49-Imaam Ibn 'Uthaymiyn: Amehirimia ‘Umrah Akapatwa Hedhi Na Mahram Wake Ilibidi Asafari
Fataawaa Mas-ala 60 Kuhusu Hedhi Na Nifaas
49-Amehirimia ‘Umrah Akapatwa Hedhi Na Mahram Wake Ilibidi Asafari
Imaam Ibn 'Uthaymiyn (Rahimahu-Allaah)
SWALI:
Mwanamke alipohirimia ‘Umrah alipofika Makkah akapatwa na hedhi na mahram wake akatakiwa asafiri haraka na hana mtu mwengine Makkah ni nini hukumu yake?
JIBU:
Anatakiwa asafiri naye akiwa pamoja na ihraam yake kisha atarejea akitwaharika ikiwa mtu huyu anaishi Saudi Arabia kwani kurudi kwake kutakua wepesi kwa sababu hahitajii passport au mfano wake. Ama akiwa ni mgeni na kurudi kwake ni kwa taabu basi itabidi atufu na kufanya Sa’y na kupunguza nywele na kumaliza ‘Umrah yake katika safari hiyo hiyo ya awali, kwani Twawaaf yake wakati huo itakuwa ni jambo la dharura na dharura huhalalisha yaliyokatazwa.