41-Fadhila Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Nabiy Pekee Aliyejaaliwa Fadhila Tele Za Kumswalia
Fadhila Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)
41-Nabiy Pekee Aliyejaaliwa Fadhila Tele Za Kumswalia
قال رَسولُ الله صلى الله عليه وسلم: ((مَنْ صَلَّى عَلَيَّ صَلَاةً صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ بِهَا عَشْرًا))
Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وسلم) amesema: ((Atakayeniswalia mara moja basi Allaah Atamswalia mara kumi)) [Hadiyth ya Abuu Hurayrah (رضي الله عنه) - Muslim (1/288) [408] Amesema Al-Bukhaariy katika Swahiyh yake: Abul Al-‘Aaaliyah amesema: “Swalaah ya Allaah ni kumsifu kwake mbele ya Malaika na Swalaah ya Malaika ni du’aa”]
وَقال رَسولُ الله صلى الله عليه وسلم: ((لا تجعلوا قبري عيدا، وصلوا علي فإن صلاتكم تبلغني حيث كنتم))
Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وسلم) amesema: ((Msilifanye kaburi langu kuwa ni mahali pa kurejewa rejewa, na niswalieni kwani kuniswalia kwenu kunanifikia popote mlipo)) [Hadiyth ya Abuu Hurayrah (رضي الله عنه) - Abu Daawuwd (2/218) [2042], Ahmad (2/367) na ameisahihisha Al-Albaaniy (رحمه الله) katika Swahiyh Abi Daawuwd (2/383)]
وَقَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: ((إِنَّ لِلَّهِ مَلائِكَةً سَيَّاحِينَ فِي الأَرْضِ يُبَلِّغُونِي مِنْ أُمَّتِي السَّلام))
Na Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وسلم) amesema: ((Hakika Allaah Ana Malaika wanamzunguka katika ardhi, wananiletea salamu kutoka kwa Ummah wangu)) [Hadiyth ya ‘Abdullaah bin Mas-‘uwd (رضي الله عنه) - An-Nasaaiy (3/43), Al-Haakim (2/421) na ameisahihisha katika Swahiyh An-Nasaaiy (1/274)]
وَقَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّم َ: ((مَا مِنْ أحَدٍ يُسَلِّمْ علَيَّ إلاَّ رَدَّ اللهُ رُوحِي حَتَّى أَرُدَّ عَلَيْهِ السَّلامَ))
Na pia Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وسلم) amesema: ((Hakuna mtu yeyote anayeniswalia ila Allaah hunirudisha roho yangu ili nimrudishie salamu)) [Hadiyth ya Abu Hurayrah (رضي الله عنه) - Abu Daawuwd (2041), na Al-Albaaniy (رحمه الله) ameipa daraja ya Hasan katika Swahiyh Abi Daawuwd (1/283)]