37-Fadhila Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Amefutiwa Madhambi Yake Yote Yaliyotangulia Na Ya Yaliyo Mbele Yake
Fadhila Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)
37-Amefutiwa Madhambi Yake Yote Yaliyotangulia Na Ya Yaliyo Mbele Yake
Anasema Allaah (عزّ وجلّ):
إِنَّا فَتَحْنَا لَكَ فَتْحًا مُّبِينًا ﴿١﴾ لِّيَغْفِرَ لَكَ اللَّـهُ مَا تَقَدَّمَ مِن ذَنبِكَ وَمَا تَأَخَّرَ وَيُتِمَّ نِعْمَتَهُ عَلَيْكَ وَيَهْدِيَكَ صِرَاطًا مُّسْتَقِيمًا ﴿٢﴾
Hakika Tumekupa ushindi (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم ambao ni) ushindi wa dhahiri. Ili Allaah Akughufurie yale yaliyotangulia katika madhambi yako na yale yanayokuja; na Akutimizie neema Yake juu yako na Akuongoze njia iliyonyooka. [Al-Fat-h: 1-2]
Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akafurahi mno kuteremshiwa kwake Aayah hiyo kama ilivyothibiti katika Hadiyth:
عَنْ أَنَسٍ، رضى الله عنه قَالَ أُنْزِلَتْ عَلَى النَّبِيِّ صلى الله عليه وسلمَ : ((ليغْفِرَ لَكَ اللَّهُ مَا تَقَدَّمَ مِنْ ذَنْبِكَ وَمَا تَأَخَّر))َ مَرْجِعَهُ مِنَ الْحُدَيْبِيَةِ فَقَالَ النَّبِيُّ صلى الله عليه وسلم " لَقَدْ أُنْزِلَتْ عَلَىَّ آيَةٌ أَحَبُّ إِلَىَّ مِمَّا عَلَى الأَرْضِ ثُمَّ قَرَأَهَا النَّبِيُّ صلى الله عليه وسلم عَلَيْهِمْ فَقَالُوا هَنِيئًا مَرِيئًا يَا نَبِيَّ اللَّهِ قَدْ بَيَّنَ اللَّهُ لَكَ مَاذَا يُفْعَلُ بِكَ فَمَاذَا يُفْعَلُ بِنَا فَنَزَلَتْ عَلَيْهِ: ((ليُدْخِلَ الْمُؤْمِنِينَ وَالْمُؤْمِنَاتِ جَنَّاتٍ تَجْرِي مِنْ تَحْتِهَا الأَنْهَارُ)) حَتَّى بَلَغَ : ((فوزًا عَظِيمًا )) قَالَ هَذَا حَدِيثٌ حَسَنٌ صَحِيحٌ .
Anas bin Maalik amehadithia kwamba: Tulipokuwa tunarudi kutoka Hudaybiyah, iliteremshwa kwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم):
لِّيَغْفِرَ لَكَ اللَّـهُ مَا تَقَدَّمَ مِن ذَنبِكَ وَمَا تَأَخَّرَ وَيُتِمَّ نِعْمَتَهُ عَلَيْكَ وَيَهْدِيَكَ صِرَاطًا مُّسْتَقِيمًا﴿٢﴾
Ili Allaah Akughufurie yale yaliyotangulia katika madhambi yako na yale yanayofuatia; na Akutimizie neema Yake juu yako na Akuongoze njia iliyonyooka.
Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akasema: “Hakika nimeteremshiwa Aayah ambayo ni kipenzi mno kuliko chochote kilichoko duniani.” Kisha Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akawasomea Aayah hiyo, wakasema: Hongera kwako ee Nabiy wa Allaah, hakika Allaah Amekubainishia Atakalokufanyia, lakini je Atatufanyia nini sisi? Hapo ikateremshwa:
لِّيُدْخِلَ الْمُؤْمِنِينَ وَالْمُؤْمِنَاتِ جَنَّاتٍ تَجْرِي مِن تَحْتِهَا الْأَنْهَارُ خَالِدِينَ فِيهَا وَيُكَفِّرَ عَنْهُمْ سَيِّئَاتِهِمْ ۚ وَكَانَ ذَٰلِكَ عِندَ اللَّـهِ فَوْزًا عَظِيمًا﴿٥﴾
Ili Awaingize Waumini wa kiume na Waumini wa kike Jannaat zipitazao chini yake mito, ni wenye kudumu humo, na Awafutie maovu yao; na kukawa huko mbele ya Allaah, ni kufuzu adhimu. [Al-Fat-h: 5]
[At-Tirmidhiy Amesema Hadiyth Hasan Swahiyh]