27-Imaam Ibn 'Uthaymiyn: Kuonja Chakula Mchana Wa Ramadhwaan Kwa Mwenye Swawm Inafaa?
Fataawaa Mas-ala 60 Kuhusu Hedhi Na Nifaas
27-Kuonja Chakula Mchana Wa Ramadhwaan Kwa Mwenye Swawm Inafaa?
Imaam Ibn 'Uthaymiyn (Rahimahu-Allaah)
SWALI:
Nini hukumu ya kuonja chakula katika mchana wa Ramadhwaan kwa mwanamke aliyefunga?
JIBU:
Si vibaya kulingana na haja iliyopo lakini ateme anachokionja baada ya kuonja.
