Tarehe Ya Hijriy

Kibainisho Muhimu

Ukumbusho Wa Swiyyaam (Funga) Za Ayyaamul-Biydhw Tarehe 13, 14, 15

 

Swiyaam (Funga) Za Siku Tatu Kila Mwezi Thawabu Zake

Ni Sawa Na Thawabu Za Swiyaam Za Milele!

Alhidaaya.com

 

 

Swiyaam (funga) za Ayyaamul-Biydhw (Masiku Meupe) ni tarehe 13, 14, 15 katika kila mwezi wa Kiislamu (Hijriyyah).  

 

 

Tanbihi: Isipowezekana kufunga Swiyaam za Ayyaamul-Biydhw, basi inajuzu kufunga siku tatu zozote nyengine katika mwezi ili kupata thawabu za Milele, na si lazima zifungwe mfululizo.

 

 

عَنْ أَبي ذَرٍّ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيهِ وَسَلَّمَ:((مَنْ صَامَ مِنْ كُلِّ شَهْرٍ ثَلاثَةَ أَيَّامٍ فَذَلِكَ صِيَامُ الدَّهْرِ)) فَأَنْزَلَ اللهُ تُصْدِيقَ ذَلِكَ في كِتَابِهِ الْكَرِيمِ: ((مَنْ جَاءَ بِالْحَسَنَةِ فَلَهُ عَشْرُ أَمْثَالِهَا))، الْيَوْمُ بِعَشَرَةِ أَيّامٍ. أخرجه أحمد والترمذي وقال حديث حسن ، والنسائي وابن ماجه وابن خزيمة

Imepokelew a kutoka kwa Abuu Dharr (Radhwiya Allaahu ‘anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Yeyote atakayefunga (Swawm) kila mwezi siku tatu, ni sawa na Swawm ya milele)) Kisha Allaah Akateremsha Aayah ithibitishayo hayo: “Atakayekuja kwa 'amali nzuri basi atapata (thawabu) kumi mfano wa hiyo.” Siku moja kwa malipo ya siku kumi. [Imepokewa na At-Tirmidhiy na amesema Hadiyth Hasan, An Nasaaiy na Ibn Maajah, Ibn Khuzaymah na ameisahihisha Al-Albaaniy katika Al-Irwaa (4/102)]. Aayah: Suwrat Al-An’aam (160)]

 

Maana Ya Al-Biydhw:  Masiku hayo yameitwa ‘Al-Biydhw’ (meupe) sababu usiku wa siku hizo hung'aa kutokana na mwanga wa mwezi. Ayyaam Al-Biydhw (Masiku Meupe) tarehe zake ni 13, 14 na 15 katika kila mwezi wa kalenda ya Kiislamu. Dalili ni Hadiyth zifuatazo:

 

Bonyeza Upate fadhila za Ayyaamul-Biydhw, fadhila za Swawm ya Jumatatu na Alkhamiys na fadhila za Swawm kwa ujumla.

 

 

Share