095-Asbaabun-Nuzuwl: At-Tawbah Aayah 095: سَيَحْلِفُونَ بِاللَّـهِ لَكُمْ إِذَا انقَلَبْتُمْ إِلَيْهِمْ لِتُعْرِضُوا عَنْهُمْ ۖ فَأَعْرِضُوا عَنْهُمْ
أسْبابُ النُّزُول
Asbaabun-Nuzuwl
Sababu Za Kuteremshwa (Baadhi Ya Suwrah Na Aayaat Za Qur-aan)
Imekusanywa na: Alhidaaya.com
Suwrah At-Tawbah: Aayah 95-96
Kauli ya Allaah (سبحانه وتعالى):
سَيَحْلِفُونَ بِاللَّـهِ لَكُمْ إِذَا انقَلَبْتُمْ إِلَيْهِمْ لِتُعْرِضُوا عَنْهُمْ ۖ فَأَعْرِضُوا عَنْهُمْ ۖ إِنَّهُمْ رِجْسٌ ۖ وَمَأْوَاهُمْ جَهَنَّمُ جَزَاءً بِمَا كَانُوا يَكْسِبُونَ﴿٩٥﴾
Watakuapieni kwa Allaah, mtakaporudi kwao ili muwapuuze. Basi wapuuzeni; hakika wao ni najsi, na makazi yao ni Jahannam. Ni jazaa kwa yale waliyokuwa wakiyachuma.
يَحْلِفُونَ لَكُمْ لِتَرْضَوْا عَنْهُمْ ۖ فَإِن تَرْضَوْا عَنْهُمْ فَإِنَّ اللَّـهَ لَا يَرْضَىٰ عَنِ الْقَوْمِ الْفَاسِقِينَ﴿٩٦﴾
Watakuapieni ili muwaridhie. Mkiwaridhia, basi hakika Allaah Haridhii watu mafasiki. [At-Tawbah: 95 – 96]
Sababun-Nuzuwl:
حدثني يونس قال أخبرنا ابن وهب قال أخبرني يونس عن ابن شهاب قال أخبرني عبد الرحمن بن عبد الله بن كعب بن مالك أن عبد الله بن كعب قال: سمعت كعب بن مالك يقول لما قدم رسول الله صلى الله عليه وعلى آله وسلم من تبوك جلس للناس فلما فعل ذلك جاءه المخلفون فطفقوا يعتذرون إليه ويحلفون له، وكانوا بضعة وثمانين رجلا، فقبل منهم رسول الله صلى الله عليه وعلى آله وسلم علانيتهم وبايعهم واستغفر لهم ووكل سرائرهم إلى الله، وصدقته حديثي فقال كعب: والله ما أنعم الله علي من نعمة قط بعد أن هداني للإسلام أعظم في نفسي من صدقي رسول الله صلى الله عليه وعلى آله وسلم ألا أكون كذبته فأهلك كما هلك الذين كذبوا، إن الله قال للذين كذبوا؟ حين أنزل الوحي شر ما قال لأحد:
Amenihadithia Yuwnus amesema, amenieleza Ibn Wahaab amesema, amenieleza Yuwnus toka kwa Ibn Shihaab amesema, amenieleza ‘Abdurrahmaan bin ‘Abdillaah bin Ka’ab bin Maalik kuwa ‘Abdullaah bin Ka’ab amesema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alipokuja toka Tabuk, alikaa ili kuzungumza na watu. Alipofanya hivyo, waliobaki majumbani wasende vitani walimjia wakaanza kumwelezea nyudhuru zao na kumwapia, walikuwa ni watu themanini na kuzidi kidogo. Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akawakubalia udhuru wao mbele ya nyuso zao, akawapa bay-‘i, akawaombea maghfirah, na waliyoficha vifuani mwao akamwachia Allaah. Mimi nilimweleza ukweli, akasema Ka’ab: Wa-Allaah, Allaah Hakunineemesha neema yoyote ile kamwe baada ya kunihidi kwenye Uislamu iliyo kubwa zaidi ndani ya nafsi yangu kuliko kumwambia ukweli Rasuli wa Allaah, nisije kuongopa kwake nikaja kuangamia kama walivyoangamia waliosema uongo. Hakika Allaah Amewaambia maneno mabaya mno wale waliosema uongo wakati Alipoteremsha wahyi, maneno ambayo Hakumwambia yeyote:
سَيَحْلِفُونَ بِاللَّـهِ لَكُمْ إِذَا انقَلَبْتُمْ إِلَيْهِمْ لِتُعْرِضُوا عَنْهُمْ ۖ فَأَعْرِضُوا عَنْهُمْ ۖ إِنَّهُمْ رِجْسٌ ۖ وَمَأْوَاهُمْ جَهَنَّمُ جَزَاءً بِمَا كَانُوا يَكْسِبُونَ﴿٩٥﴾
Watakuapieni kwa Allaah, mtakaporudi kwao ili muwapuuze. Basi wapuuzeni; hakika wao ni najsi, na makazi yao ni Jahannam. Ni jazaa kwa yale waliyokuwa wakiyachuma.
Mpaka katika Kauli Yake:
فَإِنَّ اللَّـهَ لَا يَرْضَىٰ عَنِ الْقَوْمِ الْفَاسِقِينَ﴿٩٦﴾
basi hakika Allaah Haridhii watu mafasiki.
[Wapokezi wa Hadiyth hii ni watu madhubuti waaminifu. Na Yuwnus Shaykh Atw-Twabariy ndiye yeye Ibn ‘Abdil Al-A’laa, na Yuwnus Shaykh Ibn Wahaab ndiye Ibn Yaziyd Al-Aylaa. Shaykh wetu Allaah Amhifadhi amesema: Na mfano katika Swahiyh Al-Bukhaariy katika kuhitimisha Hadiyth ya Ka’ab bin Maalik katika Kitabu cha Vita, mlango wa Vita Vya Tabuk]
Pia katika usimulizi mwengine:
عَنْ عَبْدِ الرَّحْمَنِ بْنِ عَبْدِ اللَّهِ، أَنَّ عَبْدَ اللَّهِ بْنَ كَعْبِ بْنِ مَالِكٍ، قَالَ سَمِعْتُ كَعْبَ بْنَ مَالِكٍ، حِينَ تَخَلَّفَ عَنْ تَبُوكَ، وَاللَّهِ، مَا أَنْعَمَ اللَّهُ عَلَىَّ مِنْ نِعْمَةٍ بَعْدَ إِذْ هَدَانِي أَعْظَمَ مِنْ صِدْقِي رَسُولَ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم أَنْ لاَ أَكُونَ كَذَبْتُهُ فَأَهْلِكَ كَمَا هَلَكَ الَّذِينَ كَذَبُوا حِينَ أُنْزِلَ الْوَحْىُ: ((سَيَحْلِفُونَ بِاللَّهِ لَكُمْ إِذَا انْقَلَبْتُمْ إِلَيْهِمْ)) إِلَى ((الْفَاسِقِينَ))
Kutoka kwa ‘Abdurrahmaan bin ‘Abdillaah kwamba: ‘Abdullaah bin Ka’ab bin Maalik, amesema: Nimemsikia Ka’ab bin Maalik pindi walipobakia nyuma kutokwenda (Vita vya) Tabuk, akisema: “Wa-Allaah, Allaah Hakunineemesha neema yoyote ile kamwe baada ya kunihidi, neema ambayo ni kubwa kulikoni neema ya kumwambia ukweli Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم), kwani lau ningelimwambia uongo, ningeliangamia kama walivyoangamia wale waliosema uongo pindi Wahyi ulipoteremshwa wa:
سَيَحْلِفُونَ بِاللَّـهِ لَكُمْ إِذَا انقَلَبْتُمْ إِلَيْهِمْ لِتُعْرِضُوا عَنْهُمْ ۖ فَأَعْرِضُوا عَنْهُمْ ۖ إِنَّهُمْ رِجْسٌ ۖ وَمَأْوَاهُمْ جَهَنَّمُ جَزَاءً بِمَا كَانُوا يَكْسِبُونَ﴿٩٥﴾
Watakuapieni kwa Allaah, mtakaporudi kwao ili muwapuuze. Basi wapuuzeni; hakika wao ni najsi, na makazi yao ni Jahannam. Ni jazaa kwa yale waliyokuwa wakiyachuma.
يَحْلِفُونَ لَكُمْ لِتَرْضَوْا عَنْهُمْ ۖ فَإِن تَرْضَوْا عَنْهُمْ فَإِنَّ اللَّـهَ لَا يَرْضَىٰ عَنِ الْقَوْمِ الْفَاسِقِينَ﴿٩٦﴾
Watakuapieni ili muwaridhie. Mkiwaridhia, basi hakika Allaah Haridhii watu mafasiki. [At-Tawbah: 95 – 96]
[Al-Bukhaariy – Kitaab At-Tafsiyr]