25-Imaam Ibn 'Uthaymiyn: Damu Inaendelea Na Inakatika Siku Moja Au Mbili Kisha Inarudi
Fataawaa Mas-ala 60 Kuhusu Hedhi Na Nifaas
Imaam Ibn 'Uthaymiyn (Rahimahu-Allaah)
25-Damu Inaendelea Na Inakatika Siku Moja Au Mbili Kisha Inarudi
SWALI:
Baadhi ya wanawake damu inaendelea na wakati mwingine inakatika siku moja au mbili kisha inarudi. Nini hukumu ya hali hii kwa Swalaah na Swiyaam na ‘Ibaadah zingine?
JIBU:
Kinachojulikana kwa ‘Ulamaa ni kuwa mwanamke akiwa kwenye ada yake kisha ikakatika anakoga na kuswali na kufunga na anachokiona baada ya siku mbili au tatu sio hedhi, kwa sababu tohara chache kwa ‘Ulamaa hao ni siku kumi na tatu.
Wamesema baadhi ya ‘Ulamaa kuwa “Muda wowote akiona damu basi ni hedhi na muda akitoharika kwayo basi ni tohara na hata kama sio kati ya hedhi mbili siku kumi na tatu.”