059-Asbaabun-Nuzuwl: Al-Hashr Aayah 01-04 سَبَّحَ لِلَّهِ مَا فِي السَّمَاوَاتِ وَمَا فِي الْأَرْضِ
أسْبابُ النُّزُول
Asbaabun-Nuzuwl
Sababu Za Kuteremshwa (Baadhi Ya Suwrah Na Aayaat Za Qur-aan)
Imekusanywa na: Alhidaaya.com
059-Suwrah Al-Hashr: Aayah 1 - 4
Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):
بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيم
سَبَّحَ لِلَّـهِ مَا فِي السَّمَاوَاتِ وَمَا فِي الْأَرْضِ ۖ وَهُوَ الْعَزِيزُ الْحَكِيمُ﴿١﴾
1. Vimemsabihi Allaah Pekee vilivyomo katika mbingu na vilivyomo katika ardhi, Naye ndiye Mwenye enzi ya nguvu Asiyeshindika, Mwenye hikmah wa yote.
هُوَ الَّذِي أَخْرَجَ الَّذِينَ كَفَرُوا مِنْ أَهْلِ الْكِتَابِ مِن دِيَارِهِمْ لِأَوَّلِ الْحَشْرِ ۚ مَا ظَنَنتُمْ أَن يَخْرُجُوا ۖ وَظَنُّوا أَنَّهُم مَّانِعَتُهُمْ حُصُونُهُم مِّنَ اللَّـهِ فَأَتَاهُمُ اللَّـهُ مِنْ حَيْثُ لَمْ يَحْتَسِبُوا ۖ وَقَذَفَ فِي قُلُوبِهِمُ الرُّعْبَ ۚ يُخْرِبُونَ بُيُوتَهُم بِأَيْدِيهِمْ وَأَيْدِي الْمُؤْمِنِينَ فَاعْتَبِرُوا يَا أُولِي الْأَبْصَارِ﴿٢﴾
2. Yeye Ndiye Aliyewatoa wale waliokufuru miongoni mwa Ahlil-Kitaabi kutoka majumbani mwao katika mkusanyiko wa kwanza. Hamkudhania kwamba watatoka, nao wakadhani kwamba husuni zao zitawakinga dhidi ya Allaah. Lakini hukmu ya Allaah ikawafikia kutoka ambako wasipotazamia, na Akavurumisha kiwewe katika nyoyo zao. Wanaziharibu nyumba zao kwa mikono yao na mikono ya Waumini, basi pateni funzo enyi wenye uoni wa kutia akilini.
وَلَوْلَا أَن كَتَبَ اللَّـهُ عَلَيْهِمُ الْجَلَاءَ لَعَذَّبَهُمْ فِي الدُّنْيَا ۖ وَلَهُمْ فِي الْآخِرَةِ عَذَابُ النَّارِ﴿٣﴾
3. Na lau kama Allaah Asingeliwaandikia kufukuzwa nchi, bila shaka Angeliwaadhibu duniani, na Aakhirah watapata adhabu ya moto.
ذَٰلِكَ بِأَنَّهُمْ شَاقُّوا اللَّـهَ وَرَسُولَهُ ۖ وَمَن يُشَاقِّ اللَّـهَ فَإِنَّ اللَّـهَ شَدِيدُ الْعِقَابِ﴿٤﴾
4. Hivyo kwa kuwa wao wamempinga Allaah na Rasuli Wake. Na yeyote anayempinga Allaah, basi hakika Allaah ni Mkali wa kuakibu.
Sababun-Nuzuwl:
حَدَّثَنِي عَبْدُ اللَّهِ بْنُ مُطِيعٍ، حَدَّثَنَا هُشَيْمٌ، عَنْ أَبِي بِشْرٍ، عَنْ سَعِيدِ بْنِ جُبَيْرٍ، قَالَ قُلْتُ لاِبْنِ عَبَّاسٍ سُورَةُ التَّوْبَةِ قَالَ آلتَّوْبَةِ قَالَ بَلْ هِيَ الْفَاضِحَةُ مَا زَالَتْ تَنْزِلُ وَمِنْهُمْ وَمِنْهُمْ . حَتَّى ظَنُّوا أَنْ لاَ يَبْقَى مِنَّا أَحَدٌ إِلاَّ ذُكِرَ فِيهَا . قَالَ قُلْتُ سُورَةُ الأَنْفَالِ قَالَ تِلْكَ سُورَةُ بَدْرٍ . قَالَ قُلْتُ فَالْحَشْرُ قَالَ نَزَلَتْ فِي بَنِي النَّضِيرِ .
Amenihadithia ‘Abdullaah bin Mutwiy’i, ametuhadithia Hushaym toka kwa Abiy Bishr toka kwa Sa’iyd bin Jubayr amesema: Nilimwambia Ibn ‘Abbaas: Suwrah At-Tawbah. Akasema: At-Tawbah. Akasema: Bali hiyo ni Al-Faadhwihah (Yenye kukashifu). Iliendelea kushuka (ikisema:) na miongoni mwao, na miongoni mwao mpaka wakadhani kuwa hatobaki mtu kati yetu ila atatajwa humo. Akasema: Nilisema Suwrah Al-Anfaal. Akasema: Hiyo ni Suwrah ya Badr. Akasema: Nikasema, na Al-Hashr ilishuka kwa Baniy An Nadhwiyr. [Muslim]
Na pia,
عن عائشة رضي الله عنها قالت: كانت غزوة بني النضير وهم طائفة من اليهود على رأس ستة أشهر من غزوة بدر وكان منزلهم ونخلهم بناحية المدينة فحاصرهم رسول الله صلى الله عليه وعلى آله وسلم حتى نزلوا على الجلاء، وعلى أن لهم ما أقلت الإبل من الأمتعة والأموال إلا الحلقة –يعني السلاح- فأنزل الله فيهم: ((سَبَّحَ لِلَّهِ مَا فِي السَّمَاوَاتِ وَمَا فِي الْأَرْضِ)) إلى قوله ((لِأَوَّلِ الْحَشْرِ مَا ظَنَنْتُمْ أَنْ يَخْرُجُوا)) فقاتلهم النبي صلى الله عليه وعلى آله وسلم حتى صالحهم على الجلاء، فأخلاهم إلى الشام، وكانوا من سبط لم يصبهم جلاء فيما خلا، وكان الله قد كتب عليهم ذلك، ولولا ذلك لعذبهم في الدنيا بالقتل والسبي وأما قوله: ((لِأَوَّلِ الْحَشْرِ)) فكان ذلك أول حشر في الدنيا إلى الشام.
Kutoka kwa ‘Aaishah ((رضي الله عنها) amesema: “Vita vya Baniy An-Nadhwiyr, nalo ni kundi la Mayahudi, vilikuwa vya kwanza baada ya miezi sita ya kumalizika Vita vya Badr. Makazi na mitende yao ilikuwa upande wa (kusini mwa) Al-Madiynah, na Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) aliwazingira mpaka wakakubali kuhama nchi, na akawaruhusu kuondoka na mizigo na mali zilizobebwa na ngamia wao isipokuwa silaha tu. Na hapo Allaah Akateremsha kuhusu wao:
((سَبَّحَ لِلَّهِ مَا فِي السَّمَاوَاتِ وَمَا فِي الْأَرْضِ)) إلى قوله ((لِأَوَّلِ الْحَشْرِ مَا ظَنَنْتُمْ أَنْ يَخْرُجُوا))
Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alipigana nao mpaka akawalazimisha kufikia suluhu ya wao kuondoka nchi, akawaondosha kwenda Sham. Walikuwa ni kabila (kati ya makabila ya Bani Israaiyl) ambao hawajawahi kufurushwa toka ardhi yao kabla ya hapo, na Allaah Alikuwa amewaandikia hilo, na lau si hilo, basi Angeliwaadhibu duniani kwa kuuawa na kutekwa.
Ama Neno Lake:
((لِأَوَّلِ الْحَشْر))
hili lilikuwa katika mkusanyiko wa kwanza duniani kwenda Sham.” [Al-Haakim ameikhariji katika mjeledi wa pili ukurasa 483, amesema ni Swahiyh kwa sharti ya Mashaykh wawili. Adh-Dhahabiy na Al-Bayhaqiy wameikubali katika Dalaail An Nubuwwah mjeledi wa pili ukurasa 444]
Aayah za Suwrah hiyo zinaendelea…
مَا قَطَعْتُم مِّن لِّينَةٍ أَوْ تَرَكْتُمُوهَا قَائِمَةً عَلَىٰ أُصُولِهَا فَبِإِذْنِ اللَّـهِ وَلِيُخْزِيَ الْفَاسِقِينَ﴿٥﴾
5. Hamkukata aina yoyote ya mtende au mliouacha umesimama juu ya mashina yake, basi ni kwa idhini ya Allaah na ili Awahizi mafasiki.
وَمَا أَفَاءَ اللَّـهُ عَلَىٰ رَسُولِهِ مِنْهُمْ فَمَا أَوْجَفْتُمْ عَلَيْهِ مِنْ خَيْلٍ وَلَا رِكَابٍ وَلَـٰكِنَّ اللَّـهَ يُسَلِّطُ رُسُلَهُ عَلَىٰ مَن يَشَاءُ ۚ وَاللَّـهُ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ﴿٦﴾
6. Na ngawira yeyote ile Aliyoifanya Allaah kwa Rasuli Wake kutoka kwao; basi hamkuyaendea mbio kwa farasi na wala vipando vya ngamia lakini Allaah Huwapa mamlaka na nguvu Rusuli Wake dhidi ya Amtakaye. Na Allaah juu ya kila kitu ni Muweza.
مَّا أَفَاءَ اللَّـهُ عَلَىٰ رَسُولِهِ مِنْ أَهْلِ الْقُرَىٰ فَلِلَّـهِ وَلِلرَّسُولِ وَلِذِي الْقُرْبَىٰ وَالْيَتَامَىٰ وَالْمَسَاكِينِ وَابْنِ السَّبِيلِ كَيْ لَا يَكُونَ دُولَةً بَيْنَ الْأَغْنِيَاءِ مِنكُمْ ۚ وَمَا آتَاكُمُ الرَّسُولُ فَخُذُوهُ وَمَا نَهَاكُمْ عَنْهُ فَانتَهُوا ۚ وَاتَّقُوا اللَّـهَ ۖ إِنَّ اللَّـهَ شَدِيدُ الْعِقَابِ﴿٧﴾
7. Ngawira Aliyotoa Allaah kwa Rasuli Wake kutoka kwa watu wa hivi vijiji ni kwa ajili ya Allaah na Rasuli na kwa ajili ya jamaa wa karibu, na mayatima, na masikini na msafiri aliyeharibikiwa, ili isiwe mzunguko wa zamu baina ya matajiri tu miongoni mwenu. Na lolote analokupeni Rasuli ((صلى الله عليه وآله وسلم basi lichukueni, na analokukatazeni, basi acheni. Na mcheni Allaah. Hakika Allaah ni Mkali wa kuakibu.