30-Imaam Ibn 'Uthaymiyn: Hakulipa Deni La Swiyaam Kwa Kutokujua Siku Alizofungulia Afanyeje?

 

Fataawaa Mas-ala 60 Kuhusu Hedhi Na Nifaas

 

30-Hakulipa Deni La Swiyaam Kwa Kutokujua Siku Alizofungulia  Afanyeje?

 

Imaam Ibn 'Uthaymiyn (Rahimahu-Allaah)

  

Alhidaaya.com

 

 

 

SWALI:

 

Muulizaji anauliza: Tokea imuwajibikie Swiyaam, amekuwa akifunga Ramadhawaan lakini hakuwa akilipa siku alizoshindwa kufunga kwa sababu ya ada yake ya mwezi na vile kutokujua siku alizofungua. Anaomba maelekezo cha anachotakiwa kufanya?

 

 

JIBU:

 

Inatusikitisha kutokea mas-ala kama haya  kwa wanawake Waislaam.

 

Kuacha huku, yaani kuacha kulipa deni (la Swiyaam)  za kumuwajibikia, itakuwa ni ima kwa sababu ya ujahili au kwa sababu ya uzembe, na yote hayo yote ni msiba, kwa kuwa ujahili tiba yake ni  elimu na  kuuliza.

 

Ama uzembe tiba yake  ni taqwa ya Allaah ('Azza wa Jalla)  na kuchunga maamrisho Yake na kuogopa adhabu Yake na kukimbilia kufanya yale yenye kumridhisha.

 

Hivyo ni juu ya mwanamke huyu kutubia kwa Allaah kwa alichokifanya na aombe maghfirah na kujaribu kukumbuka siku alizoacha kwa kadiri ya uwezo wake na alipe. Kwa haya dhima yake itaondoka na tunataraji Allaah Ataqabali tawbah yake.    

   

 

 

Share