03-Buluwgh Al-Maraam: Kitabu Cha Vyakula: Mlango Wa''Aqiyqah
بُلُوغُ الْمَرام
Buluwgh Al-Maraam
كِتَاب اَلْأَطْعِمَةِ
Kitabu Cha Vyakula
بَابُ اَلْعَقِيقَةِ
03-Mlango Wa ‘Aqiyqah[1]
1167.
عَنِ اِبْنِ عَبَّاسٍ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُمَا، {أَنَّ اَلنَّبِيَّ صلى الله عليه وسلم عَقَّ عَنْ اَلْحَسَنِ وَالْحُسَيْنِ كَبْشًا كَبْشًا} رَوَاهُ أَبُو دَاوُدَ، وَصَحَّحَهُ اِبْنُ خُزَيْمَةَ، وَابْنُ اَلْجَارُودِ، وَعَبْدُ اَلْحَقِّ
لَكِنْ رَجَّحَ أَبُو حَاتِمٍ إِرْسَالَهُ
وَأَخْرَجَ اِبْنُ حِبَّانَ: مِنْ حَدِيثِ أَنَسٍ نَحْوَهُ
Kutoka kwa Ibn ‘Abbaas (رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا) amesema kuwa Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ): “Alimfayia ‘Aqiyqah Hasan na Husayn[2] kondoo mmoja mmoja.”[3] [Imetolewa na Abuu Daawuwd na akaisahihisha Ibn Khuzaymah, Ibn Al-Jaaruwd na ‘Abdul Haqq. Lakini Abuu Haatim ameitilia nguvu kuwa ni Mursal]
Na amepokea Ibn Hibbaan kutoka kwa Anas mfano wake.
1168.
وَعَنْ عَائِشَةَ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهَا، {أَنَّ رَسُولَ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم أَمْرَهُمْ، أَنْ يُعَقَّ عَنْ اَلْغُلَامِ شَاتَانِ مُكَافِئَتَانِ، وَعَنْ اَلْجَارِيَةِ شَاةٌ} رَوَاهُ اَلتِّرْمِذِيُّ وَصَحَّحَهُ
وَأَخْرَجَ اَلْخَمْسَةُ عَنْ أُمِّ كُرْزٍ الْكَعْبِيَّةِ نَحْوَهُ
Kutoka kwa ‘Aaishah (رَضِيَ اللَّهُ عَنْهَا) amesema kuwa: “Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) aliwaamrisha mvulana afanyiwe ‘aqiyqah kwa mbuzi wawili wanaolingana, na mtoto wa kike afanyiwe ‘Aqiyqah mbuzi mmoja.” [Imetolewa na At-Tirmidhiy na akaisahihisha]
Al-Khamsah (At-Tirmidhiy, An-Nasaaiy, Abuu Daawuwd, Ibn Maajah, Ahmad) wameipokea kutoka kwa Ummu Kurzi Al-Ka’biyyah[4] Hadiyth kama hii.
1169.
وَعَنْ سَمُرَةَ رضى الله عنه أَنَّ رَسُولَ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم قَالَ: {"كُلُّ غُلَامٍ مُرْتَهَنٌ بِعَقِيقَتِهِ، تُذْبَحُ عَنْهُ يَوْمَ سَابِعِهِ، وَيُحْلَقُ، وَيُسَمَّى"} رَوَاهُ اَلْخَمْسَةُ، وَصَحَّحَهُ اَلتِّرْمِذِيُّ
Kutoka kwa Samurah (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema kuwa Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Kila kijana amewekwa rahani[5] kwa ‘Aqiyqah yake, huchinjiwa siku yake ya saba,[6] hunyolewa na hupewa jina.” [Imetolewa na Al-Khamsah (At-Tirmidhiy, An-Nasaaiy, Abuu Daawuwd, Ibn Maajah, Ahmad) na akaisahihisha At-Tirmidhiy]
[1] ‘Aqiyqah ni istwilaah inayotumika kwa wanyama, ni kichinjo kwa ajili ya mtoto mchanga anayezaliwa.
[2] Husayn alikuwa ni mdogo kuliko Hasan na takriban alikuwa mdogo kwa mwaka mmoja. Alikuwa ni mjukuu wa Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) na maarufu kwa taqwa yake. Aliuwawa Karbala ‘Iraq tarehe kumi ya Muharram, 61 Hijriyyah.
[3] ‘Aqiyqah ni Sunnah. Hadiyth inayofuata inaelezea kuwa kuchinja kondoo wawili anachinjiwa ikiwa mtoto mwenyewe ni wa kiume, wakati Hadiythi hii inaeleza kuwa Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) ameeleza kuwa kondoo mmoja ni kwa ajili ya mtoto mmoja. Hii inawezekana kuwa hapakuwepo na kondoo wengine wa kuchinja kwa wakati ule. Vinginevyo, ni kuwa kuchinja kondoo wawili kwa mtoto mmoja wa kiume ndiyo Sunnah.
[4] Ummu Kurzi Al-Ka’biyyah alikuwa ni Swahaabiyya katika kabila la Khuza’a na amepokea baadhi za Hadiyth.
[5] Hii ina maana ya kitu kilichowekwa kama dhamana, hakitumiwi. Kwa maelezo hayo ni kuwa huyo mtoto hawezi kumuombea baba yake siku ya Qiyaamah.
[6] Ni sawa sawa kama amechinjwa ng’ombe katika ‘Aqiyqah. Siku mtoto anapozaliwa ndipo atakaposomewa adhaana kwa sikio lake la kuume na Iqaamah katika sikio lake la kushoto, kulingana na baadhi ya ‘Ulamaa. Hata hivyo, Hadiyth iliyoripotiwa na Abuu Daawuwd na At-Tirmidhiy kuwa maelezo haya si sahihi. ‘Aqiyqah itekelezwe siku ya saba baada ya kuzaliwa kwa mtoto. Katika siku hiyo hiyo mtoto anapewa jina na ananyolewa nywele zake. Baada ya hapo, nywele zilizotolewa zinapimwa na thamani yake ya fedha inatolewa kama swadaqah. Vivyo hivyo, mtoto ataombewa du’aa na kufanyiwa tahniyk (kulainishiwa tende na kupewa mdomoni).