07-Imaam Ibn 'Uthaymiyn: Kukopa kwa Ajili ya Udhwhiya Inafaa?
Kukopa kwa Ajili ya Udhwhiya Inafaa?
Imaam Ibn ‘Uthaymiyn (Rahimahu-Allaah)
SWALI:
Fakiri ambaye hana chochote mkononi pindi 'Iydul-Adhw-haa inapofika lakini ni mwenye kutarajia kupokea mshahara wake wa mwezi basi na akope achinje kisha alipe?
JIBU:
Kama hatoweza kulipa kwa muda wa karibu basi haifai kwake kukopa ili achinje kwani hili litamfanya ashughulike na kulipa deni.
[Majmuw’ Al-Fataawaa (25/110)]