44-Fadhila Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) : Baina Ya Nyumba Yake Na Minbar Yake Amefanyiwa Kipande Cha Pepo Rawdhwatul-Jannah

Fadhila Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)

 

44-Baina Ya Nyumba Yake Na Minbar Yake Amefanyiwa

Kipande Cha Pepo Rawdhwatul-Jannah

www.alhidaaya.com

 

 

Allaah (عز وجل) Amemfanyia Nabiy Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم)  kipande cha Jannah (Pepo) baina ya nyumba yake na Minbar yake. Na nyumba yake hiyo ni ile ambayo ilikuwa ni ya Mama wa Waumini ‘Aaishah (رضي الله عنها):  

 

 

عنْ أَبِى هُرَيْرَةَ رضى الله عنه عَنِ النَّبِىِّ صلى الله عليه وسلم قَالَ : ( مَا بَيْنَ بَيْتِى وَمِنْبَرِى رَوْضَةٌ مِنْ رِيَاضِ الْجَنَّةِ )  

Kutoka kwa Abiu Hurayrah (رضي الله عنه)  kwamba Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: ((Baina ya nyumba yangu na Minbari yangu kuna Rawdhwah kutoka Rawdhwah ya Jannah)) yaani kipande cha Peponi. [Al-Bukhaari (1196), Muslim (1391)]

 

 

Na ‘Ulamaa wamekubaliana kwamba katika hiyo Rawdhwatul-Jannah, ni mustahabb (inapendekezwa) kumdhukuru Allaah (سبحانه وتعالى) kwa kila aina ya kumdhukuru; kuswali rakaa mbili, pindi mtu anapojaaliwa kutembelea Masjdi An-Nabawiy (Msikiti wa Nabiy ulioko Madiynah). Lakini kwa hali ilivyo sasa ya msongamano mkubwa wa watu, mtu anaweza kuswali katika maeneo ya kando ili kuepusha zahma na madhara kwa Waislamu na bila shaka hupata thawabu na fadhila zake sawasawa bila ya upungufu wowote wa fadhila za hicho kipande cha Rawdhwatul-Jannah, bali kwa sababu ya niyyah njema ya kuepusha msongamano baina ya Waislamu, huenda mtu akalipwa malipo zaidi kutokana na niyyah yake njema.  

 

 

 

Share