49-Fadhila Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Nabiy Pekee Aliyepewa Kauli Za Kusherehi Kitabu Chake
Fadhila Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)
49-Nabiy Pekee Aliyepewa Kauli Za Kusherehi Kitabu Chake
Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):
وَأَنزَلْنَا إِلَيْكَ الذِّكْرَ لِتُبَيِّنَ لِلنَّاسِ مَا نُزِّلَ إِلَيْهِمْ وَلَعَلَّهُمْ يَتَفَكَّرُونَ﴿٤٤﴾
(Tumewatuma) Kwa hoja bayana na vitabu. Na Tumekuteremshia Ukumbusho (Qur-aan) ili uwabainishie watu yaliyoteremshwa kwao huenda wakapata kutafakari. [An-Nahl: 44]
Maana yake: “Tumekuteremshia Qur-aan ee Rasuli, ili uwabainishie wazi watu yaliyofichikia katika maana zake, hukmu zake na ili wazingatie (Aayaat) na waongoke kwayo.” [Tafsiyr Al-Muyassar]
Hivyo basi anayoyasema katika kusherehi Aayaat za Qur-aan ni Wahyi Aliofunuliwa Na Allaah (سبحانه وتعالى) Ambaye Anasema:
مَا يَنطِقُ عَنِ الْهَوَىٰ ﴿٣﴾
Na wala hatamki kwa hawaa.
إِنْ هُوَ إِلَّا وَحْيٌ يُوحَىٰ ﴿٤﴾
Hayo si chochote isipokuwa ni Wahy unaofunuliwa. [An-Najm: 3-4]
Akasema Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) kuthibitisha hayo katika Hadiyth:
((أَلَا إِنِّي أُوتِيتُ الْقُرْآنَ وَمِثْلَهُ مَعَهُ)) صحيح رواه أبو داود
((Hakika mimi nimepewa Qur-aan na mfano wake)) [Hadiyth Swahiyh, Abuu Daawuwd]