Kufunga (Swiyaam) Ramadhwaan Bila Kuswali Ni Hukmu Yake?
Hukmu Ya Kufunga Ramadhwaan Bila Ya Kuswali
SWALI:
Ipi hukumu ya mwenye kufunga Ramadhwaan bila ya Swalaah au akaswali katika Ramadhwaan na haswali (miezi) mingine?
JIBU:
AlhamduliLLaah Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aala) Rabb wa walimwengu, Swalaah na salamu zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho.
Ama Swawm yake, Zakaah yake, Hajj yake au yasiyokuwa hayo katika ´amali zake bila ya Swalaah hazitomfaa. Kwa kuwa la sahihi ni kuwa mwenye kuacha Swalaah ni kafiri, kutokana na dalili maalumu, miongoni mwazo ni Hadiyth:
"Ahadi iliyoko baina yetu na wao (makafiri) ni Swalaah, mwenye kuiacha amekufuru."
Na Hadiyth:
"Baina ya mtu na kafiri na shirki ni kuacha Swalaah."
Hadiyth hizi mbili ni sahihi na dalili zake ziko wazi. Ama anayeswali katika Ramadhwaan na haswali (miezi) mingine, Allaah (´Azza wa Jalla) Akimfisha akiwa ni mwenye kuswali, huenda ikatarajiwa ikawa kwake hiyo ndio tawbah ya mwisho nzuri kwake.
Kwa kuwa haijulikani kwenye moyo wake kuwa ataacha Swalaah baada ya Ramadhwaan. Na akirudia kuacha Swalaah na akafiri naye ni mwenye kuacha Swalaah, atakuwa kama wengineo wenye kuacha Swalaah.
Watu watataamiliana naye kama anavyotaamiliwa mwenye kauacha Swalaah. Hakika mwenye kuacha Swalaah, sawa kaacha kwa wakati mdogo au mfupi bila ya udhuru, ni kama aliyeacha kwa wakati mrefu au zaidi – ni hali moja. Hilo linapewa nguvu na kauli ya Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam):
"Mwenye kuacha Swalaah ya Alasiri zimeporomoka ´amali zake."
Hii ni Swalaah moja akiiacha mja huporomoka (huharibika) ´amali zake.
Na Allaah Ni Mjuzi Zaidi.