياء وفضلهم
04-Mlango Wa Karama za Mawalii na Fadhila Zao
Alhidaaya.com [4]
قال الله تَعَالَى :
أَلَا إِنَّ أَوْلِيَاءَ اللَّـهِ لَا خَوْفٌ عَلَيْهِمْ وَلَا هُمْ يَحْزَنُونَ﴿٦٢﴾
Tanabahi! Hakika Vipenzi wa Allaah hawana khofu na wala hawatohuzunika.
الَّذِينَ آمَنُوا وَكَانُوا يَتَّقُونَ﴿٦٣﴾
Ambao wameamini na wakawa wana taqwa.
لَهُمُ الْبُشْرَىٰ فِي الْحَيَاةِ الدُّنْيَا وَفِي الْآخِرَةِ ۚ لَا تَبْدِيلَ لِكَلِمَاتِ اللَّـهِ ۚ ذَٰلِكَ هُوَ الْفَوْزُ الْعَظِيمُ﴿٦٤﴾
Watapata bishara katika uhai wa dunia na katika Aakhirah. Hakuna mabadiliko katika Maneno ya Allaah. Huko ndiko kufuzu adhimu. [Yuwnus: 62-64]
وَهُزِّي إِلَيْكِ بِجِذْعِ النَّخْلَةِ تُسَاقِطْ عَلَيْكِ رُطَبًا جَنِيًّا ﴿٢٥﴾
Na tingisha kuelekea kwako shina la mtende, litakuangushia tende safi zilizoiva na zilizo tayari kuchumwa.
فَكُلِي وَاشْرَبِي وَقَرِّي عَيْنًا ۖ ﴿٢٦﴾
Basi kula na kunywa. [Maryam: 25-26]
كُلَّمَا دَخَلَ عَلَيْهَا زَكَرِيَّا الْمِحْرَابَ وَجَدَ عِندَهَا رِزْقًا ۖ قَالَ يَا مَرْيَمُ أَنَّىٰ لَكِ هَـٰذَا ۖ قَالَتْ هُوَ مِنْ عِندِ اللَّـهِ ۖ إِنَّ اللَّـهَ يَرْزُقُ مَن يَشَاءُ بِغَيْرِ حِسَابٍ ﴿٣٧﴾
Kila Zakariyyaa alipoingia kwake katika chumba cha kuswalia alikuta kwake vyakula. Akasema: Ee Maryam! Umepata wapi hivi? Akasema: Hivi ni kutoka kwa Allaah. Hakika Allaah Anamruzuku Amtakaye bila ya hesabu. [Aal-'Imraan: 37]
وَإِذِ اعْتَزَلْتُمُوهُمْ وَمَا يَعْبُدُونَ إِلَّا اللَّـهَ فَأْوُوا إِلَى الْكَهْفِ يَنشُرْ لَكُمْ رَبُّكُم مِّن رَّحْمَتِهِ وَيُهَيِّئْ لَكُم مِّنْ أَمْرِكُم مِّرْفَقًا ﴿١٦﴾
Na mkijitenga nao na vile wanavyoviabudu badala ya Allaah, basi kimbilieni pangoni. Rabb wenu Atakufungulieni Rahmah Zake, na Atakutengenezeeni wepesi katika mambo yenu.
وَتَرَى الشَّمْسَ إِذَا طَلَعَت تَّزَاوَرُ عَن كَهْفِهِمْ ذَاتَ الْيَمِينِ وَإِذَا غَرَبَت تَّقْرِضُهُمْ ذَاتَ الشِّمَالِ ﴿١٧﴾
Na (ungeliwaona basi ungelikuwa) unaliona jua linapochomoza linaelemea pango lao kwa upande wa kulia, na linapokuchwa linawakwepa upande wa kushoto [Al-Kahf: 16-17]
Hadiyth – 1
وعن أَبي محمد عبد الرحمان بن أَبي بكرٍ الصديق رضي الله عنهما : أنَّ أَصْحَابَ الصُّفّةِ كَانُوا أُنَاساً فُقَرَاءَ وَأَنَّ النَّبيَّ صلى الله عليه وسلم قَالَ مَرَّةً : (( مَنْ كَانَ عِنْدَهُ طَعَامُ اثْنَيْنِ ، فَلْيَذْهَبْ بثَالِثٍ ، وَمنْ كَانَ عِنْدَهُ طَعَامُ أرْبَعَةٍ ، فَلْيَذْهَبْ بِخَامِسٍ بِسَادِسٍ )) أَوْ كما قَالَ ، وأنَّ أَبَا بكرٍ رضي اللهُ عنه ، جَاءَ بِثَلاَثَةٍ ، وانْطَلَقَ النبيّ صلى الله عليه وسلم بعَشَرَةٍ ، وأنَّ أَبَا بَكرٍ تَعَشَّى عِنْدَ النبيّ صلى الله عليه وسلم ، ثُمَّ لَبِثَ حَتَّى صَلَّى العِشَاءَ ، ثُمَّ رَجَعَ ، فجاءَ بَعْدَ مَا مَضَى مِنَ اللَّيْلِ مَا شَاءَ اللهُ . قالت امْرَأتُهُ : مَا حَبَسَكَ عَنْ أضْيَافِكَ ؟ قَالَ : أوَما عَشَّيْتِهمْ ؟ قالت: أَبَوْا حَتَّى تَجِيءَ وَقَدْ عَرَضُوا عَلَيْهِمْ ، قَالَ : فَذَهَبتُ أَنَا فَاخْتَبَأْتُ ، فَقالَ : يَا غُنْثَرُ ، فَجَدَّعَ وَسَبَّ ، وقالَ : كُلُوا لاَ هَنِيئاً وَاللهِ لا أَطْعَمُهُ أَبَداً ، قَالَ : وايْمُ اللهِ مَا كُنَّا نَأخُذُ مِنْ لُقْمَةٍ إلا ربا من أسفلِها أكثرَ منها حتى شبعوا ، وصارتْ أكثرَ مما كانتْ قبلَ ذلكَ ، فنظرَ إليها أبو بكر فقالَ لامرأتِهِ : يا أختَ بني فراسٍ ما هذا ؟ قالت : لا وقُرَّةِ عيني لهي الآنَ أكثرُ منها قبلَ ذلكَ بثلاثِ مراتٍ ! فأكل منها أبو بكرٍ وقال : إنَّما كانَ ذلكَ من الشيطانِ ، يعني : يمينَهُ . ثم أكلَ منها لقمةً ، ثُمَّ حَمَلَهَا إِلَى النَّبيِّ صلى الله عليه وسلم فَأَصْبَحَتْ عِنْدَهُ. وَكَانَ بَيْنَنَا وَبَيْنَ قَوْمٍ عَهْدٌ، فَمَضَى الأجَلُ ، فَتَفَرَّقْنَا اثْنَيْ عَشَرَ رَجُلاً ، مَعَ كُلِّ رَجُلٍ مِنْهُمْ أُنَاسٌ ، اللهُ أعْلَمُ كَمْ مَعَ كُلِّ رَجُلٍ فَأَكَلُوا مِنْهَا أَجْمَعُونَ .
وَفِي رِوَايةٍ : فَحَلَفَ أَبُو بَكْرٍ لا يَطْعَمُهُ ، فَحَلَفَت المَرْأَةُ لا تَطْعَمُهُ ، فَحَلَفَ الضَّيْفُ . - أَو الأَضْيَافُ - أنْ لاَ يَطْعَمُهُ أَوْ يَطْعَمُوهُ حَتَّى يَطْعَمَهُ . فَقَالَ أَبُو بَكْرٍ : هذِهِ مِنَ الشَّيْطَانِ ! فَدَعَا بالطَّعَامِ فَأكَلَ وأكَلُوا ، فَجَعَلُوا لا يَرْفَعُونَ لُقْمَةً إِلاَّ رَبَتْ مِنْ أسْفَلِهَا أَكْثَرُ مِنْهَا ، فَقَالَ : يَا أُخْتَ بَني فِرَاسٍ ، مَا هَذَا ؟ فَقَالَتْ : وَقُرْةِ عَيْنِي إنَّهَا الآنَ لأَكْثَرُ مِنْهَا قَبْلَ أنْ نَأكُلَ ، فَأكَلُوا ، وَبَعَثَ بِهَا إِلَى النَّبيِّ صلى الله عليه وسلم ، فَذَكَرَ أنَّهُ أكَلَ مِنْهَا .
وَفِي رِوايَةٍ : إنَّ أَبَا بكْرٍ قَالَ لِعَبْدِ الرَّحْمانِ : دُونَكَ أضْيَافَكَ ، فَإنِّي مُنْطلقٌ إِلَى النَّبيِّ صلى الله عليه وسلم ، فَافْرُغْ مِنْ قِراهُم قَبْلَ أنْ أَجِيءَ ، فَانْطَلَقَ عَبْدُ الرَّحْمانِ ، فَأَتَاهُمْ بما عِنْدَهُ ، فَقَالَ : اطْعَمُوا ؛ فقالوا : أين رَبُّ مَنْزِلِنا ؟ قَالَ : اطْعَمُوا ، قالوا : مَا نحنُ بِاكِلِينَ حَتَّى يَجِيءَ رَبُّ مَنْزِلِنَا ، قَالَ : اقْبَلُوا عَنْا قِرَاكُمْ ، فَإنَّهُ إنْ جَاءَ وَلَمْ تَطْعَمُوا ، لَنَلْقَيَنَّ مِنْهُ فأبَوْا ، فَعَرَفْتُ أنَّهُ يَجِدُ عَلَيَّ ، فَلَمَّا جَاءَ تَنَحَّيْتُ عَنْهُ ، فَقَالَ : مَا صَنَعْتُمْ ؟ فَأخْبَرُوهُ ، فَقَالَ : يَا عَبْدَ الرَّحمانِ ، فَسَكَتُّ : ثُمَّ قَالَ : يَا عَبْدَ الرَّحْمانِ ، فَسَكَتُّ ، فَقَالَ: يَا غُنْثَرُ أقْسَمْتُ عَلَيْكَ إنْ كُنْتَ تَسْمَعُ صَوتِي لَمَا جِئْتَ ! فَخَرَجْتُ ، فَقُلْتُ : سَلْ أضْيَافَكَ ، فقالُوا : صَدَقَ ، أتَانَا بِهِ ، فَقَالَ : إنَّمَا انْتَظَرْتُمُونِي والله لا أَطْعَمُهُ اللَّيْلَةَ . فَقَالَ الآخَرُونَ : واللهِ لا نَطْعَمُهُ حَتَّى تَطْعَمَهُ فَقَالَ : وَيْلَكُمْ مَا لَكُمْ لا تَقْبَلُونَ عَنَّا قِرَاكُمْ ؟ هَاتِ طَعَامَكَ ، فَجَاءَ بِهِ ، فَوَضَعَ يَدَهُ فَقَالَ : بِسْمِ اللهِ ، الأولَى مِنَ الشَّيْطَانِ ، فَأَكَلَ وَأَكَلُوا . متفق عَلَيْهِ
Kutoka kwa Abu Muhammad Abdur-Rahmaan bin Abu Bakar As-Swiddiq (Radhwiya Allaahu 'anhumaa) kuwa watu wa Suffah walikuwa ni watu mafakiri na Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Mwenye chakula cha kuwatosha watu wawili aende naye watatu (katika hao watu wa Suffah), na kama cha wanne aende naye wa tano au sita." Au kama alivyosema. Na Abu Bakar (Radhwiya Allaahu 'anhu) alichukua watu watatu na Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akaondoka na watu kumi. Abu Bakar (Radhwiya Allaahu 'anhu) alikula chakula cha jioni kwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam), kisha akabaki hadi iliposwaliwa Ishaa, kisha akarudi akabaki na Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam). Akaja nyumbani baada ya kupita usiku muda alioutaka Allaah. Mkewe akamuuliza: "Nini kilicho kuchelewesha ukawaacha wageni wako?" Akamjibu: "Kwani hukuwapa chakula cha jioni?" Mkewe akajibu: "Wamepewa wakakataa kula mpaka ufike." Abdur-Rahmaan akasema: "Mimi nikaenda kujificha, (kwa kumuogopa Abu Bakar) wakati huo huo akaniita, akasema: 'We mpumbavu!' na akanitukana na akaniambia, 'Kula, hufai kukaribishwa. Wa-Allaahi! Sili kabisa kwa yamini ya Allaah." Hatukuwa tunachukuwa tonge isipokuwa kilicho kuwa chini yake kilizidi zaidi ya kilichokuwepo. Tulikula hadi tukashiba, lakini chakula kikawa kimebaki kuliko vile kilivyokuwa kabla ya kuliwa. Abu Bakar akakiangalia akakikuta kama kilivyo kuwa au zaidi. Akamuuliza mkewe: "Ee dada wa Bani Firas! Nini hiki?" Mkewe akajibu: "Sielewi, naapa kwa tulizo la jicho langu! Hivi sasa ni kinga zaidi ya kilivyo kuwa kwa mara tatu." Abu Bakr akala, kisha akasema: "Hakika si vingine bali ile ilikuwa kutokana na shetani, akikusudia ile yamini yake." Kisha akala katika chakula hicho tonge moja kisha akakipeleka kwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam), kikaamkia kwake. Kulikuwa na mkataba kati yetu na watu fulani, muda ukapita Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akatugawa katika makundi ya watu kumi na wawili, kila kimoja kikaongozwa na mtu mmoja. Allaah Ndiye Anayejua ni wangapi katika watu hao walioongoza na kiongozi mmoja? Wakala chakula hicho wote."
Na katika riwaayah nyengine: "Abu Bakar aliapa kuwa hatakula, na mkewe pia naye akaapa kuwa hatakula na akaapa mgeni au wageni kuwa naye hatakua au hawatakula mpaka ale (Abu Bakar). Akasema Abu Bakar: 'Hii ni kutokana na shetani.' Akaitisha chakula, akala na wote wakala. Hatukuwa tunachukuwa tonge isipokuwa kilicho kuwa chini yake kilizidi zaidi ya (kilichokuwepo). Akamuuliza mkewe: 'Ee dada wa Bani Firas! Nini hiki?' Mkewe akajibu: 'Naapa kwa tulizo la jicho langu! Hivi sasa ni kinga zaidi ya kilivyo kuwa kabla hatujala.' Wakala na akakipeleka kwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam). ambaye alieleza kuwa alikula kutoka kwa hicho chakula."
Na katika riwaayah nyingine: Hakika Abu Bakar alimwambia Abdur-Rahman: "Washughulikie wageni wako kwani mimi ninakwenda kwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na uwalishe vyema kabla sijarudi." Hivyo Abdur-Rahmaan aliondoka na kuwaletea chakula walichokuwa nacho na kuwaambia: :kuleni." Wakasema: "Yu wapi mwenye nyumba?" Akawaambia: "Kuleni." Wakasema: "Sisi hatuli mpaka afike mwenye nyumba." Akawaambia: "Tafadhali kubalini ukarimu wetu na mule (chakula), kwani atakaporudi na kukuta hamjakula atakasirika sana." Lakini wageni walikataa katakata. Nikajua kuwa atakaporudi atakasirika akiona wageni hawajakula. Aliporudi nilijificha (ili asinipate), naye akasema: "Je, mumewafanyia nini wageni?" Wakampasha habari ya yaliotokea (yaani wageni kukataa kula), na hapo akaita: "Ee Abdur-Rahmaan." Nami nikanyamaza kimya. Kisha akaita tena: "Ee Abdur-Rahmaan", nami nikakaa kimya. Hapo akasema: "Ee mpumbavu! Ninaapa kuwa lau wanisikia basi utakuja hapa." Hapo nikatoka na kumwambia: "Waulize wageni wako." Nao wakasema: "Anasema kweli, kwani alikuja na chakula." Hapo Abu Bakar (Radhwiya Allaahu 'anhu) akasema: "Hakika nyinyi mumeningojea mimi bila ya udhuru wowote, Wa-Allaahi sitakula chakula usiku wa leo." Wakasema wengine: "Wa-Allaahi! Nasi hatutakula mpaka nawe ule chakula hiki." Akasema: "Ole wenu! Muna nini mbona munakataa ukarimu wetu? Leteni chakula." Kikaletwa chakula, naye (Abu Bakr) akaingiza mkono wake na kusema: "BismiLLaahi! Kiapo changu kilikuwa ni kutokana na shetani." Hivyo, yeye na kutokana na wageni wake wakala chakula hicho." [Al-Bukhaariy, Muslim na Ahmad]
Hadiyth – 2
وعن أَبي هريرة رضي اللهُ عنه قَالَ : قَالَ رسول الله صلى الله عليه وسلم : (( لَقَدْ كَانَ فيما قَبْلَكُمْ مِنَ الأُمَمِ نَاسٌ مُحَدَّثُونَ، فَإنْ يَكُ في أُمَّتِي أحدٌ فإنَّهُ عُمَرُ)) . رواه البخاري.
ورواه مسلم من رواية عائشة .
وفي روايتهما قَالَ ابن وهب : (( محَدَّثُونَ )) أيْ مُلْهَمُونَ .
Imepokewa kutoka kwa Abu Huraiyrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Hakika kulikuwa katika waliokuwa kabla yenu watu Muhaddathuwn (wanasema maneno yanayowafikiana na haki). Hivyo, kukiwa katika ummah wangu yeyote mwenye sifa hiyo basi ni 'Umar." [Al-Bukhaariy, na imepokewa na muslim kutoka riwaayah ya 'Aaishah (Radhwiya Allaahu 'anhaa)].
Hadiyth – 3
وعن جابر بنِ سُمْرَةَ رضي الله عنهما ، قَالَ : شَكَا أهْلُ الكُوفَةِ سَعْداً يعني : ابنَ أَبي وقاص رضي اللهُ عنه ، إِلَى عمر بن الخطاب رضي اللهُ عنه فَعَزَلَهُ ، واسْتَعْمَلَ عَلَيْهِمْ عَمَّاراً ، فَشَكَوا حَتَّى ذَكَرُوا أنَّهُ لا يُحْسِنُ يُصَلِّي ، فَأَرْسَلَ إِلَيْهِ ، فَقَالَ : يَا أَبَا إسْحَاقَ ، إنَّ هَؤُلاَءِ يَزْعَمُونَ أنَّكَ لا تُحْسِنُ تُصَلِّي ، فَقَالَ : أَمَّا أنا واللهِ فَإنِّي كُنْتُ أُصَلِّي بِهِمْ صَلاَةَ رسولِ الله صلى الله عليه وسلم ، لا أُخْرِمُ عَنْها ، أُصَلِّي صَلاَتَي العِشَاءِ فَأَرْكُدُ فِي الأُولَيَيْنِ ، وَأُخِفُّ في الأُخْرَيَيْنِ . قَالَ : ذَلِكَ الظَّنُّ بِكَ يَا أَبَا إسْحَاقَ ، وأَرْسَلَ مَعَهُ رَجُلاً - أَوْ رِجَالاً - إِلَى الكُوفَةِ يَسْأَلُ عَنْهُ أهْلَ الكُوفَةِ ، فَلَمْ يَدَعْ مَسْجِداً إِلاَّ سَأَلَ عَنْهُ ، وَيُثْنُونَ مَعْرُوفاً ، حَتَّى دَخَلَ مَسْجِداً لِبَنِي عَبْسٍ ، فَقَامَ رَجُلٌ مِنْهُمْ ، يُقالُ لَهُ أُسَامَةُ بْنُ قَتَادَةَ ، يُكَنَّى أَبَا سَعْدَةَ، فَقَالَ: أمَا إذْ نَشَدْتَنَا فَإنَّ سَعْداً كَانَ لا يَسِيرُ بالسَّرِيَّةِ وَلاَ يَقْسِمُ بالسَّوِيَّةِ ، وَلاَ يَعْدِلُ في القَضِيَّةِ . قَالَ سَعْدٌ : أمَا وَاللهِ لأَدْعُونَّ بِثَلاَثٍ : اللَّهُمَّ إنْ كَانَ عَبْدُكَ هَذَا كَاذِباً ، قَامَ رِيَاءً ، وَسُمْعَةً ، فَأَطِلْ عُمُرَهُ ، وَأَطِلْ فَقْرَهُ ، وَعَرِّضْهُ لِلْفِتَنِ . وَكَانَ بَعْدَ ذَلِكَ إِذَا سُئِلَ يَقُولُ : شَيْخٌ كَبيرٌ مَفْتُونٌ ، أَصَابَتْنِي دَعْوَةُ سَعْدٍ . قَالَ عَبدُ الملكِ بن عُمَيْرٍ الراوي عن جابرِ بنِ سَمُرَةَ : فَأنا رَأَيْتُهُ بَعْدُ قَدْ سَقَطَ حَاجِبَاهُ عَلَى عَيْنَيْهِ مِنَ الكِبَرِ ، وإنَّهُ لَيَتَعَرَّضُ لِلْجَوارِي فِي الطُّرُقِ فَيَغْمِزُهُنَّ . متفق عَلَيْهِ .
Amesema Jaabir bin Samurah (Radhwiya Allaahu 'anhumaa): Watu wa Kufah walimshitakia Sa'ad bin Abu Waqqaas (Radhwiya Allaahu 'anhu) ambaye alikuwa Iiwali wao kwa 'Umar bin Al-Khaattaab (Radhwiya Allaahu 'anhu). Akaondolewa na kuwekwa badala yake 'Ammaar (Radhwiya Allaahu 'anhu). Katika mashtaka yao walimshutuhumu kuwa Sa'ad haswalishi vizuri. 'Umar (Radhwiya Allaahu 'anhu)alimuita Sa'ad aje Madiynah, (alipofika) alimuuliza: "Ee Abu Ishaaq! Watu wa Kufah wanakushtaki kuwa wewe hujui kuswalisha vizuri." Akajibu: "Ama mimi Wa-Allaahi, nilikuwa nawaswalisha Swalaah ya Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) bila kubadilisha hata kidogo. Nilikuwa nawaswalisha Swalaah ya Ishaa, nikirefusha rakaa mbili za mwanzo na kuhafifisha rakaa mbili za mwisho." Akasema: "Hakika hiyo ndiyo iliyokuwa dhana yangu kwako, ee Abu Ishaaq." 'Umar (Radhwiya Allaahu 'anhu) alimtuma mtu mmoja au wawili pamoja naye kuelekea Kufah ili kuchunguza kuhusu mashtaka hayo kutoka kwa watu wa Kufah. Wachunguzi hawa walipita katika kila Msikiti na kuwauliza watu kuhusu Sa'ad na watu wote walimsifu kwa wema wake mpaka wakafika katika Msikiti wa Bani 'Abs. Na hapo alisimama mtu mmoja miongoni mwao, ambaye anaitwa Usamah bin Qataadah, aliyekuwa na kunyah ya Abu Sa'dah, akasema: "Ama mkiwa mnataka kauli yetu, basi jueni kuwa Sa'ad hashiriki katika Jihadi, wala hagawi ngawira sawasawa, wala hahukumu kwa uadilifu." Hapo akasema Sa'ad: "Ama Wa-Allaahi, nitakuombea juu ya mambo matatu: "Ee Rabb Wangu! Ikiwa mja Wako huyu ni muongo, amesimama kwa ajili ya kujionyesha na kupata umaarufu, Mrefushie umri wake, na Umzidishie ufukara wake na Mtie katika mitihani na fitna." Na alikuwa baada ya hapo akiulizwa kuhusu hali yake, husema: "Mzee mkongwe aliye fitinika, imenisibu mimi duaa ya Sa'ad." Amesema Abdul-Malik bin 'Umayr, mpokezi kutoka kwa Jaabir bin Samurah (Radhwiyah Allaahu 'anhu): "Hakika mimi nilimuona (huyu Usamah) baada ya nyusi zake kuanguka juu ya macho yake kwa sababu ya ukongwe. Na hakika yeye alikuwa akizurura barabarani huku akiwabembeleza na kuwatongoza wasichana." [Al-Bukhaariy na Muslim]
Hadiyth – 4
وعن عروة بن الزبير : أنَّ سعيد بن زيد بن عمرو بن نُفَيلٍ رضي اللهُ عنه ، خَاصَمَتْهُ أَرْوَى بِنْتُ أوْسٍ إِلَى مَرْوَانَ بْنِ الحَكَمِ ، وادَّعَتْ أنَّهُ أخَذَ شَيْئاً مِنْ أرْضِهَا ، فَقَالَ سعيدٌ : أنا كُنْتُ آخُذُ شَيئاً مِنْ أرْضِهَا بَعْدَ الَّذِي سَمِعْتُ مِنْ رسول الله صلى الله عليه وسلم !؟ قَالَ : مَاذَا سَمِعْتَ مِنْ رَسُولِ الله صلى الله عليه وسلم ؟ قَالَ : سَمِعْتُ رسولَ الله صلى الله عليه وسلم يقول : (( مَنْ أخَذَ شِبْراً مِنَ الأرْضِ ظُلْماً ، طُوِّقَهُ إِلَى سَبْعِ أرْضِينَ )) فَقَالَ لَهُ مَرْوَانُ : لا أسْألُكَ بَيِّنَةً بَعْدَ هَذَا ، فَقَالَ سعيد : اللَّهُمَّ إنْ كَانَتْ كاذِبَةً ، فَأعْمِ بَصَرَها ، وَاقْتُلْهَا في أرْضِها ، قَالَ : فَما ماتَتْ حَتَّى ذَهَبَ بَصَرُهَا ، وَبَيْنَما هِيَ تَمْشِي في أرْضِهَا إذ وَقَعَتْ في حُفْرَةٍ فَماتَتْ . متفق عَلَيْهِ .
وفي روايةٍ لِمُسْلِمٍ عن محمد بن زيد بن عبد الله بن عُمَرَ بِمَعْنَاهُ ، وأنه رآها عَمْيَاءَ تَلْتَمِسُ الجُدُرَ تقولُ : أصابَتْنِي دَعْوَةُ سَعيدٍ ، وأنَّها مَرَّتْ عَلَى بِئرٍ في الدَّارِ الَّتي خَاصَمَتْهُ فِيهَا ، فَوَقَعَتْ فِيهَا ، وكانتْ قَبْرَها .
Imepokewa kutoka kwa 'Urwah bin az-Zubayr kuwa Sa'iyd bin Zayd bin 'Amruw bin Nufayl (Radhwiya Allaahu 'anhu) alishtakiwa na Arwaa bint Aws kwa Marwaan bin al-Hakam, na kudai kuwa Sa'iyd amechukua sehemu ya ardhi yake. Akasema: "Nawezaje mimi kuchukua kipande cha ardhi yake baada ya kumsikia Rasuli wa Allaah?" Akamuuliza Marwaan: "Umemsikia nini Rasuli wa Allaah?" Akasema: "Nimemsikia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akisema: 'Mwenye kuchukua shibiri moja ya ardhi kwa dhulma, atafanywa avae mkufu wa ardhi saba." Akamwambia yeye Marwaan: "Sitokuomba ushahidi mwingine wowote baada ya huu." Sa'iyd akasema: "Ee Rabb Wangu! Ikiwa yeye (aliye leta madai) ni muongo basi mfanye kipofu na muue katika ardhi yake." Akasema: "Hakuaga dunia mpaka baada ya kuwa kipofu na alipokuwa anatembea katika ardhi yake alianguka kwenye shimo na kufariki." [Al-Bukhaariy na Muslim]
Na katika riwaayah ya Muslim kutoka kwa Muhammad bin Zayd bin 'Abdillaah bin 'Umar kwa maana yake kuwa alimuona huyu mwanamke akiwa kipofu akishika shika kuta huku akisema: "Imenipata mimi duaa ya Sa'iyd." Na wakati mmoja alipita kwenye kisima cha nyumba aliyozozana kwayo, akaanguka ndani yake na hilo ndilo likawa kaburi lake."
Hadiyth – 5
وعن جابر بن عبد الله رضي الله عنهما ، قَالَ : لَمَّا حَضَرَتْ أُحُدٌ دعَانِي أَبي من اللَّيلِ فَقَالَ : مَا أُرَاني إِلاَّ مَقْتُولاً في أوْلِ مَنْ يُقْتَلُ من أصْحَابِ النَّبيِّ صلى الله عليه وسلم ، وإنِّي لا أَتْرُكُ بَعْدِي أَعَزَّ عَلَيَّ مِنْكَ غَيْرَ نَفْسِ رسول الله صلى الله عليه وسلم ، وإنَّ عَلَيَّ دَيْناً فَاقْضِ ، وَاسْتَوْصِ بِأَخَوَاتِكَ خَيْراً ، فَأصْبَحْنَا ، فَكَانَ أَوَّلَ قَتِيلٍ ، وَدَفَنْتُ مَعَهُ آخَرَ في قَبْرِهِ ، ثُمَّ لَمْ تَطِبْ نَفْسِي أنْ أتْرُكَهُ مَعَ آخَرَ ، فَاسْتَخْرَجْتُهُ بَعْدَ سِتَّةِ أشْهُرٍ ، فإذا هُوَ كَيَوْمِ وَضَعْتُهُ غَيْرَ أُذنِهِ ، فَجَعَلْتُهُ في قَبْرٍ عَلَى حِدَةٍ . رواه البخاري .
Amesema Jaabir bin 'Abdillaah (Radhwiya Allaahu 'anhumaa): Baba yangu aliniita usiku kabla ya Vita vya Uhud, akaniambia: "Naona mimi nitakuwa wa kwanza miongoni mwa Swahaaba wa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kuuliwa kesho. Na hakika, mimi sijaacha kipenzi kwangu baada ya Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ila wewe. Na hakika mimi nina deni, hivyo lilipe na ninakuusia uwatendee wema dada zako." Kulipopambazuka (na vita kuanza, hakika akawa wa kwanza kufa shahidi na nikamzika pamoja na wengine katika kaburi moja. Kisha nafsi yangu haikupendelea kumuacha yeye (babangu) pamoja na wengine katika kaburi moja, hivyo nikamfukua baada ya miezi sita na kuukuta mwili wake katika hali ile ile aliyozikiwa nayo isipokuwa kovu (alama) iliyokuwa kwenye sikio lake. Nikauzika mwili wake katika kaburi jengine." [Al-Bukhaariy]
Hadiyth – 6
وعن أنس رضي اللهُ عنه : أنَّ رجلين مِنْ أصحاب النَّبيِّ صلى الله عليه وسلم ، خَرَجَا مِنْ عِنْدِ النَّبيِّ صلى الله عليه وسلم ، في لَيْلَةٍ مُظْلِمَةٍ وَمَعَهُمَا مِثْلُ المِصْبَاحَيْنِ بَيْنَ أَيْديهِمَا . فَلَمَّا افْتَرَقَا ، صَارَ مَعَ كُلِّ وَاحِدٍ مِنْهُمَا وَاحِدٌ حَتَّى أتَى أهْلَهُ .
رواهُ البُخاري مِنْ طُرُقٍ ؛ وفي بَعْضِهَا أنَّ الرَّجُلَيْنِ أُسَيْدُ بنُ حُضير ، وَعَبّادُ بنُ بِشْرٍ رضي الله عنهما .
Imepokewa kutoka kwa Anas (Radhwiya Allaahu 'anhu) kuwa watu wawili miongoni mwa Swahaaba wa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) walitoka kwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) usiku mmoja wa giza totoro na wakawa pamoja nao mfano wa taa mbili katika mikono yao. Lakini pindi walipoachana kila mmoja wao akawa na taa yake mpaka walipofika nyumbani kwao." [Al-Bukhaariy kwa njia tofauti]
Na katika mapokezi mengine ya Al-Bukhaariy amesema kwamba watu wawili hao ni Usayd Ibn Hudhwaiyr na Ubbada Ibn Bishri (Radhwiya Allaahu 'anhumaa)
Hadiyth – 7
وعن أَبي هريرة رضي اللهُ عنه قَالَ : بعث رسول الله صلى الله عليه وسلم عَشْرَة رَهْطٍ عَيْناً سَرِيَّة، وأمَّرَ عَلَيْهَا عاصِمَ بنَ ثَابِتٍ الأنْصَارِيَّ رضي اللهُ عنه ، فانْطلقوا حَتَّى إِذَا كَانُوا بالهَدْأةِ ؛ بَيْنَ عُسْفَانَ وَمَكَّةَ ؛ ذُكِرُوا لِحَيٍّ مِنْ هُذَيْل يُقالُ لَهُمْ : بَنُو لحيانَ ، فَنَفَرُوا لَهُمْ بِقَريبٍ مِنْ مِئَةِ رَجُلٍ رَامٍ ، فَاقْتَصُّوا آثَارَهُمْ ، فَلَمَّا أحَسَّ بِهِمْ عَاصِمٌ وأصْحَابُهُ ، لَجَأُوا إِلَى مَوْضِعٍ ، فَأَحاطَ بِهِمُ القَوْمُ ، فَقَالُوا : انْزِلُوا فَأَعْطُوا بِأيْدِيكُمْ وَلَكُمُ العَهْدُ وَالمِيثَاقُ أنْ لا نَقْتُلَ مِنْكُمْ أحَداً . فَقَالَ عَاصِمُ بنُ ثَابِتٍ : أَيُّهَا القَوْمُ ، أَمَّا أنا ، فَلاَ أنْزِلُ عَلَى ذِمَّةِ كَافِرٍ : اللَّهُمَّ أَخْبِرْ عَنَّا نَبِيَّكَ صلى الله عليه وسلم ، فَرَمُوهُمْ بِالنّبْلِ فَقَتلُوا عَاصِماً ، وَنَزَلَ إلَيْهِمْ ثَلاَثَةُ نَفَرٍ عَلَى العَهْدِ والمِيثاقِ، مِنْهُمْ خُبَيْبٌ، وَزَيدُ بنُ الدَّثِنَةِ وَرَجُلٌ آخَرُ. فَلَمَّا اسْتَمْكَنُوا مِنْهُمْ أطْلَقُوا أوْتَارَ قِسِيِّهِمْ ، فَرَبطُوهُمْ بِهَا . قَالَ الرَّجُلُ الثَّالِثُ : هَذَا أوَّلُ الغَدْرِ واللهِ لا أصْحَبُكُمْ إنَّ لِي بِهؤُلاءِ أُسْوَةً ، يُريدُ القَتْلَى ، فَجَرُّوهُ وعَالَجُوهُ ، فأبى أنْ يَصْحَبَهُمْ ، فَقَتَلُوهُ ، وانْطَلَقُوا بِخُبَيبٍ ، وزَيْدِ بنِ الدَّثِنَةِ ، حَتَّى بَاعُوهُما بِمَكَّةَ بَعْدَ وَقْعَةِ بَدْرٍ ؛ فابْتَاعَ بَنُو الحارِثِ بن عامِرِ بنِ نَوْفَلِ بنِ عبدِ مَنَافٍ خُبيباً ، وكان خُبَيْبٌ هُوَ قَتَلَ الحَارِثَ يَوْمَ بَدْرٍ . فَلِبثَ خُبَيْبٌ عِنْدَهُمْ أسيراً حَتَّى أجْمَعُوا عَلَى قَتْلِهِ ، فاسْتَعَارَ مِنْ بَعْضِ بَنَاتِ الحَارثِ مُوسَى يَسْتَحِدُّ بِهَا فَأعَارَتْهُ ، فَدَرَجَ بُنَيٌّ لَهَا وَهِيَ غَافِلَةٌ حَتَّى أَتَاهُ ، فَوَجَدتهُ مُجْلِسَهُ عَلَى فَخْذِهِ وَالموسَى بِيَدِهِ ، فَفَزِعَتْ فَزْعَةً عَرَفَهَا خُبَيْبٌ . فَقَالَ : أَتَخَشَيْنَ أن أقْتُلَهُ مَا كُنْتُ لأَفْعَلَ ذَلِكَ ! قالت : واللهِ مَا رَأيْتُ أسيراً خَيراً مِنْ خُبَيْبٍ ، فواللهِ لَقَدْ وَجَدْتُهُ يَوماً يَأكُلُ قِطْفاً مِنْ عِنَبٍ في يَدِهِ وإنَّهُ لَمُوثَقٌ بِالحَدِيدِ وَمَا بِمَكَّةَ مِنْ ثَمَرَةٍ ، وَكَانَتْ تَقُولُ : إنَّهُ لَرِزْقٌ رَزَقَهُ اللهُ خُبَيْباً . فَلَمَّا خَرَجُوا بِهِ مِنَ الحَرَمِ لِيَقْتُلُوهُ في الحِلِّ، قَالَ لَهُمْ خُبَيْبٌ : دَعُونِي أُصَلِّي رَكْعَتَيْنِ ، فَتَرَكُوهُ ، فَرَكَعَ رَكْعَتَيْنِ فَقَالَ : واللهِ لَوْلاَ أنْ تَحْسَبُوا أنَّ مَا بِي جَزَعٌ لَزِدْتُ : اللَّهُمَّ أحْصِهِمْ عَدَداً ، وَاقْتُلهُمْ بِدَدَاً ، وَلاَ تُبْقِ مِنْهُمْ أَحَداً . وقال :
فَلَسْتُ أُبَالِي حِيْنَ أُقْتَلُ مُسْلِماً |
|
عَلَى أيِّ جَنْبٍ كَانَ للهِ مَصْرَعِي
|
وَذَلِكَ في ذَاتِ الإلَهِ وإنْ يَشَأْ
|
|
يُبَارِكْ عَلَى أوْصَالِ شِلْوٍ مُمَزَّعِ |
وكان خُبَيبٌ هُوَ سَنَّ لِكُلِّ مُسْلِمٍ قُتِلَ صَبْراً الصَّلاَةَ . وأخْبَرَ - يعني : النبيّ صلى الله عليه وسلم - أصْحَابَهُ يَوْمَ أُصِيبُوا خَبَرَهُمْ ، وَبَعَثَ نَاسٌ مِنْ قُرَيْشٍ إِلَى عَاصِمِ بنِ ثَابتٍ حِيْنَ حُدِّثُوا أَنَّهُ قُتِلَ أن يُؤْتَوا بِشَيءٍ مِنْهُ يُعْرَفُ ، وكَانَ قَتَلَ رَجُلاً مِنْ عُظَمائِهِمْ ، فَبَعَثَ الله لِعَاصِمٍ مِثْلَ الظُّلَّةِ مِنَ الدَّبْرِ فَحَمَتْهُ مِنْ رُسُلِهِمْ ، فَلَمْ يَقْدِروا أنْ يَقْطَعُوا مِنْهُ شَيْئاً . رواه البخاري .
Amesema Abu Huraiyrah (Radhwiya Allaahu 'anhu): Alituma Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kikosi cha watu kumi chini ya uamiri wa 'Aaswim bin Thaabit Al-Answaariyy (Radhwiya Allaahu 'anhu). wakaondoka kuelekea sehemu waliyotumwa mpaka wakafika sehemu inayoitwa Had'ah, baina ya 'Usfaan na Makkah, waliambiwa kuhusu wao ukoo wa Lahay unaotokana na Hudhayl, wanaoitwa Banu Lahyaan. Wakawafuata wapiga mishale na mikuki wanaokaribia mia moja, wakazifuata nyayo zao. 'Aaswin na Swahaaba wenziwe walipohisi kuwa wanafuatwa walipanda kwenye mlima na kujificha hapo na wale maadui wakawazunguka. Wakawaambia: "Shukeni chini, tunaahidi kuwa iwapo mtakuja kwetu hatutamwua katika nyinyi mtu yeyote." Akasema 'Aaswim bin Thaabit: "Enyi kaumi! Ama mimi, sitashuka chini kuwa chini ya dhima na ahadi ya kafiri. Ee Rabb Wangu! Mpashe habari Nabiy Wako (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kuhusu hali yetu." Wakaanza kuwarushia mishale, hivyo kumuua 'Aaswim na wakateremka kwao watatu kwa ahadi na mkataba waliopewa, akiwemo Khubayb, na Zayd bin ad-Dathinah na mtu mwengine (wengine sita walikuwa wameuliwa pamoja na Amiri wao, 'Aaswim). Walipoteremka wakawafanyia khiana na kuwafunga kwa kamba za pinde zao, yule mtu wa tatu akasema: "Huu ni mwanzo wa khiana. Wa-Allaahi, sitafuatana nanyi na nitafuata kigezo cha wenzangu waliotangulia, akimaanisha wale waliouliwa." Wakamkokota na wakamshawishi afuatane nao, lakini alikataa katakata kufanya hivyo, nao wakamwua na kisha kuondoka na Khubayb na Zayd bin ad-Dathinah. Wakawauza huko Makkah na walikuwa wamewaua baadhi ya viongozi wa Makkah katika Vita vya Badr. Banu Al-Haariyh bin 'Aamir bin Nawfal bin 'Abdi Manaaf walimnunua Khubayb, kwani Khubayb ndiye aliyemuua Haarith katika Vita vya Badr. Khubayb alikaa kwao hali ya kuwa ni mfungwa mpaka walipoamua kumuua. Siku moja Khubayb aliomba wembe kutoka kwa mmoja wa binti za Haarith ili kukata kucha zake. Wakati huo huo mtoto wa huyu mama aliondoka huku akiwa naye. Alipomkumbuka alikuja kumkuta kwenye mapaja ya khubayb, naye akiwa na wembe mkononi mwake. Mama huyu alibabaika sana mpaka akatambua hilo Khubayb, ambaye alimwambia: "Unahofia kuwa nitamuua? Siwezi kabisa kufanya kitendo hicho." Akasema: "Wa-Allaahi! Sijauona mfungwa bora kuliko Khubayb. Wa-Allaahi, nilimuona siku moja akila kikonyo cha zabibu na hali mikono yake imefungwa na minyororo na katika mji wa Makkah hakuna matunda hayo." Na alikuwa akisema (yaani huyu mwanamke): "Ni hakika kuwa hiyo ilikuwa ni riziki aliyoruzukiwa Khubayb na Allaah." Walipotoka naye nje ya mipaka ya Haram ili kwenda kumuua, Khubayb aliwaambia: "Niacheni niswali rakaa mbili." Wakamwacha, naye akaswali hizo rakaa mbili, kisha akasema: "Naapa kwa jina la Allaah, lau si kuwa - mutasema kuwa haya ninayofanya ni kulalamika ningeongezea (kuswali rakaa zingine)." Kisha akaomba duaa: "Ee Rabb Wangu wadhibiti kwa idadi wauwe mmoja mmoja na usimbakishe katika wao mtu yeyote." Kisha akasoma mashairi yake: Sijali ninapouliwa nikiwa Muislamu, Kwa ubavu gani nitaelekea kwa Allaah. Na hiki kifo changu ni kwa ajili ya Allaah, Na Yeye Atavibariki vipande vya mwili wangu vilivyo katwa. Na alikuwa Khubayb mtu wa kwanza aliyeleta Sunnah kwa kila Muislamu aliyeuliwa akiwa katika hali ya kusubiri ya kuswali rakaa mbili. Na Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalhi wa sallam) aliwapasha habari Swahaaba zake siku waliyouliwa. Na Maquraysh waliwatuma watu kwenda kuhakikisha kifo cha 'Aaswim bin Thaabit (Radhwiya Allaahu 'anhu) pindi walipopata habari ya kuuliwa kwake na waletewe chochote katika wanachokijua katika mwili wake ili apate kujulikana kuwa ndiye. Na 'Aaswim alikuwa amemwua mtu mkubwa miongoni mwa watukufu wao (wa Makkah). Allaah Akapeleka mfano wa kiwingu cha manyigu, yakamlinda na wajumbe hao hawakuweza kutaka chochote katika mwili wake. [Al-Bukhaariy]
Hadiyth – 8
وعن ابن عمر رضي الله عنهما ، قَالَ : مَا سَمِعْتُ عمر رضي اللهُ عنه يقولُ لِشَيءٍ قَطُّ : إنِّي لأَظُنُّهُ كَذَا ، إِلاَّ كَانَ كَمَا يَظُنُّ . رواه البخاري .
Amesema Ibn 'Umar (Radhwiya Allaahu 'anhumaa): Sikumsikia 'Umar (Radhwiya Allaahu 'anhu) akisema kwa ajili ya kitu chochote kamwe: Hakika mimi nadhania kuwa jambo hili ni hivi isipokuwa huwa kama alivyo dhania. [Al-Bukhaariy]
Links
[1] https://www.alhidaaya.com/sw/taxonomy/term/280
[2] http://www.alhidaaya.com/sw/
[3] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F10330&title=16-Riyaadhw%20Asw-Swaalihiyn%3A%20Kitabu%20Cha%20Du%27aa%20-%20%D9%83%D9%90%D8%AA%D8%A7%D8%A8%D9%8F%20%D8%A7%D9%84%D8%AF%D9%91%D8%B9%D9%88%D8%A7%D8%AA
[4] http://www.alhidaaya.com/
[5] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11252&title=01-Riyaadhw%20Asw-Swaalihiyn%3A%20Mlango%20Wa%20Fadhila%20za%20Duaa
[6] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11253&title=02-Riyaadhw%20Asw-Swaalihiyn%3A%20Mlango%20Wa%20Fadhila%20za%20Kuwaombea%20Wasio%20Kuwepo
[7] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11254&title=03-Riyaadhw%20Asw-Swaalihiyn%3A%20Mlango%20Wa%20Katika%20Mas-ala%20ya%20Duaa
[8] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11255&title=04-Riyaadhw%20Asw-Swaalihiyn%3A%20Mlango%20Wa%20Karama%20za%20Mawalii%20na%20Fadhila%20Zao