09-Imaam Ibn 'Uthaymiyn: Akiona Damu Isiyothibitika Kuwa Ni Hedhi Nini Hukmu Ya Swawm Yake?
09-Akiona Damu Isiyothibitika Kuwa Ni Hedhi Nini Hukmu Ya Swawm Yake
Fataawaa Mas-ala 60 Kuhusu Hedhi Na Nifaas
Imaam Ibn 'Uthaymiyn (Rahimahu-Allaah)
SWALI:
Mwanamke akiona damu lakini hakuthibitisha au kuwa na hakika kuwa ni damu ya hedhi. Ni nini hukumu ya Swawm yake siku ile?
JIBU:
Swawm yake siku ile ni sahihi kwani asili ya jambo ni kuwa hana hedhi hadi athibitishe kuwa ana hedhi.
