02-Buluwgh Al-Maraam: Kitabu Cha Jihaad: Mlango Wa Jizya Na Kusitisha Vita

 

بُلُوغُ الْمَرام

Buluwgh Al-Maraam

 

كِتَابُ اَلْجِهَادِ

Kitabu cha Jihaad

 

بَاب اَلْجِزْيَةَ وَالْهُدْنَةَ

02-Mlango Wa Jizya Na Kusitisha Vita[1]

 

 

 

 

1122.

عَنْ عَبْدِ اَلرَّحْمَنِ بْنِ عَوْفٍ ‏ رضى الله عنه ‏ {أَنَّ اَلنَّبِيَّ ‏ صلى الله عليه وسلم ‏أَخَذَهَا ‏ يَعْنِي: اَلْجِزْيَةُ ‏ مِنْ مَجُوسِ هَجَرَ} رَوَاهُ اَلْبُخَارِيُّ ‏ ‏وَلَهُ طَرِيقٌ فِي "اَلْمَوْطَأِ" فِيهَا اِنْقِطَاعٍ

Kutoka kwa ‘Abdur-Rahmaan bin ‘Awf (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema kuwa Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ): “Alichukua Jizya kutoka kwa Majusi wa Hajar.” [Imetolewa na Al-Bukhaariy]. Nayo ina njia nyingine iliyopokewa katika kitabu cha Al-Mawtwa ambayo ni Munqatwi’.

 

 

 

1123.

وَعَنْ عَاصِمِ بْنِ عُمَرَ، عَنْ أَنَسٍ، وَعَنْ ‏ عُثْمَانَ بْنِ أَبِي سُلَيْمَانَ، {أَنَّ اَلنَّبِيَّ ‏ صلى الله عليه وسلم ‏بَعْثٍ خَالِدُ بْنُ اَلْوَلِيدِ إِلَى أُكَيْدِرِ دُومَةَ، فَأَخَذُوهُ ،‏ فَحَقَنَ دَمِهِ، وَصَالَحَهُ عَلَى اَلْجِزْيَةِ} رَوَاهُ أَبُو دَاوُدَ

Kutoka kwa ‘Aaswim[2] bin ‘Umar naye kutoka kwa Anas na kutoka kwa ‘Uthmaan bin Abiy Sulaymaan[3] amesema kuwa: “Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alimtuma Khaalid bin Al-Waliyd aende kwa Ukaydir Duwmah,[4] wakamchukua, wakamleta kwa Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) naye akahifadhi damu yake na akasuluhishiana naye kwa kutoa Jizya.” [Imetolewa na Abuu Daawuwd]

 

 

 

1124.

وَعَنْ مُعَاذِ بْنِ جَبَلٍ ‏ رضى الله عنه ‏ قَالَ: {بَعَثَنِي اَلنَّبِيُّ ‏ صلى الله عليه وسلم ‏إِلَى اَلْيَمَنِ، وَأَمَرَنِي أَنْ آخُذَ مِنْ كُلِّ حَالِمٍ دِينَاراً، أَوْ عَدْلَهُ معافرياً} أَخْرَجَهُ اَلثَّلَاثَةِ، وَصَحَّحَهُ اِبْنُ حِبَّانَ، وَالْحَاكِمُ

Kutoka kwa Mu’aadh bin Jabal (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema kuwa: “Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alinituma Yemen akaniamrisha nichukue dinari moja (Jizya)[5] kwa kila aliyebaleghe au kinacholingana na dinari katika nguo za makafiri.”[6] [Imetolewa na Ath-Thalaathah (At-Tirmidhiy, An-Nasaaiy, Abuu Daawuwd) na akaisahihisha Ibn Hibbaan na Al-Haakim]

 

 

 

1125.

وَعَنْ عَائِذٍ بْنُ عَمْرِوِ الْمُزَنِيِّ ‏ رضى الله عنه ‏ عَنْ اَلنَّبِيِّ ‏ صلى الله عليه وسلم ‏قَالَ: {"اَلْإِسْلَامِ يَعْلُو، وَلَا يُعْلَى"} أَخْرَجَهُ اَلدَّارَقُطْنِيُّ

Kutoka kwa ‘Aaidh bin ‘Amr Al-Muzaniyy[7] (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema kuwa Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Uislamu unakuwa juu wala haukaliwi juu.”[8] [Imetolewa na Ad-Daaraqutwniy]

 

 

 

1126.

وَعَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ ‏ رضى الله عنه ‏ أَنَّ رَسُولَ اَللَّهِ ‏ صلى الله عليه وسلم ‏قَالَ: {" لَا تَبْدَؤُوا اَلْيَهُودَ وَالنَّصَارَى بِالسَّلَامِ، وَإِذَا لَقِيتُمْ أَحَدَهُمْ فِي طَرِيقٍ، فَاضْطَرُّوهُ إِلَى أَضْيَقِهِ"} رَوَاهُ مُسْلِمٌ

Kutoka kwa Abuu Hurayrah (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema kuwa Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Msianze kuwasalimia Mayahudi na Manaswaara[9] mtakapokutana na mmoja wao njiani msongeni kwenye dhiki zaidi.” [Imetolewa na Muslim]

 

 

 

1127.

وَعَنْ اَلْمِسْوَرِ بْنُ مَخْرَمَةَ.‏ وَمَرْوَانُ، {أَنَّ اَلنَّبِيَّ ‏ صلى الله عليه وسلم ‏خَرَجَ عَامَ اَلْحُدَيْبِيَةِ.‏ ….‏.‏ فَذَكِّرْ اَلْحَدِيثَ بِطُولِهِ، وَفِيهِ: " هَذَا مَا صَالَحَ عَلَيْهِ مُحَمَّدُ بْنُ عَبْدِ اَللَّهِ سُهَيْلِ بْنِ عَمْرِوٍ: عَلَى وَضْعِ اَلْحَرْبِ عَشْرِ سِنِينَ، يَأْمَنُ فِيهَا اَلنَّاسُ، وَيَكُفُّ بَعْضُهُمْ عَنْ بَعْضِ"} أَخْرَجَهُ أَبُو دَاوُدَ ‏وَأَصْلِهِ فِي اَلْبُخَارِيّ

وَأَخْرُجَ مُسْلِمٍ بَعْضِهِ مِنْ حَدِيثِ أَنَسٍ، وَفِيهِ: {أَنَّ مَنْ جَاءَ مِنْكُمْ لَمْ نَرُدْهُ عَلَيْكُمْ، وَمَنْ جَاءَكُمْ مِنَّا رَدَدْتُمُوهُ عَلَيْنَا.‏ فَقَالُوا: أَنَكْتُبُ هَذَا يَا رَسُولُ اَللَّهُ؟ قَالَ: "نَعَمْ.‏ إِنَّهُ مِنْ ذَهَبٍ مِنَّا إِلَيْهِمْ فَأَبْعَدَهُ اَللَّهُ، وَمَنْ جَاءَنَا مِنْهُمْ، فَسَيَجْعَلُ اَللَّهُ لَهُ فَرَجاً وَمُخْرِجاً"}

Kutoka kwa Al-Miswari bin Makhramah na Marwaan[10] wamesema kuwa: “Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alitoka mwaka wa vita vya Hudaybiyah… akataja Hadiyth kwa urefu wake: “Hivi ndivyo[11] Muhammad bin ‘Abdillaah alivyosulihishana na Suhayl bin ‘Amr[12] juu ya kuacha vita kwa muda wa miaka kumi ndani yake watu watakuwa na amani, na baadhi yao watajizuia kushambulia wengine.” [Imetolewa na Abuu Daawuwd na asili yake imo katika Al-Bukhaariy]

Na Muslim amepokea baadhi yake kutoka katika Hadiyth ya Anas: “Anayetujia kutoka kwenu, sisi hatumrudishi na atakayewajia nyinyi miongoni mwetu mutamrudisha kwetu. Maswahaba wakamuuliza: ‘Unaandika hili Ee Rasuli wa Allaah! Akasema ndiyo. Atakayewaendea wao miongoni mwetu, Allaah Amuepushe na Rahmah Zake, na atakayetujia sisi miongoni mwao, basi Allaah Amjaalie faraja na pa kutokea.”

 

 

 

1128.

وَعَنْ عَبْدِ اَللَّهِ بْنِ عَمْرِوٍ ، ‏ عَنْ اَلنَّبِيِّ ‏ صلى الله عليه وسلم ‏قَالَ: {"مِنْ قَتْلِ مُعَاهِداً لَمْ يَرَحْ رَائِحَةَ اَلْجَنَّةِ، وَإِنَّ رِيحَهَا لِيُوجَدَ مِنْ مَسِيرَةِ أَرْبَعِينَ عَامّاً"} أَخْرَجَهُ اَلْبُخَارِيُّ

Kutoka kwa ‘Abdillaah bin ‘Amr amesema kuwa Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Mwenye kumuua Mu’aahid,[13] hatanusa harufu ya Al-Jannah, kwa hakika harufu yake husikika masafa ya mwendo wa maisha arubaini.” [Imetolewa na Al-Bukhaariy]

 

 

[1] Jizya ni kodi ya kichwa inayopatikana kutokana na kodi zinazolipwa na wasio kuwa Waislamu wanaoishi katika dola ya Kiislamu. Fedha hizo ambazo zinatumika katika usalama na ulinzi wao wenyewe na mahitaji ya jamii kwa ujumla. Ama Hudna ni mikataba ya amani ya muda ya kusitisha vita.

[2] Huyu ni Abuu ’Umar ‘Aaswim bin ‘Umar bin Qataadah bin An-Nu’maan Al-Answaar alikuwa ni madhubuti. Taabi’ ambaye amepokea Hadiyth nyingi. Elimu yake ni hazina kubwa. Wametofautiana wengi kuhusu mwaka wa kifo chake, tarehe zifuatazo zimerikodiwa kuhusu mwaka wa kifo chake, 119 Hijriyyah, 120, 121, 127 na 129 Hijriyyah.

 

[3] ‘Uthmaan bin Abiy Sulaymaan bin Jubayr bin Mut’im alikuwa ni Qadhi wa Makkah; Ahmad, Ibn Ma’in na Abuu Haatim wanamzingatia kuwa ni madhubuti.

 

[4] Duwmah Al-Jandal lilikuwa ni ngome karibu na Tabuwk lililokuwa likikaliwa na Ukaydir ambaye alikuwa ni mkristo, tukio hili lilitokea mwaka wa 9 Hijriyyah, wakati wa harakati za kuenda Tabuwk.

[5] Jizya zipo za aina mbili: ya binafsi, na ya pamoja. Ikiwa ni kutoka kwa mtu binafsi basi inawahusu wote maskini na tajiri. Kiwango cha chini kwa mwaka kutoka kwa mtu binafsi ni dinari moja. Hata hivyo, watoto na wale bado hawajawa watu wazima hawalipi. Kodi nyinginezo zitakazokatwa na serikali zinatakiwa ziwe juu ya kiwango hicho na si chini ya hapo. Ikiwa wasio kuwa Waislam wakaamua kulipa kwa pamoja basi kodi hiyo itatakiwa kutoka kwa matajiri peke yao tu.

 

[6] Hizi ni nguo zinazotengenezwa Yemen.

 

[7] Huyu ni Abuu Hubayrah aliyekuwa akikaa Basra, alikuwa miongoni mwa Maswahaba. Alihudhuria Bay’atur-Ridhwaan na alifariki wakati wa ukhalifa wa Yazid bin Mu’aawiyah.

 

[8] Hadiyth hii imetajwa kama ni kitangulizi cha kuweka mkataba. Hata kama kuna kipengele kimoja kinaonekana kuwa kiko dhidi ya maslahi ya Waislam basi watu wasivunjike moyo, kwani Allaah ndiye Atakayeunusuru Uislam.

 

[9] Hadiyth hii iko wazi inaonyesha kuwa Muislam hatakiwi kuanza kuwasalimia kwa “As-Salaam ‘alaykum” na Muislam anatakiwa amdhiki Myahudi na Mnaswaara akiwa njiani.

[10] Marwaan bin Al-Hakam Al-Umawl alikuwa ni baba wa ‘Abdul Maalik (Khalifa). Alikuwa gavana wa Madiynah wakati wa Mu’aawiyah. Alishindana na ‘Abdullaah bin Az-Zubayr katika ukhalifa baada ya kufa kwa Yazid na kung’atuka kwa mtoto wa Mu’aawiyah. Aliteka Misri na Shaam. Alikufa Damascus katika mwaka 65 Hijriyyah.

 

[11] Hii inaonesha ushariy’ah wa mkataba waliowekeana baina ya Waislam na wasio kuwa Waislam. Inaeleza pia kuwa Amiri ana uwezo wa kuendelea na kusaini mkataba ambao anaona kuwa utakuwa na faida na Waislam kwa siku za usoni.

 

[12] Alikuwa katika watukufu wa ki-Qurayshi, alikuwa ni mtu mwenye hikmah, mshairi na kiongozi. Alikamatwa katika vita vya Badr akiwa bado ni kafiri, alisilimu katika Fat-h ya Makkah. Maquraysh walibaki wakiwa Waislam wakati wa Ar-Ridda (fitna za baadhi kuritadi) kutokana na yeye Suhayl kuwashauri. Inasemekana alikufa katika vita vya Yarmuk katika mwaka 14 Hijriyyah. Mapokezi mengine yanasema kuwa alikufa katika Marj As-Safr au katika ugonjwa wa tauni wa Amwaas mwaka 18 Hijriyyah.

[13] Mu’aahid ni kafiri anayeishi nje ya mipaka ya dola ya Kiislam na ambaye amepata ruhusa ya kuishi katika dola ya Kiislam. Kumuuwa Mu’aahid ni suala zito kwa maana ya matokeo yake kwani hutoa jina baya la Uislam nje. Kumuuwa Mu’aahid ni haraam kwa mujibu wa kongomano la ‘Ulamaa wote.

Share