كِتَابُ الأَطْعِمَةِ وَالأَشْرِبةِ وَمَا يَتَعَلَّقُ بِهِمَا
Kitabu Cha Vyakula Na Vinywaji
Na Yanayohusiana Na Viwili Hivi
الصَّيْدُ وَأَحْكَامُهُ
Kuwinda Na Hukmu Zake
Abu Maalik Kamaal Bin As-Sayyid Saalim
Imetarjumiwa na 'Abdullaah Mu'aawiyah (Abu Baasim)
Alhidaaya.com
Swahiyh Fiqh As-Sunnah
كِتَابُ الأَطْعِمَةِ وَالأَشْرِبةِ وَمَا يَتَعَلَّقُ بِهِمَا
Kitabu Cha Vyakula Na Vinywaji Na Yanayohusiana Na Viwili Hivi
الصَّيْدُ وَأَحْكَامُهُ
Kuwinda Na Hukmu Zake
Alhidaaya.com [3]
01-Kuwinda Na Hukmu Zake: Taarifu Na Hukmu Ya Kuwinda:
"الصَّيْدُ" ni “maswdar” (kiini) ya kitenzi cha wakati uliopita "صَادَ" (amewinda) na cha wakati uliopo "يَصِيْدُ" (anawinda). Na katika lugha, ina tafsiri mbili:
Kwa tafsiri ya kwanza, inaweza kukusudiwa kuwinda, mkono kumfikia mnyama mwindwa, kumkamata na kumdhibiti (yaani purukushani yote ya kumsaka mnyama hadi kumtia mkononi). Ni kama Neno Lake Ta’alaa:
"وَإِذَا حَلَلْتُمْ فَاصْطَادُوا"
“Na mkishatoka kwenye ihraam basi windeni (mkitaka)”. [Al-Maaidah : 03].
Na kwa tafsiri ya pili, inaweza kukusudiwa mnyama mwindwa mwenyewe kama Alivyosema Allaah Ta’aalaa:
"يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تَقْتُلُوا الصَّيْدَ وَأَنتُمْ حُرُمٌ"
“Enyi walioamini! Msiue mawindo na hali mko k atika ihraam”. [Al-Maaidah : 95].
Na kwa mujibu wa tafsiri ya kwanza, taarifu ya "الصَّيْدُ"kiistilahi inakuwa ni kumwinda na kumkamata mnyama pori ambaye kikawaida ni halali kuliwa, asiyemilikiwa na mtu, na ambaye hawezi kuwa rafiki wa binadamu au kutiishwa (kama alivyo ng’ombe n.k).
Ama kwa tafsiri ya pili, "الصَّيْدُ"taarifu yake kiistilahi inakuwa ni mnyama pori kimaumbile, asiyemilikiwa na yeyote, na ambaye hawezekani kutulizwa au kudhibitiwa.
Hukmu Ya Kuwinda:
‘Ulamaa wamekubaliana kwa kauli moja kuwa kuwinda na kumla mnyama aliyewindwa ni jambo la halali. Na hii ni kutokana na uthibitisho toka kwenye Qur-aan na Hadiyth za Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam).
(a) Kutoka kwenye Qur-aan:
1- Ni Kauli Yake Ta’aalaa:
"أُحِلَّ لَكُمْ صَيْدُ الْبَحْرِ وَطَعَامُهُ مَتَاعًا لَّكُمْ وَلِلسَّيَّارَةِ ۖ وَحُرِّمَ عَلَيْكُمْ صَيْدُ الْبَرِّ مَا دُمْتُمْ حُرُمًا"
“Mmehalalishiwa mawindo ya bahari, na chakula chake ni manufaa kwenu na kwa wasafiri. Na mmeharamishiwa mawindo ya nchi kavu madamu mtakuwa katika ihraam”. [Al-An’aam : 96].
2- Na Kauli Yake Subhaanah:
"وَإِذَا حَلَلْتُمْ فَاصْطَادُوا"
“Na mkishatoka kwenye ihraam basi windeni (mkitaka)”. [Al-Maaidah : 03].
3- Na Kauli Yake ‘Azza wa Jalla:
"يَسْأَلُونَكَ مَاذَا أُحِلَّ لَهُمْ ۖ قُلْ أُحِلَّ لَكُمُ الطَّيِّبَاتُ ۙ وَمَا عَلَّمْتُم مِّنَ الْجَوَارِحِ مُكَلِّبِينَ تُعَلِّمُونَهُنَّ مِمَّا عَلَّمَكُمُ اللَّـهُ ۖ فَكُلُوا مِمَّا أَمْسَكْنَ عَلَيْكُمْ وَاذْكُرُوا اسْمَ اللَّـهِ عَلَيْهِ"
“Wanakuuliza wamehalalishiwa nini? Sema: Mmehalalishiwa vilivyo vizuri na mlivyowindiwa na wanyama na ndege wakali mliowafundisha kiweledi, na mnawafunza katika ambayo Allaah Amekufunzeni. Basi kuleni walichokukamatieni, na mkitajie Jina la Allaah”. [Al-Maaidah : 04].
(b) Ama kwenye Hadiyth:
Ni Hadiyth ya ‘Adiyy bin Haatim aliyesema:
"قُلْتُ يَا رَسُولَ اللَّهِ إِنِّي أُرْسِلُ الْكِلاَبَ الْمُعَلَّمَةَ فَيُمْسِكْنَ عَلَىَّ وَأَذْكُرُ اسْمَ اللَّهِ عَلَيْهِ ، فَقَالَ: "إِذَا أَرْسَلْتَ كَلْبَكَ الْمُعَلَّمَ وَذَكَرْتَ اسْمَ اللَّهِ عَلَيْهِ فَكُلْ" . قُلْتُ وَإِنْ قَتَلْنَ ، قَالَ : "وَإِنْ قَتَلْنَ مَا لَمْ يَشْرَكْهَا كَلْبٌ لَيْسَ مَعَهَا" . قُلْتُ لَهُ : فَإِنِّي أَرْمِي بِالْمِعْرَاضِ الصَّيْدَ فَأُصِيبُ ، فَقَالَ : "إِذَا رَمَيْتَ بِالْمِعْرَاضِ فَخَزَقَ فَكُلْهُ ، وَإِنْ أَصَابَهُ بِعَرْضِهِ فَلاَ تَأْكُلْهُ "
“Nilisema: Ee Rasuli wa Allaah! Mimi huwachochea mbwa wangu waliopata mafunzo wakanikamatia (wanyama), nami hulidhukuru Jina la Allaah wakati nikiwaachilia. Akasema: Ukimwachilia mbwa wako aliyepata mafunzo, na ukalitaja Jina la Allaah wakati wa kumwachilia, basi kula”. Nikamuuliza: Hata kama watamuua? Akasema: Hata kama watamuua madhali hajashirikiana nao mbwa mwingine asiye pamoja nao”. Nikamwambia: Mimi ninamrushia mnyama mi’iradh nikampata. Akasema: Ukimrushia mi’iradh ikamwingia hadi ndani ya mwili, basi mle, lakini ikimpiga kwa ubavu (na si kwa ncha yake), basi usimle”. [Hadiyth Swahiyh. Imekharijiwa na Al-Bukhaariy (2054) na Muslim (1929)].
Mi’iradh "المِعْرَاضُ"ni kipande kizito cha mti kilichochongwa nchani, au kilichofungiwa nchani mwake kipande cha chuma chenye ncha kali na kuwa mithili ya mkuki.
Swahiyh Fiqh As-Sunnah
كِتَابُ الأَطْعِمَةِ وَالأَشْرِبةِ وَمَا يَتَعَلَّقُ بِهِمَا
Kitabu Cha Vyakula Na Vinywaji Na Yanayohusiana Na Viwili Hivi
الصَّيْدُ وَأَحْكَامُهُ
Kuwinda Na Hukmu Zake
Alhidaaya.com [3]
02- Kuwinda Na Hukmu Zake: Ni Wakati Gani Kuwinda Ni Marufuku?
Kuwinda kwa asili yake ni halali, lakini inakuwa ni marufuku katika hali hizi zifuatazo:
Ya Kwanza: Ikiwa kuwinda ni kwa kujifurahisha tu, au kujipumbaza au kucheza, na si kwa ajili ya kumchinja mnyama na kunufaika na nyama yake. Ikiwa ni kwa lengo hilo la kujipumbaza, basi ni haramu. Ni kutokana na Hadiyth ya Ibn ‘Abbaas kwamba Nabiy (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
"لَا تَتَّخِذُوا شَيْئًا فِيهِ الرُّوحُ غَرَضًا"
“Msikifanye kiumbe chochote chenye roho tageti ya kulengwa shabaha”. [Hadiyth Swahiyh. Imekharijiwa na Muslim (1957), An-Nasaaiy (4443) na Ibn Maajah (3187)].
Na imepokelewa toka kwa Sa’iyd bin Jubayr kwamba amesema:
"مَرَّ ابْنُ عُمَرَ بِنَفَرٍ قَدْ نَصَبُوا دَجَاجَةً يَتَرَامَوْنَهَا ، فَلَمَّا رَأَوُا ابْنَ عُمَرَ تَفَرَّقُوا عَنْهَا . فَقَالَ ابْنُ عُمَرَ: مَنْ فَعَلَ هَذَا؟ إِنَّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ لَعَنَ مَنْ فَعَلَ هَذَا"
“Ibn ‘Umar aliwapitia watu wakiwa wamemfunga kuku huku wakimlenga shabaha kwa zamu. Walipomwona Ibn ‘Umar walitawanyika wakamwacha. Ibn ‘Umar akauliza: Nani kafanya hivi?! Hakika Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amemlaani aliyefanya hivi”. [Hadiyth Swahiyh. Imekharijiwa na Muslim (1958].
Ya Pili: Ikiwa mwindaji amehirimia Hajji au ‘Umrah, hapo ni haramu kwake kuwinda. Ni kwa Neno Lake Ta’aalaa:
"وَحُرِّمَ عَلَيْكُمْ صَيْدُ الْبَرِّ مَا دُمْتُمْ حُرُمًا"
“Na mmeharamishiwa mawindo ya nchi kavu madamu mtakuwa katika ihraam”. [Al-An’aam: 96].
Haya yashafafanuliwa katika Kitabu cha Hijjah.
Ya Tatu: Ni haramu kuwinda kwenye Al-Haramayn, yaani Makkah na Madiynah hata kwa mtu ambaye hajahirimia. Hili lishaelezwa pia kwenye Kitabu cha Hijjah.
Ya Nne: Ni haramu kuwinda kinachomilikiwa na mtu mwingine.
Swahiyh Fiqh As-Sunnah
كِتَابُ الأَطْعِمَةِ وَالأَشْرِبةِ وَمَا يَتَعَلَّقُ بِهِمَا
Kitabu Cha Vyakula Na Vinywaji Na Yanayohusiana Na Viwili Hivi
الصَّيْدُ وَأَحْكَامُهُ
Kuwinda Na Hukmu Zake
Alhidaaya.com [3]
03- Kuwinda Na Hukmu Zake: Njia Za Uwindaji: Njia Ya Kwanza
Uhalali wa kuwinda unamaanisha kumwezesha mwindaji kumkamata mnyama na kumdhibiti akiwa hai ikiwezekana, au akiwa ameuawa kwa zana ya kuwindia, kwa kuwa kumuua mnyama kwa zana ya kuwindia kunazingatiwa kuwa sawa na kumchinja chinjo la kisharia. Njia zote au ala zote za kuwindia zina masharti maalum ya kumfanya mnyama aliyeuawa kuwa kama amechinjwa chinjo la kisharia.
Njia Ya Kwanza Ya Uwindaji: Kuwinda Kwa Kutumia Wanyama Au Ndege Wakali
Wanyama wakali wakusudiwao hapa ni wale wenye meno makali ya kuulia kiwindwa kama mbwa, cheetah na kadhalika. Ama ndege, hawa ni wale wenye kucha kali za kuulia kiwindwa kama vile kozi, kipanga na kadhalika. Ni kwa Neno Lake Allaah Ta’aalaa:
"وَمَا عَلَّمْتُم مِّنَ الْجَوَارِحِ مُكَلِّبِينَ تُعَلِّمُونَهُنَّ مِمَّا عَلَّمَكُمُ اللَّـهُ"
“Na mlivyowindiwa na wanyama na ndege wakali mliowafundisha kiweledi, na mnawafunza katika ambayo Allaah Amekufunzeni”. [Al-Maaidah : 04].
Swahiyh Fiqh As-Sunnah
كِتَابُ الأَطْعِمَةِ وَالأَشْرِبةِ وَمَا يَتَعَلَّقُ بِهِمَا
Kitabu Cha Vyakula Na Vinywaji Na Yanayohusiana Na Viwili Hivi
الصَّيْدُ وَأَحْكَامُهُ
Kuwinda Na Hukmu Zake
Alhidaaya.com [3]
04-Kuwinda Na Hukmu Zake: Masharti Ya Mnyama Au Ndege Anayetumiwa Kuwinda Ili Akikamatacho Kiwe Halali Kuliwa
Sharti La Kwanza: Awe amepata mafunzo ya kuwinda
Allaah Ta’aalaa Amesema:
"وَمَا عَلَّمْتُم مِّنَ الْجَوَارِحِ مُكَلِّبِينَ تُعَلِّمُونَهُنَّ مِمَّا عَلَّمَكُمُ اللَّـهُ ۖ فَكُلُوا مِمَّا أَمْسَكْنَ عَلَيْكُمْ وَاذْكُرُوا اسْمَ اللَّـهِ عَلَيْهِ"
“Na mlivyowindiwa na wanyama na ndege wakali mliowafundisha kiweledi, na mnawafunza katika ambayo Allaah Amekufunzeni. Basi kuleni walichokukamatieni, na mkitajie Jina la Allaah”. [Al-Maaidah : 04].
Mnyama aliyekamilika kimafunzo ni lazima awe na mambo matatu:
(a) Akiamuriwa kwenda kukamata anakwenda hapo hapo.
(b) Akiamuriwa kuacha anaacha hapo hapo.
(c) Akikamata mnyama hali chochote.
Akiyatimiza haya kwa majaribio kadhaa, basi anakuwa ni mhitimu kwa mujibu wa mazoea ya watu. Majaribio haya yasipungue matatu kwa mujibu wa madhehebu ya Ash-Shaafi’iy na Hanbal.
Ikiwa mnyama huyu mwindaji atakula sehemu ya mnyama aliyemkamata, basi si halali. Ni kwa neno lake Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kwa ‘Adiyy bin Haatim:
"إِذَا أَرْسَلْتَ كِلاَبَكَ الْمُعَلَّمَةَ وَذَكَرْتَ اسْمَ اللَّهِ، فَكُلْ مِمَّا أَمْسَكْنَ عَلَيْكَ وَإِنْ قَتَلَتْ ، إِلاَّ أَنْ يَأْكُلَ الْكَلْبُ فَلَا تَأْكُلْ، فَإِنِّي أَخَافُ أَنْ يَكُونَ إِنَّمَا أَمْسَكَهُ عَلَى نَفْسِهِ"
“Ukiwaachilia mbwa wako waliopata mafunzo wakamate, na ukalitaja Jina la Allaah (wakati wa kuwaachilia), basi kula walichokukamatia hata kama watamuua mnyama, isipokuwa kama mbwa atakula (sehemu ya kiwindwa) basi hapo usimle mnyama huyo, kwani mimi ninachelea kuwa atakuwa amejikamatia mwenyewe”. [Hadiyth Swahiyh. Imetajwa nyuma kidogo].
Angalizo:
Ikiwa mbwa asiye na mafunzo atakamata mnyama na mwindaji akamkuta mnyama yungali hai, halafu akamchinja chinjo la kisharia, basi mnyama huyo ni halali kuliwa vile vile. Na hii ni kwa neno lake Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alipomwambia Abu Tha-’alabah Al-Khushaniy:
"وَمَا صِدْتَ بِكَلْبِكَ غَيْرِ الْمُعَلَّمِ فَأَدْرَكْتَ ذَكَاتَهُ فَكُلْ"
“Na ulichokiwinda kwa kumtumia mbwa wako asiye na mafunzo na ukawahi kukichinja, basi kula”. [Hadiyth Swahiyh. Imekharijiwa na Al-Bukhaariy (5478) na Muslim (1532)].
Sharti La Pili: Mwindaji alitaje Jina la Allaah wakati anapomwamuru kwenda kukamata.
Ni kwa ujumuishi wa Neno Lake Ta’aalaa:
"وَلَا تَأْكُلُوا مِمَّا لَمْ يُذْكَرِ اسْمُ اللَّـهِ عَلَيْهِ"
“Na wala msile katika ambavyo halikutajwa Jina la Allaah (wakati wa kuchinjwa)”. [Al-An’aam: 121].
Na kwa Neno Lake ‘Azza wa Jalla pia:
"فَكُلُوا مِمَّا أَمْسَكْنَ عَلَيْكُمْ وَاذْكُرُوا اسْمَ اللَّـهِ عَلَيْهِ"
“Basi kuleni walichokukamatieni, na mkitajie Jina la Allaah”. [Al-Maaidah : 04].
Na pia kwa Hadiyth ya ‘Adiyy bin Haatim: Amesema Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam):
"إذَا أَرْسَلْتَ كَلْبَكَ وَذَكَرْتَ اسْمَ اللهِ فَكُلْ"
“Ukimwachilia mbwa wako (kukamata), na ukalitaja Jina la Allaah, basi kula”. [Hadiyth Swahiyh. Imetajwa nyuma kidogo].
Na katika Hadiyth ya Abu Tha-‘alabah, Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
"وَمَا صِدْتَ بِكَلْبِكَ الْمُعَلَّمِ فَذَكَرْتَ اسْمَ اللهِ فَكُلْ "
“Na ulichokiwinda kwa kumtumia mbwa wako aliyefunzwa na ukalitaja Jina la Allaah, basi kula”. [Hadiyth Swahiyh. Imetajwa nyuma kidogo].
Sharti La Tatu: Mbwa mwingine asishirikiane na mbwa wake
Toka kwa ‘Adiyy bin Haatim, amesema:
"قُلْتُ يَا رَسُوْلَ اللهِ ، أُرْسِلُ كَلْبِيْ وَأُسَمِّيْ ، فَأَجِدُ مَعَهُ عَلَى الصَّيْدِ كَلْباً آخَرَ لَمْ أُسَمِّ عَلَيْهِ ، وَلا أَدْرِيْ أَيُّهُمَا أَخَذَ ، قَالَ: لا تَأْكُلْ ، إِنَّمَا سَمَّيْتَ عَلى كَلْبِكَ وَلَمْ تُسَمِّ عَلَى الآخَرِ"
“Nilisema: Ee Rasuli wa Allaah! Ninamtuma mbwa wangu na kulitaja Jina la Allaah, halafu nakuja kumkuta mbwa mwingine ambaye sikumtajia Jina la Allaah amekamata pamoja naye mnyama, na sijui ni yupi kati yao aliyekamata mwanzo. Akasema: Usile. Wewe kiuhakika ulilitaja Jina la Allaah kwa mbwa wako, na wala hukulitaja kwa mwingine”. [Hadiyth Swahiyh. Imetajwa nyuma kidogo].
Sharti La Nne: Mbwa amjeruhi mnyama aliyemkamata
Kama mbwa atamkaba koo na kumbana pumzi, au akamuua kwa kishindo cha kumgonga, basi kiwindwa si halali. Ni kwa neno lake Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam):
"مَا أَنْهَرَ الدَّمَ وَذُكِرَ اسْمُ اللَّهِ فَكُلْ إِلاَّ بِسِنٍّ أَوْ ظُفْرٍ"
“Chochote chenye kumwagisha damu (ya mnyama), na Jina la Allaah likatajwa, basi kula, isipokuwa mfupa au kucha (hivi havifai kutumika kama kichinjio)”. [Imekharijiwa na Al-Bukhaariy (5503) na Muslim (1986)].
Faida:
Ya Kwanza: Inajuzu kufuga mbwa kwa ajili ya kuwinda, kuchunga mifugo na ulinzi
Toka kwa ‘Abdullaah bin Mughaffal, amesema:
"أّمَرَ رَسُوْلُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ بِقَتْلِ الكِلَابِ ، ثُمَّ قَالَ : مَا بَالُهُمْ وَبَالُ الكِلاَبِ ، ثُمَّ رَخَّصَ فِيْ كَلْبِ الصَّيْدِ وَكَلْبِ الغَنَمِ"
“Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) aliamuru mbwa wauawe, kisha baadaye akasema: Yanawahusu nini wao na mambo ya mbwa (waachane nao sasa, inatosha)? Halafu akaruhusu (kumiliki) mbwa wa kuwinda na mbwa wa mifugo”. [Imekharijiwa na Muslim (280), An-Nasaaiy (67), Abu Daawuwd (74) na Ibn Maajah (3200)].
Ama kufuga na kulea mbwa kwa sababu zingine zisizo hizi tajwa, hilo halifai. Toka kwa Abu Hurayrah, kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
"مَنِ اقْتَنَى كَلْبًا لَيْسَ بِكَلْبِ صَيْدٍ، وَلَا مَاشِيَةٍ وَلَا أَرْضٍ، فَإِنَّهُ يَنْقُصُ مِنْ أَجْرِهِ قِيْرَاطَانِ كُلَّ يَوْمٍ"
“Yeyote mwenye kulea au kufuga mbwa ambaye si mbwa wa kuwinda, au wa kuchunga mifugo, au wa kulinda ardhi, basi hupungua kila siku mafungu mawili katika (jumla ya) thawabu zake.” [Hadiyth Swahiyh. Imekharijiwa na Al-Bukhaariy (5480) na Muslim (1574)].
Ya Pili: Je, inafaa kuwinda kwa kutumia mbwa mweusi ti ti ti?
Huyu ni mbwa ajulikanaye kwa Kiarabu kama "الْكَلْبُ الأَسْوَدُ الْبَهِيْمُ", ambaye ni mweusi mwili wake wote bila hata chembe ya doa jeupe. Mbwa huyu Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ameamuru auawe.
Jaabir bin ‘Abdullaah amesema:
"أَمَرَنَا رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ بِقَتْلِ الْكِلَابِ حَتَّى إِنَّ الْمَرْأَةَ تَقْدَمُ منَ الْبَادِيةِ بِكَلْبِهَا فَنَقْتُلَهُ ، ثُمَّ نَهَى رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ عَنْ قَتْلِهَا وَقَالَ : عَلَيْكُمْ بِالْأَسْوَدِ الْبَهِيمِ ذِي النُّقْطَتَيْن فَإِنَّهُ شَيْطَان"
“Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alituamuru kuwaua mbwa, hata ikawa mwanamke anakuja tokea majangwani na mbwa wake nasi tunamuua. Kisha baadaye Rasuli akakataza kuwaua, na akasema: Muueni tu mweusi mwenye vitone viwili, kwa sababu huyo ni shaytwaan”. [Hadiyth Swahiyh. Imekharijiwa na Muslim (1572) na Abu Daawuwd (2846)].
Na juu ya msingi huu, Imaam Ahmad, Ibn Hazm na Ahlu Adh-Dhwaahir wengineo wanasema kuwa haifai mbwa mweusi kuwinda, kwa kuwa kilichowajibu kukiua ni haramu kukilea na kukipa mafunzo, na kwa hivyo ilichokiwinda na kukikamata, si halali kuliwa. Si hivyo tu, bali Rasuli amemwita mbwa huyo shaytwaan, mbali na kuwa ni ruksa kula kiwindwa kilichouliwa, lakini hakihalalishwi na kilichoharamishwa kama ruksa nyinginezo.
Kundi la Masalaf wakiwemo Al-Hasan, An-Nakh’-iy, Qataadah na Is-haaq wamekirihisha kuwinda na mbwa huyo.
Lakini akina Abu Haniyfah, Maalik na Ash-Shaafi’iy, wao wamejuzisha kuwinda na mbwa mweusi ti ti ti. Na hii ni kwa ujumuishi wa dalili zilizotangulia nyuma kuhusiana na kujuzu kuwinda kwa kutumia mbwa mwenye mafunzo, na dalili hizo hazikuainisha mbwa fulani bila wengineo, bali mbwa kiujumla (muhimu tu awe amepata mafunzo).
Ninasema: “Ninaloliona kuwa na nguvu zaidi ni kuwa haijuzu kuwinda na mbwa mweusi ti ti ti. Allaah Ndiye Ajuaye zaidi”.
Swahiyh Fiqh As-Sunnah
كِتَابُ الأَطْعِمَةِ وَالأَشْرِبةِ وَمَا يَتَعَلَّقُ بِهِمَا
Kitabu Cha Vyakula Na Vinywaji Na Yanayohusiana Na Viwili Hivi
الصَّيْدُ وَأَحْكَامُهُ
Kuwinda Na Hukmu Zake
Alhidaaya.com [3]
05- Kuwinda Na Hukmu Zake: Njia Ya Pili Ya Uwindaji: Kuwinda Kwa Kutumia Silaha Za Kuwindia Kama Pinde, Mishale Na Mfano Wake.
[Al-Mughniy (9-301), na Al-Mufas-swal (3/14)].
Hakuna makhitilafiano yoyote kati ya ‘Ulamaa kuhusiana na uhalali wa kula kilichowindwa kwa kutumia pinde au mishale likitajwa Jina la Allaah wakati wa kufyetuliwa.
Katika Hadiyth ya ‘Adiyy bin Haatim, Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alimwambia:
"وَإِنْ رَمَيْتَ سَهْمَكَ فَاذْكُرِ اسْمَ اَللَّهِ ، فَإِنْ غَابَ عَنْكَ يَوْماً ، فَلَمْ تَجِدْ فِيهِ إِلَّا أَثَرَ سَهْمِكَ فَكُلْ إِنْ شِئْتَ "
“Na unapofyetua upinde wako, basi litaje Jina la Allaah. Na kama mnyama atapotea usimwone kwa siku moja, halafu usikute kwake isipokuwa athari ya mshale wako tu, basi mle ukipenda”. [Hadiyth Swahiyh. Imekharijiwa na Al-Bukhaariy (5484) na Muslim (1929), na tamshi ni lake].
Na katika Hadiyth ya Abu Tha-‘alabah, Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amemwambia:
"فَمَا أَصَبْتَ بِقَوْسِكَ فَاذْكُرِ اسْمَ اللَّهِ ، ثُمَّ كُلْ.."
“Na yule uliyempata kwa kumlenga na mshale wako, basi litaje Jina la Allaah, kisha mle”. [Hadiyth Swahiyh. Imekharijiwa na Al-Bukhaariy (5487) na Muslim (1930)]
Kuwinda Kwa Kutumia Kipande Kizito Cha Mti Chenye Ncha Mbele "الْمِعْرَاَضُ"
Kinaweza kuchongwa mbele kikawa na ncha, au kufungiwa nchani kipande cha chuma chenye ncha kali na kurushiwa nacho mnyama. Ikiwa kitampata mnyama kwa ncha yake, kikamjeruhi na mnyama akafa, basi ni halali kuliwa. Lakini kikimpata kwa ubavu wake (ubapa) –na si kwa ncha yake- kikamuua kutokana na uzito wake, basi mnyama anakuwa na hukmu ya kuuliwa kwa kupigwa na kitu kizito, na hapo anakuwa si halali kuliwa.
Hii ndio kauli ya Maimamu wanne na wengineo katika Jumhuwr. Na hii ni kwa Hadiyth ya ‘Adiyy bin Haatim aliyesema: Nilimuuliza Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kuhusiana na "الْمِعْرَاضُ" akaniambia:
"إِذَا أَصَابَ بِحَدِّهِ فَكُلْ ، وَإِذَا أَصَابَ بِعَرْضِهِ فَقُتِلَ فَلَا تَأْكُلْ ، فَإِنَّهُ وَقِيذٌ"
“Ikimpata kwa ncha yake, basi kula, lakini ikimpata kwa ubapa wake na mnyama akafa, basi usile, kwa kuwa ni mnyama aliyeuawa kwa kupigwa na kitu kizito”. [Hadiyth Swahiyh. Imekharijiwa na Al-Bukhaariy (2054) na Muslim (1929)].
Na zana au silaha zingine za kuwindia kama kipande hiki cha mti chenye ncha, ikiwa zitamuua mnyama kwa ubavu au ubapa wake bila kumjeruhi, basi mnyama si halali kuliwa. Ni kama mshale kumpiga ndege kwa ubapa wake ukamuua, au mkuki, au singe, au upanga, vyote hivyo vikipiga kwa ubapa mnyama akafa, basi ni haramu mnyama huyo kuliwa. Kadhalika, ikiwa silaha hizi zitampiga mnyama kwa ncha yake bila kumjeruhi lakini zikamuua kutokana na uzito wake, basi pia si halali kuliwa. Ni hii ni kwa neno lake Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam):
"وَإِذَا رَمَيْتَ بِالْمِعْرَاضِ فَخَزَقَ فَكُلْهُ"
“Ukimrushia mnyama mi’iradh ikamjeruhi, basi mle”. [Hadiyth Swahiyh. Imetajwa nyuma kidogo].
Rasuli amefanya ncha kupenya mwili wa mnyama na kumjeruhi, ni sharti ya kuhalalika kuliwa, na kwa kuwa kama haikumjeruhi, basi inakuwa imemua kwa uzito wake, na hapo inakuwa ni kama imemuua kwa ubapa wake. [Al-Mughniy (9/305) pamoja na nyongeza kidogo]
Swahiyh Fiqh As-Sunnah
كِتَابُ الأَطْعِمَةِ وَالأَشْرِبةِ وَمَا يَتَعَلَّقُ بِهِمَا
Kitabu Cha Vyakula Na Vinywaji Na Yanayohusiana Na Viwili Hivi
الصَّيْدُ وَأَحْكَامُهُ
Kuwinda Na Hukmu Zake
Alhidaaya.com [3]
06- Kuwinda Na Hukmu Zake: Njia Ya Tatu Ya Uwindaji: Kuwinda Kwa Bunduki
Bunduki za kuwindia za kisasa zinatumia risasi. Ziko risasi za mviringo, na ziko zenye ncha, na zote zinapenya kwenye mwili wa mnyama na kumjeruhi. Hivyo risasi hizi ni halali kuwindia.
Hapa inafaa kueleza kwamba Jumhuwr ya ‘Ulamaa wanashurutisha kwamba zana ya kuwindia ni lazima iwe na ncha kali!. Na hili linaweza kuwa ni mushkil juu ya uhalali wa kuwinda kwa kutumia bunduki yenye kutumia risasi za mviringo. Isipokuwa linaloonekana ni kwamba makusudio yao ya ncha kali ni kile chenye kupenya na kuingia ndani ya mwili wa mnyama na kumjeruhi. Na hiki ndicho kiini kama inavyoonekana katika dalili za suala hili. Na kwa muktadha huo, utata unaondoka. Allaah Ndiye Ajuaye zaidi.
Je, Inafaa Kuwinda Kwa Kutumia Jiwe, Fimbo Na Mfano Wa Hivyo?
[Al-Mughniy (9/313), Al-Muhallaa (7/460) na Naylul Awtwaar (8/156)]
Jiwe lisilo na ncha ambalo lau atapigwa nalo mnyama halitoweza kupenya ndani ya mwili wake au kumjeruhi, ikiwa jiwe hili litamuua, basi si halali kuliwa mnyama huyo, kwa kuwa anakuwa amekufa kwa kupigwa (na si kwa kujeruhiwa). Hii ndio kauli ya Fuqahaa wote. Na dalili zishaelezwa nyuma kuhusiana na sharti ya kuingia zana ya kuwindia ndani ya mwili wa mnyama na kumjeruhi, ili awe halali kuliwa.
Toka kwa ‘Abdullaah bin Mughaffal "رَضِيَ اللهُ عَنْهُ" amesema:
"أَنَّ رَسُوْلَ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ نَهَى عَنِ الْخَذْفِ وَقَالَ : "إِنَّهَا لاَ تَصِيْدُ صَيْدًا ، وَلاَ تَنْكَأُ عَدُوًا ، وَلكِنَّهَا تَكْسِرُ السِّنَّ وَتُفْقِأُ العَيْنَ"
“Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amekataza kutumia manati akisema: Manati haiwezi kuwinda mnyama, wala haiwezi kumjeruhi na kumuua adui, bali manati inavunja jino na inapofua jicho.” [Hadiyth Swahiyh. Imekharijiwa na Al-Bukhaariy (5479) na Muslim (1954)].
Akimpata Mnyama Baada Ya Masiku Kadhaa
Mwindaji akimlenga mnyama akampata kisha mnyama akapotea, halafu akaja kumpata hata baada ya kupita masiku –lakini si ndani ya maji- , basi atakuwa ni halali, lakini kwa sharti kwamba asiwe ameharibika, au ijulikane kwamba kilichomuua si silaha yake.
‘Adiyy bin Haatim amesema, Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) aliniambia:
إِذَا أَرْسَلْتَ كَلْبَكَ وَسَمَّيْتَ فَأَمْسَكَ وَقَتَلَ، فَكُلْ، وَإِنْ أَكَلَ فَلاَ تَأْكُلْ، فَإِنَّمَا أَمْسَكَ عَلَى نَفْسِهِ، وَإِذَا خَالَطَ كِلاَبًا لَمْ يُذْكَرِ اسْمُ اللَّهِ عَلَيْهَا فَأَمْسَكْنَ وَقَتَلْنَ فَلاَ تَأْكُلْ، فَإِنَّكَ لاَ تَدْرِي أَيُّهَا قَتَلَ، وَإِنْ رَمَيْتَ الصَّيْدَ فَوَجَدْتَهُ بَعْدَ يَوْمٍ أَوْ يَوْمَيْنِ، لَيْسَ بِهِ إِلاَّ أَثَرُ سَهْمِكَ، فَكُلْ، وَإِنْ وَقَعَ فِي الْمَاءِ فَلاَ تَأْكُلْ ".
“Ukimwachilia mbwa wako kukamata na ukalitaja Jina la Allaah, na mbwa akakamata na akaua, basi kula. Na kama amekula, basi usile, kwani anakuwa amejikamatia kwa ajili yake mwenyewe. Na ikiwa wamechanganyika naye mbwa wengineo ambao hawakutajiwa Jina la Allaah, wakakamata na wakaua, basi usile, kwani wewe hujui ni yupi kati yao aliyeua. Na kama utamlenga mnyama, na kisha ukampata baada ya siku moja au mbili, naye hana isipokuwa athari ya mshale wako, basi kula, lakini kama utamkuta ameanguka majini, basi usimle”. [Hadiyth Swahiyh. Imekharijiwa na Al-Bukhaariy (5484) na Muslim (1929)].
Links
[1] https://www.alhidaaya.com/sw/taxonomy/term/284
[2] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11329&title=08A-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20%D9%83%D9%90%D8%AA%D9%8E%D8%A7%D8%A8%D9%8F%20%D8%A7%D9%84%D8%A3%D9%8E%D8%B7%D9%92%D8%B9%D9%90%D9%85%D9%8E%D8%A9%D9%90%20%D9%88%D9%8E%D8%A7%D9%84%D8%A3%D9%8E%D8%B4%D9%92%D8%B1%D9%90%D8%A8%D8%A9-Kitabu%20Cha%20Vyakula%20Na%20Vinywaji%3A%20%D8%A7%D9%84%D8%B5%D9%91%D9%8E%D9%8A%D9%92%D8%AF%D9%8F%20%D9%88%D9%8E%D8%A3%D9%8E%D8%AD%D9%92%D9%83%D9%8E%D8%A7%D9%85%D9%8F%D9%87%D9%8F%20Kuwinda%20Na%20Hukmu%20Zake%20
[3] http://www.alhidaaya.com/
[4] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11332&title=01-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20Kitabu%20Cha%20Vyakula%20Na%20Vinywaji%3A%20Kuwinda%20Na%20Hukmu%20Zake%3ATaarifu%20Na%20Hukmu%20Ya%20Kuwinda%3A
[5] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11333&title=02-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20Kitabu%20Cha%20Vyakula%20Na%20Vinywaji%3A%20Kuwinda%20Na%20Hukmu%20Zake%3A%20Ni%20Wakati%20Gani%20Kuwinda%20Ni%20Marufuku%3F%20
[6] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11334&title=03-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20Kitabu%20Cha%20Vyakula%20Na%20Vinywaji%3A%20Kuwinda%20Na%20Hukmu%20Zake%3A%20Njia%20Za%20Uwindaji%3A%20Njia%20Ya%20Kwanza
[7] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11335&title=04-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20Kitabu%20Cha%20Vyakula%20Na%20Vinywaji%3A%20Kuwinda%20Na%20Hukmu%20Zake%3A%20Masharti%20Ya%20Mnyama%20Au%20Ndege%20Anayetumiwa%20Kuwinda%20Ili%20Akikamatacho%20Kiwe%20Halali%20Kuliwa%20
[8] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11336&title=05-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20Kitabu%20Cha%20Vyakula%20Na%20Vinywaji%3A%20Kuwinda%20Na%20Hukmu%20Zake%3A%20Njia%20Ya%20Pili%20Ya%20Uwindaji%3A%20Kuwinda%20Kwa%20Kutumia%20Silaha%20Za%20Kuwindia%20Kama%20Pinde%2C%20Mishale%20Na%20Mfano%20Wake
[9] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11377&title=06-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20Kitabu%20Cha%20Vyakula%20Na%20Vinywaji%3A%20Kuwinda%20Na%20Hukmu%20Zake%3A%20Njia%20Ya%20Tatu%20Ya%20Uwindaji%3A%20Kuwinda%20Kwa%20Bunduki%20