39-Fadhila Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Amepewa Al-Kawthar (Mto Ulioko PeponiWenye Kheri Nyingi)

 

Fadhila Za  Nabiy  (صلى الله عليه وآله وسلم)

 

39-Amepewa Al-Kawthar (Mto Ulioko Peponi Wenye Kheri Nyingi)

 

Alhidaaya.com

 

 

 

عَنْ أَنَسٍ (رضي الله عنه) : ((إِنَّا أَعْطَيْنَاكَ الْكَوْثَرَ)) أَنّ النَّبِيَّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، قَالَ: ((هُوَ نَهْرٌ فِي الْجَنَّةِ))

Anas (رضي الله عنه) amehadithia (kuhusu Kauli Yake Allaah): “Hakika Sisi Tumekupa Al-Kawthar”; kuwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Huo ni Mto katika Jannah.” [Al-Bukhaariy, At-Tirmidhiy]  

 

 

 

عَنْ أَنَسٍ، قَالَ: بَيْنَا رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم ذَاتَ يَوْمٍ بَيْنَ أَظْهُرِنَا إِذْ أَغْفَى إِغْفَاءَةً ثُمَّ رَفَعَ رَأْسَهُ مُتَبَسِّمًا فَقُلْنَا: مَا أَضْحَكَكَ يَا رَسُولَ اللَّهِ؟  قَالَ: ((أُنْزِلَتْ عَلَىَّ آنِفًا سُورَةٌ ))‏. فَقَرَأَ: (( بِسْمِ اللَّهِ الرَّحْمَنِ الرَّحِيمِ * إِنَّا أَعْطَيْنَاكَ الْكَوْثَرَ * فَصَلِّ لِرَبِّكَ وَانْحَرْ * إِنَّ شَانِئَكَ هُوَ الأَبْتَرُ)).‏ ثُمَّ قَالَ: ((أَتَدْرُونَ مَا الْكَوْثَرُ؟)). فَقُلْنَا اللَّهُ وَرَسُولُهُ أَعْلَمُ.‏ قَالَ: ((فَإِنَّهُ نَهْرٌ وَعَدَنِيهِ رَبِّي عَزَّ وَجَلَّ عَلَيْهِ خَيْرٌ كَثِيرٌ هُوَ حَوْضٌ تَرِدُ عَلَيْهِ أُمَّتِي يَوْمَ الْقِيَامَةِ آنِيَتُهُ عَدَدُ النُّجُومِ فَيُخْتَلَجُ الْعَبْدُ مِنْهُمْ فَأَقُولُ رَبِّ إِنَّهُ مِنْ أُمَّتِي‏.‏ فَيَقُولُ مَا تَدْرِي مَا أَحْدَثَتْ بَعْدَكَ))‏.‏ زَادَ ابْنُ حُجْرٍ فِي حَدِيثِهِ بَيْنَ أَظْهُرِنَا فِي الْمَسْجِدِ‏.‏ وَقَالَ:‏ ((مَا أَحْدَثَ بَعْدَكَ))‏.

 

Amesimulia Anas (رضي الله عنه): Siku moja Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alikuwa pamoja nasi akawa amepitiwa na lepe la usingizi kisha akanyanyua kichwa chake juu huku akitabasamu, tukasema: Ni kitu gani kimekufurahisha ee Rasuli wa Allaah? Akasema: “Imeniteremkia sasa hivi Suwrah: (Akaisoma Suwrah Al-Kawthar).

 

بِسْمِ اللَّهِ الرَّحْمَنِ الرَّحِيمِ * إِنَّا أَعْطَيْنَاكَ الْكَوْثَرَ * فَصَلِّ لِرَبِّكَ وَانْحَرْ * إِنَّ شَانِئَكَ هُوَ الأَبْتَرُ *

 [Al-Kawthar: (108)]  

 

Kisha akasema: “Je, mnajua ni nini Al-Kawthar?” Tukajibu: Allaah na Rasuli Wake Ndio Wajuao zaidi. Akasema: “Huo ni mto ambao Allaah (عزّ وجلّ) Ameniahidi. Una kheri nyingi sana, nao una hodhi lake ambalo Ummah wangu watakusudia kulifikia Siku ya Qiyaamah. Vyombo vyake (au bilauri) ni idadi ya nyota. Mja miongoni mwao atatolewa mbali atengwe. Nitasema: Ee Rabb! Hakika yeye ni katika Ummah wangu!  Allaah Atasema: Hujui nini alizusha baada yako!”

 

Ibn Hujri amezidisha katika Hadiyth yake: Alikuwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) amekaa kitako pamoja nasi Msikitini. Na (Allaah) Atasema: “Hujui walichokizusha baada yako!” [Muslim – Kitaab Asw-Swalaah - Mlango wa hoja anayesema kuwa Al-Basmalah ni Aayah katika kila mwanzo wa Suwrah isipokuwa Suwrah Al-Baraa (At-Tawbah)] 

 

 

Share