Imaam Ibn 'Uthaymiyn: Wanawake Na Wanaume Kupeana Mikono Katika Hafla Kwa Ajili Ya Kupongeza

 

Wanawake Na Wanaume Kupeana Mikono (Katika Hafla Kwa Ajili Ya Kupongeza)

 

Imaam Ibn ‘Uthaymiyn (Rahimahu-Allaah)

 

www.alhidaaya.com

 

 

SWALI:

 

Je, inaruhusiwa mwanamume kumpa mkono mwanamke ambaye si mahram wake; ukizingatia kuwa wanaume husimama kwa ajili ya kuheshimiana na hupeana  mikono?   

 

 

JIBU:

 

Haijuzu mwaname kumpa mkono wake mwanamume ambaye sio mahram wake. Vivyo hivyo haijuzu mwanamke naye kumpa mkono wake mwanamume ambaye si marham wake, kwa sababu imeharamishwa mwanamume kugusa ngozi ya mwanamke ambaye si mahram wake kwani ni sawa na haramisho la kumtazama, bali kupeana mikono ni hatari zaidi inayopelekea fitnah.

 

 

[Fataawaa Nuwr ‘Alad-Darb Swali 5852 11/276]

Share