Kumsomea Maiti Qur-aan Kama Suwrah Al-Faatihah Nini Hukmu Yake?

 

Kumsomea Maiti Qur-aan Nini Hukmu Yake?

 

Alhidaaya.com

 

 

 

SWALI:

 

Nini hukmu ya mwenye kusoma Al-Faatihah au chochote katika Qur-aan kuwasomea Maiti?

 

 

JIBU:

 

AlhamduliLLaah Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aala) Rabb wa walimwengu, Swalaah na salamu zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

 

Hili ni jambo la kuzushwa. Hakulifanya Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wasallam) wala Maswahaba zake (Ridhwaanu Allaahi ‘alayhim), hawakuwa wakiwasomea Maiti (Suwrat) Al-Faatihah, au Aayatul-Kursiy, au Al-Mu’awwidhatayn (Suwraah Al-Falaq na An-Naas), au Al-Ikhlaasw, au chochote katika Qur-aan.

 

 

Amesema (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam):

“Mwenye kuzusha katika jambo letu (Dini yetu) hili ambalo halimo, basi hurudishwa (halipokelewi).”[Al-Bukhaariy na Muslim]

 

 

Na amesema Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam):

“Hakika Allaah Kazuia tawbah ya mwenye kufanya bid’ah mpaka aache bid’ah yake.”

 

 

Inapasa (aache hilo na afanye) tawbah kwa kitendo hicho.

 

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

 

 

 

 

 
Share