00-Buluwgh Al-Maraam: Kitabu Cha Yamini Na Nadhiri
بُلُوغُ الْمَرام
Buluwgh Al-Maraam
كِتَاب اَلْأَيْمَانُ وَالنُّذُورُ
Kitabu Cha Yamini Na Nadhiri
1170.
عَنْ اِبْنِ عُمَرَ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُمَا، {عَنْ رَسُولِ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم أَنَّهُ أَدْرَكَ عُمَرَ بْنَ اَلْخَطَّابِ فِي رَكْبٍ، وَعُمَرَ يَحْلِفُ بِأَبِيهِ، فَنَادَاهُمْ رَسُولُ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم "أَلَا إِنَّ اَللَّهَ يَنْهَاكُمْ أَنْ تَحْلِفُوا بِآبَائِكُمْ، فَمَنْ كَانَ حَالِفاً فَلْيَحْلِفْ بِاَللَّهِ، أَوْ لِيَصْمُتْ"} مُتَّفَقٌ عَلَيْهِ
وَفِي رِوَايَةٍ لِأَبِي دَاوُدَ، وَالنَّسَائِيِّ: عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رضى الله عنه {لَا تَحْلِفُوا بِآبَائِكُمْ، وَلَا بِأُمَّهَاتِكُمْ، وَلَا بِالْأَنْدَادِ، وَلَا تَحْلِفُوا إِلَّا بِاَللَّهِ، وَلَا تَحْلِفُوا بِاَللَّهِ إِلَّا وَأَنْتُمْ صَادِقُونَ"}
Kutoka kwa Ibn ‘Umar (رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا) amesema kuwa: “Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alimkuta ‘Umar bin Al-Khatwaab katika kundi la watu, na ‘Umar anaapa kwa baba yake. Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) akawaita akawaambia: Kwa Yaqini Allaah Anawakataza kuapa kwa baba zenu.[1] Ambaye ataapa basi aape kwa Allaah au anyamaze.” [Bukhaariy, Muslim]
Na katika riwaayah nyingine ya Abuu Daawuwd na An-Nasaaiy kutoka kwa Abuu Hurayrah: “Msiape kwa baba zenu wala kwa mama zenu wala kwa masanamu. Na msiape kwa Allaah isipokuwa muwe wakweli.”
1171.
وَعَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رضى الله عنه قَالَ: قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم {" يَمِينُكَ عَلَى مَا يُصَدِّقُكَ بِهِ صَاحِبُكَ"} وَفِي رِوَايَةٍ: {"اَلْيَمِينُ عَلَى نِيَّةِ اَلْمُسْتَحْلِفِ"} أَخْرَجَهُمَا مُسْلِمٌ
Kutoka kwa Abuu Hurayrah (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Yamini yako ni kwa jambo analokusadiki mwenzio.”[2]
Na katika riwaayah nyingine: “Yamini ni kwa niyyah ya aliyeapisha (Al-Mustahlif).” [Riwaayah zote zimetolewa na Muslim]
1172.
وَعَنْ عَبْدِ اَلرَّحْمَنِ بْنِ سَمُرَةٍ رضى الله عنه قَالَ: قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم {وَإِذَا حَلَفْتَ عَلَى يَمِينٍ، فَرَأَيْتُ غَيْرَهَا خَيْراً مِنْهَا، فَكَفِّرْ عَنْ يَمِينِكَ، وَائْتِ اَلَّذِي هُوَ خَيْرٌ"} مُتَّفَقٌ عَلَيْهِ . وَفِي لَفْظٍ لِلْبُخَارِيِّ: {" فَائِت اَلَّذِي هُوَ خَيْرٌ، وَكَفِّرْ عَنْ يَمِينِكَ"}
وَفِي رِوَايَةٍ لِأَبِي دَاوُدَ: {" فَكَفِّرْ عَنْ يَمِينِكَ، ثُمَّ اِئْتِ اَلَّذِي هُوَ خَيْرٌ"} وَإِسْنَادُهَا صَحِيحٌ
Kutoka kwa ‘Abdur-Rahmaan bin Samurah [3](رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Utakapoapa kiapo kasha ukaona vinginevyo ni kheri kuliko hilo, basi utolee kafara[4] yamini yako na utende lililo bora.” [Bukhaariy, Muslim]
Na katika tamshi la Al-Bukhaariy: “…tolea kafara yamini yako kisha ufanye lililo bora.”
Na katika riwaayah ya Abuu Daawuwd: “…basi utolee kafara yamini yako kisha ufanye lililo bora.” [Isnaadi zake ni sahihi]
1173.
وَعَنْ اِبْنِ عُمَرَ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُمَا، أَنَّ رَسُولَ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم قَالَ: {"مَنْ حَلِفِ عَلَى يَمِينٍ فَقَالَ: إِنْ شَاءَ اَللَّهُ، فَلَا حِنْثَ عَلَيْهِ"} رَوَاهُ اَلْخَمْسَةُ . وَصَحَّحَهُ اِبْنُ حِبَّانَ
Kutoka kwa Ibn ‘Umar (رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا) amesema kuwa Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Mwenye kuapa yamini na akasema In Shaa Allaah (Allaah Akipenda) atakuwa hakuvunja yamini.”[5] [Imetolewa na Al-Khamsah (At-Tirmidhiy, An-Nasaaiy, Abuu Daawuwd, Ibn Maajah, Ahmad) na akaisahihisha Ibn Hibbaan]
1174.
وَعَنْ اِبْنِ عُمَرَ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُمَا قَالَ: {كَانَتْ يَمِينُ اَلنَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم "لَا، وَمُقَلِّبِ اَلْقُلُوبِ"} رَوَاهُ اَلْبُخَارِيُّ
Kutoka kwa Ibn ‘Umar (رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا) amesema: “Ilikuwa yamini ya Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) akisema: Naapa kwa Anayezigeuza nyoyo.”[6] [Imetolewa na Al-Bukhaariy]
1175.
وَعَنْ عَبْدِ اَللَّهِ بْنِ عَمْرِوٍ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُمَا قَالَ: {جَاءَ أَعْرَابِيٌّ إِلَى اَلنَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم فَقَالَ: يَا رَسُولَ اَللَّهِ! مَا اَلْكَبَائِرُ ؟. … فَذَكَرَ اَلْحَدِيثَ، وَفِيهِ قُلْتُ: وَمَا اَلْيَمِينُ اَلْغَمُوسُ ؟ قَالَ: " اَلَّذِي يَقْتَطِعُ مَالَ امْرِئٍ مُسْلِمٍ، هُوَ فِيهَا كَاذِبٌ"} أَخْرَجَهُ اَلْبُخَارِيُّ.
Kutoka kwa ‘Abdullaah bin ‘Amr (رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا) amesema: “Mbedui mmoja alimjia Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) akasema: Ee Rasuli wa Allaah! Ni yapi madhambi makubwa? Akataja Hadiyth yote, ndani yake: Yamini ya uongo.[7] Nikasema ni ipi yamini ya uongo? akasema: ni ambayo mtu huchukua mali ya mtu Muislaam naye ndani ya kiapo chake anakusudia uongo.” [Imetolewa na Al-Bukhaariy]
1176.
وَعَنْ عَائِشَةَ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهَا {فِي قَوْلِهِ تَعَالَى: ﴿ لَا يُؤَاخِذُكُمُ اَللَّهُ بِاللَّغْوِ فِي أَيْمَانِكُمْ ﴾
قَالَتْ: هُوَ قَوْلُ اَلرَّجُلِ: لَا وَاَللَّهِ. بَلَى وَاَللَّهِ} أَخْرَجَهُ اَلْبُخَارِيُّ . وَأَوْرَدَهُ أَبُو دَاوُدَ مَرْفُوعاً
Kutoka kwa ‘Aaishah (رَضِيَ اللَّهُ عَنْهَا) amesema kuhusiana na aayah hii: “Allaah Hatokuchukulieni kwa viapo vyenu vya upuuzi…[8] [Al-Maaidah: 89] imeteremshwa kuhusu mtu anavyosema Hapana Wa-Allaahi! Ndio Wa-Allaahi.”[9] [Imetolewa na Al-Bukhaariy, na Abuu Daawuwd ameipokea ikiwa ni marfuw’a]
1177.
وَعَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رضى الله عنه قَالَ: قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم {"إِنَّ لِلَّهِ تِسْعًا وَتِسْعِينَ اِسْماً، مَنْ أَحْصَاهَا دَخَلَ اَلْجَنَّةَ"} مُتَّفَقٌ عَلَيْهِ . وَسَاقَ اَلتِّرْمِذِيُّ وَابْنُ حِبَّانَ اَلْأَسْمَاءِ، وَالتَّحْقِيقُ أَنَّ سَرْدَهَا إِدْرَاجٌ مِنْ بَعْضِ اَلرُّوَاةِ
Kutoka kwa Abuu Hurayrah (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Kwa hakika Allaah Ana Majina tisini na tisa,[10] mwenye kuyahifadhi ataingia Al-Jannah.”[11] [Bukhaariy, Muslim. Tirmidhiy na Ibn Hibbaan wametaja majina hayo. Lakini uhakiki ni kuwa utajo wake ni (Idraaj) si Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ)]
1178.
وَعَنْ أُسَامَةَ بْنِ زَيْدٍ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُمَا قَالَ: قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم {"مَنْ صُنِعَ إِلَيْهِ مَعْرُوفٌ، فَقَالَ لِفَاعِلِهِ: جَزَاكِ اَللَّهُ خَيْراً. فَقَدْ أَبْلَغَ فِي اَلثَّنَاءِ"} أَخْرَجَهُ اَلتِّرْمِذِيُّ، وَصَحَّحَهُ اِبْنُ حِبَّانَ
Kutoka kwa Usaamah bin Zayd (رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا) amesema Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Anayefanyiwa wema na akamuambia aliyemfanyia Jazaaka-Allaahu khayran (Allaah Akujaze kheri) hakika atakuwa amekamilisha hisani kwa ukamilifu.”[12] [Imetolewa na At-Tirmidhiy na akaisahihisha Ibn Hibbaan]
1179.
وَعَنْ اِبْنِ عُمَرَ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُمَا، {عَنْ اَلنَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم أَنَّهُ نَهَى عَنْ اَلنَّذْرِ وَقَالَ: " إِنَّهُ لَا يَأْتِي بِخَيْرٍ وَإِنَّمَا يُسْتَخْرَجُ بِهِ مِنْ اَلْبَخِيلِ"} مُتَّفَقٌ عَلَيْهِ
Kutoka kwa Ibn ‘Umar (رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا) amesema kuwa: “Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alikataza kuweka nadhiri[13] na akasema: Haileti kheri bali kutoka kwa bakhili hutolewa nadhiri.” [Bukhaariy, Muslim]
1180.
وَعَنْ عُقْبَةَ بْنِ عَامِرٍ رضى الله عنه قَالَ: قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم {"كَفَّارَةُ اَلنَّذْرِ كَفَّارَةُ يَمِينٍ"} رَوَاهُ مُسْلِمٌ. وَزَادَ اَلتِّرْمِذِيُّ فِيهِ: {إِذَا لَمْ يُسَمِّ} ، وَصَحَّحَهُ.
وَلِأَبِي دَاوُدَ: مِنْ حَدِيثِ اِبْنِ عَبَّاسٍ مَرْفُوعاً: {"مِنْ نَذَرَ نَذْراً لَمْ يُسَمِّهِ، فَكَفَّارَتُهُ كَفَّارَةُ يَمِينٍ، وَمَنْ نَذَرَ نَذْراً فِي مَعْصِيَةٍ، فَكَفَّارَتُهُ كَفَّارَةُ يَمِينٍ، وَمَنْ نَذَرَ نَذْراً لَا يُطِيقُهُ، فَكَفَّارَتُهُ كَفَّارَةُ يَمِينٍ"} وَإِسْنَادُهُ صَحِيحٌ، إِلَّا أَنَّ اَلْحُفَّاظَ رَجَّحُوا وَقْفَهُ.
وَلِلْبُخَارِيِّ: مِنْ حَدِيثِ عَائِشَةَ: {" وَمَنْ نَذَرَ أَنْ يَعْصِيَ اَللَّهَ فَلَا يَعْصِهِ"}
وَلِمُسْلِمٍ: مِنْ حَدِيثِ عِمْرَانَ: {" لَا وَفَاءَ لِنَذْرٍ فِي مَعْصِيَةٍ"}
Kutoka kwa ‘Uqbah bin ‘Aamir (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Kafara ya nadhiri ndio kafara ya yamini.”[14] [Imetolewa na Muslim] na akazidisha At-Tirmidhiy: “…asipoitaja.” [Na ameisahihisha]
Na Abuu Daawuwd ameipokea kutoka katika Hadiyth ya Ibn ‘Abbaas (رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا) ikiwa ni Marfuw’: “Mwenye kuweka nadhiri ambayo haikutajwa, basi kafara yake ni kafara ya yamini. Na mwenye kuweka nadhiri ya katika maasi, basi kafara yake ni kafara ya yamini. Na mwenye kuweka nadhiri ya jambo asiloweza, basi kafara yake ni kafara ya yamini.” [Isnaad yake ni sahihi isipokuwa Wanazuoni wa Hadiyth wameitilia nguvu kuwa ni Mawquwf]
Bukhaariy ameipokea kutoka katika Hadiyth ya ‘Aaishah: “… na mwenye kuweka nadhiri ya kumuasi Allaah asimuasi.”
Muslim amepokea katika Hadiyth ya ‘Imraan: “Hakuna kutekeleza nadhiri katika maasia.”
1181.
وَعَنْ عُقْبَةَ بْنِ عَامِرٍ رضى الله عنه قَالَ: {نَذَرَتْ أُخْتِي أَنْ تَمْشِيَ إِلَى بَيْتِ اَللَّهِ حَافِيَةً، فَقَالَ اَلنَّبِيُّ صلى الله عليه وسلم "لِتَمْشِ وَلْتَرْكَبْ"} مُتَّفَقٌ عَلَيْهِ، وَاللَّفْظُ لِمُسْلِمٍ.
وَلِلْخَمْسَةِ. فَقَالَ: {" إِنَّ اَللَّهَ لَا يَصْنَعُ بِشَقَاءِ أُخْتِكَ شَيْئاً، مُرْهَا: فَلْتَخْتَمِرْ ، وَلْتَرْكَبْ، وَلْتَصُمْ ثَلَاثَةَ أَيَّامٍ"}
Kutoka kwa ‘Uqbah bin ‘Aamir (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema: “Dada yangu aliweka nadhiri ya kutembea hadi katika nyumba ya Allaah bila viatu. Akaniamuru kutaka Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) fatwa yake. Nami nikamuuliza, Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) akasema: “Atembee na apande.” [Al-Bukhaariy, Muslim na tamshi hili ni la Muslim]
Al-Khamsah (At-Tirmidhiy, An-Nasaaiy, Abuu Daawuwd, Ibn Maajah, Ahmad) wamepokea: “Kwa hakika Allaah Hana haja ya Kumtesa dada yako kwa jambo lolote. Muambie avae mtandio, apande (mnyama) na afunge siku tatu.”
1182.
وَعَنْ اِبْنِ عَبَّاسٍ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُمَا قَالَ: {اِسْتَفْتَى سَعْدُ بْنُ عُبَادَةَ رضى الله عنه رَسُولَ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم فِي نَذْرٍ كَانَ عَلَى أُمِّهِ، تُوُفِّيَتْ قَبْلِ أَنْ تَقْضِيَهُ ؟ فَقَالَ: "اِقْضِهِ عَنْهَا"} مُتَّفَقٌ عَلَيْهِ
Kutoka kwa Ibn ‘Abbaas (رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا) amesema: “Sa’d bin ‘Ubaada[15] (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) alimuuliza Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) juu ya nadhiri iliyompasa mama yake,[16] akafariki kabla ya kuilipa. Akasema: “Mlipie.” [Bukhaariy, Muslim]
1183.
وَعَنْ ثَابِتِ بْنِ اَلضَّحَّاكِ رضى الله عنه قَالَ: {نَذَرَ رَجُلٌ عَلَى عَهْدِ رَسُولِ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم أَنْ يَنْحَرَ إِبِلاً بِبُوَانَةَ، فَأَتَى رَسُولَ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم فَسَأَلَهُ: فَقَالَ: "هَلْ كَانَ فِيهَا وَثَنٌ يُعْبَدُ ؟" . قَالَ: لَا. قَالَ: "فَهَلْ كَانَ فِيهَا عِيدٌ مِنْ أَعْيَادِهِمْ ؟" فَقَالَ: لَا. فَقَالَ: "أَوْفِ بِنَذْرِكَ، فَإِنَّهُ لَا وَفَاءَ لِنَذْرٍ فِي مَعْصِيَةِ اَللَّهِ، وَلَا فِي قَطِيعَةِ رَحِمٍ، وَلَا فِيمَا لَا يَمْلِكُ اِبْنُ آدَمَ"} رَوَاهُ أَبُو دَاوُدَ، وَالطَّبَرَانِيُّ وَاللَّفْظُ لَهُ، وَهُوَ صَحِيحُ اَلْإِسْنَادِ.
وَلَهُ شَاهِدٌ: مِنْ حَدِيثِ كَرْدَمٍ. عِنْدَ أَحْمَدَ
Kutoka kwa Thaabit bin Adw-Dwahhaak (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema: “Mtu mmoja katika zama za Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) aliweka nadhiri ya kuchinja ngamia Buwaanah, akamuendea Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) akamuuliza. Akasema: Je ndani yake kulikuwa na sanamu anayeabudiwa?[17] Akasema: Hapana. Akasema: Tekeleza nadhiri yako, kwa hakika si ruhusa kutekeleza nadhiri katika kumuasi Allaah wala katika kukata kizazi wala katika asichomiliki mwana Aadam.” [Imetolewa na Abuu Daawuwd na Atw-Twabaraaniyy. Isnaad yake ni sahihi na ina ushahidi kutoka katika Hadiyth ya Kardam[18] kwa Ahmad]
1184.
وَعَنْ جَابِرٍ رضى الله عنه {أَنَّ رَجُلاً قَالَ يَوْمَ اَلْفَتْحِ: يَا رَسُولَ اَللَّهِ! إِنِّي نَذَرْتُ إِنْ فَتَحَ اَللَّهُ عَلَيْكَ مَكَّةَ أَنْ أُصَلِّيَ فِي بَيْتِ اَلْمَقْدِسِ، فَقَالَ: "صَلِّ هَا هُنَا" . فَسَأَلَهُ، فَقَالَ: "صَلِّ هَا هُنَا". فَسَأَلَهُ، فَقَالَ: "شَأْنُكَ إِذًا"} رَوَاهُ أَحْمَدُ، أَبُو دَاوُدَ، وَصَحَّحَهُ اَلْحَاكِمُ
Kutoka kwa Jaabir (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema kuwa: “Mtu mmoja siku ya Fat-h Makkah alisema: Ee Rasuli wa Allaah! Mimi nimeweka nadhiri iwapo Allaah Atakufungulia mji wa Makkah nitaswali katika Msikiti wa Baytul-Maqdis (Jerusalem). Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) akasema: Swali hapa hapa.[19] Akamuuliza tena, Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) akasema: Swali hapa hapa. Akamuuliza tena, Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) akasema: kwa hivyo ni shauri yako.” [Imetolewa na Ahmad na Abuu Daawuwd na akaisahihisha Al-Haakim]
1185.
وَعَنْ أَبِي سَعِيدٍ اَلْخُدْرِيِّ رضى الله عنه عَنْ اَلنَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم قَالَ: {"لَا تُشَدُّ اَلرِّحَالُ إِلَّا إِلَى ثَلَاثَةِ مَسَاجِدَ: مَسْجِد اَلْحَرَامِ، وَمَسْجِدِ اَلْأَقْصَى، وَمَسْجِدِي"} مُتَّفَقٌ عَلَيْهِ، وَاللَّفْظُ لِلْبُخَارِيِّ
Kutoka kwa Abiy Sa’iyd Al-Khudriyy (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema kuwa Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Si ruhusa kufunga safari ila katika Miskiti mitatu: Masjidil-Haraam, Masjidil-Aqswaa na Msikiti wangu huu.” [Bukhaariy, Muslim na tamshi hili ni la Al-Bukhaariy]
1186.
وَعَنْ عُمَرَ رضى الله عنه قَالَ: {قُلْتُ: يَا رَسُولَ اَللَّهِ! إِنِّي نَذَرْتُ فِي اَلْجَاهِلِيَّةِ، أَنْ أَعْتَكِفَ لَيْلَةً فِي اَلْمَسْجِدِ اَلْحَرَامِ. قَالَ: "فَأَوْفِ بِنَذْرِكَ" } مُتَّفَقٌ عَلَيْهِ وَزَادَ اَلْبُخَارِيُّ فِي رِوَايَةٍ {فَاعْتَكَفَ لَيْلَةً}
Kutoka kwa ‘Umar (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema: “Nilisema: Ee Rasuli wa Allaah! Nilikuwa nimeweka nadhiri zama za ujahiliya,[20] nikakaa I’tikaaf usiku mmoja katika Al-Masjid Al-Haraam. Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) akaniambia: tekeleza nadhiri yako.” [Bukhaariy, Muslim]
Katika riwaayah nyingine Bukhaariy ameongezea: “…akakaa I’tikaaf usiku mmoja.”
[1] Ilikuwa ni tabia ya Waarabu kuapa kwa majina ya baba zao na babu zao. ‘Umar alipoapa mbele ya Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alikatazwa kufanya hivyo, na kuwa akitaka kuapa na aape kwa jina la Allaah. Maelezo kama ‘Nakuapia’, ‘Naapa kwa kichwa chako’ ‘Naapa kwa Husain’ ‘Naapa kwa Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ)’. Matumizi ya viapo vyote hivi havifai, bali viapo kama hivyo huwa ni shirki.
[2] Hadiyth hii inaelezea ikiwa muapaji (Al-Halif) kwa kumtaka anayeambiwa (Al-Mustahlif) mwenye haki, kiapo kitachukuliwa kuwa ni cha jambo maalumu tu. Niyyah iliyojificha ya anayeapa (Al-Halif) haitozingatiwa. Kitakachozingatiwa ni ile niyyah ya Al-Mustahlif aliyeomba kiapo kifanyike. Hata hivyo ikiwa mtu ataapa mwenyewe bila ya kutakiwa kiapo, basi chochote atakachofanya ndicho kitakachozingatiwa.
[3] ‘Abdur-Rahmaan bin Samurah: Lakabu yake ni Abuu Sa’iyd alikuwa ni Swahaba. Alisilimu baada ya Fat-h na alifungua Sijistan na Kabul. Aliishi Basra ‘Iraaq na alifariki mwaka 50 Hijriyyah
[4] Kafara ya kiapo ni a: Kumuachia huru mtumwa, b) kulisha watu kumi, c) Kuwapa nguo watu, d) Kufunga (Swiyaam) siku tatu.
[5] Hadiyth hii inataka watu wafungamanishe viapo vyao na Atakavyo Allaah kwa kusema In Shaa Allaah wakati wa kuapa.
[6] Hadiyth hii inaonesha kuwa suala la kuapia si kwa majina ya Allaah (Al-Asmaa) peke yake. Inaruhusiwa kuapia kwa sifa zake (Asw-Swifaat). Hili linaruhusiwa kama mtu ataapia kwa sifa zake (Asw-Swifaat Adh-dhaatiyya) kama vile elimu, nguvu na sifa za Ilaah (Asw-Swifaat Al-Fi’liyyah) kama vile hasira, ridhaa n.k.
[7] Katika lugha ya Kiarabu, Yamiyn ghamuws (Kiapo cha uongo) ni kile kiapo kinachokusudia kuhadaa, kudanganya kwa niyyah ya kuchuka mali ya mtu bila ya haki. Ikiwa jambo hilo la kuapa halikusudii mali basi kiapo chenyewe kitajulikana kama Yamiyn faajir. Hakuna kafara kwa Yamiyn ghamuws. Kafara pekee ya hili ni kurudisha mali ya watu, kumuomba Allaah maghfirah.
[8] Rejea Suwrat Al-Maaidah Aayah ya 89.
[9] Mazungumzo anayotoa mtu bila ya kufikiriwa hayazigatiwi, hayachukuliwi kama ni viapo. Katika hali hii hamna kafara au adhabu, hata hivyo ni tabia ambayo haipendezi.
[10] Mbali na majina haya kuna majina mengine yanayonasibishwa na Allaah. Majina mengine ni nyongeza lakini nayo ni Matukufu
[11] Maana yake na inakusudiwa vile vile kuyahifadhi na kuyatumia mara kwa mara na kuyatumia maana yake kiutekelezaji katika maisha ya kila siku.
[12] Mtu aliyefanyiwa jambo fulani nae ajitahidi amfanyie aliyemfanyia vizuri zaidi. Kama hatoweza kufanya basi na amuombee du’aa.
[13] Nadhiri iliyokatazwa ni kama vile mtu kusema: “Ikiwa mgonjwa wangu atapona, nitatoa swadaqah kiasi kadhaa.” Hii ina maana kuwa hatoi Swadaqah kwa dhati ya Allaah bali ameifungamanisha na anachokitaka. Vivyo hivyo, ndiyo hali ya bakhili kwani mara nyingi hatoi mali yake ila kwa makusudio ya kupata kitu fulani. Inabidi watu kufahamu kuwa kuweka nadhiri hakubadilishi Qadar ya mtu. Hili linahusu nadhiri iliyokokotezwa kwa jina la Allaah, sembuse nadhiri zilizoapiwa kwa kaburi la fulani, au mtu kuamini kuwa aliyelala katika kaburi fulani ndiye mwenye uwezo wa kubadilisha hali ya fulani au kuleta maslahi fulani? kwa hakika siyo kwamba aina hii ya nadhiri zinakatazwa bali ni ushirikina kwa dhati yake.
[14] Ikiwa nadhiri inajitegemea bila kuainisha na jambo lolote kama vile mtu kusema: “Nimeweka nadhiri kwa Jina la Allaah.” Nadhiri au kiapo cha aina hii hakijakamilika, atalazimika kutoa kafara ya kiapo. Ikiwa kiapo chenyewe kimeainishwa, na mtu ana uwezo wa kuitekeleza basi ni wajibu kwake kuitekeleza. Ikiwa aliyeapa hana uwezo wa kutekeleza, itabidi atoe kafara ya kiapo kama ilivyo ya yamini. Ikiwa kiapo chenyewe kimefungamanishwa na kumuasi Allaah au kufanya jambo lolote la dhambi, baadhi ya Wanazuoni wana rai ya kutotolewa kafara yoyote, wakati wengine wana rai kuwa ni lazima atoe kafara ya kiapo (Kaffaarah Al-Yamiyn)
[15] Sa’d bin ‘Ubaada: Alikuwa kiongozi wa Al-Khazraj, mbeba bendera wa Answaar katika vita vyote na kiongozi wa msafara wa Bay’atul-‘Aqaba. Alikuwa mtu mwenye heshima, mkarimu na alikuwa mwandishi. Alikuwa hodari katika kuogelea na kutupa mishale, alijulikana kwa jina Al-Kaamil (mkamilifu) kwa sababu ya tabia na sifa alizokuwa nazo. Alikuwa akitoa swadaqah nyingi mara kwa mara. Aliwahi kuondoka Madiynah kabla ya Abuu Bakr kutoa kiapo cha ukhalifa. Alikufa mwaka 14 Hijriyyah na wengine wanasema 15 au 16.
[16] Mapokezi haya hayakuelezea aina ya kiapo kilichotolewa. Katika Hadiyth nyingine inaonesha ni kiapo cha kuacha mtumwa. Hii inaelezea kuwa mtu aliyekufa katika hali hii warithi wake wanatakiwa wamlipie kiapo chake.
[17] Hadiyth inatuelezea kuwa ikiwa mtu ameweka nadhiri au kiapo cha kufanya ‘ibaadah katika sehemu fulani, basi ni wajibu kwake kutekeleza kiapo kile, maadamu ya kuwa sehemu ile anayotaka kufanyia ‘ibaadah hakuna ‘ibaadah za kijahiliya zinazofanyika. Hata hivyo pamoja na kukubalika huko, si lazima atekeleze ‘ibaadah ile sehemu ile ile.
[18] Kardam bin Sufyaan Ath-Thaqafi alikuwa Swahaba na binti yake Maymuwna aliyekuwa Swahabiya na aliyepokea Hadiyth kutoka kwake alikuwa ni ‘Abdullaah bin ‘Amr bin Al-‘Aasw.
[19] Hadiyth hii inagusia kanuni ya msingi kuwa ikiwa mtu ameapa kuwa atafanya ‘ibaadah sehemu fulani, ni wajibu kutekeleza kiapo kile kwa kiwango cha ‘ibaadah cha Msikiti mwingine wenye hadhi kama Msikiti ule. Kama ataswali Msikiti wenye hadhi ya chini basi atakuwa hajatekeleza kiapo kile. Hapa kuswali kwake katika Msikiti wa Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) Madiynah au Al-Ka’bah atakuwa ametekeleza kile kiapo. Ama akitoa kiapo cha kuswali katika Masjid Al-Haram Makkah hawezi kutekeleza kiapo kile kwa kuswali Baytul-Maqdis au Masjid Nabawi Madiynah. Ni lazima aswali katika Masjid Al-Haram Makkah.
[20] Watu wanaona kuwa kiapo cha kafiri hakina nafasi katika Uislaam. Katika Hadiyth hii ni dalili kama kafiri atakuwa ameweka kiapo chake kisha akasilimu ni lazima atekeleze kile kiapo chake. Huu ni muono wa Al-Bukhaariy, Ibn Jariyr na wengineo.