51-Imaam Ibn 'Uthaymiyn: Ametekeleza ‘Ibaadah Zote Za Hajj Isipokuwa Twawaaf Al-Ifaadhwah Na Al-Widaa’ Akarudi Nyumbani Akajivua Katika Ihraam
Fataawaa Mas-ala 60 Kuhusu Hedhi Na Nifaas
51-Ametekeleza ‘Ibaadah Zote Za Hajj Isipokuwa Twawaaf Al-Ifaadhwah
Na Al-Widaa’ Akarudi Nyumbani Akajivua Katika Ihraam
Imaam Ibn 'Uthaymiyn (Rahimahu-Allaah)
SWALI:
Muulizaji anauliza: Nilitekeleza ‘Ibaadah ya Hajj mwaka uliopita na nikatekeleza ‘ibaadah zote za Hijjah isipokuwa Twawaaf Al-Ifaadhwah na Twawaaf Al-Widaa’ na kilichonizuia ni udhuru wa ki-Shariy’ah na hivyo nikarejea nyumbani kwangu Madinah Al-Munawwarah ili baadae nirejee siku nyingine na nipate kufanya Twawaaf Al-Ifaadhwah na Twawaaf Al-Widaa’. Isipokuwa sijui baadhi ya mambo ya dini hivyo nilitahallal (kujivua Ihraam) na nikaacha kila kitu chenye kukatazwa wakati wa Ihraam na nikauliza kuhusu kurudi kwangu ili nifanye Twawaaf, nikaambiwa kuwa haisihi kwangu kutufu kwani nilishaharibu kila kitu na natakiwa nihiji tena kwa mara nyingine mwakani pamoja na kuchinja ng’ombe au ngamia. Je hii ni sahihi? Je kuna utatuzi mwingine zaidi ya huu? Ni kweli Hijjah yangu imeharibika? Na juu yangu kurejea upya? Nijulisheni ninachoweza kukifanya Baaraka Allaahu Fiykum.
JIBU:
Hili nalo ni balaa lingine kutoa Fatwa pasina kuwa na elimu. Katika hali yako hii inabidi urudi tena Makka na ufanye Twaaf Al-Ifaadhwah peke yake. Ama Twawaaf Al-Widaa’ sio juu yako kwani madamu ulikuwa na hedhi ulipokuwa unatoka Makkah na hilo ni kwa sababu mwenye hedhi haiwi lazima kwako Twawaaf Al-Widaa’ kwa Hadiyth ya Ibn ‘Abaas (Radhwiya-Allaahu ‘anhumaa): “Watu wameamrishwa ahadi yao katika nyumba isipokuwa imewepesishwa kwa mwenye hedhi.” Katika riwaya ya Abuu Daawuwd “Ili ahadi yao ya mwisho na kutufu nyumba.”
Kwa sababu Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alipoambiwa kuwa Swafiyyah ametufu Twawaaf Al-Ifaadhwah alisema, “Basi na achukie au aache basi.” Na imetoa dalili hili kuwa Twawaaf Al-Widaa’ huanguka kwa mwenye hedhi. Ama Twawaaf Al-Ifaadhwah huna budi nayo. Na kwa sababu ulishatahallal (uliondoka kwenye ihraam) kwa kila kitu ukiwa hufahamu basi hili halitokudhuru kitu katika yaliyokatazwa kwa aliyehirimia hakuna kitu juu yake kwa kauli yake Ta’aala:
رَبَّنَا لاَ تُؤَاخِذْنَا إِن نَّسِينَا أَوْ أَخْطَأْنَا
“Rabb wetu Usituchukulie tukisahau au tukikosea. [Al-Baqarah:286]
Na kauli Yake Ta’alaa vile vile:
وَلَيْسَ عَلَيْكُمْ جُنَاحٌ فِيمَا أَخْطَأْتُم بِهِ وَلَـٰكِن مَّا تَعَمَّدَتْ قُلُوبُكُمْ
Na walio katika ulinzi wenu, na wala hakuna dhambi juu yenu katika yale mliyoyakosea, lakini isipokuwa katika yale yaliyoyakusudia nyoyo zenu. [Al-Ahzaab : 5]
Hivyo makatazo yote ambayo Allsah Amekataza kwa aliyehirimia akifanya asiyefahamu au mtu aliyesahau au kulazimishwa hana kitu juu yake, lakini muda wowote utakapoondoka udhuru wake basi inampasa aache lililomchanganya.